Hotuba ya Waziri wa Elimu na
Utamaduni
Mhe Joseph J Mungai MB Kuhusu Makadirio
ya Matumizi ya Fedha Kwa Mwaka 2005/06
I.
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge
lako tukufu baada ya kuzingatia taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya
Bunge ya Huduma za Jamii likae
2.
Mheshimiwa Spika nawashukuru; (a)
Mheshimiwa, Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji kwa hotuba yake
iliyotoa tathmini ya hali na mwelekeo wa Uchumi; na (b) Mheshimiwa, Waziri wa
Fedha, kwa hotuba yake iliyofafanua kwa ufasaha Bajeti ya Serikali ya mwaka
2005/06 pamoja na MKUKUTA. Aidha namshukuru
3.
Mheshimiwa Spika, Aidha, naishukuru
Kamati ya Bunge ya Huduma za Jamii, kwa ushauri wao mahili na kwa kupendekeza
Bajeti ya Wizara yangu ipitishwe na Bunge hili heshimika.
Majukumu ya Wizara
4.
Mheshimiwa Spika, katika kutekeleza
majukumu yake Wizara inaongozwa na (a) Sheria ya Elimu Na. 25 ya 1978; (b) Taarifa ya Mfumo wa Elimu ya Tanzania kwa Karne ya
21; (c) Sera ya Elimu na Mafunzo; (d) Sera ya Utamaduni; (e) Dira ya Maendeleo
ya Tanzania 2025; (f) Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini (MKUKUTA);
na (g) Ilani ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2000 ya Chama Tawala cha CCM.
II.
MAENDELEO YA ELIMU
NA UTAMADUNI YA MIAKA KUMI YA SERIKALI YA AWAMU YA TATU 1995 – 2005
5.
Mheshimiwa Spika, kwa kuwa huu ni
mwaka wa mwisho wa Serikali ya Awamu ya Tatu inayoongozwa na Rais Benjamin
William Mkapa, ningependa kulitaarifu Bunge kuhusu maendeleo makubwa ya Elimu
na Utamaduni yaliyopatikana katika kipindi hicho cha miaka kumi (1995 – 2005). Serikali ya Awamu ya Tatu ilianza kwa
kuchukua hatua mbili muhimu:
(i)
(ii)
Pili: Ilihakikisha
inatimiza masharti magumu ya HIPC
ili tuweze tena kukopesheka na kupewa misaada ya maendeleo. MMEM
na MMES ni matokeo ya hatua hii
muhimu.
(a) Elimu ya Msingi
6. Mheshimiwa Spika ,mafanikio ya Elimu ya Msingi yamekuwa:
· Shule za Msingi zimeongezeka 3,330 sawa na asilimia 30 kutoka 10,927 mwaka 1995 hadi
14,257 mwaka 2005.
· Watoto wa Rika la
Elimu ya Msingi (miaka 7–13) walioko
shuleni wameongezeka kutoka
asilimia 55 mwaka 1995 hadi asilimia 95 mwaka 2005.
· Kwa hiyo Watoto wa
rika
· Wanafunzi wa umri wa juu kuliko rika lengwa la miaka
7–13 wamepungua kutoka asilimia 22
mwaka 1995 hadi asilimia 15 mwaka 2005.
(b) Elimu ya
Sekondari
7.
Mheshimiwa Spika, Mafanikio ya Elimu ya Sekondari yamekuwa:
·
Shule za Sekondari
zimeongezeka kwa asilimia 195 kutoka
595 mwaka 1995 hadi 1,755 mwaka 2005, zikiwemo 1,206 za Serikali na 549 Zisizo
za Serikali sawa na asilimia 31.
·
Wanafunzi wa Shule
za Sekondari Kidato cha 1-6 wameongezeka
zaidi ya maradufu kutoka 196,375 wakiwemo asilimia 5.5 (NER) ya rika husika
mwaka 1995, hadi 524,325 wakiwemo asilimia 11.7 (NER) ya rika husika mwaka
2005.
·
Aidha, Huu ni
mwaka wa pili wa utekelezaji wa MMES, mpango
ambao utaongeza wanafunzi Kidato cha 1 hadi 4 kufikia 2,000,000, sawa na
asilimia 50 ya rika hilo, na Kidato cha 5 na 6 hadi 250,000 sawa na asilimia 25
ya rika hilo ifikapo mwaka 2010; na
· Umeanzishwa Mtaala Mpya ambamo masomo ya sekondari
yamepunguzwa kutoka 13 hadi 8 kwa kuunganisha masomo ya mchepuo na ya kawaida. Mtaala
huo mpya utampatia mwanafunzi elimu bora zaidi ya Sekondari yenye msingi imara
wa kuendelea na elimu ya juu au kujifunza ufundi au kujiajiri. Hatua hii ni utekelezaji wa taarifa maalumu iitwayo: The
Tanzania Education System for the 21st Century iliyoandaliwa
na Tume Maalumu ya Wataalamu iliyoteuliwa na Serikali mwaka 1990 ambayo ilizaa
Sera ya Elimu na Mafunzo ya mwaka 1995 (The Education and Training Policy 1995) na
Programu ya Maendeleo ya Sekta ya Elimu (Education Sector Development Programme –
ESDP) ya mwaka 1997.
(c) Elimu ya Ualimu
8. Mheshimiwa Spika, mafanikio ya Elimu ya Ualimu yamekuwa:
· Walimu Tarajali katika
Vyuo vya Ualimu wameongezeka kutoka 12,417 mwaka 1995 hadi 29,952 mwaka 2004,
ambalo ni ongezeko la 17,535 sawa na asilimia 141
· Vyuo vya Ualimu,
vimeongezeka kutoka 34 mwaka 1995 hadi 52 mwaka 2005 vikiwemo 18 vizivyo vya
Serikali sawa na asilimia 35
· Kuanzia mwaka huu,
Shule ya Sekondari ya Mkwawa, na Chuo cha Ualimu cha
· Mafunzo ya Kompyuta
na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA)
yanaanzishwa katika Vyuo vyote vya Ualimu.
Somo hilo litakuwa ni la lazima kwa
kila Mwalimu Tarajali.
(d) Ubora wa Elimu
9. Mheshimiwa Spika, katika miaka hii kumi kumekuwepo pia
ongezeko la ubora wa Elimu itolewayo katika shule kwa vipimo vya mitihani ya
Baraza la Mitihani
· Asilimia ya kufaulu
(Pass
Rate) Darasa la VII imeongezeka kutoka 15 mwaka 1995 hadi 49 mwaka
2004.
· Asilimia ya kufaulu
(Pass
Rate) Kidato cha 4 katika
Daraja la I–III imeongezeka kutoka 25 mwaka 1995 hadi 39 mwaka 2004 kwa shule
zote kwa pamoja na 53 kwa Sekondari za Serikali peke yake.
· Asilimia ya kufaulu
Kidato cha 6 katika Daraja la I–III imeongezeka kutoka 71 mwaka 1995 hadi 94 mwaka 2005.
(e) Maendeleo ya Utamaduni
10.
Mheshimiwa Spika, katika kuendeleza Utamaduni:
·
Sera ya Utamaduni
ilipitishwa mwaka1997;
·
Vikundi vya
burudani vilivyosajiliwa vimeongezeka kwa asilimia 377 kutoka 133 mwaka 1995
hadi 634 mwaka 2005; na
·
Wanafunzi wa
Stashahada ya Sanaa wa Chuo cha Sanaa Bagamoyo wameongezeka kwa asilimia 180
kutoka 30 mwaka 1995 hadi 84 mwaka 2005.
III.
MAFANIKIO YA UTEKELEZAJI WA
ILANI YA CCM YA MWAKA 2000
11. Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kufanikisha utekelezaji wa Ilani ya
Uchaguzi Mkuu ya CCM ya mwaka 2000, Serikali ya CCM ilichukua hatua tatu
muhimu:
(i) Kwanza
imeifanya elimu ya msingi kuwa ya bure na ya lazima.
(ii)
Pili kwa
ushirikiano na wabia na wadau wetu wote wa maendeleo ya elimu imeandaa MMEM
2002-2006 na MMES 2004-2009 inayotoa Ruzuku za Maendeleo na Uendeshaji kwa
wananchi wanaojenga shule.
(iii)
Tatu imepunguza
ada ya Sekondari za kutwa kwa asilimia 50 kutoka shs.40,000 kuwa shs.20,000 na
kuongeza maradufu ruzuku ya kuwasomesha watoto wa familia zisizo na uwezo ili
nao wajikomboe kwa elimu ya Sekondari.
Baada ya hatua hizo utekelezaji wa Ilani umekuwa na mafanikio makubwa yafuatayo katika
kipindi cha miaka mitano ya Bunge hili la 2000-2005:
(a) Elimu ya Msingi
12. Mheshimiwa
spika, kuhusu Elimu ya msingi:
(i)
Shule za msingi
zimeongezeka 2,603 kutoka 11,608 kufikia 14,257
sawa na asilimia 23.
(ii)
Wanafunzi
wameongezeka kwa asilimia 72 kutoka 4,382,410 wakiwemo asilimia 59 (NER) wa
rika lengwa hadi 7,541,208 wakiwemo asilimia 95 (NER) wa rika lengwa.
(iii)
Ruzuku ya Maendeleo ya Shs.Bn 147.733 imetolewa
kukamilishia ujenzi wa madarasa 32,539
na Nyumba za Walimu 9,664, Madawati 566,664, na Maliwato 14,417.
(iv)
Ruzuku ya Uendeshaji ya Shs.Bn 136.336 imetolewa
kwa ajili ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia. Hali ya vitabu imeboreka kutoka Kitabu 1 au 2
kwa Darasa hadi Kitabu 1 kwa wanafunzi 3.
(v)
Walimu wapya 45,451
wameajiriwa wakiwemo 37,261 wa Daraja A, na 7,152 wa Stashahada.
(vi)
Waliofaulu Mtihani
wa DVII wameongezeka kutoka asilimia
19 mwaka 1999 hadi 49 mwaka 2004.
(b) Elimu ya Sekondari
13. Mheshimiwa spika, Kuhusu Elimu ya Sekondari katika miaka mitano ya Bunge
hili:
(i) Zimeongezeka Sekondari 828 sawa na asilimia 89 kufikia Sekondari
1,755.
(ii) Wanafunzi
wameongezeka maradufu kutoka 266,896 hadi 524,325.
(iii) Jumla
ya Shs.Bn 43.100 zimetumwa shuleni
kwa ajili ya utekelezaji wa MMES ikiwemo:
(a) Ruzuku ya Maendeleo ya:
· Shs.Bn 10.500 za ujenzi wa madarasa 1,499:
na
· Shs.Bn 7.600 za
ujenzi wa Nyumba za Walimu 848: na
(b) Ruzuku
ya Uendeshaji ya Shilingi Bn 11.900 za vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
(iv)
Wanafunzi 24,000 wa familia zisizo na uwezo wanapewa
Ruzuku ya Sekondari ya Shs. Bn 1.600 katika Vidato vya 1 na 2.
(v)
Watahiniwa wa shuleni waliofaulu KIV katika DI-III wameongezeka kutoka asilimia 26 mwaka 2000 hadi 39 mwaka
2004.
(vi)
Watahiniwa wa shuleni waliofaulu K6 katika DI-III wameongezeka kutoka asilimia 82 mwaka 2000 hadi 94 mwaka
2005.
IV.
MALENGO
YA MWAKA 2005/06
A.
Idara ya Elimu ya Msingi
14. Meshimiwa Spika, Kupitia Idara ya Elimu ya Msingi mwaka 2005/06 unakuwa wa tano wa utekelezaji wa MMEM wenye malengo yafuatayo:
(a)
Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya shilingi Bilioni 5.556 ya kukamilishia ujenzi wa
madarasa 1,792.
(b) Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya shilingi Bilioni 3.312 kukamilishia ujenzi wa Nyumba za Walimu 920.
(c) Kuajiri Walimu wapya 7,286 ili kukidhi ongezeko la wanafunzi
wa Shule za Msingi.
(d)
Kutoa mafunzo kwa Walimu tarajali 9,000 wa Daraja A.
(e)
Kuendelea kutekeleza MEMKWA
na MUKEJA.
(f)
Kutoa Ruzuku ya
Uendeshaji wa Shule ya Shilingi Bilioni 62.145 ya vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili pia kufikia
uwiano wa kitabu kimoja kwa mwanafunzi (1:1)
(g)
Kuimarisha ubora wa elimu kwa kutekeleza mtaala mpya wa Elimu ya Msingi; na
kuboresha mfumo wa mitihani na upimaji wa Elimu ya Msingi na Ualimu ngazi ya
Cheti.
(h)
Kufuatilia na kuratibu utekelezaji wa MMEM katika kila
ngazi; na ukaguzi wa hesabu za MMEM
katika ngazi hizo na asasi za Wizara za TET
na NECTA.
(i)
Kuendelea kuimarisha utoaji wa elimu maalumu kwa watoto
wenye ulemavu katika ngazi ya elimu ya msingi.
15. Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Sekta ya Elimu ya mwaka huu ya jumla ya shilingi Bn 384.189 inaombwa kama ifuatavyo:
·
Kupitia Fungu 56 la TAMISEMI Shs.Bn 44.999
·
HAZINA moja kwa moja Halmashauri
Shs.Bn 307.322 ; na
· Kupitia Fungu 46 la Wizara yangu Shs.Bn 31.868
Jumla Shs.Bn.384.189
=============
16. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu Idara ya Elimu ya Sekondari imepangiwa malengo yafuatayo ya
MMES:
(a)
Kutoa Ruzuku ya Maendeleo ya Shs.Bn12.355 za kukamilishia ujenzi wa
madarasa zikiwemo:
·
Shilingi Bn 2.989 za madarasa mapya 427 katika Sekondari zilizopo.
·
Shs.Bn 8.470 za madarasa 1,210 ya Sekondari mpya za ngazi ya kawaida; na
·
Shs.Milioni 896.0 za madarasa mengine 128 ya Sekondari zilizopo za ngazi ya
juu K5 na K6.
(b)
Kutoa Ruzuku ya Maendeleo Shs.Bilioni 9.0 za kukamilishia ujenzi
wa Nyumba za Walimu zikiwemo :
·
Shs.Bn 3.843 za Nyumba 427 za Sekondari zilizopo.
·
Shs.Bn 5.157 za Nyumba za Walimu 573 za Sekondari mpya za kawaida.
(c)
Kujenga kwa tenda ya
Serikali maabara 88 katika shule zilizopo za ngazi za kawaida na ya juu wakati
mahitaji ni Maabara 1,278.
(d) Kujenga Maliwato, Hosteli, Mabweni, Maktaba na Kumbi za Mikutano kwa Shs.Bn 12.468.
(e) Kufanya
ukarabati wa shule za zamani kwa Shs. Bn
3.280.
(f) Kutoa
Ruzuku ya elimu ya Sekondari kwa wanafunzi 36,000 wa kidato cha 1 - 3 wa
familia zisizo na uwezo:Shs.6.480.
17. Mheshimiwa Spika, mwaka huu Idara ya
Elimu ya Ualimu imepangiwa majukumu yafuatayo :
(a) Kuanzisha miundo mbinu na mtandao wa Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) katika
Vyuo vya Ualimu vyote kwa ajili ya Kufundishia na Kujifunzia. Somo hili litakuwa la lazima kwa kila Mwalimu
Tarajali. Nawashukuru sana SIDA Sweden
kwa msaada wa Shs.Bn 4.168 pamoja na
huduma za kiufundi.
(b) Kutenganisha Vyuo
vya Stashahada viwe 14; na vya cheti Daraja A viwe 18.
(c) Kufuatilia uandaaji
wa muhtasari wa Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHEMA) kwa ajili ya Vyuo
vya Ualimu.
(d) Kuandaa Mkakati wa
Kuboresha Menejimenti na Elimu ya Ualimu.
D. Idara ya Ukaguzi wa Shule
18. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu Idara ya Ukaguzi wa Shule itafanya ukaguzi wa asasi mbalimbali
za Elimu 19,905, na itanunua magari 18 na kutoa mafunzo ya awali kwa Wakaguzi
wa shule wapya 127.
19. Mheshimiwa Spika, Idara pia itaendesha mafunzo ya mbinu shirikishi za ufundishaji kwa
Wakaguzi wa masomo ya English, Kiswahili, Physics, Chemistry, Biology na
Ualimu.
E. Idara
ya Maendeleo ya Utamaduni
20. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu, Idara ya Maendeleo ya Utamaduni itaendesha Tamasha Maalumu la kuimarisha umoja, amani, mshikamano na upendo
miongoni mwa Watanzania. Aidha
itaendesha katika Mikoa 10 utafiti wa kubaini mila na desturi nzuri za
kuimarisha ufanisi katika vita dhidi ya umaskini, rushwa, ubaguzi wa kijinsia, VVU
na UKIMWI.
21. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu Idara ya Utawala na Utumishi itaajiri watumishi 795 wa kada
mbalimbali ; na walimu 3,094 wa Shule za Sekondari. Aidha, Watumishi 150 watapelekwa kwenye
mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na
nje ya nchi.
22. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu, ADEM itatoa mafunzo mbalimbali kwa : Viongozi Watendaji wa
Elimu 21,294, na ya Stashahada ya
Uongozi wa Elimu kwa Wanachuo 100.
23. Mheshimiwa Spika, Mwaka huu Idara ya Sera na Mipango itatekeleza majukumu kumi na mbili yaliyoainishwa
ndani ya Hotuba ya Bajeti.
H. Ofisi
ya Afisa Elimu Kiongozi
24. Mheshimiwa Spika, Afisa Elimu Kiongozi ataendelea kutoa miongozo ya kuboresha Elimu na
Utamaduni, na kuongoza vitengo maalumu vilivyo katika ofisi yake. Aidha, ataendelea
kusimamia mambo ya uhusiano wa kielimu
wa kimataifa ukiwemo na SADC na EAC
I TAASISI NA
MABARAZA YALIYO CHINI YA WIZARA
25.
Mheshimiwa Spika, Wizara itaendelea
kusimamia Taasisi, Mabaraza na Mashirika yake Saba katika ukurasa wa 78-90.
V.
MATATIZO KATIKA
UTEKELEZAJI
26.
Mheshimiwa Spika, Katika uendeshaji wa
elimu na programu za MMEM na MMES yamejitokeza matatizo yafuatayo:
(a)
Kutokusoma au kutokuelewa
kwa usahihi Sheria na maamuzi yaliyomo katika maandiko muhimu ya Serikali
kumesababisha baadhi ya wadau, na watendaji kutokujua na hata kudiriki kupinga mabadiliko yanayoendana
na wakati likiwemo badiliko maalumu
la mtaala wa elimu ya Sekondari !!
(b)
Kuchelewa kuzibwa
pengo la fedha la MMEM kutokana na kumalizika utumiaji wa mkopo wa USD 150
milioni kutoka Benki ya Dunia na wahisani wengine kuwa katika mchakato wa
badiliko kutoka “Pooled Fund” kuingia “Budget Support” ambao
haujakamilika.
(c)
Kuwepo kwa pengo kubwa
la fedha katika programu ya MMES kutokana na kuwa na chanzo kimoja tu cha
uhakika ambacho ni mkopo nafuu wa Benki ya Dunia, wa USD 150 Milioni wakati
bado tunasubiri ahadi za wabia wetu wengine ambao nawaomba wafanye upesi.
(d)
Kuwepo kwa tatizo la
uelewa juu ya uendelevu wa programu ya MMEM baada ya 2006. Inafaa kila mdau, aelewe kwamba Elimu ya Msingi ni jambo la kudumu kwa
sababu watoto wataendelea kuwepo na kuongezeka.
Kipindi cha miaka mitano ya MMEM ni cha mpango kwa lengo la kufikia Elimu ya Msingi kwa wote; na ilihitajika kujenga majengo mengi ya shule kukidhi ongezeko
kubwa la wanafunzi na walimu. Baada ya
mpango kukamilika ongezeko la miundo mbinu ya shule litakuwa la kawaida kuendana
na ongezeko la idadi ya watu na watoto ambalo hatimaye litabebeka katika Bajeti
ya ndani.
VI.
MAAMUZI MUHIMU
27.
Mheshimiwa Spika, Mwaka huu Wizara
yangu itatekeleza maamuzi muhimu yafuatayo:
(a) Kuboresha utekelezaji wa Programu ya MMES kwa kuziimarisha
Shule za Sekondari kupokea, na kusimamia fedha za Ruzuku za Uendeshaji na Maendeleo
bila kupitia Hazina Ndogo.
(b) Kuendelea kuimarisha
mtaala wa Elimu ya Sekondari ili kukidhi changamoto za utandawazi, soko
huria na ushindani wa kielimu wa kimataifa. Nimetoa pamoja na Hotuba ya Bajeti
makala maalumu ya Maelezo ya Mtaala Mpya
wa Sekondari niliyoyatoa kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii. Wale ambao mpaka sasa bado hawajauelewa
mtaala mpya wanashauriwa wayasome kwa makini maelezo hayo, na maandiko niliyoyataja ambayo ndiyo
chimbuko la mtaala huo.
(c) Kuedelea kutoa Ruzuku ya Maendeleo na Uendeshaji
kwa wananchi wanaojenga shule za Msingi na Sekondari.
(d) Kuendelea na sera sahihi za CCM za kupunguza ada ya Sekondari za kutwa kuwa
shs.20,000/=; na kutoa elimu ya
msingi ya bure na ya lazima. Mheshimiwa spika nachukua fursa hii
kulitaarifu Bunge lako heshimika kuwa katika Azimio la Algiers la tarehe 11 April 2005 la Mawaziri wa Elimu wa
Africa kutokana na uzoefu na ushauri wetu kifungu cha 7 kinasomeka "TAKE
all necessary measures to make primary education free and compulsory for all
children of Africa" Huo
ndio ushauri wetu Mawaziri wa Elimu wa Afrika utakaofikishwa kwa Wakuu wa Nchi
za AU katika kikao chao cha mapema mwaka kesho.
Mheshimiwa Spika, kwa wale wanaopenda kusema mafanikio ya Rais Mkapa hayana ‘‘TRICKLE
DOWN’’ naomba kuwapasha kuwa (i) ada
ya Sekondari iiliyopunguzwa kuwa shs.20,000/= ; na (ii) elimu ya msingi ya bure inaingia
karibu KILA KAYA ya Tanzania nzima kupitia
mlangoni, na umasikini umeanza kutokea madirishani! Kwa mipango hii tumeanza kuandaa Rika Jipya la Watanzania ambao asilimia
100 watakuwa na elimu ya Msimi na
asilimia 50 watakuwa na elimu ya
Sekondari.
VII SHUKRANI NA PONGEZI
28. Mheshimiwa
spika, nawashukuru na nawapongeza wanachi wa
Mikoa yote na Halmashauri zao kwa moyo wao wa kujitolea kujenga na kuendesha Shule
za Msingi na za Sekondari. Aidha,
nawashukuru Waheshimiwa Wabunge na viongozi wote wa Mikoa, Wilaya, na Vijiji
kwa ushirikiano wao kuhimiza na kufanikisha ujenzi na uendeshaji wa Shule
katika maeneo yao.
29. Mheshimiwa
spika, naliomba Bunge hili liniunge mkono kuwashukuru nchi rafiki,
mashirika ya fedha ya kimataifa, wadau wote na wabia wetu wa maendeleo ya elimu
kwa misaada na ushirikiano wao kama nilivyowataja ukurasa 94 wa Hotuba ya
Bajeti.
30. Mheshimiwa
spika, nawashukuru sana wafuatao :
·
Naibu Waziri wangu Mheshimiwa Bujiku Sakila, Mbunge wa
Kwimba, kwa kunisaidia kwa uaminifu na bidii yake yote.
·
Katibu Mkuu wa Wizara
yetu Dr. Naomi Katunzi kwa ushauri
wa kitaalam na kitaaluma ; na
·
Aidha, Afisaelimu
Kiongozi, Wakurugenzi wa Idara wote, Wakuu wa Shule na Vyuo, Walimu Wakuu,
Walimu wote ; na Wafanyakazi wengine wote wa Wizara yangu ; kwa
ushirikiano wao katika kutekeleza majukumu ya wizara na pia katika kuandaa
Bajeti hii.
31. Mheshimiwa
spika, nawashukuru pia Viongozi na Wafanyakazi
wote wa Mabaraza na Taasisi zote zilizo chini ya Wizara yangu. Aidha, nawashukuru CWT na tawi la TUGHE la
Makao Makuu ya Wizara kwa ushirikiano na ushauri wao unaoepusha migogoro
kazini.
VIII MWAKA WA MWISHO
32. Mheshimiwa
Spika, kwa kuwa huu ndio mwaka wa
mwisho wa Serikali ya Awamu ya Tatu na wa Bunge hili ; nachukua nafasi hii
kutoa shukrani zangu za dhati kwa wafutao :
·
Kwanza kwa
Mheshimiwa Rais Benjamin Mkapa kwa kuniteua na kunipa fursa ya kuitumikia nchi
yangu kama Waziri wa Elimu na Utamaduni wa kipindi hiki cha mwanzoni mwa Karne
ya 21 yenye changamoto za Dunia ya Utandawazi
na Soko Huria.
·
Pili Mheshimiwa
Waziri Mkuu kwa ushiriki wake wa
kikatiba katika uteuzi wangu na kwa uongozi wake mzuri ; na
Waheshimiwa Mawaziri na Wabunge wenzangu wote kwa uashirikiano wao mzuri
sana. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa
kunijalia kuwa katika Timu nzuri ya Serikali ya Awamu ya Tatu iliyofunga mabao
mengi ya maendeleo.
·
Tatu Nawashukuru
sana wananchi wenzangu wa Jimbo la
Mufindi Kaskazini kwa fursa hii
waliyonipa, na nawaomba iwe Tena ! Tena ! Octoba mwaka huu ! Na ikiwa hivyo naahidi kuendelea kuwatumikia kama
Mbunge wao KWA LUHALA NA UPIFU; KWA BUSARA NA USHUJAA kama isemavyo motto
ya Hehe
Council iliyobuniwa na Hayati Mtwa Adamu Sapi Mkwawa: ‘Lidege Lingi Siliwhana amayago’.
·
Nne Nakushukuru
sana Mheshimiwa Spika, kwa uongozi wako uliotulizana wa ‘‘Nyumba ya Malumbano’’
kama wanavyoliita Bunge kule Malawi !!
Kwa uongozi wako uliotulizana tumelumbana kwa utulivu sana.
IX USHAURI
33. Mheshimiwa Spika, baada ya kuwa na jukumu la kusimamia na kuongoza
maendeleo ya elimu kwa miaka hii mitano ya mwisho ya Serikali ya Awamu ya Tatu
na ya mwanzo ya Karne ya 21 najipa uhuru wa kutoa ushauri ufuatao kwa Serikali
ya Awamu ya Nne.
(i) Kwanza
Kukamilisha bila kuchelewa uandaaji ambao tayari unaendelea wa: (a) Mpango wa Maendeleo ya Mafunzo ya Ufundi
(Vocational
Education Development Plan – VEDP) ili kupanua mafunzo ya ufundi kwa
ajili ya asilimia 50 ya wanafunzi ambao hawataendelea ngazi inayofuata ya elimu
ya kawaida baada ya DVII, Kidato cha
4 na Kidato cha 6; na (b) Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Juu (Higher
Education Development Plan – HEDP) ili kumudu ongezeko kubwa la
wahitimu wa Kidato cha 6 kutokana na
upanuaji wa Elimu ya Sekondari ya Juu uanoendelea. Wakati mwaka huu jumla ya
wanafunzi wa sekondari K1-6 ni 524,325; ifikapo mwaka 2010 wanaohitimu Kidato
cha 4 na Kidato cha 6 watakuwa zaidi ya 600,000 kwa mwaka.
(ii) Pili Inahitajika mapema iwezekanavyo kuanza kuandaa na
kukamilisha Awamu ya Pili ya SEDP
kwa lengo la kufikia Elimu ya Sekondari kwa Wote (Universal Secondary Education –
USE) ifikapo mwaka 2015 au mapema zaidi kwa sababu nusu USE iliyomo katika mpango wa sasa
haitoshi.
34. Mheshimiwa spika, mimi naamini hatua hizo mbili za (i) kukamilisha VEDP na HEDP na (ii) kuanzisha USE zitakuwa ni kichocheo muhimu cha
kusukuma gurudumu la maendeleo ‘kwa kasi
mpya, nguvu mpya na ari mpya’.
X MAKADIRIO YA
BAJETI YA WIZARA
35. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo yote hayo, ninaliomba sasa Bunge lako heshimika
lipitishe makadirio ya matumizi ya Shilingi
175,434,506,800 ili kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake ya
mwaka 2005/06. Kati ya fedha hizo:
(a)
Shilingi 66,070,411,000 zinaombwa kwa ajili ya
matumizi ya kawaida ya Wizara ya Elimu
na Utamaduni; na
(b)
Shilingi
109,364,095,800 zinaombwa
kwa ajili ya
Mipango ya Maendeleo ya Wizara ya Elimu na Utamaduni.
36. Mheshimiwa Spika, Hotuba hii ; na Hotuba
ya Bajeti inapatikana pia katika Tovuti ya Wizara yangu :
www.moec.go.tz
37. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.