HOTUBA
YA WAZIRI WA AFYA MHESHIMIWA ANNA MARGARETH ABDALLAH, MBUNGE, KUHUSU MAKADIRIO
YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2002/2003
1. Mheshimiwa Spika,
kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya
Kisekta inayohusu Wizara yangu, naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge likubali
kupitisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Afya kwa mwaka wa fedha wa
2002/2003.
2. Mheshimiwa Spika,
naomba nianze hotuba yangu kwa kutoa pongezi nyingi kwa Mheshimiwa Rais
Benjamin William Mkapa, kwa kusimamia vizuri na kwa ushupavu mkubwa, hatua
mbalimbali zilizowezesha vyama vya CCM na CUF kufikia muafaka. Mfarakano mkubwa
baina ya vyama hivyo, uliojitokeza baada ya uchaguzi wa mwezi Oktoba 2000,
ulikuwa ni tishio kwa amani na mustakabali wa taifa letu. Hivyo Watanzania wote
tuna kila sababu ya kujivunia makubaliano ya muafaka kati ya CCM na CUF.
3. Mheshimiwa Spika,
napenda kuchukua nafasi hii pia kuwapongeza kwa dhati wale wote ambao katika
kipindi cha kuanzia mwezi Agosti 2001 hadi leo wameteuliwa kushika nafasi
mbalimbali za uongozi wa juu wa taifa letu. Hao ni Mheshimiwa Dr. Ali Mohamed
Shein, aliyeteuliwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano ya Tanzania,
Mheshimiwa Dk. Juma Ngasongwa, Mb. Waziri wa Biashara na Viwanda na Mheshimiwa
Ritha Mlaki, Mb. Naibu Waziri wa Biashara na Viwanda. Hali kadhalika
nawapongeza Mheshimiwa Masumbuko Lamwai
na Mheshimiwa Hamad Rashid Mohamed, kwa kuteuliwa kwao na Mheshimiwa Rais kuwa
wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano la Tanzania.
4. Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha mwaka 2001/2002, Bunge lako Tukufu limewapoteza Wabunge
wafuatao; Mhe. John Mangwangwa - Mbunge wa Mpanda Kati na Mhe. Sebastian
Kinyondo - Mbunge wa Bukoba Vijijini. Mwenyezi Mungu aziweke roho zao mahali
pema peponi. Amin. Hali kadhalika
katika kipindi hiki taifa lilipata majanga makuu mbalimbali; ajali mbaya ya
gari moshi (treni) iliyotokea tarehe 24/6/02 kati ya vituo vya reli vya Igandu
na Msagani ambapo Watanzania zaidi ya 286 walipoteza maisha na wengine zaidi
800 walijeruhiwa. Pia ajali mbaya ya
basi lililopinduka katika barabara ya Iringa ambapo watu takribani 38
walipoteza maisha, ajali ya basi katika barabara ya Songea Makambako
iliyosababisha vifo vya watu 37, ajali
ya kuzama kwa kivuko cha mto Kilombero ambapo inahofiwa kuwa watu zaidi ya 30
walipoteza maisha yao, ajali ya wanamichezo iliyotokea huko Kikatiti - Arusha
ambapo watu kumi walipoteza maisha na ajali iliyotokea katika machimbo ya
madini huko Mererani ambapo inakadiriwa kuwa watu 40 wamepoteza maisha yao.
Tunamwomba Mwenyezi Mungu aziweke mahali pema peponi roho za marehemu wote.
Natoa pole nyingi kwa familia, ndugu, jamaa na marafiki wa marehemu hao.
Kwa niaba ya serikali na kwa niaba yangu mwenyewe natoa shukrani za dhati kwa wale wote walioshiriki katika uokoaji wa majeruhi, uopoaji na uhifadhi wa maiti katika ajali zote zilizotokea hapa nchini. Hatua makini na za haraka katika ajali zinasaidia sana kuponya maisha. Napenda kuchukua nafasi hii kuwapongeza waganga na wauguzi katika hospitali zote zinazopokea majeruhi wa ajali kwa kufanya kazi nzuri sana, pia wapiganaji wa Majeshi yetu yote ya Ulinzi na Usalama, pamoja na wananchi ambao walijitokeza kuwaokoa majeruhi, na kuwasitiri marehemu, pia waliojitolea damu, chakula, maji, mavazi na dawa kwa waliopatwa na ajali. Nawashukuru wote kwa niaba ya Serikali kwa upendo mkubwa waliouonyesha kwa wenzetu waliofikwa na majanga haya.
5. Mheshimiwa Spika,
niruhusu nitoe shukrani zangu kwa Kamati ya Kisekta ya Huduma za Jamii ya Bunge
lako Tukufu chini ya uenyekiti wake Mheshimiwa
Omar S. Kwaang, Mbunge wa Babati Mashariki kwa maelekezo yao na kwa
ushauri mbali mbali walioutoa ambao ulisadia sana kukamilisha bajeti ya Wizara
ya Afya. Ushauri na maelekezo ya Kamati
hii yamekuwa dira muhimu iliyowezesha kutoa mwelekeo sahihi.
6. Mheshimiwa Spika,
Mfuko wa Bima ya Afya ni jambo lililozua mjadala miongoni mwa watumishi na
vyombo vya habari kuanzia makato yalipoanza kufanyika katika mishahara ya
watumishi wa Serikali mwezi Julai 2001, kwa mujibu wa Sheria Na.8 ya mwaka
1999. Wako walioshangilia kuwa Mfuko ni hatua muhimu ya kimaendeleo na wale
walioona kuwa haiwasaidii kuwemo katika utaratibu huu. Kwa sehemu kubwa hali hii ilisababishwa na
matatizo makuu mawili. Tatizo la kwanza lilikuwa ni kukosekana kwa elimu ya
kutosha miongoni mwa wadau juu ya dhana, umuhimu na madhumuni ya Bima na la
pili ni kutokamilishwa kwa usajili wa hospitali, vituo vya afya na zahanati za
kutoa huduma kwa wanachama. Mapungufu haya sasa yamerekebishwa. Hadi kufikia
mwishoni mwa mwezi Mei 2002 watendaji wakuu wa Mfuko wa Bima ya Afya walikuwa
wametembelea mikoa yote kutoa ufafanuzi wa kina kuhusu Bima na wamechukua hatua
madhubuti kukamilisha usajili wa hospitali, na vituo vya matibabu vyenye sifa
ya kutoa huduma kwa wanachama wa Mfuko. Baada ya kufanikisha hatua hizo
watumishi wa Serikali wameanza kutambua manufaa makubwa ya Mfuko ambayo ni
pamoja na:
·
Familia kupata huduma bora za matibabu bila kuzilipia papo kwa papo.
·
Serikali kuchangia asilimia tatu ya mshahara wa mtumishi kila mwezi kwa
matibabu ya kila mwanachama na familia yake ya watu wasiozidi 6.
·
Huduma za vituo vya matibabu kuimarika kutokana na malipo ya Bima baada
ya kuwahudumia wanachama.
Wizara ya Afya inapenda kurudia wito wake
kwa viongozi wa sehemu za kazi, wanachama na vyama huru vya wafanyakazi kuwa
Bima ya Afya kwa hakika ni ukombozi kwa watumishi wa Serikali.
7. Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi cha mwaka wa fedha 2001/2002 viongozi wa Wizara ya Afya
wameendeleza kwa nguvu vita dhidi ya rushwa katika vituo vya kutolea huduma za
matibabu na sehemu nyingine za kazi. Hatua muhimu zilizochukuliwa ni pamoja na:
·
Kuwaagiza wakuu wa sehemu za kazi wasimamie kikamilifu watumishi kuvaa
vitambulisho wakati wote wawapo kazini.
·
Kuendelea kuwakumbusha wananchi kupitia vyombo vya habari kuhusu haki
zao na jinsi haki hizo zinavyoweza kuathirika kutokana na kutoa au kupokea
rushwa.
·
Kuendelea kuwakumbusha wataalam
na watumishi wengine wa afya, kwa njia za mikutano, mabango na vipeperushi,
kuwa kudai rushwa ni tabia mbaya ya mtu binafsi na kamwe haihusiani na udogo wa
mishahara au upungufu wa vitendea kazi. Walikumbushwa pia kwamba Serikali haitasita kutoa adhabu kali kwa
yeyote atakayedhihirika kuvunja maadili kwa njia hiyo.
Ni matumaini yetu kwamba juhudi hizi
zikiendelezwa bila kupunguza msisitizo au kasi yake wananchi wataanza kuona mabadiliko
katika sekta hii nyeti hivi karibuni.
8. Mheshimiwa Spika,
ugonjwa wa malaria umeendelea kuwa tishio kwa maisha. Ningependa kurudia
kuwakumbusha wananchi na Bunge lako Tukufu kuwa inakadiriwa Watanzania takribani 100,000 hupoteza maisha kila
mwaka kutokana na ugonjwa wa malaria. Hali kadhalika, takwimu zinaonyesha kuwa
malaria inaongoza kwa wagonjwa wa kulazwa, katika vituo vya matibabu ikiwa ni
asilimia 54 kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano na asilimia 35 kwa watu
wazima. Kinachosikitisha ni kuwa ugonjwa huu unaweza kuzuilika iwapo mambo
muhimu yafuatayo yatazingatiwa:
·
Kila kaya itasafisha maeneo ya makazi yake na kufukia au kuondoa
maji yaliyotuama katika mifereji na
karo.
·
Kila familia itatumia vyandarua vilivyotiwa dawa ya kuua mbu.
·
Kila Jiji, mji na manispaa itahakikisha kuwa nyumba zinajengwa
kulingana na mpango uliotayarishwa ili kuepuka misongamano ya nyumba
zisizofikika kwa huduma (squatter homes) na pia inakarabati
mifereji yote ya maji taka.
Serikali kwa
upande wake inaendelea kuchukua hatua madhubuti zikiwa ni pamoja na
kuukamilisha Mpango Kamambe wa Udhibiti wa Malaria ambao utaanza kutekelezwa
mwaka 2002/03, kuondoa kodi katika vyandarua na kutoa elimu ya afya kwa
wananchi juu ya kutambua dalili za malaria na tiba sahihi.
9. Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha mwaka 2001/2002 Wizara ya Afya ilitengewa kiasi cha shilingi bilioni 40.505 kwa ajili ya
utekelezaji wa miradi ya maendeleo katika sekta ya afya. Kati ya fedha hiyo, jumla ya shilingi bilioni 3.245 ilitolewa na Serikali ya Tanzania shilingi bilioni 37.260 ilitoka Mfuko wa Pamoja (Health Basket Fund)
unaochangiwa na wahisani kutoka nchi marafiki.
Fedha hiyo ilitumika kutekeleza miradi ifuatayo:-
·
Kuimarisha uendeshaji wa upangaji mipango katika Sekta ya Afya.
·
Programu ya Kuimarishaa Afya (HSPS II).
·
Kuimarisha Hospitali za Taifa.
·
Kuimarisha Huduma za X-ray.
·
Ukarabati wa vyuo 17 vya afya.
·
Ukarabati na Ujenzi wa Hospitali za Muhimbili, Taasisi ya Mifupa (MOI)
na Taasisi ya Saratani (Ocean Road Cancer Institute).
·
Ukarabati wa Majengo ya Mkemia Mkuu wa Serikali.
·
Udhibiti wa Magonjwa ya Kumabukiza.
·
Ukarabati wa majengo yaTaasisi ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu.
·
Mpango wa Maendeleo wa Kisekta (HSDP).
·
Ukarabati wa majengo ya Taasisi ya Chakula na Lishe.
·
Ukarabati wa majengo ya Tume ya Udhibiti wa Vyakula (TUKUTA).
·
Kuimarisha utendaji katika vyuo vya afya.
Udhibiti wa Magonjwa ya
Kuambukiza (Epidemiologia).
10. Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha 2001/2002 tatizo la magonjwa ya milipuko limeendelea kuwepo
ingawaje takwimu zimeonyesha unafuu wa kiasi, kwa mfano, kwa upande wa ugonjwa
wa kipindupindu mwaka 2000/2001 wagonjwa walikuwa 4,637 ikilinganishwa na mwaka
2001/2002 ambapo wagonjwa walikuwa 2,154.
Hii inaonyesha nafuu ya takribani asilimia 53.5. Hali kadhalika, kwa upande wa vifo
vilivyotokana na kipindupindu, mwaka juzi kulikuwa na vifo 153 wakati mwaka
jana vifo vilikuwa 87, ambayo ni nafuu ya karibu asilimia 43. Hata hivyo Wizara inarudia kusisitiza kuwa
juhudi kubwa zinahitajika ili kutokomeza tatizo la milipuko ya magonjwa.
11. Mheshimiwa Spika, kuhusu
ugonjwa wa tauni bado milipuko imeendelea kutokea wilayani Lushoto. Katika kipindi cha mwaka 2001/2002 jumla ya
watu 21 waliugua ugonjwa huu na kati yao 5 walifariki dunia. Uchunguzi wa
kitaalam uliofanyika umeonyesha kuwa mlipuko uliotokea 2001/2002 uliwaathiri
zaidi watoto wa umri kati ya miaka mitano hadi kumi. Hii inaonyesha kuwa juhudi za ziada zinahitajika kukabili tatizo
hilo.
12.Mheshimiwa Spika, Wizara
ya Afya imeendelea
kuchukua tahadhari
kuhakikisha kuwa ugonjwa wa Ebola, ulioathiri nchi jirani, hauingii hapa
kwetu. Vituo vyote vya mipakani
vilihimizwa kufuatilia magonjwa yote ya kuambukiza kama tahadhari ya kuzuia
kuzuka kwa ugonjwa wa Ebola. Hali
kadhalika Elimu ya Afya juu ya kinga ya kuenea magonjwa ya milipuko ilipewa
umuhimu mkubwa katika maeneo ya mpakani.
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti
Malaria
13.Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekuwa
ikifanya jitihada mbalimbali dhidi ya ugonjwa wa malaria ambao bado ni tishio kubwa kwa afya na maisha ya Watanzania. Katika kipindi cha mwaka 2001/2002, Wizara ya Afya ilitekeleza majukumu yafuatayo:-.
·
Tiba sahihi kwa
Wagonjwa wa Malaria
Kuanzia mwezi
Agosti 2001 Wizara ilianza utekelezaji wa Mwongozo mpya wa matibabu ya ugonjwa
wa Malaria. Katika mwongozo huu mpya,
dawa ya Sulphadoxine – Pyrimethamine (SP) ilianza kutumika
rasmi kama dawa ya safu ya kwanza ya kutibu malaria badala ya dawa ya Klorokwini. Kwa takribani mwaka mmoja sasa tangu dawa
hii ianze kutumika kwa wingi, kulingana na taarifa tunazopokea kutoka kwa watoa
huduma na wagonjwa, kuwa dawa hii imeonyesha kuwadhuru baadhi ya wagonjwa.
Wagonjwa hao ni wale wanaodhurika na kemikali ya sulphur ambayo ipo katika dawa
hiyo. Wizara inafanya uchunguzi wa kiwango cha madhara hayo iwapo yapo katika
kiwango cha kawaida cha madhara yanayotokana na matumizi ya dawa za aina
nyingine. Iwapo itathibitika kuwa kiwango hicho ni kikubwa kuliko ilivyo kwa dawa
nyinginezo, Wizara itachukua uamuzi wa kuibadilisha dawa hiyo. Aidha matumizi ya dawa hii yamewasaidia
wagonjwa wa malaria kupona mapema kuliko hapo awali wakati dawa ya Klorokwini
ilipokuwa ikitumika.
·
Mafunzo
Katika kipindi
hicho, Wizara yangu imetoa mafunzo ya rejea kwa Waganga, Wauguzi na Mafundi
Sanifu Maabara kuhusu tiba sahihi ya malaria.
Jumla ya Watumishi wa Afya 176 kutoka Wilaya zote nchini walipata
mafunzo hayo. Watumishi hawa wanategemewa kuwa walimu wa kuwafundisha wataalam
wengine wanaotoka katika wilaya zao.
14.Mheshimiwa Spika,
pamoja na kuongezeka kwa
ufanisi wa utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu bado idadi ya
wagonjwa inaendelea kuongezeka kutoka wagonjwa 54,000 mwaka 2000 hadi kufikia
wagonjwa 60,000 mwaka 2001. Hili ni
ongezeko la karibu asilimia 10. Hii
inaashiria kwamba bado kuna idadi kubwa ya wagonjwa wa Kifua Kikuu katika
jamii. Kwa upande mwingine ongezeko hilo lina uhusiano mkubwa na kuenea kwa
ugonjwa wa UKIMWI.
15.Mheshimiwa Spika,
katika kikao cha
Bunge la
bajeti mwaka 2001/2002, Wizara ya Afya iliahidi
kutekeleza mpango maalum wa kudhibiti Kifua Kikuu hususan katika miji mikubwa
ikiwemo Dar es salaam, Mwanza na Mbeya. Katika jiji la Dar es salaam, vituo vipya 7
vya kuchunguza wagonjwa wa Kifua Kikuu vimefunguliwa na hivyo kuongeza uwezo wa
jiji wa kuchunguza wagonjwa wa Kifua Kikuu na kupunguza msongamano wa wagonjwa. Kwa upande wa Mwanza tayari jiji hilo limeshagawanywa
katika sehemu tatu na waratibu wapya wawili waliteuliwa kudhibiti Kifua Kikuu
na Ukoma na tayari wameshaanza kazi.
Tathimini ya kuongeza vituo vipya vitakavyotoa huduma ya kudhibiti Kifua
Kikuu imefanyika. Mategemeo ni kuongeza angalau vituo vipya vinane. Hii itaongeza uwezo wa serikali wa kutoa
huduma hii muhimu na hivyo kupunguza usumbufu kwa wananchi ikiwemo kusafiri
mwendo mrefu kupata huduma hizo. Aidha
mawasiliano ya awali katika kupanua huduma hizo yameanza katika mikoa ya Arusha
na Mbeya.
16.Mheshimiwa Spika, Kuhusu ugonjwa wa Ukoma,
takwimu zinaonyesha kwamba ugonjwa huu unazidi kupungua. Kwa mfano mwaka 2000 kulikuwa na wagonjwa wapya 5,200 na mwaka 2001 kulikuwa na wagonjwa wapya 4,743. Hii inaonyesha kupungua kwa wagonjwa wapya kwa asilimia 9. Licha ya kuwa ugonjwa huu unapungua, lakini karibu asilimia 15 ya wagonjwa hao wana ulemavu wa kudumu. Ulemavu huo unajionesha katika upotevu wa baadhi ya viungo vikiwemo vidole vya miguu, mikono au sehemu nyingine za mwili. Hivyo basi wagonjwa hawa wanahitaji msaada wa matibabu na huduma nyingine za kijamii kwa maisha yao yote. Pamoja na mafanikio hayo, takwimu zinadhihirisha wazi kuwa Tanzania haitaweza kufikia kiwango cha kimataifa cha kutokomeza ugonjwa wa Ukoma duniani ifikapo mwaka 2005. Jitihada zaidi zitaongezwa za kuhamasisha wananchi wenye dalili za ugonjwa wa Ukoma wajitokeze haraka ili kupata matibabu ambayo hutolewa bila malipo katika vituo vya kutolea huduma.
17.Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha 2001/2002
Wizara iliahidi
kutekeleza Kampeni maalum ya kutokomeza Ukoma katika mikoa ya Tanga na
Pwani. Napenda kulieleza Bunge lako tukufu kuwa kampeni hizo zimeanza
kutekelezwa katika mikoa hiyo na kupanuliwa
katika mikoa mingine miwili zaidi ya Lindi na Kagera. Matokeo ya kampeni hizo yatatolewa hapa
Bungeni katika kipndi cha 2003/2004.
18. Mheshimiwa Spika, ugonjwa wa
UKIMWI ni miongoni mwa magonjwa yanayoongoza kwa kusababisha vifo vingi. Wakati takwimu kwa ujumla zinaonyesha
kuwepo viwango vya juu vya maambukizi ya virusi vya UKIMWI, kuna dalili kuwa
katika baadhi ya mikoa hapa nchini ishara za awali za mafanikio zimeanza
kuonekana.
19. Mheshimiwa Spika, katika
ufuatiliaji wa idadi ya wagonjwa wa UKIMWI, Mkoani Mbeya kwa kipindi cha Oktoba
hadi Desemba 2001, takwimu zifuatazo zimejitokeza. Matokeo ya tafiti kwa rika zote kwa mwaka 2001/02 yalionesha kuwa
asilimia 11.9 wameambukizwa virusi vya UKIMWI ukilinganisha na asilimia 20.3
mwaka 1994/95. Mchanganuo zaidi wa
vipimo hivi ni kama ifuatavyo:
a. Sehemu za mijini
– Asilimia 17.0 kwa mwaka
2001 ikilinganishwa na
asilimia 20.7 mwaka 1994/95.
b. Sehemu za kando
kando ya barabara kuu – Asilimia 9.8 mwaka 2001 ikilinganishwa na 25.6 mwaka
1994/95.
c. Sehemu za
mipakani – Asilimia 18.3 mwaka 2001 ikilinganishwa na asilimia 33.8 mwaka
1994/95.
20. Mheshimiwa Spika, hali ya
maambukizi kwa vijana wenye umri wa miaka 15 –24 yanatoa matumaini zaidi. Kwa ujumla viwango katika kundi hili
vimeshuka hadi wastani wa asilimia 11.75 mwaka 2001 kutoka asilimia 20.6 mwaka
1994/95. Mabadiliko ya kushuka kwa
viwango miongoni mwa vijana sehemu za vijijini, kando kando ya barabara kuu na
sehemu za mipakani ni kama ifuatavyo:-
·
Vijijini – Asilimia 4.7 mwaka 2001 ikilinganishwa na asilimia 15.6
mwaka 1994/95.
·
Kando kando ya barabara kuu – Asilimia 7.5 mwaka 2001 ikilinganishwa na
asilimia 26.5 mwaka 1994/95.
·
Vituo vya mipakani – Asilimia 19.5 mwaka 2001 ikilinganishwa na 36.1
mwaka 1994/95.
21. Mheshimiwa Spika, nimetoa
takwimu hizi kwa nia ya kusisitiza jambo moja kwamba UKIMWI unaweza
kudhibitiwa. Mambo yaliyopelekea
kushuka kwa viwango hivyo nilivyovitaja mkoani Mbeya ni wananchi kutumia
kikamilifu huduma zitolewazo kwa ajili ya udhibiti wa ugonjwa wa UKIMWI. Huduma hizo ni pamoja na upimaji, tiba ya
magonjwa ya zinaa, matumizi ya kondomu, dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa
mama kwenda kwa mtoto, usalama wa damu na elimu ya kubadili tabia za vijana
kutofanya ngono mpaka wakati wanapooa au kuolewa na kuwa mwaminifu kwa mwenza. Changamoto kwa taifa letu sasa ni kuinua
upatikanaji wa huduma hizi nchini kote na kuwashawishi wananchi kuzitumia kwa
ukamilifu. Kutokana na mwelekeo huu,
ninapenda kuwahakikishia Watanzania wote kuwa tukiamua tunaweza kudhibiti janga
la kuenea kwa UKIMWI ikiwa kila Mtanzania atachukua hatua za dhati za
kujikinga.
22. Mheshimiwa Spika, upatikanaji wa dawa za kurefusha
maisha ya
waathirika wa virusi vya UKIMWI ni mkakati sahihi kabisa katika mapambano dhidi
ya ugonjwa wa UKIMWI. Kwa mantiki hiyo, Wizara ya Afya sasa imesajili madawa aina kumi yanayoongezea
maisha watu wenye virusi vya UKIMWI.
Madawa yaliyosajiliwa ni: Nevirapine Stavudine, Lamivudine, Efavirenz,
Nelfinavir, Zakitabine, proguanil HCL, Zidovudine, Abacavir na
Delavirdine mesylate. Madawa
haya yamesajiliwa na Kampuni sita za Madawa ambazo ni Baehriinger Ingelhein
Pharma KG, Bristol Myers Squibb, Cipla, Dupont, Merck na Haffman, la Roche na Glaxo- Smithkline. Aidha, katika jitihada za kuimarisha
utaratibu huu, shughuli zifuatazo zimefanyika:
·
Wizara imeandaa utaratibu utakaowezesha waathirika wa virusi vya UKIMWI
kupata taarifa juu ya matumizi ya madawa ya kurefusha maisha.
·
Hospitali zote za rufaa zimepatiwa machine za kupima chembechembe hai
za CD4 ambacho ni kipimo muhimu katika matumizi ya madawa ya UKIMWI. Kipimo cha CD4 ni lazima kifanyike
kuweza kufahamu wakati wa kuanza matibabu na baadaye hutoa dira ya maendeleo ya
matibabu.
·
Mwongozo wa kuwahudumia wagonjwa wa UKIMWI, hususan matumizi ya madawa
ya UKIMWI umeandaliwa na utasambazwa kwa watumishi wa afya nchini kote.
23. Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha mwaka 2001/2002 Wizara ya Afya imeweza kutoa tiba ya ugonjwa wa
vikope ( trachoma), katika mikoa yenye ugonjwa huo, kwa kutumia dawa ya zithromax.
Dawa hizo zilitolewa
katika wilaya 9 za mikoa ya Dodoma, Singida, Morogoro,
Iringa na Kilimanjaro ambapo watu 310,671 walitibiwa. Hii ni moja ya juhudi za kitaifa na kimataifa za kutokomeza ugonjwa
wa vikope ulimwenguni ifikapo mwaka 2020. Aidha Mpango wa kudhibiti ugonjwa wa
usubi kitaifa ulizindua miradi mipya
ambayo ni Kilosa Focus na Tunduru Focus katika kipindi cha mwaka 2001/2002 na kufanya idadi ya watu waliyopewa dawa ya Mectizan kufikia 624,290 katika vijiji
468, ikilinganishwa na watu 338,886 waliotibiwa
mwaka 2000/2001.
24. Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha 2001/2002 Wizara iliendesha mafunzo kwa walengwa wafuatao:
·
Watoa Huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto 52 kutoka wilaya za Rukwa
Singida na Lindi.
·
Wakufunzi wa Wakunga wa Jadi 18 toka katika wilaya za Tabora na Kigoma.
·
Timu za utoaji huduma za afya ngazi ya mkoa na wilaya toka Wilaya zote
za mikoa ya Dodoma, Singida, Mwanza na Mara.
Sambamba na mafunzo
hayo Wizara pia ilisambaza kadi za Huduma za Mama na Mtoto (MCH 1, 4 na 5),
dawa na vifaa vya uzazi wa mpango katika vituo vyote vya kutolea huduma.
Mpango
wa Taifa wa Chanjo
25. Mheshimiwa Spika, Mpango wa
Taifa wa Chanjo umeendelea kutoa chanjo kwa watoto chini ya umri wa miaka
mitano na mama wajawazito. Mwaka 2001/2002 Wizara ya Afya iliendesha zoezi
maalum la chanjo ya Polio kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano katika
wilaya 16 na kupata mafanikio ya asilimia 100 kwa mzunguko wa awamu ya kwanza
na ya pili. Sambamba na zoezi hilo
maalum la chanjo ya Polio, Wizara pia iliendesha Kampeni ya chanjo ya Surua kwa
watoto wenye umri kati ya miezi tisa hadi miaka 15 katika wilaya 31 na kupata
pia mafanikio kwa asilimia 100.
Ninachukua nafasi hii kutoa shukrani za dhati kwa Halmashauri, Wahisani,
Taasisi na Mashirika ya kiserikali na yasiyo ya kiserikali, Mashirika ya
kimataifa, na Waheshimiwa Wabunge kwa kushiriki kikamilifu katika kufanikisha
kampeni hizi.Wakati huo huo shughuli za kawaida za chanjo ziliendelea katika
vituo vyote nchini ambapo wastani wa asilimia 87 ya walengwa walichanjwa.
26. Mheshimiwa Spika katika mwaka 2001 Wizara yangu iliweza kufunga
majokofu yatumiayo mionzi ya jua 29 Mkoa wa Tabora na 51 Mkoa wa Kigoma. Pia imefanikiwa kubadilisha majokofu
yanayotumia mafuta ya taa na kuanza kutumia gesi katika mikoa sita ya Tanga,
Mtwara, Dodoma, Morogoro, Pwani na Lindi. Hali kadhalika, kuanzia mwezi Januari
2002 tulipozindua chanjo ya ugonjwa wa homa ya ini (Hepatitis B), tulizindua
mpango wa kutumia mabomba ya sindano maalum yanayotumika mara moja tu, kwa
ajili ya kuimarisha na kuboresha utoaji sindano salama wa chanjo zote nchini.
Aidha Vituo vyote vinatumia vikasha maalum (safety boxes) kwa ajili ya
kukusanyia mabomba na sindano zilizotumika.
Wizara yangu pia imejenga matanuru nane ya kuchomea taka (medical
incinerators) katika Hospitali za Rufaa za Muhimbili na Mbeya,
Hospitali za Wilaya za Bagamoyo, Korogwe, Kilombero, na Kondoa, na vituo vya afya vya Morogoro Mjini na Ngerengere.
Wizara ina mpango wa kujenga matanuru haya katika Hospitali zote za Wilaya,
Vituo vya Afya na Zahanati zote nchini.
Huduma za Elimu ya Afya kwa
Umma.
27. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya imeendelea
kutoa elimu ya afya kwa wananchi kuhusu kubadilisha mitindo ya maisha na
mienendo ili kujenga jamii yenye siha nzuri na uwezo wa kuchangia kikamilifu
katika shughuli za kiuchumi na kijamii.
Wizara ya Afya imeendelea kutayarisha vipindi mbalimbali vinavyotangazwa
katika magazeti, redio na televisheni.
Mwaka uliopita niliahidi kuwa Wizara yangu itaandaa mpango wa miaka
mitano wa mawasiliano ya Elimu ya afya na mwongozo wa utoaji huduma hizo hapa
nchini. Napenda kuliarifu Bunge lako
tukufu kuwa mpango huo umekamilika na mwongozo utasambazwa kwa wahusika katika
kipindi cha mwaka 2002/03.
28. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya inatilia maanani umuhimu wa usafi
wa mazingira katika uimarishaji wa afya ya jamii. Katika kipindi cha 2001/2002 Wizara imetayarisha miongozo miwili
inayotoa dira ya uimarishaji wa afya ya mazingira nchini. Miongozo hiyo ni Mwongozo wa Udhibiti wa
Taka na Mwongozo wa Sera ya Afya na Usafi wa Mazingira (Policy Guidelines on
Environmental Health and Sanitation). Aidha Wizara kwa kutambua umuhimu
wa afya bora ya wafanyakazi hasa viwandani na kwenye mashamba, iliendesha
mafunzo kwa waganga wa mikoa ya Shinyanga na Mwanza. Mafunzo hayo yalilenga katika upimaji wa afya za wafanyakazi na
udhibiti wa magonjwa yatokanayo na kazi.
Mafunzo hayo yalishirikisha waganga wa mikoa ya Mwanza na Shinyanga kwa
kuzingatia kuwepo kwa kazi za uzalishaji wa pamba mashambani, viwanda vya kuchambua pamba, viwanda vya
samaki na migodi katika mikoa hiyo.
29. Mheshimiwa Spika, napenda kulifahamisha
Bunge lako kwamba tarehe 22 – 28 Novemba 2001, Wizara ya Afya ilikuwa mwenyeji
wa Kongamano la Kimataifa la Afya ya Mazingira (International Conference on
Environmental Health) lililofanyika Bagamoyo. Sambamba na Kongamano hilo, ulifanyika uzinduzi wa maktaba kubwa
katika chuo cha Maafisa Afya – Muhimbili.
Huduma ya Bandarini, Vituo
vya Mipakani na Viwanja vya Ndege.
30.
Mheshimiwa Spika, moja ya kazi za Wizara ya Afya ni udhibiti wa afya sehemu za
bandarini, viwanja vya ndege na vituo vya mipakani, ili kuhakikisha kwamba watu
na bidhaa zitokazo na kuingia nchini zipo katika hali bora. Katika kipindi cha 2001/2002 jumla ya tani
439,453 za vyakula zilikaguliwa na kuruhusiwa kuingia nchini baada ya kuonekana
zinafaa kuliwa na binadamu. Tani 487
zilionekana kuwa hazifai na hivyo ziliteketezwa.
Mradi
wa Uimarishaji wa Huduma za Afya (MUHUMA)
(Tanzania Essential Health
Interventions Project – TEHIP)
31.
Mheshimiwa Spika, Mradi wa Uimarishaji
Huduma Muhimu za Afya (MUHUMA) ambao ni ushirikiano kati ya kituo cha kimataifa
cha utafiti cha Canada (IDRC) pamoja na Wizara ya Afya unaendelea kusaidia Timu
za Uendeshaji Huduma za Afya na Halmashauri za Wilaya za Morogoro Vijijini na
Rufiji katika kupanga mpango wa Afya wa Wilaya, kuandaa makadirio na kutoa
huduma muhimu za afya kwa kupitia mfumo wa Afya ya Jamii. Katika kipindi cha
mwaka 2001/2002 mradi ulitumia shilingi
billioni 1.6 kwa kugharamia
huduma katika vituo vya afya na zahanati, kufanya utafiti na kusadia katika
uimarishaji wa mipango ya afya ya halmashauri za wilaya za Rufiji na Morogoro
Vijijini na kutoa mafunzo kwa watumishi wa afya.
33. Mheshimiwa
Spika, zahanati na vituo vya afya vya Serikali viliendelea kupelekewa masanduku
ya dawa (Essential Drug Kits) kila
mwezi. Aidha, orodha ya dawa na vifaa iliongezeka kutoka 54 hadi 67 ili kukidhi
mabadiliko ya tiba ya malaria na kukabiliana na maradhi ambayo husababisha vifo
kwa watoto chini ya miaka mitano. Ili
kuboresha upatikanaji wa dawa katika zahanati na vituo vya afya, Halmashauri zilizoanzisha Mfuko wa Afya ya
Jamii (CHF) ziliandaliwa kutekeleza
mfumo wa uagizaji na usimamizi wa matumizi ya dawa na vifaa (Indent System). Halmashauri hizo ni
Hanang, Igunga, Nzega, Iramba, Singida Vijijini, Iringa Vijijini, Songea
Vijijini, Songea Mjini, Kilosa na Mbinga.
34. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka
2001/2002 Wizara ya Afya ilianza maandalizi ya mkakati wa uanzishaji wa mpango
wa kitaifa wa upatikanaji wa damu salama na ya kutosha kwa wagonjwa. Maandalizi ya kuunda taasisi ya kitaifa
itakayoshughulikia huduma ya upatikanaji wa damu salama yaani, National
Blood Transfusion Services, yameanza kwa kufanya upembuzi yakinifu wa
mahitaji ya vifaa, watumishi, miongozo na mafunzo kwa ajili ya shughuli hiyo. Taasisi hiyo itakuwa na ofisi za kanda
kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili, Hospitali za Rufaa za KCMC, Bugando na
Mbeya. Mpango wa utekelezaji wa
kuanzisha huduma hii kwenye hospitali ya Rufaa ya Mbeya kwa ajili ya Kanda ya
Nyanda za juu Kusini umeandaliwa.
Aidha, mwongozo wa matumizi ya damu katika utoaji huduma umeandaliwa.
35. Mheshimiwa Spika,
kupitia mradi wa kuimarisha huduma za uchunguzi wa wagonjwa unaogharamiwa na
serikali za Tanzania na Uholanzi (ORET), Wizara ya Afya imefunga mitambo mipya
ya X-ray
na Ultrasound
katika hospitali zilizoko katika mikoa ya Rukwa, Mbeya, Singida, Dodoma,
Kilimanjaro na Arusha, hii ni awamu ya pili ya ufungaji wa vifaa hivi. Aidha, katika awamu hii, nasikitika
kuliarifu Bunge lako kuwa mitambo ya X-ray na Ultrasound ambayo
imekwisha wasili, haikufungwa katika hospitali za mikoa ya Mbeya, Singida na
Arusha na Hospitali za wilaya za Hanang, Babati na Chunya kwa kuwa hazikuwa na
vyumba au nyumba ya x-ray, au hali ya vyumba haikukidhi viwango vinavyotakiwa ili kufungwa
mashine hizo. Viongozi wa huduma za
afya katika mikoa na wilaya hizo wanahimizwa kukamilisha matayarisho hayo ili
mitambo ifungwe na huduma ianze kutolewa.
36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa
2001/2002, Wizara ya Afya imekamilisha mwongozo wa kisera juu ya vifaa vya
kitaalam vya kutolea huduma za afya (Policy Guidelines for Health Care
Technology). Kupitia mwongozo
huu, utaratibu wa kuchagua, kununua, kusimika na kutumia vifaa vya kitaalaam
vya kutolea huduma za afya umeainishwa.
Pia mwongozo huu una lengo la kuimarisha mpango wa kuvifanyia
matengenezo ya kinga (Planned Preventive Maintenance)
vifaa hivi katika hospitali zote. Aidha, karakana za kanda za kutengeneza vifaa
vya kitaalam vya kutolea huduma za afya zilizopo kwenye hospitali za Muhimbili,
Mtwara, Mbeya, KCMC na Bugando zimeimarishwa kwa kupatiwa vifaa vya kufanyia
kazi na mafunzo. Wahandisi na mafundi
15 kutoka kwenye hospitali hizo walipewa mafunzo hayo na vifaa kupitia Mradi wa
ORET.
37. Mheshimiwa Spika kwa upande wa huduma za
afya ya kinywa, mwaka 2001/2002 Wizara yangu imefanikiwa kuagiza vifaa kwa
ajili ya tiba ya meno kwa hospitali
zifuatazo; Monduli, Kasulu, Ilala, Lindi, Mwanza, Musoma, Bukoba, Shinyanga,
Magu, Dodoma na Ulanga. Pia, madawa
muhimu kwa ajili ya tiba ya meno yamenunuliwa kwa kushirikiana na Idara ya
Bohari Kuu ya Dawa. Hali kadhalika
mtaala kwa ajili ya kufundishia Madaktari wa Meno Wasaidizi umefanyiwa
marekebisho.
Huduma za Afya ya Akili na Madawa ya Kulevya
38. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka
wa fedha 2001/2002 Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Sheria na Mambo ya
Katiba imekuwa ikiandaa mapendekezo ya muswada wa sheria ya kuboresha huduma za
afya ya akili nchini. Wizara inakusudia kuwasilisha muswada huo wa sheria
Bungeni katika mwaka wa fedha 2002/2003.
Aidha Wizara imeandaa vitabu vya elimu ya msingi juu ya afya ya akili
kwa wafanyakazi wa afya, ambavyo vikichapishwa vitasambazwa nchi nzima. Vitabu hivi vitasaidia kuboresha ustadi wa
wataalam wa ngazi ya msingi katika kukabiliana na maradhi ya akili.
40. Mheshimiwa
Spika, Hospitali ya Taifa Muhimbili imeundwa upya baada ya Bunge lako Tukufu
kupitisha Sheria Na 5 ya mwaka 2000. Sheria hiyo ilitenganisha uendeshaji wa
taasisi mbili zilizokuwa chini ya Shirika la Afya Muhimbili, yaani Hospitali ya
Taifa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi ya Afya. Katika utekelezaji wa sheria hiyo Wizara iliendelea kusimamia
mabadiliko ya Hospitali kwa kuunda Kamati ya Mpito (Transition Management Committee)
na Baraza la Wadhamini la Hospitali.
Kamati ya Mpito imekuwa ikisimamia utekelezaji wa mgawanyo wa rasilimali
na wafanyakazi kati ya Hospitali ya Taifa na Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi
ya Afya Muhimbili. Kazi hii imekamilika
na hivi sasa Kamati inakamilisha taarifa na mapendekezo yake ili yawasilishwe
Serikalini kwa ajili ya maamuzi ya mwisho juu ya mgawanyo huo. Napenda kuchukua fursa hii kumpongeza
Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe. Milton Makongoro Mahanga, Mbunge wa Ukonga, kwa
kazi nzuri inayofanywa na kamati hiyo. Hali kadhalika, Baraza la Wadhamini la
Hospitali ya Taifa Muhimbili chini ya Mweyekiti wake Mheshimiwa Abdulrahman
Kinana, Spika wa Bunge la Afrika Mashariki limeshaanza kazi ya kushughulikia
mabadiliko ya Muundo wa Hospitali pamoja na uteuzi wa Menejimenti mpya ya
Hospitali.
41. Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha 2000/2001 hospitali ya Taifa Muhimbili ilitumia shilingi
milioni 600.0 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa
ghorofa ya kwanza ya jengo la wodi ya watoto.
Pia hospitali ilifanya ukarabati wa baadhi ya majengo ya hospitali kwa
kutumia fedha zitokanazo na mifuko ya kujitegemea.
42. Mheshimiwa spika, katika mwaka 2001/2002
hospitali
ya
KCMC iliendelea kutekeleza mipango yake ya utoaji wa huduma ya tiba, utoaji wa
elimu na uendeshaji wa utafiti.
Wagonjwa wa kulazwa 17,421 na wagonjwa wa nje 99,747 walitibiwa katika mwaka 2001. Katika mwaka
2001/2002 Hospitali ya KCMC ilikamilisha ukarabati wa kitengo cha wagonjwa
mahututi waliofanyiwa upasuaji (Surgical Intensive Care Unit) kwa
gharama ya shilingi milioni 16.0
zilizotolewa na Shirika la Msamaria Mwema.
Aidha, ujenzi wa ofisi na madarasa ya Chuo Kikuu kishiriki cha Tiba cha
KCMC ulikamilika mwezi wa Agosti 2001. Fedha za kugaharmia ujenzi wa jengo hilo
zilitolewa na wadau wa Shirika la Msamaria Mwema. Sambamba na ujenzi uliofanyika, hospitali ilifanya ukarabati wa
bweni la wanafunzi wanaochukua mafunzo ya Madaktari Wasaidizi (Assistant
Medical Officers) na Wazoesha Viungo (Physiotherapists).
43. Mheshimiwa Spika, Hospitali ya Rufaa ya
Mbeya inayotoa huduma za rufaa kwa hospitali za mikoa ya Kanda ya Nyanda za juu
Kusini ilipatwa na msiba mkubwa baada ya kufariki aliyekuwa Mganga Mkuu wa
Hospitali Dr. Titus Nkulila. Mungu
aiweke roho yake mahali pema peponi.
Amin.
44. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2001/2002 ufanisi wa kazi katika hospitali ya Rufaa ya
Mbeya uliongezeka baada ya watumishi kutiwa moyo na Wizara kwa kukamilisha
zoezi la kuwapandisha madaraja watumishi wengi kuliko miaka ya nyuma. Pia Wizara ilitoa fedha za kulipia deni la
posho za zamu ya kuitwa kazini wakati wa mapumziko (on call allowance) na posho za
sare kwa maafisa wauguzi. Aidha, ubora
wa huduma za hospitali uliimarika kwa upatikanaji mzuri wa dawa kutokana na
ruzuku ya serikali inayopitia Idara ya Bohari Kuu ya Dawa, mfuko wa dawa wa
hospitali (Drug Revolving
Fund) na mpango wa uchangiaji wa huduma za
Afya (Cost Sharing
Fund).
Kuanzia Machi 2002, hospitali ilianza kutoa huduma kwa watumishi wote wa
idara za serikali kupitia mpango wa Bima ya Afya. Uongozi wa hospitali umeamua kusimamia kikamilifu zoezi hili ili
kuhakikisha kuwa wateja wanapata huduma bora na kwa haraka. Aidha, hospitali imekamilisha ukarabati wa
wodi mbili, mitambo ya hospitali na vifaa vya kitaalam. Ukarabati huo
ulifanikiwa kutokana na kutenga shilingi milioni 38 kutoka kwenye bajeti ya serikali. Pia, hospitali imetumia shilingi
milioni 67.0 kukamilisha ukarabati wa mabweni ya madaktari
walio mazoezini (Interns Hostel) na imeanza ukarabati wa hospitali ya wazazi Meta
utakaogharimu shilingi milioni 53.0
na ukarabati wa wodi ya wagonjwa wa akili kwa shilingi milioni
30.0
45. Mheshimiwa
Spika, Hospitali ya Rufaa Mbeya imekuwa mstari wa mbele katika shughuli za
utafiti. Katika mwaka 2001/2002
hospitali ya Rufaa ya Mbeya ilinufaika kwa ushirikiano wake na Chuo Kikuu cha
Munich, Ujerumani, Chuo Kikuu cha Johannesburg, Afrika Kusini na Walter Reed
Foundation ya Washington, Marekani. Kupitia
ushirikiano huo, hospitali ya Rufaa Mbeya iliweza kujenga ofisi na kliniki ya
kufuatilia utafiti wa chanjo ya kinga ya maambukizo ya UKIMWI kwa gharama ya shilingi
milioni 75.0
46. Mheshimiwa
Spika, Hospitali ya Bugando yenye vitanda 820 inatoa huduma za rufaa katika
Kanda ya Ziwa. Katika mwaka uliopita
hospitali hiyo imetoa huduma kwa wagonjwa 109,317. Kati ya wagonjwa hao 83,749 walikuwa wagonjwa wa nje, hii ni sawa
na wagonjwa 247 kwa kila siku. Jumla ya wagonjwa 25,568 walilazwa, hii ni sawa
na wagonjwa 71 wa kulazwa kila siku.
Hospitali ya Bugando inatoa matibabu maalum ya upasuaji wa akina mama
waliopata matatizo wakati wa kujifungua na kupata madhara ya njia ya mkojo (V.V.F). Matibabu haya huendeshwa kwa msaada wa shirika
la Maryknol kutoka Marekani na AMREF Tanzania, hivyo wagonjwa hawa hutibiwa
bila malipo. Huduma hii inawafikia
wagonjwa wengi kutoka sehemu mbalimbali za Kanda ya Ziwa Victoria. Mwaka uliopita walitibiwa wagonjwa wa V.V.F
220 na kupona.
47. Mheshimiwa
spika, Hospitali ya Bugando imeweza kuanzisha kliniki za huduma binafsi za
kulipia (Private
Clinics) ambazo hutoa huduma baada ya saa za
kazi za kawaida. Hii imesaidia kwa
sehemu kubwa ya wataalam kubaki katika kliniki za Bugando baada ya saa za kazi kwisha,
kwani kabla ya hapo madaktari na wauguzi walikuwa wakienda kutafuta au kufanya
kazi mjini kwenye hospitali binafsi.
48. Mheshimiwa
spika, pamoja na kutoa huduma za tiba, taasisi hii vile vile inatoa mafunzo kwa
wataalam wa afya katika fani zifuatazo:
·
Madaktari wasaidizi (AMO).
·
Wauguzi daraja la kwanza.
·
Wafamasia Wasaidizi.
·
Fundi sanifu maabara.
·
Fundi sanifu mionzi (Radiographers).
·
Watoa dawa za usingizi.
·
Ushauri Nasaha
Wizara imekubali vyuo vitoavyo mafunzo ya Famasia,
Radiolojia na Maabara vianze kutoa mafunzo ya Stashahada kuanzia mwaka
huu. Pamoja na mafunzo haya ya vyuoni,
Hospitali ya Bugando ina kitengo ambacho hutoa elimu kwa njia ya kujiendeleza
kwa wafanyakazi wa fani mbalimbali za uganga.
Huduma hii imelenga zaidi kwa wafanyakazi ambao wako katika Kanda ya
Ziwa. Masomo haya yanalengo la kuinua elimu ya wafanyakazi na vile vile ni
motisha kwa wale ambao wamekaa kazini bila kujiendeleza kwa muda mrefu.
49 Mheshimiwa
Spika, Ili kupunguza tatizo la nyumba
kwa wafanyakazi, Hospitali ya Bugando ilifanikiwa kununua nyumba 10 za ghorofa
zinazoweza kukaa familia 40 zilizokuwa zinamilikiwa na kiwanda cha nguo cha
Mwanza (Mwatex). Pia taasisi
ilinunua basi moja kwa ajili ya usafiri wa wafanyakazi. Magari mawili ya huduma, yaani lori na pickup,
yamefanyiwa ukarabati.
50. Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Saratani ya
Ocean Road pamoja na ongezeko la wagonjwa na hali ngumu ya kifedha imezidi
kuboresha huduma kwa wagonjwa wa Saratani nchini. Pamoja na sera ya wananchi kuchangia huduma za afya, wagonjwa wa
Saratani wamesamehewa kulipia gharama za matibabu. Katika mwaka wa fedha uliopita, Taasisi ya Saratani ilipata
mashine ya kuhakiki matibabu ya mionzi inayoitwa Simulator yenye thamani
ya dola 400,000 ukiwa ni msaada
kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (International Atomic Energy
Agency -IAEA). Mashine hii
imeipa Taasisi uwezo wa kuhakikisha kwamba sehemu ya mwili inayotibiwa na
mionzi ni ile iliyoathirika tu na hivyo kuzuia uwezekano wa kuziathiri sehemu
ambazo hazina maradhi. Pia, katika
mwaka wa fedha uliopita Taasisi ilipata msaada wa vifaa vya kuboresha huduma za
tiba ya mionzi (Nuclear Medicine) kutoka Shirika la Kimataifa la Nguvu za
Atomiki (IAEA) vyenye thamani ya dola
200,000. Vile vile, Taasisi ya Saratani imekamilsha kazi ya ukarabati wa
majengo yenye vyumba vya matibabu, X-ray, Ultrasound, Nuclear Medicine,
Maabara na Mapumziko ya Wagonjwa kwa kutumia shilingi milioni 100.0 ambazo zilitokana na bajeti ya Serikali.
Taasisi ya Mifupa ya Muhimbili – MOI – (Mifupa na Ajali)
51.
Mheshimiwa Spika katika mwaka wa fedha wa 2001/2002 , Taasisi ya Mifupa
ya Muhimbili iliendelea kutoa huduma za matibabu ya mifupa na magonjwa
yatokanayo na ajali, kufundisha na kutafiti kuhusu matibabu ya magonjwa ya
mifupa, majeruhi, mifumo ya fahamu na ubongo. Kwa kushirikiana na Chuo Kikuu
Kishiriki cha Tiba, Taasisi imefanikiwa kuanzisha mafunzo ya shahada ya uzamili
katika fani ya mifupa na ajali. Kozi hii ilianza oktoba 2001 ikiwa na wanachuo
wanne. Imefanikiwa pia kuandaa kitabu cha Mwongozo wa Matibabu ya Magonjwa ya
Mifupa, majeruhi, mfumo wa fahamu na ubongo.
Hospitali
ya Mirembe na Taasisi ya wagonjwa wa akili ya Isanga
52. Mheshimiwa
Spika, Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya
Isanga
ni Hospitali maalum za kutoa huduma za tiba na ukarabati wa mienendo ya
wagonjwa wa akili nchini. Hospitali ya
Mirembe inatoa huduma za afya ya akili kwa wagonjwa wa kawaida na Taasisi ya Isanga inatoa huduma za afya
ya akili kwa Wagonjwa waliotenda makosa ya jinai.
Kwa mwaka wa
fedha 2001/2002 hospitali ilihudumia jumla ya wagonjwa 20,397 kati ya hao
wagonjwa 2,209 walilazwa, wagonjwa 18,188 walikuwa ni wagonjwa wa nje. Wagonjwa waliolazwa walikuwa wanashumbuliwa
na magonjwa yafuatayo:-
·
Kuchanganyikiwa kwa kushindwa kumiliki na kutawala fikra
(Schizophrenia) kwa asilimia 15 na marudio kwa asilimia 77,
·
Madawa ya kulevya asilimia 15 marudio asilimia 3,
·
Kifafa cha kuchanganyikiwa asilimia 14 marudio 11.
·
Kuchanganyikiwa kutokana na maradhi ya ubongo (Organic Brain Sydrome),
asilimia 11 marudio asilimia moja (1%).
·
Kuchanganyikiwa au kusononeka kupita kiasi kunakotokana na mabadiliko
makubwa ya hisia (Mania) asilimia 4, marudio asilimia 7.
·
Ugonjwa wa kifafa uliongoza kwa asilimia 70 kwa wagonjwa wa nje.
Magonjwa ya akili
yanakaribia kufikia kiwango cha mlipuko kwa sababu zifuatazo:
·
Ongezeko la matumizi ya madawa ya kulevya nchini.
·
Kutopewa uzito unaostahili katika Huduma za Afya ya Msingi kwa wagonjwa
wa afya ya akili. Wagonjwa wengi
hurudiwa na ugonjwa mara baada ya matibabu na kuruhusiwa kurudi nyumbani kwa
kukosa huduma inayostahili hasa upendo toka kwa ndungu na jamii inayowazunguka.
·
Ongezeko la Ugonjwa wa UKIMWI ambao sasa unaathiri afya ya akili.
·
Jamii kutojua dalili za mwanzo za magonjwa ya akili na kuyapatia
tafsiri potofu, hasa imani za kishirikina.
Huduma kwa
wagonjwa wa kawaida.
Pamoja na kutibu wagonjwa
wenye matatizo ya afya ya akili, hospitali ya Mirembe inahudumia pia wakazi wa
Manispaa ya Dodoma wanaoumwa magonjwa ya kawaida. Ugonjwa wa malaria uliongoza kwa idadi ya wagonjwa waliolazwa kwa
asilimia 52 na kwa wagonjwa wa nje kwa asilimia 40.
53. Mheshimiwa Spika,
Katika mwaka 2001/2002 Wizara
ilianza kufanya ukarabati wa mifumo ya maji machafu ya hospitali na kuiunganisha na mfumo wa maji machafu wa mji wa Dodoma. Aidha mfumo wa maji safi wa Taasisi ya Isanga nao ulifanyiwa pia ukarabati kwa kurekebisha mabomba na tanki la maji. Ukamilishaji wa kazi hizi unatarajiwa katika mwaka huu wa fedha 2002/2003.
54. Mheshimiwa Spika, Hospitali
ya Kibong’oto ambayo ilikuwa inatumika kama kituo cha kuwatenga wagonjwa na
kuwaweka mahali penye mazingira mazuri ya matibabu, hivi sasa bado inatoa
mchango mkubwa katika tiba na utafiti wa ugonjwa wa Kifua Kikuu. Aidha
hospitali hiyo pia inahudumia wagonjwa
wa kawaida. Takwimu zinaonyesha kuwa mwaka 2001/2002, Hospitali ya Kibong’oto
ilitibu wagonjwa wa kifua kikuu 6,961, wakiwemo wagonjwa 810 wakulazwa na
wagonjwa 6,151 wa nje. Vile vile hospitali ilitoa huduma kwa wagonjwa 3,566 wa
kawaida. Kati yao wagonjwa 494 walilazwa na wagonjwa 3,072 walitibiwa na kurudi
nyunbani.
55. Mheshimiwa
Spika, Hospitali zote za Rufaa hazikubaki nyuma katika kupiga vita UKIMWI na
kutafuta njia za kuwasaidia waaathirika wa janga hili. Hospitali za Rufaa za Muhimbili, KCMC,
Bugando na Mbeya, na Hospitali ya Mkoa wa Kagera zilishiriki katika kuanzisha
kwa majaribio ya mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya UKIMWI kutoka kwa
mama wajawazito walioathirika na virusi vya UKIMWI kwenda kwa watoto
watakaozaliwa. Mpango huo unagharamiwa
na serikali ya Tanzania, Shirika la Umoja wa Mataifa Linalohudumia Watoto (UNICEF), Shirika la Medicins du Monde la Ufaransa na
Shirika la Maendeleo la Ujerumani (GTZ).
Katika mpango huo mama wajawazito hupewa ushauri nasaha juu ya UKIMWI na
chaguo la kupima kama wameambukizwa virusi vya UKIMWI au la. Wale walioambukizwa hupewa dawa za kuzuia
maambukizi kwa mtoto akiwa tumboni.
Aidha huduma makini hutolewa wakati wa kujifungua ili mtoto
asiambukizwe. Kabla ya kuruhusiwa
kwenda nyumbani, wazazi hupewa ushauri nasaha juu ya njia salama za kumlisha
mtoto mchanga ili asiambukizwe wakati wa kunyonyesha. Kuanzia Julai 2000 hadi Juni 2001, mpango huu umefanikiwa
kuwafikia mama wajawazito 24,000.
56. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio mazuri ya mpango huu,
kumekuwa na matatizo katika utekelezaji wake.
Matatizo hayo ni pamoja na ushiriki mdogo wa wanaume, upungufu wa
wataalam wa kutoa ushauri nasaha na wasiwasi wa kujulikana walioathirika
kutokana na unyanyapaaji (stigma) ulioenea katika jamii.
Pia mpango huu unaonekana kujali kuzuia maambukizi ya mtoto lakini
hauwafikii vyema akina mama baada ya kujifungua. Vilevile, wanaonufaika na mpango huu ni mama wanaopata huduma
kwenye hospitali za rufaa. Ili kukabili
matatizo haya na kurekebisha mapungufu, mpango huu utafanyiwa tathmini katika
mwaka wa fedha wa 2002/2003 kwa ushirikiano kati ya Wizara ya Afya, UNICEF, Axios International na Shirika la kudhibiti magonjwa (Center for Disease Control-CDC) la Marekani. Kwa
madhumuni ya kurekebisha mapungufu hayo na kisha kuusambaza katika hospitali za
Mikoa.
57. Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya serikali, napenda kutoa
shukurani za dhati kwa mashirika na makampuni mbalimbali yaliyotuwezesha kutekeleza
mpango huu. Kampuni ya Abbot Laboratories kupitia shirika la Axios International ilitoa msaada
wa vifaa vya kisasa vya maabara kwa hospitali ya Mkoa wa Mbeya na Hospitali ya
Taifa Muhimbili. Pamoja na msaada wa
vifaa hivyo, kampuni ya Abbot
Laboratories imetoa msaada wa kiufundi katika
kuandaa mwongozo wa kutoa huduma kwa walioathirika na virusi vya UKIMWI.
Huduma ya Utawala
Ununuzi wa magari
59. Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha
mwaka
2001/2002.
Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali
za Mitaa ilinunua magari 11 kwa gharama ya shilingi milioni 239.93. Magari hayo yaligawanywa kwa Mganga Mkuu wa
Mkoa wa Mwanza na Halmashauri za wilaya za Shinyanga, Kahama, Maswa, Meatu,
Bukombe, Newala, Kongwa, Bunda, Muleba na Ngara.
Huduma za
Utumishi
60. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2001/2002 Wizara
ya Afya ilihuisha miundo ya
Utumishi (Scheme of Service) ya watumishi chini ya Wizara kutoka miundo
30 hadi kufikia 20. Baada ya zoezi hilo
wataalam wa Wizara ya Afya waliichambua miundo hiyo na kufanya marekebisho;
kuunganisha ile iliyokuwa na kazi zinazofanana; kupunguza au kuongeza upeo wa
ngazi ya mishahara, kuboresha sifa za kuingilia kazini na kuongeza muundo mpya
wa Medical
Entomologist ambao awali
uliunganishwa na ule wa Maafisa Afya.
61. Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya miundo
hiyo mipya iliwasilishwa mbele ya kikao cha kwanza cha Baraza la Wafanyakazi wa
Wizara (TUGHE) tarehe 4 na 5 Oktoba, 2001. Katika kikao hicho iliamuliwa kuwa miundo ya Mafundi Sanifu
iunganishwe. Kutokana na hatua hiyo,
miundo ilipungua tena kutoka 20 hadi 17 baada ya kuunganishwa miundo ya Mafundi
Sanifu. Miundo hiyo baada ya
kupitishwa katika Baraza la Wafanyakazi la Wizara; iliwasilishwa katika Baraza
Kuu la Taifa katika kikao chake kilichofanyika tarehe 19 na 20 Novemba 2001
hapa Dodoma. Ni matumaini yangu kuwa
miundo hiyo itakapoanza kutumika watumishi wa Sekta ya Afya watanufaika.
62. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha
2001/2002 Wizara ya Afya iliendeleza jitihada za kuwapandisha vyeo watumishi
katika ngazi mbalimbali. Ninayo furaha
kulifahamisha Bunge lako tukufu kwamba watumishi wa kada mbalimbali 6,029
walipandishwa vyeo. Aidha mapendenezo
ya kuwapandisha vyeo watumishi wengine 3,545 yamekamilishwa na kuwasilishwa
kwenye mamlaka husika. Zoezi hili bado
litapewa kipaumbele katika mwaka huu wa fedha.
63. Mheshimiwa Spika, Mafunzo ya kuimarisha
utendaji wa watumishi wa sekta ya afya katika Halmashauri na kuzipa uwezo wa
kupanga na kusimamia uendeshaji na utoaji wa huduma za Afya, yanaendelea
kutolewa na Wizara nchini kote. Jumla
ya halmashauri 73 zimekwishapata mafunzo hayo. Aidha uendeshaji wa mafunzo hayo
umefanyiwa tathmini ya kati (Mid-Term
Evaluation) na kuonyesha kuwa na
mafanikio hususan katika kuongeza uwezo wa Kamati za Uendeshaji wa Huduma za
Afya za Wilaya (Council Health Management Team) kupanga na kutekeleza mipango
ya afya, ukilinganisha na Halmashuri ambazo bado hazijapata mafunzo hayo.
64. Mheshimiwa Spika, ili kuinua ubora wa
mafunzo, Wizara yangu inashirikiana na Baraza la Elimu ya Ufundi (National Council for Technical Education) kuhakiki viwango vya
ufundishaji katika vyuo vya afya. Aidha, kwa kushirikiana na Chuo Kikuu
Kishiriki Muhimbili, Chuo Kikuu Cha Johns Hopkins na Taasisi ya Magonjwa
ya Kuambukiza ya Atlanta Marekani (Center
for Disease Control, Atlanta)
sehemu kubwa ya mitaala inayotumika kufundishia wataalam wa kada mbalimbali
imepitiwa na kufanyiwa marekebisho ikiwa ni pamoja na mtaala wa Tiba ya Dharura
kwa ajili ya wanafunzi wa udaktari na uuguzi.
65. Mheshimiwa Spika, ninafurahi kulifahamisha
Bunge lako Tukufu kwamba Mafunzo ya Shahada ya Afya ya Mazingira (BSc. Enviromental Health) yameaanza
katika chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi ya Afya (MUCHS). Katika mwaka 2001/2002. Jumla ya wanafunzi 23 wamejiunga
na kozi hiyo. Matarajio yetu ni kwamba wataalam watakaofuzu kozi hiyo
watatuwezesha kukabiliana kikamilifu zaidi na magonjwa yanayotokana na
mazingira duni.
66. Mheshimiwa Spika, kutokana na kuchakaa kwa
majengo ya vyuo vya afya, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2001/2002 wizara
yangu imekamilisha ukarabati wa majengo ya vyuo 17 kwa kutumia
gharama ya shilingi millioni 226.04
67. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa masomo
uliopita wanafunzi katika fani mbalimbali za vyuo vya afya wamehitimu kama
ifuatavyo; waliopata vyeti ni 1,290
waliopata stashahada ni 638 na
waliopata stashahada ya juu 195. Jumla ya wahitimu wote ni 2,123. Aidha idadi ya madaktari imeongezeka na kufikia wahitimu 100 kwa mwaka kutoka vyuo vya Muhimbili
, KCMC, na kutoka vyuo vya nje.
68. Mheshimiwa Spika, katika
kuimarisha huduma za
Wauguzi nchini, Wizara
imefanya mapitio ya mwongozo wa kisera wa Uuguzi na Ukunga ili uweze kukidhi
mahitaji ya maadili mapya ya Uuguzi na mabadiliko ya utendaji wa huduma za afya
pia imeandaa rasimu ya mwongozo wa maadili ya Uuguzi na Ukunga. Rasimu hiyo
imesambazwa katika Mikoa yote kwa ajili ya kupata maoni na mapendekezo zaidi.
Wizara imefanya ukaguzi wa huduma za Uuguzi katika mikoa mitano. Ilikuendeleza huduma
za uuguzi nchini Wizara imeandaa mpango wa kuendeleza huduma hizo kwa kipindi
cha mwaka 2002-2004. Aidha Wauguzi viongozi wa wodi wamefundishwa mbinu za
kufanya utafiti wa kutatua matatizo ya utoaji huduma katika sehemu zao za kazi.
Mafunzo hayo yamefanyika kwa Wauguzi wa mikoa ifuatayo:- Ruvuma, Mtwara, Tanga,
Morogoro, Iringa, Pwani, Dodoma, Tabora, Rukwa na Mbeya.
Ukaguzi wa Huduma za Afya
69. Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha
2001/02, Wizara ya Afya, iliandaa na kusambaza Mwongozo wa Viwango vya Huduma
za Afya (National Norms, Guidelines and Standards on Cross Cutting Issues in
Health Care Practice in Tanzania). Aidha, Kitengo kimeandaa na
kusambaza mwongozo wa uoanishaji wa huduma za afya (Integration of Health Services).
Kitengo pia kilifanya ukaguzi wa utoaji wa huduma za afya katika mikoa 8
ikijumuisha wilaya 17 yaani wilaya 2 kila mkoa kwa mikoa 7 na wilaya 3 katika
mkoa mmoja na kilitoa maelekezo juu ya marekebisho yaliyopasa kufanyika katika
maeneo ambayo matatizo yalijitokeza.
Huduma za Dharura na Maafa
70. Mheshimiwa Spika, Kitengo cha Dharura na
Maafa cha Wizara ya Afya kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2001/2002, kilitembelea
hospitali za mikoa ya Ruvuma, Lindi, Mtwara, Mara, Kagera na Mwanza ili kutoa
ushauri na maelekezo ya kitaalamu kwa ajili ya kuboresha huduma za dharura na
maafa. Hali kadhalika, mafunzo ya huduma za dharura na maafa, yalitolewa kwa
madaktari na wauguzi wa hospitali za rufaa na hospitali za mikoa ya Morogoro,
Pwani, Dodoma, Iringa, Tanga,
Kilimanjaro, pamoja na hospitali za Wilaya za Jiji la Dar-es-Salaam. Kazi
nyingine muhimu zilizokamilshwa ni kama ifutavyo:
·
Watumishi 2 walishiriki katika warsha ya mafunzo ya utoaji huduma za
Dharura na Maafa nchini Msumbiji.
·
Mwongozo wa Utoaji huduma za Dharura na Maafa ulikamilika (Health
Sector Guideline and Protocol on Emergency and Disaster Management).
·
Upembuzi yakinifu (Situation Analysis) katika
hospitali, kuhusu hali halisi ya kukabiliana na Dharura na Maafa hapa nchini
ulifanyika kwa kushirikiana na Shirika la Afya Duniani (WHO) na Shirika la
Misaada la Marekani (USAID) katika hospitali zote za rufaa na za mikoa ya Tanga,
Iringa Pwani , Dodoma na Morogoro.
Taasisi ya Taifa ya Utafiti
wa Magonjwa ya Binadamu
(National Institute for
Medical Research –NIMR)
71. Mheshimiwa Spika, Taasisi imefanya utafiti
kupima uwezo wa dawa ya Amodiaquine katika kutoa tiba ya muda mfupi kwa watoto
wachanga wanaogua ugonjwa wa Malaria kupitia
Mpango wa Taifa wa Chanjo.
Utafiti huu umeendeshwa chini ya mradi wa Presumptive Malaria Intermittent
Treatment in Infants. Matokeo
ya Utafiti huu yameonyesha mafanikio mazuri kwa asilimia kati ya 60 na 70. Hali kadhalika, utafiti juu ya matumizi ya vyandarua vyenye kutiwa dawa ili
kupunguza ugonjwa wa malaria uliendeshwa katika maeneo ya nyanda za juu na vijiji vya Muheza. Matokeo ya utafiti huo yameonyesha kwamba
kiasi cha maambukizo ya vimelea ya malaria kwa watoto wadogo vimepungua kwa
asilimia 16.4 kwa watoto wanaotumia vyandarua hivi.
72. Mheshimiwa
Spika milipuko ya Malaria
inayotokea
mara kwa mara katika Wilaya za Babati, Hanang, Dodoma, Mpwapwa, Muleba na Lushoto inaleta athari kubwa kwa wananchi. Utafiti wa milipuko hiyo katika mkoa wa Dodoma umebaini kuwa milipuko hiyo imekuwa ikiandamana na mvua baada ya kipindi kirefu cha kiangazi pamoja na ongezeko la hali ya joto. Hii imekuwa dhahiri hasa katika wilaya ya Mpwapwa. Utafiti umeonyesha pia kuwa kutokana na takwimu za hali ya hewa inawezekana kabisa kutabiri lini milipuko ya malaria inategemewa kutokea ili matayarisho ya kudhibiti milipuko hiyo yaweze kufanyika. Kufuatia utafiti huu taasisi ilitumia jedwali maalum la kutabiri milipuko ya Malaria katika tarafa ya Kibakwe Wilayani Mpwapwa na imeonekana kwamba kuna uwezekano mkubwa wa kutumia takwimu za hali ya hewa kutabiri milipuko hiyo.
73. Mheshimiwa Spika, mfuko wa utafiti wa Afya (Health
Research User Trust Fund) umeendelea kupata fedha toka Serikalini na
kwa Wahisani. Katika mwaka wa fedha
2001/2002 mfuko uliweza kulipia mada za utafiti zenye
thamani ya shilingi milioni 47.7 Mfuko pia ulitoa tangazo la kuomba miradi mipya ili uweze kuichambua na hatimaye kuipatia fedha. Kufuatia tangazo hilo mada za utafiti 18
zilipokelewa na bado zinaendelea kuchambuliwa.
Taasisi
ya Chakula na Lishe
75. Mheshimiwa Spika, Taasisi pia ilifuatilia
upatikanaji wa chumvi yenye madini joto katika ngazi ya kaya. Mpango huu
huwashirikisha walimu na wanafunzi wa shule za msingi katika kila wilaya.
Walimu wote katika shule zilizoteuliwa hupatiwa mafunzo ya kupima chumvi kama
ina madini joto au la. Taarifa za upatikanaji wa chumvi yenye madini joto
zinawasilishwa Wilayani na ngazi ya kitaifa ili kufanyiwa kazi. Katika kipindi
cha 2001/2002. Mpango huu ulianza kutekelezwa katika wilaya za Rombo, Arumeru,
Monduli na Mpwapwa. Nyingine ni Songea, Mbinga, Ludewa na Makete. Upimaji wa
chumvi uliofanyika katika wilaya hizo ulionyesha kuwa wastani wa asilimia 79 ya
kaya katika maeneo hayo zilikuwa zikitumia chumvi yenye madini joto. Haya ni mafanikio mazuri, lakini bado kuna
kazi ya kuhamasisha matumizi ya chumvi yenye madini joto.
76.Mheshimiwa
Spika, Taasisi pia iliendelea na juhudi
za kudhibiti
tatizo la upungufu wa damu ambalo bado ni kubwa nchini mwetu hasa kwa akina
mama na watoto. Watoto wote wenye umri chini ya miaka mitano wilayani Bagamoyo,
walipewa dawa ya kuongeza damu (ferrous sulphate syrup) pamoja na
vidonge vya kutibu minyoo (mebendazole tablets). Katika
kipindi hicho cha mwaka 2001/2002, Taasisi pia ilisambaza vidonge 65,000,000 vya kuongeza damu
(ferrous sulphate/Folic acid) kwa ajili ya akina mama wajawazito katika
hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa nchini kote. Dawa hizo zilitolewa na
Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF).
77. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, Taasisi
ilipokea mashine 76 za kupimia kiwango cha damu “colorimeters”
kutoka serikali ya Japan. Wataalamu wa maabara 71 kutoka katika
hospitali za wilaya 67 walipata mafunzo kuhusu namna ya kutumia mashine hizo.
Jumla ya hospitali 17 zimekwishapokea mashine hizo nazo ni Tumbi, Kongwa, Hospital ya Rufaa Mbeya,
Tukuyu, Igogwe, Rujewa, Iringa, Makete. Hospitali nyingine ni Ndanda,
Mkomaindo, Lugarawa, Ludewa, Kolandoto, Mwadui, Mugana, Nkinga, na St Francis
ya Ifakara. Hospitali nyingine 59 zilizobaki za wilaya zitapatiwa mashine hizo
katika mwaka wa fedha wa 2002/2003.
78. Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana
na Wizara ya Afya, Shirika la Kuhudumia Watoto Duniani (UNICEF) na Halmashauri za Wilaya saba nchini
imeanza maandalizi ya mpango wa kuzuia
watoto kuzaliwa na uzito pungufu. Wilaya zinazoshiriki katika mpango huu ni
Hai, Magu, Kibaha, Kilosa, Mbarali, Mtwara vijijini na Masasi.
79. Katika kutekeleza mpango huo, mafunzo
yametolewa kwa viongozi 197 wa Wilaya, wajumbe 104 wa kamati za utekelezaji wa
mpango wa wilaya na wafanyakazi 339 wa sekta ya afya kutoka vituo vinavyotoa
huduma ya mama na mtoto katika wilaya hizo.
Mafunzo hayo yalihusu lengo la mpango, jinsi mpango utakavyotekelezwa na
uhamasishaji wananchi ili kushiriki kikamilifu katika utekelezaji mpango. Vile
vile, vifaa na dawa kwa ajili ya mpango zimekwishanunuliwa na tayari usambazaji
umeanza.
80. Mheshimiwa Spika, Taasisi kwa kushirikiana
na Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na Hospitali za Manispaa ya Ilala, Temeke na
Kinondoni imekuwa ikitoa ushauri na ushauri nasaha na elimu ya lishe bora kwa
wagonjwa wa kisukari na shinikizo la damu. Jumla ya wagonjwa 155 walipata
ushauri huo.
81. Mheshimiwa
Spika, katika kuboresha lishe ya wananchi, mradi wa majaribio wa kuongeza
virutubisho kwenye unga wa mahindi umeanzishwa katika tarafa ya Mazombe, wilaya
ya Iringa vijijini. Kupitia mradi huu, virutubisho vya madini na vitamini mbali
mbali vitachanganywa katika unga wa mahindi kwenye mashine za kusagia mahindi
zilizopo kwenye jamii. Mradi huu utasaidia kuboresha afya za wananchi kwenye
eneo hilo, hasa za mama na watoto ambao ni waathirika wakuu wa tatizo la
utapiamlo.
82. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki suala
la lishe na afya bora kwa watoto wachanga limezidi kupewa kipaumbele kwa
kuendeleza mikakati ya kuimarisha unyonyeshaji wa ziwa la mama na ulishaji wa
mtoto. Juhudi zimefanyika kutafsiri maandiko ya kiingereza kwa kiswahili ya
kufundishia stadi za utoaji wa ushauri nasaha juu ya unyonyeshaji na ulishaji
wa watoto kwa wakati huu tunapopambana na gonjwa la UKIMWI. Mafunzo haya yatatolewa kwa watoa huduma za
msingi, wakiwemo wahudumu wa afya na wafanyakazi wengine wa ugani. Aidha, vipeperushi, vijitabu, vijarida na
mabango vimeandaliwa kwa ajili ya kutoa elimu kwa umma kuhusu unyonyeshaji na
ulishaji wa watoto na UKIMWI, Lishe na UKIMWI na ushauri nasaha juu ya kupima
UKIMWI.
83. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya bado
inasisitiza kuwa unyonyeshaji wa ziwa la mama pekee bado ndio njia bora ya
kumlisha mtoto kwa mama ambaye hana maambukizo ya UKIMWI. Kwa mama ambaye amepata maambukizo
awasiliane na wahudumu wa afya kwa ushauri zaidi.
84. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha
2001/2002, Taasisi katika kuendeleza makuzi bora ya mtoto, ilikuwa iongeze
idadi ya hospitali zilizo na sifa ya huduma bora kwa watoto (Hospitali rafiki
wa mtoto) nchini kutoka hospitali za sasa 55 hadi 65. Kutokana na uhaba wa
fedha wa kuthathimini hospitali hizo, lengo hilo halikufikiwa. Kazi hiyo
itafanyika katika kipindi cha 2002/2003 kwenye mikoa ya Arusha, Mwanza na
Kagera.
85. Mheshimiwa Spika, katika mpango wa
kuboresha lishe na afya ya watoto kwa mwaka 2001/2002, Taasisi iliendelea
kuelimisha na kutoa mafunzo kwa vikundi na watu mbali mbali juu ya uboreshaji
wa vyakula vya kulikiza kwa kutumia mchanganyiko wa mazao ya nafaka na mikunde.
Aidha kwa kushirikiana na Taasisi mbalimbali, Taasisi iliendelea na utafiti
kuhusu uboreshaji na upatikanaji wa virutubisho katika vyakula vya kulikiza kwa
kutumia njia zilizo sahihi na rahisi. Lengo la tafiti hizo ni kubaini mbinu za
kuinua kiwango cha hali ya lishe ya watoto ikiwa ni pamoja na kuongeza
upatikanaji wa madini ya chuma na hivyo kuchangia kupunguza tatizo la upungufu wa
damu kwa watoto.
86. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka
2001/2002 Wizara ya Afya kupitia Taasisi yake ya Chakula na Lishe iliendesha
kampeni ya kitaifa ya utoaji matone ya vitamini A kwa watoto wote wenye umri
kati ya miezi 6 na miaka 5 katika mikoa yote ya Tanzania Bara. Kampeni hii
ilifanyika kwa awamu mbili zilizopishana kwa miezi 6 ambapo awamu ya kwanza
ilifanyika sambamba na Siku ya Mtoto wa Afrika tarehe 16 Juni 2001, na awamu ya
pili ilifanyika sambamba na Siku ya Ukimwi Duniani tarehe 1 Desemba 2001.
Katika awamu ya kwanza watoto 4,645,568,
sawa na asilimia 80 ya watoto walengwa
5,842,953 walipatiwa matone ya
vitamini A katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Katika awamu ya pili, watoto 5,285,641, sawa na asilimia 91 ya watoto
walengwa 5,870,822 walipatiwa matone ya
vitamini A katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
Tume ya kudhibiti vyakula ya Taifa (TUKUTA)
87. Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2001/2002
TUKUTA iliendesha
mafunzo kwa Maafisa Afya na Wenye Viwanda kuhusu mfumo makini wa utengenezaji
wa vyakula salama katika wilaya 74 za Tanzania Bara. Maafisa wa Forodha wa
vituo vya mipakani walipewa mafunzo kuhusu taratibu za uagizaji na uingizaji wa
vyakula nchini. Aidha Tume iliandaa rasimu za sheria ndogo za uhifadhi wa vyakula
kwa kutumia mionzi ( Food Irradiation). Ilitoa mafunzo kwa Maafisa Afya wa
mikoa ya kanda ya ziwa kuhusu usimamizi na utekelezaji wa Sheria ndogo ya
Unyonyeshaji na Vyakula vya Kulikiza watoto ya mwaka 1994 katika mikoa yao.
Aidha ilitoa pia mafunzo kwa Maafisa Afya na Madaktari kuhusu uchunguzi na
uratibu wa magonjwa yaeneayo kwa njia ya chakula. Pia Tume iliendesha mafunzo
kwa wazalishaji wa vyakula 92 wenye viwanda vidogo vidogo (Small Scale Food
Producers/Entrepreneurs) kuhusu utengenezaji wa vyakula bora na salama katika
mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Iringa, Tanga, Arusha, Kilimanjaro,
Mwanza na Shinyanga. Kuendesha warsha juu ya usimamizi na utekelezaji wa sheria
ya madini joto. Katika kipindi hiki TUKUTA
ilitoa leseni 163 kwa viwanda vinavyotengeneza vyakula hapa nchini na ilisajili
waagizaji wa vyakula 115.
Bohari Kuu ya
dawa
88. Mheshimiwa Spika,
zoezi la kuteketeza
dawa za
Medical Stores
zilizoharibika kati ya mwaka 1994 hadi 2000 limekamilika. Dawa zenye uzito wa
kilo 193,925 za thamani ya Tshs. 2,734,922,910 ziliteketezwa kwa awamu kuanzia
Juni 2001 hadi Mei 2002. Ili kudhibiti
uharibifu huu usitokee tena, hatua zifuatazo zinachukuliwa; tunafunga mashine
za computer katika Bohari Kuu ya Dawa ambazo zitarahisisha kufahamu mwenendo wa
kiasi na aina ya dawa pamoja na kujua tarehe zake za muda wa kumaliza uwezo wa
kutibu. Aidha tumebadilisha utaratibu wa kuagiza dawa kwa kuwataka wazabuni
kutuletea dawa katika awamu mbili tofauti zinazopishana kwa kipindi cha miezi
sita badala ya kuzileta zote kwa mara moja kama ilivyokuwa hapo awali. Hatua
hizi zitapunguza mlundikano wa dawa na pia kuwezesha Bohari Kuu ya Dawa kuuza
dawa mapema iwezekanavyo kabla ya kwisha muda wake wa uwezo wa kutibu.
Mkemia Mkuu wa Serikali
89.Mheshimiwa Spika,
katika kipindi
cha mwaka
2001/2002 Wakala
wa Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ilipata kiasi cha Tshs 1,183,000,000
kutoka serikalini, nchi wahisani na mikopo kutoka Benki ya Dunia. Fedha hiyo
zilitumika kununulia kemikali, mitambo ya kisasa na vitendea kazi muhimu vya
kufanyia uchunguzi wa kimaabara pamoja na ukarabati wa majengo. Vitendea kazi
hivyo vimewezesha jumla ya sampuli 2849 za dawa, maji, makosa ya jinai, ubora
wa malighafi na bidhaa kufanyiwa uchunguzi.
Bodi ya Madawa
90.Mheshimiwa Spika, Bodi ya
Madawa katika kipindi cha
2001/2002 iliendelea kutekeleza wajibu wake wa kisheria wa kudhibiti shughuli za dawa ikiwa ni pamoja na usajili wa wafamasia, usajili wa dawa, ukaguzi wa viwanda vya madawa na sehemu mbalimbali zitoazo huduma za dawa, uchunguzi wa viwango vya ubora wa dawa yanayoingia na kutumika nchini na pia kutoa ushauri kuhusiana na masuala ya dawa. Hadi kufikia mwezi Desemba 2001 jumla ya dawa 347 zilisajiliwa. Kiasi hiki ni asilimia 65% ya dawa zote zilizo katika orodha ya dawa muhimu nchini. Maabra imeweza kufanya uchunguzi wa dawa aina 308 kati ya hizo asilimia 18.5 ya dawa haikufikia viwango.
91.Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi cha
2002/2003
Wizara ya
Afya imetengewa kiasi
cha shilingi
51,096,671,000 kwa ajili ya utekelezaji wa
Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hii
kiasi cha shilingi 3,552,448,200 ni
kutoka Serikali ya Tanzania na kiasi cha shilingi
47,544,222,800 ni mchango kutoka nchi na taasisi za kimataifa zinazochangia
Mfuko wa Pamoja wa Afya. Taasisi na nchi hizo ni Benki ya Dunia, Serikali za
Uingereza, Uholanzi, Ujerumani, Uswisi, Denmark, Ireland na Norway. Wahisani
hawa wote wanachangia katika Mfuko wa Pamoja ili kuiwezesha Wizara kutekeleza majukumu muhimu yaliyopangwa katika matumizi ya kawaida na miradi ya
maendeleo.
92. Mheshimiwa Spika, fedha hii
imepangiwa kutekeleza shughuli na miradi ambayo ni kipaumbele kwa Wizara ambayo
kwa mwaka 2002/03 inalenga maeneo makuu yafuatayo:
·
Tathmini na usimamizi wa miradi ya maendeleo, ukusanyaji takwimu sahihi
na mafunzo ya muda mfupi kwa timu za wilaya kuhusu mbinu za utafiti wenye
malengo thabiti (Action Oriented Research Methods), shillingi millioni 79.6.
·
Kutoa msaada wa utaalam na uendeshaji wilayani ikiwa ni pamoja na dawa
za chanjo na vifaa vya hospitali, fedha hizi zitatolewa na DANIDA, shillingi billioni 1.9.
·
Wizara katika kuhakikisha kuwa ukarabati wa majengo ya serikali ya
kutolea huduma za afya unafanyika, Mpango wa Maendeleo wa Miaka 10 wa
Kukarabati Hospitali za Wilaya, Mikoa na Rufaa utaandaliwa. Sambamba na mpango huu, Wizara, kwa
kushirikiana na Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB), itafanya upembuzi
yakinifu wa ukarabati wa hospitali za mikoa mitatu ambayo ni Mara, Tabora na
Mtwara. Matokeo ya utafiti huu
yatatumika katika mikoa mingine. Pia
Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili itaanza kufanyiwa ukarabati kwa
kutumia fedha za mkopo wa Benki ya Maendeleo ya Afrika (ADB) na za Serikali ya
Tanzania. Jumla ya shillingi billioni 4.3 zinapendekezwa kutumika.
·
Katika kuimarisha Hospitali za Taifa, fedha zimetengwa ili kukarabati
Wodi za Wazazi hospitali ya Meta/ Mbeya, Jengo la Maabara, Jengo la utawala na
wagonjwa wa nje katika hospitali ya Rufaa Mbeya. Pia ukarabati wa wodi tatu, uzio wa Taasisi maalumu ya Isanga na ukarabati wa majengo ya
kijiji cha wagonjwa wa Akili, pamoja na mfumo wa maji safi hospitali ya Mirembe
utafanyika. Jumla ya shillingi millioni 367.02
zinapendekezwa kutumika kwa kazi hii.
·
Kukamilisha ujenzi wa wodi ya watoto Muhimbili ambayo ni Awamu ya kwanza inayojumuisha ujenzi wa sakafu iliyo
chini ya usawa wa ardhi (Basement
floor), sakafu iliyo usawa wa
ardhi (Ground floor) na sakafu ya kwanza (First Floor). Jumla ya shillingi
millioni 720 zinapendekezwa kutumika kwa kazi hii. Ujenzi wa awamu ya
pili ambayo ni sakafu ya pili na ya tatu utaanza kufanyika katika mwaka
2003/2004.
·
Hospitali ya Mifupa – Muhimbili Orthopaedic Institute (MOI)
imetengewa jumla ya shillingi millioni 850 ikiwa ni mchango wa Serikali ya Tanzania
katika kukamilisha ujenzi wa Chumba cha Wagonjwa Mahututi (ICU), Maabara ya Benki ya Damu, vyumba vya Xray na upasuaji wa
moyo (Open Heart Surgery).
.
·
Taasisi ya Saratani (Ocean
Road Cancer Institute) imetengewa jumla ya shillingi millioni 900 kwa ajili ya kubadilisha na kufanya
matengenezo makubwa ya mashine ya uchunguzi wa magonjwa ya saratani, pamoja na
ununuzi wa mashine nyingine mpya.
·
Wakala wa Mkemia Mkuu wa Serikali imetengewa jumla ya shillingi
millioni 590.5 kwa ajili ya kununua na kufunga vifaa vya maabara,
kuendeleza ujenzi wa maabara ya kudhibiti ubora wa dawa nchini (Drug
Quality Control Laboratory) na kufanya upembuzi yakinifu ili kuweza
kuanzisha maabara ya Kanda Mwanza.
·
Uzuiaji wa magonjwa ya kuambukiza umetengewa jumla ya shillingi
billioni 8.3 kwa ajili ya kugomboa toka bandarini na kusambaza dawa za
Kifua Kikuu na Ukoma, kampeni za kitaifa juu ya taarifa, elimu na mawasiliano
kuhusu malaria, kununua dawa ya kuzuia mazalio ya mbu pamoja na kujenga uzio
kuzunguka majengo ya Mpango wa Taifa wa Chanjo na ukarabati wa ofisi na mfumo
wa umeme majengo ya Elimu ya Afya kwa Umma.
·
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR)
imetengewa jumla ya shillingi millioni 387.4 kwa ajili ya kuanzisha kituo kipya cha
ugunduzi na uendelezaji wa dawa za asili Mabibo, ukarabati wa majengo ya vituo
vya utafiti Mwanza, Gonja, Amani, Bombo, Muheza pamoja na mchango wa Serikali
katika Mfuko wa Utafiti (Research Users Trust Fund).
·
Kuendelea na uanzishwaji wa Mfuko wa Afya ya Jamii katika wilaya
nyingine 20 na kufanya majaribio ya Mfuko wa Afya ya Jamii Mijini, ujulikanao
kama Tiba kwa Kadi (TIKA), Jumla ya shillingi billioni 1.9 zinapendekezwa
kutumika kwa kazi hii.
·
Kuendelea kuupatia fedha Mfuko wa Bima ya Afya ili uweze kuelimisha
wadau wote kuhusu mfuko huo, kuhamasisha watoa huduma za afya, kulipia pango la
ofisi, kuanzisha ofisi za kanda na kununua vitendea kazi kwa ajili ya
kutunza takwimu za mfuko, Jumla ya shillingi
billioni 1.3 zinapendekezwa kutumika katika kazi hii.
·
Kuendelea kuhamasisha umma wa Tanzania kuhusu mabadiliko yanayofanyika
katika sekta ya Afya katika ngazi zote pamoja na kuimarisha huduma za afya
Wilayani kwa kuzipatia zana, dawa na vifaa mbalimbali vya hospitali shillingi
billioni 28.8 zinapendekezwa kutumika kwa kazi hii.
·
Katika kuimarisha utoaji wa mafunzo ya Afya, vyuo vya afya 26 vilivyo
katika hali mbaya vitafanyiwa ukarabati wa majengo, Jumla ya shillingi
millioni 730.8 zinapendekezwa kutumika kwa kazi hii..
Udhibiti wa magonjwa ya kuambukiza
93. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hiki
Wizara yangu itaendelea kupambana na magonjwa yanayoenezwa na wadudu wanaoruka,
wasioruka, pamoja na wanyama (vectors and vector borne diseases)
kwa kutoa kozi fupi zinazohusu njia
mbalimbali za kudhibiti magonjwa haya kwa wafanyakazi wa afya wapatao 40 kutoka
mikoa inayoathirika mara kwa mara. Aidha ufuatiliaji wa ugonjwa wa kichaa cha
mbwa pamoja na matumizi ya chanjo ya kichaa cha mbwa utafanyika katika
mikoa kumi na moja ya Tanzania Bara.
Mpango
wa chanjo wa Taifa
94. Mheshimiwa Spika, kampeni ya chanjo ya
Polio na Surua itaendelea tena mwaka huu 2002/2003 katika baadhi ya wilaya. Kwa
chanjo ya Polio, Wilaya 16 zitakuwemo katika kampeni na kwa chanjo ya Surua
Wilaya 82 zenye wagonjwa wengi zitahusishwa.
Kutokana na zoezi la kuhesabu idadi ya watu (Sensa) litakalofanyika nchi
nzima mwezi Agosti, kampeni za chanjo zitafanyika mwezi wa Oktoba kwa chanjo ya
kwanza ya Polio na mwezi Novemba kwa chanjo ya pili ya Polio pamoja na Surua.
95. Mheshimiwa Spika, mwaka huu wa fedha Wizara
yangu itafunga majokofu 720 yanayotumia gesi katika Mikoa ya Ruvuma, Iringa,
Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza, Mara na Kagera kwa kutegemea upatikanaji wa
fedha za kununulia majokofu toka fedha za Wizara zilizotengwa kwa ununuzi huo
pamoja na msaada toka Serikali ya Japan.
Mradi wa Taifa wa Kudhibiti Malaria
96. Mheshimiwa spika, mtazamo wa sasa wa kutibu
magonjwa kama malaria, TB na UKIMWI ni kutumia dawa zaidi ya moja (dawa mseto)
Faida ya dawa mseto ni kwamba huboresha tiba na pia hupunguza kuzuka kwa
vimelea sugu. Wizara yangu imeanza kutafiti mseto wa dawa utakaofaa kutibu
malaria ambao katika miaka michache ijayo utaanza kutumika rasmi badala ya dawa
za sasa za mstari wa kwanza. Katika mpango wa utekelezaji wa mwaka 2002/2003
Wizara yangu inakusudia kuendelea kutoa mafunzo kwa wataalamu mabalimbali wa
afya juu ya udhibiti sahihi wa malaria katika wilaya zote 32 zilizo katika
awamu ya tatu ya utekelezaji wa mpango wa mabadiliko wa utoaji huduma za afya
nchini. Aidha uhamasishaji juu ya utumiaji wa vyandarua vilivyo tiwa dawa
utafanyika nchi nzima. Utafiti wa usugu wa vimelea vya malaria na tiba mseto
utaendelea kufanyika.
Mpango
wa Taifa wa Kudhibiti Kifua Kikuu na Ukoma
97. Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha 2002/03, Wizara
itaendelea kuimarisha utafiti katika mikoa yote ya Tanzania Bara na
Visiwani ili kubaini kiwango cha uambukizo wa Kifua Kikuu katika jamii. Tayari
mikoa 11 imeshafanyiwa utafiti huu. Matarajio ni kukamilisha mikoa yote ya
Tanzania ifikapo mwaka 2004. Kwa upande wa ugonjwa wa Ukoma, mikoa mingine
miwili itaingizwa katika kampeni za kutokomeza ugonjwa huu ambayo ni Dar es
Salaam na Rukwa. Matarajio ni kupanua
kampeni hizi katika mikoa yote hapa nchini kwa awamu. Aidha wananchi na
watumishi wa afya katika mikoa hiyo watapewa elimu zaidi ya kutambua dalili za
ukoma katika jitihada ya kutokomeza ugonjwa huu.
Huduma ya Afya ya Uzazi Mama na Mtoto
98. Mheshimiwa
Spika, katika kuimarisha huduma za Afya ya Mama na Mtoto, Wizara imepanga kutoa
mafunzo ya huduma za dharura kwa wazazi (emergency
obstetric care) kwa kufundisha waalimu wa waalimu 12 kitaifa, na
waalimu 84 (kila mkoa waalimu wanne). Hawa watatumika kufundisha wafanyakazi
katika hospitali, vituo vya Afya na Zahanati njia bora za kutoa huduma ya
dharura wakati wa uzazi. Vile vile
wafanyakazi wa afya wanotoa huduma za mama na mtoto 234 katika mikoa ya Kagera,
Ruvuma, Tabora, Shinyanga, Rukwa, Singida na Kigoma, watapata mafunzo rejea
kuhusu uzazi wa mpango na uzazi salama ili kuboresha huduma hizo. Aidha, Wizara
itaendelea kununua na kusambaza dawa na vifaa vya uzazi wa mpango nchi nzima kwa kushirikiana na wahisani. Pia vipeperushi, vielelezo na mabango mbali
mbali yanayotoa ushauri kuhusu maswala ya Afya ya uzazi mama na mtoto yatachapishwa
na kusambazwa katika vituo vya kutolea huduma za afya na ofisi mbalimbali za
serikali za mitaa nchi nzima ili kuwaelimisha wananchi na kuwahamasisha kutumia
hudumia hizi. Sambamba na mipango hii, Wizara ya Afya itaandaa Mkakati wa
Kitaifa wa Kuboresha Afya ya Uzazi na Mtoto awamu ya pili 2003 – 2007.
Mpango wa Taifa wa Kudhibiti
UKIMWI
99. Mheshimiwa
Spika, Mkakati wa Kitaifa wa Kudhibiti UKIMWI wa mwaka 1998-2002 ( MTP III)
umemaliza muda wake wa utekelezaji. Mkakati huo ulikuwa umetoa dira kwa wadau wote kuhusu vipaumbele na mikakati ya kuzingatia katika
mapambano ya UKIMWI kwa kipindi cha miaka mitano iliyopita. Wizara yangu sasa
imeanza maadalizi ya kuandaa mpango
mpya wa miaka mitatu utakaoendeleza mapambano katika sekta ya afya. Mpango huu utakuwa wa kwanza tangu ianzishwe
Tume ya Taifa ya Kudhibiti UKIMWI (TACAIDS)
na utazingatia majukumu mapya ya sekta ya afya kama tulivyokubaliana na TACAIDS. Mkazo
mkubwa utaelekezwa kwenye suala la kuongeza huduma zilizothibitika kuwa ni bora
kwa kudhibiti UKIMWI na kujenga uwezo wa sekta katika kumudu majukumu yake
katika udhibiti wa UKIMWI. Mkakati huu
utaweka vile vile utaratibu wa kutoa ushauri kwa sekta nyingine pamoja na
kuziwezesha halmashauri za wilaya kutekeleza majukumu yao.
100. Mheshimiwa Spika, shabaha ya kuelimisha na
kuhamasisha jamii itambue matatizo yake ya kiafya iko palepale. Wizara yangu
inalenga katika kuwapa wananchi mbinu mbali mbali za kubadili tabia na mitindo
ya maisha inayoathiri afya zao. Aidha lengo lingine ni kuiwezesha jamii
kupanga, kutekeleza na kutathmini mipango ya kuzuia na kudhibiti magonjwa.
Katika kipindi cha 2002/2003 Kitengo cha Elimu ya Afya kitaweka mkazo katika
kuimarisha kamati na bodi za Wilaya
katika kubuni na kutayarisha vielelezo bora vya afya kulingana na sehemu zao.
Kitengo pia kitalenga katika kuziwezesha wilaya katika kupanga na kutathimini
utoaji wa elimu ya afya.
Mpango
wa Taifa wa Kudhibiti Ugonjwa wa vikope (trachoma) na Usubi (onchocerciasis)
101.Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2002/2003,
Wizara ya Afya inatarajia kutibu watu 700,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa
usubi. Ukilinganisha na idadi ya wagonjwa 338,886 waliotibiwa mwaka 2000/2001
na wagonjwa 624,290 waliotibiwa mwaka 2001/2002. Gharama za kutibu wagonjwa hao
zinakadiriwa kuwa shillingi
millioni105.7. Aidha kuhusu ugonjwa wa vikope katika kipindi hiki
Wizara inatarajia kuongeza juhudi za kudhibiti ugonjwa huu kwa kutumia mbinu
ijulikanayo kama SAFI yaani (Sawazisha
kope, Anza
matibabu mapema, Fanya usafi wa mwili, na Imarisha
mazingira) kutoka vijiji 150 vya sasa hadi kufikia vijiji 204.
Mradi wa Uimarishaji wa
Huduma Muhimu za Afya
102.
Mheshimiwa Spika, Mradi wa
Uimarishaji wa Huduma Muhimu za Afya, umekuwa chombo cha kutusaidia kufanya majaribio
ya matumizi ya rasilimali mbalimbali katika sekta ya afya na jinsi rasilimali
hizo zinavyoweza kuongeza ufanisi na ubora wa huduma za afya .Matokeo ya
majaribio hayo yaliyofanyika kuanzia mwaka 1995 yamepatikana. Matokeo hayo
yamewezesha kuandaa miongozo ya jinsi ya kupata viwango vya magonjwa vya
wilaya, hali ya matumzi ya afya ya wilaya, hali ya huduma za afya wilayani na
mfumo wa taarifa za afya wilayani.
Katika mwaka wa fedha wa 2002/2003 mradi utashughulikia kuandaa
utaratibu utakaowezesha miongozo hiyo kutumika katika wilaya nyingine.
HUDUMA ZA TIBA
103 Mheshimiwa
Spika, Jumla ya fedha zilizotengwa kwa ununuzi na usambazaji wa dawa na vifaa
katika mwaka wa fedha wa 2002/2003 ni shilingi bilioni 16.2. Ingawa kuna ongezeko la shilingi bilioni
1.5 ikilinganishwa na Shilingi bilioni
14.7 za mwaka uliopita, bado ongezeko hilo halikidhi
mahitaji halisi ya vituo vya kutolea huduma. Hii inatokana na kupanda kwa bei
ya dawa na vifaa kwani asilimia 80 ya dawa na vifaa vinanunuliwa kutoka nje na
gharama yake inategemea thamani ya shilingi kwa fedha za kigeni.
104. Mheshimiwa
Spika, zahanati na vituo vya afya vitaendelea kupewa kipaumbele kupata dawa kwa
kuzingatia kwamba vituo hivyo vipo vijijini ambapo wananchi hawana sehemu
nyingine za kupata huduma ya afya kama ilivyo mijini. Hivyo, zahanati na vituo
vya afya vitapelekewa masanduku ya dawa (drug kits) kila mwezi. Ili
kuboresha upatikanaji wa dawa na vifaa katika zahanati na vituo vya afya, mfumo
wa uagizaji kulingana na mahitaji (Indent
System) utatumika katika halmashauri 16 ambazo
zimeanzisha Mfuko wa Afya wa Jamii (Community
Health Fund). Chini ya mfumo huo, Serikali itatoa
fedha sawa na thamani ya makasha ya dawa (drug kits) na Mfuko wa Afya wa
Jamii utatoa fedha kugharimia dawa na vifaa vya ziada kukidhi mahitaji halisi
vya vituo hivyo. Halmashauri 6 ambazo
ni Monduli, Mbulu, Karatu, Masasi, Mtwara Mjini na Vijijini zitaanza kutekeleza
mfumo huo wakati Halmashauri nyingine 10 zitaandaliwa katika mwaka wa fedha
2002/2003.
105.
Mheshimiwa Spika, katika kuboresha
upatikanaji wa
dawa katika hospitali za wilaya, teule, mikoa na rufaa,
mfumo wa mfuko wa dawa, unaowezesha hospitali hizo kununua dawa kulingana na
fedha zinazopatikana na mauzo ya dawa hizo (Capitalization of Hospital Pharmacies) utaimarishwa kwa kuzipatia hospitali hizo vitendea kazi
vya kudhibiti matumizi ya dawa na makusanyo ya fedha kutokana na uchangiaji wa
huduma ya afya. Pia watumishi katika hospitali hizo watapewa mafunzo ili
kufanikisha udhibiti wa dawa na makusanyo ya fedha. Fedha itakazokusanywa chini
ya mfumo huo itatumika kununua dawa na vifaa vya ziada.
106. Mheshimiwa
Spika, Wizara ya Afya kwa kushirikiana na Shirika la Kimataifa la Maendeleo la
Marekani (USAID) chini ya Mpango wa Ushirikiano wa Japani na Marekani (Japan – USA Common Agenda) itandaa mfumo wa ugavi (Integrated Logistics System)
ambao utatumika kufuatilia uagizaji na usambazaji wa dawa na vifaa katika Sekta
ya Afya ili kupima uwiano wa uagizaji na matumizi halisi. Mfumo huo utakapokamilika
utaunganishwa na Mfumo wa Taarifa za Dawa (Medical Stores
Management Information System). Chini ya
mfumo huo, zahanati, vituo vya afya na hospitali zitatakiwa kuonyesha salio la
dawa na vifaa vilivyopo, wakati wa kuagiza vitu hivyo kutoka Bohari Kuu ya
Dawa. Salio la kila dawa na kifaa
vitaingizwa kwenye mtandao wa kompyuta kubaini kama uagizaji wa dawa na vifaa
unaendana na matumizi halisi katika vituo vya kutolea huduma ya afya. Mfumo huo
unatarajiwa kurahisisha ukusanyaji wa takwimu za uagizaji, usambazaji na
matumizi ya dawa na vifaa na hivyo kuboresha mfumo wa upatikanaji wa dawa na
vifaa nchini na vilivile kudhibiti wizi na ubadhirifu.
Huduma za
Uchunguzi wa Magonjwa
107. Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha mwaka 2002/2003, Wizara ya Afya itaendelea na
uimarishaji wa upatikanaji wa damu salama na ya kutosha kwa wagonjwa kwa
kukamilisha taratibu za uanzishaji wa Huduma ya Kitaifa ya Damu Salama (National Blood Transfusion Services). Aidha, huduma ya
damu salama itaanzishwa katika Kanda ya Nyanda za juu Kusini chini ya hospitali
ya Rufaa Mbeya kwa kutoa mafunzo ya wataalamu wa kutoa ushauri nasaha na
kuhamasisha wananchi kujitolea damu.
Mafunzo hayo yatagharamiwa na Shirika la Maendeleo la Umoja wa
Mataifa (UNDP). Mpango huo utatekelezwa sambamba na
ukarabati wa majengo na ununuzi wa vifaa vya kutolea huduma ya damu salama
katika kanda zote nne zinazosimamiwa na hospitali za rufaa za Muhimbili, Mbeya,
KCMC na Bugando. Taasisi ya Kudhibiti Magonjwa ya Marekani (CDC)
imetenga jumla ya dola za marekani milioni 2.0
kwa ajili ya ukarabati na ununuzi wa vifaa hivyo.
.
108. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka huu wa fedha, Wizara ya Afya itaendelea kukamilisha
ufungaji wa mashine za X-ray
na Ultrasound katika hospitali za
wilaya na mikoa iliyokuwa bado kuwekewa
mitambo hiyo. Mikoa hiyo ni Mwanza, Mara, Shinyanga, Kagera, Kigoma na
Tabora. Aidha, karakana za kutengeneza
vifaa vya kutolea huduma za afya zilizoko kwenye hospitali za KCMC, Bugando, Muhimbili, Mbeya na Mtwara
zitaimarishwa kwa kupatiwa vifaa na magari (Mobile Maintenance Workshop Vehicles) ili viwe na uwezo wa kutengeneza mashine za X-Ray
na Ultrasound.
109. Mheshimiwa
Spika, Mwongozo wa kisera wa Vifaa vya Kitaalamu vya Kutolea Huduma za Afya “Policy Guidelines for Heath Care Technology” ulioandaliwa mwaka 2001/2002 utaanza kutekelezwa kwa
majaribio katika hospitali nne za Rufaa (Muhimbili, Bugando, KCMC na Mbeya) na
katika hospitali mbili za Mkoa (Kagera na Tanga). Aidha, mpango ya kufanya na
kufuatilia matengenzo ya kinga (Planned
Preventive Maintenance) kwa kutumia utaalamu
wa kompyuta utaanzishwa katika hospitali hizi.
Wizara inatarajia kujifunza kutokana na uzoefu utakaopatikana katika
hospital hizi ili uenezwe katika hospitali zote za mikoa na wilaya. Aidha, kwa kushirikiana na Kamisheni ya
Huduma za Jamii za Kikristo na Baraza kuu la Waislam Tanzania, huduma hizi
zitaenezwa pia katika hospitali zinazomilikiwa na mashirika ya dini.
Huduma za Afya
ya Kinywa
110. Katika
kipindi cha 2002/2003 Wizara yangu inakusudia kununua vifaa vya tiba ya meno
kwa ajili ya hospitali za Halmashauri zifuatazo; Arumeru, Rombo, Manyoni,
Kibaha, Bagamoyo, Kilosa, Makete, Mufindi, Mpanda, na Tunduru. Pia madawa muhimu kwa ajili ya tiba ya meno
yatanunuliwa na kusambazwa katika kliniki za meno mikoani na wilayani. Aidha, katika kuimarisha kinga ya magonjwa
ya kinywa, vijitabu, mabango na vipeperushi vitatayarishwa kwa ajili ya
kufundishia afya ya kinywa kwenye kliniki za mama wajawazito na watoto wenye
umri chini ya miaka mitano nchini.
Huduma za Afya
ya Akili na Madawa ya Kulevya
111. Mheshimiwa
Spika, Wizara imekusanya taarifa zinazohusu masuala ya afya ya Akili kutoka
mikoa ya Kigoma, Mbeya, Morogoro, Mtwara, Pwani, Shinyanga Singida na Tabora.
Taarifa hizo zitachambuliwa na kutolewa ripoti katika mwaka wa fedha 2002/2003.
Tunategemea kuwa mchanganuo wa taarifa hizo utasaidia katika kufanya mapitio na
Miongozo ya Sera ya afya ya akili nchini. Pia shughuli za kusimamia na
kuendeleza mafunzo ya stadi za kukabiliana na maradhi ya akili zitaimarishwa
katika mikoa ya Arusha, Kilimanjaro, Tanga, Dodoma, Mbeya, Mwanza, Mtwara na
Dar es Salaam
Huduma ya Tiba
za Asili
112. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa 2002/2003 Wizara ya Afya itaandaa mkakakati na mpango wa
muda mrefu wa kuimarisha na kufanya utafiti wa huduma za tiba za asili na tiba
mbadala. Wadau mbalimbali
watahamasishwa na kutakiwa kuchangia maendeleo ya sekta hii. Aidha rasimu ya
muswada wa sheria itakayosimamia masuala ya dawa na tiba ya asili imekamilika
na inatarajiwa kuwasilishwa katika Bunge lako tukufu katika mwaka wa fedha wa
2002/2003.
Hospitali za
Rufaa
113. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa 2002/2003 Wizara ya Afya imetenga shilingi
bilioni 15.0 kwa ajili ya ruzuku kwa hospitali za
rufaa, hospitali teule za wilaya na hospitali za mashirika ya dini. Kati ya fedha hizo shilingi bilioni
13.8 zitatolewa na serikali wakati shilingi bilioni 1.6 zitatolewa na mfuko wa pamoja wa sekta ya
afya. Aidha, hospitali za rufaa, na hospitali za mikoa zimetengewa shilingi milioni 198.0
kwa ajili ya kupanua mpango wa kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka
kwa mama kwenda kwa mtoto. Aidha shilingi bilioni 1.4 zimetengwa kwa kuendeleza mabadiliko ya uendeshaji wa
huduma za hospitali na shilingi milioni 996.0 kwa ajili ya ukarabati na ununuzi wa vifaa vya kutolea
huduma za afya.
Hospitali ya Taifa Muhimbili
114. Mheshimiwa
Spika, uimarishaji wa Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kipindi cha mwaka
2002/2003 utalingana na mwelekeo mpya wa uendeshaji wa hospitali. Hata hivyo
mipango iliyokuwepo kabla ya mabadiliko inatarajiwa kuendelezwa. Kati ya
mipango hii ni pamoja na kuendeleza ujenzi wa wodi ya watoto kufikia ghorofa ya
pili. Pia utekelzaji wa awamu ya kwanza
ya ukarabati mkubwa wa majengo ya hospitali, njia za umeme na njia za
mawasiliano unaogharamiwa na mkopo kutoka Benki ya Maendeleo ya Afrika utaanza
mapema katika mwaka wa fedha 2002/2003.
Hospitali ya Rufaa ya KCMC
115. Mheshimiwa
spika, sambamba na mabadiliko yanayoendelea katika sekta ya afya hospitali ya
KCMC imefanya mabadiliko yenye lengo la kuongeza ufanisi. Katika mabadiliko
haya hospitali inatarajia kuweka viwango vya utekelezaji wa wafanyakazi ili
kila mmoja apimwe utendaji wake kufuatana na viwango hivyo. Hospitali pia
inatarajia kuajiri mafundi sanifu wa maaabara wa kutosha ili kuleta ufanisi
katika huduma inayo tolewa na maabara.
Kwa upande wa menejimenti hospitali inatarajia kuendesha warsha kwa
ajili ya viongozi katika ngazi mbalimbali ili kuongeza uwezo wa watumishi na
kuwezesha utawala bora.
Taasisi ya Saratani ya Ocean Road
116 Mheshimiwa
Spika, Ili Taasisi ya Saratani iweze
kuyamudu majukumu yake ya kutibu wagonjwa wa Saratani ambao wamekuwa
wakiongezeka mwaka hadi mwaka, katika mwaka huu wa fedha Taasisi itanunua
mitambo mipya ya mionzi ambayo thamani yake ni shilingi
milioni 250.0
na mashine mpya ya matibabu ya saratani
ya thamani ya shilingi milioni 400.0.
Hospitali ya Bugando
117 Mheshimiwa
Spika, Hospitali ya Bugando imeazimia kupunguza matatizo ya nyumba na usafiri
yanayo wakabili watumishi wake. Hivo,
hospitali imeazimia kujenga nyumba mbili kila mwaka kwa ajili ya wafanyakazi
katika maeneo ya Hospitali. Pia katika
mwaka 2002/2003 hospitali itanunua basi moja kwa ajili ya wafanyakazi. Kwa upande wa huduma za wagonjwa, hospitali
itajenga wodi maalum kwa ajili ya matatizo ya uzazi (V.V.F) kwa kuwa wagonjwa wa
tatizo hili wamekuwa wengi na hakuna wodi maalum ya kuwalaza wagonjwa wa aina
hii. Pia Hospitali ya Bugando
itaanzisha sehemu ya wagonjwa mahututi ambao wanahitaji uangalizi wa karibu
sana kama vile wagonjwa wanaotoka upasuaji mkubwa. Katika eneo la mafunzo
hospitali ya Bugando inatarajia mwezi septemba mwaka huu kufungua mafunzo ya
shahada ya udaktari wa matibabu chini ya Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino.
Taasisi ya Mifupa ya
Muhimbili (Muhimbili Orthoaepadics Institute)/MOI
118.
Katika kipindi cha mwaka 2002/2003, MOI inatarajia kukamilisha ujenzi wa awamu ya pili ya MOI na inatarajiwa
kufunguliwa rasmi mwezi Septemba 2002. Kukamilika kwa awamu hii kutaifanya MOI
kuwa Taasisi na hospitali yenye hadhi ya kipekee hapa nchini na hata Afrika
Mashariki na Kati katika kutoa huduma kwa kutumia teknolojia ya kisasa. Ujenzi
wa awamu ya pili unajumuisha huduma zifuatazo:
·
Chumba cha upasuaji kwa dharura (Emergency Theatre).
·
Vyumba vinne vya upasuaji (theatres) vyenye teknolojia ya kisasa.
·
Vyumba viwili kwa ajili ya wagonjwa mahututi (Intensive Care Unit),
vyenye vitanda nane.
·
Chumba cha upasuaji wa moyo (open heart surgery theatre) chenye
teknolojia ya kisasa.
·
Maabara, Chumba cha kutunzia damu , X-ray na sterilization.
·
Wodi ya vitanda 17 kwa ajili ya wagonjwa binafsi (private patients).
·
Vyumba vya Ofisi za wafanyakazi.
·
Karakana ya umeme na mitambo mingine ya hospitali.
Hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Isanga
119.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2002/2003, Hospitali itaendelea
kutoa huduma zake kwa wagonjwa wa afya ya akili pia Wizara inakusudia
kuendeleza ukarabati wa hospitali ya Mirembe na Taasisi ya Isanga kwa
kukarabati wodi tatu za hospitali ya Mirembe na kujenga uzio wa ukuta katika
Taasisi ya Isanga. Na kumalizia ukarabati wa mfumo wa Safi na maji taka.
Hospitali ya Kibong’oto
120.
Mheshimiwa Spika, katika
mwaka 2002/2003
Hospitali ya
Kifua Kikuu itafanya tathmini ili kulinganisha mahitaji, gharama na faida
itakayopatikana kwa kubadili muundo na mfumo wa utoaji huduma kulingana na
mpango wa mabadiliko ya sekta ya Afya.
Aidha Hospitli ya Kibong’oto itatekeleza mpango wa kuinua ubora wa
huduma zinazotolewa kwa kutoa mafunzo kwa watumishi, kukarabati majengo,
kununua vifaa vya kutolea huduma na kuimarisha mkakati dhidi ya ukimwi. Wizara ya Afya imetenga Jumla ya Shs. 357
milioni kwa ajili ya shughuli hizi, ambapo Shs. 220 milioni ni kutoka bajeti ya
Serikali na Shs. 137 milioni ni kutoka mfuko wa pamoja wa wahisani.
Huduma
za hospitali, Vituo vya Afya, Zahanati na Maduka ya dawa ya watu binafsi
121.
Mheshimiwa Spika, Wizara inathamini mchango wa hospitali, Vituo vya
Afya, Zahanati na maduka ya dawa ya watu binafsi katika kutoa huduma kwa
wananchi. Hadi sasa kuna jumla ya hospitali 125 Vituo vya Afya 137 Zahanati
1537 na maduka ya dawa ya Part I 520 yaliyosajiliwa na Msajili wa Hospitali
Binafsi pamoja na Msajili wa Bodi ya Madawa. Katika kuimarisha ushirikiano
uliopo baina ya Sekta Binafsi na Wizara,Wizara imekuwa ikiwaalika wawakilishi
wa Chama Cha Wenye Kumiliki Hospitali binafsi katika mikutano mbalimbali ya
kujadili maendeleo ya sekta hii kama vile mapitio ya utekelezaji wa mipango ya
maendeleo ya sekta ya afya yanayofanyika kila mwaka pamoja na kumteua
mwakilishi wa Chama hicho katika Bodi ya Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa. Wizara
inakusudia pia kupunguza muda wa kutoa leseni baada ya kupokelewa maombi kutoka
wastani wa siku zaidi 120 hadi 30. Aidha Wizara itaongeza idadi ya ukaguzi wa
huduma hizi ili kuzifanya ziwe bora zaidi.Wizara inatoa shukurani nyingi kwa
watu binafsi ambao wamesaidia kusogeza huduma za afya kwa wananchi. Tunawaomba
wananchi katika siku zijazo kuendelea kufungua huduma hasa zile za matibabu
maalumu kama vile ya upasuaji wa moyo, ubadilishaji wa figo na kadhalika. Ili watu
waweze kutibiwa ndani ya nchi. Serikali inaahidi kuimarisha na kuongeza
ushirikiano uliopo baina yake na sekta ya watoa huduma za matibabu binafsi.
HUDUMA
ZA UTAWALA NA UTUMISHI
122.Mheshimiwa Spika, Wizara
ya Afya imetenga fedha
kiasi cha shilingi milioni 897.5 za kununua
magari kwa
ajili ya
usimamizi ambayo yatagawanywa katika halmashauri zifuatazo; Arumeru , Korogwe,
Handeni, Kwimba, Mtwara, Nzega, Musoma, Rungwe, Mbarali, Ukerewe, Pangani,
Kilosa, Kibaha, Arusha, Mbinga, Bukoba, Same, Mbeya, Mwanga, Dodoma, Mafia,
Kisarawe, Mufindi, Tarime, Morogoro, Mbozi, Geita, Nachingwea, Misungwi,
Kinondoni, Igunga, Makete, Kibondo, Temeke, Sikonge na Ilala. .Magari hayo
yatasaidia kuongeza usimamizi na ufuatiliaji wa huduma za afya wilayani Aidha,
Wizara itaendelea na zoezi la kuwapandisha vyeo watumishi wa sekta ya Afya.
Katika mwaka wa fedha wa 2002/2003, Wizara inatarajia kuwapandisha vyeo watumishi 10,000.
123.
Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2002/2003 huduma ya
mafunzo ya watumishi wa sekta ya afya imepanga kutekeleza mambo muhimu
yafuatayo;_
·
Kuendelea kukarabati vyuo vingine 20 ilikuboresha
majengo ya kufundishia.
·
Kuendesha mafunzo ya menejimenti kwa wilaya arobaini
na moja zilizobali (41) ili kuzipa uwezo wa wa kiutendaji na utekelezaji wa
huduma zinazotolewa.
·
Kununua magari matano mengine kwa ajili ya vyuo
ilikuboresha mafunzo kwa vitendo kwa kuwawezesha wanafunzi kufika sehemu za
mazoezi.
·
Kuendesha kozi mbili za mafunzo ya menejimenti kwa
madaktari wanaohitimu inter doctors)
kabla ya kupangiwa vituo.
·
Kununua vitabu na vijarida kwa ajili ya maktaba vyuo
thelasini (30).
·
Kutoa mafunzo ya kujiendeleza kwa walimu 48
ilikuinua uwezo wao wa ufundishaji katika vyuo.
·
Kuendelea kupitia upya mitaala minane zaidi ili
iendane na mahitaji ya wakati uliopo na mabadiliko ya kisekta yanayoendelea.
OFISI
YA MGANGA MKUU KIONGOZI
Huduma
za Uuguzi
124.Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha mwaka wa
fedha wa
2002/2003, Wizara inatarajia kufanya usimamizi wa huduma za uuguzi katika mikoa
tisa. Pia Wizara, itafanya utafiti wa jinsi huduma za uuguzi zinavyopokelewa na
wananchi na ubora wa huduma za uuguzi. Utafiti huu utafanyika katika mikoa
mitatu itakayochaguliwa hapo baadaye, kufuatana na miongozo ya uchaguzi wa
sampuli za utafiti. Wizara pia imekubali kuwa mwenyeji wa Mkutano Mkuu wa
wauguzi wa nchi kumi na nne ambao ni wanachama wa Chuo Kikuu cha Wauguzi wa
Afrika Mashariki, Kati na Kusini (ECSACON).
125.Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha fedha
cha
2002/2003 Wizara
imepanga kutekeleza kazi zifuatazo;
kufanya ukaguzi wa utoaji huduma za afya katika mikoa 8 ikiwa inajumuisha
wilaya 16 yaani wilaya 2 kila mkoa, kutathmini ubora wa huduma za afya zinazotolewa katika jamii ya
Tanzania na kuendelea kusambaza mwongozo wa viwango vya utendaji kazi katika
huduma za afya nchini.
Huduma za Dharura na Maafa
126.
Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha mwaka
2002/2003, Kitengo kinakusudia
kufanya kazi
zifuatazo; kutembelea mikoa
12 ya Tanzania Bara na baadhi ya wilaya zake kwa lengo la kufanya ufuatiliaji
na usimamizi wa huduma za afya za maafa, ili kutoa ushauri na maelekezo ya
kitaalam katika kuboresha huduma hizo nchini. Vilevile,kitakamilisha mwongozo
wa utoaji huduma za Dharura na Maafa (Health Sector Guideline and Protocol on
Emergency and Disaster Management) na kuusambaza katika vituo vyote vya
huduma nchini. Kitengo pia kitatoa mafunzo ya Tiba ya Dharura na Maafa kwa
wanafunzi Madaktari na Wauguzi wa Chuo Kikuu Kishiriki cha Muhimbili, kwa
kutumia mitaala maalumu iliyoandaliwa kwa ushirikiano na Taasisi ya Magonjwa ya
kuambukiza cha CDC (USA), Chuo Kikuu cha John Hopkins (USA) na Chuo Kikuu cha
Muhmbili.
TAASISI, TUME NA BODI ZILIZOPO CHINI YA
WIZARA YA AFYA
Taasisi
ya Chakula na Lishe Tanzania
127. Mheshimiwa
Spika, kwa mwaka wa fedha 2002/2003,
kampeni
za utoaji wa matone ya vitamini A kwa watoto wote wenye umri wa miezi 6 hadi
miaka 5 katika mikoa yote ya Tanzania bara.
Sambamba na utoaji wa matone ya vitamini A, Taasisi itaendelea na
kuhamasisha viongozi na jamii kuhusu umuhimu wa uzalishaji na ulaji wa vyakula
vyenye vitamini A kwa wingi ikiwa ni hatua ya kudumu ya kuzuia na kudhibiti
matatizo yatokanayo na upungufu wa vitamini A kwa jamii yote ya Tanzania.
128.Mheshimiwa
Spika, Taasisi vilevile, itaendelea na
usambazaji wa
machine za kupimia damu katika Wilaya 59 zilizobaki na kusimamia utoaji wa dawa
za kuongeza damu na kutibu minyoo kwa watoto wenye umri chini ya miaka mitano wilayani Bagamoyo.
Aidha, Taasisi itaendelea na mikakati ya kuboresha vyakula vya kulikiza pamoja
na vile vya watoto walioathirika na ukimwi na makundi mengine maalum. Taasisi
pia itaendelea kutoa mafunzo na kuelimisha vikundi na watu mbalimbali juu ya
uboreshaji wa vyakula vya kulikiza kwa kutumia teknolojia rahisi na
kuandaa mwongozo wa utengenezaji wa
vyakula kwa makundi maalum.
129.Mheshimiwa Spika,
Taasisi itaelekeza juhudi
zake
katika kueneza
teknolojia rahisi ya usindikaji na hifadhi
ya mhogo, viazi
vitamu, mboga na matunda na kuhamasisha
jamii kuhusu umuhimu wa kutumia chakula kwa uangalifu ili kuhakikisha
upatikanaji katika ngazi ya kaya kwa mwaka mzima. Vile vile Taasisi kwa
kushirikiana na Taasisi husika itaendelea kufuatilia usalama na ubora wa
vyakula vinavyotumika humu nchini.
Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa
Magonjwa ya Binadamu
130.Mheshimiwa Spika,
katika kipindi cha
mwaka
2002/2003 Taasisi
imepanga kutoa dawa
za kuzuia
ugonjwa wa
matende na ngiri maji kwa wananchi wa wilaya zote ili kuhakikisha kuwa hakuna
mwananchi atakaye athirika kwa ugonjwa wa matende na ngiri maji ifikapo mwaka 2020.
Hali kadhalika, ili kuimarisha
shughuli za utafiti taasisi itapatiwa msaada wa kujenga majengo mapya ya ofisi
na kuyavunja yale ya zamani. Msaada huu
utatolewa na Center for Disease Control ya Marekani na Serikali imepanga
kuchangia shilingi milioni 10.0 kwa
ajili ya ujenzi wa maabara na ofisi za taasisi
tawi la Tukuyu. Aidha, Taasisi imetayarisha mradi utakaochangia ujenzi
wa kituo cha Centre for Enhancement of Malaria Intervention (CEEMI), Joint Malaria
Programme na ofisi za National Malaria Control Program. Mradi unafadhaliwa na Bill and Melinda Gates
Foundation kupitia London School of Hygine and Tropical Medicine. Mfadhili ametoa ahadi kutoa msaada zaidi kwa
ajili ya ujenzi wa Malaria Reference Laboratory katika hospitali ya Bombo, Tanga.
Bodi ya Madawa
131.Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2002/2003, Bodi ya
Madawa itaendelea
na ufuatiliaji wa usalama wa dawa
kwenye soko kwa
kuzingatia utaratibu wa usajili wa dawa ambao umekuwepo kuanzia mwaka
1998. Katika zoezi hili dawa za
malaria, Kifua Kikuu na zile zinazosaidia kupunguza makali kwa wagonjwa wenye
virusi vya ukimwi zitapewa kipaumbele.
Bodi ya Madawa inalenga kukabiliana na tatizo la uingizaji nchini wa
dawa zisizofikia viwango na dawa bandia ambazo zinaaminika kuingizwa kwa
kupitia njia za zisizohalali au kwa udanganyifu. Bodi pia ina malengo ya
kuelimisha wananchi juu ya matumizi sahihi ya dawa na jinsi ya kuweza kupata
huduma ya uhakika ya dawa.
132.Mheshimiwa Spika,
ili Bodi ya
Madawa iweze
kukabiliana na matatizo haya, Bodi imejiwekea mkakati wa kutimiza malengo muhimu yafuatayo:
·
Kuongeza idadi ya wakaguzi katika ngazi mbalimbali hususan katika
mipaka na kanda zake za ukaguzi .
·
Kufanyia ukaguzi wa mara kwa mara wa maduka ya dawa.
·
Kuimarisha maabara ya uchunguzi wa dawa kwa kuongezea vifaa vya kisasa
na wataalam.
·
Kwa kushirikiana na taasisi nyingine za Serikali, Bodi ya Madawa
itaimarisha mikakati ya kukabiliana na tatizo la madawa ya kulevya:
133.Mheshimiwa Spika, Wizara
ya Afya iko katika hatua
za mwisho za
kuunganisha Bodi ya Madawa na Tume
ya Taifa ya
Kudhibiti Ubora wa Vyakula ili kuunda chombo madhubuti cha kudhibiti biashara
ya dawa, chakula na vipodozi. Ili
kutimiza azma hiyo, Sheria Na. 9 ya Dawa na Sumu na Sheria Na. 10 ya Kudhibiti
Ubora wa vyakula zote za mwaka 1978, zitafutwa na kuunda sheria mpya itakayosimamia
udhibiti wa vyakula, dawa na vipodozi. Muswada wa sheria hiyo umekwishasomwa
kwa mara ya kwanza Bungeni. Aidha
masuala ya usimamizi wa maadili ya fani ya famasia yatasimamiwa na Baraza la
Famasia ambalo litafanya kazi zake chini ya Sheria mpya ya Famasia ya mwaka
2002.
Maabara
ya Mkemia Mkuu wa Serikali:
134.
Mheshimiwa Spika Ofisi ya Maabara ya Mkemia Mkuu wa Serikali ni mojawapo ya wakala za serikali zilizo chini
ya Wizara ya Afya. Katika mwaka wa fedha wa 2002/2003, Ofisi ya Mkemia Mkuu wa
Serikali itaendelea na kazi za uchunguzi wa sampuli mbalimbali kwa nia ya kutoa
vidhibiti mahakamani na kuhakikisha usalama wa bidhaa mbalimbali zinazotumiwa
na binadamu. Ilikuwezesha wakala hii kufanya kazi zake vizuri ipasavyo. Wizara
imepanga kujenga chumba cha kuteketezea kemikali zilizoharibika na kufunga
mashine itakayofanya kazi hiyo (Incinerator). Kununua mashine ya kuzalisha
umeme pamoja na kujenga chumba cha kuifunga mashine hiyo. Kuweka mfumo wa
kuzuia moto. Kuweka mfumo wa mashine za kupoza hewa katika ofisi zote. Kufanya
utafiti wa jinsi ya kuanzisha maabara za kanda.
Tume
ya kudhibiti vyakula ya Taifa (TUKUTA)
135.
Mheshimiwa Spika, hata baada ya TUKUTA kuunganishwa na Bodi ya Madawa
kazi zilizopangwa kutekelezwa mwaka huu zitaendelea kutekelezwa chini ya
Taasisi mpya kama ifuatavyo:- Kuendelea kutoa mafunzo kwa Maafisa Afya na wenye
viwanda kuhusu mfumo makini wa utengenezaji vyakula salama na bora katika
wilaya zote za Tanzania Bara. Kutoa mafunzo kwa Maafisa Afya kuhusu namna ya
kutumia mwongozo wa kitaifa wa ukaguzi wa viwanda vya chakula. Kutayarisha
miongozo kuhusu mfumo wa usajili wa majengo ya kuuzia na kutengenezea vyakula
na utoaji wa leseni. Kufanya ukaguzi wa vyakula katika mikoa 21 ya Tanzania
Bara. Kuchunguza kiwango cha masalio ya madawa na kemikali nyingine mbalimbali
katika vyakula. Kuendelea kufanya utafiti juu ya athari zinazoweza kumpata
mlaji kutokana na vifaa mbalimbali vya kufungia vyakula, ikiwemo mifuko ya
plastiki. Kukusanya na kutafiti viwango vya madawa katika nyama na mazao
yatokanayo na maziwa.
Mfuko wa Taifa wa Bima ya
Afya
136.
Mheshiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha Wizara yangu inakusudia
kuimarisha Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kwa kuupatia fedha za kutoa elimu kwa
wanaonufaika na Mfuko huo. Kuwawezesha kuanzisha Ofisi za Kanda. Kuwapatia
vitendea kazi iliwaweze kushughulikia madai ya hospitali kwa haraka
iwezekanavyo. Aidha, Wizara inaandaa mapendekezo ya marekebisho ya sheria
iliyounda Mfuko huo iliiweze kutatua matatizo yaliyojitokeza wakati wa
utekelezaji wa Mfuko huo.
Nchi
na Mashirika kutoka nje
137.
Mheshimiwa Spika, katika
kipindi cha mwaka 2001/ 2002 sekta ya afya imeendelea kupata ushirikiano mkubwa
kutoka nchi za nje na mashirika ya kimataifa. Ushirikiano huo ulilenga zaidi
katika maeneo ya mabadiliko ya sekta ya afya, uboreshaji huduma, ununuzi wa
dawa na vifaa, ukarabati wa majengo na masomo ya nchi za nje. Nchi hizo na
mashirika mbalimbali tuliyoshirikiana nayo ni:- China, Cuba, Canada, Denmark,
Hispania, India, Ireland, Italia,
Japan, Korea ya Kusini, Marekani, Misri, Norway, Switzerland, Sweden, Uholanzi,
Uingereza, Ufaransa, Ujerumani, , Benki ya Dunia , Benki ya Maendeleo ya
Afrika, Benki ya Nchi za Kiarabu kwa ajili ya Maendeleo ya Kiuchumi ya Nchi za
Afrika ( BADEA), OPEC, Jumuia ya Nchi za Ulaya (EU), Shirika la Afya
Ulimwenguni (WHO), Shirika la kuhudumia Watoto
(UNICEF), Shirika la Kimataifa la Uzazi wa Mpango (UNFPA), UNAIDS,
Shirika la Kimataifa la kuhudumia Wakimbizi (UNHCR) na Madaktari Wasio na
Mipaka, (Medicins Sans Frontieres),
MISERIOR, African Programme for Onchorcerciasis Control, Hellen Keller
Foundation na International Trachoma Initiatives, Bill & Melinda Gates
Foundation, Abott Laboratories, Axios International, Merck, Pfizer Inc. Wizara
ya Afya inatoa shukrani za dhati kwa nchi na mashirika yote yanayoendelea
kushirikina nasi katika kuinua afya ya Watanzania.
138. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Afya ina furaha
kulifahamisha Bunge lako Tukufu kuwa
hapa nchini sekta ya afya inayo pia washiriki wengi.Ingawaje sitaweza kuataja
washiriki wote, napenda kutoa shukrani za dhati kwa mashirika yafuatayo:-
Shirika la Aga Khan, AMREF, BAKWATA, CCBRT, TAC AIDS, CCT, CSSC, ELCT, TEC,
Msalaba Mwekundu, Shree Hindu Mandal na TANESA na mashirika yote yasiyo ya kiserikali
yanayoshirikiana na Wizara. Kwa ushirikiano wao katika kukuza sekta ya afya.
139.Mheshimiwa Spika,
naomba nimalizie hotuba yangu kwa kutoa shukrani zangu za dhati kwa viongozi wa
Wizara ya Afya, Mheshimiwa Dk. Hussein Alli Mwinyi, Mb. Naibu Waziri wa Afya,
Mbunge wa Mkuranga, Ndugu Mariam Joy Mwaffisi, Katibu Mkuu, Dk. Gabriel Upunda,
Mganga Mkuu Kiongozi, Wakurugenzi wa Idara Wizara ya Afya, Wakurugenzi wa
Hospitali za Rufaa na Taasisi za Afya na Waganga Wakuu wa Mikoa Wilaya na
wafanyakazi wote wa sekta ya Afya popote walipo. Ushirikiano wao wa karibu
ndiyo ulioiwezesha Wizara kupiga hatua kubwa ya maendeleo katika kipindi chote
cha mwaka uliopita. Vilevile nawashukuru na kuwapongeza wafanyakazi wote wa
sekta ya afya popote pale walipo kwa kuendelea na moyo wa uadilifu katika
kuwatumikia wananchi. Nina waomba waendelee kuzingatia maadili yao ya kazi hii
nyeti. Nachukua pia nafasi hii kuwashukuru wananchi wa jimbo la Lulindi
walioniwezesha kupata nafasi hii ya kulitumikia taifa.
140. Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Wizara ya
Afya kutekeleza hayo niliyoyaeleza naliomba Bunge lako Tukufu litafakari,
lijadili na kuidhinisha Makadirio ya Wizara ya Afya ya jumla ya shillingi 103,100,021,600 kati ya hizo shillingi 52,003,350,600, ni kwa ajili ya Matumizi
ya Kawaida na shilingi 51,096,671,000 kwa
ajili ya Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2002/2003. Kati ya fedha ya maendeleo shilingi 3,552,448,200 ni fedha ya ndani na shilingi 47,544,222,800 ikiwa ni fedha kutoka nje ya nchi.
141.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.
Kiambatanisho Na.1
KIREFU
CHA MAJINA YA MASHIRIKA YA KITAIFA NA KIMATAIFA YANAYOSAIDIA HUDUMA ZA AFYA.
ADB = African
Development Bank
AMREF = African
Medical and Research Foundation
BAKWATA = Baraza Kuu la
Waislam Tanzania
CBM = Christoffel
Blinden Mission
CCT = Christian
Council of Tanzania
CSSC = Christian
Social Services Commission
CUAMM = International
College for Health Cooperation
in Developing Countries
DANIDA = Danish
International Development Agency
DFID = Department
For International Development
DSE = Deutsche
Stiftung fur Internationale
Entwicklung
ELCT = Evangelical
Lutheran Church of Tanzania
EU = European
Union
FINNIDA = Finnish
International Development Agency
GSF = Good
Samaritan Foundation
GTZ = Gesellschaft
fuer Technische Zusammenarbeit
IDRC = International
Development Research Centre of
Canada
JICA = Japan
International Cooperation Agency
NBC = National
bank of Commerce
NIMR = National
Institute of Medical Research
NORAD = Norwegian
Agency for Development
NSSF = National
Social Security Fund
SAREC = Swedish
Agency for Research Cooperation in
Developing Countries
SDC = Swiss
Agency for Development and
Cooperation
SIDA = Swedish
International Development Authority
TAMWA = Tanzania
Media Women Association
TANESA = Tanzania
Netherlands Support to AIDS control
TANESCO = Tanzania Electric
Supply Company
TBL = Tanzania
Breweries Limited
TEC = Tanzania
Episcopal Conference
TPDC = Tanzania
Petroleum Development
Corporation
TRA = Tanzania
Revenue Authority
TTCL = Tanzania
Telecommunication Company
Limited
UNDP = United
Nations Development Programme
UNFPA = United
Nations Fund for Population Activities
UNHCR = United
Nations High Commission for Refugees
UNICEF = United Nations
Children Fund
USADEFU = Usambara
Development Fund
USAID = United
State Agency for International
Development
WHO = World
Health Organisation
Kiambatanisho Na. 2
Wanafunzi waliohitimu katika
Vyuo vya Wizara ya Afya kwa Mwaka 2001
|
Na. |
KADA |
IDADI |
|
1. |
Stashahada ya Juu Uuguzi (Afya ya Jamii) |
20 |
|
2. |
Stashahada ya Uuguzi |
403 |
|
3. |
Cheti cha Uuguzi |
522 |
|
4. |
Cheti cha Uuguzi/Ukunga |
408 |
|
5. |
Uuguzi Afya ya Jamii (B) |
197 |
|
6. |
Maafisa kumbukumbu za Afya |
15 |
|
7. |
Mafundi Sanifu Maabara
Wasaidizi |
108 |
|
8. |
Mafundi Dawa Wasaidizi |
18 |
|
9. |
Mafundi wa Eksrei
Wasaidizi |
10 |
|
10 |
Tabibu |
235 |
|
11. |
Wazoeza Viungo
(Physiotherapists) |
9 |
|
12. |
Fundi Mewani (Optometry) |
12 |
|
13. |
Madaktari Wasaidizi (AMO) |
165 |
|
14. |
Madaktari Wasaidizi (Meno) |
8 |
|
|
JUMLA |
2,130 |
Kiambatanisho Na. 4
Orodha ya Wilaya ambazo zitaanza mpango wa kuagiza dawa na vifaa vya hospitali kulingana na Mahitaji (indent system).
1. Igunga+
2. Nzega+
3. Iramba+
4. Singida(V)+
5. Hanang+
6. Kilosa+
7. Iringa(V)+
8. Songea(M)+
9. Songea(V)+
10. Mbinga+
11. Babati*
12. Monduli*
13. Simanjiro*
14. Kiteto
15. Masasi*
16. Ulanga
17. Hai*
18. Karatu*
19. Mufindi
20. Njombe
21. Mtwara(V)*
22. Kisarawe
23. Kasulu
24. Mbulu*
25. Mwanga
26. Sumbawanga(V)
27. Tandahimba*
28. Arusha Munispaa*
29. Rombo*
Mtiririko
wa wagonjwa wa Ukoma, Tanzania:2000 - 2001
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||||||||||
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|
|||||||||
|
Mkoa |
|
2000 |
|
|
2001 |
|
|
2002 January - March |
|
||||||||||
|
|
|
Wapya |
Waza mani |
Jumla |
Wapya |
Waza mani |
Jumla |
Wapya |
Waza mani |
Jumla |
|
||||||||
|
Arusha |
PB + MB |
17 |
2 |
19 |
3 |
2 |
5 |
2 |
0 |
2 |
|
||||||||
|
Dar es salaam |
PB + MB |
370 |
43 |
413 |
385 |
46 |
431 |
117 |
6 |
123 |
|
||||||||
|
Dodoma |
PB + MB |
144 |
18 |
162 |
206 |
29 |
235 |
41 |
8 |
49 |
|
||||||||
|
Iringa |
PB + MB |
28 |
5 |
||||||||||||||||