HOTUBA YA WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU, MH.DK.PIUS Y. NG’WANDU(MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2005/2006

 

UTANGULIZI

 

1.     Mheshimiwa Spika, kutokana na taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii inayohusu Wizara yangu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2005/2006.

 

2.     Mheshimiwa Spika, aidha, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge, ndugu na marafiki katika kuwafariji na kuwapa salamu za rambirambi familia, ndugu na wapiga kura wa marehemu Mheshimiwa Abu Towegale Kiwanga aliyekuwa Mbunge wa Kilombero.  Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina.  Vilevile ningependa kutoa salamu za rambirambi na kuwapa pole ndugu na wananchi wa Majimbo yaliyofiwa na Wabunge wao katika kipindi hiki cha mwaka 2004/2005.  Wabunge hao waliofariki ni marehemu Balozi Ahmed Hassan Diria, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Raha Leo, marehemu Kapteni Theodos James Kasapira, aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Ulanga Mashariki, marehemu Frank Michael Mussati, aliyekuwa Mbunge wa Kasulu Mashariki na marehemu Yete Sintemule Mwalyego, aliyekuwa Mbunge wa Mbeya Vijijini.  Mwenyezi Mungu azilaze roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

 

3.     Mheshimiwa Spika, niruhusu pia niungane na Waheshimiwa Wabunge wenzangu katika kumpongeza; Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Mbunge wa Chalinze (CCM), kwa kuchaguliwa kwake kuwa mgombea urais kwa tiketi ya Chama Cha Mapinduzi.  Aidha, ningependa kuwapongeza wagombea urais watarajiwa waliokwishateuliwa na vyama vyao. Wote ninawatakia mafanikio katika uteuzi wao na Tume ya Uchaguzi.

 

 

4.     Mheshimiwa Spika, napenda kutoa shukrani zangu za dhati kwa wale wote waliotuwezesha kutekeleza majukumu ya Wizara yetu kwa kipindi kilichopita, na ambao wametuwezesha kupanga mipango ya mwaka 2005/2006 na kuboresha hoja zetu ambazo tunaziwasilisha katika hotuba hii.  Aidha, natoa shukrani kwa wananchi wote wa Tanzania kwa mchango wao katika kutekeleza majukumu ya Wizara yangu. Natoa shukrani zangu za dhati kwa Naibu Waziri wangu, Mheshimiwa Zabein Muhaji Mhita (MB); Katibu Mkuu wangu, Bibi Ruth H. Mollel, Watumishi wa Wizara yangu pamoja na taasisi na mashirika mbalimbali ya ndani na nje kwa misaada na ushauri wao, bila kumsahau Mheshimiwa Benedicto Mutachoka Mutungirehi, Mbunge wa Kyerwa (TLP) na Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani, kwa ushirikiano wake na mchango wake katika kuiboresha hoja hii. Kwa namna ya pekee natoa shukrani zangu kwa Waheshimiwa Wabunge wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii chini ya Mwenyekiti wao Mheshimiwa Omar Kwaang’w, Mbunge wa Babati Mashariki (CCM), kwa uchambuzi na ushauri wao.

 

Mwisho, ningependa kuelekeza shukrani zangu kwa wananchi wote hususan wananchi wa Jimbo langu la Maswa kwa kunienzi na kunifikisha hapa nilipo leo. Baada ya kikao hiki na baada ya Rais kulivunja Bunge lako Tukufu nitakuwa nimetimiza takriban miaka 25 mfululizo kama Mbunge. Nachukua nafasi hii kuwashukuru wananchi wa Jimbo langu la Maswa kwa heshima waliyonitunuku. Kwa heshima na unyenyekevu, ningependa kuchukua fursa hii kuwathibitishia nia yangu ya kustaafu sasa Ubunge wa Jimbo la Maswa kama nilivyowaomba hapo mwaka 2000 mara tu baada ya kunichagua. Kwako Mheshimiwa Spika, pokea shukrani zangu maalum kwa ushirikiano na mwongozo wako wa karibu. Kwa Wabunge wenzangu nasema kwa kheri ya kuonana. Asanteni sana kwa ushirikiano wenu. Wale mtakaogombea tena nafasi zenu nawatakieni mafanikio.

 

MUHTASARI WA UTEKELEZAJI WA ILANI YA UCHAGUZI  (NOVEMBA 1995 HADI 2005)

 

5.     Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha miaka kumi utekelezaji wa majukumu na mipango ya Wizara yangu umezingatia Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 1995 na 2000, Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025, Mkakati wa Kupunguza Umaskini, Sera ya Elimu ya Juu, Sera ya Ufundi na Mafunzo, Sera ya Sayansi na Teknolojia pamoja na Mpango Kabambe wa Wizara.

 

Nafurahi kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba mafanikio katika kipindi hicho ni zaidi ya asilimia tisini.  Baadhi ya malengo yaliyotekelezwa ni kama ifuatavyo:

       

·        kuweka utaratibu wa kuwasaidia wanafunzi waliofaulu vizuri ambao wazazi wao hawana uwezo wa kugharamia mafunzo ya elimu ya juu na ufundi;

 

·        kupanua, kuimarisha na kuboresha elimu ya juu na ya ufundi pamoja na ujasiriamali ili kusaidia ujenzi wa uchumi wa kisasa;

 

·        kuongeza nafasi ya elimu kwa wanawake na kuweka mazingira mazuri ya kupata elimu hiyo kuanzia elimu ya msingi hadi ya chuo kikuu;

 

·        kubuni mpango wa kuwaandaa mabingwa katika fani mbalimbali za sayansi na teknolojia ya viwanda nchini na nchi za nje;

 

·        kutoa kipaumbele na kuweka mtandao bora wa vituo vya tafiti nchini na kusambaza matokeo ya utafiti kwenye masoko; na

 

·        kuhakikisha sayansi na teknolojia za kisasa zinabuniwa na kusambazwa kwa wanawake ili kuwapunguzia harubu za kazi.

 

6.     Mheshimiwa Spika, mafanikio katika maeneo mengine ni kama ifuatavyo:

 

·        Mamlaka ya Elimu Tanzania iliyoanzishwa mwaka 2001 hadi mwezi Mei 2005 imetoa ruzuku na mikopo kwa taasisi za umma na binafsi yenye thamani ya Sh 12,537,979,195/= kwa lengo la kuboresha miundombinu.

·        Wizara yangu imeunda Bodi ya Mikopo kwa wanafunzi wa Elimu ya Juu na Ufundi. Bodi ilizinduliwa rasmi tarehe 30 Machi, 2005 kupitia chombo hiki, ni imani yangu kitawasaidia Watanzania wengi kupata nafasi za elimu ya juu na ufundi.

 

·        Mpango Kabambe kwa kipindi cha 2003-2018 ulikamilishwa ili kuongoza utekelezaji wa shughuli za sekta za sayansi na teknolojia, elimu ya juu na ufundi.

 

·        Serikali imetoa udhamini kwa wanafunzi 262 wanaosomea udaktari katika vyuo vikuu binafsi ili kuongeza idadi ya madaktari nchini.

 

·        Bunge lako Tukufu lilipitisha Azimio Na. 5 la Mwaka 2005 hapo tarehe 21 Aprili, 2005 Ili kukibadili Chuo cha Ufundi Mbeya kuwa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia kuanzia tarehe 1 Julai, 2005.

 

·        Wizara imefanya marekebisho ya Sheria ya iliyokuwa Tume ya Taifa ya Mionzi (NRC) ambayo kwa sasa ni Taasisi ya Nguvu za Atomiki - “Tanzania Atomic Energy Commission –TAEC”.

 

·        imekamilisha na kupitisha Bungeni Sheria ya Vyuo Vikuu ya mwaka 2005 (Universities Act).

 

·        imehusisha sekta binafsi katika kutoa huduma za usafi, ulinzi na mapokezi kuanzia tarehe 1 Desemba, 2004

 

·        Serikali imekamilisha mfumo wa kutumia gharama ya mwanafunzi katika vyuo vikuu na vyuo vya ufundi.

 

·        idadi ya vyuo vya elimu ya juu na ufundi nchini imeongezeka kutoka vyuo 23 mwaka 1995 hadi vyuo 43 mwaka 2005 na hivyo kutoa fursa kwa Watanzania wengi zaidi kupata elimu ya juu. Ili kuhakikisha kuwa vyuo hivyo vina hadhi na ubora unaohitajiwa, Baraza la Ithibati la Elimu ya Juu na Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi limechambua na kutoa ithibati na usajili kama ifuatavyo:

 

-                     vyuo vinne vimepewa barua ya mamlaka ya kuvianzisha ambayo ni Chuo Kikuu cha Arusha, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika cha Stadi za Biashara-Moshi na Chuo Kikuu Kishiriki kitarajiwa cha Tumaini Dar es Salaam.

 

-                     vyuo vinne vimepewa Hati ya Usajili wa muda. Vyuo hivyo ni Chuo Kikuu cha Mount Meru-Arusha, Kituo cha Elimu ya Jamii Changanyikeni-Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Afya cha Bugando-Mwanza na Taasisi ya Elimu ya Juu ya Chuo Kikuu cha Aga Khan-Dar es Salaam,

 

-                     vyuo saba vilipata Hati ya Usajili kamili navyo ni Chuo Kikuu cha Taifa-Zanzibar, Chuo Kikuu cha Mzumbe, Chuo Kikuu cha Zanzibar-Tunguu, Chuo Kikuu Kishiriki cha Iringa, Chuo Kikuu Kishiriki cha Tiba cha Kilimanjaro (KCMC)-Moshi, Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu-Zanzibar na Chuo Kikuu Kishiriki cha Makumira.

 

-                     vyuo vikuu vinane vina Hati ya Ithibati kama ifuatavyo:-Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki, Mikocheni- Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Augustino cha Tanzania-Mwanza, Chuo Kikuu cha Tumaini- Moshi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu Kishiriki cha Usanifu Majengo, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine, Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi na Tiba cha Muhimbili na Chuo Kikuu Huria cha Tanzania.

 

        MAFANIKIO YALIYOFIKIWA NA WIZARA TANGU 1995 HADI 2005        

7.       Mheshimiwa Spika, kwa upande wa mafanikio kwa kipindi cha miaka kumi, serikali imepata mafanikio katika maeneo mbalimbali ya elimu ya juu na ufundi, sayansi na teknolojia kama vile maeneo ya udahili, ushirikishwaji wa sekta binafsi katika utoaji wa elimu na huduma, kuboresha mazingira ya ufundishaji pamoja na urekebishaji wa mitaala ili iendane na mahitaji ya soko la ajira na matumizi ya sayansi na teknolojia.

 

8.       Mheshimiwa Spika, kwa upande wa udahili, idadi ya wanafunzi waliojiunga na vyuo vya elimu ya juu na ufundi iliongezeka kutoka wanafunzi 14,076 mwaka 1995/96 hadi wanafunzi 48,236 mwaka 2004/05. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 243. Idadi ya wanafunzi wa kike waliojiunga na vyuo hivyo katika kipindi hicho iliongezekea kutoka 2,369 mwaka 1995 na kufikia 15,782 mwaka 2004/05, ongezeko hilo la wanafunzi 13,413 ni sawa na asilimia 566.

 

9.       Mheshimiwa Spika, Wizara imeendelea na kuboresha miundombinu katika taasisi kwa kutekeleza miradi ifuatayo:

 

·        ujenzi wa mabweni Chuo Kikuu cha Dar es Salaam eneo la Mabibo yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 4,200 na mabweni mengine eneo la chuo yenye uwezo wa kulaza na wanafunzi 250.

 

·        ununuzi wa majengo ya Tanzania Audit Corporation barabara ya Chole kwa ajili ya Hostel ya Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili, yenye uwezo wa kutoa malazi kwa wanafunzi 595.

 

·        ujenzi wa mabweni matatu Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 620.

 

·        ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara vyenye uwezo wa kuhudumia wanafunzi 500  - Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

·        ukamilishaji wa ujenzi wa vyumba vya mihadhara vyenye uwezo wa kukaa wanafunzi 600 - Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi na Tiba Muhimbili.

 

·        ujenzi wa chanzo cha maji Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine na Chuo Kikuu Mzumbe na tanki la maji Chuo Kikuu Kishiriki cha Ardhi na Usanifu Majengo.

 

10.     Mheshimiwa Spika, kwa lengo la kuimarisha utoaji wa huduma za elimu ya juu na ufundi, serikali kupitia Bunge lako Tukufu limepitisha Sheria ya Vyuo Vikuu inayotoa taratibu rahisi za kuanzisha vyuo vikuu na vile vya ufundi. Aidha kwa ajili ya kutoa elimu yenye kukidhi mahitaji ya soko la ajira vyuo vya elimu ya juu na ufundi vimefanya uchambuzi wa mitaala yake, matokeo ya uchambuzi huo yamesaidia kurekebisha programmu zinazotolewa ili ziendane na mahitaji ya soko la ajira.

 

11.     Mheshimiwa Spika, serikali imeendelea kuhamasisha wananchi kupitia vyombo mbalimbali vya habari kuhusu umuhimu wa kutumia sayansi na teknolojia katika maisha yao ya kila siku. Kuanzia mwaka 1995, vipindi 52 vilitangazwa kila mwaka kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam. Aidha, serikali iliandaa mpango wa miaka mitano (2003-2008) wa uendelezaji wa sayansi ya msingi nchini pamoja na mwongozo wa kuwaendeleza wabunifu na wavumbuzi. Serikali pia iliendelea kuwatunuku wananchi waliofanya vizuri hasa wanawake ambapo Tuzo ya Sayansi ilitolewa kwa wasichana 27 waliofanya vizuri katika mitihani ya kumaliza Kidato cha Nne mwaka 2001 hadi 2003 na wasichana watano waliomaliza Kidato cha Sita mwezi Mei 2002 na 2003 katika masomo ya Hisabati, Kemia, Bailojia na Fizikia. Wanafunzi wasichana waliopata Tuzo ya Kidato cha Nne mwaka 2001, wanagharamiwa masomo yao ya Kidato cha Tano na Sita hadi Chuo Kikuu kulingana na maendeleo yao ya kimasomo.

 

12.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05 Wizara iliandaa mkakati wa kuongeza idadi ya Walimu utakaokidhi mahitaji ya Mpango wa Elimu ya Sekondari, hivyo imehuisha Vyuo viwili, Chang’ombe na Mkwawa kuwa Vyuo Vishiriki vya Elimu vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.


MAPITIO YA MWAKA 2004/2005

 

UTAWALA NA UTUMISHI MAKAO MAKUU

 

13.   Mheshimiwa Spika, kwa upande wa Utawala na Utumishi Makao Makuu katika mwaka 2004/05, Wizara yangu imetekeleza yafuatayo:

 

·        imeajiri watumishi 20 kwa ajili ya Makao Makuu na Vyuo vya Ufundi Mbeya na Arusha.

 

·        imewadhamini watumishi 36 kwa ajili ya mafunzo ya muda mrefu na mfupi.

 

·        imetayarisha mkataba wa utoaji huduma kwa wateja (Client Service Charter) kwa lengo la kuboresha huduma zitolewazo na wizara.

 

·        imeshirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma za mapokezi, ulinzi na usafi  kuanzia Desemba 2004.

 

·        imeendelea kutumia mfumo wa wazi wa upimaji wa utendaji kazi kwa watumishi wa umma (Open Performance Review and Appraisal System).

 

·        imeendesha mafunzo kwa watumishi 43 kuhusu Sheria ya Manunuzi na Misingi ya Maadili katika Utumishi wa Umma kwa lengo la kupambana na rushwa sehemu za kazi. Aidha, imeendesha mafunzo ya kompyuta kwa watumishi 70.

 

·        imeendesha mafunzo kuhusu masuala ya UKIMWI kama ifuatavyo:-

 

-                     uelimishaji rika (HIV/AIDS Peer Educators) kwa watumishi 37 na wanafunzi 34 toka Makao Makuu ya Wizara, Vyuo Vikuu na Taasisi zake.

 

-                     imejenga uwezo wa kuratibu shughuli za UKIMWI kwa watumishi 20 toka Makao Makuu ya Wizara, Vyuo Vikuu na Taasisi zake.

 

-                     imetoa ushauri nasaha kuhusu masuala ya UKIMWI  (HIV/AIDS Para-Counseling) kwa watumishi 70 Wizara Makao Makuu, Vyuo Vikuu na Taasisi zake.

 

TUME YA TAIFA YA UNESCO

 

14.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2004/2005 Tume ya Taifa ya UNESCO imetekeleza maamuzi ya kikao cha 32 cha mkutano mkuu wa UNESCO.  Katika kikao hiki miradi ifuatayo iliidhinishwa kutekelezwa:

 

-         Mradi wa Kuboresha Maktaba ya Kituo cha Madini cha Kusini na Mashariki mwa Afrika (Southern and Eastern Africa Mineral Centre).

 

-         Mradi wa Kuimarisha Ufundishaji wa Elimu ya Wanyama kwa kutumia Teknolojia ya Mawasiliano katika Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.

 

-         kuadhimisha miaka mia moja (100) ya Seminari ya Rubya. Ushirikiano wa UNESCO utaiwezesha Seminari kutafakari jukumu lake la kutoa elimu ya sekondari na kubuni mikakati mipya ya kuimarisha elimu hiyo ikiwa ni pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii inayoizunguka.

 

-         Mafunzo ya Uzamili kwa mtumishi mmoja katika eneo la Haki za Binadamu.

 

-         Mradi wa Kikanda wa Kuimarisha Mtandao wa Shule zilizoshirikishwa na shughuli za UNESCO katika Kanda ya Ziwa Victoria (UNESCO Associated Schools’ Project).

 

-         Mradi wa kutoa mafunzo na kuimarisha vitendea kazi kwa kituo cha Televisheni ya Taifa.

-         Tume iliratibu mafunzo ya muda mrefu na mfupi yaliyofadhiliwa na UNESCO kwa kushirikiana na nchi wanachama.

 

·        kufanya tathmini ya miradi iliyotekelezwa mwaka 2003/2004 na taarifa zake kuwasilishwa UNESCO.

 

·        kufanikisha uwekaji saini Makubaliano kati ya UNESCO na Serikali kuhusu uendeshaji wa Ofisi ya UNESCO Kanda ya Dar es Salaam. Ofisi hii inawakilisha nchi za Comoro, Madagascar, Mauritius, Seychelles na Tanzania yenyewe kama mwenyeji.

 

·        kuchapisha Jarida la TANZANIA AND UNESCO na kusambaza nakala zake kwa walengwa ndani na nje ya nchi.

 

ELIMU YA JUU

 

15.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Wizara yangu ilitekeleza yafuatayo:

 

·        kuunda Bodi ya kuratibu Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu na Elimu ya Ufundi nchini na nje ya nchi.

 

·        kutayarisha kanuni za mikopo ya wanafunzi wa elimu ya juu na elimu ya ufundi nchini na nje ya nchi.

 

·        kuratibu uboreshwaji wa mitaala na mbinu za kufundishia kwa lengo la kuboresha elimu ya juu.

 

·        kutathmini utekelezaji wa mpango wa ugharamiaji endelevu wa elimu ya juu.

 

·        kuelimisha wadau kuhusu upatikanaji na ugharimiaji wa elimu ya juu ndani na nje ya nchi.

 

·        kuendeleza ushirikiano wa kielimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Madola, Ushirika wa Maendeleo ya Kusini mwa Afrika na nchi mbalimbali ambazo zina ushirikiano wa kielimu na Tanzania.

 

·        kuendeleza udhamini wa wanafunzi 1,100 wa Shahada ya Kwanza ya Udaktari ambao kati yao, 262 wapo katika vyuo vikuu binafsi.

 

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 

16.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05 Chuo Kikuu cha Dar es salaam kilitekeleza yafuatayo:

 

·        kuendesha mifuko ya kugharimia utafiti na kudhamini wanafunzi.

 

·        kuendeleza eneo lililotolewa kwa ajili ya Taasisi ya Sayansi za Bahari kwa kutayarisha michoro na ‘geosurvey’.

 

·        kupanua Maktaba ya Chuo ili iweze kutumiwa na wanafunzi kwa saa 24.

 

·        kuendeleza utaratibu wa kudahili wanafunzi wa udhamini binafsi.

 

·        kuongeza idadi ya wanafunzi wa kike kutoka wastani wa asilimia 31 hadi kufikia asilimia 33.

 

·        kutoa mafunzo ya awali (pre-entry) kwa wanafunzi wa kike katika masomo ya sayansi, uhandisi, teknolojia na takwimu.

 

·        kufanya tathmini ya kuvipandisha hadhi Vyuo vya Ualimu vya Dar es salaam, Mtwara na Shule ya Sekondari ya Mkwawa kuwa Vyuo Vikuu Vishiriki na Ambatanishi vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

 

·        kukamilisha ukarabati wa sehemu ya kafeteria kuwezesha kutumika na wanafunzi wenye walemavu.

 

·        kutoa mafunzo kwa Wahadhiri katika utumiaji wa vifaa vya ‘Video Conference’.

 

·        kudahili wanafunzi 4,514 wa mwaka wa kwanza kwenye programu za Shahada ya Kwanza.

 

·        kuboresha mitaala kulingana na hali halisi ya matakwa ya wadau.

 

·        kuendeleza mikakati ya kuanzisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Madini, Nzega.

 

·        kutathmini mitaala (academic audit) kwa kutumia wataalam kutoka nje.

 

·        kushirikisha sekta binafsi katika kutoa huduma zisizo rasmi kama njia ya kuongeza ufanisi.

 

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ARDHI NA USANIFU MAJENGO

 

17.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Chuo   Kikuu cha Ardhi na Usanifu Majengo kilitekeleza yafuatayo:

 

·        kuunda mitaala ya masomo ya Shahada nyingine za Kwanza 12 na kusimamia kazi za kurekebisha mitaala ili kozi za msingi zinazofanana zifundishwe kwa pamoja .

 

·        kutathmini na kuhuisha mitaala 12 na kufanya mabadiliko pale panapostahili.

 

·        kuimarisha, kutangaza na kusimamia masuala ya kukuza uhusiano kati ya Chuo na taasisi mbalimbali za kitaifa zisizopungua 50 na kimataifa zisizopungua 20.

 

·        kuendelea na ujenzi wa jengo la ofisi 27 za Walimu na madarasa 11 na kukarabati barabara za ndani na maegesho ya magari.

 

·        kukamilisha jengo la Utawala kwa fedha za ndani.

 

·        kudahili wanafunzi 1,060 kati yao wanafunzi wa kike ni 188 ikiwa ni asilimia 18, waliodahiliwa kwa mwaka wa kwanza ni 279, kati ya hao, wanafunzi 250 walipata udhamini wa serikali.

 

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA SAYANSI ZA AFYA MUHIMBILI

 

18.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili kilitekeleza yafuatayo:

 

·        kukarabati na kuongeza uwezo wa maktaba ili iweze kuchukua wanafunzi kufikia 80 na kuongeza matumizi ya jarida za elektronik.

 

·        kuwekeana mkataba wa maelewano na Hospitali Kuu ya Taifa Muhimbili kuhusu utaratibu wa namna ya kuendesha sehemu ya shughuli zao kwa pamoja.

 

·        kupata ardhi ya ukubwa wa ekari 3,800 huko Kibamba na Kisarawe kwa ajili ya upanuzi wa Chuo.

 

·        kuendelea na matayarisho ya ukarabati wa hosteli zilizoko Barabara ya Chole, Oystebay, zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 595.

 

·        kudahili wanafunzi wa Shahada mpya za BSc. Nursing Midwifery na BSc. Nursing Management.

 

·        kusajili wanafunzi 1,467 kati yao wanafunzi wa kike ni 462 ikiwa ni asilimia 31.5. Wanafunzi waliodahiliwa katika mwaka wa kwanza ni 325.

 

·        kutoa mafunzo ya kompyuta kwa wahadhiri 32.

 

·        kuongeza uwezo wa nguvu za mtandao wa mawasiliano kutoka megabit 10 kwa sekunde kuwa 100 megabit kwa sekunde.

 

·        kudhamini wafanyakazi 23 masomo ya sekondari na 9 masomo mengine

 

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO

 

19.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kilitekeleza yafuatayo:

 

·        miradi mbalimbali inayojumuisha utafiti na mafunzo ya mbinu bora za kilimo kwa wakulima ikiwemo mradi wa bustani ya uzalishaji mboga na matunda, mradi wa kilimo cha mseto (agro-forestry), mradi wa uhakika wa chakula kwa wakulima wadogo wadogo, mradi wa mbuzi wa kienyeji wa kuzalisha maziwa na nyama, mradi wa utafiti wa kufichua mabomu kwa kutumia panya buku na mradi wa vanilla.

 

·        kutoa huduma za ushauri wa kilimo, utunzaji na usimamizi wa mali ya asili, misitu na ufugaji kwa wakulima na wafanyakazi.

 

·        kukarabati majengo na mtandao wa mabomba ya maji.

 

·        kujenga maabara ya zoolojia na kituo cha ujasiriamali na biashara.

 

·        kupanua jengo la maktaba ya kampasi ya Solomon Mahlangu na kukamilisha tathmini ya ujenzi wa chanzo mbadala cha maji kwa ajili ya kampasi hiyo. Kuendeleza ujenzi wa jengo la ‘Patholojia’ ya mbegu kwa ufadhili wa DANIDA.

 

·        kukamilisha taratibu za kukifanya Chuo cha Ushirika Moshi kuwa Chuo Kikuu Kishiriki cha Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo.

 

·        kuongeza idadi ya wanafunzi kutoka 2,280 kwa mwaka 2003/04 hadi wanafunzi 2,480 mwaka 2004/05 ongezeko hilo ni sawa na asilimia 8.

 

·        kununua majengo mawili (Balhabou hostels) kwa ajili ya kulaza wanafunzi 188.

 

·        kuhuisha mitaala 15 ya Shahada za Kwanza ili kukidhi mahitaji ya soko.

 

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

 

20.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/2005, Chuo Kikuu Huria kilitekeleza yafuatayo:

 

·                    kujenga mtandao wa kompyuta makao makuu (Local Area Network) na kuunganisha katika mtandao mkuu (Wide Area Network) vituo viwili vya mikoa, yaani Dar es Salaam na Mtwara pamoja na kununua kompyuta.

 

·                    kujenga maabara ya kompyuta (30) pamoja na kununua kompyuta kwa matumizi ya mafunzo kwa wanafunzi na wafanyakazi.

 

·                    kutayarisha mpango mkakati (Rolling Strategic Plan) wa chuo wa 2004/2005 – 2008/2009 ambao umeanza kutekelezwa.

 

·                    kutayarisha Sera ya Matumizi ya Mawasiliano ya Kompyuta (ICT Policy) na mpango thabiti wa kutekeleza sera ya matumizi ya kompyuta (ICT Masterplan) katika kufundishia na kuboresha utawala.

 

·                    kudahili wanafunzi 3,759 kati yao wanawake 1,033 na wanaume 2,721.

 

·                    kuhamasisha na kufikia uwiano wa asilimia 27 kati ya wanafunzi wa kike na wakiume waliodahiliwa mwaka 2005. Lengo la muda mrefu ni kufikia asilimia 40 ifikapo mwaka 2009.

 

CHUO KIKUU MZUMBE

 

21.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Chuo Kikuu Mzumbe kilitekeleza yafuatayo:

 

·        kuendeleza ujenzi wa maktaba ya Chuo kwa msaada wa fedha kutoka Mfuko wa Elimu.

 

·        kuendeleza ukarabati wa majengo ya Chuo kwa ajili ya malazi ya wanafunzi.

 

·        kukamilisha ukarabati wa jengo la zamani lililogeuzwa kuwa bweni.

 

·        kununua majengo manne ya iliyokuwa benki ya NBC huko Mbeya. Majengo hayo yanauwezo wa kuchukua wanafunzi 168 wa Shahada ya Kwanza au 84 wa Shahada ya Uzamili. Pia yana uwezo wa kuchukua wanasemina 27.

 

·        kusomesha Walimu saba katika ngazi ya Shahada ya Udaktari wa Falsafa (PhD).

 

·        kusajili wanafunzi 2,550, kati yao wanafunzi wa kike ni 955 ikiwa ni asilimia 37.5. Waliodahiliwa kwa mwaka wa kwanza ni 945.

 

BARAZA LA ITHIBATI LA ELIMU YA JUU

 

22.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Baraza la Ithibati la Elimu ya Juu lilitekeleza yafuatayo:

 

·        kukagua na kutathmini mipango ya kuanzisha vyuo na hatimaye kutoa Hati za Mamlaka ya kuanzisha vyuo vikuu vitano vya Mwenge (Moshi), Ruaha (Iringa), Muslim (Morogoro),  Bishop Kisanji (Mbeya) na Azad (Zanzibar).

·        kukagua na kutoa Hati Stahili za Usajili katika vyuo vinne vya Mzumbe, Chuo Kikuu cha Arusha, Chuo Kikuu cha Taifa cha Zanzibar na Chuo Kikuu Kishiriki cha Bugando.

 

·        kukagua kwa dharura kwa lengo la kutatua matatizo yaliyojitokeza katika uendeshaji na utawala wa Chuo Kikuu Zanzibar na Chuo Kikuu cha Mount Meru.

 

·        kutathmini kwa lengo la kuidhinisha programmu za masomo katika vyuo mbalimbali.

 

·        kufanya tathmini, kwa lengo la kutambua hadhi na uhalali wa Vyeti, Stashahada na Shahada za Kawaida na Kanuni za Uzamili kulingana na maombi ya wadau.

 

·        kuendesha warsha mbili za wadau wa sekta ya elimu ya juu kuhusu taratibu za kuanzisha vyuo bila kukiuka maelekezo katika Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na pia kuhusu nafasi ya elimu ya juu katika maendeleo ya Tanzania.

 

·        kutoa machapisho na taarifa za kuelimisha umma kuhusu mipango na taratibu za kupata elimu ya juu nchini na nje ya nchi (Guide to Higher Education in Tanzania).

 

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA

 

23.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/05, Mamlaka ya Elimu Tanzania ilitekeleza yafuatayo:

 

·        kukamilisha ziara za mikoa, kufikia ishirini, kwa madhumuni ya kuwahamasisha wadau kuchangia katika Mfuko wa Elimu, kuanzisha Mifuko ya Elimu katika Halmashauri za Wilaya na kuwekeza zaidi katika miradi ya elimu.

 

·        kuanzisha kipindi maalum cha redio kijulikanacho kama UJUE MFUKO WA ELIMU, madhumuni yake ikiwa ni kuwashirikisha wadau kutoa maoni yao juu ya Mfuko wa Elimu na kuwahamasisha kuchangia katika Mfuko na kuwekeza kwenye miradi ya elimu. Kipindi hiki hurushwa kila siku ya Jumapili saa 12.15 hadi saa 12.30 kupitia Radio Tanzania.

 

·        kutoa machapisho na vipeperushi vinavyoelimisha kuhusu Mfuko na shughuli za Mamlaka ya Elimu Tanzania.

 

·        kutoa ruzuku na mikopo yenye jumla ya Sh. 5,778,445,647 hadi mwezi April 2005 katika vyuo na shule 27.

 

·        Mfuko wa Elimu ulizinduliwa rasmi na Makamu wa Rais, Mheshimiwa Dokta Ali Mohamed Shein tarehe 11 Machi, 2005 na kiasi cha Sh 106 million zilichangishwa.

 

·        kuandaa mpango mkakati (strategic plan) wa miaka mitano wa kuanzia 2005/06 hadi 2009/10.   

  

IDARA YA UFUNDI

 

24.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2004/2005, Wizara yangu imefanya yafuatayo:

 

·        kugharamia mafunzo ya watumishi 20 wa Vyuo vya Ufundi vya Mbeya, Arusha na Makao Makuu katika ngazi ya Udaktari wa Falsafa, Shahada ya Uzamili, Diploma ya Uzamili na Stashahada ya Juu ya Uhandisi.

 

·        kukarabati mitambo, majengo na vifaa mbalimbali katika Vyuo vya Ufundi vya Arusha na Mbeya kwa gharama ya shilingi 64,281,200/=. Aidha, imenunua vifaa vya kufundishia vyuoni vyenye thamani ya shilingi 195,597,000/=.

 

·        kutoa mafunzo maalumu (Access Course) kwa wasichana 19 katika mpango maalumu wa kujiunga na elimu ya ufundi katika vyuo vya Arusha na Mbeya.

 

·        kutoa mafunzo maalumu ya ualimu (Pedagogical Training) kwa Maafisa Elimu 25 walioajiriwa katika Vyuo vya Mbeya na Arusha.

 

·        kununua mashine na mitambo yenye thamani ya shilingi milioni 400 kwa ajili ya Chuo cha Ufundi Mbeya katika kuimarisha ufundishaji wa Stashahada ya Juu ya Uhandisi.

 

·        kununua vitabu vya kiada na rejea vyenye thamani ya shilingi milioni 85 katika fani za mitambo, umeme, magari, usanifu majengo, ujenzi na masomo ya jumla kwa Vyuo vya Ufundi vya Arusha na Mbeya.

 

·        kumpata Mtaalamu Mwelekezaji (Consultant) kwa ajili ya kuhuisha Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo ya mwaka 1996.

 

·        kuendelea kujenga bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kike katika Chuo cha Ufundi Mbeya lenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 64.

 

·        kuongeza udahili wa wanafunzi katika Chuo cha Sayansi za Jamii Kivukoni kutoka 108 hadi 202.

 

·        kukamilisha upatikanaji wa hati miliki ya eneo la Bububu Zanzibar kwa matumizi ya Chuo cha Sayansi za Jamii Kivukoni.

 

·        kukamilisha mtandao wa “Internet” na tovuti ya Chuo cha Sayansi za Jamii Kivukoni.

 

·        kununua kompyuta 35, printa, mashine ya kurudufu na vitabu.

 

·        kukibadili Chuo cha Ufundi Mbeya (Mbeya Technical College) kuwa Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (Mbeya Institute of Science and Technology – MIST).

 

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM

 

25.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2004/2005 Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam imefanikiwa kutekeleza yafuatayo:

 

·        kuanza kutumia mitaala mipya ya masomo katika ngazi ya Shahada ya Uhandisi (Bachelor of Engineering) katika fani za Ujenzi, Mitambo, Umeme, na Mawasiliano Angani

 

·        kukarabati maabara 3 za Taasisi, hosteli 1 ya wanafunzi iliyoko Chang’ombe pamoja na mabweni 3 yaliyopo kwenye eneo la Taasisi baada ya kupata kiasi cha Shilingi milioni 165 kutoka Mfuko wa Elimu.

 

·        kugharamia mafunzo kwa watumishi 41 katika ngazi ya Diploma (1), Stashahada ya Juu ya Uhandisi/Shahada ya Uhandisi (5), Shahada ya Uzamili (18) na Udaktari wa falsafa (17).

 

·        kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi wahisani, mashirika ya kimataifa, vyuo vya elimu ya juu na vya ufundi vilivyo nchini na vya kimataifa kama ifuatavyo:-

 

-         kuendeleza mkataba na Serikali ya Watu wa China kwa kupeleka watumishi watatu China kwa ajili ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

 

-         kushirikiana na Chuo cha “Leeds Metropolitan University” kuendesha  kozi ya Uzamili “MSc. in Facilities Management” kwa udhamini wa “Association of Commonwealth Universities”.

 

-         kuendeleza mradi wa utafiti juu ya taka ngumu (Solid Waste Management) chini ya udhamini wa “British Council”.

 

-         kuendeleza ushirikiano na “Cape Town University of Technology” kupitia mikutano kati ya vyuo husika na kubadilishana watumishi kwa muda mfupi.

 

-         kuendeleza ushirikiano na Taasisi ya “e-Degree” (Afrika Kusini) kutoa mafunzo ya shahada mbalimbali kupitia mtandao wa kompyuta.

 

-         kuendeleza ushirikiano na Vyuo vya Ufundi barani Afrika chini ya utaratibu wa “Commonwealth Association of Polytechnics in Africa” (CAPA) kwa kushirikisha wahadhiri watatu (3) katika warsha ya kujenga uwezo kwenye usimamizi wa mafunzo na masuala ya jinsia.

 

-         kuendeleza mkataba na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT) kwa kuanza kufundisha programu mpya inayotoa cheti cha IT-Basic Technician.

 

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

 

26.   Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha wa 2004/2005, Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi limetekeleza yafuatayo:

 

·        kusajili vyuo vya ufundi 52 kati ya hivyo 35 vimepewa Hati ya Usajili Kamili (Full Registration) na 17 Usajili wa Muda (Provisional Registration).

 

·        kukagua na kutoa Hati ya Ithibati Kamili (Full Accreditation) kwa vyuo 5 na Ithibati ya Muda (Provisional Accreditation) vyuo 17.

 

·        kuidhinisha kuanzishwa na kuanza kutolewa kwa elimu na mafunzo ya ufundi katika chuo kimoja binafsi cha “St. Joseph College of Engineering and Technology” cha Dar es Salaam.

 

·        kuweka viwango vya mafunzo (standards of training programmes) kwa programu 12 za elimu na mafunzo ya ufundi.

 

·        kuidhinisha mitaala inayozingatia umahiri wa wanafunzi kwa programu za mafunzo 36. Mitaala hiyo tayari imeanza kufundishwa katika Taasisi ya Teknolojia Dar - es - Salaam na chuo binafsi cha “St. Joseph College of Engineering and Technology”. Aidha, mitaala mipya inayozingatia umahiri itaanza kufundishwa pia katika Chuo cha Mipango cha Dodoma, Chuo cha Bahari cha Dar es Salaam mara mwaka mpya wa masomo utakapoanza.

 

·        kutayarisha mitaala mipya kwa progamu za mafunzo 6 katika eneo la mafunzo la Uhandisi na Sayansi zingine. Mitaala hiyo itaanza kufundishwa katika vyuo vya ufundi vya Arusha, Karume (Zanzibar) na Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Mbeya (MIST) mara mwaka mpya wa masomo utakapoanza.

 

·        kuendelea kuratibu Mitihani ya Kitaifa ya Ufundi Sanifu (Full Technician Certificate) na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (Advanced Diploma in Engineering) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA).

 

·        kutayarisha taratibu na kanuni za usajili wa wataalam, walimu na mafundi wengine wanaofundisha katika vyuo vya ufundi kwa lengo la kuhakiki sifa za wataalam hao. Aidha Baraza limeendesha mafunzo katika kanda sita kuhusu usajili wa wataalam wanaofundisha katika vyuo vya ufundi.

 

 

IDARA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

27.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha cha 2004/2005 Wizara yangu imetekeleza yafuatayo:

 

·        kuwasilisha kwenye Bunge lako Tukufu na kuridhia mikataba minne na itifaki moja inayolenga kukuza na kusimamia matumizi salama na ya amani ya nishati ya nyuklia kwa maendeleo ya Taifa, kama ifuatayo:-

 

-         azma ya kutokomeza au kutoendeleza utengenezaji na matumizi ya silaha za nyuklia (Non-Proliferation of Nuclear Weapons Treaty-NPT).

 

-         kutumia Nishati ya Nyuklia kwa shughuli za amani tu na siyo katika utengenezaji wa Silaha za Nyuklia (Safeguards Agreement).

 

-         Itifaki ya Kimataifa “Additional Protocol to Safeguards Agreement”.

 

-         azma ya kutoa Taarifa ya Ajali ya Nyuklia Mapema (Early Notification of Nuclear Accident).

 

-         Misaada ya Kushughulikia Ajali ya Nyuklia au Dharura ya Ki-Radiolojia (Convention on Assistance in Case of a Nuclear Accident or Radiological Accidents).

 

·        kuandaa Mkataba unaolenga Kusimamia Utunzaji wa Ulinzi wa Vyanzo vya Nyuklia “Convetion on Physical, Protection on Nuclear Material”, Maazimio ya Mkataba huu yaliwasilishwa na kupitishwa katika Kikao cha Bunge cha mwezi Aprili mwaka 2005.

 

·        kuandaa na kupitishwa Bungeni katika kikao chake cha mwezi Aprili 2005 Sheria iliyounda Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (The Mwalimu Nyerere Memorial Academy).

 

·        kuwasilisha Baraza la Mawaziri, Waraka wa Baraza la Mawaziri kuhusu Utungaji wa Sera ya Bioteknolojia baada ya kujadiliwa na wadau mbalimbali.

 

·        kuandaa na kuboresha maeneo ya ushirikiano katika sayansi  na teknolojia kati ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali za Cuba, Korea, Vietnam na Switzerland.

·        kufanya maandilizi ya uanzishwaji wa Kituo cha Radianuclide Monitoring Chuo Kikuu cha Dar es Salaam chini ya CTBTO.

 

·        kusaini Hati ya Maelewano “Memorandum of Understanding” ya Ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uswiss katika kuendeleza ujuzi na mafunzo katika maeneo ya utafiti wa kisayansi na kiteknolojia pamoja na uboreshwaji wa miundo mbinu ya asasi, taasisi za utafiti na maendeleo.

                         

·        kufanya mazungumzo mapya ya mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuhusu Mradi wa Nishati ya Jua utakaotekelezwa katika Kijiji cha Mwasayi, Wilayani Maswa. Aidha taarifa ya Maelewano “Memorandum of Understanding” ya Ushirikiano kati ya Serikali hizo mbili imeandaliwa na inatarajiwa kusainiwa hivi karibuni.

 

·        kuandaa na kurusha hewani vipindi 52 kupitia Redio Tanzania Dar es Salaam, vinavyohusu umuhimu wa kutumia sayansi na teknolojia.

 

 

28.   Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliendelea kutoa Tuzo ya Wizara kwa wasichana ishirini (Kidato cha Nne wasichana kumi na moja na Kidato cha Sita wasichana tisa) waliofanya vizuri na kuongoza kwa upande wa wasichana katika masomo ya sayansi ya msingi (hisabati, kemia, fizikia na bailojia) katika mwaka wa 2004. Vile vile ilitoa Tuzo hiyo kwa wasichana kumi na tatu waliofaulu mwaka wa kwanza wa 2003/2004 na kuongoza katika masomo ya sayansi katika Chuo Kikuu cha Dar Es Salaam na Chuo Kikuu cha Kumbukumbu ya Hubert Kairuki. 

 

29.   Mheshimiwa Spika, Wizara yangu kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais - Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI)  ilifanya mkutano wa pamoja kuhusu uundwaji wa Kamati za Sayansi na Teknolojia katika ngazi za Mikoa na Wilaya ili kufikisha dhana ya sayansi na teknolojia.

 

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

30.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2004/2005, Tume ya Taifa ya Sayansi ya Teknolojia ilitekeleza yafuatayo: -

 

·        kufuatilia wabunifu na wagunduzi wenye vipaji maalum katika mikoa ya  Iringa, Mbeya, Mwanza, Rukwa na Kagera na jumla ya vijana 26 walipatikana.

 

·        kuendelea kufadhili miradi ya utafiti kulingana na vipaumbele.

 

·        kuendelea kutoa mafunzo mbalimbali kwa watafiti ili kuweza kutayarisha miradi ya utafiti inayokubalika kitaaluma.

 

·        kubuni jiko sanifu na kuwapatia mafunzo mafundi wadogo wadogo 52 katika mkoa wa Dar es Dalaam na Dodoma.  Jumla ya majiko 500 yamesambazwa mikoani.

 

·        kushirikiana na Shirika la Nyumbu kutengeneza trekta dogo linaloongozwa kwa mkono ambalo linafanyiwa majaribio.

 

·        kushirikiana na Wakala wa Usajili wa Leseni za Biashara, Tume imeanzisha na kuisajili kama kampuni IP – Forum inayojumuisha wanataaluma, watafiti, wagunduzi na wanachi kwa ujumla kwa lengo la kulinda bunifu za wanasayansi na teknolojia.

 

·        kuendelea kukarabati jengo la Tume.

 

·        kukamilisha uanzishaji wa Masjala ya Taifa ya Utafiti (MTU) itakayowezesha upatikanaji wa taarifa mbali mbali za utafiti kutoka ndani na nje ya nchi.  Taarifa kamili ya Masijala hiyo inapatikana katika: http://www.research.or.tz

 

·        Kuimarisha mtandao wa mawasiliano kwa kusambaza leseni za “software” za “Microsoft Office” kama vile za “Windows 2000” na “Microsoft Office XP” ili kuwanusuru Watanzania kutumia “Microsoft” zisizo halali. Aidha iliweza kununua kompyuta 1000 kutoka kwa taasisi zisizo za Kiserikali kutoka nje ya nchi na kuzisambaza.

 

·        Kutoa mafunzo ya kompyuta kwa watumishi 300 kutoka Serikalini, wafanya biashara, wanasiasa (Waheshimiwa Wabunge na Madiwani).

 

TUME YA TAIFA YA NGUVU ZA ATOMIKI

31.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka wa fedha 2004/2005 Tume ya Taifa ya Nguvu za Atomiki ilitekeleza yafuatayo:

 

·        kutoa huduma ya upimaji wa mionzi (Personnel Radiation Monitoring) kwa wafanyakazi wa mionzi 1,000 kati ya 1,200 kutoka katika vituo 121 kati ya vituo 250. Aidha ilikagua vituo 135 kati ya vituo 250 vya mionzi.

·        kufuatilia vituo 23 vilivyokuwa vimefungiwa ili kuhakikisha havikiuki agizo la kusimamisha huduma za X-ray ambapo vituo tisa (9) vilirekebisha kasoro zilizoonekana wakati wa ukaguzi na kuruhusiwa tena kuendelea na kutoa huduma za X-ray. 

 

·        kufanya marejeo ya kanuni za kinga ya mionzi “The Protection from Radiation (Code of Practice) Regulations 1990” ambapo kanuni mpya, zinazoitwa “The Atomic Energy Protection from Ionizing Radiation Regulations 2004” zimetayarishwa. 

 

·        kutoa elimu ya kinga ya mionzi kwa njia za redio na vipindi vya television. Aidha Tume iliendesha semina nne (4), moja kati ya hizo zikiwa ni kwa watumiaji wa mionzi (Radiographers), mbili kwa ajili wafanya kazi katika migodi na nyingine ya “power conditioning”.

 

·        kuratibu na kusimamia utekelezaji wa miradi minane (8) mradi wa kutokomeza mbung’o Mafia na Babati; na ule wa kuendeleza mifugo, Zanzibar baada ya utokomezaji wa mbung’o inayogharamiwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomic (IAEA) inayotumia teknolojia ya mionzi hapa nchini. Miradi ambayo Taasisi husika zilipatiwa zaidi ya dola za kimarekani 770,000 kama vifaa, mafunzo kwa wataalamu wake, na ushauri wa kitaalamu. 

 

·        kutoa leseni ya kutumia mionzi kwa vituo 145 

 

·        kuanza kutumia jengo la Kuhifadhi mabaki ya vyanzo vya mionzi.

 

·        kukagua sampuli 2,800 za vyakula, mbolea na bidhaa nyingine za vyakula ili kudhibiti viwango vya mionzi katika vyakula viingizwavyo na viendavyo nje ya nchi (imports and exports).

 

·        kufanya matengenezo ya mashine 18 za x-ray na vifaa vingine vya nyuklia. 

 

·        kuhakiki (calibrate) vifaa 28 vya kupima mionzi ambapo vifaa kumi na mbili(12) vikiwa vya hapa nchini na 16 kutoka nchi za Kenya, Uganda na Zambia.

 

·        kugharamia masomo ya Shahada ya Uzamili katika Sayansi (Msc) na Sheria  (LLM) kwa wafanyakazi wawili wa Taasisi. 

 

·        kuanzisha maabara ya X-Ray (XRF) Fluorescence Spectroscopy na X-Ray Diffraction (XRD).

 

·        kuanzisha maktaba ya kupatia taarifa za Kimataifa za Nyuklia (International Nuclear Information System-INIS), kupitia mradi wa IAEA.

 

·        kuimarisha usalama katika vituo vyenye vyanzo vya mionzi kwa kuweka vyombo vya kutoa tahadhari (Security Alarm Systems na Radio Call) katika Vituo vyake vilivyopo Ocean Road Cancer Institute, Tanga, Central Radioactive Waste Management Facility ya Tume iliyoko Njiro, katika ofisi za Tume - Arusha, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam na Hospital ya Taifa ya Muhimbili.

 

·        kutangaza katika Gazeti la Serikali orodha ya watumiaji wa vyanzo vya mionzi ayonisha ambao walikidhi masharti ya usalama wa utumiaji wa vyanzo vya mionzi na kupata leseni kwa kipindi 2003/2004.

 

MPANGO WA MWAKA 2005/2006

 

UTAWALA NA UTUMISHI MAKAO MAKUU

 

32.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Idara ya Utawala na Utumishi inatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kudhamini watumishi 49 mafunzo ya muda mrefu na mfupi ndani na nje ya nchi.

 

·        kuendesha mafunzo ya kompyuta na mifumo ya habari (IT) kwa watumishi 150 katika sehemu za kazi (in-house training).

 

·        kushirikisha sekta binafsi katika utoaji wa huduma zisizo rasmi (no-core functions) katika Vyuo vya Ufundi Mbeya na Arusha hususan huduma za ulinzi, usafi na chakula.

 

·        kutekeleza mfumo wa uwazi wa upimaji utendaji kazi kwa watumishi (Open Performance Review and Appraisal System).

 

·        kuajiri watumishi 73 kwa ajili ya Makao Makuu ya Wizara, Vyuo vya Ufundi Mbeya na Arusha. Aidha, Wizara inatarajia kuajiri wanataaluma na watumishi wengine 405 kwa ajili ya Vyuo Vikuu, Taasisi zake kwa lengo la kupunguza uhaba wa wafanyakazi.

 

·        kuendelea kuwaelimisha watumishi wa Wizara kuhusu mpango wa serikali wa kuboresha utendaji kazi na huduma bora kwa umma.

 

·        kuhamasisha watumishi kupima afya zao na kutoa huduma kwa watakaojitokeza kwa hiari yao.

 

·        kuendelea kutekeleza mkakati wa kuwaelimisha wananchi na watumishi kupitia vyombo vya habari kuhusu taratibu za kupata huduma zitolewazo na Wizara kwa lengo la kupiga vita rushwa.

 

TUME YA UNESCO

 

33.   Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2005/2006 Tume ya Taifa ya UNESCO inatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuandaa, kwa kushirikiana na asasi za kiserikali na zisizo za kiserikali, Programu na Bajeti ya UNESCO kwa kipindi cha 2006-2007.

 

·        kuratibu utekelezaji na kufanya tathmini ya miradi inayoendelea na ile itakayoidhinishwa kwa kipindi cha 2006-2007 kama itakavyoamuliwa na Kikao cha 33 cha Mkutano Mkuu wa UNESCO.

 

·        kuifanyia mapitio Katiba ya Tume ya UNESCO kwa lengo la kuipa Tume na Sekretarieti yake nguvu zaidi za kiutendaji.

 

 

ELIMU YA JUU

 

34.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Wizara yangu inatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kuelimisha wanafunzi na umma kwa ujumla kuhusu nafasi za elimu ya juu nchini na nje ya nchi.

 

·        kukamilisha utayarishaji wa kanuni chini ya Sheria ya Vyuo               Vikuu ya mwaka 2005 na kusimamia utekelezaji wake.

 

·        kuelimisha wadau kuhusu upatikanaji wa mikopo kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu na Ufundi.

 

·        kutathmini Sera ya Elimu ya Juu na kutoa mapendekezo ya kuiboresha.

 

·        kuratibu mafunzo kwa viongozi wa serikali na mashirika ya umma wa ngazi ya kati na juu. Mafunzo hayo ambayo yatagharamiwa baina ya serikali na watendaji wakuu wa mashirika mbalimbali (CEO) yanalenga kuboresha ufanisi ili kuimarisha mchango wa sekta binafsi katika kukuza uchumi wa Taifa.

 

·        kushughulikia urejeshwaji wa utaratibu wa serikali wa kudhamini wanafunzi nje ya nchi kwa baadhi ya fani muhimu kitaifa ambazo hazipatikani nchini au nafasi zake ni finyu.

 

·        kuendeleza ushirikiano wa kielimu katika Jumuiya ya Afrika Mashariki, Jumuiya ya Madola, Ushirika wa Maendeleo ya Nchi zilizo Kusini mwa Afrika na nchi mbalimbali zilizo na ushirikiano wa kielimu na Tanzania.

 

·        kuendelea kudhamini wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Udaktari. Kwa mwaka 2005/06, Wizara itadhamini wanafunzi 1,427 (1,060 katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili na 367 katika Vyuo Vikuu binafsi).

 

·        kudhamini wafanyakazi na wanataaluma 40 katika Shahada za Uzamili na Shahada za Juu za Falsafa. Kati yao 27 ni wa Shahada ya Uzamili na 13 ni wa Shahada ya Juu ya Falsafa. Hatua hii inachangia katika kuongeza idadi na uimarishaji wa wanataaluma katika vyuo vikuu nchini.

 

CHUO KIKUU CHA DAR ES SALAAM

 

35.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06 Chuo, Kikuu cha Dar es salaam kinatarajia kutekeleza yafuatayo;

 

·        kudahili wanafunzi 3,440 wa Shahada ya Kwanza na 420 wa Stashahada ya Ualimu.

 

·        kukamilisha ujenzi wa madarasa makubwa mawili yenye uwezo wa kila moja kukaliwa na wanafunzi 1,000.

 

·        kuendeleza Sehemu ya Buyu iliyotolewa na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

 

·        kuanzisha Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam.

 

·        kuanzisha programu za Stashahada na Shahada za Ualimu kwenye Chuo Kikuu Kishiriki cha Elimu cha Dar es Salaam.

 

·        kuboresha huduma ya maji kwenye Mabweni ya Mabibo.

 

·        kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wanafunzi wengi chuoni.

·        kuanzisha ukarabati wa Chuo Kikuu cha Elimu cha Chang’ombe na Mkwawa.

 

·        kutoa mafunzo maalum kwa wadahiliwa wa kike kwenye fani za Sayansi, Teknolojia, Uchumi na Takwimu kwa lengo la kuongeza wahitimu wa kike kwenye fani hizo.

 

·        kuchapisha na kusambaza matokeo ya utafiti kwa wadau kupitia majarida mbalimbali ya ndani na nje ya nchi.

 

·        kushirikiana na taasisi zingine ndani na nje ya nchi katika kufanya utafiti.

 

·        kuendelea kutoa elimu juu ya UKIMWI na ushauri nasaha kwa jumuiya ya Chuo Kikuu.

 

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA ARDHI NA USANIFU MAJENGO

 

36.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Chuo Kikuu cha Ardhi na Usanifu Majengo kinatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

·        Kuendelea na utayarishaji wa sera na programu katika kuboresha ufanisi wa uendeshaji wa Chuo.

 

·        kuongeza udahili wa wanafunzi, kufikia 350 sawa na ongezeko la asilimia 40.

 

·        kuendelea kurekebisha mitaala ili kuruhusu kozi nyingi za msingi na zingine zinazofanana zifundishwe kwa pamoja katika idara mbalimbali ili kuimarisha ufanisi wa utoaji mafunzo.

 

·        kuendeleza wafanyakazi wa Chuo kimasomo.

 

·        kuimarisha uwiano kati ya wanawake na wanaume kwa kukamilisha na kutekeleza Sera ya Jinsia itakayosimamia shughuli za jinsia.

 

·        kuimarisha mahusiano na taasisi mbalimbali za kitaifa na kimataifa zinazohusiana na taaluma za makazi na mazingira.

 

·        kuimarisha na kuratibu matumizi ya teknolojia ya mawasilano (ICT) katika shughuli za ufundishaji na uendeshaji wa Chuo.

 

·        kukarabati mabweni matatu, ofisi 13, vyoo 10, na nyumba 10 wanazoishi wafanyakazi wa Chuo.

 

·        kujenga madarasa makubwa 6 yenye uwezo wa wanafunzi 200 kila moja.

 

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA SAYANSI ZA AFYA MUHIMBILI

 

37.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili kinatarajia kufanya

        yafuatayo:

 

·        kuendeleza ukarabati wa nyumba zilizonunuliwa kwa ajili ya matumizi ya hosteli za wanafunzi zilizopo Barabara ya Chole, Dar es salaam.

 

·        kujenga kumbi kubwa mbili za kisasa za kufundishia, zenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 350 kila moja, ambazo pia zitakuwa na jumla ya vyumba 40 vya ofisi.

 

·        kuendelea na upanuzi wa maktaba, kuweza kuhudumia watumiaji 1,300 kwa wakati mmoja, ikilinganishwa na uwezo wa watumiaji 200 hivi sasa.

 

·        kuanza kuendeleza ardhi ya Chuo iliyoko Kibamba/Kisarawe.

 

 

 

 

 

 

TAASISI YA UANDISHI WA HABARI NA MAWASILIANO YA UMMA

 

38.   Mheshimiwa Spika, Taasisi ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya Umma, inatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuongeza madarasa matano yenye uwezo wa kutumika na wanafunzi 480.

 

·        kudahili wanafunzi 100, kati yao 80 kwa udhamini wa serikali 20 udhamini binafsi.

 

·        kuzungusha ukuta katika eneo la Taasisi ili kuimarisha usalama wa mali na vifaa vya taasisi.

 

·        kuendeleza tafiti mbalimbali na kutoa ushauri.

 

·        kuimarisha kituo cha Redio kwa kununua “Outside Broadcasting Van–OBVAN” na “transmitter” (Radio Mlimani FM) ili matangazo yake yaweze kusikika sehemu nyingi nchini.

 

CHUO KIKUU CHA SOKOINE CHA KILIMO

 

39.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo kinatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuendelea kushirikiana na wahisani pamoja na serikali katika kutoa huduma za ushauri wa kilimo, utunzaji wa mali ya asili, misitu na ufugaji kwa wakulima na wafanyakazi.

 

·        kudahili wanafunzi 1,000 wa Shahada za Kwanza na wanafunzi 300 wa Shahada za Juu.

 

·        kuendeleza miradi ya utafiti kama ifuatavyo:

 

-         miradi inayojumuisha utafiti na mafunzo ya mbinu bora za kilimo kwa wakulima.

 

-         kushirikiana na vyuo vingine vya nchi zilizoendelea na zinazoendelea katika utafiti na kutoa taarifa za utafiti ndani na nje ya nchi.

 

·        kuendeleza miradi ya maendeleo kama ifuatavyo:

 

-         kuanza ujenzi wa mabweni 10 ya wanafunzi yenye uwezo wa kulaza wanafunzi 3,000.

 

-         kukamilisha uwekaji wa Mtandao wa Kompyuta (LAN) katika Kampasi ya Solomon Mahlangu.

 

-         kukarabati vyumba 25 na mtandao wa mabomba ya maji chuoni.

 

-         kuanza ujenzi wa vyumba viwili vya mihadhara vyenye uwezo wa wanafunzi 500 kila moja.

 

-         kuboresha mazingira ya sehemu wanamoishi wanafunzi na wafanyakazi.

 

-         kuboresha mazingira ya kusomea na kufundishia.

 

-         kukamilisha ujenzi wa maabara ya zoolojia.

 

-         kukamilisha upanuzi wa maktaba iliyopo Solomon Mahlangu ili kuongeza uwezo wa kuhudumia watumiaji kutoka 300 hadi 1,000.

 

-         kukamilisha ujenzi wa Kituo cha Ujasiriamali na Biashara

 

-          kukamilisha ujenzi wa Maabara ya Patholojia ya Mimea.

 

 

 

 

 

CHUO KIKUU KISHIRIKI CHA USHIRIKA NA STADI ZA BIASHARA

 

40.     Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Chuo Kikuu Kishiriki cha Ushirika na Stadi za Biashara - Moshi kinatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuboresha miundombinu kwa kuweka mtandao wa kisasa kwenye maktaba na kutengeneza upya mpango kabambe wa Chuo.

 

·        kuendeleza mafunzo ya walimu 10 ili wafikie kiwango cha Udaktari wa Falsafa.

 

·        kufanya tafiti ndogo 10 na kubwa 4.

 

·        kuchapisha makala: “3 Journals of Co-operative Business, 2 Research Report Series, 1 Research Abstract Series, 1 Manual”.

 

·        kuboresha kiwango cha huduma za uelekezi na ushauri.

 

·        kuongeza udahili wa wanafunzi kutoka 721 kufikia 1,500.

 

 

CHUO KIKUU HURIA CHA TANZANIA

 

41.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2005/06, Chuo Kikuu Huria cha Tanzania kinatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuongeza idadi ya wanafunzi waliodahiliwa kufikia 21,429 baada ya kuondoa waliohitimu ama kuondoka chuoni kwa sababu mbalimbali.

 

·        kuongeza uwiano wa idadi ya wanafunzi wa kike kutoka asilimia ishirini na saba ya sasa kufikia asilimia thelathini.

 

·        kuanzisha programu mbili mpya: Shahada ya Kwanza ya Sayansi ya Kompyuta (BSc. Computer Science); na Shahada ya Uzamili ya Sayansi za Mazingira (MSc. Environmental Studies);

 

·        kuimarisha ofisi za kanda ama kwa kununua majengo au kushawishi mikoa kukipatia Chuo majengo ya kudumu ili kupunguza mzigo wa kodi ya pango na kuweka mazingira mazuri ya kusoma;

 

·        kuimarisha matumizi ya mawasiliano ya kompyuta (ICT) ili kuboresha mafunzo, mawasiliano na kumiliki takwimu. Katika hili Chuo kinatarajia kufanya yafuatayo:

 

-         kujenga maabara ya pili ya kompyuta Makao Makuu;

 

-         kuimarisha matumizi ya kompyuta katika kuandaa nyaraka za taaluma (study materials), kumbukumbu za wanafunzi (Student records) na utawala;

 

-         kushirikiana na African Virtual University (AVU) kuanzisha kituo cha kuratibu na kuendesha mafunzo kwa walimu kwa kutumia mitandao ya mawasiliano ya kompyuta kama sehemu ya mpango wa NEPAD wa kuboresha taaluma za Waalimu wa Shule za Msingi na Sekondari nchini;

 

-         kufungua maabara za kompyuta na kuweka mtandao wa ndani (LAN) katika vituo vya mikoa kufikia 10 (kumi);

 

-         kuunganisha mtandao mpana (WAN) kati ya Makao Makuu na vituo vya mikoa 10;

 

-         kuwa na jukwaa la electroniki (electronic teaching and learning platform) la kuboresha kutoa na kupokea taaluma kutoka mbali;

 

-         kuongeza uzoefu na umahiri wa kutumia kompyuta kwa wafanyakazi na wanafunzi.

-         kuhamasisha uandishi wa vitabu vya masomo kwa kutumia wataalam wa hapa nchini;

 

·        kuboresha mazingira ya kazi na hasa ofisi za wafanyakazi Makao Makuu na katika mikoa;

 

·        kukamilisha kutengeneza mipango ya matumizi ya ardhi ya Chuo (land use plan).

 

 

CHUO KIKUU MZUMBE

 

42.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Chuo Kikuu Mzumbe kinatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuanza ujenzi wa mabweni yatakayoweza kuchukua wanachuo 1,000, ofisi za waalimu 100 na ukumbi mmoja wa mihadhara.

 

·        kuendeleza ujenzi wa maktaba mpya ya Chuo.

 

·        kuweka samani na kuanza masomo kwenye kampasi ya Dar es Salaam.

 

·        kukarabati, kuweka samani na kuanza masomo kwenye kampasi yake ya Mbeya.

 

·        kusomesha Walimu saba katika ngazi ya Udaktari wa Falsafa (PhD) na Walimu sita katika ngazi ya Uzamili.

 

·        kudahili wanafunzi wa Shahada ya Kwanza 893, kati ya hao 250 ni kwa udhamini wa serikali na 643, udhamini binafsi.

 

BARAZA LA ITHIBATI LA ELIMU YA JUU

 

43.   Mheshimiwa Spika, Baraza la Ithibati la Elimu ya Juu, katika mwaka wa fedha 2005/06 linatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuratibu na kusimamia mipango na taratibu mpya za kuanzisha, kusajili na kudhibiti vyuo vikuu, programu za masomo na udahili wa wanafunzi chini ya vyuo vikuu.

 

·        kukamilisha mpango mkakati (strategic plan) wa kutekeleza Sheria mpya ya Vyuo Vikuu iliyounda Kamisheni ya Vyuo Vikuu.

 

·        kuendesha semina kwa wakuu wa vyuo vikuu na taasisi zao kuhusu uongozi bora wa taasisi hizo.

 

·        kuandaa na kuratibu maonyesho (exhibition) ya vyuo vikuu.

 

·        kukamilisha mfumo wa tuzo kitaifa (National Qualifications Framework) kwa kushirikisha wadau wa ubora wa elimu na mafunzo nchini.

 

·        kukamilisha vigezo vya ubora (standards) wa majengo, vifaa na huduma katika vyuo vikuu na kuratibu uzingatiaji wa vigezo hivyo.

 

·        kuendelea kutoa machapisho ya kuelimisha umma kuhusu mipango na taratibu za kupata na kuthibiti ubora wa elimu katika vyuo vikuu.

 

·        kuanza ukarabati wa jengo la ofisi za kudumu za Baraza

 

·        kuendelea kuhamasisha wafanyakazi kuhusu ugonjwa hatari wa UKIMWI na magonjwa mengine pamoja na mapambano dhidi ya rushwa.

 

MAMLAKA YA ELIMU TANZANIA

 

44.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/06, Mamlaka ya Elimu Tanzania inatarajia kufanya yafuatayo:

 

·        kuendelea kuhamasisha na kuelimisha wadau kuchangia na kuwekeza kwenye miradi ya elimu na kupanua wigo wa uchangiaji katika Mfuko wa Elimu kwa kushirikisha wadau katika ngazi ya Wilaya. Aidha, Mamlaka itaendelea kuishauri serikali juu ya kupanua wigo wa vyanzo vya mapato ya Mfuko wa Elimu.

 

·        kuingia na kKuimarisha mashirikiano na Mifuko ya Elimu ya Halmashauri za Wilaya ili kuchochea uchangiaji.

 

·        kuendelea kutoa ruzuku na mikopo, kwa vyuo na shule kwa ajili ya miradi mbalimbali ya kuboresha elimu.

 

·        kuanzisha mashirikiano na jumuiya za wananchi, mashirika yasiyo ya kiserikali, mashirika ya dini na asasi mbalimbali katika kuhamasisha wadau kuchangia Mfuko wa Elimu na kushirikiana kugharamia miradi ya elimu nchini.

 

·        kuboresha ufanisi na utoaji huduma kwa kutekeleza mpango mkakati wa mwaka 2005/06 hadi 2009/10.

 

ELIMU YA UFUNDI

 

45.     Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/2006, Wizara yangu inakusudia kufanya yafuatayo:

       

·        kununua vitabu vya kiada na rejea kwa Chuo cha Ufundi Arusha.

 

·        kugharamia mafunzo maalum ya ualimu kwa walimu wahandisi watakaoajiriwa katika Chuo cha Ufundi Arusha.

 

·        kutoa mafunzo maalum kwa wasichana katika mpango maalum wa kujiunga na elimu ya ufundi katika Chuo cha Ufundi Arusha.

 

·        kukarabati majengo, mitambo na vifaa mbalimbali kwa Chuo cha Ufundi Arusha.

 

·        kugharamia mafunzo ya watumishi 9 wa Chuo cha Ufundi Arusha na Makao Makuu katika ngazi ya Udaktari wa Falsafa (3), Shahada ya Uzamili (1), Diploma ya Uzamili na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (5).

 

·        kukamilisha kuhuisha Sera ya Elimu ya Ufundi na Mafunzo.

 

·        kukifufua Chuo cha Tanesco Kidatu kuwa Chuo cha Ufundi Morogoro.

 

·        kuratibu matumizi ya mitaala mipya ya “National Technical Awards” (NTA 4-6) katika ngazi ya Ufundi Sanifu katika Vyuo na Taasisi za Ufundi.

 

TAASISI YA TEKNOLOJIA DAR ES SALAAM

 

46.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/2006, Taasisi ya Teknolojia Dar-es-Salaam inakusudia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kuanza mafunzo ya Uhandisi Migodi katika ngazi ya Ufundi Sanifu.

 

·        kuanza kutumia mitaala mipya inayozingatia umahiri na kutoa vyeti vya “National Technical Awards (NTA 4-6)” katika ngazi ya Ufundi Sanifu.

 

·        kuanza kutoa mafunzo ya Shahada ya Uhandisi wa Kompyuta (Bachelor of Engineering in Computer Engineering).

 

·        kukamilisha matayarisho ya mitaala na taratibu za kuanzisha  programu ya mafunzo ya Shahada ya Uzamili Juu ya Ukarabati (Maintenance Management).

 

·        kuendesha mashindano ya Ubunifu katika Fani ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano yaitwayo “Tanzania ICT Challenge Award” kwa msaada wa TCRA, SIDA na Kampuni ya Erickson ya Sweden.

 

·         kuendelea kuimarisha ushirikiano na nchi wahisani, Mashirika ya Kimataifa, Vyuo vya Elimu ya Juu na vya Ufundi vilivyo nchini na vya kimataifa sehemu mbalimbali kama ifuatavyo:

 

-         kuendeleza mkataba na serikali ya Watu wa China kwa kupeleka watumishi China kwa ajili ya mafunzo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

 

-         kuendesha kozi ya Shahada ya Uzamili “MSc. in Facilities Management” kwa ushirikiano na Chuo Kikuu cha Leeds Metropolitan (Uingereza) kwa udhamini wa Association of Commonwealth Universities.

 

-          kuendeleza mkataba na Shirika la Maendeleo la Sweden (SIDA) wa kukuza Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT).

 

-         kuendeleza mradi wa utafiti juu ya taka ngumu (Solid Waste Management) chini ya udhamini wa British Council.

 

-         kuendeleza ushirikiano na Cape University of Technology kwa kupitia mikutano kati ya vyuo husika na kubadilishana watumishi kwa muda mfupi.

 

-         kuendeleza ushirikiano na Vyuo vya Ufundi barani Afrika chini ya uratibu wa Commonwealth Association of Polytechnics in Africa (CAPA).

TAASISI YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA MBEYA

47.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/2006, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya inakusudia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kununua na kufunga mashine na mitambo kwa lengo la kuboresha mafunzo yatolewayo.

 

·        kugharamia mafunzo maalum ya ualimu kwa walimu wahandisi watakaoajiriwa.

 

·        kununua vitabu vya kiada na rejea.

 

·        kugharamia mafunzo ya watumishi 24 katika ngazi ya Udaktari wa Falsafa (6), Shahada ya Uzamili (10), Diploma ya Uzamili na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (8).

 

·        kuendeleza ushirikiano na Vyuo vya Ufundi barani Afrika chini ya uratibu wa “Commonwealth Association of Polytechnics in Africa” (CAPA).

TAASISI YA KUMBUKUMBU YA MWALIMU NYERERE

 

48.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2005/2006, Taasisi ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inakusudia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kukamilisha mitaala mitatu ya Shahada ya Kwanza katika fani za Sayansi Jamii, Jinsia katika Maendeleo na Maendeleo ya Uchumi.

 

·        kupata hadhi ya ithibati kamili kutoka Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi.

 

·        kudahili wanafunzi 250 katika kiwango cha Stashahada (210) na Cheti (40).

 

·        kuajiri wanataaluma 21 na watumishi wengine 20.

 

·        kukarabati jengo la utawala, madarasa 4 na maktaba 1.

 

·        kuanza kuendesha mafunzo katika tawi la Taasisi-Zanzibar.

BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI

 

49.   Mheshimiwa Spika, kwa mwaka wa fedha 2005/2006 Baraza linakusudia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kukagua na kutathmini kwa ajili ya ithibati uwezo wa uendeshaji na uhakiki wa ubora wa mafunzo katika taasisi 20 za ufundi;

 

·        kusajili vyuo 15 vyenye uwezo wa kutoa elimu na mafunzo ya  ufundi;

 

·        kuandaa, kukuza na kuidhinisha mitaala ya programu za mafunzo 30 yenye kuzingatia umahir na mahitaji ya soko la ajira.

 

·        kuweka viwango vya mafunzo (Setting Standards of Training Programmes) kwa ajili ya programu 20 za mafunzo;

 

·        kuratibu mitihani ya ufundi ya kitaifa katika ngazi ya Ufundi Sanifu (Full Technician Course) na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (Advanced Diploma in Engineering) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Mitihani (NECTA).

 

·        kusajili walimu wa ufundi na wataalamu wengine 1,000 katika vyuo vya ufundi;

 

·        kusimamia na kuhakiki ubora wa mafunzo (quality control and quality assurance) katika taasisi na vyuo vya ufundi;

 

·        kuweka mfumo wa uwekaji kumbukumbu za mitihani kwa njia ya kompyuta (examinations database) kwa ajili ya mitihani yote itakayotolewa na kuidhinishwa na Baraza kuhusiana na elimu na mafunzo ya ufundi.

 

·        kuimarisha ushirikiano na baadhi ya taasisi za ndani na nje zilizo na majukumu yanayofanana na ya Baraza hili.

 

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

 

50.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2005/2006, Wizara yangu inatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kuhuisha Sheria Na. 7 ya Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia.

 

·        kukamilisha mipango ya kuanzisha vituo vya sayansi (Science Parks).

 

·        kuanzisha Kituo cha Millenium Science Initiative (MSI).

 

·        kukamilisha mashirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Jamhuri ya Watu wa China kuhusu Mradi wa Nishati ya Jua utakaotekelezwa katika Kijiji cha Mwasayi, Wilayani Maswa.

 

·         kukamilisha uanzishwaji wa kamati za sayansi na teknolojia nchini.

 

·        kuanzisha Taasisi ya kujenga uwezo wa maarifa na kuendeleza sayansi na teknolojia nchini itakayojulikana kwa jina la Taasisi ya Nelson Mandela Arusha.

 

·        kuendelea na maandalizi ya kutunga Sera ya Taifa ya Utafiti.

 

·        kuandaa mikakati ya utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Bioteknolojia.

 

·        kuendelea na ufuatiliaji wa utekelezaji wa makubaliano na mikataba mbalimbali ya kikanda na Kimataifa katika Sayansi na Teknolojia mfano ni mkataba kati ya serikali ya Tanzania na Uswiss.

·        kuendelea kufuatilia utekelezaji wa miradi ya Sayansi na Teknolojia nchini (outreach projects).

 

·        kutoa mapendekekezo ya kuweka utaratibu wa kufuatilia na kutathmini utekelezaji wa mashirikiano na kutoa mapendekezo ya kuboresha.

 

·        kuendelea kuandaa mwongozo na kutunga sera ya wabunifu, wagunduzi na wavumbuzi.

 

·        kuendelea kuelimisha jamii kupitia Radio na Televisheni kuhusu sayansi na teknolojia.

 

·        kuendelea kutoa msukumo kwa wasichana wachukue masomo ya sayansi na teknolojia kwa kutoa zawadi na kuwalipia karo.

 

·        kuandaa nyaraka za kuridhia mikataba iliyo chini ya IAEA kama ifuatavyo:

 

-         Joint Convention on the Safety of Spent Fuel Management and on the Safety of Radioactive Waste Management.

 

-         African Nuclear Weapon Free (Pelindaba Treaty)

 

TUME YA TAIFA YA SAYANSI NA TEKNOLOJIA

51.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2005/2006, Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia itatekeleza yafuatayo:

 

·        kusambaza teknolojia ya matumizi ya makaa ya mawe yaliyoboreshwa kwa matumizi ya nyumbani kwa kushirikiana na Shirika la Viwanda Vidogo Vidogo (SIDO) na watu binafsi. 

 

·        kuhawilisha matumizi ya gesi ya samadi kwenye magereza pamoja na jiko bora la mkaa kwenye wilaya 6 za mikoa ya kati.

 

·        kuhawilisha teknolojia ya matumizi ya nishati ya jua na upepo kwa kuweka mtambo mmoja unaofanya kazi kutumia jua na upepo kwa pamoja huko Olduvai Gorge (Mary Leakey’s Camp).

 

·        kuhawilisha teknolojia ya ujenzi wa nyumba kwa gharama nafuu.

 

·        kuunganisha ugunduzi wa pampu inayoendeshwa kwa mkono na nishati ya upepo ya gharama nafuu, kwa ajili ya kuvuta maji kutoka visima virefu mkoani Iringa.

 

·        kusimamia ufufuaji upya wa chama cha wagunduzi (TAI) na Chama cha Walimu wa Sayansi Tanzania (STAURT).

 

·        kuimarisha asasi mpya ya mambo ya asilia.  LINKS – Local/Indigenous Knowledge System Trust.

 

·        kutoa mafunzo juu ya haki miliki na ubunifu kwa watafiti na wagunduzi.

 

·        kuendeleza masijala ya utafiti.

 

·        kuendelea kufadhili miradi ya utafiti na kutoa mafunzo kwa watafiti juu ya utayarishaji wa miradi ya utafiti.

 

·        kusambaza matokeo ya tafiti mbalimbali.

 

TUME YA NGUVU ZA ATOMIKI

52.   Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha wa 2005/2006, Tume ya Taifa ya Mionzi itatekeleza yafuatayo:

 

·        kufanya ukaguzi wa minara ya simu za mikononi, migodi na mazingira ili kubaini viwango vya mionzi na hali ya usalama.

 

·        kuendelea kutekeleza sheria ndogo ya kudhibiti viwango vya mionzi kwenye vyakula (Protection from Radiation, Control of Radiation Contaminated Foodstuffs Regulations, 1998) kwa kupima sampuli za vyakula viingiavyo na kutoka nje ya nchi.

 

·         kuratibu uanzishaji na usimamizi wa kituo cha kuthibiti majaribio ya silaha za nyuklia (Comprehensive Test Ban Treaty of Nuclear Weapons-CTBT). 

 

·        kuratibu misaada ya zaidi ya USD 900,000 kwa Taasisi nane (8) za Kitaifa kupitia miradi ya Kitaifa na Kikanda (Afrika) inayogharamiwa na Shirika la Kimataifa la Nguvu za Atomiki (IAEA). 

 

·        kutoa elimu ya kinga ya mionzi kwa wafanyakazi wanaohusika, na kuendelea na utafiti wa madhara ya mionzi kwa nia ya kubuni mbinu nzuri ya matumizi salama ya mionzi katika vituo vyote; na kutoa elimu ya kinga ya mionzi kwa umma kwa njia ya radio, televisheni na semina.

 

·         kutoa semina kwa Waheshimiwa Wabunge, wafanyakazi wa mionzi na umma kuhusu shughuli za Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (Tanzania Atomic Energy Commssion-TAEC) 

 

·        kuimarisha huduma za matengenezo ya vifaa vya elektroniki na mashine za x-ray.

 

·        kukamilisha mpango wa kushughulikia dharura za mionzi kitaifa (Radiological Emergency Plan and Preparedness) na usalama wa vyanzo vya mionzi (security of radioactive sources).

 

·        kuanzisha ofisi ndogo Zanzibar katika kutekeleza majukumu yanahusiana na Sheria ya Nguvu za Atomiki ya mwaka 2003 

MWELEKEO WA BAJETI YA MWAKA 2005/2006

 

53.   Mheshimiwa Spika, dira ya Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kufikia mwaka 2025, ni kujenga jamii iliyoelimika yenye uwiano wa kijinsia na inayoweza kujiletea maendeleo kwa kutumia sayansi na teknolojia. Ili kufanikisha azma yake, Wizara katika mwaka wa fedha 2005/2006 inatarajia kutekeleza yafuatayo:

 

·        kuratibu utekelezaji wa miradi inayoendelea na ile itakayoidhinishwa katika kipindi cha mwaka 2005/2006.

 

·        kuelimisha wanafunzi kuhusu nafasi za elimu ya juu nchini na nje ya nchi.

 

·        kuelimisha wadau kuhusu upatikanaji wa mikopo ya elimu ya juu kupitia Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Taasisi za Elimu ya Juu na Ufundi.

 

·        kutathmini na kuhuisha Sera ya Elimu ya Juu na kutoa mapendekezo ya kuboresha.

 

·        kuendeleza udhamini wa wanafunzi wa Shahada ya Kwanza ya Udaktari katika Vyuo Vikuu binafsi na wanafunzi wa udhamini binafsi katika Chuo Kikuu Kishiriki cha Sayansi za Afya Muhimbili.  Kwa mwaka 2005/06, Wizara itadhamini wanafunzi 424 (168 wa mwaka wa kwanza na 256 wanaoendelea).

 

·        kudhamini wafanyakazi na wanataaluma 209 katika Vyuo Vikuu kwa Shahada za Uzamili na Shahada za Juu za Falsafa.

 

·        kununua na kufunga mashine na mitambo katika Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya (MIST) kwa lengo la kuboresha mafunzo yatolewayo.

 

·        kugharamia mafunzo ya watumishi 27 wa Chuo cha Ufundi Arusha, Taasisi ya Sayansi na Teknolojia Mbeya na Makao Makuu katika ngazi ya Udaktari wa Falsafa (8), Shahada ya Uzamili (14), Diploma ya Uzamili na Stashahada ya Juu ya Uhandisi (5).

 

·        kuratibu utekelezaji wa miradi inayoendelea na ile itakayoidhinishwa na mkutano mkuu wa UNESCO Januari 2006.

 

·        kukamilisha mipango ya kuanzisha vituo vya sayansi (Science Parks)

 

·        kukamilisha uanzishwaji wa Kamati za Sayansi na Teknolojia nchini.

 

·        kuanzisha Taasisi ya kujenga uwezo wa maarifa na kuendeleza sayansi na teknolojia nchini itakayojulikana kwa jina la Taasisi ya Nelson Mandela Arusha.

 

·        kuanzisha Kituo cha Millenium Science Initiative (MSI).

 
MWISHO

 

54.   Mheshimiwa Spika, mwisho ningependa kutoa shukrani zangu za dhati kwa wahisani na wadau mbalimbali kwa mchango wao mkubwa wanaoutoa katika Wizara yangu.  Ni dhahiri kuwa msaada walioutoa na wanaoendelea kutoa hususan katika kuboresha sayansi na teknolojia, elimu ya juu na ufundi, katika vyuo na taasisi umesaidia kwa kiasi kikubwa kuchangia pale ambapo serikali imekuwa ikishindwa kutokana na ufinyu wa bajeti.  Nchi hizo ni pamoja na Norway, Sweden, Uholanzi, Japan, Ubeligiji, Canada, Jamhuri ya Korea, Jamhuri ya watu wa China, na Umoja wa Nchi za Ulaya. Aidha, mashirika ni pamoja na Benki ya Dunia, UNESCO na Shirika la Kimaendeleo la Sweden Sida/SAREC, Carnegie Foundation, DANIDA. Naomba waendelee na moyo huo nasi tunaahidi kuendeleza ushirikiano huu kikamilifu.

 

55.   Mheshimiwa Spika, ili kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza mipango iliyojiwekea katika mwaka wa fedha 2005/2006 sasa naliomba Bunge lako Tukufu liidhinishe jumla ya Sh. 138,058,526,400.  Kati ya fedha hizo, Sh. 111,113,449,700 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na Sh. 26,945,076,700 ni kwa matumizi ya maendeleo.

 

Mwisho kabisa, nachukua fursa hii kukushukuru wewe binafsi pamoja na Waheshimiwa Wabunge kwa kunisikiliza wakati nikiwasilisha hotuba yangu.

 

56.   Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja.


KIAMBATISHO NA. 1

 

 

 

 

 

FEDHA ZINAZOOMBWA KWA MATUMIZI YA KAWAIDA

FUNGU 68 MWAKA 2005/2006

 

KIFUNGU

IDARA

FEDHA ZILIZOIDHINISHWA MWAKA 2004/2005

FEDHA ZINAZOOMBWA MWAKA 2005/2006

1001

UTAWALA

1,204,284,612

1,590,470,900

1002

UHASIBU

108,049,900

191,184,800

1003

SERA NA MIPANGO

512,578,800

694,067,600

2001

TUME YA UNESCO

280,186,900

382,550,600

3001

ELIMU YA JUU

60,831,224,292

95,564,912,600

3002

ELIMU YA UFUNDI

6,168,151,400

9,936,457,000

3003

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

1,810,896,973

2,753,806,200

 

JUMLA

70,915,372,877

111,113,449,700


KIAMBATISHO NA. 2

 

 

 

       

FEDHA ZINAZOOMBWA KWA MATUMIZI YA MAENDELEO FUNGU 68 MWAKA 2005/2006

 

KIFUNGU

IDARA

FEDHA ZILIZOIDHINISHWA MWAKA 2004/2005

FEDHA ZINAZOOMBWA MWAKA 2005/2006

FEDHA ZA TANZANIA

FEDHA ZA NJE

FEDHA ZA TANZANIA

FEDHA ZA NJE

1001

UTAWALA NA UTUMISHI

 

256,000,000

 

256,000,000

1002

UHASIBU

 

 

 

 

1003

SERA NA MIPANGO

192,436,300

 

200,000,000

2,000,000,000

2001

UNESCO

 

 

 

 

3001

ELIMU YA JUU

1,300,000,000

11,582,014,500

8,901,000,000

13,893,451,700

3002

ELIMU YA UFUNDI

450,000,000

 

800,000,000

394,625,000

3003

SAYANSI NA TEKNOLOJIA

250,000,000

 

500,000,000

 

 

JUMLA NDOGO

2,192,436,300

11,838,014,500

10,401,000,000

16,544,076,700

 

JUMLA KUU

14,030,450,800.00

26,945,076,700

 

 


KIAMBATISHO NA 3 

 

 

 

 MAOMBI YA FEDHA FUNGU 68

 

KIFUNGU

IDARA

                 FEDHA ZA ZILIZOIDHINISHWA 2004/2005

FEDHA ZINAZOOMBWA 2005/2006

 

 

FEDHA

ZA

FEDHA ZA MAENDELEO

JUMLA KUU

FEDHA

ZA

  FEDHA ZA MAENDELEO

JUMLA KUU

 

 

KAWAIDA

FEDHA ZA TZ

FEDHA ZA  NJE

 

        KAWAIDA

FEDHA ZA TZ

FEDHA ZA NJE

 

1001

Utawala

1,204,284,612

 

256,000,000

1,460,284,612

1,590,470,900

 

256,000,000

1.846,470,900

1002

Uhasibu

108,049,900

 

 

108,049,900

191,184,800

 

 

191,184,800

1003

Sera na Mipango

512,578,800

192,436,300

 

705,015,100

694,067,600

200,000,000

2,000,000,000

2,894,067,600

2001

Tume ya UNESCO

280,186,900

 

 

280,186,900

382,550,600

 

 

382,550,600

3001

Elimu ya Juu

60,831,224,292

1,300,000,000

11,582,014,500

73,713,238,792

95,564,912,600

8,901,000,000

13,893,451,700

118,359,364,300

3002

Elimu ya Ufundi

6,168,151,400

450,000,000

 

6,618,151,400

9,936,457,000

800,000,000

394,625,000

11,131,082,000

3003

Sayansi na Teknolojia

1,810,896,973

250,000,000

 

2,060,896,973

2,753,806,200

500,000,000

 

3,253,806,200

JUMLA YA MAOMBI

70,915,372,877

2,192,436,300

11,838,014,500

84,945,823,677

111,113,449,700

10,401,000,000

16,544,076,700

138,058,526,400

FUNGU 68

 

84,945,823,677

 

 

138,058,526,400