HOTUBA YA BAJETI
1.
Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo
hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya kisekta inayohusu Wizara yangu, naomba
kutoa hoja kwamba Bunge sasa likubali kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara
ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na taasisi zake kwa mwaka wa fedha
2002/2003.
2.
Mheshimiwa
Spika, aidha niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge,
ndugu na marafiki katika kuwafariji na kuwapa salamu za rambi rambi familia,
ndugu na wapiga kura wa marehemu Mheshimiwa
Sebastian Rukiza Kinyondo aliyekuwa Mbunge wa Bukoba Vijijini, marehemu Mheshimiwa John Mangwangwa aliyekuwa
Mbunge wa Mpanda Magharibi, aliyekuwa Katibu Mkuu katika Wizara yangu marehemu Alfred Edward Chale, pamoja na aliyekuwa Mwandishi Mkuu wa Sheria Ndugu
Sigfrid Lushagara, Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi,
Amina.
3.
Mheshimiwa
Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wote
wale waliotuwezesha kutekeleza majukumu ya Wizara yetu kwa kipindi cha mwaka
uliopita na wale, ambao wametuwezesha kupanga mipango ya mwaka 2002/2003 na
kuboresha maandalizi ya hoja zetu ambazo tunawasilisha katika hotuba hii. Shukrani za
kwanza ziende kwa wananchi
wote na walipa kodi wa Tanzania. Shukrani zangu za pekee zimwendee Naibu Waziri wangu, Mheshimiwa Zabein
Muhaji Mhita, Mbunge na Kaimu Katibu Mkuu wa Wizara yangu Ndugu Raphael Peter Kabende kwa
msaada na ushauri wanaonipa katika utekelezaji wa majukumu ya Wizara. Shukrani
za Tatu , ziende kwa watumishi wa
Wizara hii pamoja na taasisi na mashirika yake kwa bidii, uvumilivu na ubunifu
wao kikazi. Shukrani za Nne ziende
kwa Mashirika mbalimbali ya nje na ndani ya nchi kwa misaada na ushauri wao.
Aidha , ninapenda kutoa shukrani kwa Mheshimiwa Benedicto Mutachoka Mutungilehi, Mbunge wa Kyerwa (TLP) na Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu, kwa ushirikiano wake na mchango wake katika kuboresha hoja hii. Mwisho shukrani zetu ziwaendee waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Huduma za Jamii chini ya uongozi wa Mwenyekiti wao Mheshimiwa Omar Kwaang’w Mbunge wa Babati Mashariki (CCM) kwa uchambuzi na ushauri wao.
4.
Mheshimiwa
Spika, Elimu katika Ulimwengu wa sasa ni mojawapo ya
kigezo muhimu kwa ukuaji wa Uchumi endelevu na katika uboreshaji wa maisha ya binadamu. Tafiti nyingi
zilizokwisha fanyika zimedhihirisha kuwa mchango wa Elimu, hususan elimu ya juu
una uhusiano wa moja kwa moja na ukuaji wa Uchumi endelevu. Ni katika kutambua
hali hiyo, Wizara yangu inalenga katika kuhakikisha Taifa linakuwa na Jamii
iliyoelimika, yenye uwiano wa kijinsia na inayoweza kujiletea maendeleo kwa
kutumia Sayansi na Teknolojia.
5.
Mheshimiwa
Spika, katika hatua za kwanza za kuwa na mwelekeo thabiti
na pia kuwa na uwezo wa kupambana na ushindani unaotokana na utandawazi (
Globalization ), Wizara yangu imekamilisha maandalizi ya Mpango Kabambe (Master
plan) utakaoongoza ukuaji wa sekta za Sayansi na Teknolojia pamoja na elimu ya
juu na ufundi. Aidha, Wizara yangu
imekamilisha Utafiti (study) kuhusu
gharama ya kumwelimisha mwanafunzi (student unit cost) katika vyuo vya elimu ya
juu na ufundi kwa lengo la utoaji fedha katika vyuo kulingana na idadi ya
wahitimu wanaotarajiwa (outputs) badala ya utaratibu wa sasa wa utoaji fedha
kulingana na idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa (inputs). Aidha mfumo huu utahakikisha matumizi bora ya
rasilimali na ufanisi katika utoaji wa elimu ya juu na ufundi katika vyuo na
taasisi mbalimbali za Serikali na binafsi .
Mheshimiwa Spika,
baada ya utangulizi huu, napenda sasa kutoa maelezo yafuatayo katika mapitio ya
mwaka 2001/2002.
ELIMU YA JUU
6.
Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2001/2002 Wizara yangu
ilifanikiwa kutekeleza yafuatayo:
v Kuongeza
idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa katika vyuo vikuu vya umma toka wanafunzi
3,805 mwaka 2000/2001 hadi wanafunzi
4,755 mwaka 2001/2002.
v Kufanya
tathmini ya uchangiaji gharama za elimu
ya juu hususan awamu ya I na ya II, kwa lengo la kuiwezesha Serikali kuunda
bodi huru ya kuratibu utoaji na urejeshwaji wa mikopo.
v Kukamilisha
hatua za awali za utekelezaji wa mradi wa uhuishaji wa taasisi za elimu ya juu
kwa lengo la kuongeza udahili na ufanisi.
v Kuandaa
na kuratibu Warsha ili kubadilishana mawazo na mbinu juu ya kudhibiti
udanganyifu katika udahili, kwa kuwashirikisha wadau.
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
7.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam,
yafuatayo yametekelezwa:
v Kuboresha
njia za kufundishia na kujifunzia zikiwemo:
-
Matumizi ya mfumo wa “Semester” katika masomo ya
shahada ya kwanza
-
Utoaji wa mafunzo kwa kutumia mtandao wa tovuti
(Website)
-
Ufungaji mitambo ya “video – conferencing” katika
vyumba viwili vya mihadhara, vyenye
uwezo wa kuchukua jumla ya wanafunzi 500 kwa wakati mmoja.
v Kuanzisha
programu 13 mpya katika Kitivo cha Uhandisi zinazoendana na mahitaji ya soko.
Programu hizo ni,
-
Computer Engineering & Information Technology
-
Electro Power Engineering
-
Chemical and processing Engineering
-
Electro Mechanical Engineering
-
Mechanical Engineering
-
Mining Engineering
-
Mineral Processing Engineering
-
Civil and Structural Engineering
-
Telecommunication Engineering
-
Transportation Engineering
-
Production Engineering
-
Civil and Water Resources Engineering
-
Electrical
Engineering.
v Kuboresha
uwiano wa wanafunzi wa kike na kiume kupitia mafunzo maalum kwa wanafunzi wa
kike (Pre-Entry Training).
v Kutoa
huduma za ushauri wa kitaalam ikiwa ni hatua za makusudi za kuviunganisha vyuo
na wananchi.
v Kuboresha
na kupanua shughuli za utafiti. Mkazo
zaidi uliwekwa katika kuimarisha miundo mbinu ya utafiti ikiwemo
-
Kuimarishwa kwa Kurugenzi ya Utafiti na
Uchapishaji.
-
Kuanzishwa kwa kitengo cha Upashanaji Habari za
Taarifa za Utafiti.
CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE
8.
Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu cha Sokoine kimetekeleza yafuatayo:
v Kufanya
utafiti, ambapo baadhi ya tafiti zilizofanyika na zinazoendelea ni pamoja na:-
-
Mradi wa kufichua mabomu kwa kutumia panya-buku
unaendeshwa na SUA kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Antwerp ( Ubeligiji ).
-
Mradi wa Bustani na matunda unaoendeshwa katika
maeneo ya Mgeta, Mkuyuni na Kinole,
Mkoa wa Morogoro.
-
Mradi wa kutumia Mbuzi Chotara kuzalisha maziwa.
v Kuboresha
na kupanua miundo mbinu na vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Baadhi ya shughuli zilizofanyika ni:
-
Ukarabati wa majengo ikiwemo maktaba iliyopo
kampasi ya Solomon Mahlangu, na mabweni ( 8) ya wanafunzi yaliyopo kampasi kuu.
-
Ukamilishaji wa chanzo pekee cha maji.
-
Ununuzi wa nyumba 2 za ghorofa za iliyokuwa Benki
ya Taifa ya Biashara kwa ajili ya mabweni ya
wanafunzi wa Shahada ya Uzamili.
v Kuongeza
idadi ya wanafunzi wanaodahiliwa toka wanafunzi 774 mwaka 2000/2001 hadi
wanafunzi 788 mwaka 2001/2002.
v Kuboresha
shughuli za mafunzo, mkazo zaidi uliwekwa katika:
-
Kuimarisha kumbukumbu za wanafunzi kwa kufunga
programu maalum ijulikanayo kama CELCAT. Mfumo huu utawezesha kuzuia
udanganyifu katika udahili.
-
Kupitia upya mitaala yote ili iweze kukidhi
mahitaji ya “semester”.
-
Kurekebisha ratiba ya masomo ili kuongeza matumizi
ya vyumba vya madarasa na maabara (capacity utilization).
CHUO KIKUU HURIA
9.
Mheshimiwa Spika, Chuo Kikuu Huria kimetekeleza yafuatayo:
v Kufanya
ukarabati katika majengo ya makazi yake mapya, ambapo jumla ya Shs. 200 milioni
zimetumika.
v Kuanzisha
programu za Shahada ya Uzamili na Falsafa katika fani za Sayansi za Jamii,
Teknolojia na Elimu ya Mazingira, Sheria na Elimu.
v Kuendelea
kuimarisha vituo vyake mikoani ili viweze kutimiza majukumu yake vizuri.
v Kuchapisha
aina ya vitabu 112 kwa ajili ya kufundishia na kujifunzia.
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA SAYANSI NA TIBA MUHIMBILI
10.
Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi na Tiba cha
Muhimbili kimetekeleza yafuatayo:
v Kuendeleza ukarabati katika jengo la Kitivo cha Tiba ya
meno.
v Kuongeza
udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 232
mwaka 2000/2001 hadi wanafunzi
290 mwaka 2001/2002.
v Kuendelea
na shughuli za utafiti katika nyanja mbalimbali za Sayansi za Afya na Tiba.
v Kuimarisha
miundo mbinu ya mawasiliano ikiwemo mawasiliano ya mtandao wa tovuti.
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ARDHI NA USANIFU MAJENGO
11.
Mheshimiwa Spika, Chuo
Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu
Majengo kimetekeleza yafuatayo:
v Kuanzishwa
kwa kitengo maalum cha uendeshaji na usimamizi wa miradi “Programme Management
Unit”.
v Kuanzishwa
kwa kitengo cha kusimamia miradi ya ushauri wa kitaalam kijulikanacho kama
UCLAS Consultancy Unit (UCU)
v Kuendelea
na ujenzi wa jengo la Utawala ambalo linatarajia kugharimu jumla ya Sh
304,057,453. Asilimia 80 ya gharama za ujenzi huu zitatokana na Fedha
zitakazozalishwa na Chuo ambapo hadi sasa Chuo kimechangia jumla ya Sh.
71,166,868 katika ujenzi huu.
v Kuweka
uwiano mzuri baina ya idadi ya walimu na wafanyakazi wengine ili kupunguza
gharama za uendeshaji na kuongeza ufanisi.
Kazi hii imekamilika kwa kupunguza
wafanyakazi 118
v Kukamilika
kwa maandalizi ya kuanzisha masomo ya uzamili katika Mipango na Maendeleo ya
Miji.
v Kuendelea
kupitia mitaala kwa lengo la kuiboresha.
v Kuanzisha
Kitengo cha kutoa elimu ya kukabiliana
na Maafa.
BARAZA LA ITHIBATI LA ELIMU YA JUU
12.
Mheshimiwa
Spika, Baraza la Ithibati la Elimu ya Juu limetekeleza
yafuatayo:
v Kutoa
hati za usajili wa muda kwa vyuo vikuu vitatu ambavyo ni Chuo Kikuu cha Mzumbe,
Chuo Kikuu Kishiriki cha Waldorf na Chuo Kikuu cha Aga Khan Kampasi ya
Tanzania. Aidha, Baraza limekifuta Chuo Kikuu cha Lake – Mwanza kwa kushindwa
kutimiza masharti ya uanzishwaji wa Vyuo Vikuu.
v Kutoa
hati za usajili kamili kwa vyuo vikuu vitatu ambavyo ni Chuo Kikuu Kishiriki
cha Elimu Zanzibar, Chuo Kikuu cha Tumaini na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba
na Teknolojia.
v Kuratibu
kazi ya udahili wa wanafunzi katika vyuo vikuu na taasisi za elimu ya juu.
13.
Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Elimu ya Ufundi Wizara yangu
imetekeleza yafuatayo:
v Imekarabati
majengo, mitambo na vifaa mbali mbali katika karakana na maabara ya vyuo vya
Ufundi Arusha na Mbeya.
v Imetoa
mafunzo ya muda mrefu ndani na nje ya nchi kwa walimu wa vyuo vya Ufundi Arusha na Mbeya. Walimu watatu (3) kwa Kiwango cha Udaktari wa Falsafa (PhD), sita
(6) Shahada ya Pili (MSc), wanne (4) Diploma ya Uzamili na wawili (2)
Stashahada ya Juu ya Uhandisi (ADE). Walimu ( 6 ) wamehitimu masomo yao na
kurejea katika vituo vyao vya kazi. Aidha, walimu ( 9 ) bado wanaendelea na
masomo.
v Imeendelea
na programu ya kuwahamasisha wasichana ili waweze kujiunga na elimu ya ufundi.
v Imeweka
mashine na mitambo yenye thamani ya Shs. Million 87 kwa Chuo cha Ufundi Mbeya
katika juhudi za kukiimarisha ili kutoa mafunzo zaidi ya ngazi ya juu ya elimu
ya ufundi.
v Imeongeza
vitabu vya kiada na rejea kwa vyuo vya Ufundi vya Arusha na Mbeya.
v Imeanza
na kuendelea na ujenzi wa bweni la wanafunzi kwa Chuo cha Ufundi Mbeya lenye
uwezo wa nafasi 240 za malazi.
v Imekamilisha
mpango wa kuanzisha Stashahada ya juu ya uhandisi kwa Chuo cha Ufundi Mbeya.
v Imeajiri
walimu watano (5) wenye kiwango cha elimu ya Shahada ya Pili (MSc) kwa ajili ya
Chuo cha Ufundi Mbeya.
v Imetoa
mafunzo ya uongozi kwa wakuu wa Idara za taaluma (25) katika vyuo vya Ufundi
Arusha na Mbeya.
14.
Mheshimiwa
Spika, Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaa imetekeleza
yafuatayo:
v Imekarabati
majengo, vifaa vya karakana na maabara katika juhudi za kuboresha mazingira ya
utoaji elimu.
v Imewapatia
mafunzo walimu kumi na moja (11) kwa kiwango cha Udaktari wa Falsafa, (PhD),
sita (6) Shahada ya Uzamili (MSc), sita (6) Diploma ya Uzamili na wawili (2)
Stashahada ya Juu ya Uhandisi (ADE).
v Imewapatia
mafunzo ya uongozi wakuu wa Idara za Taaluma.
v Imeanzisha
maabara mpya na ya kisasa ya kompyuta ikiwa na kompyuta hamsini (50) za kuanzia
kwa msaada wa Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China.
v Imepata
mitambo na vifaa vya karakana kutoka kituo cha “High Precision Technology
Centre” (HPTC) ambacho kilikuwa chini ya Wizara ya Viwanda na Biashara.
15. Mheshimiwa
Spika, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi limetekeleza yafuatayo:
v Limetoa
usajili kamili kwa vyuo ishirini na mbili (22) vyenye uwezo wa kutoa mafunzo ya
elimu ya ufundi.
v Limeandaa
na kukamilisha jumla ya miongozo na
taratibu tano (5) za kuwezesha kutoa ithibati, kutayarisha na kukuza mitaala ya
ufundi, kudhibiti ubora wa mafunzo,
kufanya utafiti na ushauri wa kitaalamu na
kuendesha mitihani ya elimu ya ufundi.
v Limepata
ofisi za kudumu Katika Majengo ya kilichokuwa Kituo cha HPTC.
16. Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Sayansi na Teknolojia imetekeleza
yafuatayo:
v Iliendelea
na uhamasishaji wa wananchi kupitia vyombo mbali mbali vya habari kama vile
redio, televisheni na magazeti juu ya umuhimu wa utumiaji wa Sayansi na
Teknolojia katika maisha yao ya kila siku ambapo vipindi 56 vilitangazwa
kupitia Redio Tanzania Dar Es Salaam.
v Aidha,
Wizara ilifanya tathmini ya usikivu wa vipindi hivyo katika mikoa ya Shinyanga,
Morogoro, Dodoma, Mbeya, Mwanza na Kagera kwa lengo la uboreshwaji.
v Kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu na Utamaduni Wizara yangu ilifanya maandalizi
ya awali ya uundaji wa Kamati ya Kitaifa itakayoshughulikia uendelezaji wa
Elimu ya Sayansi nchini. Aidha, iliendelea kufanya mawasiliano na Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa juu ya uundaji upya wa Kamati za
Sayansi na Teknolojia katika ngazi za Mikoa na Wilaya.
v Imeshirikiana
na taasisi ya Maendeleo ya Utafiti na Viwanda Nchini (Tanzania Industrial
Research Organization – TIRDO) kufanya utafiti wa awali kuhusu usambazaji wa matokeo ya Utafiti katika
Mikoa ya Shinyanga, Tanga na Ruvuma.
Utafiti huo ni juu ya kuimarisha mfumo wa Maji na “Development and
Dissemination of Biomass stove for rural Shinyanga”, “Food preservation/processing Training Cum and Improving Water
System.
v Ilikukusanya
takwimu mbalimbali zinazohusu hali ya Sayansi na Teknolojia katika Mikoa 10
hapa nchini.Mikoa hiyo ni pamoja na
Kilimanjaro,Arusha,Mbeya,Iringa,Tanga,Dodoma,Morogoro,Shinyanga,Ruvuma, na
Mwanza.
v Kwa
kushirikiana na Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam, Idara ya Hisabati, Tume ya Taifa
ya Sayansi na Teknolojia pamoja na Shirika la Kimataifa lijulikanalo kama “ The
Third World Academy of Sciences” Wizara
yangu iliendesha Warsha ya Kimataifa ya hisabati, warsha iliyofanyika tarehe
19-21 Novemba 2001, mjini Arusha kwa lengo la kuelewa ukubalikaji wa hisabati
katika nchi za Kusini mwa Jangwa la Sahara.
v Aidha,
kwa kushirikiana na Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia nchini, Wizara yangu
iliandaa na kuendesha warsha ya kujadili mpango wa miaka mitano wa uendelezaji
wa sayansi ya msingi nchini, warsha iliyofanyika tarehe 13 – 14 Mei, 2002,
jijini Dar Es Salaam.kwa kuwashirikisha wadau.
v Ilitoa
Tuzo ya Sayansi kwa wasichana wanne waliofanya vizuri katika mitihani ya
kumaliza kidato cha nne mwaka 2001.Tuzo hiyo ilitolewa katika somo la Hisabati,
Kemia, Fizikia na Baiolojia, kwa lengo la kuhamasisha wanawake na wasichana
wengi kujiunga na fani ya Sayansi na Teknolojia.
v Kwa
kushirikiana na wataalamu katika fani ya Nishati ya Jua kutoka Chuo Kikuu cha
Dar Es Salaam, Kitivo cha Sayansi, Wizara yangu ilifanya tathmini ya awali ya
vijiji vitakavyonufaika na mradi wa matumizi ya Nishati ya Jua katika Wilaya ya
Maswa, mkoani Shinyanga. Aidha, mradi huu unagharimiwa na Serikali ya Jamhuri
ya Watu wa China.
v Wizara
imepokea maamuzi ya Baraza la Mawaziri kuhusu kufutwa kwa Sheria Na. 5 ya mwaka
1983 iliyounda Tume ya Taifa ya Mionzi na kuanzisha kutungwa kwa Sheria mpya
itakayounda Mamlaka ya nguvu za Atomiki nchini.
17. Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Tume ya Taifa ya Mionzi imetekeleza
yafuatayo:
v Tume
iliendelea na utoaji wa huduma ya upimaji mionzi kwa wafanyakazi 943 wanaotumia
mionzi katika vituo 95 kati ya vituo 125 vilivyopo nchini.
v Sampuli
2,143 za vyakula, mbolea na bidhaa nyingine zilipimwa.
v Ilikagua
vituo 135 vya X- ray ambapo vituo 11 vilifungiwa kutoa huduma hiyo kutokana na
kutokidhi viwango salama vilivyokubaliwa kimataifa katika huduma za uchunguzi
wa magonjwa mahospitalini.
v Ilitengeneza
mashine 15 za X-ray, na vifaa 18 vya electroniki.
v Ilihakiki
vifaa 31 vya kupimia mionzi ambapo vifaa 9 vilitoka nchini Kenya. Aidha,
ilivipatia vituo 6 vifaa vya kinga vya mionzi (Lead glass).
v Iliendelea
kutoa elimu ya kinga ya mionzi kwa kupitia njia za redio na televisheni
v Tume
iliendelea kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi minne inayogharimiwa na
na Shirika la Kimatifa la Nguvu za Atomiki (IAEA) ambapo taasisi husika
zilipewa zaidi ya dola za Kimarekani zipatazo 500,000 kwa ajili ya mafunzo,
ununuzi wa vifaa na ushauri wa kitaalamu.
v Ili
kuepusha athari zitokanazo na mabaki ya vyanzo vya mionzi, Tume iliweza
kukusanya mabaki hayo kutoka Taasisi ya Saratani ya Hospitali ya Ocean Road,
Kiwanda cha Bia Dar es Salaam, Ofisi za Ushuru wa Forodha zilizoko uwanja wa
ndege wa Dar es Salaam na shule ya Sekondari ya Shaaban Robert iliyoko jijini
Dar Es Salaam na kuyapeleka katika hifadhi ya muda iliyoko Arusha.
18. Mheshimiwa
Spika, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia imetekeleza
yafuatayo:
v Iliendelea
na ukamilishaji wa rasimu ya uanzishaji wa Masijala ya Taifa ya Takwimu za
Utafiti nchini ( The National Research Registry) kwa kuzingatia maoni toka kwa
wadau mbalimbali ambapo hadi hivi sasa Tume imesajili tafiti 353.
v Iliendesha
mafunzo ya wakufunzi kuhusu kilimo cha Uyoga katika kituo cha utafiti cha
Ukiruguru, Mwanza, ambapo washiriki 20 walihudhuria mafunzo hayo.
v Ilishiriki
katika utafiti wa miradi miwili ya nishati mbadala ya upepo kwa ajili ya
kuzalisha umeme kwa kushirikiana na Wizara ya Nishati na Madini, Tanzania
Technology Development Organization
(TATEDO) na Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.
v
Ilishirikiana
na wafadhili mbalimbali kutekeleza miradi ya Teknolojia ya mawasiliano kama:
(i) Teknolojia
ya mawasiliano kwa ajili ya Utawala bora katika Wilaya ya Kinondoni.
(ii)
Kuanzisha vituo vya mawasiliano katika kambi ya
wakimbizi ya Lukole wilayani Ngara, Lugoba wilayani Bagamoyo na Dakawa mkoani
Morogoro.
(iii)
Iliendesha mafunzo ya kompyuta kwa washiriki 308 na
imeunganisha mawasiliano ya kompyuta
katika vituo 14 jijini Dar es Salaam
v
Ilishirikiana na Wizara ya Maliasili na Utalii,
kufanya utafiti kuhusu kupungua kwa barafu katika mlima Kilimanjaro.
v Kwa
kushirikiana na Ofisi ya Makamu wa Rais, Tume iliendesha warsha tatu ili kupata
maoni yatakayopelekea kuundwa kwa Sera ya Baioteknolojia nchini.
v Ilianzisha
mradi wa utafiti wa tekinolojia asilia kwa lengo la kuweka kumbu kumbu za
Teknolojia hizo.
19. Mheshimiwa
Spika, Tume ya Taifa ya UNESCO imetekeleza yafuatayo:
v
Ilishirikisha
Taifa katika Kikao cha 31 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO kilichofanyika mjini
Paris, Ufaransa Oktoba/Novemba, 2001 ambacho kilipitisha mpango wa miaka 6
(2002 –2007) na programu ya kazi na bajeti ya miaka miwili (2002-2003). Katika
kikao hicho Tanzania ilichaguliwa kwa
mara nyingine tena kuwa mjumbe wa Bodi
ya Utendaji wa Shirika hilo kwa kipindi
cha miaka mine ijayo ( 2002-2005).
v
Serikali
imemteua Naibu Mwakilishi wa Kudumu wa Tanzania UNESCO Prof. Mohamed Sheya kuiwakilisha katika Bodi hiyo.
v
Aidha,
Tanzania ilichaguliwa kushiriki katika mabaraza matano ya kitaalam ambapo
wawakilishi wake wameteuliwa kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ikiwa ni
pamoja na Taasisi ya Mambo ya Bahari, Tume ya Sayansi na Teknolojia na Chuo cha
Usimamizi wa Fedha.
v Iliratibu
utekelezaji wa miradi ya mashirikiano na UNESCO kama ifuatavyo:-
- Kuipatia makazi
mapya Ofisi ya Kanda ya UNESCO inayosimamia shughuli zake hapa Tanzania,
Comoro, Shelisheli, Madagascar na Mauritius.
- Mradi wa Mawasiliano Vijijini huko
Sengerema mkoani Mwanza.
- Mradi wa kuimarisha Utawala bora kwa
kutumia Teknolojia ya
kisasa ya mawasiliano katika Manispaa ya Zanzibar.
- Mradi wa kuanzisha Maktaba ya Wilaya
ya Bagamoyo.
- Mradi wa hifadhi ya magofu ya Kilwa
Kisiwani na Songo Mnara kama sehemu
ya mradi wa tamaduni za Dunia.
- Mradi wa Uchunguzi/Utafiti wa kuanzisha kumbukumbu na makumbusho ya Msafara wa Biashara ya Utumwa.
v Kwa
kushirikiana na taasisi zingine Wizara yangu imetekeleza yafuatayo.
-
Mradi wa kuboresha utunzaji wa Nyaraka za Taifa.
v Mpango
wa kuimarisha Elimu kwa Wote (Education for All Programme). Mpango huu
unafuatilia utekelezaji wa maamuzi ya mkutano wa Elimu kwa wote uliofanyika
Jomtien, Thailand mwaka 1990 na ule uliofanyika Dakar Senegal , mwaka 2000.
Wizara ya Elimu na Utamaduni (Tanzania Bara ) na ile ya Elimu, Utamaduni na
Michezo (Zanzibar) zimetekeleza maamuzi ya mikutano hiyo. Tanzania ni miongoni
mwa nchi zitakazoshirikishwa katika Warsha za Waratibu zitakazofanyika Abijan,
Nigeria na Paris, Ufaransa.
v Maandalizi
ya Mkutano wa Wahisani wa Kuanzishwa kwa Kituo cha Kanda ya Mashariki na Kusini
mwa Afrika kitakachotoa mafunzo juu ya mwamko wa kutunza mashine, mitambo,
miundo mbinu (Culture of Maintenance) katika Taasisi ya Teknolojia Dar es
Salaam.
v Iliratibu
ushiriki wa watanzania katika baadhi ya
warsha, mikutano na “Scholarship” zilizoendeshwa na UNESCO kama
ifuatavyo:-
- Mkutano
wa Kimataifa wa Walimu uliofanyika Geneva, Uswisi Septemba 2001. Mada kuu ya
Mkutano ilikuwa ni Elimu kwa ajili ya kujifunza kuishi pamoja. Ujumbe wa
Serikali kwenye Mkutano huo uliongozwa na Waziri wa Elimu na Utamaduni Mh.
Joseph Mungai ( MB ).
- Warsha
za mafunzo kwa Wakufunzi wa matumizi ya Nishati ya Jua zilizofanyika Zimbabwe,
Oktoba 2001 na Mjini Bagamoyo, Januari 2002. Madhumuni ya Warsha hizo yalikuwa
ni kuhamasisha na kuwapatia wakufunzi wa vituo husika mbinu bora zaidi za
mafunzo kuhusu ufungaji wa mitambo, utunzaji wake na matumizi ya nishati ya
jua.
- Warsha
ya kuandaa mradi wa Uhifadhi wa Urithi Asilia wa Dunia nchini Tanzania
iliyofanyika Mjini Moshi mwezi Januari 2002. Warsha hii iliandaliwa kwa
kushirikiana na Shirika la Wanyama Pori (TANAPA) na Chuo Cha Wanyama Pori,
Mweka. Madhumuni ya Warsha hiyo ilikuwa kuandaa mradi ambao utaziwezesha
taasisi za Utafiti wa Wanyama Pori kupata vifaa, miundombinu na utaalam utakao
zisaidia kufanya Utafiti na kutoa mafunzo bora zaidi.
-
Warsha ya Uendelezaji wa Sehemu Kame Kusini mwa
Afrika iliyofanyika Botswana, Februari 2002. Washiriki walitoka Idara za
Mazingira Tanzania Bara na Visiwani. Azimio la Mkutano huo lilitaka kila
mshiriki kutafuta mbinu mwafaka za utekelezaji wa maamuzi kulingana na
mazingira ya nchi husika. Tanzania imeshawasilisha msimamo wake.
- Warsha
ya Elimu Endelevu iliyofanyika Kampala, Uganda, Aprili 2002. Serikali
iliwakilishwa kwenye Mkutano
huo na Wizara ya Elimu na Utamaduni (Tanzania Bara) na Wizara ya Elimu,
Utamaduni na Michezo(
Zanzibar ). Warsha iliandaa zana za utafiti wa kutathmini
ubora wa uelewa wa wanafunzi katika ngazi ya
Kidato cha Kwanza katika Masomo ya Hisabati, Fizikia,
Kemia na Baiolojia katika nchi zinazozungumza Kiingereza
Barani Afrika.
v Mafunzo chini ya programmu ya UNESCO kuhusu
uendelezaji wa fani ya mawasiliano. Katika kipindi kilichopita mfanyakazi mmoja
kutoka Kituo cha Televisheni cha ITV alipatiwa mafunzo nchini Korea Kusini.
20. Mheshimiwa
Spika, kwa upande wa Utawala na Utumishi Wizara yangu imetekeleza yafuatayo:
v Imewapandisha cheo
watumishi 80 wa kada mbalimbali.
v Imewapatia
mafunzo ya muda mrefu watumishi 6 na muda mfupi watumishi 37 ndani na nje ya
nchi.
v
Imeajiri
watumishi 11 kwa ajili ya kupunguza uhaba wa Wafanyakazi wa Wizara na kuratibu
upatikanaji wa vibali 51vya ajira za Wanataaluma Wageni kwa ajili ya Vyuo Vikuu
nchini.
v Imeendesha
Semina moja na Warsha moja kuwaelimisha Wafanyakazi na Wanafunzi wa Taasisi za
Elimu ya Juu kuhusu athari ya ugonjwa wa UKIMWI.
v Imekamilisha
uundaji wa Baraza la Wafanyakazi la
Wizara kwa lengo la kushirikisha wafanyakazi katika sehemu ya kazi. Baraza
lilizinduliwa rasmi tarehe 22 Machi, 2002.
v Imeendesha
Semina za maadili katika utumishi wa Umma kwa Watumishi wote wa Wizara Makao
Makuu kwa lengo la kuzielewa vyema Sheria na Kanuni za Utumishi wa Umma ili
Kuboresha utoaji huduma kwa Wananchi.
21. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2002/2003 Wizara yangu inatarajia kutekeleza
mambo yafuatayo:
ELIMU YA JUU
v Kuanzisha
chombo cha kusimamia utoaji na urejeshwaji wa mikopo ya wanafunzi.
v Kuimarisha
mfuko wa elimu ili uweze kutekeleza majukumu yake ipasavyo.
v Kuendelea
na utekelezaji wa mradi wa uhuishaji wa vyuo vya elimu ya juu.
v kuendelea
kuratibu udahili wa wanafunzi katika vyuo vya elimu ya juu.
v Kuwasilisha
Mswada wa Sheria ya Elimu ya Juu Bungeni.
CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM
22. Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kinatarajia kutekeleza mambo yafuatayo:
v Kuongeza
idadi ya wanafunzi wanaodhaminiwa na Serikali kutoka wanafunzi 2,246 wa mwaka
wa kwanza hadi 2,358 na kutoka
wanafunzi 600 hadi 650 wa Shahada za Uzamili.
v Kuanzisha
kitengo cha AUDIOVISUAL ili kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kupata elimu ya
juu kupitia mtandao wa kompyuta
v Kuendeleza
utafiti na kuimarisha kitengo cha kumbukumbu za utafiti na usambazaji wa
matokeo ya utafiti.
v Kujenga
jengo la kupumzikia wanafunzi na kufanya ukarabati wa majengo na viwanja vya
michezo.
v Kuendelea
kuimarisha na kuboresha uwiano kati ya wanafunzi wa kike na kiume kutoka
asilimia 26 hadi asilimia 30 ifikapo mwaka 2003/2004.
CHUO KIKUU CHA KILIMO CHA SOKOINE
23. Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine kinatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kufanya
tathmini ya mahitaji ya elimu kwa wakulima na kueneza matumizi ya stadi za
uongozi bora katika jamii ya wakulima.
v Kuendelea
kutekeleza mpango wa chuo na kukiwezesha kuongeza mapato yake.
v Kuendelea
kuimarisha mafunzo ya Shahada ya kwanza kwa kuanzisha Kozi nyingi zaidi
zinazokidhi mahitaji ya Soko na kuimarisha mafunzo ya vitendo.
v Kuongeza
udahili wa wanafunzi kutoka wanafunzi 788 hadi kufikia wanafunzi 842 wa mwaka
wa kwanza.
v Kuendeleza
shughuli za utafiti katika maeneo ya Kilimo, Misitu, Tiba na Sayansi ya
Wanyama.
CHUO KIKUU HURIA
24. Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu Huria kinakusudia kutekeleza
yafuatayo:
v Kuendelea
na shughuli za ukarabati wa majengo ya makao makuu ya chuo.
v Kuimarisha
mawasiliano baina ya mikoa na makao makuu., na kuendelea kuhamasisha wataalamu
mbalimbali kuandaa vitabu vya kiada kwa ajili ya wanafunzi wa chuo.
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA AFYA NA TIBA MUHIMBILI
25. Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba na Afya Muhimbili kimekusudia kutekeleza
yafuatayo:
v Kuongeza
nafasi za kulala wanafunzi kwa kununua majengo ya lililokuwa Shirika la Ukaguzi
wa Mahesabu la Taifa (TAC) huko Masaki.
v Kutoa
mafunzo kwa utaratibu wa ‘Semester’
v Kuongeza
udahili wa wanafunzi wa mwaka wa kwanza kutoka wanafunzi 290 hadi wanafunzi
300.
v Kupanua
na kuongeza idadi ya maabara na vifaa.
CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ARDHI NA USANIFU MAJENGO
26. Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu
Majengo kinatarajia kutekeleza
yafuatayo:
v Kuandaa
upya na kuboresha mitaala na mbinu za kufundishia Shahada za Uzamili.
v Kuendelaea
kuweka uwiano mzuri kati ya idadi ya wanafunzi wanawake na ile ya wanaume ili
kufikia kiwango cha asilimia 20 ya idadi ya wanawake kwa mwaka 2002/ 2003.
v Kuendelea
na shughuli za Ujenzi wa Jengo la Utawala.
v Kuimarisha
Kitengo cha Elimu Endelevu kwa kutoa mafunzo zaidi kuhusu kukabili majanga.
v Kuimarisha
kutumia mtandao wa teknolojia ya kisasa ya mawasiliano.
v Kupanua
jengo la Maktaba kwa msaada wa NORAD.
CHUO KIKUU CHA MZUMBE
27.
Mheshimiwa
Spika, Chuo Kikuu cha Mzumbe kinatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kukamilisha
muundo wa Utawala wa Chuo ambao utakuwa na,
-
Mkuu wa Chuo ( Chancellor )
-
Baraza la Chuo ambalo litakuwa na mamlaka ya mwisho
juu maamuzi ya Kisera, uendeshaji na Utawala wa Chuo.
-
Seneti, ambacho ni chombo cha juu cha ushauri juu
ya Sera za Kitaaluma na kitawajibika kwa Baraza.
-
Makamu Mkuu wa Chuo ambaye ndiye Mtendaji Mkuu wa
Chuo, ambaye atawajibika kwa Baraza la Chuo kwa masuala yote ya uratibu,
usimamizi na Utawala wa Chuo. Makamu Mkuu wa Chuo atasaidiwa na Naibu Makamu wa
Mkuu wa Chuo katika masuala ya taaluma na Mrajisi katika masuala ya Utawala na
fedha.
-
Bodi ya Kitivo / Taasisi / Kurugenzi ambayo
itawajibika kwa Seneti katika masuala ya Programu za Kitaaluma, kuboresha, kudhibiti
na kuoanisha shughuli zote za kitaaluma katika ngazi ya Kitivo/ Taasisi na
Kurugenzi.
-
Kamati za Idara ambazo zitakuwa ni chombo cha
msingi katika utaratibu wa kutoa maamuzi.
-
Kamati ndogo za Baraza la Chuo zitakazohusika na
maendeleo ya Wafanyakazi, fedha, maendeleo na mipango.
-
Chuo kinatarajia kuwa na Vitivo, Taasisi na
kurugenzi zifuatazo
Taasisi ya Elimu Endelevu.
Taasisi ya Taaluma za Maendeleo.
Kitivo Cha Sayansi za Jamii.
Kitivo cha Biashara.
Kitivo Cha Sayansi na Teknolojia.
Kitivo Cha Sheria.
Kurugezi ya Utafiti, Uchapishaji na masomo ya
Uzamili.
Kurugenzi ya Maktaba na Huduma za Kiufundi.
Kurugenzi ya Teknolojia, Habari na
Mawasiliano.
v Chuo
Kikuu cha Mzumbe kitakuwa na jumla ya wanafunzi 1,154 wanaoendelea na masomo na
wanafunzi 300 watakaodahiliwa kwa mwaka wa masomo 2002/2003.
v Chuo
kitaanza na jumla ya Wahadhiri 129, kati ya hao 24 ni wahadhiri wa kike na 105
ni wa kiume. Sifa za walimu hawa kitaaluma ni kama ifuatavyo.
-
Walimu wenye Shahada ya Udaktari wa Falsafa 15
-
Wanaosomea Shahada ya Udaktari wa Falsafa 19
-
Walimu wenye Shahada ya Uzamili 81
-
Wanaosomea Shahada ya Uzamili 5
-
Walimu wenye Shahada ya Kwanza 9
v Kuendesha
mafunzo ya muda mrefu kwa wanachuo 1,500 wa Vitivo vya Biashara, Sheria na
Sayansi za Kijamii.
v Kuendesha
kozi fupi 48 katika Taasisi ya Uongozi.
v Kuendesha
ushauri kwa wateja 12.
v Kufanya
tafiti tisa katika nyanja mbali mbali kwenye fani za Sayansi ya Kijamii.
v Kupanua
Kitengo cha Kompyuta ili kiweze kuhuisha matumizi ya Teknolojia ya mawasiliano
katika kufundisha na kujifunza.
BARAZA LA ITHIBATI LA ELIMU YA JUU
28.
Mheshimiwa Spika, Baraza
la Ithibati la Elimu ya Juu linatarajia kutekeleza
yafuatayo:
v Kutayarisha
mfumo wa vyeti vitakavyotolewa baada ya kuhitimu elimu ya juu.
v Kuwaendeleza
wafanyakazi kwa kuinua viwango vya elimu zao.
29.
Mheshimiwa Spika,
katika mwaka wa fedha 2002/2003 inakusudia kutekeleza
yafuatayo:-
v Kutoa
mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa walimu na watumishi wengine ndani na nje ya
nchi.
v Kukarabati
majengo, mitambo na vifaa mbalimbali katika vyuo vya Ufundi Arusha na Mbeya.
v Kutoa
mafunzo maalumu ili kuinua viwango vya taaluma ya wasichana kabla ya kujiunga
na elimu ya ufundi katika vyuo vya Ufundi Arusha na Mbeya.
v Kutoa
mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Uhandisi (ADE) kwa Chuo cha Ufundi Mbeya katika
hatua ya kukibadili kuwa Taasisi ya Teknolojia na hatimaye baadaye kukiwezesha
kutoa mafunzo ya ngazi ya Chuo Kikuu.
v Kununua
mashine na mitambo ya kufundishia kwa gharama ya jumla ya Shs. 150 Milioni kwa
ajili ya Chuo cha Ufundi Mbeya.
v Kuongeza
vitabu vya kiada na rejea katika fani za mitambo, umeme, magari, usanifu
majengo, ujenzi na masomo ya jumla kwa vyuo vya Ufundi Arusha na Mbeya.
30.
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka wa fedha 2002/2003 Taasisi inakusudia
kutekeleza yafuatayo:-
v Kuboresha
maktaba kwa kuongeza vitabu na nyenzo za kufundishia.
v Kukarabati
majengo, mitambo na vifaa mbali mbali katika karakana ya Taasisi.
v Kuwapa
mafunzo ya muda mrefu walimu na wafanyakazi wengine ndani na nje ya nchi.
v Kuandaa
mpango wa kutoa mafunzo ya uzamili kwa kozi mbali mbali zitolewazo katika
Taasisi.
v Kuandaa
mpango wa kutoa mafunzo ya Stashahada ya Juu ya Uhandisi kwa nyakati za jioni.
v Kuandaa
mtaala mpya wa kozi ya mafunzo ya kompyuta, kuanzisha maabara tatu za kompyuta,
kuboresha mawasiliano ya mtandao katika Taasisi kwa kushirikiana na Shirika la
Maendeleo la Sweden (Sida).
v Kuandaa
mtaala wa mafunzo ya Ufundi Sanifu (FTC) wa migodi na madini (“Mining &
Mineral Processing Engineering)”.
v Kuratibu
utekelezaji wa mpango wa kujenga utamaduni wa ukarabati “(Culture of
Maintenance and Maintenance Network)”.
31.
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka wa fedha 2002/2003 Baraza linakusudia kutekeleza yafuatayo:-
v
Kusajili vyuo arobaini (40) vyenye uwezo wa kutoa
mafunzo ya elimu ya ufundi.
v
Kutayarisha mitaala ya kufundishia masomo ya ufundi
kwa programu za masomo matano (5).
v
Kuratibu mitihani ya ufundi kwa ngazi ya Ufundi
Sanifu (FTC) na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (ADE).
v
Kuratibu mafunzo juu ya utayarishaji na ukuzaji wa
mitaala inayozingatia umahiri (‘competence based curricula)”.
32.
Mheshimiwa Spika,
Sayansi na Teknolojia inatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kuendelea
na maandalizi ya kuunda upya kamati za Sayansi na Teknolojia katika ngazi za
Mkoa na Wilaya na kuanza maandalizi ya kuweka Vituo vya Sayansi ( Science Parks
)
v Kuandaa Sera ya Utafiti wa sayansi na Teknolojia
nchini.
v Kutunga
Sheria Mpya itakayoipa Tume ya Taifa ya Mionzi uwezo na majukumu mapya.
v Kurejea
Sheria Na. 7 ya mwaka 1986 iliyounda Tume ya Sayansi na Teknolojia.
v Kukamilisha
uundaji wa Kamati ya Kitaifa ya Elimu ya Sayansi na Teknolojia nchini.
33.
Mheshimiwa Spika, Tume
ya Taifa ya Mionzi inatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kuendelea
na uimarishaji wa huduma za kinga za mionzi kwa watumiaji mionzi pamoja na
kuendelea na ukaguzi wa mionzi hiyo kwenye sampuli za vyakula na mazingira.
v Kuendelea
kuratibu na kusimamia matumizi ya Teknolojia za mionzi katika miradi inayofadhiliwa
na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki nchini.
v Kuendelea
na huduma za matengenezo ya vifaa vya elektroniki na mashine za X- ray
v Kukamilisha
mpango wa kushughulikia dharura za mionzi kitaifa (Radiological Emergency Plans
and Preparedness).
v Kujenga
Kituo cha kudumu cha kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi aionisha na isiyo
aionisha.
v Kutumia
vipimo vipya maalum kwa mfumo unaokubalika Kimataifa ( Basic Safety Standards )
34. Mheshimiwa
Spika, Tume ya Sayansi na Teknolojia inatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kukamilisha
Masijala ya Taifa ya Utafiti itakayojengwa COSTECH.
v Kufuatilia
utekelezaji wa miradi ya matumizi ya nishati mbadala kama vile makaa ya mawe,
mionzi ya jua, upepo na gesi ya samadi majumbani
v Kuandaa
Kongamano la wanasayansi na watafiti litakalofanyika sambamba na maonyesho ya
sayansi ya vijana kwa lengo la kujadili maendeleo ya sayansi nchini.
v Kuendelea
na upanuzi wa mtandao wa mawasiliano kwa njia ya kompyuta ili kuboresha
mawasiliano kati ya taasisi, asasi na
mtandao wa watafiti wa nchi za nje
35. Mheshimiwa Spika, Tume ya Taifa ya
UNESCO inatarajia kutekeleza yafuatayo:
v Kuratibu
utekelezaji wa maamuzi ya Kikao cha 31 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO kwa
kushirikiana na vyombo vya Serikali na Taasisi nyingine.
v Kuratibu
utekelezaji wa miradi itakayopata
ushirikiano wa UNESCO.
v Kuimarisha
Tume kimuundo na Ofisi za UNESCO kulingana na Mkataba kati ya Serikali na
Shirika hilo.
v Kwa
kushirikiana na Wizara ya Elimu na Utamaduni ( Bara ) na Wizara ya Elimu na
Michezo (Visiwani ), Tume itaratibu
maandalizi ya Mkutano wa nane wa Mawaziri wa Elimu Barani Afrika ( MINEDAF VIII
) utakaofanyika nchini tarehe 2 – 6 Desemba 2002. Mkutano huu utatanguliwa na
Kikao cha Waheshimiwa Wabunge wenye taaluma ya elimu Barani Afrika tarehe 28
Novemba 2002
v Kushiriki
mkutano wa Wahisani kwa ajili ya kuchangisha fedha za kugharamia mradi wa kutoa
mafunzo ya utamaduni wa ukarabati wa vifaa/miundo mbinu katika Taasisi ya
Teknolojia Dar es Salaam. Mkutano huu
unatarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka 2002.
v Kuimarisha
mpango wa Klabu za UNESCO na mtandao wa shule za kushirikishwa katika mipango
ya UNESCO, kwa lengo la kuimarisha utamaduni wa amani.
36. Mheshimiwa
Spika, Utawala na Utumishi inatarajia kutekeleza
yafuatayo.
v Itaendelea
kushirikiana na Mamlaka husika ili kupata kibali cha kuajiri Wanataaluma,
Walimu na Watumishi wengine kwa lengo la kupunguza uhaba wa wafanyakazi
katikaVyuo, Taasisi za Wizara pamoja na Wizara yenyewe.
v Itaendelea
kuendesha Semina na Warsha za kuelimisha Wafanyakazi na Wanafunzi wa Taasisi za
Elimu ya Juu na Ufundi kuhusu athari za ugonjwa hatari wa Ukimwi.
v Kuwapandisha
cheo watumishi 60 wa kada mbalimbali ambao wametimiza masharti ya kupanda
daraja.
v Kudhamini
watumishi 40 mafunzo ya muda mfupi na watumishi 12 kwa mafunzo ya muda mrefu.
v Kuendelea
kuendesha Semina za maadili Wizarani
kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwa wananchi.
MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA 2002/2003
37. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu itatoa
kipaumbele katika maeneo yafuatayo:
v Kuratibu
uanzishwaji wa chombo cha kutoa na kurejesha mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya
Juu.
v Kuimarisha
Chuo cha Ufundi Mbeya ili kiweze kutoa mafunzo ya Stashahada ya Elimu ya
Ufundi, kwa lengo la kufikia hadhi ya Chuo Kikuu.
v Kuendelea
kupitia upya mitaala ili mafunzo yatolewayo yaweze kukidhi mahitaji ya soko
huria na utandawazi.Mkazo zaidi utawekwa katika kujenga uwezo wa vyuo ili
viweze kutoa wataalamu watakaoweza kujiariri wenyewe badala ya kutegemea
kuajiriwa.
v Kuendelea
kuongeza idadi ya wanafunzi katika vyuo vikuu na vya ufundi kwa kutumia njia
mbalimbali.
v Kuendelea
kuweka uwiano mzuri kati ya idadi ya wanafunzi wa Kike na Kiume katika vyuo vya
elimu ya juu na Ufundi.
v Kuratibu
na kuhakiki uanzishwaji wa vyuo bora vya elimu ya juu na ufundi, kuvikagua ,
kuvisajili na kuvipa ithibati.
v Kuendelea
kuhamasisha matumizi ya Sayansi na Teknolojia.
v Kuendelea
kuhamasisha wananchi kuhusu dhana ya uchangiaji, uendelezaji na uwekezaji
katika Elimu ya Juu na Ufundi, kama vile uanzishaji mifuko ya hiari ya
Skolashipu, ujenzi wa miundombinu ya Elimu ya Juu, Ufundi, Sayansi na Utafiti.
v Kuboresha
mazingira ya kazi ikiwa ni pamoja na uendelezaji wanataaluma, kuimarisha miundo
mbinu ya vyuo.
v Kushiriki
katika shughuli za Tume ya Taifa ya UNESCO.
v Kuendelea
kuhamasisha wanafunzi na wafanyakazi madhara ya ugonjwa hatari wa UKIMWI.
v Kuendeleza
juhudi za kupambana na rushwa katika Wizara na Taasisi zake.
v Kufuatilia
utekelezaji wa miradi ya nishati mbadala
v Kuendelea
na upanuzi wa mtandao wa mawasiliano kwa njia ya Kompyuta ili kuboresha
mawasiliano kati ya taasisi na mtandao wa watafiti wa nchi za nje.
v Kuimarisha
shughuli za utafiti ili ziweze kutatua kero za wananchi Mkazo zaidi utakuwa
kuimarisha mbinu za usambazaji wa matokeo ya utafiti kwa sekta za viwanda na
wananchi kwa ujumla.
v Kuandaa
Takwimu sahihi za nguvu kazi kwa lengo la kuainisha maeneo yanayopaswa kupewa
kipaumbele katika mafunzo
v Kusimamia
utekelezaji wa mradi wa uhuishaji wa vyuo vya elimu ya juu nchini.
v Kuimarisha
utekelezaji wa Sheria ya Mfuko wa
Elimu.
v Kuanza
maandalizi ya kuanzisha Vituo vya Sayansi (Science Parks) Mikoani.
v Kuanzisha
Sheria Mama ya Elimu ya Juu na Sheria Mpya ya kukigeuza Chuo Kikuu Kishiriki
cha Sayansi na Tiba Muhimbili kuwa Chuo Kikuu kamili.
v Kuanzisha
Sheria ya kuunda Mamlaka ya nguvu za Atomiki.
MWISHO
38. Mheshimiwa
Spika, mwisho ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wahisani na
washikadau mbalimbali kwa mchango wao mkubwa katika Wizara yangu. Ni wazi kuwa msaada walioutoa na
wanaoendelea kutoa hususan katika kuboresha Sayansi na Teknolojia, elimu ya juu
na ya ufundi katika vyuo na taasisi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia pale
ambapo Serikali imekuwa ikishindwa kutokana na ufinyu wa bajeti. Nchi hizo ni pamoja na Sweden, Norway,
Uholanzi, Japan, Ubeligiji, Korea, China, Benki ya Dunia na Umoja wa Mataifa.
Aidha,Mashirika mengine ni pamoja na, Common Wealth Science Council,
International Atomic Energy Agency, Third World Academy of Sciences, International
Foundation for Sciences na Shirika la Kimaendeleo la Sweden. Naomba waendelee
na moyo huo nasi tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kikamilifu.
39.
Mheshimiwa Spika,
ili kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza mipango
iliyojiwekea katika mwaka wa fedha 2002/2003 sasa naliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Sh.70,226,556,600.00
Kati ya fedha hizo, Sh
59,090,803,800.00. ni kwa ajili
ya matumizi ya kawaida na Sh
11,135,752,800.00 ni kwa matumizi
ya maendeleo.
40. Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa hoja.
KIAMBATISHO NA. 1: FEDHA ZINAZOOMBWA KWA MATUMIZI YA KAWAIDA
FUNGU 68 MWAKA 2002/2003
|
KIFUNGU |
IDARA |
FEDHA ZILIZOIDHINISHWA MWAKA 2001/2002 |
FEDHA ZINAOOMBWA MWAKA 2002/2003 |
|
1001 |
UTAWALA |
881,677,900 |
939,971,300 |
|
1002 |
UHASIBU |
67,162,000 |
71,856,900 |
|
1003 |
SERA NA MIPANGO |
108,593,100 |
311,390,200 |
|
2001 |
TUME YA UNESCO |
243,206,700 |
251,718,800 |
|
3001 |
ELIMU YA JUU |
45,201,171,000 |
51,012,100,100 |
|
3002 |
ELIMU YA UFUNDI |
4,877,417,700 |
5,027,600,600 |
|
3003 |
SAYANSI NA TEKNOLOJIA |
1,338,657,000 |
1,476,165,900 |
JUMLA |
52,717,885,400 |
59,090,803,800 |
|
FEDHA ZINAZOOMBWA KWA MATUMIZI YA MAENDELEO
FUNGU 68 MWAKA 2002/2003
|
KIFUNGU |
IDARA |
FEDHA ZILIZOIDHINISHWA MWAKA 2001/2002 |
FEDHA ZINAZOOMBWA 2002/2003 |
||
|
FEDHA ZA TANZANIA |
FEDHA ZA NJE |
FEDHA ZA TANZANIA |
FEDHA ZA NJE |
||
|
1003 |
SERA NA MIPANGO |
100,000,000 |
1,215,000,000 |
122,436,300 |
1,200,000,000 |
|
3001 |
ELIMU YA JUU |
1,230,000,000 |
1,164,000,000 |
1,750,000,000 |
7,743,316,500 |
|
3002 |
ELIMU YA UFUNDI |
350,000,000 |
- |
200,000,000 |
- |
|
3003 |
SAYANSI NA TEKNOLOJIA |
140,000,000 |
- |
120,000,000 |
- |
JUMLA |
1,820,000,000 |
2,379,000,000 |
2,192,436,300 |
8,943,316,500 |
|
KIAMBATISHO
NA. 3
MAOMBI YA FEDHA
FUNGU: 68
|
KIFUNGU |
IDARA |
FEDHA
ZILIZOIDHINISHWA 2001/2002
|
FEDHA ZINAZOOMBWA 2002/2003 |
||||||
|
FEDHA ZA KAWAIDA |
FEDHA ZA MAENDELEO |
JUMLA KUU |
FEDHA ZA KAWAIDA |
FEDHA ZA MAENDELEO |
JUMLA
KUU |
||||
|
FEDHA ZA TZ |
FEDHA ZA NJE |
FEDHA ZA TZ |
FEDHA ZA NJE |
||||||
|
1001 |
Utawala |
881,677,900 |
-- |
-- |
881,677,900 |
939,971,300 |
-- |
-- |
939,971,300 |
|
1002 |
Uhasibu |
67,162,000 |
-- |
-- |
67,162,000 |
71,856,900 |
-- |
-- |
71,856,900 |
|
1003 |
Sera na Mipango |
108,593,100 |
100,000,000 |
1,215,000,000 |
1,423,593,100 |
311,390,200 |
122,436,300 |
1,200,000,000 |
1,633,826,500 |
|
2001 |
Tume ya UNESCO |
243,206,700 |
-- |
-- |
243,206,700 |
251,718,800 |
-- |
-- |
251,718,800 |
|
3001 |
Elimu ya Juu |
45,201,171,000 |
1,230,000,000 |
1,164,000,000 |
47,595,171,000 |
51,012,100,100 |
1,750,000,000 |
7,743,316,500 |
60,505,416,600 |
|
3002 |
Elimu ya Ufundi |
4,877,417,700 |
350,000,000 |
-- |
5,227,417,700 |
5,027,600,600 |
200,000,000 |
-- |
5,227,600,600 |
|
3003 |
Sayansi &
Teknolojia |
1,338,657,000 |
140,000,000 |
-- |
1,478,657,000 |
1,476,165,900 |
120,000,000 |
-- |
1,596,165,900 |
|
JUMLA
YA MAOMBI FUNGU 68 |
52,717,885,400 |
1,820,000,000 |
2,379,000,000 |
56,916,885,400 |
59,090,803,800 |
2,192,436,300 |
8,943,316,500 |
70,226,556,600 |
|
|
4,199,000,000 |
11,135,752,800 |
||||||||