Hotuba ya Waziri wa Elimu na Utamaduni

Mhe. Joseph J. Mungai (MB) Kuhusu Makadirio

ya Matumizi ya Fedha kwa Mwaka 2004/05

 

I.                   UTANGULIZI

1.         Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu baada ya kuzingatia taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii lijadili na kupitisha makadirio ya matumizi ya kawaida na ya maendeleo ya Wizara ya Elimu na Utamaduni kwa mwaka wa fedha 2004/05.

 

2          Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kuwapongeza Mhe. Getrude Mongella, Mbunge wa Ukerewe, kuwa Rais wa Bunge la Afrika, Mhe. Dkt. William Shija, Mbunge wa Sengerema, Mhe. Dkt. Amani W.A. Kabourou, Mbunge wa Kigoma Mjini, Mhe. Dkt. Remigius Edington Kissassi, Mbunge wa Dimani Zanzibar na Mhe. Athumani Janguo, Mbunge wa Kisarawe kwa kuchaguliwa kuwa Wabunge wa Bunge la Umoja wa Afrika.  Aidha, nawapongeza Mhe. Sophia Simba, Mbunge wa Viti Maalum na pia Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Maendeleo ya Jamii kwa kuteuliwa kuiwakilisha Tanzania katika Baraza la Wabunge wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC).  Nampongeza Mhe. Arcado Ntagazwa, Mbunge wa Muhambwe, kwa kuchaguliwa kuwa Rais wa Baraza la Kimataifa la Mazingira.  Pia nawapongeza, Mheshimiwa Makongoro Nyerere, kwa kuteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mbunge na Mheshimiwa Danhi Makanga, Mbunge wa Jimbo la Bariadi Mashariki kwa ushindi aliopata katika uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 30 Mei 2004.  Napenda kutoa pole kwako wewe binafsi Mheshimiwa Spika na Bunge lako tukufu kwa kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini na Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu Mheshimiwa Yte Mwalyego.  Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi.  Aidha nawapa pole Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda, Mbunge wa Handeni na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mipango na Ubinafsishaji), pamoja na Mhe. Dkt. Aisha O. Kigoda, Mbunge Viti Maalumu kwa msiba wa kufiwa na baba yao mzazi.  Mhe. Dkt. Laurence M. Gama (Songea Mjini) na Mhe. Parmukh Singh Hoogan (Kikwajuni) kwa kufiwa na watoto wao, pia natoa pole kwa Wabunge wengine waliopata mikasa ya ajali wakati wakija Bungeni - Dodoma.

 

            Mheshimiwa Spika, naomba kutumia nafasi hii ya mwanzo kuwapongeza na kuwashukuru; (a) Mheshimiwa Dkt. Abdallah Kigoda (MB), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji kwa hotuba yake ambayo imetoa tathmini, mwenendo na mwelekeo wa uchumi wa Taifa kwa jumla; na (b) Mheshimiwa Basil Pesambili Mramba (MB), Waziri wa Fedha, kwa hotuba yake iliyofafanua kwa ufasaha Bajeti ya Serikali ya mwaka 2004/05 ambayo imetoa kipaumbele kwa sekta muhimu katika kukuza uchumi ikiwemo Sekta ya Elimu ambayo inao wajibu mkubwa katika Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU) na kuboresha ufanisi wa nguvu kazi ya taifa kwa njia ya elimu.  Aidha, namshukuru Mheshimiwa Waziri Mkuu katika Hotuba yake ya bajeti kwa kufafanua mambo muhimu ya elimu yaliyoamuliwa na Serikali, na kwa uamuzi na maagizo yake kuhusu madai ya walimu.

 

3.         Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, inayoongozwa na mwenyekiti wake Mheshimiwa Omar S. Kwaangw’ Mbunge wa Babati Mashariki kwa kutoa ushauri na maelekezo ya kuboresha Bajeti na utekelezaji wa Wizara ya Elimu na Utamaduni baada ya uchambuzi wa kina.   

 

Majukumu ya Wizara

4.                  Mheshimiwa Spika, Wizara ya Elimu na Utamaduni imeendelea kuwa na majukumu yake kama nilivyoeleza katika hatouba ya bajeti ya mwaka 2003/2004.  Majukumu hayo ni kusimamia na kuendesha:

(a)      Elimu ya Msingi na Elimu ya Awali

(b)      Elimu ya Sekondari ya Kawaida (Ordinary Level): Kidato cha 1 hadi 4; na Elimu ya Sekondari ya Juu (Advanced Level): Kidato cha 5 hadi 6

(c)      Elimu Maalumu (Special Education) itolewayo kwa wenye ulemavu kama vile wasioona, viziwi, wenye ulemavu wa akili, n.k.

(d)      Elimu ya Watu Wazima (Adult Education) ikiwa ni pamoja na utoaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari kwa mfumo usio rasmi kwa watoto na watu wazima walioikosa.

(e)      Utamaduni wa Taifa ikiwemo Lugha, Sanaa, Mila na Desturi na Ukaguzi wa Filamu.

(f)        Mafunzo ya Ualimu Daraja A na Stashahada (Diploma).

(g)      Ukaguzi wa Shule katika ngazi zote (Elimu ya Awali hadi Kidato cha 6) na Vyuo vya Ualimu.

(h)      Kupanga na kuratibu mipango yote ya elimu kuanzia Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu.

(i)        Taasisi na Mabaraza yaliyo chini ya Wizara ambayo ni:

                                          (i)            Taasisi ya Elimu Tanzania (TET);

                                        (ii)            Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW);

                                       (iii)            Baraza la Mitihani Tanzania (BAMITA);

                                      (iv)             Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA);

                                        (v)            Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA);

                                      (vi)            Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (BOHUMATA) na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).

 

Katika kutekeleza majukumu hayo Wizara inaongozwa na (a) Sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978; (b) Sera ya Elimu na Mafunzo; (c) Sera ya Utamaduni; (d) Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025; (e) Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU); na (f) Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2000 ya Chama Tawala cha CCM.  Ili kuhakiki ubora wa elimu itolewayo katika shule zote nchini, Wizara huendesha ukaguzi wa shule na hutoa mitihani ya kitaifa ya Darasa la IV, VII; Vidato vya 2, 4 na 6 na mitihani ya Elimu ya Ualimu.

 

II.                UTEKELEZAJI WA MIPANGO YA MWAKA 2003/04

NA

MALENGO YA MWAKA 2004/05

5.                  Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mipango ya Wizara yangu kwa Mwaka 2003/04 na malengo ya mwaka 2004/05 kwa kila Idara, Taasisi na ngazi ya elimu ni kama ifuatavyo:

 

A:      Idara ya Elimu ya Msingi

Malengo Maalumu ya Elimu ya Msingi

6.       Mheshimiwa Spika, Idara ya Elimu ya Msingi inayo Malengo Maalum yafuatayo:

(a)           Kurejesha Elimu ya Msingi kwa Wote (Universal Primary Education - UPE) yaani kwa kuwaingiza Darasa la Kwanza kila mwaka watoto wote wa miaka 7 na kuwaendeleza mpaka wahitimu Darasa la VII kwa kuzingatia Kifungu Na. 35 cha Sheria ya Elimu Na. 25 ya mwaka 1978 kama kilivyorekebishwa na Sheria Na.10 ya mwaka 1995.

(b)          Kuongeza asilimia ya rika la Elimu ya Msingi (miaka 7-13) waliomo shuleni kutoka 57% mwaka 2001 hadi 95% mwaka 2005.

(c)           Kupunguza kasi ya kuacha shule (Drop Out Rate) kutoka 6.6% kwa mwaka hadi 3.0 % kwa mwaka ifikapo 2005 katika kila shule.

(d)          Kuboresha Elimu ya Msingi kutoka waliofaulu 22 % mwaka 2000 hadi zaidi ya 50% mwaka 2005.

(e)           Kuongeza wahitimu wa Darasa la VII wanaoingia Sekondari kutoka 19.5% mwaka 2000 hadi 50% mwaka 2010.

 

6.         Mheshimiwa Spika, mwaka 2003/04 shughuli za Elimu ya Msingi zimeongezeka ifuatavyo:

 

6.1     Shule za Awali zimeongezaka 2,753 kutoka 6,948 hadi 9,701 ambalo ni ongezeko la 39.6%.

6.2     Shule za Msingi zimeongezeka 884 kutoka 12,649 mwaka 2003 hadi 13,533 mwaka 2004 sawa na ongezeko la 7%; na Wanafunzi wameongezeka kwa 8% kutoka 6,562,772 mwaka 2003 hadi 7,083,063 mwaka 2004 ambayo vilevile ni 61.6% ukilinganisha na wanafunzi 4,382,410 mwaka 2000 Bunge hili lilipochaguliwa.

6.3     Walimu 14,261 wameajiriwa.

6.4     Wanafunzi 196,273 sawa na 40.1% waliofaulu Mtihani wa Darasa la VII mwaka 2003 wameongezeka kwa 62,599 sawa na 46.8% kutoka 133,674 mwaka 2002.

 

Kielelezo Na. 6:  Matokeo ya Mtihani ya DVII 1998 – 2003

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TANBIHI:        Alama ya kufaulu mwaka 2003 ilikuwa 85/200, badala ya 65/150 baada ya kuongezwa somo la nne.

 

Nawapongeza sana Maafisa Elimu,Walimu Wakuu na Walimu wote wa Shule za Msingi kwa mafanikio hayo.

 

(i) Mafanikio ya Mwaka wa Tatu wa MMEM

7.         Mheshimiwa Spika, mafanikio ya utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) 2002-2006 ni kama ifuatavyo:

 

7.1    Mwaka 2004 watoto 1,368,315 waliandikishwa Darasa la I sawa na 83.4% ya kulinganisha na lengo la 1,640,969 wakiwemo wavulana 697,594 na wasichana 670,721.  Kati yao shule za Serikali zina watoto 1,361,446 na shule binafsi watoto 6,869.

7.2    Jumla ya wanafunzi katika shule za msingi mwaka 2004 ni 7,083,063. ikilinganishwa na 6,562,772 mwaka 2003 ambalo ni ongezeko la wanafunzi 520,291 sawa na 8.0%.

Kielelezo 7.1:  Wanafunzi wa DI na DI-VII Kulinganisha na

Idadi ya Watoto wa Miaka 7-13 [2000-2004]

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

7.3         Kwa mujibu wa takwimu zilizooneshwa katika Kielelezo 7.1

(a)      Wanafunzi wa rika la elimu ya msingi (miaka 7-13) walioko shuleni (Net Enrolment Ratio – NER) imeongezeka kutoka 58.8% mwaka 2000 hadi 90.5% mwaka 2004.  Kwa hiyo malengo yaliyokuwa yamepangwa ya kufikia NER ya 77% na GER ya 85% yaliyomo katika Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU) kwa mwaka 2003 yamevukwa.

(b)     Wanafunzi wote shuleni kama asilimia ya idadi ya watoto wa rika lengwa (Gross Enrolment Ratio – GER) imeongezeka kutoka 77.6% mwaka 2000 hadi 106.3% mwaka 2004.

(c)      Mikoa ya Lindi, Morogoro, Kigoma, Dodoma, na Tabora haijafikia kiwango cha GER ya asilimia 100 ambayo ni hatua ya lazima ingawaje si ya kutosha kabla ya kufikia Elimu ya Msingi kwa Wote.


 

Kielelezo 7.2:   Mikoa kwa (GER) Katika Shule za Msingi Kama % ya Idadi

ya Watoto wa Rika la Elimu ya Msingi: Miaka 7-13 [2004]

Mkoa

Idadi ya Watoto Miaka 7- 13

Wanafunzi Darasa 1-V11

GER

NER

1.        Mara

289,901

366,307

126.2

100.0

2.        Ruvuma

216,082

257,950

119.4

99.3

3.        Mbeya

411,670

488,131

118.6

99.3

4.        Kilimanjaro

298,704

345,885

115.8

100.0

5.        Mwanza

596,045

689,735

115.7

99.5

6.        Tanga

341,054

387,514

113.6

97.9

7.        Iringa

318,046

359,418

113.0

99.1

8.        Pwani

165,323

184,687

111.7

94.5

9.        Mtwara

190,773

209,622

109.9

94.2

10.     Dar es Salaam

386,121

419,590

108.7

93.1

11.     Manyara

209,724

224,673

107.1

89.5

12.     Singida

228,952

242,586

106.0

85.0

13.     Kagera

417,192

431,729

103.5

86.8

14.     Arusha

256,240

264,930

103.4

91.9

15.     Rukwa

234,903

242,313

103.2

87.9

16.     Shinyanga

588,946

594,253

100.9

86.3

17.     Lindi

140,446

139,401

99.3

84.1

18.     Morogoro

336,658

329,528

97.9

81.9

19.     Kigoma

355,092

328,440

92.5

77.2

20.     Dodoma

335,920

301,770

89.8

76.3

21.     Tabora

347,549

274,601

79.0

68.2

Jumla

6,665,341

7,083,063

106.3

90.5

 

7.4    Walimu 14,261 wameajiriwa hadi 30 Juni, 2004 sawa na asilimia 91.8% ya lengo la walimu 15,533 waliotarajiwa kuwa wameripoti na kuanza kazi.

7.5    Walimu Tarajali wanaochukua mafunzo ya Ualimu Daraja A ni 10,788, ikilinganishwa na lengo la mwaka 2004 la wanachuo 10,000.

7.6    Ruzuku ya Maendeleo ya shilingi 1,185,000,000 imetolewa na Serikali Kuu kwa Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vya madarasa, nyumba za walimu na ununuzi wa madawati.  Albaki ya Shilingi 65,742,120,600 ya Ruzuku ya Maendeleo itatolewa wakati wowote kutokana na mchango wa Wahisani ili kukamilisha malengo ya mwaka 2003/04.

7.7    Ruzuku ya Uendeshaji ya shilingi 56,172,632,210 ilitolewa kwa Halmashauri kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada, penseli, kalamu, chaki na madaftari, vivunge vya sayansi (Science kits), matengenezo na mitihani ya ndani ya shule na shughuli za utawala ngazi ya shule. Kiwango hiki ni sawa na shilingi 7,930.55 kwa kila mwanafunzi. Albaki ya shilingi 14,762,862,790 sawa na shilingi 2,069.45 kwa mwanafunzi zitatumwa kwa Halmashauri wakati wowote baada ya kuzipokea kutoka kwa wahisani.

 

Utekelezaji wa Miradi ya Elimu ya Msingi

8.         Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04 utekelezaji wa miradi mingine ya Elimu ya Msingi uliendelea kama ifuatavyo:

 

8.1    Mradi wa Lishe Shuleni

Mradi huu unaendeshwa kwa ushirikiano na Shirika la Mpango wa Chakula Duniani yaani World Food Programme (WFP)” na utaendelea hadi mwaka 2006 katika mikoa ya Arusha, Dodoma, Singida na Manyara ambapo wilaya 11 zipo katika mpango huu.  Lengo la mpango huu ni kutoa chakula kwa shule za msingi zinazowasomesha watoto wa jamii zinazohamahama kama vile wafugaji, wanaoishi kwa kuwinda, kula matunda na kurina asali.


Wilaya za Mradi wa Lishe Shuleni

(1) Monduli; (2) Ngorongoro; (3) Simanjiro; (4) Kiteto; (5) Dodoma [V];  (6) Kondoa; (7) Mpwapwa; (8) Singida [V]; (9) Iramba; (10) Manyoni, (11) Karatu. Jumla ya shule 230 zinanufaika na mpango huu zikiwemo 10 za bweni na 220 za kutwa. Aidha, jumla ya wanafunzi 99,511 wananufaika na mpango huu. Kati ya hao wavulana ni 52,697 na wasichana ni 46,814.

 

8.2    Mradi wa Shule Zenye Mazingira Yanayomjali Mtoto Child Friendly School Project (CFS)” unatekelezwa kwa msaada wa UNICEF katika Wilaya 11 zifuatazo:

 

Shule Zenye Mazingira Yanayomjali Mtoto

(1) Kisarawe; (2) Masasi;(3) Songea [V]; (4) Musoma [V]; (5) Ngara; (6) Magu; (7) Mufindi; (8) Hai; (9) Ilala; (10) Kinondoni na (11) Temeke. Utafiti wa awali [Baseline Survey] na majadiliano na Jamii [Community Dialogue] ulifanyika na kukamilika katika Wilaya 5 (1) Kisarawe; (2) Masasi; (3) Songea [V];  (4) Musoma [V]; na (5) Ngara. Aidha, uchapishaji wa zana ya upimaji wa utekelezaji wa  shule zinazomjali mtoto umekamilika, semina kwa walimu  60 toka wilaya za Kisarawe na Masasi zimefanyika.

 

8.3         Mradi wa Uboreshaji wa Elimu Ngazi ya Kata (UBEKA) au WABEM [Ward Based Education Management] unatekelezwa katika wilaya sita.

Wilaya za Mradi wa uboreshaji Elimu Ngazi ya Kata

(1) Kisarawe;  (2) Masasi; (3) Hai;  (4) Musoma [V];  (5) Mufindi; na (6) Songea [V].  Semina za awali katika ngazi ya Kata zilikwishafanyika.  Katika gharama za awali mradi ulikadiriwa kutumia Dola za Kimarekani 1,189,553 ambazo zimetolewa kwa uhisani wa UNICEF.  Kwa makubaliano ya UNICEF na Wizara shughuli hizi zitakwenda kwa pamoja na Mradi wa Shule zenye mazingira yanayomjali mtoto. 

 

8.4     Mradi wa Utafiti wa Hali Halisi na Mipango ya Elimu ya Shule [School Mapping and Micro-Planning]. Vilevile, hadi kufikia Juni 2004 Halmashauri 76 ambayo ni asilimia 64 ya Halmashauri zote nchini zimeshafanyiwa ‘School Mapping na Microplaning’.  Aidha, Halmashauri 16 zimeshaanza kufanyiwa “School Mapping na Microplanning” kuanzia Juni 2004.

 

Halmashauri  zinazofanyiwa School Mapping na Microplaning’

Kuanzia Juni 2004

(1) Monduli; .(2) Hanang; (3) Kondoa, (V); (4) Dodoma (V); (5) Mpwapwa; (6) Ludewa; (7) Same; (8) Kiteto; (9) Ngorogoro; (10) Mbozi; (11) Kwimba; (12) Sengerema; (13) Iramba; (14) Singida(V); (15) Igunga na (16) Urambo.

 

8.5     Mheshimiwa Spika, Mwaka 2003/04 Kutokana na uhisani wa Serikali ya Japan yamejengwa Madarasa 107, Ofisi za Walimu 9, na Matangi ya Maji 24 na maliwato matundu 107 pamoja na samani yakiwemo madawati, mbao za kuandikia na za matangazo katika shule 15 za Manispaa za Ilala, Temeke na Kinondoni.  Aidha, ujenzi wa madarasa 250 kwa uhisani wa Japan ulikamilika katika mkoa wa Shinyanga.

 

Shule Zilizojengewa Vyumba vya Madarasa Mkoa wa Dar es Salaam

(1) Boma;  (2) Mchikichini;  (3) Gongo la Mboto (B);  (4)Msongola;  (5) Mvuti;  (6) Kimara (B);  (7) Uzuri;  (8) Mbezi;  (9) Mabibo;  (10) Mwananyamala B;  (11) Azimio;  (12) Sokoine;  (13) Madenge;  (14) Rangi Tatu; na  (15) Temeke.

 

8.6         Mradi wa Kuzuia Ajira Mbaya ya Watoto kupitia MEMKWA.  Mradi huu unaendeshwa kwa ushirikiano na Shirika la Kazi la Dunia, Halmashauri husika na Wizara yangu.  Madhumuni ya Mradi huu ni kupunguza ajira mbaya ya watoto kwa kuwapatia Elimu kwa utaratibu wa MEMKWA.  Mradi huu unatekelezwa katika Wilaya 11.


 

(1) Ilala, (2) Kinondoni, (3) Temeke, (B); (4) Mufindi; (5) Iringa (V); (6) Simanjiro, (B); (7) Arumeru; (8) Arusha; (9) Kondoa; (10) Iramba; na (11) Urambo.

 

(ii) Malengo ya Elimu ya Msingi 2004/05

9.         Mheshimiwa Spika, 2004/05 ni Mwaka wa Nne wa utekelezaji wa MMEM ambao una malengo yafuatayo ya kutoa Elimu bora ya Msingi kwa wote:

9.1         Kujenga jumla ya madarasa 7,794 na nyumba za Walimu 6,000 yakiwemo madarasa ya MMEM 6,794 na nyumba za walimu 2,186;

9.2         Kuajiri walimu 7,286 na Walimu tarajali 10,000;

9.3         Kuandikisha Darasa la I watoto wote 1,041,880 wa miaka 7

9.4         Kutoa Ruzuku za Maendeleo na Uendeshaji; na

9.5         Kutekeleza MEMKWA kwa ukamilifu zaidi katika Wilaya zote.

 

10.       Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka 2004/05 ili kutekeleza malengo hayo zimetengwa Shilingi 271,222,783,504.  Kati ya hizo shilingi 230,394,438,504 zimeombwa kupitia katika Mafungu yanayosimamiwa na mwenzangu mwenye dhamana ya TAMISEMI.  Aidha, shilingi 40,829,345,000 zinaombwa kwa ajili ya kazi za MMEM zinazosimamiwa na Wizara yangu.

 

B:      Idara ya Elimu ya Sekondari

Malengo Maalumu ya Elimu ya Sekondari

(a)      Kuongeza nafasi ya utoaji Elimu ya Sekondari kwa rika la Elimu ya Sekondari (miaka 14 - 17) kutoka 7% ya mwaka 2003 hadi kufikia 50% ifikapo 2010.

(b)      Kupanua Elimu ya Sekondari katika kutekeleza Mpango wa Elimu ya Sekondari (MMES) kwa kuongeza nafasi ya kidato cha 1 kutoka 21% mwaka 2003 hadi 45% ifikapo mwaka 2009.

(c)      Kuboresha Elimu ya Sekondari kwa kuongeza asilimia ya wanaofaulu mitihani ya kitaifa ya Kidato cha 4 katika madaraja I, II na III kutoka 39.1% mwaka 2003 hadi zaidi ya 50% ifikapo mwaka 2005.

(d)      Kutoa Elimu ya Sekondari kwa usawa kwa jinsi zote, Wilaya zote kwa kuzingatia maelekezo ya kifungu 11 (3) cha Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kinachosema:

“Serikali itafanya jitihada kuhakikisha kwamba watu wote wanapata fursa sawa za kutosha kuwawezesha kupata elimu na mafunzo ya ufundi katika ngazi zote za shule na vyuo vingine vya mafunzo”.

 

(i)      Mafanikio ya Mwaka 2003/04

11.       Mheshimiwa Spika, mwaka 2003/04 Idara ya Elimu ya Sekondari imekuwa na mafanikio yafuatayo:

(a)          Ongezeko la shule 208 za sekondari na la wanafunzi 47,746 wa Kidato cha Kwanza na 82,111 wa Kidato cha 1 hadi 4.

(b)          Shule za Sekondari za Serikali zimeongezeka kutoka 649 mwaka 2003 hadi 828 mwaka 2004.  Hili ni ongezeko la shule 179 (27.6%).  Aidha, shule za Sekondari zisizo za Serikali zimeongezeka kutoka 434 mwaka 2003 hadi 463 mwaka 2004.  Hili ni ongezeko la shule 29 (6.7%).

 

Kielelezo Na. 11.1:  Ongezeko la Sekondari na Wanafunzi 2004

Aina ya Sekondari

Mwaka

Ongezeko

2003

2004

Sekondari za Serikali

649

828

179 (27.6%)

Sekondari Zisizo za Serikali

434

463

29 (6.7%)

Jumla Sekondari zote

1083

1,291

208 (19.2%)

Wanafunzi wa Kidato cha 1

99,744

147,490

47,746 (47.9%)

Wanafunzi wa K.1 - 4

319,487

401,598

82,111 (25.7%)

 

(c)          Jumla Shule za Sekondari zimeongezeka kutoka 1,083 mwaka 2003 hadi 1,291 mwaka 2004.  Hili ni ongezeko la shule 208 sawa na 19.2%.

(d)          Wanafunzi wa Kidato cha 1 wameongezeka kutoka 99,744 mwaka 2003 hadi 147,490 mwaka 2004.  Hili ni ongezeko la wanafunzi 47,746 au 47.9%.

Kielelezo Na.11.2:  Idadi ya Wanafunzi K1 kwa Jinsi, 2000-2004

 

Text Box:   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

(e)      Wanafunzi wote wa Kidato cha 1 hadi cha 4 wameongezeka kutoka 319,487 mwaka 2003 hadi 401,598 mwaka 2004 ikiwa ni ongezeko la 25.7%.  Ongezeko hili ni kubwa kuliko mwaka wowote uliopita.

 

Kielelezo Na.11.3:  Wanafunzi Shule za Sekondari K.1-K.4, [2000-2004]

 

Text Box:   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

11.2  Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia kwa:

 

(a)     Kukarabati kwa uhisani wa Serikali ya Japan shule za Serikali 14 ambazo ni: (1) Utete;  (2) Korogwe;  (3) Nyang’wale;  (4) Itengule;  (5) Iringa Wasichana;  (6) Kibiti;  (7) Zunzuli;  (8) Tabora Wavulana;  (9) Bwabuki;  (10) Maneromango;  (11) Makambako;  (12) Kilwa;  (13) Manyara na  (14) Itandula.

(b)     Kuzipa magari Shule 5 katika mikoa 5 ambayo ilikuwa haijapewa magari mapya kwa ajili ya huduma za shule hizo na pia kuhudumia shule nyingine zilizomo katika mikoa hiyo.  Shule zilizopewa magari ni:  Loleza, Kantalamba, Mwenge, Wotta na Musoma Kutwa.

(c)     Kununua Kompyuta 80 kwa ajili ya Shule za Sekondari.

 

11.3     Idadi ya Shule za Sekondari za Serikali zinazotoa elimu ya Kidato cha 5 na Kidato cha 6 imeongezeka kutoka 81 mwaka 2003 hadi 84 mwaka 2004.  Shule zilizoongezwa ni Kahororo, Mara na Longido.  Shule zisizo za Serikali zinazotoa elimu ya Kidato cha 5 na Kidato cha 6 ni 127.  Kwa hiyo jumla ya sekondari zenye Kidato cha 5 na ni 211.

 

11.4     Mikondo mipya ya Kidato cha 5 imeongezwa katika Shule za Sekondari za Kilakala, Tabora Wavulana, Msalato, Tanga Ufundi, Musoma Ufundi, Minaki, Lindi, Songea Wasichana, Mawenzi, Ifunda, Bwiru Wasichana na Mwakaleli.

 

11.5     Wanafunzi waliochaguliwa kuingia Kidato cha 5 waliongezeka kutoka 10,158 mwaka 2003 hadi 12,253 mwaka 2004.  Hili ni ongezeko la wanafunzi 2,075 sawa na 9.5%.  Wanafunzi wengine 1,130 watachaguliwa kujaza nafasi katika shule za Serikali zitakazopanuliwa mwezi Julai/Agosti, 2004, na kufanya jumla kuwa wanafunzi 13,383 wa Kidato cha 5.

Kielelezo Na.11.4:  Jumla ya Wanafunzi na % Wasichana K5

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

11.6     Jumla ya Wanafunzi wa Kidato cha 5 na 6 imeongezeka kutoka 25,954 mwaka 2003 hadi 31,001 mwaka 2004.

 

Kielelezo  Na.11.5: Jumla Wanafunzi Shule za Sekondari K5-K62000-2004

 

Text Box:   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

11.7.   Jumla ya wanafunzi wa Sekondari Kidato cha 1 hadi 6 imeongezeka kutoka 261,896 mwaka 2000 hadi kufikia 432,599 mwaka 2004.

 

Kielelezo  Na.11.6:  Wanafunzi Shule za Sekondari K1-K6, 2000-2004

 

Text Box:   

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

11.8.  Katika kutoa Elimu ya Sekondari kwa usawa, Serikali imeendelea:

(a)    Kuhakikisha kuwa idadi sawa ya wasichana na wavulana wanachaguliwa kuingia Kidato cha 1 kila mwaka.

(b)   Kulipia gharama za elimu kwa wanafunzi kutoka familia zisizo na uwezo kiuchumi.  Jumla ya wanafunzi 12,000 wanagharimiwa mpaka sasa.

(c)    Kulipia Elimu ya Sekondari kwa Wasichana 2,361 wa Kidato cha 3 hadi 6 ambao wazazi wao hawana uwezo wa kuwalipia.

(d)   Kuhamasisha ufunguzi wa shule za sekondari za kutwa hususan kwenye maeneo ambayo hayakuwa na shule za kutosha.  Shule mpya 179 zimefunguliwa.  Napenda kuipongeza Mikoa, Wilaya/Halmashauri zilizofungua shule nyingi mpya mwaka huu.

Wilaya/ Halmashauri hizo ni:  (1) Moshi Vijijini 9,  (2) Rungwe 8,  (3) Mbozi 7,  (4) Geita 7,  (5) Magu 5,  (6) Masasi 5, na  (7) Mbinga 5.  Mikoa iliyofungua shule nyingi zaidi ni :  (1) Mbeya 27;  (2) Kilimanjaro 18;  (3) Mtwara 16;  (4) Iringa 15;  (5) Mwanza 14; (6) Kigoma 9;  (7) Ruvuma 8;  (8) Pwani 6 na  (9) Rukwa 5.  Nawapongeza hao wote kwa juhudi zao.

 

11.9     Mheshimiwa Spika, katika kuboresha Elimu ya Sekondari yafuatayo yalifanyika:

(a)    Shule za sekondari za Serikali 51 zilipewa jumla ya Shilingi 330,432,530 kwa ajili ya ukarabati wa majengo.  Utekelezaji ulivuka lengo kwa 70%.

(b)   Shule za Sekondari za Serikali 644 zilipewa kiasi cha shilingi 490,152,400 kwa ajili ya ununuzi wa vitabu vya Sayansi na Hisabati.

(c)    Walimu 461 walipatiwa mafunzo kazini: 327 mafunzo ya mbinu bora za ufundishaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati; 87 Programu maalumu ya Shahada ya Hisabati katika Chuo Kikuu cha Tumaini; 39 mafunzo ya Stashahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; 5 mafunzo ya Shahada ya Uzamili katika Chuo Kikuu cha Dar es Salaam; na 3 mafunzo ya kompyuta katika Chuo cha Usimamizi wa Fedha;

(d)   Walimu 102 wa Shahada na 1,000 wa Stashahada waliajiriwa.  Aidha, walimu 615 wasiokuwa na ualimu kwa kusomea wameajiriwa kufundisha kwa liseni baada ya mafunzo mafupi ya pedagogia.

(e)    Ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi uliendelea katika shule 11 za:  Mbekenyera, Makiba, Mwaya, Mitole, Matekwe, Zingibari, Kongwa, Mangaka, Meatu, Mahiwa na Runzewe.  Ukamilikaji wa ujenzi uko kati ya 60% na 88% katika shule mbalimbali.

(f)     Ufaulu katika mitihani ya Kidato cha 4 Daraja la I hadi III umeongezeka kutoka 36.2% mwaka 2002 hadi 39.1% mwaka 2003.

 

11.10   Katika kuimarisha na kuboresha uongozi na usimamizi wa kutoa Elimu, Wizara ilipata mafanikio katika:

 

(a)    Kuwapatia mafunzo ya Uongozi ya mwezi mmoja Wakuu wa Shule 132 na Makamu Wakuu wa shule 126 wa shule za Serikali.

(b)   Jumla ya Wakuu wa shule 360 walishiriki katika mkutano mkuu wa Elimu uliofanyika Arusha tarehe 8-12/12/2003 na kuweka mikakati ya kuboresha huduma za Elimu katika ngazi mbalimbali.

 

Utekelezaji wa Miradi ya Elimu ya Sekondari 2003/2004

12.       Mheshimiwa Spika, miradi mbalimbali ilitekelezwa na Wizara yangu kwa lengo la kuboresha Elimu ya Sekondari.

12.1       Mradi wa Uboreshaji wa Elimu ya Sayansi (Science Education for Secondary Schools (SESS):  Mradi huu una sehemu mbili.  Sehemu ya kwanza inalenga kuboresha ufundishaji wa masomo ya Sayansi na Hisabati (Science Education for Secondary Schools - SESS) na sehemu ya pili ni Elimu dhidi ya UKIMWI, “Prevention and Awareness in Schools of HIV and AIDS” (PASHA) ambao ulianza rasmi Julai, 2003.  Mradi wa SESS ulitoa mafunzo ya mbinu bora za kufundisha masomo ya Sayansi na Hisabati kwa walimu.  Kazi mahsusi zilizofanywa na mradi huo katika kipindi hiki ni:

(a)    Kutoa mafunzo kwa wawezeshaji (trainers) 60 kutoka mikoa ya Tabora, Kigoma na Shinyanga.

(b)   Kuwalipatia mafunzo mahali pa kazi (cluster workshop) walimu 243 katika mikoa ya Iringa, Dodoma, Pwani, na Mwanza.

(c)    Kuwalipatia mafunzo ya kufundisha mada za HIV/AIDS walimu 24 kutoka mikoa ya Dodoma, Pwani na Iringa.

(d)   Kuwalishirikisha katika kambi ya Sayansi wanafunzi wasichana 187 kutoka Mikoa ya Tanga, Pwani na Morogoro.

 

12.2     Mradi wa Pili wa Elimu (Education II Project)

(a)    Uliendelea na ujenzi wa maabara za masomo ya Sayansi katika Shule za Sekondari 36 za Serikali zilizojengwa na wananchi.  Hadi kufikia Machi 2004 maendeleo ya ujenzi wa maabara katika shule 36 za awamu zote tatu ulikuwa kama ifuatavyo:

 

Awamu

%

Wastani wa Matarajio

%

Kiwango Kilichojengwa

1

100

88.05

2

100

63.37

3

87.39

42.96

 

(b)   Kwa wastani ujenzi wa maabara zote umekamilika kwa 71.6%.

(c)    Shule 18 zimepatiwa samani za maabara.  Aidha, samani kwa ajili ya shule 8 zimenunuliwa na zinasubiri ukamilishwaji wa maabara husika.

 

(ii)     Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) 2004-2009

13.      Mheshimiwa Spika, katika hotuba yangu ya bajeti ya mwaka 2003/04 niliahidi kuwa Serikali ingekamilisha Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES).  Ninafurahi kulitaarifu Bunge lako tukufu kwamba utayarishaji wa Mpango huo umekamilika na utagharimu jumla ya Shilingi bilioni 1,433.084 kwa miaka mitano ya 2004-2009.  Katika bajeti ya mwaka 2004/05 zimetengwa jumla ya Shilingi 91,481,468,500 zikiwemo Shilingi 59,413,581,900 za Maendeleo na Shilingi 32,067,586,900 za matumizi ya kawaida.  Hii mara ya kwanza kuwa na bajeti kubwa kiasi hiki kwa Elimu ya Sekondari.  Namshukuru Rais wetu Mheshimiwa Benjamini William Mkapa kwa jitihada zake anazofanya kuhusu Elimu.

 

14.       Mheshimiwa Spika, lengo kuu la Mpango 2004/05 ni kuongeza vijana wa Tanzania wanaosoma na kuhitimu Elimu ya Sekondari wakiwa na matokeo mazuri ya kujifunza kutoka 345,000 mwaka 2003 hadi 2,000,000 mwaka 2010.  Mpango huu unazo programu tano zifuatazo:

14.1 Kuongeza wanaojiunga na sekondari (improvement of access) kufikia 50 % ya rika lengwa (miaka 14-17) na 50% ua wahitimu wa Darasa la VII; pia 50% ya wahitimu wa Kidato cha 4 kujiunga Kidato cha 5 kila mwaka.  Lengo hili litafikiwa kwa kufanya yafuatayo:

(a)    Upanuaji wa shule zilizopo na ujenzi wa shule mpya hususan kule ambako haziko.  Inatarajiwa kujenga shule mpya 1500 katika kipindi cha mpango.

(b)   Kuongeza nafasi za Kidato cha 5 na 6 zaidi ya mara tano za mwaka 2003.

(c)    Utumiaji mzuri wa walimu waliopo, na upanuaji wa mafunzo na ajira ya walimu.  Chuo cha Ualimu Dar es Salaam na Shule ya Sekondari Mkwawa vitabadilishwa kuwa Vyuo Vikuu Vishiriki vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam ili pamoja na Stashahada za Elimu vitoe pia Shahada ya Ualimu katika miaka 3.  Aidha, mafunzo ya Stashahada na Shahada yataoanishwa ili mafunzo ya Stashadada yatosheleze sehemu ya Shahada ya Ualimu ya mwaka wa kwanza.  Kwa hiyo, mwenye Stashahada ya Ualimu ataweza kujiunga na Chuo Kikuu kukamilisha miaka 2 iliyobakia ili apate Shahada yake ya Ualimu.

(d)    Kuisaidia Sekta binafsi inayotoa Elimu ili iboreshe shule zake kwa sababu inasaidia Serikali kutoa elimu.

(e)    Kupanua elimu ya sekondari kwa njia ya posta

(f)     Kupunguza viwango vya kuacha shule, kurudia na kufeli katika ngazi zote.

(g)    Kupunguza mzigo wa elimu ya sekondari kwa familia kwa kupunguza ada na michango.

 

Kielelezo 14:  Malengo ya MMES 2004-2009

 

Na.

 

MALENGO

MWAKA

2004

2005

2006

2007

2008

2009

2010

1..

Wanafunzi K1

132,146

171,793

225,317

297,971

397.097

532,786

719,328

2.

Wanafunzi K1-K4

379,534

461,384

585,298

768,749

1,030,256

1,386,043

1,869,903

3.

Kidato cha 5

18,229

23,558

31,687

42,912

58,454

80,017

109,987

4.

Jumla Wanafunzi

K1-K6

411,973

503,170

640,543

843,348

1,131,622

1,524,513

2,059,907

5.

Walimu wapya

1,124

2,740

4,593

7,023

9,481

13,269

16,194

6.

Madarasa mapya

885

1,678

2,788

3,442

5,633

6,596

 

7.

Nyumba za Walimu

1,633

2,414

3,890

6,337

5,910

3,298

 

8.

Maabara

682

596

1,039

1,773

3,470

3,298

 

9.

Maktaba

335

199

346

591

1,157

1,649

 

 

14.2      Kuongeza usawa (improvement of equity) kwa jinsi zote, wilaya zote, wenye ulemavu na makundi tofauti ya mapato kwa:

(a)      Kuelekeza uwekezaji kule kwenye uhaba wa shule pamoja na kukamilisha shule zilizopo.

(b)     Kuwalipia ada watoto wa familia maskini.

(c)      Kuongeza kujiunga, kubakia shuleni na kufaulu kwa wasichana.

(d)     Kuboresha majengo na vifaa katika shule zenye wanafunzi wenye ulemavu.

(e)      Kuboresha utoaji wa elimu kwa jamii zilizo nyuma kielimu na zisizofikika kwa urahisi.

(f)      Kupunguza ada katika Sekondari za Serikali za kutwa.

 

14.3     Kuongeza ubora (quality improvement) wa elimu ili wanaofaulu Kidato cha 4 katika Madaraja I-III waongezeke kutoka 36% mwaka 2003 hadi 70% mwaka 2009; kwa kuchukua hatua zifuatazo;

(a)      Kuongeza na kuimarisha Mafunzo ya Ualimu Kazini.

(b)     Kuboresha sifa za kujiunga na mafunzo ya ualimu wa Stashahada na Shahada.

(c)      Kuboresha mitaala kwa kuzingatia masomo sahihi ya Elimu ya Sekondari na kuingiza ndani yake Elimu ya Kujitegemea na kuacha kufundisha masomo ya michepuo hususan ya Ufundi Kilimo na Biashara.

(d)     Kuboresha maktaba za shule.

(e)      Kutoa Ruzuku ya Uendeshaji wa Shule kwa kwa ajili ya mahitaji ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia.

(f)      Kuboresha muundo na ubora wa mitihani.

(g)      Kupanua mafunzo ya Elimu ya Ualimu ya Stashahada na Shahada.

(h)      Kuingiza katika mitaala masuala mtambuka kama vile: Elimu ya Jinsia na Mazingira; na Elimu Dhidi ya UKIMWI (HIV and AIDS).

 

14.4Kufanya mageuzi ya kutoa madaraka (Devolution of powers) kwa Mikoa, Wilaya na Shule ili kuboresha usimamiaji na uendeshaji wa shule za sekondari.  Madaraka ya uamuzi, utendaji, usimamiaji wa fedha yatahamishwa kutoka Wizara kwenda ngazi za Mkoa, Wilaya na Bodi za Shule.

 

14.5     Kuboresha Mfumo wa Usimamiaji wa Elimu kwa lengo la kuhakikisha kuwa Wizara inatekeleza majukumu yake ya msingi (core functions) wa kubuni sera, kufuatilia na kutathmini, kutunga kanuni, kuainisha, na kuhakiki utumiaji wa raslimali.  Lengo hili litafikiwa kwa;

(a)      Kuimarisha Ukaguzi wa Shule na kuimarisha Uongozi wa Shule.

(b)     Kuboresha upatikanaji na utumiaji wa mfumo wa taarifa na mawasiliano ya Kielimu (Education Management Information System - EMIS).

(c)      Kujenga uwezo (capacity building) katika ngazi zote.

(d)     Kuimarisha mawasiliano na ufahamikaji wa mpango

(e)      Kuimarisha ufuatiliaji na tathmini (monitoring and evaluation).

 

(iii)       Mkakati wa Kibajeti wa Utekelezaji wa MMES 2004-2009

15.     Mheshimiwa Spika, mkakati wa utekelezaji wa mpango huu utakua kwa kuongeza uwekezaji katika elimu kwa njia ya bajeti ya Serikali inayokwenda moja kwa moja kwa walengwa.  Hatua na njia muhimu zitakazotumika kuanzia Bajeti ya mwaka 2004/05 zitakuwa:

 

15.1   Kutoa Ruzuku ya Maendeleo kwa ajili ya shule za Serikali zinazojengwa na wananchi kama ifuatavyo:

(a)   Shilingi 7.0 milioni kwa ajili ya ujenzi wa darasa ili kununulia vifaa vya ujenzi kutoka viwandani (mabati, saruji, nondo, misumari, rangi na vioo) pamoja na madawati, kabati, mbao za kuandikia, meza na viti.

(b)   Shilingi 9.0 milioni kwa ajili ya ujenzi wa nyumba ya mwalimu ili kununulia vifaa vya ujenzi vinavyotengenezwa viwandani (mabati, saruji, nondo, misumari, rangi na vioo).

(c)   Ujenzi wa maabara na maktaba kwa zabuni ya serikali ngazi ya Wilaya

(d)   Kusaidia ujenzi wa hosteli pale inapohitajika kwa kulipia vifaa vya ujenzi vinavyotengenezwa viwandani (mabati, saruji, nondo, misumari, rangi, na vioo vya madirisha).

 

15.2   Kutoa Ruzuku ya Uendeshaji wa Shule (capitation grant) kwa ajili ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia ya:

(a)     Shilingi 30,000 kwa kila mwanafunzi kwa Sekondari za Serikali;

(b)     Shilingi 15,000 kwa mwanafunzi kwa Sekondari zisizo za Serikali ambazo haziendeshwi kibiashara na siyo seminari.

 

15.3   Kutoa Ruzuku ya Maendeleo kwa mwenye shule asiye Serikali aliyeidhinishwa na Afisa Elimu Kiongozi kwa ajili ya ujenzi wa shule za wanafunzi wenye ulemavu kwa viwango sawa na ile inayotolewa kwa ajili ya Sekondari za Serikali zinazojengwa na wananchi.

 

15.4   Kupunguza ada ya Sekondari za Kutwa za Serikali kutoka Shilingi 40,000 kuwa Shilingi 20,000 kuanzia Januari 2005.  Hatua hii imechukuliwa ili watoto wengi wa familia zenye mapato ya chini waweze kujiunga na sekondari kwa kulipia angalau shilingi 10,000 kwa muhula.  Ada yote ya shilingi 20,000 itabakia shuleni na Serikali itatoa kwa kila shule kutokana na bajeti hii shilingi 20,000 nyingine kwa mwanafunzi kufidia punguzo la ada. Ikumbukwe kuwa Serikali itatoa pia ile Ruzuku ya Uendeshaji ya shilingi 30,000 kwa mwanafunzi.  Kwa hiyo kwa Sekondari za kutwa jumla zitakuwepo shilingi 70,000 kwa mwanafunzi kwa ajili ya uendeshaji wa shule ili kukidhi haja ya mahitaji ya shule.

15.5   Kuongeza maradufu Ruzuku ya Elimu ya Sekondari kwa watoto wa familia maskini ili watakaonufaika waongezeke kutoka 6,000 kwa mwaka kuwa 12,000 kwa mwaka kuanzia mwaka 2005.

 

16.       Mheshimiwa Spika, Mpango huu umeongeza uwezekano wa watoto wa familia maskini kujiunga na Sekondari za Bweni kwa Serikali kufanya yafuatayo:

(a)          Kubakiza shuleni ada yote ya shilingi 70,000;

(b)          Kutoa pia shilingi 30,000 za Ruzuku ya Uendeshaji na kufanya jumla iwe shilingi 100,000 kwa mwanafunzi kwa mwaka; na pia

(c)          Zimepangwa shilingi 862.47 za chakula kwa mwanafunzi kwa siku.

 

17.       Mheshimiwa Spika, kutokana na hatua hizo za kibajeti Sekondari zote za Serikali zitapewa fedha ya kutosha ya uendeshaji wa shule.  Kwa hiyo Bodi za shule haziruhusiwi kutoza michango yoyote kwa ajili ya uendeshaji wa sekondari zote za Serikali.  Serikali inataka watoto wote wanaochaguliwa kwenda sekondari, wawe wanajiunga na kuendelea bila kuacha shule mpaka wahitimu ili tuweze kuyafikia malengo ya Mpango huu ya kuwa na wanafunzi wa Sekondari 2,000,000 ifikapo mwaka 2010, na wahitimu wa Sekondari wasiopungua 500,000 kila mwaka.

 

(iv) Mwaka wa Kwanza wa MMES 2004-2005

18.  Mheshimiwa Spika, utekelezaji wa mwaka wa kwanza wa Mpango huu utakuwa ifuatavyo:

18.1             Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya Shilingi 7.0 milioni kwa darasa kukamilisha ujenzi wa madarasa 1,456 katika shule zilizopo za mikondo 2 na 3 ili ziwe za mikondo minne.  Jumla ya Shilingi 10,192,000,000 zimetengwa kwa ajili hiyo.

18.2             Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya Shilingi 7.0 milioni kwa ujenzi wa darasa kukamilisha ujenzi wa madarasa 458 katika sekondari mpya katika maeneo yasiyo na sekondari za kutosha (underserved areas).  Jumla zimetengwa Shilingi 3,206,000,000.

18.3             Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya Shilingi 9.0 milioni kwa ujenzi wa kila nyumba ili kukamilishia ujenzi wa Nyumba za Walimu 957.  Jumla ya Shilingi 8,613,000,000 zimetengwa kwa ajili hiyo.

18.4             Kukarabati shule 40 za Serikali zilizopo kwa Shilingi 2,734,000,000.

18.5             Kukarabati shule 8 za sekondari zenye wanafunzi wenye ulemavu na kuchangia ujenzi wa shule mpya 2 za wenye ulemavu Shilingi 1,231,400,000.

18.6             Kukamilisha ujenzi wa maabara 90 katika shule 36 kwa Shilingi 1,109,273,900.

18.7             Kujenga majengo yanayohitajika katika sekondari 14 za Serikali ili kuzibadilisha mwaka unaofuata zitoe elimu ya Kidato cha 5 na 6 tu na kupanua nyingine 64 za “A - level” kwa Shilingi 3,132,000,000.

18.8             Kugharimia Elimu ya Sekondari kwa watoto 12,000 wa familia maskini kwa Shilingi 2,160,000,000 kwa Kidato cha 1 mwaka 2005.

18.9             Kutoa Elimu ya Sekondari kwa mfumo usio rasmi (Open and distance learning)  kwa Shilingi 1,878,000,000.

18.10        Kutoa Ruzuku ya Shilingi 20,000 kwa kila mwanafunzi wa Sekondari ya Serikali ya Kutwa kufidia punguzo la karo.  Jumla Shilingi 4,939,000,000 zimetengwa.

18.11        Kutoa Ruzuku ya Uendeshaji ya Shilingi 20,000 kwa mwanafunzi kwa sekondari za Serikali na sh. 10,000 kwa Sekondari zisizo za Serikali ambazo sio za kibiashara na sio Seminari.  Jumla Shilingi 7,074,219,000 zimetengwa.

18.12        Kupunguza masomo ya Sekondari kutoka 13 kuwa 8 yakiwemo Mathematics, Lugha (Kiswahili na English), masomo ya Sayansi (Biology, Physics na Chemistry) na Sayansi ya Jamii (History, Geography na Civics); na kuacha kufundisha michepuo (Technical Studies, Agriculture na Commerce) ambayo ina vyuo vyake chini ya Wizara husika.

18.13        Kuongeza nafasi za Mafunzo ya Ualimu wa sekondari, kwa kukibadilisha Chuo cha Ualimu Dar es Salaam na Shule ya Sekondari Mkwawa kuwa Vyuo Vikuu Vishiriki vya Elimu ya Ualimu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

18.14        Kutoa chakula sekondari za bweni: Shilingi. 9,417,173,200 sawa na sh 862.47 kwa mwanafunzi kwa siku;

18.15        Mheshimiwa Spika, Serikali inaendelea na mazungumzo na Wabia na Wahisani ili kupata fedha za kutosha kutekeleza malengo yote ya Mpango.  Naishukuru sana Bodi ya Benki ya Dunia ambayo tarehe 8/6/2004 ilipitisha mkopo wa masharti nafuu wa Dola za Kimarekani 124 milioni na Ruzuku ya Dola za Kimarekani 26 milioni.  Fedha hii imewezesha MMES uanze katika Bajeti ya mwaka huu kwa Shilingi 53.8 bilioni .

 

 

Kielelezo: 18  Shughuli Kuu Zitakazofanyika Katika MMES Mwaka wa Kwanza

 

No

Shughuli

Kiasi cha Kazi/Idadi

Jumla (Sh.’000)

1

Ujenzi madarasa katika shule 728 zilizoko

Madarasa 1,456

10,192,000

2

Ujenzi wa madarasa katika shule mpya

Madarasa 458

3,206,000

3

Ujenzi wa nyumba za walimu katika shule zilizoko na mpya

Nyumba za walimu 957

8,613,000

4

Matengenezo shule za zamani

Shule  40

2,734,000

5

Upanuzi wa "A - level" tupu

Shule 14

1,000,000

6

Upanuzi wa  "A - level" katika shule nyingine 64

Shule 64

2,132,000

7

Ujenzi wa madarasa na miundombinu shule zenye walemavu

Shule 10

1,231,400

8

Upanuzi wa Elimu ya Ualimu-Stashahada

Vyuo 12

1,396,200

9

Upanuzi wa Elimu ya Ualimu-Shahada

Vyuo 2

390,000

10

Upanuzi na uimarishaji wa Open and Distance learning

Kazi mbalimbali

1,878,000

11

Kutayarisha Curriculum and Examination Framework

Kazi mbalimbali

88,000

12

Ruzuku ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia shule za Serikali na zisizo za Serikali

Aina mbalibali

6,054,219

13

Ruzuku ya uendeshaji kufidia ada

Wanafunzi 246,950

4,939,000

14

Kulipia ada wanafunzi kutoka  familia masikini

Wanafunzi 12,000

2,160,000

15

Chakula cha wanafunzi

Wanafunzi 40,440

9,417,173

16

Ujenzi wa Uwezo (Capacity Building)

Makundi mbali mbali

788,175.9

JUMLA

56,219,167.9

 

C:      Idara ya Elimu ya Ualimu

Malengo Maalumu ya Elimu ya Ualimu

(a)    Kuandaa walimu wa ngazi ya cheti Daraja A na Stashahada ili kukidhi mahitaji kwa shule za Awali, Msingi, Sekondari na Vyuo vya Ualimu.

(b)   Kuboresha mazingira ya kutolea mafunzo katika Vyuo vya Ualimu kwa kutoa vifaa bora na vya kutosha vya kufundishia na kujifunzia.

(c)    Kuimarisha Vituo vya Walimu (“Teachers’ Resource Centres – TRCs”) katika ngazi ya Wilaya, Kanda na Taifa.

(d)   Kuboresha taaluma na utaalamu wa ufundishaji wa masomo ya shule za msingi hususan kwa kuwapatia mafunzo maalumu kazini ya Daraja A (“In-Service Grade A”) walimu wote wa Daraja B/C na kuwatahini.

(e)    Kupanua mafunzo ya Ualimu sambamba na upanuaji wa Elimu ya Msingi na Sekondari.

 

19.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Idara ya Elimu ya Ualimu ilitoa mafunzo kwa:

(a)           Walimu tarajali wa Daraja A ambapo walimu 6,578 walihitimu kwa kufaulu baada ya mazoezi kwa vitendo.

(b)          Mwaka 2003, wanachuo 15,283 waliandikishwa kufanya mitihani; na kati yao 14,836 walifaulu na kuendelea mwaka wa pili wa mafunzo kwa vitendo shuleni.

(c)           Walimu wa Stashahada 2,390 wamehitimu.  Wizara ilifanya ukarabati Vyuo vya Elimu ya Ualimu 10 kwa gharama ya Shilingi 130,300,000.  Vyuo vilivyofanyiwa ukarabati ni: Marangu, Dar es Salaam, Kleruu, Ilonga, Nachingwea, Tandala, Sumbawanga, Morogoro, Tarime na Mpuguso.

(d)          Mwaka 2004, wanachuo 10,037 wamejiunga na Mafunzo ya Ualimu Daraja A tarajali katika Vyuo vya Ualimu vya Serikali na 751 katika vyuo visivyo vya Serikali.

 

Wanachuo Vyuo vya Elimu ya Ualimu 2003/04

AWAMU

MAELEZO

IDADI

Kwanza

2002

Wanachuo walioandikishwa Daraja A Tarajali

Wanachuo Waliofanya mtihani (na kufaulu mwaka wa kwanza)

7,284

7,070

2003

Wanachuo waliofanya mazoezi shuleni (mwaka wa pili)

Wanachuo waliohitimu mwaka wa pili

Wanachuo walioshindwa mwaka wa pili

Wanachuo ambao hawakutahiniwa mwaka wa pili

6,607

6,578

4

25

Pili

2003

Wanachuo Daraja A Tarajali walioandikishwa

Wanachuo waliofanya mtihani na kufaulu mwaka wa kwanza

15,283

14,836

Tatu

(2004)

Wanachuo Daraja A Tarajali walioandikishwa

Wanachuo Stashahada walioandikishwa

Wanachuo Stashahada waliohitimu

10.037

3,105

2,390

 

19.5     Wawezeshaji 763 walipatiwa mafunzo kwa ajili ya kuwaendeleza walimu wa C/B kufikia Daraja la A (Inservice Grade A).  Walimu 25,000 wa Daraja C/B, wameandikishwa kwa ajili ya mafunzo hayo.


Mafunzo Kwa Wawezeshaji

Maelezo

Idadi

Wawezeshaji Ngazi ya Taifa

35

Wawezeshaji Ngazi ya Kanda

300

Wawezeshaji Ngazi ya Wilaya

428

Jumla

763

 

19.6     Walimu 16 ambao hawajasomea taaluma ya Ualimu wanalipiwa gharama ya mafunzo ya Stashahada ya Uzamili katika Elimu («Post Graduate Diploma in Education»).  Aidha, wakufunzi 250 wanasoma Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kwa kugharamiwa na Serikali.

 

20.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, wanachuo tarajali 10,000 wa Daraja A na 3,624 wa Stashahada watajiunga na mafunzo ya Ualimu.  Walimu 25,000 wa Daraja C/B watajiunga na mafunzo ya kujiendeleza.  Walimu 49,000 watajiunga na mafunzo kazini ya ufundishaji kwa kutumia njia na mbinu shirikishi kupitia Vituo vya Ualimu (TRCs).  Aidha, walimu wa shule za msingi wa Daraja A watapewa mafunzo kazini ya aina mbalimbali kwa kutumia njia na mbinu shirikishi.

 

Wanachuo Wapya,Mafunzo ya Ualimu 2004/05

Maelezo

Idadi

Wanachuo Daraja A tarajali

10,000

Wanachuo tarajali Stashahada

3,624

Jumla ya Walimu wapya

13,624

Mafunzo kazini

 

Mafunzo kazini kwa walimu wa Daraja la A (Elimu ya Awali 200, fani za Sanaa na Ufundi 70, Elimu Maalumu 60, Sayansi Kimu Cheti 140, Stashahada Elimu Maalumu 30 na  Sayansi Kimu 50)

550

Mafunzo Kazini kwa walimu ya ufundishaji kutumia njia na mbinu shirikishi kupitia Vituo vya Walimu (TRCs)

49,000

Mafunzo Kazini kwa Walimu wa Daraja C/B

25,000

Jumla mafunzo Kazini

74,550

 


D:      Idara ya Ukaguzi wa Shule

21.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Idara ya Ukaguzi wa Shule ilikagua jumla ya asasi za elimu 15,733 sawa na 82% ya lengo la mwaka.  Katika kuboresha kazi ya ukaguzi wa shule, Wizara imenunua magari mawili, kwa ajili ya ukaguzi wa shule na imeendesha mafunzo ya awali ya ukaguzi wa shule kwa wakaguzi wa shule wapya 127.

 

Malengo na Utekelezaji wa Ukaguzi wa Shule 2003/04

Aina ya Asasi

Lengo

Utekelezaji wa Lengo

% Lengo

Shule za Awali

Shule za Msingi

Vituo vya Ufundi Stadi

Shule za Elimu Maalumu

Vituo vya Elimu ya Watu Wazima

Shule za Sekondari

Vyuo vya Elimu ya Ualimu

2,812

7,747

182

113

 

7,747

617

41

2,810

6,552

160

74

 

5,557

539

41

99.9

84.5

88

65

 

72

87

100

Jumla

19,259

15,733

82

 

Shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na:

(a)      Kutoa Jarida la FAHAMU ELIMU Na. 6 kuhusu somo la Kiswahili kwa lengo la kubaini maendeleo ya somo hilo.

(b)       Kufanya ukaguzi maalumu wa shule za Sekondari 179 kwa ajili ya upanuzi wa Elimu ya Sekondari.

 

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, Wizara imepanga kufanya ukaguzi wa asasi mbalimbali za Elimu 19,332.  Aidha, Idara itanunua magari 13 na kutoa mafunzo ya awali ya Ukaguzi wa Shule kwa wakaguzi wa shule wapya 127.

Malengo ya Ukaguzi wa Shule 2004/05

Aina ya Asasi

Lengo

Shule za Awali

2,812

Shule za Msingi

7,747

Vituo vya Ufundi Stadi

182

Vituo vya Elimu Maalumu

113

Vituo vya Elimu ya Watu Wazima

7,747

Shule za Sekondari

690

Vyuo vya Elimu ya Ualimu

41

Jumla

19,332

 

Shughuli nyingine zitakazofanyika ni pamoja na:

21.3       Utafiti kuhusu maendeleo ya ufundishaji wa somo la Stadi za Kazi katika Shule za Msingi na Vyuo vya Ualimu Daraja la A.

21.4       Kuandika Jarida la FAHAMU ELIMU Na. 7 kuhusu somo la Civics.

 

E:      Idara ya Maendeleo ya Utamaduni

Malengo Maalumu ya Maendeleo ya Utamaduni

(a)    Kupanua kiwango cha Ushiriki wa wananchi katika shughuli za Utamaduni.

(d)   Kuboresha Usimamizi na Uendeshaji wa shughuli za Utamaduni.

(e)    Kuimarisha Elimu na Mafunzo ya Fani za Utamaduni.

(f)     Kuimarisha na kukuza Tasnia na Miundo Mbinu ya Utamaduni.

(g)    Kulinda na kuimarisha Maadili na Utambulisho wa Taifa.

(h)    Kuimarisha Ushirikiano wa Kimataifa katika Utamaduni.

 

22.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilitekeleza mambo yafuatayo:

(a)      Iliandaa mashindano ya kupata Vazi la Taifa kwa wanaume na wanawake.

(b)      Ilitoa misaada kwa miradi mbalimbali ya Utamaduni kupitia Mfuko wa Utamaduni.

(c)      Iliendesha mradi wa Sanaa kwa wanafunzi wa shule za Msingi katika mikoa ya Dar es Salaam, Morogoro na Pwani.  Aidha, Wizara iliendesha Mradi wa TUSEME katika shule 16 za Sekondari za Wasichana na za mchanganyiko 7.

(d)      Iliendesha tamasha la Sanaa la Ishirini na mbili la Bagamoyo lililoshirikisha wasanii wa Vikundi 64 vya ndani na nje ya nchi.

(e)      Ilitoa Mafunzo ya Stashahada kwa wanafunzi 87 na mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 60 katika Chuo cha Sanaa, Bagamoyo.

(f)        Ilitoa mafunzo kwa Maafisa Utamaduni wa Wilaya 96 juu ya jinsi ya kubadili mila na desturi zinazoongeza kasi ya maambukizi ya UKIMWI.

(g)      Iliendesha Mkutano Mkuu wa Sekta ya Utamaduni.

 

Katika mwaka 2004/05, Idara ya Utamaduni itatekeleza mambo kumi kuhusu utafiti wa mila na desturi, maonesho ya utamaduni na mafunzo ya utamaduni yafuatayo:

(a)      Itafuatilia matokeo ya mchakato wa mashindano ya Vazi la Taifa kwa wanaume na wanawake.

(b)      Itaendesha mafunzo ya ukusanyaji, uhifadhi na usambazaji wa takwimu za Utamaduni kwa Maafisa Utamaduni 113 wa Halmashauri .

(c)      Itaendesha mkutano wa Sekta ya Utamaduni utakaowashirikisha wajumbe 300 kutoka Serikali Kuu, Serikali za Mitaa, Mashirika, Vyama vya Hiari na Asasi zisizo za Serikali.

(d)      Itaendesha programu za Sanaa kwa wanafunzi wa shule za msingi 70 katika mikoa ya Dar es Salaam, Pwani, Morogoro na Jiji la Mwanza pamoja na programu ya TUSEME kwa shule za sekondari 23 za mikoa 19 ya Tanzania Bara.

(e)      Itaendesha mafunzo ya Stashahada kwa wanafunzi 90 na mafunzo ya muda mfupi kwa washiriki 60.

(f)       Itaendesha Tamasha la ishirini na tatu la Sanaa Bagamoyo.

(g)      Itaendelea kusaidia miradi ya utamaduni kupitia Mfuko wa Utamaduni.

(h)      Itaendesha tamasha la Utamaduni la Taifa litakaloshirikisha Mikoa yote.

(i)        Itaendesha warsha ya mapambano dhidi ya UKIMWI.

(j)        Itatengeneza filamu moja juu ya UKIMWI itakayooneshwa nchini kote.

 

F:      Idara ya Utawala na Utumishi

23.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Idara ya Utawala na Utumishi ilishughulikia ajira ya walimu wapya 2,904 wa shule za Sekondari, Vyuo vya Elimu ya Ualimu na watumishi wasio walimu 28.

Ajira ya Walimu na Watumishi Wasio Walimu

Walimu

1.       Walimu wa Sekondari wapya

 

2,839

2.       Walimu mbadala wa sekondari

65

Jumla ya Walimu wa Sekondari

2,904

Watumishi Wasio Walimu

 

1.       Karani Masijala

1

2.      Maafisa Maghala Wasaidizi

1

3.       Mkutubi

1

4.       Wasaidizi wa Hesabu na Wahasibu

9

5.       Fundi Sanifu

2

6.       Madereva

9

7.       Katibu Mahususi

4

8.       Wahudumu

1

Jumla ya Watumishi Wasio Walimu

28

 

 

Mambo Mengine ya Ajira

1. Watumishi waliopandishwa vyeo

173

2. Waliothibitishwa kazini

168

3. Waliopewa barua za ajira ya kudumu

156

Jumla

497

 

Aidha, jumla ya watumishi 275 walipata mafunzo mbalimbali ya muda mfupi na mrefu ndani na nje ya nchi.

Mafunzo kwa Wafanyakazi

1. Mafunzo ya Shahada ya kwanza

2. Mafunzo ya Shahada ya pili

3. Mafunzo ya Muda Mfupi Fani Mchanganyiko

4. Mafunzo ya Stashahada

5. Mafunzo ya Cheti

6. Stashahada za Uzamili

75

25

72

46

15

42

Jumla Kuu

275

 

Katika mwaka 2004/05, Wizara inatarajia kuomba kibali cha ajira mpya ya watumishi 2,780 wa kada mbalimbali.  Katika jitihada za kujenga uwezo wa watumishi, Wizara itapeleka Watumishi 100 kwenye mafunzo ya muda mrefu na 50 ya muda mfupi ndani na nje ya nchi.

 

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, Idara itahakikisha Programu ya kuboresha Utumishi wa Umma inatekelezwa kwa kushirikisha Sekta binafsi katika kutoa huduma za usafi, ulinzi na mapokezi katika jengo la Wizara Makao Makuu.  Aidha, kuanzia Julai 2004 Wizara itaanza utekelezaji wa mpango wa mwaka wa tathmini ya utendaji kazi wa watumishi kwa utaratibu mpya unaolenga kuweka malengo na matokeo katika utendaji kazi (“Performance Management System”) kwa watumishi wa Makao Makuu ya Wizara na kwenye Shule na Vyuo.

 

24.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (Agency for the Development of Education Management – ADEM), walitoa mafunzo ya menejimenti na utawala kwa viongozi watendaji wa elimu wa ngazi mbalimbali 518.

Mafunzo ya Menejimenti ADEM 2003/04

Mdau na Aina ya Mafunzo

Walengwa

1.Stashahada ya Uongozi wa Elimu kwa Viongozi wa Idara mbalimbali za Elimu

147

2. Mafunzo Mafupi ya wakuu wa shule za Sekondari za Serikali na zisizo za Serikali.

 

113

3. Maafisaelimu wa Wilaya (Wiki 1-2)

4

4. Waratibu wa Elimu Kata

69

5. Walimu Wakuu wa Shule za Msingi

185

Jumla Kuu

518

 

Katika mwaka 2004/05, ADEM itatoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi watendaji wa elimu 6,108 wakiwemo Stashahada ya Uongozi wa Elimu kwa wanachuo 90.

 

Mafunzo ya Wafanyakazi

Aina ya Mafunzo

Wingi

1. Stashahada ya Uongozi wa Elimu Wanachuo

2. Mafunzo ya miezi 3 kwa Walimu Wakuu wa Shule za Msingi

3. Mafunzo mafupi kwa Waratibu wa Elimu wa Kata

4. Maafisa Elimu wa Wilaya

5. Wakuu wa Shule za Sekondari

90

3,200

2,500

118

200

Jumla Kuu

6,108

 

 

G:      Idara ya Sera na Mipango

25.              Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Idara ya Sera na Mipango ilishirikiana na Idara nyingine:

(a)        Kupanga, kuratibu na kutekeleza mipango ya elimu kulingana na Sera ya Elimu na Mafunzo na Utamaduni.

(b)       Imesimamia ufuatiliaji na tathmini ya utekelezaji wa mipango ya kazi

(c)        Imesimamia na kuratibu ukarabati wa shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Ualimu.

(d)       Imetekeleza wajibu wake wa kuwa kiungo kati ya Wizara yangu, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafisishaji, Wizara ya Fedha, Wahisani na Wadau mbalimbali

(e)        Shughuli nyingine zilizofanyika ni pamoja na kutayarisha programu na mipango ya muda mfupi, muda wa kati na muda mrefu ya sab-sekta ya elimu ya awali, msingi, sekondari, ualimu, elimu ya watu wazima na utamaduni, pamoja na kuandaa na kuratibu rasimu za maandiko mbalimbali zikiwemo hotuba za bajeti.

 

Katika mwaka 2004/05, Idara ya Sera na Mipango itashughulikia masuala mbalimbali pamoja na:

(a)        Kufanya utafiti na tathmini kwa matumizi ya baadaye, kufuatilia mwenendo na utoaji wa huduma za elimu na utamaduni na kutoa ushauri wa kitaalamu.

(b)       taendelea kuandaa na kuratibu rasimu na maandiko mbalimbali ya kitaalamu yanayohusu miradi na mipango, sera, takwimu, hotuba na makala mbalimbali.

(c)        Itaendelea kuandaa mapitio ya matumizi ya fedha za umma (“Public Expenditure Review”) kuandaa “Medium Term Expenditure Framework - MTEF)” za Wizara na Sekta ya Elimu kwa ujumla kwa kushirikiana na sab sekta nyingine za elimu.

(d)       Itaendelea kusimamia na kuratibu ukarabati wa shule za Sekondari na Vyuo vya Elimu ya Ualimu.

(e)        Itatoa mafunzo kwa jumuiya za shule na vyuo kuhusu matengenezo madogo madogo na dhana ya utunzaji wa majengo na mazingira yake.

(f)         Kuratibu misaada ya wahisani pamoja na kusimamia uimarishaji wa EMIS.

(g)        Itasimamia uthibiti wa ubora wa vitabu na zana za kufundishia zinazotumika shuleni na vyuoni.

 

H:      Ofisi ya Afisa Elimu Kiongozi

26.       Mheshimiwa Spika, Afisa Elimu Kiongozi pamoja na kuratibu utekelezaji wa Sera za Elimu na Mafunzo, na Utamaduni na kutoa miongozo ya kuboresha Elimu na Utamaduni, huongoza vitengo maalumu vilivyo katika ofisi yake.  Aidha, Afisa Elimu Kiongozi husimamia shughuli za uhusiano wa Kimataifa ikiwa ni pamoja na nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki na SADC.

Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima

26.1.        Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04 Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima kilihamasisha Viongozi 759 wa Mikoa na Halmashauri kuhusu utekelezaji wa mkakati wa Kitaifa wa Elimu ya Watu Wazima na MEMKWA.  Aidha, Kitengo kilitoa mafunzo ya wiki tatu kwa wawezeshaji wa MEMKWA 496 wa ngazi ya Halmashauri, watendaji wa ngazi ya Mikoa, watendaji wa Kanda na washiriki kutoka Zanzibar.

 

Wawezeshaji Waliopewa Mafunzo ya MEMKWA

Na.

Ngazi ya Washiriki

Idadi

1.

Halmashauri

456

2.

Mikoa

21

3.

Kanda

14

4.

Zanzibar

5

 

Jumla

496

 

Mheshimiwa Spika, katika kuboresha elimu itolewayo katika madarasa ya EWW na MEMKWA, Kitengo kiliendesha mafunzo ya wawezeshaji 73 wa Elimu ya Watu Wazima na 96 wa MEMKWA katika Manispaa za Ilala, Kinondoni na Temeke.

 

Mheshimiwa Spika, idadi ya wanafunzi wanaosoma kupitia MEMKWA na wanakisomo kupitia MUKEJA ni 340,060:

 

Wanafunzi/Wanakisomo wa MEMKWA na MUKEJA

1.       

Mpango

WV/ME

WS/KE

Jumla

2.       

MEMKWA

35,850

44,210

80,060

3.       

MUKEJA

158,706

101,294

260,000

 

JUMLA

194,556

145,504

340,060

 

Katika mwaka 2004/05, Kitengo cha Elimu ya Watu Wazima kitatekeleza yafuatayo:

(a)      Kutoa mafunzo kwa wawezeshaji wa MEMKWA 1,475 na MUKEJA 2,706.

(b)     Kununua na kusambaza moduli za MEMKWA 81,132 na nakala 570 za Miongozo ya Elimu ya Watu Wazima katika Halmashauri.

(c)      Kufuatilia maendeleo ya madarasa ya MEMKWA

(d)     Kuratibu masomo ya Elimu ya Sekondari kwa njia ya Posta utakaotekelezwa chini ya Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES) 2004-2009.

(e)      Kutoa miongozo ya uendeshaji wa MEMKWA na MUKEJA

 

Kitengo cha Elimu Maalumu

26.2     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Wizara ilitoa mafunzo ya muda mfupi kwa walimu 164 wasio wataalamu wa Elimu Maalumu kuhusu Elimu Ujumuisho.  Pia, ilichapisha na kusambaza jumla ya nakala 1,500 za vitabu vya masomo mbalimbali ya shule za msingi kwa wanafunzi wasioona.

Vitabu vya Wanafunzi Wasioona Vilivyochapishwa

 

Aina

Idadi ya Nakala

1.

Hisabati Darasa la VII

500

2.

Stadi za Kazi Darasa la V

600

3.

Stadi za Kazi Darasa VI

400

 

Jumla

1,500

 

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, Wizara itanunua mtambo mpya kwa ajili ya kuchapa vitabu na makala mbalimbali za “Braille” na itatoa mafunzo ya muda mfupi kwa walimu wataalamu 36 wa wanafunzi Viziwi kuhusu Lugha ya Alama, matengenezo ya Shime Sikio (“Hearing Aids”) na utunzaji wake.  Pia, itatoa mafunzo ya muda mfupi kwa walimu 128 wasio wataalamu wa Elimu Maalumu kuhusu Elimu Ujumuisho.  Vilevile, Wizara itatengeneza na kusambaza michoro mguso 100, ramani mguso 500 na Shime Sikio 500.

 

Kitengo cha Usajili wa Shule

26.3.    Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Kitengo cha Usajili wa Shule, kilisajili shule zisizo za serikali 90.  Aidha, shule103 zimethibitishwa Mwenye Shule na Meneja.

Shule Zilizosajiliwa

Na.

Aina ya Asasi

Idadi

1.

Shule za awali

5

2.

Shule za msingi

6

3.

Shule za awali na msingi

43

4.

Shule za Sekondari

35

5.

Chuo cha Elimu  ya Ualimu

1

 

Jumla

90

 

 

Shule Zilizothibitishwa Mwenye Shule na Meneja

Na.

Aina ya Asasi

Idadi

1.

Shule za Awali

24

2.

Shule za Msingi

37

3.

Shule za Sekondari

42

Jumla

103

 

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04 shule 179 zilizojengwa kwa nguvu za wananchi zilipewa kibali cha kuanzishwa. Aidha, katika mwaka 2003/04 waombaji 326 walipewa leseni za kufundisha baada ya kuwa na sifa zinazostahili.

 

Waombaji Waliopewa Leseni za Kufundisha

Na.

Aina ya Asasi

Idadi

1.

Shahada ya Uzamili

48

2.

Shahada ya Kwanza

180

3.

Stashahada

42

4.

Cheti cha Ualimu

38

5.

Kidato cha 6

18

Jumla

326

 

Mwaka 2004/05 Kitengo cha Usajili wa Shule kimepanga:

(a)    Kushughulikia maombi 130 ya kuanzisha na kuthibitishwa Meneja, Mwenye Shule zisizo za serikali.

(b)   Kushughulikia maombi 229 ya vibali vya kuanzisha shule za sekondari.

(c)    Kushughulikia maombi 400 ya leseni za kufundisha.

(d)   Kuchapisha nakala 200,000 za vyeti vya usajili wa walimu.

(e)    Kukusanya takwimu za walimu walio kazini na kuendelea kuwasajili.

(f)     Kuratibu masuala ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Jumuiya ya Kusini mwa Afrika.

(g)    Kuratibu Utafiti Na. 3 wa Ubora wa Elimu Katika Nchi 15 za Kusini mwa Afrika.


 

Kitengo cha Elimu kwa Redio

(a)        Sehemu ya Redio

26.4     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Wizara yangu kwa kushirikiana na Redio Tanzania Dar es Salaam (RTD) iliandaa na kutangaza vipindi 104 kama ifuatavyo:- Ufundishaji Vipindi 52 na Boresha Elimu Vipindi 52.  Aidha, vipindi 96 vya masomo ya Kiingereza na Maarifa ya Jamii darasa la VI na VII vilitangazwa.  Hivyo, jumla ya vipindi vyote vilivyotangazwa vilikuwa 200.

 

Mheshimiwa Spika, mwaka 2004/05 vipindi 248 vitatangazwa kama ifuatavyo:

(a)          Itaandaa na kutangaza vipindi 52 vya ‘Boresha Elimu’ ili kuendelea kuwaelimisha wananchi kuhusu MMEM 2002-2006 na MMES 2004-2009.

(b)          Itaandaa na kutangaza vipindi 52 vya Ufundishaji mitaala mipya kwa walimu.

(c)          Itatangaza vipindi 96 vya Kiingereza na Maarifa ya Jamii darasa la VI na VII.

(d)          Itaandaa na kutangaza vipindi 48 vya Kiingereza na Maarifa ya Jamii la DV.

 

(b) Sehemu ya Elimu Dhidi ya UKIMWI

26.5.    Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Wizara iliendesha semina za wadau wanaohusika na utekelezaji wa Mpango wa Elimu Dhidi ya UKIMWI kwa waelimishaji wenza katika Asasi na Idara mbalimbali.  Aidha, mafunzo ya elimu hiyo yalitolewa kwa walimu 48 wasioona, walimu wa shule za msingi 800, walimu wa shule za sekondari 1,620, pamoja na wafanyakazi wa Baraza la Mitihani la Tanzania, Taasisi ya Elimu Tanzania, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).  Vilevile, wizara imechapisha vitabu 13,314 vya Elimu Dhidi ya UKIMWI kwa wanafunzi wa darasa la V, VI, VII na kiongozi cha mwalimu nakala 19,600.

 

Katika mwaka 2004/05, Wizara itatekeleza mambo yafuatayo kuhusu Elimu Dhidi ya UKIMWI

(a)    Kukamilisha mada za Elimu ya Kujikinga na UKIMWI kwa ajili ya kuingizwa kwenye mihtasari ya masomo chukuzi katika shule za Sekondari na vyuo vya Elimu ya Ualimu.

(b)   Itaendelea kuchapisha na kusambaza maandiko ya mafunzo ya Elimu ya Kujikinga na UKIMWI shuleni na vyuo vya Elimu ya Ualimu.

(c)    Itaendesha mafunzo kwa walimu wa shule za sekondari.

(d)   Itafanya ufuatiliaji na tathmini ya programu ya UKIMWI shuleni.

(e)    Itaendelea kutekeleza programu ya UKIMWI shuleni.

 

I:       Taasisi na Mabaraza yaliyo chini ya Wizara

Taasisi ya Elimu Tanzania (TET)

27.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04,

27.1           Taasisi ya Elimu Tanzania (TET) ilitekeleza mambo sita yafuatayo:

(a)      Ilikamilisha Mfumo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala. (“National Curriculum Development Framework”).

(b)     Ilitoa mafunzo ya MEMKWA kwa wawezeshaji 371 toka kanda zote 7 za elimu.

(c)      Ilitoa mafunzo mbalimbali kwa wakuza mitaala 33 na wafanyakazi waendeshaji 42.

(d)     Iliandaa miongozo miwili ya kufundishia na kujifunzia Hisabati na Sayansi kwa shule za msingi.

(e)      Ilifanya tathmini ya Mtaala wa Elimu ya Msingi.

(f)       Ilirekebisha Mihtasari ya Mafunzo ya Ualimu ngazi ya Cheti kwa masomo yote na kuandikia moduli .za masomo hayo.

 

Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, TET itatekeleza mambo makuu yafuatayo:

(a)          Kuchapisha na kusambaza Mfumo wa Taifa wa Ukuzaji Mitaala (“National Curriculum Development Framework”).

(b)          Kuendesha mafunzo kwa wawezeshaji wa MEMKWA mwaka wa pili na wa tatu na kufanya tathmini ya ufundishaji wa masomo sita ya MEMKWA.

(c)          Kufaragua visanduku viwili vya Sayansi na Maarifa ya Jamii kwa shule za msingi.

(d)          Kuboresha mtaala wa elimu ya msingi.

(e)          Kugharimia mafunzo ya Wakuzaji Mitaala 3 na waendeshaji 3.

(f)            Kuandika “Instructional Manual” ya masomo ya Arts, Crafts, Muziki na Michezo.

(g)          Kuitisha mikutano 12 ya majopo ya masomo.

(h)          Kuandika “Instructional Manual” 2 kwa ajili ya shule za msingi na shule za awali.

(i)            Kurekebisha mihtasari ya sekondari na ualimu ngazi ya Stashahada.

(j)            Kuandika “Methods Manuals” kwa ajili ya walimu.

(k)          Kutayarisha Moduli tatu za chati za masomo ya Sayansi, Hisabati, Maarifa Jamii na Stadi za Kazi kwa shule za msingi.

(l)            Kuandaa na kurekodi vipindi vinne vya masomo sita ya shule za msingi katika redio na televisheni.

(m)        Kuandika miongozo miwili ya kufaragua zana zinazotumika kufundishia na kujifunzia.

(n)          Kufanya semina tatu za taaluma kwa wakuza mitaala.

(o)          Kununua gari moja kwa ajili ya usimamizi, utafiti na ufuatiliaji.

(p)          Kuendesha semina sita za wakuu wa shule za msingi na sekondari.

(q)          Kuandika na kuchapisha maandiko kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake pamoja na kujumuisha mada za UKIMWI katika baadhi ya masomo ya shule za msingi na sekondari.

(r)           Kununua vifaa mbalimbali kwa ajili ya Kituo cha Maarifa Kielimu, Vyumba vya majaribio ya Sayansi na kuboresha mandhari katika maeneo ya TET.

(s)            Kuchapisha na kusambaza kijarida cha TET (TIE Newsletter) na jarida la ‘Tanzania Educational Journal’ (TEJ).

(t)            Kununua vitabu vya Dewey “Decimal Classification” kwa ajili ya maktaba ya TET.

(u)           Kuendesha semina za kuwahisisha (sensitize) wafanyakazi kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na athari zake.

(v)          Kujaribisha, kurekebisha na kusambaza maandiko kuhusu ugonjwa wa UKIMWI na madhara yake katika Shule za Msingi, Sekondari na Vyuo Elimu ya Ualimu.

 

Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW)

27.2     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima (TEWW) imetekeleza mambo yafuatayo:

(a)      Imekarabati majengo ya Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima katika Mkoa wa Morogoro (WAMO).

(b)     Imetoa mafunzo ya muda mfupi kwa watumishi 12 kuinua viwango vya elimu.

(c)      Imetoa nakala 1,000 za majarida ya “Studies in Adult Education No. 60” na Journal of “Adult Education No. 12”.

(d)     Imeboresha masomo ya Elimu kwa Njia ya Posta kwa kuhariri na kuchapa makala za Historia na Kiswahili.

(e)      Imeendesha mafunzo ya cheti cha sheria kwa wanafunzi 166, stashahada ya Elimu ya watu Wazima 159 na mafunzo ya ushonaji 12.

(f)       Imenunua kiwanja mkoa wa Dar es Salaam cha kujenga kituo cha elimu ya kujiendeleza pamoja na jengo la ofisi ya kituo cha Sumbawanga.

(g)      Imerekebisha mihtasari ya mafunzo ya Cheti na Stashahada ya juu ya EWW.

 

Katika mwaka 2004/05, Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima itatekeleza mpango wenye mambo yafuatayo kwa lengo la kuimarisha utoaji wa Elimu ya Watu Wazima na Elimu ya Kujiendeleza nje ya mfumo rasmi kwa walioikosa walipokuwa katika umri sahihi wa kuwa shuleni;

(a)      Kuendesha mafunzo ya Stashahada ya EWW kwa watendaji 150.

(b)     Kuimarisha, kurekebisha na kuchapa masomo kwa Njia ya Posta.

(c)      Kutoa mafunzo kwa wakufunzi na walimu wa muda 200.

(d)     Kuongeza wanafunzi wa Elimu ya Sekondari kwa Njia ya Posta kutoka 4,000 hadi 10,000.

(e)      Kutoa majarida ya “Studies in Adult Education No. 61” na “Journal of Adult Education 13,” (nakala 1000).

(f)       Kuongeza wanafunzi wa mafunzo ya Cheti cha Sheria kutoka 166 hadi 250.

(g)      Kutoa mafunzo ya muda mfupi kulingana na mahitaji kwa washiriki 200.

(h)      Kutoa mafunzo kwa wafanyakazi wa TEWW 60.

(i)        Kukarabati vituo vya Iringa na Tabora.

(j)       Kujenga/kununua majengo kwa ajili ya vituo vya TEWW.

(k)     Kuajiri wakufunzi 20 ili kuimarisha utendaji mikoani na Makao Makuu.

(l)        Kuimarisha kitengo cha Utafiti na kununua magari matatu kwa ajili ya ufuatiliaji wa shughuli za Taasisi mikoani.

(m)    Itaendelea kutoa elimu ya UKIMWI kwa jamii kwa kuendesha kampeni ya kitaifa ambayo inawalenga wananchi vijijini ambao hawapati taarifa sahihi juu ya mbinu za kupambana na janga la UKIMWI.

 

Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania (BOHUMATA)

27.3     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Bodi ya Huduma za Maktaba Tanzania ilitekeleza mambo yafuatayo:

(a)      Iliongeza vitabu 37,759 katika maktaba.

(b)     Ilitembelea shule na taasisi mbalimbali 227 kwa ajili ya kuhamasisha.

(c)      Iliendesha kambi za kujisomea katika vituo 5 vya Korogwe, Singida, Tukuyu, Kilosa na Songea.

(d)     Iliendesha Tamasha la Wiki ya Vitabu katika vituo 10 vya maktaba za mikoa.

(e)      Ilitoa matangazo ya zabuni kwa ajili ya ukarabati maktaba za Kagera na Tabora pamoja na kuboresha maktaba ya Mwl. J.K. Nyerere ya Butiama.

(f)       Iliendelea na ujenzi wa Maktaba ya Mkoa wa Dodoma.

(g)      Ilitoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa watumishi 57.

 

Mheshimiwa Spika, mwaka 2004/05, BOHUMATA itatekeleza mambo yafuatayo katika mpango wake wa kuendeleza maktaba nchini;

(a)      Kuimarisha na kuboresha huduma kwa kuongeza machapisho 40,000.

(b)      Kuendeleza ujenzi wa maktaba  ya mkoa wa Dodoma.

(c)      Kujenga majengo mahsusi ya Chuo cha Ukutubi na Uhifadhi Nyaraka, Bagamoyo.

(d)      Kuendesha Tamasha la Wiki ya Vitabu katika mikoa ya Kilimanjaro, Arusha, Iringa, Mbeya, Songea, Tabora, Singida, Musoma, Mwanza na Morogoro.

(e)      Kuendesha warsha na semina 4 za kuongeza uelewa na athari za UKIMWI.

 

Baraza la Mitihani la Tanzania (BAMITA)

27.4          Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Baraza la Mitihani liliendesha mitihani ya Kitaifa ya kumaliza:  (a) Elimu ya Msingi ya Darasa la VII Tanzania Bara,  (b) Elimu ya Sekondari ya Kidato cha 4;  (c) ya Kidato cha 6 na  (d) Mitihani ya Ualimu Tanzania Bara na Tanzania Visiwani.

 

Mheshimiwa Spika, kuhusu Mtihani wa Kitaifa wa kumaliza Elimu ya Msingi, yaani Darasa la VII mwaka 2003 kati ya watahiniwa 490,018 waliofanya mtihani waliofaulu walikuwa 196,273 sawa na 40.1% ikilinganishwa na 133,674 sawa na 27.1% waliofaulu mwaka 2002.

           Kielelezo Na. 27.1  Matokeo ya Mtihani ya D.VII 1998 – 2003

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

TANBIHI:  Alama ya kufaulu mwaka 2003 ilikuwa 85/200, badala ya 65/150 baada ya kuongezwa somo la nne

 

Mheshimiwa Spika, kuhusu mtihani wa kitaifa wa kidato cha 4 mwaka 2003, kati ya watahiniwa 54,904 wa shule, waliofaulu katika Daraja I, II, na III walikuwa 23,751 sawa na 38.1% ikilinganishwa na 17,939 sawa na 36.2% waliofaulu mwaka 2002.  Nawapongeza wakuu wa shule na walimu wote waliohusika na ongezeko la waliofaulu 5,812 pamoja na wanafunzi husika wote 23,751.

 

Kielelezo Na.27.2:       Matokeo ya Mtihani wa K. 4 kwa

Wanafunzi wa Shule 1998-2003

Mwaka

Idadi ya Watahiniwa

Waliofaulu

Daraja I-III

Daraja I-IV

1998

42,887

12,404

(28.9%)

32,468

(75.7%)

1999

44,172

12,774

(28.9%)

35,468

(80.0%)

2000

47,397

12,237

(25.8%)

37,140

(78.4%)

2001

50,820

14,397

(28.3%)

39,326

(77.4%)

2002

49,512

17,939

(36.1%)

42,746

(86.3%)

2003

62,359

23,751

[38.1%]

54,904

[88.1%]

 

 


Kielelezo Na27.3:  Waliofaulu K.4 D. I-III na D. 0 Shule za Serikali

[Pamoja na Zilizojengwa na Wananchi] 1999 – 2003

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Kielelezo Na.27.4:  Matokeo ya Mtihani wa Kitaifa wa Kidato cha 4 Daraja I-III Shule zote (za Serikali na zisizo za Serikali) 1998 - 2003

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 


 

Kielelezo Na. 27.5: Asilimia ya Kufaulu Kidato cha 4 katika kila Daraja

Tanzania Bara 1998 – 2003

Text Box:

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

 

Mheshimiwa Spika, uchambuzi wa matokeo ya Mtihani wa Taifa wa Kidato cha 4 mwaka 2003 unaonesha kuwa juhudi za kuboresha Elimu ya Sekondari zinazaa matunda mema kama inavyooneshwa katika kielelezo 27.5:

 

Kielelezo Na.27.6:  Matokeo ya Mtihani wa K. 4 Sekondari za Serikali na

Zisizo za Serikali kwa Pamoja, Tanzania Bara 2003

D.I+D.II+D.III = 39.1%

 


Kielelezo Na. 27.7:  Matokeo ya Mtihani wa K. 4 Sekondari za

Serikali, Tanzania Bara 2003

D.I+D.II+D.III = 45.9%

 

 

 

Kielelezo Na. 27.8:  Matokeo ya Mtihani wa K. 4 Sekondari

Zisizo za Serikali Tanzania Bara 2003

D.I+D.II+D.III = 40.4%

 


 

Kielelezo Na27.9:  Matokeo ya Mtihani wa K. 4 Sekondari

Tanzania Zanzibar 2003

D.I+D.II+D.III = 19.5%

 

Mheshimiwa Spika, kuhusu mtihani wa Kitaifa Kidato cha 6 mwaka 2002/03 kati ya watahiniwa 12,003, waliofaulu katika Daraja I, II na III walikuwa 10,584 sawa na 88.2% ikilinganishwa na 9,992 sawa na 86.3% waliofaulu mwaka 2001/02.

 

Text Box:  Kielelezo Na. 27.10:  Matokeo ya Mtihani wa K. 6, Watahiniwa Shuleni : 1998-2002/03

 

 

Text Box:  Kielelezo Na.27.11:  Matokeo ya Mtihani wa K. 6,

Watahiniwa Binafsi: 1997/98-2002/03

 

Mheshimiwa Spika, katika mitihani ya Ualimu ya mwaka 2003 waliofaulu walikuwa 18,522 sawa na 94.7% ya watahiniwa wote 19,569.  Katika mitihani ya Elimu ya Ufundi ya mwaka 2003 waliofaulu walikuwa 514 sawa na 54.6% ya watahiniwa 942 wa mitihani hiyo.

 

Text Box:  Kielelezo Na. 27.12:  Matokeo ya Mtihani wa Ualimu , 2000-2003

 

 

Text Box:  Kielelezo Na. 27.13:  Matokeo ya Mitihani wa Ufundi , 2000-2003

 

Mheshimiwa Spika, mwaka 2003/04, BAMITA imetekeleza mambo muhimu yafuatayo yaliyopendekezwa na Tume Maalumu ya Serikali iliyochunguza mianya ya uvujaji wa mitihani miaka iliopita;

(a)           Ujenzi wa Jengo la Usajili wanapofikia wageni bila kuingia ofisi zingine za Baraza la Mitihani Tanzania.

(b)          Ukarabati wa jengo la Kitengo cha Chapa na Uchapishaji.

(c)           Ununuzi wa baadhi ya mashine za uchapaji mitihani.

(d)          Ununuzi wa baadhi ya kompyuta na vifaa vyake kwa ajili ya kuandaa na kutoa matokeo ya mitihani.

(e)           Kuweka mtandao wa Kompyuta (Local Area Network-LAN) kwa madhumuni ya kutoa huduma bora.

(f)            Kufanya maandalizi ya awali ya ujenzi wa kituo cha Usahihishaji Mitihani Mbezi Wani

 

Mheshimiwa Spika, kutokana na utekelezaji huo ninayo furaha kulitaarifu Bunge lako Tukufu kuwa kuanzia mwaka jana mitihani ya Kitaifa ya Darasa la VII, Kidato cha 4 na Kidato cha 6 imeanza kuchapwa hapa nchini kwa usalama. 

 

Katika mwaka 2004/05, Baraza la Mitihani la Tanzania limejiandaa kwa ukamilifu zaidi kutekeleza wajibu wake wa kutunga na kuendesha mitihani yote ya kitaifa kwa ufanisi unaohitajika, ikiwa ni pamoja na kuendesha na kusimamia mitihani itolewayo na Bodi 9 za mitihani ya nje.  BAMITA itatekeleza malengo yafuatayo:

 

(a)      Litafanya utafiti, tathmini, usanifu na ukuzaji mitihani mbalimbali ya kitaifa.

(b)     Litaendesha mitihani ya: kumaliza elimu ya msingi; Maarifa (Qualifying Test); Kidato cha 4 na 6; kuhitimu Elimu ya Ualimu daraja la A na Stashahada (Diploma) ya Ualimu.

(c)      Litaendesha mitihani ya: Cheti cha Ufundi Sanifu (Full Technician Certificate - FTC); na Stashahada ya juu ya Uhandisi kwa niaba ya Baraza la Taifa la elimu ya Ufundi.

(d)     Litasimamia mitihani ya nje inayofanywa na watahiniwa hapa nchini.

(e)      Litaendeleza ujenzi wa kituo cha kusahihishia mitihani.

(f)       Litatengeneza programu ya kompyuta itakayowezesha utoaji wa matokeo ya kufaulu mtihani wa Kidato cha 4 na uchaguzi wa wanafunzi wa kuingia Kidato cha 5 kwa pamoja ili kuongeza ufanisi wa utoaji wa elimu.

 

Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA)

27.5     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04 Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) lilitekeleza mambo yafuatayo:

(a)          Lilitoa elimu ya sanaa na uongozi kwa wasanii 104 katika taaluma zifuatazo: Uongozi wa vikundi, sarakasi, majukwaa, uingizaji, utengenezaji ala za muziki wa kiasili, ubunifu wa ngoma na miondoko, utawala bora na utunzi wa nyimbo za kuhamasisha maendeleo ya jamii

(b)          Lilihamasisha Umma kutambua na kuthamini sanaa kwa kupitia  mashindano ya kuchora, nyimbo za halaiki, matamasha ya sanaa kwa watoto na watu wazima

(c)          Liliendesha kwa kushirikiana na Baraka Women Group, mafunzo ya kuimarisha miradi kwa kazi za ufundi wa mikono kwa akina mama katika mikoa ya Dodoma, Morogoro na Tanga.

(d)          Liliendesha warsha na semina juu ya elimu ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa wasanii 304 mikoa ya Dar es Salaam , Dodoma, Morogoro na Tanga.

(e)          Lilikamilisha michoro ya ujenzi wa ukumbi wa wazi (Open Air Theatre) na kuiwasilisha kwa Mhandishi wa Halmashauri ya Jiji kwa uhakiki.

(f)            Liliendelea na ujenzi wa ukuta kuzunguka eneo la BASATA ambapo asilimia 75 imekamilika.

(g)          Lilitoa elimu ya UKIMWI kwa mikoa 4 kwa kuendesha mashindano ya kuchora, maonyesho, matamasha na mashindano ya sanaa.

 

Katika mwaka 2004/05, BASATA litatekeleza mpango wenye mambo yafuatyo ya kukuza sanaa;

(a)      Litakuza ujuzi, elimu ya kisanii kwa wasanii wa ufundi, maonyesho na muziki kwa kuendesha kozi fupi fupi 27.

(b)     Litaendelea kutoa elimu ya Hakimiliki na Hakishiriki kwa wasanii 600, wakuzaji sanaa 90 na viongozi 13 wa vyama vya sanaa.

(c)      Litahimiza jamii kuthamini na kuboresha muziki, kuanzisha/kuimarisha matamasha, halaiki na mashindano ya sanaa mbalimbali vijijini.

(d)     Litaendesha Elimu ya Uongozi na Bajeti kwa watendaji 10.

(e)      Litaanzisha ujenzi wa ukumbi wa wazi (“Open Air Theatre”).

(f)       Litakamilisha ujenzi wa uzio.

 

Baraza la Kiswahili la Taifa (BAKITA)

27.6     Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2003/04, Baraza la Kiswahili la Taifa limetekeleza mambo yafuatayo;

(a)      Lilisanifu Istilahi mpya za mchanganyiko kwa ajili ya kuziba pengo la msamiati katika mawasiliano ya kila siku serikalini, mashirika na sekta binafsi na kuzisambaza kwa watumiaji kupitia vyombo vya habari.

(b)     Lilikusanya na kusahihisha makosa kutoka vyombo mbalimbali vya habari na kuyawasilisha katika sehemu husika ili wayazingatie.

(c)      Liliendesha semina kwa wafasiri, wakalimani, waandishi wa habari na watayarishaji wa vipindi vya Redio na Televisheni.

 

Katika mwaka wa 2004/05, Baraza la Kiswahili la Taifa litatekeleza mambo yafuatayo katika kukuza Kiswahili:

(a)          Litafanya maadhimisho ya Nane ya Siku ya Kiswahili kwa kushirikiana na asasi mbalimbali za Kiswahili, kuwatunukia na kuwaenzi waliochangia maendeleo ya Kiswahili kwa kuzingatia kauli mbiu ya «Kiswahili na Janga la UKIMWI, 2004/05».

(b)          Litaendeleza vuguvugu la kuhamasisha matumizi ya Kiswahili kwenye sekta ya biashara na viwanda kwa kufanya utafiti kupitia Shirika la Viwango Tanzania .

(c)          Litaratibu matumizi fasaha ya Kiswahili kwa vyombo vya habari kwa kuendesha Semina kwa Wahariri wa Vyombo vya Habari.

(d)          Litaendesha Warsha ya Kusanifu Istilahi 250 mchanganyiko ili kuziba pengo la msamiati na kuleta uwiano wa matumizi.

 

III.             MATATIZO KATIKA UTEKELEZAJI

28.       Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imebaini matatizo yafuatayo:

 

28.1     Baadhi ya Halmashauri zimeonesha udhaifu katika kutoa taarifa za utekelezaji na kutokufunga hesabu za mwaka za fedha za Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) kwa wakati, jambo ambalo ni kinyume na sheria, kanuni na taratibu za usimamizi bora wa fedha za umma.  Kasoro hii sharti irekebishwe mara moja kwa kuimarisha mfumo wa ukaguzi wa ndani.  Udhaifu huu umesababisha kuchelewa kwa fedha za mwaka wa tatu kutoka kwa wahisani.  Kila Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri na Maafisaelimu (Wilaya) warekebishe kasoro hii.

 

28.2          Bado baadhi ya wakurugenzi wa HALMASHAURI hawataarifu Walimu Wakuu na Kamati za Shule kiwango kilichotolewa kwa kila mwanafunzi cha Ruzuku ya Uendeshaji iliyopokelewa kutoka Serikali Kuu. Narudia maagizo yangu ya mwaka jana kuwa lazima Walimu Wakuu na Kamati za Shule wapewe taarifa hiyo ili wafuatilie fedha zao kulingana na jumla ya wanafunzi walionao ili wazipangie matumizi.

 

28.3     Baadhi ya Halmashauri kuendelea kutokuzingatia vigezo sahihi katika ujenzi na uendeshaji wa Shule za Msingi, hivyo naagiza tena:

(a)      Ujenzi wa majengo ya madarasa na nyumba za walimu uzingatie vipimo sahihi vilivyoelekezwa na Wizara.

(b)     Ukubwa wa Shule ya Msingi kwa wingi wa wanafunzi vijijini usizidi mikondo miwili yaani wanafunzi 40 wa mkondo mmoja x mikondo 2 x 7 (D I-VII)= wanafunzi 560; na MIJINI usizidi mikondo mitatu yaani 40 x 3 x 7= wanafunzi 840.

(c)      Wingi wa Wanafunzi Darasani (Class Size) wasiwe zaidi ya wanafunzi 40; wa umri sawa au karibu sawa ili wafundishike vizuri kwa kasi moja.

 

IV.             MAAMUZI MUHIMU

29.       Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/05, Wizara yangu itatekeleza maamuzi yafuatayo:

(a)           Kupunguza ada ya wanafunzi wa kutwa wa Elimu ya Sekondari kutoka Shilingi. 40,000/- na kuwa Shilingi 20,000/- kwa mwaka, na kuendelea kutoa elimu ya msingi ya bure na ya lazima kwa kila mtoto.

(b)          Kutoa Ruzuku ya Uendeshaji ya Shilingi 20,000 kwa mwanafunzi kwa Sekondari  za kutwa za Serikali kufidia punguzo la ada.

(c)           Kujenga Maabara na Maktaba katika Shule za Sekondari za Serikali zinazojengwa na wananchi kwa tenda ya Serikali.

(d)          Kuimarisha Mitaala ya Elimu ya Sekondari kwa kuingiza Elimu ya Kujitegemea; na Stadi za Kazi; na Masuala Mtambuka (Cross-cutting Issues) katika kila somo na kupunguza idadi ya masomo yatolewayo kutoka 13 kuwa 8 ili kubakia na masomo ya msingi (Core subjects) Civics, Kiswahili, English, Mathematics, Biology, History, Geography, Physics na Chemistry.  Masomo ya hiari  (options) yaani Home Economics, Computing & Information Science, Music, Fine Art, French, Arabic, Bible Knowledge, Islamic Studies, Pysical Education na Additional Maths yatafundishwa katika shule zitakazoteuliwa kwa ajili hiyo.

(e)           Kupeleka fedha na madaraka ya ununuzi wa vitabu vya kiada na ziada kwa Kamati za Shule, badala ya Halmashauri ili kuboresha uwiano wa kitabu kwa mwanafunzi kufikia kitabu kimoja kwa mwanafunzi katika shule zote za msingi za Serikali

(f)            Kutoa Ruzuku ya uendeshaji ya Shilingi 10,000 kwa mwanafunzi kwa Shule za Sekondari zisizo za Serikali ambazo sio za kibiashara na siyo seminari.

(g)           Kutoa Ruzuku ya maendeleo kwa wananchi wanaojenga sekondari ya Shilingi milioni 7.0 kwa darasa na Shilingi milioni 9.0 kwa nyumba ya mwalimu na kusaidia ujenzi wa Hosteli. Aidha, aliyeidhinishwa kuendesha Sekondari kwa ajili ya walemavu atapewa Ruzuku viwango hivyo hivyo vya Ruzuku ya maendeleo.

(h)           Kusambaza nakala za kutosha za miongozo yote muhimu ya MMEM na MMES kwa kila Halmashauri na shule zote za msingi na sekondari nchini.

 

V.                SHUKRANI NA PONGEZI

30.       Mheshimiwa Spika, mafanikio ya mwaka 2003/04, yametokana na ushirikiano mkubwa uliotolewa na wananchi kwa mchango wao wa hali na mali katika kushiriki na kuchangia mipango ya elimu na utamaduni. Waheshimiwa Wabunge, kama mnavyofahamu sehemu kubwa ya maendeleo katika Sekta ya elimu hutokana na moyo wa kujitolea katika kujenga majengo ya shule hususan madarasa na Nyumba za Walimu. Nachukua fursa hii kuwapongeza wananchi pamoja na viongozi wote wa Mikoa, Wilaya, Vijiji pamoja na Waheshimiwa Wabunge na Waheshimiwa Madiwani kwa mchango wao walioutoa katika kufanikisha ujenzi wa shule na utoaji na uendeshaji wa elimu na utamaduni.

 

31.       Mheshimiwa Spika, nazishukuru nchi rafiki na mashirika ya kimataifa kwa michango yao katika kuandaa na kufanikisha utekelezaji wa mipango ya elimu na utamaduni katika mwaka 2003/04. Nchi hizo rafiki na wahisani ni: Sweden, Japan, Norway, Uingereza, Ufaransa, Ireland, Uholanzi, Finland, Canada, Ujerumani, Ubelgiji, China na Korea ya Kusini.  Mashirika yaliyochangia elimu na utamaduni ni Benki ya Dunia, ADB, Sida, NORAD, ,GTZ, DFID,  WFP, UNICEF, UNESCO, UNFPA , UNDP, CIDA, ILO, EU, JICA, USAID, JOVC, VSO,Celtel, CBP, Peace Corps, Book Aid International, Aga Khan Education Foundation, Plan International, World Vision, Ireland Aid, Care International na Mashirika mbalimbali yasiyokuwa ya kiserikali.

 

32.       Mheshimiwa Spika, pamoja na misaada utekelezaji wa mipango ya elimu na utamaduni kwa mwaka 2003/04 haungefanikiwa na kukamilika katika kiwango nilichoelezea bila jitihada, ushirikiano na uongozi wa pamoja katika Wizara yangu.  Natoa shukrani zangu za pekee kwa Naibu Waziri wa Wizara ya Elimu na Utamaduni, Mheshimiwa Bujiku K. P. Sakila, Mbunge wa Jimbo la Kwimba, kwa ushirikiano, uaminifu na uadilifu wake aliouonesha kwangu na kwa viongozi wetu Wakuu na kwa ushirikiano wake na wenzetu wote Wizarani.  Ninapenda pia kutoa shukrani zangu kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Elimu na Utamaduni Bibi Mwatumu J. Malale, pamoja na wasaidizi wake akiwemo Afisaelimu Kiongozi, Wakurugenzi wa Idara wote, Viongozi wa Elimu katika ngazi mbalimbali, Waalimu na Wafanyakazi wengine wote wa Wizara yangu kwa ushirikiano walionipa katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara hususan jukumu mama la utoaji elimu na ukuzaji wa utamaduni kwa mwaka 2003/04; na katika maandalizi ya Bajeti hii.

 

33.       Mheshimiwa Spika, natoa shukrani zangu pia kwa Wenyeviti, Wakurugenzi Watendaji, Makatibu Watendaji na Wajumbe wa Mabaraza na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara yangu na wafanyakazi wengine wote katika ngazi mbalimbali kwa kazi nzuri waliyoifanya ya kuimarisha na kuendeleza elimu na utamaduni. Pia, natoa shukurani na pongezi za pekee kwa uongozi wa Chama cha Walimu Tanzania (CWT) kwa ushirikiano wao mzuri na ari yao ya kutatua matatizo ya walimu kwa kushirikiana na Wizara yangu na Serikali kwa ujumla.  Napenda kuwashukuru viongozi wa tawi la TUGHE la Makao Makuu ya Wizara kwa ushirikiano na ushauri wao katika kushughulikia masuala ya wafanyakazi.

 

VI        MAKADIRIO YA BAJETI YA WIZARA

 

34.       Mheshimiwa Spika, baada ya kueleza yote hayo, ninaomba sasa Bunge lako Tukufu baada ya kuijadili hoja yangu pamoja na kuzingatia Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, lipitishe makadirio ya matumizi ya