HOTUBA YA WAZIRI WA
UJENZI, MHESHIMIWA JOHN P. MAGUFULI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO WA
MAENDELEO NA MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2004/05
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba
Bunge lako Tukufu likubali kupitisha makadirio ya matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha wa 2004/2005.
2.
Mheshimiwa Spika,
DIRA YA WIZARA
3.
Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ya Ujenzi ni kuendeleza Sekta ya Ujenzi ili iwe endelevu,
yenye ufanisi na inayotoa huduma bora na nafuu katika
mazingira ya ushindani ili kuchochea na kuleta ufanisi katika maendeleo ya
jamii na kiuchumi na hivyo kuchangia kikamilifu katika ukuaji wa uchumi wa
nchi.
Aidha, katika kuendeleza
Sekta ya Ujenzi, ili kutumia kikamilifu faida ya Kijiografia iliyonayo Tanzania
katika kuziunganisha nchi kadhaa tunazopakana nazo na Bandari za Dar es Salaam,
Tanga, Mwanza, Kigoma, Bukoba na Mtwara, Wizara yangu inaendelea kutekeleza
ukarabati na ujenzi wa Barabara Kuu kwa kiwango cha lami katika Kanda Kuu Tisa
za Usafirishaji kwa kadri hali ya uchumi wetu na bajeti inavyoruhusu.
4. Mheshimiwa
Spika, baada ya kukamilika uanzishwaji wa
Wakala wa Barabara (TANROADS) na Wakala wa Majengo (TBA), Taasisi hizi sasa
ndizo zenye majukumu ya utekelezaji wa kazi za barabara na majengo na nyumba za
Serikali. Kazi hizi zilikuwa zinafanywa na Wizara moja
kwa moja hapo awali. Majukumu
yaliyobaki yanayoendelea kutekelezwa na Wizara
yanahusu:
·
Kuandaa Sera, kubuni Mikakati na
kupanga Mipango inayolenga katika ukuzaji, uimarishaji na uendelezaji wa sekta
ya ujenzi nchini katika muda mfupi, wa kati na mrefu.
·
Kusimamia utekelezaji wa Sera
ya Taifa ya Ujenzi kwa kuzingatia mikakati iliyowekwa.
·
Kusimamia uendeshaji wa shughuli za Bodi ya Mfuko wa
Barabara, Wakala wa Barabara, Wakala wa Majengo pamoja na Wakala nyingine
zinazotarajiwa kuundwa chini ya Wizara kama vile Wakala wa Ufundi na Umeme
(Tanzania Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency - TEMESA) na
Wakala wa Bohari Kuu ya Serikali (Government Stores Agency – GSA).
·
Kuratibu shughuli za Taasisi zilizo chini ya Wizara ya
Ujenzi ambazo ni Baraza la Taifa la Ujenzi na Bodi za
Usajili wa Makandarasi, Wahandisi, Wasanifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi na
Usimamizi wa Vifaa.
·
Kutafuta fedha za nje na za
ndani za kugharamia miradi ya barabara, madaraja, vivuko n.k.
·
Kuandaa na kusimamia viwango
vya ubora wa kazi za ujenzi, ukarabati pamoja na matengenezo ya barabara;
ujenzi nyumba na majengo ya Serikali; vifaa vya kawaida vitumiwavyo na
Serikali; mitambo; magari na vifaa vya umeme.
·
Kusimamia shughuli za Usalama wa Barabara (Road
Safety)
·
Kusimamia shughuli za ununuzi, ukarabati na matengenezo ya magari, viyoyozi na vifaa vya elektroniki;
kuendesha vivuko na ukodishaji wa magari, mitambo ya kokoto na mitambo ya
barabara ambavyo ni
·
Kusimamia Maendeleo ya Watumishi wa
Wizara.
Aidha,
majukumu mengine ya Wizara yanayotekelezwa kupitia Wakala, Baraza la Ujenzi,
Bodi na Vituo/Vyuo vilivyo chini ya Wizara ni
Mikakati ya
Utekelezaji
5. Mheshimiwa
Spika, ili kufanikisha majukumu
yaliyotajwa hapo juu Wizara imejiwekea mikakati ifuatayo:-
·
Kutafuta vyanzo vya ziada vya fedha za Mfuko wa Barabara ili kukidhi mahitaji ya matengenezo ya mtandao
mzima wa barabara.
·
Kutoa kipaumbele katika ukarabati na
ujenzi wa barabara kwa kufuata Kanda Kuu za Usafirishaji, Barabara za Mikoa na
za Wilaya ambazo ni muhimu kwa huduma za usafirishaji wa mazao ya kilimo na
huduma nyingine muhimu za kitaifa.
·
·
Kuweka mazingira mazuri ya upatikanaji wa mitambo ya ujenzi kwa kuimarisha karakana za Serikali na
kuhamasisha watu binafsi kuanzisha kampuni za kukodisha mitambo.
·
Kukaribisha Sekta binafsi kushiriki katika ujenzi wa miradi ya barabara na majengo ya Serikali. Aidha, Wizara
yangu inakamilisha Mwongozo rasmi utakaoweka wazi utaratibu wa
Ushiriki wa Sekta Binafsi katika shughuli za ujenzi wa barabara, majengo na
madaraja.
·
Kuendeleza mafunzo kwa
Wahandisi Washauri na Makandarasi wa kizalendo ili wasimamie na kutekeleza
vizuri mikataba ya ujenzi na matengenezo ya barabara.
·
Kusimamia Sheria ya Udhibiti wa
Uzito wa Magari na matumizi bora ya barabara kwa kuwashirikisha wadau wote.
·
Kuimarisha huduma za vivuko nchini kwa
kununua vivuko vingine vipya vyenye uwezo mkubwa na kuvifanyia ukarabati vivuko
vilivyopo hivi sasa.
·
Kuwaelimisha wananchi ili
waweze kutambua mipaka ya maeneo ya barabara (Road Reserve) na kutayarisha
ramani za barabara zitakazoonyesha mipaka ya miliki ya barabara zote nchini.
Aidha uwekaji wa alama za kuonyesha mipaka ya maeneo
ya barabara nao sasa umepewa umuhimu katika miradi yote inayotekelezwa.
·
Kuendeleza teknolojia ya nguvu kazi ili
kuwapa uwezo wananchi wengi zaidi kushiriki katika kazi za matengenezo ya
barabara katika maeneo
·
Kuimarisha uwezo wa
kiutendaji wa Bodi na Taasisi zilizo chini ya Wizara ili ziweze kufanya kazi
zake kwa ufanisi zaidi.
·
Kuendesha mafunzo kwa
Wafanyakazi wa Wizara ili kuwajengea uwezo wao wa kufanya kazi.
·
Kukamilisha uanzishwaji wa
Wakala wa Ufundi na Umeme (TEMESA) na Wakala wa Bohari Kuu ya Serikali (GSA).
USHIRIKIANO WA KIKANDA
Mtandao wa Barabara za Jumuiya ya Afrika Mashariki na NEPAD
6. Mheshimiwa
Spika, Nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC) zimepanga
kutekeleza miradi ya barabara katika Kanda tano (5). Miradi inayohusika ni ile iliyokubaliwa katika Mkutano wa mwaka 1998 (Kiambatanisho
Na. 11) na pia miradi mipya ambayo ilikubaliwa iongezwe kwenye mtandao wa
miradi ya barabara ya Jumuiya ya Afrika Mashariki katika Mkutano wa mashauriano
kati ya Wahisani na Nchi Wanachama wa Jumuia ya Afrika Mashariki uliofanyika
tarehe 29 – 30 Aprili, 2003 (Kiambatanisho Na. 11A). Wahisani walikubaliana na
utekelezaji wa miradi iliyokuwepo toka mwaka 1998 na miradi mipya iliyoongezwa.
Nchi wanachama wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki kwa
kushirikiana na Sekretariati ya Jumuiya hiyo tunaendelea kuwasiliana na
Wahisani kwa lengo la kufanikisha ahadi hiyo. Hali halisi ya maendeleo ya
upatikanaji fedha ama utekelezaji wa kila mradi ni
7. Mheshimiwa
Spika, mwezi Oktoba mwaka 2003 kilifanyika kikao cha Wakuu wa Nchi na Serikali za nchi za Mashariki mwa Afrika (Eastern
Africa Sub-region Summit) mjini
Ukanda
wa Maendeleo wa Mtwara (Mtwara Development Corridor –
MtDC)
8. Mheshimiwa Spika,
Utekelezaji wa Programu ya uendelezaji wa Ukanda wa
Maendeleo wa Mtwara unaendelea kwa miradi mikubwa (anchor projects)
mitatu. Hatua zilizofikiwa kwa sasa ni
i) Barabara ya Mtwara – Masasi – Songea –
Kazi ya upembuzi yakinifu
(Feasibility Study) ilimalizika mwezi Januari 2004. Kazi ya usanifu wa kilomita 200 kati ya Songea na Matemanga itafanyika
katika mwaka wa fedha 2004/05 kwa kugharamiwa na fedha zilizobaki baada ya
kukamilisha upembuzi yakinifu.
ii)
Daraja la Umoja kati ya Tanzania na Msumbiji
Juhudi
za kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa Daraja hili
zinaendelea. Serikali ya Japan imekubali kimsingi tangu mwezi Oktoba 2003 kuwa
itasaidia ujenzi wa daraja hili na imeahidi kuleta
ujumbe
iii)
Mradi wa uzalishaji umeme kwa kutumia makaa ya mawe ya
Mchuchuma – Katewaka
Serikali
imeendelea kufanya majadiliano na wawekezaji wa mradi
huu kwa lengo la kuhakikisha kuwa mradi utakapotekelezwa utakuwa na manufaa kwa
uchumi wa nchi hususan sekta ya umeme. Serikali iliona ni
vema kwanza ijiridhishe na matokeo ya awali ya utafiti uliofanywa na wawekezaji
kwa kuzingatia vigezo vya kiuchumi, kiufundi, kifedha na pia masuala ya
mazingira. Mnamo mwezi wa Mei 2004 Serikali
imewaelekeza NDC na Wizara ya Nishati na Madini kufanya majadiliano na
wawekezaji wa mradi kwa kuzingatia vigezo vilivyotajwa hapo juu.
9. Mheshimiwa Spika, Mwezi Mei
2004 ulifanyika mkutano huko
MAPITIO
YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA WIZARA KWA MWAKA 2003/04.
10. Mheshimiwa Spika, Baada ya kutoa maelezo kuhusu Dira,
Majukumu na Mikakati ya Wizara yangu, naomba sasa
kulieleza Bunge lako Tukufu hali ya utekelezaji wa malengo ya Wizara kwa mwaka
wa fedha wa 2003/04.
Ukusanyaji wa Mapato kwa mwaka 2003/04
11. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha wa 2003/2004, Wizara ilipanga kukusanya jumla ya
shilingi 3,724,943,000.00 kupitia Idara zake zinazokusanya Mapato ambazo ni
Ufundi na Umeme, Ugavi na Huduma na Utawala. Hadi kufikia mwishoni mwa mwezi
Mei, 2004, jumla ya shilingi 3,072,020,781.58 zilikusanywa ambazo ni
asilimia 82.5 ya malengo
yaliyowekwa. Mchanganuo wa mapato hayo kwa kila idara
umeonyeshwa kwenye Kiambatanisho
Na. 1 kilichoko ukurasa wa 58.
Matumizi ya
Kawaida Mwaka 2003/04
12. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2003/04
Wizara ilitengewa jumla ya shilingi 59,689,799,900 za Matumizi ya Kawaida. Kati
ya fedha hizi shilingi 45,156,999,600 zilikuwa fedha za Mfuko wa Barabara na shilingi 14,522,800,300 zilikuwa za Matumizi
Mengineyo na Mishahara.
13. Mheshimiwa
Spika, hadi kufikia mwishoni mwa mwezi Mei, 2004 jumla ya shilingi
11,381,802,114 za Matumizi ya Kawaida zilikuwa zimetumika ambazo ni sawa na asilimia 78.4 ya fedha zote zilizotengwa kwa
mwaka huu. Pia hadi Mei, 2004
jumla ya shilingi milioni 43,940 za Mfuko wa Barabara
sawa na asilimia 97 ya fedha zilizotengwa kwa mwaka huu zilikuwa zimetolewa kwa
Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi.
Muhtasari wa Matumizi ya Kawaida kwa
mwaka 2003/04, umeonyeshwa katika Kiambatanisho
Na. 2 kilichoko ukurasa wa 59.
Mpango wa Matengenezo ya Barabara Kuu na za Mikoa kwa Mwaka 2003/04
14. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2003/04, matengenezo ya Barabara Kuu na zile za Mikoa yaliyopangwa yalilenga kuhudumia kilomita
16,274 na madaraja 1,809 kwa kutumia jumla ya shilingi 61,399,954,000 ambapo
shilingi 40,234,901,000 ni kutoka Mfuko wa Barabara na shilingi 21,165,063,000
zilikuwa fedha za kigeni.
15.
Mheshimiwa Spika, hadi kufikia mwishoni mwa
mwezi Mei 2004, kazi zilizokuwa zimeanza na zinaendelea
kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara zinahusisha mikataba 705 ya makandarasi
yenye thamani ya shilingi 31,024,700,000 na kazi zinazofanywa na TANROADS moja
kwa moja (Force Account) zenye thamani ya shilingi 2,861,210,000
Aidha, hadi
mwishoni mwa mwezi Mei 2004, jumla ya barabara zenye kilomita 10,898 na madaraja 1,119 vilifanyiwa matengenezo ya aina
mbalimbali.
Matengenezo ya Miundo Mbinu iliyoharibiwa na Mvua za El-Nino
16. Mheshimiwa
Spika, mradi huu unahusisha Ukarabati na
Matengenezo ya Barabara Kuu katika Kanda nne zenye urefu wa km 2,643
zilizoharibiwa na mvua za El Nino za Mwaka 1997/98. Kazi zinazofanywa kwenye
Barabara za Kanda hizi ni pamoja na ukarabati/matengenezo
ya madaraja madogo na makalavati, kutengeneza matuta ya barabara na kuweka
changarawe kwenye sehemu zilizoharibika.
17. Mheshimiwa
Spika, urefu halisi unaohusika na
Ukarabati/Matengenezo haya kwenye Kanda zote nne ni Km 845 ambazo zimegawanywa
·
Ukanda wa Ziwa (Mwanza na
Mara) km 128; barabara za Usagara-Katoro, Nyamswa-Ikoma na Nyanguge-Musoma.
Sehemu kubwa ya matengenezo zaidi ya asilimia 90 imekamilika.
·
Ukanda wa Kati –Magharibi
(Tabora, Rukwa na Singida) km 325; Barabara za Tabora-Nzega, Tabora-Ipole-Koga,
Ipole-Rungwa, Manyoni-Rungwa na Mpanda-Koga. Kazi zinatarajiwa kukamilika mwezi
Oktoba 2004.
·
Ukanda wa Kusini (Iringa,
·
Ukanda wa Magharibi (Kigoma
na Rukwa) km 189, barabara za Sumbawanga-Kasesya, Mpanda-Uvinza, Uvinza-Kanyani
na Mwandiga-Manyovu. Mkandarasi anaendelea na kazi.
Mradi
huu unafadhiliwa kwa pamoja kati ya Benki ya Maendeleo
ya Afrika (ADB) na Serikali ya
Matengenezo ya Barabara chini ya RUSIRM
18. Mheshimiwa Spika, mradi wa RUSIRM ni wa muda wa Miaka 5
ya matengenezo ya barabara kwa mikoa ya Iringa Kusini na
Mradi
unagharamiwa kwa pamoja kati ya Jumuiya ya nchi za
Ulaya (EU) na Serikali ya
Hadi kufikia Machi 2004 zaidi ya km
600 kati ya km 898 zimefanyiwa ukarabati mkubwa kwa
mikoa ya Iringa na
Utekelezaji wa Miradi ya Maendeleo ya Barabara Kuu na za Mikoa kwa mwaka
2003/04
19. Mheshimiwa Spika, Katika mwaka wa fedha 2003/2004 Wizara ilitengewa jumla ya shilingi
milioni 157,180.04 kwa Miradi ya Maendeleo ambapo shilingi milioni 48,989.47
zilikuwa fedha za hapa na shilingi milioni 108,191.57 zilikuwa fedha za nje.
Kati ya fedha za hapa shilingi milioni 4,470.47 zilikuwa fedha za Mfuko wa Barabara na shilingi milioni 44,519.00 zilikuwa fedha za
Maendeleo kutoka Hazina.
Hadi
kufikia mwishoni mwa mwezi Mei 2004, shilingi milioni 43,340.95 sawa na 97.4% ya fedha zote za Maendeleo kutoka HAZINA na
shilingi milioni 3,994 sawa na asilimia 89 ya fedha za Mfuko wa Barabara
zilizopangwa kwa mwaka 2003/04 zilikwishatolewa. Aidha, katika kipindi hiki Bajeti ya
Maendeleo ilipunguzwa kwa shilingi bilioni 1.178 ili
kuchangia dharura za ununuzi na usambazaji wa chakula cha njaa na kusaidia gharama
za uzalishaji umeme.
Taarifa ya
utekelezaji ya mradi kwa mradi zimeonyeshwa kwenye Kiambatanisho Na. 3 ukurasa wa 60 hadi
62 kwa miradi ya Barabara Kuu na Kiambatanisho
Na. 4 ukurasa wa 63 kwa miradi ya Barabara za Mikoa.
Utelelezaji wa
mwaka 2003/04 wa Wakala, Bodi, Baraza la Ujenzi, Vituo na Vyuo vilivyo
chini ya Wizara
20. Mheshimiwa
Spika, utekelezaji wa Taasisi zilizo chini ya
Wizara kwa mwaka 2003/04 ni
Mafanikio na Matatizo
yaliyojitokeza Wakati wa Utekelezaji wa Malengo ya mwaka 2003/04
21. Mheshimiwa
Spika, Kwa ujumla Wizara imepata mafanikio mengi katika utekelezaji wa mipango ya mwaka 2003/04,
i)
Kukamilika na kufunguliwa
rasmi kwa Daraja la Mkapa katika Mto Rufiji tarehe 2.8.2003. Aidha,
madaraja mengine 23 kati ya Tunduma – Sumbawanga, Tanga – Horohoro na barabara ya TANZAM yamekamilika.
ii)
Kuweka Mawe ya Msingi kwa ajili ya ujenzi unaoendelea
wa kiwango cha lami wa barabara zifuatazo:
·
Mbwemkulu-Mingoyo (km 95)
·
Dodoma-Manyoni-Singida (km
246)
·
Ilula-Tinde/Isaka-Nzega (km
168)
·
Songwe – Tunduma (km 70)
Aidha,
barabara nyingi zinaendelea kukarabatiwa kwa kiwango
cha lami na changarawe ili nchi yote iendelee kupitika. Pia,
madaraja yanaendelea kutengenezwa katika barabara mbalimbali.
iii)
Daraja la Umoja: Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
iv)
Daraja la
Kigamboni: Katika mwaka huu 2004 Mfuko wa
Hifadhi ya Jamii (NSSF) wameonyesha nia ya kuwekeza katika daraja la Kigamboni.
Serikali na NSSF tumeingia katika Mkataba wa Maelewano
ambapo katika kipindi cha miezi sita, NSSF watawasilisha Serikalini mpango wao
madhubuti wa kujenga daraja hili. Baada
ya hapo mapendekezo
v) Kivuko cha
Ukara: Kivuko hiki kimeshanunuliwa na
kazi ya kukifunga itakamilika mwezi Juni mwaka 2004. Aidha,
Kivuko cha Kilombero ambacho kilinunuliwa mwaka 2002/03 kinaendelea kufanya
kazi vizuri.
vi) Usajili wa magari
kwa namba za Serikali: Usajili wa magari ya Serikali na
ya miradi uliendelea kufanyika ili kupunguza matumizi mabaya ya magari,
pikipiki na mitambo ya Serikali. Kuanzia mwezi Januari 2002 hadi kufikia Mei
2004, usajili umefanyika kama ifuatavyo: - magari 3,204 yamesajiliwa kwa namba
za ST, magari 2,834 kwa namba za SU, magari 477 kwa namba za SM, magari 4,301
kwa namba za DFP na magari 105 kwa namba za PT. Aidha pikipiki 1207
zilisajiliwa kwa namba za ST, 338 kwa namba za SU, 215 kwa namba za SM, 1,487
kwa namba za DFP na 3 kwa namba za PT. Halikadhalika ilisajiliwa mitambo 199
kwa namba za CW, 93 kwa namba za SU, 21 kwa namba za SM na 81 kwa namba za DFP. Hivyo kwa
kipindi hicho jumla ya magari 11,026, pikipiki 3,250 na mitambo 394 imesajiliwa
kwa namba za Serikali na kufanya jumla ya vifaa vilivyosajiliwa tangu zoezi
lianze kuwa 15,064.
vii) Uuzaji na Ujenzi wa Nyumba za Watumishi:
Wakala wa
Majengo umewauzia watumishi wa Serikali na wa Mashirika ya Umma nyumba zipatazo
5,248 kuanzia mwaka 2002 hadi sasa na fedha zinazopatikana zinatumika kujenga
nyumba nyingine. Jumla ya shilingi 41,567,805,337.00 zinatarajiwa kukusanywa
kutokana na mauzo ya nyumba hizi. Katika nyumba 5,248
zilizouzwa, nyumba 4,234 wameuziwa Wafanyakazi wa
Serikali na nyumba 1,188 zimeuzwa kwa Wafanyakazi wa Mamlaka ya Bandari (THA).
Aidha nyumba zipatazo 2,580 za Shirika la Reli (TRC) zitauzwa kwa Watumishi wanaoishi katika nyumba hizo.
Wakala pia umejenga
nyumba 173
Aidha, Wakala kwa kushirikiana na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu hivi karibuni
umekamilisha kuandaa mwongozo wa utaratibu wa kuingia ubia wa wawekezaji
binafsi kwa ajili ya kuendeleza “Prime Areas” zilizo chini ya Wakala. Mwongozo huo utaanza kutumika mwaka 2004/05.
viii) Kupungua kwa Tatizo
la Kuzidisha Uzito wa Magari katika Barabara zetu: Tatizo la
kuzidisha uzito katika barabara zetu linaendelea kupungua ambapo mpaka sasa
magari yanayozidisha uzito ni chini ya asilimia 10 ukilinganisha na asilimia 30
kwa mwaka 1998. Mafanikio haya yote yanatokana na
Wizara kuchukua hatua zifuatazo:
·
Kuendesha kampeni za kuwaelimisha wadau wetu kuhusu
suala la Usalama Barabarani kupitia vipindi vya Radio na
Televisheni pia makala katika magazeti.
·
Kufunga mizani ya kisasa na
kununua mizani 18 inayohamishika (mobile).
·
Kufukuza wafanyakazi 140 katika vituo vya mizani baada
ya kutuhumiwa kujihusisha na rushwa.
22. Mheshimiwa
Spika, baadhi ya matatizo yaliyoathiri utekelezaji wa kazi zilizopangwa kwa mwaka 2003/04 ni pamoja na:
·
Ufanisi duni wa baadhi ya
makandarasi katika kutekeleza kazi za barabara.
·
Upungufu wa mitambo ya
kuwawezesha makandarasi wazalendo kumudu utekelezaji wa kazi za barabara.
·
Baadhi ya wahisani kuchelewa kutoa fedha kufuatana na ratiba iliyowekwa hivyo kuchelewesha miradi kuanza ama
malipo kwa makandarasi kwa muda uliokubaliwa katika mikataba.
·
Upungufu wa fedha
kulinganisha na mahitaji halisi ya miradi ya maendeleo na kazi za ujenzi na
matengenezo ya barabara pamoja na ujenzi wa nyumba za kuwauzia wafanyakazi wa
Serikali.
·
Utaratibu mrefu wa kutoa
zabuni (hasa kwa miradi ya Wahisani) umechelewesha kuanza kwa utekelezaji wa
baadhi ya miradi.
KAZI
ZILIZOPANGWA KUFANYIKA KATIKA MWAKA WA FEDHA 2004/05
Mpango wa Matengenezo ya Barabara Kuu na za Mikoa 2004/05
23. Mheshimiwa
Spika, malengo ya mwaka wa 2004/05 ni
kufanyia matengenezo Barabara Kuu na Barabara za Mikoa zenye urefu wa kilomita
13,328 na madaraja 1,692. Fedha zilizopangwa kutumika ni
shilingi 56,784,146,000 ambapo shilingi 45,788,352,000 ni za Mfuko wa Barabara
na shilingi 10,995,794,000 ni fedha za kigeni.
Mchanganuo
kamili wa Mpango wa Matengenezo ya Barabara Kuu na za
Mikoa kwa mwaka 2004/05 ni
Mpango wa Ukarabati wa Barabara Kuu
na za Mikoa kwa mwaka 2004/05
24. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi
inakadiria kutumia jumla ya shilingi milioni 89,606.6 fedha za ndani na shilingi milioni 129,623.4 fedha za kigeni katika
utekelezaji wa miradi mbalimbali ya upembuzi yakinifu, usanifu, ukarabati na
ujenzi wa Barabara Kuu na za Mikoa. Kati ya fedha za ndani, shilingi milioni
5,087.6 ni fedha za Mfuko wa Barabara na shilingi
milioni 84,519 ni fedha za Maendeleo kutoka Hazina.
25. Mheshimiwa
Spika, mgawanyo wa fedha za ndani kwa
mwaka 2004/05 umezingatia mambo yafuatayo:
(i)
Utekelezaji wa Mpango Maalum
wa ujenzi wa barabara za Somanga-Lindi-Mingoyo na Dodoma-Manyoni-Singida kwa
kutumia fedha za ndani. Jumla ya shilingi 49,950,000,000.00 fedha za hapa
zimetengwa kwa mradi huu.
(ii)
Kuelekeza mgawanyo wa
rasilimali kwenye miradi ya Barabara Kuu na za Mikoa inayoendelea. Jumla ya
shilingi zipatazo 29,334,000,000.00 fedha za hapa kutoka Mfuko Mkuu wa Serikali na shilingi 5,087,600,000.00 kutoka Mfuko wa
Barabara zimetengwa kwa miradi hii.
(iii)
Kutenga rasilimali za kutosha kwenye miradi mipya
yenye fedha za kigeni na miradi mipya ya upembuzi
yakinifu na usanifu wa barabara mbalimbali zinazotarajiwa kujengwa. Jumla ya
shilingi zipatazo milioni 5,235,000,000.00 fedha za ndani zimetengwa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi hii.
Muhtasari
wa Mpango wa Ujenzi/Ukarabati wa Barabara Kuu
umeonyeshwa katika Kiambatanisho Na. 5 kilichoko
ukurasa wa 64 hadi 70 na ule wa Barabara za Mikoa katika
Kiambatanisho Na. 6 kilichoko ukurasa wa 71 hadi 76.
USALAMA
BARABARANI NA UDHIBITI WA UZITO WA MAGARI
26. Mheshimiwa
Spika, ajali
za barabarani ni tatizo kubwa hapa nchini. Tathmini ya
hasara zitokanazo na ajali za barabarani inaonyesha
kuwa ajali huchangia hasara ya kati ya asilimia 1 na 2 katika pato la Taifa kwa
mwaka. Wizara ya Ujenzi imekuwa ikichukua hatua mbalimbali za kupunguza ajali na uharibifu wa barabara. Hatua hizo ni
pamoja na:-
·
Kuanzisha mfumo wa kisasa wa uwekaji wa takwimu za
ajali kwenye Kompyuta ili kurahisisha upatikanaji na uchambuzi wa takwimu,
kufahamu sehemu sugu za ajali na kuzifanyia utafiti na kuzirekebisha ili
kuondoa vyanzo vya ajali. Mafunzo yametolewa kwa
Askari wa usalama barabarani na Wahandisi kuhusu uwekaji na uchambuzi wa
Takwimu za ajali kwa kutumia Kompyuta. Aidha, tafiti za vyanzo vya ajali
zinaendelea kufanyika na kuchukua hatua za kuzuia
ajali.
·
Kwa kushirikiana na Taasisi
ya Elimu Tanzania (TIE) iliyoko chini ya Wizara ya Elimu tumeandaa mitaala kwa
ajili ya somo la elimu ya usalama barabarani katika Shule za Msingi, Sekondari
na Vyuo vya Walimu nchini. Majaribio ya kufundisha somo hili katika baadhi ya
Shule za Msingi na Sekondari katika mikoa ya Pwani,
·
Kufanya Utafiti na
kupendekeza mifumo bora ya ukaguzi wa magari, shule za udereva na utoaji wa
leseni za udereva.
·
Kutoa elimu ya usalama barabarani kwa
njia ya redio, televisheni, magazeti, vipeperushi n.k. kwa watumiaji wa
barabara wa aina zote.
·
Kudhibiti uzito wa magari
makubwa katika barabara zetu kwa kutumia mizani pamoja na kuwaelemisha
wasafirishaji kuhusu ufungaji wa mizigo na athari za uzidishaji uzito. Aidha,
mzani mmoja unaohamishika umenunuliwa, Ujenzi wa
Mizani ya Mwendakulima (Shinyanga) na Mikumi (Morogoro) umekamilika na Mzani wa
Mikese (Morogoro) uko katika hatua za mwisho kukamilika.
·
Kuandaa mfumo wa usalama
barabarani utakaozingatiwa katika kila hatua ya ujenzi wa barabara, yaani ‘Road
Safety Audit System’.
·
Kuandaa rasimu za kanuni za barabara, miongozo ya
uendeshaji magari na ya kufundishia wakaguzi wa
magari.
·
·
Kukamilisha Mpango Kabambe kuhusu masuala ya usalama
barabarani (Road Safety Master Plan) mnamo Juni, 2004.
Malengo
ya Mwaka 2004/2005
27. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha wa 2004/2005
kazi zifuatazo zimepangwa kutekelezwa:
·
Kuendelea kuwaelemisha Wananchi juu ya utumiaji salama
wa barabara zetu kupitia vyombo mbalimbali vya habari.
·
Kujenga mzani wa kisasa
katika eneo la Mpemba (Tunduma) na kuanza maandalizi ya ujenzi wa mizani
mingine maeneo ya Nangurukuru na Mingoyo mkoani Lindi na mwigine mkoani
·
Kuendelea kudhibiti uzito wa
magari katika barabara zetu.
·
Kuendelea kuendesha mafunzo ya uwekaji wa takwimu za ajali kwenye kompyuta na uchambuzi wake.
·
Kuendelea na tathimini ya
mpango wa kufundisha somo la elimu ya usalama barabarani katika Shule za Msingi
na Sekondari.
MATUMIZI YA
TEKNOLOJIA YA NGUVU KAZI KATIKA UJENZI NA MATENGENEZO YA BARABARA
28. Mheshimiwa
Spika, Nia ya Serikali ni kuondoa umaskini
ifikapo mwaka 2025. Katika kutekeleza
azma hii, Wizara yangu imeweza kuwaongezea wananchi kipato kwa
kuwapatia ajira za matengenezo ya barabara kwa kutumia nguvu kazi ambapo sio tu
wanapata kipato, bali pia huboresha barabara zetu kwa kuzikarabati na
kuzitengeneza.
Katika
mwaka wa fedha wa 2003/04 Wizara yangu imeendelea kuratibu
na kutoa miongozo ya matumizi ya teknolojia hii, kufuatilia utendaji na
kutathmini ubora wa kazi katika miradi ya barabara. Aidha, Wizara imeendelea
kukiwezesha Chuo chake cha “ Appropriate Technology
Trainining Institute”(ATTI) - Mbeya kutoa mafunzo ya teknolojia sahihi ya nguvu
kazi kwa kazi za barabara kwa mafundi wasimamizi wa kazi za barabara wapatao 85
kutoka Halmashauri za Wilaya mbalimbali nchini.
Katika kutoa umuhimu wa matumizi ya
teknolojia hii, Wizara yangu kwa kushirikiana na TAMISEMI, imeandaa na
kukamilisha Mwongozo wa Kitaifa wa kuratibu shughuli zote zinazohusiana na
matumizi ya teknolojia ya nguvu kazi. Utekelezaji wa
Mpango huu utaanza mwaka wa fedha wa 2004/05. Aidha, Wizara yangu kwa kushirikiana na Shirika la kazi Duniani (ILO) iliandaa
na kuwa mwenyeji wa semina ya kimataifa ya wadau wa nguvu kazi (Labour Based
Practitioners) ambayo iliwashirikisha washiriki 210 kutoka nchi mbalimbali 24
duniani. Semina hii ilifanyika Arusha
mnamo Mwezi Oktoba 2003 na ilitoa changamoto kubwa
katika kuboresha na kudumisha matumizi ya nguvu kazi katika kazi za barabara.
29. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha wa 2004/05,
Wizara yangu itatekeleza Mpango wa Kitaifa wa matumizi ya nguvukazi katika
matengenezo ya barabara ambao utaratibu shughuli zote za matumizi ya teknolojia
ya nguvu kazi katika kazi za barabara nchini kwa kuzingatia ushirikishwaji wa
sekta binafsi. Vilevile, Wizara itakiendeleza na
kukipatia nyenzo, miundo mbinu na vitendea kazi Chuo cha ATTI-Mbeya ili kiweze
kujitegemea na kufanya kazi kwa ufanisi zaidi. Aidha, Wizara itaimarisha
maktaba (Labour Based Documentation Centre) ambapo nyaraka mbalimbali za
shughuli za teknolojia ya nguvu kazi na rejea
mbalimbali zinazohusiana nayo zinahifadhiwa. Wizara itashiriki na kuratibu shughuli za utafiti kwa lengo la kutathimini
ubora wa kazi za barabara zinazojengwa na kutunzwa kwa kutumia teknolojia hii.
USHIRIKISHWAJI WA WANAWAKE KATIKA KAZI ZA
BARABARA NCHINI
30. Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu kwa kipindi cha 2003/04
imeendelea kuhamasisha na kuelimisha wanawake na jamii kwa ujumla ili wanawake
waweze kushiriki kwa wingi zaidi katika kazi za barabara. Ushirikishwaji huu unatofautiana mkoa kwa mkoa kulingana na mila na desturi, jitihada za wataalam
walioko kwenye mikoa za kuhamasisha na kushirikisha na uelewa wa jamii husika.
Wizara yangu imeendelea kuchapisha na kusambaza
kwa wadau makala mbalimbali
IDARA YA UGAVI NA HUDUMA
32. Mheshimiwa Spika, Idara ya
Ugavi na Huduma ina majukumu ya kusimamia Ununuzi,
Utunzaji Usambazaji wa vifaa na upatikanaji wa huduma mbalimbali kwa ajili ya
shughuli za Serikali (Procurement and
Supply Management). Aidha Idara ya Ugavi na
Huduma inasimamia Taratibu za Ugomboaji na usafirishaji wa shehena za Serikali
(Clearing and Forwarding Agent) pamoja na shughuli za uendeshaji wa Bohari Kuu
ya Serikali.
Takwimu
kutoka vyanzo mbali mbali zinaonyesha kwamba kati ya asilimia 60 hadi 70 ya
matumizi ya Serikali hutumika katika ununuzi wa vifaa,
kazi na huduma (Goods, Works and Services). Serikali pia
hutumia fedha nyingi katika kugomboa shehena zake kutoka nje ya nchi
zinazoletwa kupitia bandari, viwanja vya ndege na
mipakani.
Malengo ya mwaka 2003/2004 na
utekelezaji wake.
33. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2003/2004
Idara ilipanga kutekeleza yafuatayo:-
·
Kuongeza utoaji na usambazaji
wa vifaa na huduma kwa Wizara, Idara, Taasisi za Serikali na Bohari za Mikoa
kufikia Shilingi bilioni 18.
·
Kuimarisha uwezo wa
kiutendaji wa Maafisa Ugavi katika shughuli za ununuzi na utunzaji wa vifaa vya
Serikali kwa kuwapa mafunzo ya muda mrefu na mfupi.
·
Kuongeza usimamizi wa ukaguzi
wa vifaa na huduma kwa mikoa yote kwa kutembelea na kukagua vituo hivyo.
Utekelezaji
wa malengo haya ni
·
Hadi Mei 2004 bidhaa zenye thamani ya Shilingi bilioni
13.568 zimeuzwa kwa wateja,
·
Wafanyakazi 28 walipelekwa kusoma Shahada ya juu ya
Biashara inayohusu masuala ya Manunuzi. Aidha, wafanyakazi 37 walipelekwa
kusomea kozi mbalimbali hapa nchini.
·
Ukaguzi umefanyika Bohari 10
za Mikoa ya Tanga, Arusha, Moshi, Kigoma, Singida, Kagera, Mara,
Shinyanga,
·
Bohari za Mikoa ya Mara, Kigoma, Morogoro na Singida zimekarabatiwa.
34.
Mheshimiwa
Spika, malengo ya mwaka 2004/05 ni:
·
Kuongeza vitendea kazi
·
Kuhakikisha kwamba taratibu zinaendelea kufanyika ili kukamilisha uanzishaji wa Wakala wa Bohari Kuu ya
Serikali ifikapo Juni, 2006.
·
Kuandaa orodha ya viwango vya vifaa ambavyo vinatumika
Serikalini kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali.
·
Kutoa mafunzo kwa Watumishi
wa Ugavi Serikalini kuhusu sheria, kanuni na taratibu
·
Kuhakikisha kwamba Watumishi wa
Ugavi Serikalini wanaendelea kupewa mafunzo ya muda mrefu na mfupi katika
taaluma
·
Kuimarisha shughuli za Kitengo cha Wakala wa Ugomboaji na Usafirishaji wa Shehena za Serikali kwa
kukiongezea vitendea kazi ili kiweze kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi na
kwa gharama nafuu.
·
Kuongeza vitendea kazi ikiwa ni
pamoja na kununua magari ya kusambaza vifaa mikoani.
IDARA YA UFUNDI
NA UMEME
Utekelezaji wa
mwaka 2003/04
35. Mheshimiwa Spika, Idara ya Ufundi na Umeme kwa kutumia
vitengo vyake mbalimbali imeweza kutekeleza majukumu yake ya kuratibu,
kutathmini, kusajili, kufuta, kukodisha na kufanya matengenezo ya magari na
mitambo ya Serikali, uendeshaji wa Vivuko na Mitambo ya kusaga mawe, ushauri,
usimamizi wa miradi, usimikaji na matengenezo ya mitambo ya umeme, mabarafu,
viyoyozi na vifaa vya Electoniki. Aidha, Idara imeendelea na
zoezi la kusajili magari, mitambo na pikipiki za Serikali kwa kwa namba za
Serikali
Katika
kuboresha huduma kwa Wananchi, Wizara yangu katika mwaka 2003/04 imenunua kivuko
kimoja cha Bugolora-Ukerewe mkoani Mwanza kwa Shilingi 1,000,000,000
kitakachofanya kazi kati ya Mwanza na Ukerewe, na hivyo kupunguza kero kubwa
iliyokuwa inawakabili wananchi wa maeneo hayo.
Pia,
mkataba wa ununuzi wa Boti mbili (2) za uokoaji umesainiwa na boti hizo
zinategemewa kupatikana mwishoni mwa mwezi Agosti, 2004 na zitatumika katika
kivuko cha Magogoni
Magari 5
yamenunuliwa kwa ajili ya kuimarisha karakana katika Mikoa ya
Pia, Idara imeendelea
kutoa ushauri kuhusu utekelezaji wa miradi ya umeme.
Miradi 17 kati ya 58 imekamilika na iliyobaki 41
inaendelea. Jumla ya Shilingi 110,000,000 zimepatikana.
36. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa
fedha wa 2004/05, malengo yafuatayo yamepangwa:
·
Kununua
kivuko kipya cha Kigongo - Busisi mkoani Mwanza,
·
Kununua
kivuko kilichokuwa kinamilikiwa na TAMOFA katika mto
·
Kununua
“Vending Machine” ya kukatia tiketi katika Kivuko cha Magogoni kwa lengo la kuongeza ufanisi na kuimarisha ukusanyaji wa
mapato.
·
Kukarabati
vivuko vya Mv. Kigamboni, Mv. Rufiji, Mv. Sengerema, Mv. Pangani, Mv. Kilombero
na kile cha Kyanyabasa kilichopo Mkoani Kagera.
·
Kubadilisha
mfumo wa uendeshaji kutoka uvutaji wa kamba unaofanywa
na watu na badala yake kutumia winchi katika kivuko cha mto Ruhuhu Mkoa wa
·
Kununua
Boti 2 za uokoaji, magari 3 (4WD) na Vifaa vya karakana
(Workshop tools).
37. Mheshimiwa Spika, taratibu za kuifanya Idara ya Ufundi na Umeme kuwa Wakala utakaojulikana kama “Tanzania
Electrical, Mechanical and Electronics Services Agency” (TEMESA), zinaendelea
na utekelezaji wake umefikia asilimia 60. Inatarajiwa kuwa,
Wakala utaanza kufanya kazi rasmi mwezi Januari 2005.
BODI YA MFUKO WA BARABARA (RFB)
38. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2003/2004
Bodi ya Mfuko wa Barabara imezidi kujiimarisha kwa kuongeza ufanisi katika
ukusanyaji na usimamizi wa fedha za Mfuko wa Barabara. Napenda kuliarifu Bunge
lako Tukufu kwamba katika mwaka wa fedha 2003/2004
Bodi ilitarajia kukusanya shilingi milioni 64,510 kwa ajili ya kazi za
barabara. Hadi Mei 2004, shilingi milioni 61,616 (96%) ya
lengo, zilikuwa zimekusanywa.
Kati ya kiasi hicho Bodi ilipokea na kugawa
jumla ya shilingi milioni 57,675
Aidha, Bodi
imeshiriki katika semina mbalimbali zinazoendeshwa na
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (CRB) na TAMISEMI kwa Watendaji wa Halmashauri
na Makandarasi ili kutumia nafasi hiyo katika kuwaelimisha washiriki umuhimu wa
matumizi bora ya fedha za Mfuko. Bodi ya
Mfuko itaendeleza juhudi hizi katika mwaka ujao wa
fedha.
Vilevile,
Bodi kwa kutumia ofisi ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa
Serikali, imeendelea kufanya ukaguzi wa kawaida pamoja na ukaguzi maalum wa
kuhakiki mapato yake kutoka kwa wakala wa ukusanyaji.
Katika
juhudi za kuongeza mapato ya Mfuko, Bodi imeandaa mapendekezo ya kuongeza
vyanzo vya mapato ambayo yanafanyiwa kazi na Serikali.
Bodi imeweza pia kutoa mafunzo ya usimamizi wa Mfuko
kwa watumishi na wajumbe wa Bodi. Pia
Bodi imechapisha Kijarida kinachotoa mwongozo juu ya matumizi ya fedha za Mfuko
ambacho kimegawiwa kwa wadau mbalimbali.
39. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2004/2005
Serikali inategemea kukusanya jumla ya shilingi 71,443 milioni kwa ajili ya
Mfuko wa Barabara. Kati ya fedha hizi shilingi 50.01 milioni (70%) zitapelekwa Wizara
ya Ujenzi na shilingi 21.433 milioni (30%) zitapelekwa
TAMISEMI.
Aidha mfuko
unatarajia kupata kiasi cha shilingi 8,000 milioni kutoka Jumuia ya Ulaya ikiwa
ni msaada kwa ajili ya matengenezo ya barabara katika
mwaka wa fedha wa 2004/2005. Katika fedha hizi, Wizara ya Ujenzi itapata
Shilingi bilioni 5.6 na TAMISEMI Shilingi bilioni
2.4.
40. Mheshimiwa
Spika, katika kipindi cha 2004/05, Bodi ya Mfuko wa Barabara
inategemea kuendelea kuboresha makubaliano ya utendaji (Performance Agreements)
na taasisi zinazotekeleza kazi za barabara na kutoa ushauri wa kuboresha
utendaji kwa kuzingatia uzoefu wa nchi nyingine ili kuhakikisha kwamba ubora wa
kazi unalingana na fedha zinazotolewa. Aidha, Bodi kwa
kushirikiana na Wizara ya Fedha, itaendelea kuimarisha ufanisi katika
ukusanyaji wa mapato ya Mfuko kutoka vyanzo mbalimbali na kusimamia vizuri
matumizi ya fedha hizo kwa kuimarisha ukaguzi wa ubora wa kazi na Fedha.
Katika
kufanikisha malengo na majukumu yake, Bodi itaandaa
Mpango wa muda mrefu (Strategic Plan) uwe dira ya kuiongoza na katika kuongeza
ufanisi wa utunzaji wa kumbukumbu za fedha na itaanza kutumia mfumo mpya wa
kompyuta wa kudhibiti matumizi ya fedha (Computerized Financial Management
System).
WAKALA WA
BARABARA (TANROADS)
41. Mheshimiwa Spika,
Wakala wa Barabara una miaka minne tangu
ulipoanzishwa. Katika kipindi hicho, umeendelea kutekeleza vizuri majukumu yake
ya ujenzi, ukarabati na matengenezo ya Barabara Kuu na
za Mikoa zenye jumla ya kilometa 35,000. Aidha muundo wa
TANROADS umepitishwa rasmi na ofisi za kanda sasa zimeondolewa Mikoani na
zimehamishiwa Makao Makuu ya Wakala. Katika kipindi hiki cha miaka minne Wakala
umefanikiwa kuweka mifumo ya kisasa ya menejimenti na
mawasiliano Makao Makuu na Ofisi zote za mikoa.
42. Mheshimiwa Spika,
kutokana na kuimarika kwa Wakala na ukweli kwamba
fedha za matengenezo zimekuwa zinapatikana kwa wakati na kwa kiasi
kilichopangwa, Wakala
umejitahidi kuongeza ufanisi na kuongeza uzuri wa hali ya barabara zetu.
43. Mheshimiwa Spika, Wizara
yangu kupitia TANROADS itaendelea kutunza barabara zetu kwa
kusisitiza pamoja na mambo mengine masuala yafuatayo:
·
Samani za barabara
Wenye magari wanatakiwa kuwa
waangalifu ili wasizigonge alama za barabarani. Baadhi
ya wananchi wamekuwa waking’oa alama na samani
nyingine za barabara. Ukosefu wa alama na samani
unachangia kuwepo kwa ajali. Wananchi wanaombwa kulinda na
kutunza alama za barabarani.
·
Usalama barabarani
Mwendo wa
kasi ni kichocheo kikubwa cha ajali. Madereva na wenye
magari wanatahadharishwa kuhusu jambo hili. Pamoja na
kuhakikisha kunakuwepo na alama za tahadhari barabarani, ukaguzi wa mwendo wa
magari na ubora wa magari vitafanyika mara kwa mara.
·
Uzito wa magari
Shughuli ya upimaji wa uzito wa magari itaendelea kuboreshwa ili kuhakikisha
magari yanazingatia sheria na taratibu zilizowekwa.
·
Hifadhi ya barabara (Road Reserve)
Wananchi wanaojenga au
wanaofanyia shughuli zao kando ya barabara katika eneo la mita 22.5 kila upande
wa Barabara Kuu na zile za Mikoa, wanatakiwa
kuzingatia sheria ya barabara inayowataka kuheshimu eneo
·
Waheshimiwa Wabunge, Viongozi wa
Mikoa na Wilaya wanaombwa kutoa ushirikiano kwa Wizara/Wakala kwa kutoa ushauri
na kujadili kwa makini taarifa za matengenezo na matumizi ya fedha wakati wa
vikao vya Bodi za Barabara.
Aidha, ni
vema ieleweke kwamba kazi nyingi za matengenezo zinafanywa na makandarasi
wazalendo hivyo zinachangia kutoa ajira kwa wananchi walio wengi na hivyo
kuboresha hali zao za maisha.
WAKALA WA MAJENGO YA SERIKALI (TBA)
44. Mheshimiwa
Spika, Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA)
umeanzishwa chini ya Sheria Na 30 ya mwaka 1997 ya Wakala wa Serikali na
kuzinduliwa rasmi mwezi Mei, 2002. Madhumuni ya kuanzishwa Wakala huu ni pamoja na kuweka utaratibu na kanuni zitakazowawezesha
wafanyakazi wa Serikali kumudu kugharamia makazi bora wakiwa bado kazini na
baada ya kustaafu.
Kwa kuzingatia hayo, majukumu ya
Wakala ni
·
Kujenga
majengo ya Serikali kwa viwango vinavyotakiwa na
kuyatunza.
·
Kutoa
ushauri wa kitaalam na kusimamia miradi ya ujenzi wa
nyumba na majengo ya Serikali.
·
Kuuza
nyumba za serikali kwa kuwakopesha wafanyakazi wa ngazi zote ili waweze
kuzimiliki kabla ya kustaafu
·
Kuendelea
kujenga nyumba mpya na kuwauzia wafanyakazi.
Mapitio ya Utekelezaji wa 2003/04
45. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka
2003/04, Wakala ulipanga kufanya kazi zifuatazo:
·
Kuzifanyia
matengenezo nyumba za Serikali 262 katika mikoa yote ya Tanzania Bara.
·
Kuuza
pamoja na kujenga nyumba 500 za gharama nafuu.
·
Kufanya
kazi za ushauri zitakazoingiza kiasi cha Shilingi 372,086,700
Hadi Aprili, 2004,
jumla ya nyumba 177 zimefanyiwa matengenezo katika mikoa mbalimbali. Aidha, Wakala umeanza ujenzi wa nyumba 300 kwa ajili ya viongozi wa Serikali katika
Manispaa ya
Malengo ya mwaka 2004/05
46. Mheshimiwa
Spika, katika
mwaka 2004/05 Wakala umepanga kukusanya jumla ya shilingi 9,284,134,361
kutokana na mauzo ya nyumba kwa watumishi wa Serikali,
upangishaji wa nyumba za kibiashara, huduma za ushauri na ruzuku kutoka
Serikalini kwa ajili ya kulipia mishahara ya watumishi. Mapato haya
yataelekezwa kwanza katika kukamilisha nyumba 300, ambazo ujenzi wake
unaendelea pamoja na kujenga nyumba nyingine. Aidha,
Wakala utaendelea na matengenezo ya kawaida ya nyumba
za Serikali.
BODI YA
USAJILI WA MAKANDARASI (CRB)
47. Mheshimiwa Spika,
Bodi ya Usajili wa Makandarasi (Contractors
Registration Board) ilianzishwa kwa sheria ya Bunge Namba 17 ya mwaka 1997, na
kupewa majukumu yafuatayo:
(i)
Kusajili makandarasi
wa aina zote
(ii)
Kuratibu
shughuli na mwenendo wa makandarasi wote, na
(iii)
Kujenga
uwezo wa makandarasi wa Kitanzania.
Bodi imetayarisha Dira ya Miaka
Mitano ya 2004-08 kwa mashauriano na wadau wa sekta ya
ujenzi. Dira hii inalenga katika maeneo makuu sita ambayo ni:
·
Kuboresha
uwezo, ujuzi na maadili ya Makandarasi
·
Kuhakikisha
kwamba makandarasi wa kizalendo wanatumika ndani na
nje ya nchi.
·
Kuongeza
ubora wa kazi za ujenzi
·
Kuhakikisha
kwamba afya na usalama kazini unazingatiwa
·
Kuongeza
ufanisi wa shughuli za Bodi
48. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa
2003/04, Bodi imepata mafanikio yafuatayo:
(i)
Kusajili
jumla ya makandarasi 968. Hii inafanya jumla ya makandarasi waliosajiliwa hadi
Mei, 2004 kuwa 3,094.
(ii)
Bodi
imefuta usajili wa makandarasi 135 mwezi Januari 2004
kwa kushindwa kutimiza masharti ya Sheria ya Usajili wa Makandarasi Na. 17 ya
1997 ikiwa ni pamoja na utendaji mbaya wa kazi. Hii imefanya jumla ya
makandarasi waliofutwa tangu mwaka 1999 kufikia 1,448.
(iii)
Bodi
imefanya ukaguzi wa miradi ya ujenzi 946 katika
kipindi cha 1999 – Mei 2004. Kati ya hiyo, miradi 414 ilikuwa na mapungufu mbali mbali ya uvunjaji wa sheria ambapo
wahusika walichukuliwa hatua za kisheria. Hadi Mei, 2004 jumla ya kesi 25 zipo
Polisi na kati ya hizo kesi 15 ziko mahakamani.
(iv)
Hadi
Mei, 2004, Bodi imeshaendesha kozi 12 chini ya Mpango Endelevu wa Mafunzo ya Makandarasi (Sustainable Structured Training
Program) ambapo Makandarasi 300 walihudhuria. Tangu Mpango huu uzinduliwe mwaka
2001, jumla ya kozi 29 zimeshaendeshwa na kuhudhuriwa
na makandarasi 900.
(v)
Mfuko
wa kusaidia Makandarasi (Contractors Assistance Fund)
umeboreshwa kwa kuongeza fedha na sasa Mfuko huo una zaidi ya Shilingi milioni
600. Aidha, wanachama wa mfuko huo maalum wa kusaidia
makandarasi kupata dhamana za malipo ya awali (Advance Payment Guarantee) na
dhamana za zabuni (Bid Bond), waliongezeka hadi kufikia 251. Hadi Mei, 2004
jumla ya wanachama 198 wa Mfuko huo walikuwa
wamefaidika. Mfuko unalenga kuwasaidia makandarasi wadogowadogo wazalendo.
(vi)
Bodi
ilifanya marekebisho ya sheria yake ndogo ili
kuboresha mazingira katika sekta hii, na kutoa uwezo zaidi wa kuendeleza
makandarasi wazalendo. Mabadiliko haya yanahusu: -
§
Kuongeza
thamani ya viwango vya juu vya kazi katika kila daraja la Ukandarasi kwa kuzingatia thamani ya fedha za
§
Kuweka
sifa za chini (minimum qualifications) za nafasi ya Mkurugenzi Mmiliki wa kampuni ya Ukandarasi ili kuhakikisha kwamba biashara ya
ukandarasi inafanywa na wenye fani zinazotakiwa.
§
49. Mheshimiwa
Spika, matatizo
makubwa yanayowakabili makandarasi nchini ni pamoja na :
-
·
Mitaji
midogo na masharti magumu ya kupata mikopo ya kufanyia
kazi kutoka mabenki na taasisi zingine za fedha.
·
Udhaifu
wa uendeshaji na usimamizi wa miradi miongoni mwa
makandarasi.
·
Ukosefu
wa vifaa na mitambo ya ujenzi kwa makandarasi wenyewe, hii ni pamoja na
kutokuwa na uwezo wa kuimiliki, bei kubwa za kukodisha mitambo na uchache wa
sehemu za kuikodisha.
50. Mheshimiwa
Spika, malengo ya mwaka 2004/05 ni pamoja
na haya yafuatayo:
·
Kuendelea na zoezi la kusajili makandarasi wa ngazi
zote
·
Kuendelea kusimamia Mfuko wa Kusaidia Makandarasi
nchini
·
Kutoa
mafunzo chini ya Mpango Endelevu wa Mafunzo ya Makandarasi (Sustainable
Structured Training Program)
·
Kufanya
ukaguzi wa miradi ya ujenzi katika sehemu mbali mbali
·
Kuendelea
na zoezi la usimamizi wa Sheria ya usajili wa makandarasi
BODI YA TAIFA YA USIMAMIZI WA VIFAA (NBMM)
51. Mheshimiwa Spika, Bodi ya Taifa
ya Usimamizi wa Vifaa (National Board for Materials
Management – NBMM) ni Taasisi ya Serikali iliyoanzishwa mwaka 1981 kwa Sheria
ya Bunge Na. 9. Bodi ina
majukumu ya kusimamia, kuratibu na kuendeleza fani ya Ununuzi na Ugavi. Bodi
pia huendesha mitihani, kudhibiti mienendo ya wanataaluma na
kusajili wataalamu.
Katika mwaka wa fedha wa 2003/04
Bodi imetekeleza yafuatayo:
·
Imesajili wataalamu 112 hivyo kufanya idadi ya
wataalamu waliosajiliwa kufikia 1,609.
·
Imetahini Wanataaluma 1,967 kwenye ngazi mbalimbali
·
Bodi imeweza kutembelea na
kukagua sehemu za kazi mkoani
·
Mafunzo endelevu (Continued Professional Development)
yameendelea kutolewa ambapo warsha na semina 24 ziliendeshwa kwa watendaji wa
ngazi zote za Serikali Kuu, Wilaya, Miji, Manispaa n.k. Mafunzo haya, yalihusu
pia sheria ya Manunuzi ya Umma.
·
Utaratibu wa kutoa mafunzo
kwa vitendo (Internship) yameanzishwa kwa wanataaluma wanaotoka vyuoni ili
wapate uzoefu katika kazi.
·
Bodi ikishirikiana na Crown
Agents –
·
Mafunzo mengine yaliyotolewa ni
pamoja na namna ya kupambana na janga la UKIMWI, kuondoa kero za rushwa na
kudumisha maadili ya kazi.
·
Katika kuboresha mfumo wa
mafunzo, Bodi imebadili mitaala ili ikidhi mabadiliko yanayoletwa na ukuaji wa
utaalamu ulimwenguni, teknolojia na sheria za ununuzi.
·
Bodi imetoa ushauri wa
kitaalamu kwenye Serikali na Asasi zake, pia imeandaa miongozo ya kazi
(operations manuals), mfumo wa kazi na utunzaji wa kumbukumbu kwenye shughuli
za ununuzi na ugavi.
52. Mheshimiwa Spika, Baadhi ya
matatizo ambayo Bodi inakumbana nayo katika utekelezaji ni
pamoja na:
·
Upungufu wa vitendea kazi,
nyenzo muhimu za kufanyia kazi na usafiri.
·
Uhaba wa fedha za kutoa elimu
kwa vitendo.
·
Waajiri wengi kushindwa kuajiri wanataaluma wanaotoka
vyuoni moja kwa moja kwa kuwa hawana uzoefu kazini
kutokana na ama kutojua sheria ama kuidharau na kufanya utekelezaji kuwa mgumu
hasa kuhusu suala la kuajiri wataalamu wasio na sifa.
53. Mheshimiwa Spika, malengo
ya Bodi kwa mwaka wa fedha 2004/2005 ni pamoja na:
·
Kuendelea kutekeleza majukumu yake kwa
mujibu wa Sheria Na. 9 ya 1981.
·
Kuongeza idadi na kiwango cha wanaofaulu mitihani toka
wastani wa asilimia 39.5 ya sasa hadi kufikia asilimia 50,
·
Kuboresha uwezo wa maktaba na
kupata wakufunzi wenye upeo mkubwa zaidi na kuboresha mafunzo kwa wakufunzi.
·
Kufungua vituo vya kutahini katika mikoa ambayo huduma
za Bodi hazijafika.
·
Kuimarisha usimamizi wa
sheria Na.9 ili waajiri wengi waweze kuitii sheria na kupata fursa ya kutumia
wataalamu waliopo ipasavyo.
·
Bodi itatoa huduma zaidi kwa
njia ya warsha, semina na ushauri wa kitaalamu
·
Bodi itaendelea kushirikiana na
taasisi nyingine zikiwemo Bodi za kitaaluma na vyuo mbalimbali ili kuweza
kupata ufumbuzi wa matizo yanayoathiri ukuaji wa taaluma. Kwa kushirikiana na vyombo husika, itakamilisha muswada wa marekebisho ya
Sheria Na.9 na kuuwakilisha Bungeni.
·
Katika kuleta ufanisi zaidi na
kukuza uwezo wao kitaaluma, Bodi itaendelea kuwapatia wafanyakazi mafunzo ya
muda mrefu na mfupi.
BODI YA USAJILI WA WAHANDISI (ERB)
54. Mheshimiwa
Spika, Bodi ya usajili ya wahandisi ilianzishwa na Serikali kwa sheria Na. 15 ya mwaka 1997 na imepewa
madaraka ya kusimamia mienendo na shughuli za kihandisi zinazofanywa na
wahandisi pamoja na kampuni za ushauri wa kihandisi.
Jukumu kubwa la bodi ni kulinda masilahi ya taifa na
watumiaji wa huduma za kihandisi kwa kuhakikisha kuwa shughuli zote za
kihandisi zinafanywa na wahandisi waliosajiliwa au na makampuni ya ushauri wa
kihandisi yaliyosajiliwa kwa kuzingatia viwango na maadili ya kihandisi ili
kuhakikisha usalama wa maisha, mali na mazingira. Katika kutekeleza jukumu
hili, bodi inafanya yafuatayo:
·
Kusajili wahandisi pamoja na
makampuni yanayotoa ushauri wa kihandisi,
·
Kupitia na kutoa maamuzi juu ya
maombi ya kusajiliwa,
·
Kuwaendeleza wahandisi kitaaluma,
ikiwa pamoja na kusimamia programu ya mafunzo kwa wahandisi wahitimu
(internship),
·
Kuratibu mienendo na shughuli za
kihandisi za wahandisi na makampuni ya ushauri wa kihandisi,
·
Kujenga uwezo (capacity building)
wa wahandisi na makampuni ya ushauri wa kihandisi, na
·
Kuandaa machapisho mbalimbali
yanayohusu shughuli za Bodi.
Mafanikio
na Matatizo katika mwaka wa fedha 2003/04.
55. Mheshimiwa
Spika, hadi kufikia mwezi Mei, 2004 Bodi imefanikiwa kutekeleza
yafuatayo:
·
Kusajili Wahandisi – 909 ikiwa ni
asilimia 152 ya lengo la mwaka
·
Kusajili Kampuni za Ushauri – 9,
ikiwa ni asilimia 81.8 ya lengo la mwaka.
·
Ziara za kanda – 4 zimefanyika
ikiwa ni asilimia 57.1 ya lengo la mwaka.
·
Kuendesha mihadhara 4 ikiwa ni
asilimia 66.7 ya lengo la mwaka,
·
Kuendesha kozi fupifupi – 4 ikiwa
ni asilimia 200 ya lengo la mwaka.
·
Kuandaa na
kuendesha mtihani wa kitaaluma –1 ikiwa ni asilimia 50 ya lengo la mwaka.
·
Kuendesha na
kusimamia mafunzo kwa vitendo kwa wahandisi - 250 ikiwa ni asilimia 48 ya lengo
la mwaka.
·
Kuratibu Siku ya Wahandisi – 1
ikiwa ni asilimia 100 ya lengo la mwaka.
56. Mheshimiwa
Spika, pamoja na mafanikio haya,
Bodi ilikabiliwa na changamoto zifuatazo:
·
Ufinyu wa
Bajeti: Shughuli za Bodi zimepanuka hivyo
ada
·
Ukosefu wa
ajira kwa wahandisi wahitimu. Wahandisi wahitimu wazalendo hukosa ajira kwa kutokuwa na uzoefu wa kufanya kazi na hivyo kusababisha
waajiri kuajiri wahandisi wa kigeni.
Hata hivyo, tatizo hili linatazamiwa kupungua baada ya kuanzishwa kwa utaratibu wa mafunzo ya vitendo kwa wahandisi wahitimu.
·
Idadi ndogo ya kampuni za Ushauri
wa kihandisi mikoani.
Ni azma ya Bodi kuendelea kuyatafutia ufumbuzi
matatizo haya ili kuimarisha ufanisi katika
utekelezaji wa majukumu yake.
Malengo
ya Mwaka wa Fedha wa 2004/2005
57. Mheshimiwa
Spika, Malengo ya mwaka wa fedha
2004/05 ni kutekeleza kazi zifuatazo:
·
Usajili wa Wahandisi - 1,030
·
Usajili wa Kampuni za Ushauri wa
Kihandisi - 15
·
Kufanya ukaguzi mikoani kwa kutembelea kanda 5 zenye mikoa 16.
·
Kuandaa mihadhara ya kitaalamu
·
Mafunzo ya vitendo kwa Wahandisi
wahitimu na kozi fupi
·
Kuratibu Siku ya Wahandisi
·
Mtihani wa Kitaaluma
·
Kushughulikia uanzishwaji wa Kampuni za Ushauri wa
Kihandisi mikoani ili kusogeza huduma hii karibu na watumiaji
·
Kukamilisha maandalizi ya programu ya mafunzo ya
kujiendeleza kwa wahandisi.
58. Mheshimiwa
Spika, nafurahi kulijulisha Bunge lako Tukufu kuwa Bodi imeanzisha
utaratibu wa kusherehekea – Annual Engineers’
Day. Siku hii maalum ina lengo la kuwatambua
wahandisi na makampuni ya kihandisi yaliyotoa michango mikubwa katika maendeleo
ya kijamii na kiuchumi nchini na kuwahamasisha Wahandisi kuwa wabunifu na hivyo
kuharakisha maendeleo ya taifa. Sherehe kama hizi zitakuwa zinafanyika kila mwaka.
BODI YA
WABUNIFU MAJENGO NA WAKADIRIAJI MAJENZI (AQSRB)
59. Mheshimiwa
Spika, Bodi ya
Usajili wa Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi ilianzishwa
kwa Sheria Na. 16 ya mwaka 1997. Majukumu makubwa ya Bodi ni
pamoja na: -
·
Kusajili,
kusimamia, kuangalia na kuratibu mwenendo wa Wabunifu
Majengo na Wakadiriaji Majenzi na kampuni za kitaalamu na za ushauri
zinazohusiana na kuhusika na fani hizo. Lengo la Bodi ni
kuhakikisha kuwa wataalam hawa, wanatoa huduma za kitaalamu zinazokidhi
mahitaji ya wananchi na mazingira
·
Kulinda
utaalamu (Professionalism).
·
Kuhamasisha
umma na wataalamu, kushirikiana na wadau wengine
Katika mwaka wa
fedha 2003 /2004, Bodi ilifanikisha kutekeleza yafuatayo:
·
Kusajili
Wabunifu na Wakadiriaji Majenzi wa ndani 22 na wa nje
5. Aidha, Bodi ilisajili kampuni za ndani 9 na za nje
2 na kufikisha jumla ya wataalam wa ndani na nje waliosajiliwa tangu Bodi ianze
kuwa 293 na kampuni za ndani na za nje kuwa 123.
·
Kutembelea
na kukagua sehemu za majenzi katika mikoa 12 ya
·
Kukamilisha
Mapendekezo ya Marekebisho ya Sheria Na. 16 ya mwaka 1997
·
Kuandaa
na kuendesha makongamano mawili ya taaluma hizi mbili
katika kuwanoa wana taaluma chini ya Mpango wa Taaluma ya Elimu Endelevu
(Continued Professional Development).
·
Kutayarisha
na kutahini wana taaluma wanaoomba kusajiliwa na Bodi.
·
Katika
kuhakikisha Sheria Na. 16 ya 1997 na sheria ndogondogo
GN No.168/2000 za Bodi zinafuatwa, Bodi iliweza kutoa adhabu, maonyo na
kuwapeleka mahakamani wale walioonekana kukaidi sheria.
·
Kukamilisha
matayarisho ya Rasimu ya Sheria ya Taifa ya Majengo- (
·
Kuzindua
Mpango wa Mihadhara ya Kitaaluma yenye lengo la
kutambua michango ya wana taaluma wa Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi,
kuhamasisha kizazi kipya kujiunga na fani hizi mbili na kubadilishana uzoefu.
·
Kutayarisha
na kuwasilisha kwenye vyombo husika taarifa ya
utendaji ya mwaka 2002 kwa mujibu wa sheria Na. 16 ya 1997.
·
Kutayarisha
“Standard Documents” kwa ajili ya kurahisisha
usimamiaji wa Sheria Na. 16ya mwaka 1997 na Sheria ndogondogo namba 168 ya 2000
kwenye sehemu za majenzi.
·
Kuhusu
mitihani ya Bodi, maombi 76 ya wataalamu yalipokelewa. Wataalam 57 waliotimiza
masharti waliruhusiwa kufanya mitihani na kati ya hao
17 walifaulu na 11 walisajiliwa na Bodi. Aidha wataalam 4 na
kampuni 3 za Ubunifu Majengo na Ukadiriaji Majenzi zilifutiwa usajili kwa
kukiuka Sheria Na.16 ya 1997 na kufanya jumla ya wataalam waliofutiwa usajili
tangu Bodi ianze kuwa 272 na makampuni 8.
60. Mheshimiwa Spika, pamoja na mafanikio haya Bodi ilikabiliana na changamoto zifuatazo:
-
·
Upungufu
wa fedha uliathiri kwa kiwango kikubwa utekelezaji wa malengo yaliwekwa na Bodi
·
Kutojitokeza
kwa wana taaluma wa sifa za kati kutahiniwa kwa ajili
ya usajili kunashusha idadi ya watahiniwa na hivyo kuathiri mpango wa usajili.
·
Mapato
ni kidogo, hayakidhi mahitaji ya Bodi. Kwa hiyo Bodi inakabiliwa na
matatizo ya upatikanaji wa vitendea kazi, utekelezaji wa mipango mizuri, kutoa
elimu kwa umma n.k. Hii inatokana na kutokuwa na vyanzo vya kutosha vya mapato.
61. Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2004/2005, Bodi
inatarajia kutekeleza yafuatayo:
·
Kusajili
wataalam 50
·
Kuimarisha taratibu za usajili,
·
Kuimarisha sera na mfumo wa
sheria wa Bodi.
·
Kuendelea na ukaguzi wa sehemu za majenzi katika mikoa
yenye shughuli nyingi za ujenzi ikiwemo Dar es Salaam, Pwani, Morogoro, Dodoma,
Iringa, Mbeya, Mwanza, Shinyanga, Arusha, Kilimanjaro na Tanga.
·
Bodi inaandaa mafunzo maalum ya vitendo kwa ajili ya kuwasaidia wahitimu wa taaluma husika ili
waweze kutimiza masharti ya kuweza kusajiliwa kwa mujibu wa sheria.
·
Vilevile, Bodi itaendelea kupiga vita rushwa kwa kuwaelimisha wataalam wake kuhusu kufuata sheria na
imetayarisha “practice note” itakayowataka watekelezaji miradi yenye maslahi
kitaifa km. hospitali, shule, nyumba za wageni, hoteli, nyumba za kupangisha na
maofisi kuwatumia wataalam waliosajiliwa na wasimike mabango yanayoonyesha
hivyo.
62. Mheshimiwa
Spika, Baraza la Taifa la Ujenzi
limeanzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 20 ya mwaka 1979.
Majukumu makuu ya Baraza ni pamoja na:
·
Kusimamia na kuratibu
maendeleo ya sekta ya ujenzi nchini na kushauri kuhusu Sera, Mipango na
mikakati ya kukuza sekta,
·
Kutoa ushauri wa
kiufundi (“technical audit”),
·
Kutoa mafunzo kwa
washauri wazalendo
·
Ukusanyaji wa takwimu za
ujenzi na kufanya utafiti
·
Kuchapisha na kusambaza
habari kuhusu shughuli za sekta,
·
Utoaji wa miongozo ya kiufundi ikiwa ni pamoja na kanuni za zabuni.
63. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka 2003/2004 Baraza lilipanga kutekeleza
yafuatayo:
·
Kutoa msukumo katika utekelezaji wa Sera ya Ujenzi,
·
Kutoa mafunzo kwa makandarasi, wahandisi washauri,
watendaji wakuu hasa wa Serikali za Mitaa kuhusu masuala mbalimbali ya sekta
ikiwemo sheria ya Manunuzi ya Umma (Public Procurement Act No.3 of 2001),
usimamizi wa mikataba ya ujenzi,
·
Kuboresha upatikanaji wa takwimu za shughuli za
ujenzi,
·
Kutoa huduma za ushauri kuhusu ukaguzi wa miradi,
ujenzi wa barabara, ukadiriaji wa gharama za ujenzi,
·
Kutoa mafunzo ya utekelezaji wa
miradi ya miundo mbinu kwa njia ya ubia kati ya sekta ya umma na sekta binafsi
(Public Private Partnerships - PPPs) na usuluhishi wa migogoro.
·
Kufuatilia kukamilishwa kwa
uundwaji wa Mfuko wa Fedha wa Maendeleo ya Sekta ya Ujenzi (Construction
Industry Develoment Fund -CIDF).
64. Mheshimiwa
Spika, hadi kufikia mwezi Mei 2004 kazi zifuatazo zilitekelezwa:
·
Baraza lilikamilisha utayarishaji wa
Mikakati ya utekelezaji wa Sera ya Ujenzi na kuisambaza kwa wadau mbalimbali
ili kutolewa maoni.
·
Mfuko wa Fedha wa Maendeleo
ya Sekta ya Ujenzi (Construction Industry Develoment Fund -CIDF) una mtaji wa
Shilingi bilioni 5 na utatoa mitaji ya kufanyia kazi kwa wadau wa sekta ya
ujenzi kwa masharti nafuu kuliko benki.
Mitaji hii ni pamoja na dhamana, mikopo ya
kufanyia kazi (working capital) na mikopo ya kununulia vifaa na mitambo ya
ujenzi.
·
Kwa kushirikiana na “Tanzania
Investment Centre” na wadau wengine, Baraza limekuwa likishughulikia
upatikanaji wa mapendekezo ya kuboresha mazingira bora ya utekelezaji wa miradi
ya miundo mbinu ya kiuchumi kwa njia ya “(Public Private Partnerships -PPPs).”
·
Baraza pia limeandaa mapendekezo ya marekebisho ya
Sheria Na.20 iliyounda Baraza ambayo yanashughulikiwa na
Serikali ili iendane na Sera ya Taifa ya Ujenzi ya mwaka 2003.
65. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/2005,
Baraza litatoa msukumo wa utekelezaji wa Sera ya Ujenzi. Kipaumbele kitatolewa kwa malengo na mikakati inayolenga kuondoa matatizo makuu ya
sekta ya ujenzi ambayo ni uwezo mdogo, tija ndogo na ubora hafifu wa kazi. Aidha, Baraza litaendelea kusimamia Mfuko wa
CIDF, kutoa huduma za ushauri wa kiufundi kwa Wadau mbalimbali kuhusiana na
tathmini za zabuni, uteuzi wa Washauri, utayarishaji wa makabrasha ya Zabuni,
madai, usuluhishi wa migogoro, usimamizi wa miradi na uchapishaji wa majarida.
CHUO CHA UJENZI - MOROGORO
66. Mheshimiwa
Spika, Chuo cha Ujenzi - Morogoro kilianzishwa kwa lengo la kufundisha Mafundi Sanifu, Mchundo na Wahandisi
wa Wizara ya Ujenzi na Halmashauri za wilaya. Kwa sasa, chuo kinatoa pia
mafunzo kwa mafundi Sanifu na Stadi wa fani mbalimbali
wanaoshiriki kazi za ujenzi kwenye sekta za umma na binafsi. Katika mwaka wa
fedha 2003/04, Chuo kilipanga kufundisha mafundi Sanifu150 katika fani za
matengenezo ya barabara, majengo na ufundi, mafundi stadi 60 katika stadi
mbalimbali, madereva wapya 120 na kuendeleza madereva wa umma 90, kukarabati
majengo mawili na kununua samani na pia kununua gari 1 mini – bus.
Hadi kufikia Mei, 2004 Chuo kimefanikiwa kufundisha mafundi
Sanifu 124 wa fani mbalimbali, madereva wapya 142, kuendesha mafunzo ya mafundi
stadi mbalimbali 60 na kuendesha mafunzo kwa madereva wa umma – 26.
67. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, chuo
kimepanga kutoa mafunzo kwa mafundi Sanifu 75, madereva mahiri 30, wanafunzi wa
udereva wa awali 80 na mafundi stadi mbalimbali 60.
KITUO CHA USAMBAZAJI TEKNOLOJIA
68. Mheshimiwa
Spika, kituo hiki kilianzishwa mwaka 1997 kwa madhumuni ya kuimarisha/kuboresha sekta ya usafirishaji
kwa kutumia mbinu ya usambazaji wa teknolojia kwa wadau wa sekta nzima ya
usafirishaji.
Katika mwaka wa fedha wa 2003/04 kituo kilipanga kuimarisha
na kuboresha huduma ya maktaba ya kituo, kutekeleza kwa majaribio mradi wa TRAC
katika shule za sekondari za Azania, Jangwani na Mzizima jijini Dar Es Salaam,
kuandaa, kuchapisha na kusambaza kwa wadau makala na majarida kuhusu kituo,
kuanzisha tovuti ya kituo na takwimu mbalimbali. Aidha kituo kilipanga kuandaa
kozi 4 na warsha 2 kwa wadau, kuendelea kutangaza/kunadi kwa wadau huduma
zinazotolewa na kituo ili kuongeza matumizi ya huduma zinazotolewa, na
kushiriki katika mikutano ya kimataifa ya utafiti na usambazaji wa teknolojia
katika sekta ya barabara na usafirishaji kwa ujumla.
Hadi Mei, 2004 kituo kilisambaza kwa
wadau 668 makala na taarifa zinazoelezea teknolojia mbalimbali katika sekta ya
usafirishaji. Kwa kushirikiana na Wizara ya
Mawasiliano na Uchukuzi, Baraza la Taifa la Ujenzi, Taasisi ya Barabara ya
Marekani (US FHWA) na Tanzania Global Development Learning Centre, kituo
kimeendesha warsha ya “Public-Private Partnerships in Transport Sector:
Reforms, Development and Management”. Kituo,
kimeshiriki katika makongamano 3 ya kimataifa na
kongamano, mikutano na semina 12 nchini ili kujifunza, kubadilishana uzoefu na
kubaini teknolojia zinazofaa kutumika hapa nchini. Wadau 141 walitumia huduma
ya Maktaba ya kituo na kwa kushirikiana na taasisi
nyingine 20 za wadau mbalimbali wa sekta ya ujenzi hapa nchini, kimeendelea
kuratibu uandaaji wa mradi unaolenga kujenga uwezo wa sekta nzima ya ujenzi
hapa nchini. Ripoti yenye mapendekezo ya mradi huo imekamilika na inafanyiwa kazi.
69. Mheshimiwa Spika, Malengo ya Kituo kwa mwaka 2004/05 ni
·
Kuandaa, kuchapisha na kusambaza kwa wadau makala na
majarida kuhusu kituo,
·
Kuandaa na kuendesha kozi na warsha kwa wadau,
·
Kuendelea kutangaza/kunadi kwa wadau huduma
zinazotolewa na kituo ili kuongeza matumizi ya huduma zinazotolewa,
·
Kushiriki katika mikutano ya kimataifa ya utafiti na usambazaji wa teknolojia katika sekta ya barabara na
usafirishaji.
MAENDELEO
YA WATUMISHI
70. Mheshimiwa
Spika, Katika mwaka wa fedha 2003/2004 watumishi wapya 38
waliajiriwa, 1,412 wa kada mbali mbali walipandishwa vyeo na 138
walithibitishwa kazini. Aidha, katika mwaka wa fedha
2003/2004 watumishi 26 walihudhuria mafunzo ya muda mrefu na 935 walihudhuria
mafunzo ya muda mfupi katika fani mbalimbali.
Lengo la mafunzo hayo ni kuwaongezea ujuzi na
ufanisi katika kazi zao. Wizara yangu
itaendelea na juhudi za kuwapatia mafunzo zaidi
wafanyakazi wake katika mwaka wa fedha 2004/2005.
Uboreshaji wa Utumishi wa Umma Serikalini
71. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2003/2004
Wizara ya Ujenzi, iliendelea kutekeleza Mpango wa Uboreshaji Utumishi wa Umma
Serikalini. Mradi wa kuanzishwa Mfumo wa Uendeshaji na
Usimamizi (Performance Management System) katika Wizara hii ulianzishwa
Januari, 2003. Wizara imeshiriki hatua kwa hatua
katika kutayarisha na kuandika Mpango Mkakati (Strategic Plan) kwa kipindi cha
mwaka 2003/2004 hadi 2005/2006 na Mkataba wa Huduma kwa Mteja. Aidha utaratibu mpya wa
kupima Utendaji Kazi kwa Watumishi wa Umma umeanza kwa kuwahusisha kwanza
Watendaji Wakuu wa Wizara.
Mikakati ya
kupambana na UKIMWI
72. Mheshimiwa
Spika, Katika kipindi cha mwaka 2003/04 Wizara
kupitia Kamati ya Ukimwi imeendesha Warsha za kuhamasisha Wafanyakazi wa ngazi zote kupambana na ukimwi. Aidha Warsha kama
hizo zimeendeshwa kwa Wafanyakazi wa baadhi ya Miradi ya Ujenzi wa Barabara
kama vile miradi ya barabara za Makuyuni-Ngorongoro, Chalinze-Melela n.k.
Halikadhalika,
Kamati ya ukimwi ya Wizara kwa kushirikiana na Mtaalam
Mshauri (Consultant) imeandaa Mpango Mkakati (Strategic Plan) ya utekelezaji wa
shughuli za kupambana na UKIMWI Wizarani kwa kipindi cha kuanzia 2004 – 2007.
73. Mheshimiwa Spika, ili kukabiliana na mmomonyoko wa maadili, Wizara ya Ujenzi
imeunda Kamati ya Maadili
Vita dhidi
ya Rushwa
74. Mheshimiwa
Spika, mikakati ya kupiga vita rushwa katika Sekta ya Ujenzi ambayo
Wizara yangu inaendelea kuitekeleza ni pamoja na
kuendelea kutekeleza kikamilifu Sheria Na. 3 ya mwaka 2001 (Public Procurement
Act No.3) ambayo inapunguza
Makusanyo ya Mapato kwa Mwaka 2004/05
75. Mheshimiwa
Spika, Wizara ya Ujenzi inatarajia kukusanya jumla ya shilingi
3,109,483,490 kutokana na vianzio vyake mbalimbali.
Idara zinazokusanya maduhuli ni Utawala, Ugavi na
Huduma pamoja na Ufundi na Umeme. Idara za Ufundi na
Umeme pamoja na Ugavi na Huduma ziko chini ya “Retention Scheme” hivyo
huruhusiwa kutumia kiasi fulani cha makusanyo
Matumizi ya Kawaida mwaka 2004/05
76. Mheshimiwa
Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05,
Wizara ya Ujenzi imetengewa jumla ya shilingi 62,099,569,100.00 fedha za
hapa kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida.
Fedha hizi zinajumuisha:
·
Mfuko wa Barabara – Shs. 50,010,100,000.00
·
Mishahara ya Wizara - Shs. 2,552,525,400.00
·
Mishahara ya Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara -
Shs. 4,634,749,400.00
·
Ruzuku kwa Taasisi nyingine zilizo chini ya Wizara -
Shs. 533,262,900.00
·
Retention - Shs. 2,329,623,840.00
·
Matumizi Mengineyo kwa Wizara - Shs. 1,760,212,060.00
Muhtasari wa makisio ya Matumizi ya
Kawaida kwa mwaka 2004/05 umeonyeshwa katika Kiambatanisho Na 9 kilichoko
ukurasa wa 90.
HITIMISHO
77. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua mchango mkubwa na muhimu wa
Wahisani katika kufanikisha malengo ya sekta hii. Napenda
nitumie nafasi hii kuwashukuru wahisani wote kutoka nchi mbalimbali, kwa moyo wao wa kusaidia nchi hii. Wahisani hao ni pamoja na
Serikali za nchi za Denmark, Finland, Italia, Japan, Marekani, Norway, Saudi
Arabia, Switzerland na Uingereza ambazo kwa kiasi kikubwa zimeisaidia sana
sekta ya Ujenzi. Pia nayashukuru mashirika ya kimataifa ya ADB, EU, IDA na Mfuko wa Maendeleo wa
78. Mheshimiwa Spika, naomba pia
nichukue nafasi hii kuishukuru kwa mara nyingine
Kamati ya Bunge ya Miundo Mbinu chini ya Uenyekiti wa Mheshimiwa Prof. Henry
Mgombelo, Mbunge wa Tabora Mjini, kwa ushauri mzuri waliotupa katika kuandaa
bajeti hii. Nawashukuru pia viongozi wa ngazi mbalimbali katika Wizara ya Ujenzi ambao ni Naibu
Waziri, Mheshimiwa Hamza Mwenegoha (Mb), Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini,
Katibu Mkuu Eng. John Kijazi, Wenyeviti wa Bodi za RFB, NCC, CRB, ERB, AQSRB na
NBMM. Aidha, nawashukuru Wakurugenzi na Watendaji Wakuu wa Taasisi na Wakala zote zilizo chini ya
Wizara yangu pamoja na wafanyakazi wote wa Wizara kwa kuonyesha utendaji mzuri
wa kazi na uwajibikaji.
79. Mheshimiwa
Spika, Wizara yangu inatambua umuhimu wa
Miundombinu, hususan barabara katika kukuza uchumi. Lengo la Wizara yangu ni
kuhakikisha Barabara Kuu zote Tanzania Bara zenye urefu wa kilomita 10,300 ziwe
zimekamilika kujengwa kwa kiwango cha lami ifikapo mwaka 2012. Hivyo hatua
mbalimbali tunazochukua ndani ya Wizara ni katika
kufanikisha lengo hili. Tunatambua tatizo la upatikanaji wa
fedha lakini siku zote tutaendelea kujitahidi ili fedha kidogo inayopatikana
itumike katika ujenzi wa barabara. Siku zote penye nia pana
njia. Naamini lengo letu litafanikiwa kutokana na
kasi ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami unaoendelea sasa katika nchi
nzima.
Makadirio ya Bajeti ya Wizara 2004/05
80. Mheshimiwa Spika, ili Wizara yangu iweze kutekeleza majukumu na malengo yake
ya mwaka 2004/05, naomba Bunge lako Tukufu liidhinishe bajeti ya jumla ya
Shilingi 287,237,763,100 ambapo kati ya hizo, Shilingi 146,618,569,100
ni za hapa na Shilingi 140,619,194,000 ni za nje.
Fedha za
hapa zinajumuisha:
·
Fedha za Matumizi ya Kawaida
shilingi 62,099,569,100
·
Fedha za Maendeleo Shilingi
84,519,000,000
Fedha za nje zinajumuisha:
·
Shilingi 129,623,400,000 kwa
ajili ya Miradi ya Maendeleo ya Barabara Kuu na za Mikoa.
·
Shilingi 10,995,794,000 za matengenezo ya Barabara Kuu
na za Mikoa.
81. Mheshimiwa
Spika, naomba kutoa hoja.