HOTUBA YA
WAZIRI WA MIPANGO, UCHUMI NA
UWEZESHAJI MHE. DKT. JUMA NGASONGWA (MB), AKIWASILISHA BUNGENI
MUHTASARI WA HALI YA UCHUMI WA TAIFA KWA MWAKA 2005 NA MAPENDEKEZO YA
MPANGO WA MUDA WA KATI NA MFUMO WA MATUMIZI YA SERIKALI KWA KIPINDI CHA
MWAKA 2006/07–2008/09
UTANGULIZI
1.
Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako
Tukufu sasa likae kama kamati ili liweze kupokea na kujadili Taarifa ya Hali ya
Uchumi wa Taifa kwa
mwaka 2005 na mapendekezo ya Mpango wa Muda wa Kati na Mfumo wa Matumizi ya
Serikali kwa kipindi cha mwaka 2006/07–2008/09. Pamoja na hotuba hii nawasilisha kitabu cha Hali ya Uchumi wa
Taifa kwa mwaka 2005 na kitabu cha Mpango wa Maendeleo wa mwaka 2006/07.
2.
Mheshimiwa Spika, Awali ya yote napenda kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete pamoja na Makamu wake Dkt. Ali Mohamed
Shein kwa kuchaguliwa kwao kwa ushindi mkubwa wa kishindo. Aidha, ninapenda
kumpongeza Mhe. Amani Abeid Karume kwa kuchaguliwa kwake kwa kipindi cha pili
kuwa Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
3.
Aidha, napenda
kukupongeza wewe Mhe. Samwel John Sitta (Mb.) na Naibu wako Mhe. Anna Makinda
(Mb.) kwa kuchaguliwa kushika nyadhifa hizo za juu katika Bunge la Awamu ya
Nne. Nawapongeza pia Mawaziri wenzangu wote pamoja na Naibu Mawaziri wote kwa
kuteuliwa kwao na Mhe. Rais. Mwisho napenda niwapongeze wabunge wote kwa
kuchaguliwa au kuteuliwa kwao kuingia katika Bunge hili Tukufu. Aidha,
nawashukuru kipekee wapiga kura wangu wa Jimbo la Ulanga Magharibi kwa
kunichagua kwa mara ya tatu kuwa mbunge wao.
Tutaendelea kushirikiana katika kuliletea maendeleo jimbo letu.
4.
Mheshimiwa Spika, Napenda kutoa shukurani zangu za dhati kwa Kamati ya Bunge ya Fedha na
Uchumi ikiongozwa na Mwenyekiti wake Mhe. Dkt. Abdallah Omari Kigoda (Mb), kwa kutupatia ushauri na maelekezo
wakati wa kujadili muhtasari wa hotuba hii. Aidha, ninawashukuru wale wote
tulioshirikiana nao katika maandalizi ya Taarifa hii na Mpango ninaouwasilisha
leo.
5.
Mheshimiwa Spika, Baada ya kusema hayo, sasa naomba nianze kutoa muhtasari wa mapitio ya
hali ya uchumi na maendeleo kwa mwaka 2005, ikiwa ni mapitio ya mwaka wa kwanza
wa utekelezaji wa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania
(MKUKUTA) wenye mwelekeo na azma ya kutufikisha kwenye malengo ya jumla ya Dira
ya Taifa ya Maendeleo 2025. Kwa kipindi cha mwaka 2005/06, bajeti iliendelea
kujikita zaidi katika kuendeleza mageuzi ya kiuchumi na kijamii yaliyolenga
katika kukuza na kutengemaza uchumi, kwa kutekeleza sera, mipango, programu na
mikakati mbali mbali ya kuharakisha maendeleo ya kiuchumi na kijamii ya Taifa
letu. Aidha, ikumbukwe kwamba taarifa hii ni ya kipindi cha kuanzia Januari
hadi Desemba 2005 na sehemu chache zimegusia robo ya kwanza ya mwaka 2006.
MAPITIO YA HALI
YA UCHUMI JUMLA
Pato la Taifa
6.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, Pato la Taifa lilikua kwa asilimia 6.8[1] ikilinganishwa na lengo la ukuaji wa asilimia 6.9, na
ukuaji halisi wa asilimia 6.7 mwaka 2004. Ukuaji huu ulichangiwa zaidi na
ukuaji wa sekta za uuzaji wa jumla, rejareja na mahoteli, ikijumuisha utalii;
bidhaa za viwandani; ujenzi; madini na uchimbaji mawe na mawasiliano na
uchukuzi. Vile vile, mchango mwingine ulitokana na ongezeko la viwango vya
ukuaji wa sekta za umeme na maji; huduma za kibiashara na fedha; na uendeshaji
wa serikali na huduma nyingine. Pamoja na mambo mengine, ukuaji huu haukufikia
lengo kutokana na ukame uliotokea katika maeneo mengi nchini, hasa katika
kipindi cha robo ya nne ya mwaka 2005.
7.
Mheshimiwa Spika, Pato la wastani kwa kila mtu
liliongezeka hadi sh. 360,865 mwaka 2005 kutoka sh. 319,754 mwaka 2004 kwa bei
za miaka husika, sawa na ongezeko la asilimia 12.9. Aidha, kwa bei za mwaka 1992, wastani ulikuwa
sh. 61,798 mwaka 2005 ikilinganishwa na sh. 59,335 mwaka 2004, sawa na ongezeko
la asilimia 4.2.
8.
Mheshimiwa Spika, Mchango wa sekta ya kilimo katika Pato
la Taifa uliendelea kupungua kidogo kidogo ambapo mchango wa sekta nyingine
hasa bidhaa za viwandani; uuzaji wa jumla, reja reja na mahoteli, ikijumuisha
utalii; madini; na ujenzi uliendelea kuongezeka. Hali hii inaonyesha kubadilika
kwa muundo wa uchumi ambao sasa hautegemei kuchangiwa kwa kiasi kikubwa na
kilimo pekee. Hata hivyo, mchango wa sekta ya kilimo katika Pato la Taifa
uliendelea kuwa mkubwa ikilinganishwa na sekta nyingine. Katika mwaka 2005, sekta ya kilimo ilichangia asilimia 45.6 ya Pato la
Taifa ikilinganishwa na asilimia 46.3 mwaka 2004.
9.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, sekta ya kilimo
ilikua kwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.8 mwaka 2004. Kupungua kwa
ukuaji wa sekta hii kulitokana hasa na kushuka kwa uzalishaji katika sekta
ndogo za mazao na mifugo. Ukuaji wa sekta hizi ndogo ulishuka kutoka asilimia
6.0 na 4.8 mwaka 2004 hadi asilimia 5.2
na 4.2 mwaka 2005 kwa mtiririko huo. Hata hivyo, viwango vya ukuaji vya sekta
ndogo za uvuvi; na misitu na uwindaji viliongezeka kutoka asilimia 6.7 na 3.8
mwaka 2004 hadi asilimia 7.3 na 4.5 mwaka 2005, kwa mtiririko huo.
10.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya bidhaa za viwandani ilikua kwa
asilimia 9.0 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 8.6 mwaka 2004. Ukuaji huo
ulitokana na kuongezeka kwa uzalishaji bidhaa katika baadhi ya viwanda hususan
saruji, aluminiamu na bati. Mchango wa sekta ya uzalishaji bidhaa viwandani
uliongezeka hadi kufikia asilimia 9.0 mwaka 2005 kutoka asilimia 8.8 mwaka
2004.
11.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya mahoteli, uuzaji jumla na reja
reja ikijumuisha utalii, ilikua kwa asilimia 8.2 mwaka 2005, ikilinganishwa na
asilimia 7.8 mwaka 2004. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa ulikuwa
asilimia 17.2 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 16.9 mwaka 2004.
12.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya madini na uchimbaji mawe ilikua
kwa asilimia 15.7 mwaka 2005, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 15.4 mwaka
2004. Kuongezeka kwa ukuaji wa sekta hii kulitokana hasa na uwekezaji mpya
katika machimbo ya dhahabu ya Tulawaka yaliyoko wilaya ya Biharamulo. Mchango
wa sekta ya madini na uchimbaji mawe katika Pato la Taifa uliongezeka hadi
asilimia 3.5 mwaka 2005 kutoka asilimia 3.2 mwaka 2004.
13.
Mheshimiwa Spika, Mchango wa sekta ya ujenzi katika Pato
la Taifa ulikuwa asilimia 5.7 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 5.4 mwaka
2004. Sekta ilikua kwa asilimia 11.9 mwaka 2005, kutoka asilimia 10.8 mwaka
2004. Ukuaji huu ulitokana hasa na
ujenzi wa majengo yasiyo ya kuishi na nyumba za kuishi, ujenzi wa barabara na
madaraja, pamoja na uendelezaji wa ardhi.
14.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya mawasiliano na uchukuzi
ilikua kwa asilimia 6.4 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 6.0 mwaka 2004.
Ukuaji huu ulitokana na kuboreshwa kwa miundombinu ya usafirishaji na
kuongezeka kwa huduma za mawasiliano hasa kwa njia ya simu. Hata hivyo, mchango
wa sekta ya mawasiliano na uchukuzi katika Pato la Taifa ulibakia kuwa asilimia
5.4 mwaka 2005 kama ilivyokuwa mwaka 2004.
15.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya umeme na maji ilikua kwa
asilimia 5.1 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 4.5 mwaka 2004. Kuongezeka
kwa ukuaji huu kulitokana na kukua kwa sekta ndogo za umeme na maji kutoka
asilimia 4.7 na 2.8 mwaka 2004 hadi asilimia 5.3 na 3.4 mwaka 2005 kwa mtiririko
huo. Mchango wa sekta ya umeme na maji katika Pato la Taifa ulibakia kuwa
asilimia 1.6 kama ilivyokuwa mwaka 2004.
16.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya huduma za fedha na kibiashara
ilikua kwa asilimia 5.3 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 4.4 mwaka 2004.
Ukuaji huu ulitokana na kuongezeka katika ukuaji wa sekta ndogo za fedha na
bima, upangishaji majengo na huduma za kibiashara wa asilimia 5.7, 5.0 na 6.1
mwaka 2005, ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 4.4, 4.3 na 5.5 mwaka 2004,
kwa mtiririko huo. Sekta hii
ilichangia asilimia 9.6 katika Pato la Taifa mwaka 2005, ikilinganishwa na
asilimia 9.7 mwaka 2004.
17.
Mheshimiwa Spika, Sekta ya uendeshaji serikali na huduma nyingine
ilikua kwa asilimia 5.1 mwaka 2005, kutoka asilimia 4.3 mwaka 2004. Ukuaji huu
ulichangiwa na sekta ndogo ya utawala kwa asilimia 4.7 mwaka 2005, kutoka
asilimia 2.8 mwaka 2004. Sekta ndogo za elimu, afya na huduma nyinginezo
zilikua kwa asilimia 6.3, 5.7 na 4.9, viwango ambavyo ni pungufu ya vile
vilivyofikiwa katika mwaka 2004 vya asilimia 6.6, 6.0 na 5.8, kwa mtiririko
huo. Mchango wa sekta ya uendeshaji serikali na huduma nyingine katika Pato la
Taifa ulikuwa asilimia 7.0 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka
2004.
Kasi ya Upandaji
Bei
18.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, wastani wa kasi ya upandaji bei ulikuwa asilimia 4.3
ikilinganishwa na lengo la asilimia 4.0 na kasi halisi ya asilimia 4.2 mwaka
2004. Kuongezeka kwa kasi ya upandaji bei kulitokana na kupanda kwa bei ya
bidhaa za chakula kutokana na hali ya ukame na kupanda kwa wastani wa bei za
bidhaa za mafuta ya petroli zilizosababisha kuongezeka kwa gharama za
usafirishaji na umeme. Aidha kwa mwezi Machi 2006 kasi ya upandaji bei ilifikia
asilimia 6.9 kupanda huku kulitokana na ukame uliopandisha bei ya vyakula na gharama
za umeme.
BAJETI YA
SERIKALI
Mapato
19.
Mheshimiwa Spika, Katika nusu ya
kwanza ya mwaka 2005/06, mapato ya ndani yalifikia sh. 1,013.8 bilioni,
ikilinganishwa na sh. 869.9 bilioni katika kipindi
Matumizi
20.
Mheshimiwa Spika, Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2005/06, matumizi yalifikia sh. 2,122.9
bilioni, ikilinganishwa na sh. 1,641.3 bilioni katika kipindi
Ujazi wa Fedha na Karadha
21.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, ujazi wa fedha kwa tafsiri pana (M2)
uliongezeka kwa asilimia 36.2, ikilinganishwa na asilimia 19.2 mwaka 2004,
ambapo ujazi wa fedha kwa tafsiri pana zaidi (M3)[2]
uliongezeka kwa asilimia 38.2 mwaka ulioshia Desemba 2005, kutoka asilimia 19.3
Desemba 2004. Ongezeko
Ukuzaji Rasilimali
22.
Mheshimiwa Spika, Ukuzaji rasilimali uliongezeka kufikia sh. 735,180 milioni mwaka 2005
kutoka sh. 624,371 milioni mwaka 2004 kwa bei za mwaka 1992, sawa na ongezeko
la asilimia 17.7. Ukuzaji rasilimali kwa bei za miaka husika uliongezeka kutoka
sh. 2,598,974 milioni mwaka 2004 hadi sh. 3,149,402 milioni mwaka 2005 sawa na
ongezeko la asilimia 21.2. Kuongezeka kwa ukuzaji rasilimali kulitokana hasa na
ujenzi wa majengo; uagizaji wa vifaa; na kuongezeka kwa shughuli nyinginezo za
ukuzaji rasilimali zikiwemo uendelezaji ardhi, barabara na madaraja, pamoja na
maji. Aidha, uwiano wa ukuzaji rasilimali na Pato la Taifa ulikuwa asilimia
32.9 ikilinganishwa na asilimia 29.8 mwaka 2004, kwa bei za mwaka 1992.
23.
Mheshimiwa Spika, Mchango wa sekta binafsi katika ukuzaji
rasilimali ulikuwa asilimia 65.1 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia 62.4
mwaka 2004. Kwa upande wa sekta ya umma, ukuzaji rasilimali uliongezeka hadi
sh. 1,068,171 milioni kutoka sh. 950,077 milioni mwaka 2004 kwa bei za miaka
husika, sawa na ongezeko la asilimia 12.4. Mchango wa sekta ya umma katika
ukuzaji rasilimali kwa jumla ulikuwa asilimia 33.9 mwaka 2005, ikilinganishwa
na asilimia 36.6 mwaka 2004.
Mikopo Kutoka Benki za Biashara kwa Sekta Mbalimbali
24.
Mheshimiwa Spika, Mikopo iliyotolewa na benki za
biashara kwa sekta mbalimbali iliongezeka kutoka sh. 965,985.9 milioni mwaka
2003/04 hadi sh.1,219,305.6 milioni mwaka 2004/05, sawa na ongezeko la asilimia
26.2. Kufikia mwishoni mwa Desemba 2005, mikopo kwa sekta binafsi iliongezeka
hadi sh. 1,425,062.3 milioni ikilinganishwa na sh. 1,060,077.3 milioni mwishoni
mwa Desemba 2004. Ongezeko hilo ni sawa na asilimia 34.4 ikilinganishwa na
asilimia 30.0 mwishoni mwa Desemba 2004.
Mauzo na Uagizaji Bidhaa Nje
25.
Mheshimiwa Spika, Thamani ya mauzo ya bidhaa nje
iliongezeka kufikia dola za Kimarekani 1,676.3 milioni mwaka 2005 kutoka dola
za Kimarekani 1,473.1 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 13.8.
Thamani ya mauzo ya bidhaa asilia iliongezeka na kufikia dola za Kimarekani
354.4 milioni mwaka 2005 kutoka dola za Kimarekani 297.8 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la
asilimia 19.0. Ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka kwa mauzo ya mazao ya
kahawa, tumbaku na pamba. Thamani ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia iliongezeka
na kufikia dola za Kimarekani 1,321.8 milioni mwaka 2005 kutoka dola za
Kimarekani 1,175.3 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 12.5. Bidhaa zisizo asilia zilichangia asilimia 78.8 ya mauzo
yote, wakati bidhaa asilia zilichangia asilimia 21.2. Pamoja na mafanikio hayo,
mapato yatokanayo na mauzo nje yamekuwa na uwezo wa kugharamia asilimia 63.0 tu
ya uagizaji nje. Changamoto iliyopo ni kuongeza mauzo nje na kuhamasisha
uzalishaji na uuzaji wa bidhaa zenye viwango vya kuweza kuhimili ushindani
26.
Mheshimiwa Spika, Thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka
nje (f.o.b) iliongezeka kutoka dola za Kimarekani 2,339.7 milioni mwaka
2004, hadi dola za Kimarekani 2,661.8 milioni mwaka 2005 sawa na ongezeko la
asilimia 13.8. Thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ilikuwa kubwa kuliko
thamani ya bidhaa zilizouzwa nje na hivyo kuleta nakisi kubwa katika urari wa
biashara ya bidhaa. Thamani ya bidhaa za matumizi ya kawaida ilipungua kwa
asilimia 1.8 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa mazao ya chakula hususan
mahindi. Uagizaji wa bidhaa nyingine za matumizi ya kawaida uliongezeka kutoka
dola za Kimarekani 515.9 milioni mwaka 2004 hadi dola za Kimarekani 583.0
milioni mwaka 2005 sawa na ongezeko la asilimia 13.0.
27.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, urari wa malipo
yote ulikuwa na nakisi ya dola za Kimarekani 437.5 milioni ikilinganishwa na
ziada ya dola za Kimarekani 43.4 milioni mwaka 2004. Nakisi hii ilitokana na
kuongezeka kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa, ambapo mwaka 2005, urari
wa biashara ya bidhaa ulikuwa na nakisi ya dola za Kimarekani 985.5, sawa na
asilimia 13.7, ikilinganishwa na nakisi ya dola za Kimarekani 866.6 mwaka 2004.
Akiba ya Fedha za Kigeni
28.
Mheshimiwa Spika, Akiba ya fedha za kigeni ilipungua hadi dola za Kimarekani 2,048.4
milioni mwaka 2005, kutoka dola za Kimarekani 2,296.1 milioni mwaka 2004, sawa
na upungufu wa asilimia 10.8. Kiasi cha akiba ya fedha za kigeni mwaka 2005,
kilikuwa na uwezo wa kuagiza bidhaa na kulipia huduma miezi 6.4 ikilinganishwa
na kiasi cha mwaka 2004 kilichokuwa na uwezo wa miezi 8.2. Kiasi hiki ni chini
ya lengo lilokusudiwa la uwezo wa kuagiza bidhaa na kulipia huduma kwa zaidi ya
miezi 7.
Thamani ya Shilingi
29.
Mheshimiwa Spika, Thamani ya shilingi imeendelea kufuata mabadiliko ya hali ya soko.
Mwaka 2005, thamani ya shilingi ya
Misaada na Mikopo ya Nje
30.
Mheshimiwa Spika, Misaada na mikopo imeendelea
kupatikana kwa kiwango cha kuridhisha kutokana na kwamba wahisani wengi
wameonyesha kuitikia mwito wa kuisaidia nchi yetu katika kutekeleza Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza
Umasikini. Misaada na mikopo ya bajeti ya kawaida ilifikia sh. 576,956
milioni mwezi Machi 2006 ikilinganishwa na makadirio ya sh. 589,913
milioni,sawa na asilimia 97.8. Pungufu hiyo ilitokana na baadhi ya nchi
wahisani pamoja na Benki ya Dunia kupunguza misaada na mikopo pamoja na wengine
kuchelewesha utoaji wa misaada na mikopo yao hasa ile ya ‘‘Basket Funding’’. Hata
hivyo idadi kubwa ya wahisani walitoa misaada waliyoahidi. Kwa upande wa
misaada na mikopo kwa ajili ya bajeti ya maendeleo, sh. 731,711 milioni, zilipatikana
ikilinganishwa na sh. 783,467 milioni zilizoahidiwa sawa na asilimia 80.7.
Deni la Taifa
31.
Mheshimiwa Spika, Hadi Desemba 2005, deni la Taifa lilifikia dola za Kimarekani 9,961.3[3]
milioni ikilinganishwa na dola za Kimarekani 9,726.9 milioni, Desemba 2004,
sawa na ongezeko la asilimia 2.4. Kati
ya deni
32.
Pamoja na kuzingatia tahadhari ya mzigo wa madeni, hatuwezi
kusita kukopa mikopo nafuu na stahimilivu, ambayo itaelekezwa katika kuchangia
kujenga uwezo wa uchumi na kuongeza uwekezaji hatimaye kuibua ongezeko la
ajira, mauzo nje, mapato ya serikali, kuboresha miundombinu, na maendeleo ya
rasilimali watu.
33.
Mheshimiwa Spika, Ulipaji wa deni la nje uliongezeka kutoka dola za Kimarekani 77.8
milioni mwaka 2004 hadi dola za Kimarekani 91.1 milioni mwaka 2005. Deni
Deni la Ndani
34.
Mheshimiwa Spika, Hadi Desemba 2005, deni la ndani lilifikia sh. 2,362.5 bilioni, ikilinganishwa
na deni la sh. 1,813.1 bilioni, katika kipindi kama hicho mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 30.3.
Ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka kwa matumizi ya serikali. Kiasi cha sh. 716.8 bilioni za deni la ndani
zililipwa katika mwaka 2005. Kati ya fedha hizo, sh. 616.4 bilioni zilikuwa ni
mkopo na sh. 100.4 bilioni ilikuwa ni riba.
HALI YA UCHUMI DUNIANI NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
Hali ya Uchumi
Duniani
35.
Mheshimiwa Spika, Pato la dunia lilikua kwa asilimia 4.8 mwaka 2005, ikilinganishwa na asilimia
5.3 mwaka 2004. Kushuka kwa ukuaji wa pato la dunia kulichangiwa kwa kiasi
kikubwa na kuyumba kwa uchumi wa nchi zilizoendelea hasa katika Bara la Ulaya
hususan Ufaransa, Ujerumani, Italia na Uingereza; pamoja na ongezeko kubwa la
bei ya mafuta na majanga mbali mbali yaliyoikumba dunia. Pamoja na kushuka kwa
kasi ya ukuaji wa uchumi wa dunia, baadhi ya nchi za Asia zinazochipukia
kiviwanda zilikuwa na ukuaji wa haraka wa uchumi, kwa mfano ukuaji wa uchumi wa
China ulifikia asilimia 9.9 mwaka 2005.
36.
Mheshimiwa Spika, Pato la nchi zilizoendelea lilikua kwa asilimia 2.7 mwaka 2005,
ikilinganishwa na asilimia 3.4 mwaka 2004. Kushuka kwa ukuaji wa pato la nchi
zilizoendelea kulichangiwa hasa na kupanda kwa bei za mafuta na kupungua kwa
mauzo nje. Kwa upande wa nchi zinazoendelea na nchi za Asia zinazoinukia
kiviwanda wastani wa pato lilipungua hadi asilimia 7.2 na 8.6 kwa mwaka 2005
ikilinganishwa na asilimia 7.6 na 8.8 mwaka 2004, kwa mtiririko huo. Ukuaji wa
pato la nchi zinazoendelea, ikilinganishwa na ukuaji wa pato la dunia,
umeendelea kuimarika kutokana na kukua kwa biashara na shughuli za uzalishaji
viwandani na utekelezaji mzuri wa sera za kurekebisha uchumi.
37.
Mheshimiwa Spika, Pato la nchi za Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara lilikua kwa wastani
wa asilimia 5.5 mwaka 2005, ikilinganishwa na wastani wa asilimia 5.6 mwaka
2004. Mwaka 2005, ukuaji wa pato la Bara la Afrika ulishuka hadi wastani wa
asilimia 5.2 kutoka wastani wa asilimia 5.5 mwaka 2004. Ukuaji wa pato la Bara
la Afrika ulitokana na kuongezeka kwa mauzo ya mafuta, madini na ongezeko la
bei kwa baadhi ya bidhaa za kilimo. Aidha, utekelezaji wa sera na mageuzi ya
kiuchumi kwa baadhi ya nchi barani Afrika kulichangia katika ukuaji huo. Hata
hivyo, ukuaji ulipungua kutokana na matatizo ya ukame na migogoro ya kisiasa
iliyozikumba baadhi ya nchi za Kiafrika.
38.
Mheshimiwa Spika, Kwa nchi za maziwa makuu ikiwemo
39.
Hivyo, ukuaji
waasilimia 6.8 wa pato la taifa letu kwa mwaka 2005 ni hatua nzuri zaidi siyo
tu katika kanda hii ya Afrika Mashariki na kati, bali pia katika Kanda yote ya
Afrika Kusini mwa Jangwa la
USHIRIKIANO WA KIKANDA NA KIMATAIFA
40.
Mheshimiwa Spika, Uhusiano wa nchi yetu na mataifa mengine duniani pamoja na mashirika ya
kimataifa na ushirikiano wa kikanda umeendelea kuimarika kwa kiwango kikubwa na
hivyo kuendelea kulijengea Taifa letu mazingira mazuri ya shughuli za kiuchumi
na kijamii.
Jumuiya ya Afrika Mashariki
41.
Mheshimiwa Spika, Itifaki ya Ushuru wa Pamoja wa Forodha
kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki ilianza kutumika tarehe 1 Januari 2005 baada ya kusainiwa na Marais wa nchi
wanachama wa Jumuiya na kuridhiwa na Mabunge ya nchi hizo. Aidha, Jumuiya
iliendelea kuandaa Mkakati wa Maendeleo wa Miaka Mitano. Mkakati huo unafuatia
kukamilika kwa kipindi cha mkakati wa awali wa mwaka 2001-2005 ambao kwa kiasi
kikubwa ulifanikisha kuanzishwa kwa Ushirikiano wa Ushuru wa Pamoja wa Forodha,
pamoja na kuweka misingi ya kuanzishwa kwa Soko la Pamoja la Afrika ya
Mashariki.
42.
Mheshimiwa Spika, Kwa upande wa miradi ya maendeleo,
Jumuiya iliendelea kutekeleza shughuli za Mamlaka ya Uendelezaji wa Bonde la
Ziwa Victoria kama ifuatavyo; mradi wa Ushirikiano wa Uvuvi katika Ziwa
Victoria; matayarisho ya miradi ya miundombinu ikijumuisha barabara, reli,
usafiri wa majini, uzalishaji na usambazaji wa nishati; na miradi ya kilimo.
Aidha, katika kutimiza azma ya kuwa na majengo ya kudumu, maandalizi ya ujenzi
wa makao makuu ya Jumuiya yalifikia hatua nzuri baada ya Tanzania kutoa eneo,
pamoja na mshauri mwelekezi wa ujenzi kupatikana.
43.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, mkutano wa Kamati
ya Mawaziri wa Mkutano wa Kimataifa kuhusu Eneo la Maziwa Makuu ulifanyika
Lusaka Zambia chini ya uenyekiti wa Tanzania. Mkutano huo ulijadili itifaki ya
mpango na programu za muda mfupi, kati na mrefu na kupitisha miradi
inayokusudiwa kutekelezwa kwenye maeneo makubwa manne yafuatayo ni: Amani na
Usalama; Demokrasia na Utawala Bora; Maendeleo ya kiuchumi na ushirikiano
kikanda; na Haki za Binadamu na Masuala ya Kijamii. Aidha, katika mkutano huo
nchi ya Misri ilikubaliwa kuwa mwanachama wa nchi za eneo la Maziwa Makuu.
Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)
44.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, SADC ilifikisha miaka 25 tangu kuanzishwa
kwake. Mambo yaliyofanyika katika kipindi cha 2005/06 ni pamoja na: kupitisha
azimio la kuongeza lengo la chini la
ushiriki wa wanawake katika maamuzi ya kisiasa na uongozi wa ngazi za
juu kutoka asilimia 30 hadi asilimia 50 ifikapo mwaka 2010 ikiwa ni sambamba na
malengo ya Jumuiya ya Afrika; kupitisha uamuzi wa kujenga Makao Makuu ya SADC Gaborone, Botswana katika kipindi cha
miaka kumi na mitano; na kukubaliana juu ya taratibu zinazohusu utatuzi wa
migogoro ya kibiashara kwa lengo la kurekebisha na kuboresha itifaki ya
biashara ya SADC.
45.
Aidha, taratibu za kuunganisha njia za umeme kati ya Tanzania na Zambia
(Zambia–Tanzania Inter connector) ziliendelea kukamilishwa na
Sekretariati ya SADC baada ya fedha za kutekeleza mradi kupatikana ili
Tanzania iweze kuunganishwa rasmi kwenye mradi wa “Southern African Power
Pool (SAPP)” kama nchi nyingine za SADC.
Mpango Mpya wa
Ushirikiano Ili Kuleta Maendeleo Afrika (NEPAD)
46.
Mheshimiwa Spika, Serikali ilitoa mwaliko kwa
sekretariati ya African Peer Review Mechanism (APRM) kuja nchini
kuhakiki ni kwa jinsi gani Tanzania inatekeleza makubaliano yaliyofikiwa chini
ya NEPAD ambayo yanajumuisha utawala wa sheria, haki za binadamu, uhuru
wa vyombo vya habari, uhuru wa vyama vya siasa, mageuzi katika uchumi yenye
kulenga katika ukuaji wa uchumi na kupunguza umaskini na kuendeleza ushirikiano
kati ya serikali na sekta binafsi. Haya ni matokeo ya mkataba wa kujiunga na
utaratibu unaotoa fursa kwa nchi kujitathmini na kujipima zenyewe kuhusiana na
utekelezaji wa vigezo muhimu vya NEPAD, ulioridhiwa na Bunge la Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania Februari, 2005.
47.
Mheshimiwa Spika, Kufuatia mageuzi ya kiuchumi
yanayoendelea hapa nchini kama ilivyoainishwa kwenye Dira ya Maendeleo ya Taifa
2025, serikali iliwasilisha miradi ifuatayo kwa sekretariati ya NEPAD:
Ujenzi wa daraja la Umoja linalounganisha nchi za Tanzania na Msumbiji, upanuzi
wa bandari ya Dar es salaam, uunganishaji wa umeme kutoka Zambia hadi Kenya,
maendeleo ya ukanda wa Mtwara na uboreshaji wa barabara za Jumuiya ya Afrika ya
Mashariki.
Ushirikiano wa Kiufundi Baina ya Nchi
Zinazoendelea
48.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005 Tanzania iliendelea
kutumia fursa mbali mbali zilizotolewa na Serikali ya China chini ya mpango wa
ushirikiano kwa nchi zinazoendelea zinazosaidiwa na Shirika la Maendeleo la
Umoja wa Mataifa. Wataalam wa Kitanzania kutoka Wizara na Taasisi mbali mbali
walihudhuria mafunzo ya Uvunaji wa Maji ya Mvua, Nishati Mbadala na
Televisheni nchini China.
MAENDELEO YA SEKTA
Kilimo
49.
Mheshimiwa Spika, Mwaka 2005/06, uzalishaji wa mazao ya
chakula ulipungua kwa baadhi ya mazao yakiwemo: ngano, mahindi, mtama na
ndizi. Uzalishaji uliongezeka kwa mazao
mengine kama muhogo, kunde na mpunga. Kwa upande wa mazao ya biashara
uzalishaji uliongezeka kwa mazao ya pareto, tumbaku na pamba, wakati ambapo
uzalishaji wa kahawa na korosho ulipungua. Aidha, eneo lililo chini ya kilimo
cha umwagiliaji lilipungua kutoka hekta 23,970 mwaka 2004, hadi hekta 22,506,
mwaka 2005. Kupungua kwa uzalishaji kwa baadhi ya mazao kulitokana na ukame, huduma
duni za ughani, na hali ya bei za mazao kwa wakulima ambazo hazitabiriki. Hivyo
kuanzia sasa suala la kilimo cha umwagiliaji kama sehemu ya Mkakati wa
Mapinduzi ya kilimo nchini kitapewa msukumo zaidi.
50.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, mkazo katika
sekta ya kilimo utakuwa ni pamoja na: kuendelea kuboresha upatikanaji wa
chakula cha kutosha; kupanua kilimo cha umwagiliaji; na kuongeza Hifadhi ya
Taifa ya Chakula.
Viwanda
51.
Mheshimiwa Spika, Mwaka 2005/06, mafanikio ya kuridhisha yalipatikana katika sekta ya
viwanda yakiwemo kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa kulingana na mahitaji ya
soko la ndani na nje. Viwanda vya
usindikaji wa mazao ya kilimo cha chakula vilihamasika na kuanza kutumia
teknolojia sahihi za uzalishaji na usindikaji wa bidhaa mbali mbali kama
matumizi ya teknolojia ya ‘‘biogas’’,
teknolojia ya kukausha tumbaku kwa usalama zaidi, usindikaji wa mafuta ya
kupikia na teknolojia ya kusafisha chumvi katika kiwango cha mataifa; na
kuimarishwa kwa maabara ya upimaji ubora wa vyakula za Shirika la Viwango
Tanzania (TBS).
52.
Aidha, katika
kuhamasisha uwekezaji katika ujenzi wa maeneo mapya ya kuzalisha bidhaa kwa
ajili ya mauzo nje (EPZ), viwanda viwili vilianzishwa na kuanza
uzalishaji. Viwanda hivyo ni A-Z
kilichopo Kisongo-Arusha, kinachozalisha vyandarua vyenye dawa na Kiwanda cha African
Packaging System kilichopo “Millenium Business Park”
53.
Mheshimiwa Spika, Mpango wa mwaka 2006/07, unalenga katika yafuatayo: kujenga uwezo wa
sekta binafsi wa kuongeza thamani na ubora wa bidhaa kwa kuzingatia matakwa ya
soko la kimataifa; kuongeza juhudi zaidi za kuhamasisha uanzishaji wa maeneo
maalum ya uwekezaji na uzalishaji kwa ajili ya uuzaji nje (EPZ);
kuhamasisha uwekezaji katika sekta ya viwanda vya nguo, ngozi na usindikaji
mazao ya kilimo na mifugo; kuboresha mazingira ya uzalishaji viwandani; na
kuimarisha mahusiano ya kiuchumi kati ya nchi yetu na jumuia za kikanda na
kimataifa. Juhudi zitaongezwa katika mwaka 2006/07 kutumia fursa za masoko
nafuu ya AGOA, EBA, Canadian PACT pamoja na yale ya Japan,
Madini
54.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005/06, sekta ya madini imepata mafanikio ya kuridhisha
yakiwemo: kuanza kwa utekelezaji wa mfumo maalumu unaolenga kuimarisha utoaji
wa leseni za madini na kuongeza maduhuli ya serikali; kukamilika kwa upimaji wa
viwanja vidogo vya madini mkoani Morogoro; kukamilika kwa ufungaji na kuanza
kutumika mashine za kuchonga na kusanifu madini kwenye kituo cha uchongaji na
usafishaji vito Arusha; na kutoa elimu na mafunzo mbalimbali kwa wachimbaji
wadogo. Mapato yatokanayo na madini hayaridhishi hivyo serikali imeunda kamati
maalum ya kutathmini suala hili kwa kina.
55.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, sekta ya madini inalenga: kuboresha mahusiano kati ya wachimbaji wadogo na
wakubwa; kuongeza nafasi za ajira; kuhakikisha uchimbaji salama na unaozingatia
utunzaji mazingira; kuunda kitengo cha kuratibu maendeleo ya wachimbaji wadogo;
kuhamasisha sekta binafsi kuwekeza zaidi; na kuhakikisha kwamba madini
yanayozalishwa yanaongezewa thamani kabla ya kuzwa nje.
Nishati
56.
Mheshimiwa Spika, Mafanikio yaliyopatikana mwaka 2005/06, katika sekta ya nishati ni
pamoja na: kuanza kwa uzalishaji umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo;
kusainiwa kwa makubaliano ya makusudio (Agreement
of Intent) kati ya Serikali na mwekezaji wa mradi wa gesi ya Mnazi Bay
utakaozalisha umeme wa MW 14 kwa Mkoa wa Lindi na Mtwara; na kukamilika
kwa ufafiti uliofanyika mkoani Mwanza wa kubaini vikwazo katika kutumia umeme
utokanao na jua kama nishati mbadala. Vilevile, TANESCO iliingia mkataba
na kampuni ya Wartisila ili kurekebisha mtambo wa IPTL utumie gasi
kuzalisha umeme badala ya mafuta ya petroli. Mafanikio mengine ni pamoja na:
kukamilika kwa mradi wa umeme wa Lower Kihansi; kukamilika kwa miradi ya
kupeleka umeme wilaya za Serengeti na Ukerewe; na kuendelea na mradi wa Urambo.
57.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, sekta ya nishati inalenga kuendeleza miradi ya
kuzalisha umeme kwa kutumia gesi ya Songosongo. Kiasi cha umeme kinachotegemewa
kuzalishwa ni: MW 45 (IPTL-Tegeta), MW 200 (Kinyerezi), MW 60
(Ubungo-Awamu ya
Barabara
58.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005/06, kulikuwa na mafanikio yafuatayo katika sekta ya
barabara: barabara zenye kilometa 10,062 za mikoa na kilometa 5,968 za barabara
kuu zilifanyiwa matengenezo na kuwa na hali nzuri; madaraja 699 yalifanyiwa
matengenezo na 17 mapya yalijengwa; na jumla ya makandarasi 315 walipatiwa
mafunzo muhimu kwa lengo la kujengewa uwezo zaidi.
59.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2006/07, Serikali inalenga kutekeleza yafuatayo:
kukarabati jumla ya kilometa 15,000 za barabara za mikoa na wilaya; kuendeleza
utekelezaji wa mradi maalum wa kuboresha miundombinu katika mikoa sita ya
Lindi, Mtwara, Ruvuma, Kigoma, Rukwa na Tabora; kuendelea kuwajengea uwezo
makandarasi wazalendo na wadau wengine; na kuzifanyia mapitio sera mbalimbali
za sekta hii kwa lengo la kuziboresha.
Mawasiliano na Uchukuzi
60.
Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha 2005/06, katika sekta ya uchukuzi na mawasiliano
Serikali ilitekeleza yafuatayo: kuendelea na ujenzi wa uwanja mpya wa ndege wa
Songwe na kulifikia asilimia 40; kukamilisha ukarabati wa njia za kuruka na
kutua ndege katika viwanja vya ndege vya Mwanza, Arusha na Kigoma; kuendelea na
matengenezo ya miundombinu katika uwanja wa ndege wa Singida; na kuendelea
kukarabati magati katika bandari za maziwa makuu. Vilevile, kazi mbalimbali za
ukarabati katika reli ya kati kwa lengo la kuboresha huduma zimeendelea
kufanyika.
61.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka 2006/07, Serikali inalenga kutekeleza
yafuatayo: kuanza kutekeleza mpango wa kubadilisha mfumo wa reli ya kati ikiwa
ni pamoja na kubadilisha na kuweka mataruma ya uzito wa ratili 80; kuendeleza
ujenzi na ukarabati wa miundombinu ya viwanja vya ndege, bandari, magati, reli
na mtandao wa mawasiliano; kuendeleza mpango wa kuoanisha viwango vya
usafirishaji na mawasiliano vya ndani na vya kimataifa; kuboresha huduma za
Mamlaka ya Hali ya Hewa; na kuratibu vyombo vya usafiri wa abiria ili kupunguza
ajali.
Teknolojia ya
Habari na Mawasiliano (TEKNOHAMA)
62.
Mheshimiwa Spika, Serikali katika mwaka 2005/06, iliendelea kutoa kipaumbele katika
masuala ya TEKNOHAMA kwa kutekeleza yafuatayo: kufanya tathmini kuhusu
uendelezaji wa Mkonga wa Taifa wa Mawasiliano; kuunda Timu ya Waratibu wa
TEKNOHAMA; kuanzisha vituo vya mawasiliano katika miji ya Singida, Morogoro,
Mtwara, Mpwapwa, Rungwe na Pemba; na kuendelea kutekeleza mradi wa kujumuisha
masomo ya TEKNOHAMA kwenye mitaala nchini (e-schools, e-education,
e-learning).
63.
Mheshimiwa Spika, Malengo ya serikali kwa kipindi cha 2006/07 ni
Maliasili
64.
Mheshimiwa Spika, Kwa kipindi cha 2005/06, katika sekta ya Maliasili Serikali ilitekeleza yafuatayo: Jumla ya miche 66, 182, 502 ilioteshwa
iklinganishwa na miche 65,558,138 ya mwaka 2004, ongezeko hilo sawa na asilimia
0.95; kukamilisha upimaji wa misitu ya hifadhi katika maeneo ya Kapingo,
Engoma, Mikikagi na Itira katika kisiwa cha Ukerewe; na kukamilisha kazi za
kuhesabu rasilimali za misitu katika
wilaya za Morogoro, Mvomero, Kilombero, Ulanga, Handeni, Kilindi, Kilwa,
Nachingwea, Liwale, Tunduru, Mpanda na Rufiji.
65.
Mheshimiwa Spika, Malengo ya Serikali katika mwaka
2006/07 ni: kuweka misingi madhubuti ya usimamizi wa rasilimali za maliasili
ili kuongeza mchango wake katika Pato la Taifa; kuendeleza uhifadhi na uvunaji
endelevu wa maliasili kwa kuboresha usimamizi na utendaji kazi unaofuata kanuni
na sheria; kujenga mfumo madhubuti wa kiutawala ili kuboresha utoaji wa huduma;
na kupanua wigo wa ushiriki wa sekta binafsi,mashirika yasiyo ya kiserikali na
wadau mbalimbali katika mipango inayohusu kulinda, kuhifadhi, na kusimamia
matumizi endelevu ya maliasili.
UTEKELEZAJI WA MASUALA MTAMBUKA
66.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, Serikali iliendelea kutekeleza maamuzi mbalimbali ya
kisera na yanayozingatia masuala mtambuka.
Nitaelezea kwa kifupi kuhusu utekelezaji wa masuala hayo kama
ifuatavyo:-
(i) Utawala Bora
67.
Mheshimiwa Spika, Serikali iliendelea kutathimini hali
ya rushwa kwa kutumia viashiria vilivyowekwa. Aidha, Serikali iliunda kamati za
maadili makazini pamoja na kuendelea kutayarisha mkakati wa pili wa kupambana
na rushwa mahali pa kazi katika ofisi za umma.
68.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, mambo yatakayosisitizwa ni: kuendelea kuboresha
usimamizi wa fedha za umma na uwajibikaji; kushirikisha wadau mbalimbali katika
mchakato wa maandalizi, ufuatiliaji wa
utekelezaji wa sera, mipango na mikakati ya maendeleo; kuendelea kutekeleza
Mpango wa Maboresho ya Serikali za Mitaa; kuimarisha kampeni ya kupambana na
rushwa; kupambana na wahalifu; kuendelea kurekebisha kanuni na sheria ikiwa ni
pamoja na mfumo wa uendeshaji; na kuimarisha upatikanaji wa taarifa
zitakazosaidia kufanya maamuzi sahihi.
(ii) Vita Dhidi ya UKIMWI
69.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, Serikali iliendelea
kuchukua hatua mbalimbali zikiwemo uhuishwaji wa shughuli za kudhibiti UKIMWI
katika wizara, taasisi za serikali na sekta binafsi; na uandaaji wa mikakati ya
kudhibiti UKIMWI kwa lengo la kuainisha shughuli zitakazofanyika katika
kupambana na UKIMWI. Taarifa ya utafiti
ya kila mwaka kuhusu UKIMWI na magonjwa ya zinaa (Oktoba 2005) inaonyesha kuwa
maambukizi mapya ya virusi vya UKIMWI yameongezeka kutoka watu 188,140 mwaka
2004, hadi watu 188,400 mwaka 2005. Kati ya hao wanawake ni 97,130 sawa na asilimia 51.6
70.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha mwaka 2005, mafunzo
yaliendelea kutolewa katika ngazi
mbalimbali. Mwongozo wa kudhibiti UKIMWI
katika sekta ya umma uliandaliwa ambao
uliweka bayana taratibu za kuzingatia wakati wa kutoa matunzo na msaada
kwa watu waishio na virusi vya UKIMWI. Aidha, hadi Desemba 2005, vituo 96
vilikuwa vinatoa dawa za kurefusha maisha kwa watu waishio na virusi vya UKIMWI
na watu 25,840 waishio na virusi vya UKIMWI
walisajiliwa katika mpango wa matibabu na matunzo.
71.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2006/07, Serikali
itaendelea kuongeza idadi ya vituo vya kutolea dawa za kurefusha maisha kwa
watu waishio na virusi vya UKIMWI na kuendelea kusajili watu waishio na virusi
vya UKIMWI katika mpango wa matibabu na
matunzo pamoja na kuendelea na juhudi za kutoa elimu katika ngazi mbalimbai.
(iii) Masuala ya Jinsia
72.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005, Serikali kwa
kushirikiana na wadau mbalimbali iliendelea kutekeleza sera, mipango na
mikakati inayolenga katika kuboresha masuala ya jinsia. Aidha, uwakilishi wa
wanawake umeendelea kuongezeka kutokana na marekebisho yaliyofanywa katika
katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania pamoja na kuendelea kurekebisha
sheria za uchaguzi ili kuwa na uwakilishi wa wabunge wanawake unaofikia
asilimia 30. Aidha, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Mhe. Rais kwa
kuwateua wanawake wengi katika nyadhifa nyeti za kufanya maamuzi makubwa
serikalini. Kwa upande wa Waheshimiwa Wabunge wanawake wamefikia asilimia 30.41
ikiwa ni zaidi ya lengo la kiwango cha chini kilichowekwa kwenye katiba ya nchi
yetu na makubaliano ya nchi wanachama wa
SADC.
73.
Mheshimiwa Spika, Katika kuwawezesha wanawake kupanua
uelewa wao kibiashara, wanawake 127 walishiriki maonyesho ya Biashara ya
Kimataifa ya Dar es Salaam kwa kuwezeshwa na Serikali ikishirikiana na Mfuko wa
Fursa Sawa kwa Wote (Equal Oppotunities Trust Fund-EOTF) mwaka
2005, ikilinganishwa na wanawake 130 mwaka 2004.
74.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, Serikali
itaendelea kuhamasisha matumizi ya takwimu zilizochambuliwa kijinsia katika
maamuzi mbalimbali pamoja na kuhuisha sheria zinazoendelea kuwakandamiza
wanawake. Serikali itahakikisha kiwango cha uwakilishi wa wanawake katika ngazi
mbalimbali kinazingatiwa pamoja na kuhakikisha kuwa wanawake wanaendelea kupewa
fursa ya kujiendeleza kielimu na kiuchumi ili waweze kufaidika zaidi katika
maendeleo ya taifa.
(iv) Idadi
ya Watu
75.
Mheshimiwa Spika, Makadirio ya idadi ya watu Tanzania
kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 yanaonyesha kwamba
kwa mwaka 2005, idadi ya watu ilikuwa 37,267,530, kati ya hao, wanawake ni
19,009,051, sawa na asilimia 51.01 na wanaume 18,258,479, sawa na asilimia
48.99. Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu 36,197,313 wakati Tanzania
Zanzibar ilikadiriwa kuwa na watu
1,070,217.
76.
Mheshimiwa Spika, Kutokana na makadirio hayo Mkoa wa Dar
es salaam ulionyesha kuwa na msongamano wa wastani wa watu 2,010 kwa kilomita
ya mraba, ukifuatiwa na Mwanza watu 163, na Kilimanjaro watu 108. Mikoa iliyo
na msongamano mdogo ilionyesha kuwa ni Lindi yenye watu 12 kwa kilomita ya
mraba, ikifuatiwa na Rukwa watu 18. Kwa Tanzania Zanzibar karibu mikoa yote ina
msongamano mkubwa wa kati ya watu 117 na 1,919 katika kilomita ya mraba.
77.
Mheshimiwa Spika, Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu
ilikamilika kuhuishwa katika mwaka 2005, na Mpango wa Utekelezaji ulianza kuandaliwa. Mafunzo ya namna ya kujumuisha
masuala ya idadi ya watu katika mipango ya maendeleo yaliendelea kutolewa
katika ngazi za wilaya na kata, mashirika yasiyokuwa ya kiserikali na Wabunge.
(v) Mazingira
78.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005/06 Serikali iliandaa
Mkakati wa kuhifadhi mazingira ya Ardhi na Vyanzo vya Maji. Mkakati umelenga kukabiliana na tatizo kubwa
la uharibifu wa mazingira utokanao na shughuli za ufugaji na kilimo kwenye
maeneo ya vyanzo vya maji. Pia mkakati
huu unalenga kukabiliana na uharibufu wa mazingira utokanao na ukataji miti
ovyo kwa ajili ya kuni, mkaa na matumizi mengine.
79.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07 Serikali
inategemea kuchukua hatua zifuatazo: kudhibiti shughuli za kilimo na ufugaji
kwenye vyanzo vya maji; kuendelea kuhamasisha wafugaji kuondokana na ufugaji
holela na kuhamahama; kuandaa mipango mizuri ya matumizi ya ardhi; kuendeleza
kampeni ya kitaifa ya upandaji miti na kuitunza; kujenga na kuendeleza malambo, visima na
mabwawa katika maeneo ya wafugaji na wakulima; kuendeleza matumzi ya teknolojia sahihi za kuvuna,
kuhifadhi na kusambaza maji ya mvua na ya ardhini kwa ajili ya shughuli za
kilimo na ufugaji; kuhamasisha taasisi,
wakulima wa tumbaku na watumiaji wengine wakubwa wa miti, kuni, na mkaa, kwa
mfano taasisi za elimu, majeshi na viwanda kuwa na mashamba yao ya miti;
kuendelea kudhibiti uchomaji wa misitu na ukataji miti holela, kudhibiti
shughuli za umwagiliaji; na kupanda miti ifaayo kwenye vyanzo vya maji.
MIPANGO MAALUMU
YA MAENDELEO YA KIUCHUMI NA KIJAMII
80.
Mheshimiwa Spika, Katika muda wa kati, Serikali imeandaa
kuendelea kutekeleza mipango na mikakati mbalimbali inayojumuisha: MKUKUTA;
Mkakati wa Maendeleo wa Sekta ya Kilimo; Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara Tanzania (MKURABITA); Tanzania Mini-Tiger Plan 2020 (TMTP 2020);
Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (MKUMBITA); Mkakati wa
Madeni wa Taifa na Mkakati wa Pamoja wa Kusimamia Misaada Tanzania. Aidha,
Serikali imetayarisha Mfumo wa ufuatiliaji wa utekelezaji wa MKUKUTA utakaotumika kufanya tathmini ya matokeo ya
utekelezaji katika kipindi chote cha miaka mitano. Mfumo huu pia utabainisha
mafanikio na mapungufu yatakayoweza kujitokeza ili kutoa maamuzi ya jinsi ya
kuboresha uchumi na maendeleo ya jamii.
81.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005/06, Serikali iliendelea kutekeleza mipango na mikakati
hiyo kama ifuatavyo:-
(i) Mkakati
wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini
82.
Mheshimiwa Spika,
MKUKUTA ulianza kutekelezwa
mwaka 2005/06 ambapo sekta zote na
taasisi mbali mbali zilizo za Serikali na zisizo za Serikali zinahusika katika
utekelezaji wa maeneo makuu matatu
ya MKUKUTA ambayo ni:- (i) ukuaji wa uchumi na upunguzaji wa umasikini wa
kipato; (ii) uboreshaji wa maisha na ustawi wa jamii; na (iii) utawala bora na
uwajibikaji. Baadhi ya mambo ya jumla ambayo yametekelezwa hadi sasa ni pamoja
na: kuoanisha MKUKUTA na mipango mikakati
pamoja na bajeti ya serikali; kukamilisha mwongozo wa jinsi ya kuoanisha mipango ya
sekta na MKUKUTA na kukamilisha utayarishaji wa Mfumo wa Ufuatiliaji wa Hali ya
Umaskini Kitaifa; na kuelimisha mikoa na halmashauri za serikali za mitaa
kuhusu mwongozo wa uaonishaji wa mipango ya sekta na MKUKUTA. Aidha, zoezi la kuanisha gharama za utekelezaji wa malengo
ya MKUKUTA lilianzishwa.
83.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha 2006/07, Serikali
itaendelea na zoezi la kuainisha gharama za utekelezaji wa malengo ya maeneo
yote ya MKUKUTA na kuendelea na utekelezaji wa mipango, programu na mikakati
mbalimbali ya kufanikisha malengo ya jumla ya MKUKUTA. Vilevile, Zoezi la kuainisha gharama za utekelezaji
wa Ilani ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 litaanzishwa rasmi katika
kipindi hicho.
(ii) Utekelezaji
wa Mpango wa Kuboresha Mazingira ya Biashara Tanzania (MKUMBITA)
84.
Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea
kutekeleza MKUMBITA kwa lengo la kupunguza gharama za uanzishwaji na uendeshaji
wa biashara kwa kuondoa vikwazo vikiwemo vya kisera, kisheria, kanuni,
kiutaratibu na kitaasisi ambavyo vinakwamisha ukuaji wa sekta binafsi. Katika
mwaka 2005/06 MKUMBITA uliendelea kuboresha mazingira ya biashara nchini. Hii ilikuwa ni pamoja na:
·
Kukamilisha mapitio ya sheria na kanuni mbalimbali kwa lengo la kuimarisha
mazingira ya biashara nchini. Sheria na
Kanuni hizi ni pamoja na Dhamana ya Ardhi ambazo zilianza kutumika mwezi
Agosti, 2005 na Sheria ya Kusajili Shughuli za Biashara ya mwaka 2006; na
·
Kutayarisha rasimu za miswada kwa ajili ya sheria mbalimbali kama vile
Miswada ya Kuthamanisha Ardhi; Usalama
Kazini; Fidia kwa Wafanyakazi; Hifadhi ya Jamii na Uwakala wa Soko la
Ardhi ambayo imekwishawasilishwa kwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali; na kuwezesha
maandalizi ya Mkakati wa Kuendeleza Sekta Binafsi.
85.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07,
Serikali itaendelea kuratibu MKUMBITA kwa kutoa msukumo wa pekee na thabiti
katika kuendeleza sekta binafsi kwa kuweka mazingira bora ya kufanyia biashara
na uwezeshaji nchini hususan kuendelea kuboresha sera, sheria na taratibu
zinazokwaza sekta binafsi; kubadilisha mtazamo
wa watendaji wa serikali kwa sekta binafsi, kuimarisha Kituo cha
Uwekezaji cha Taifa na kuleta mageuzi
katika Mahakama ya Biashara.
(iii) Mpango
Maalum wa Kuharakisha Maendeleo Tanzania (Tanzania Mini-Tiger Plan 2020)
86.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2005 Serikali ilianza kutekeleza Mpango Maalumu wa Kuharakisha
Maendeleo ya Tanzania “(Tanzania Mini-Tiger Plan 2020)” kwa kuzingatia
uzoefu na mafanikio ya nchi za Kusini Mashariki mwa Asia. Lengo la mpango huu
ni kuongeza kasi ya ukuaji uchumi kama msingi wa kuongeza wastani wa kipato cha
Mtanzania; kuongeza mauzo ya bidhaa na huduma nchi za nje; na kuongeza fursa za ajira nchini kwa shabaha
ya kukabiliana vizuri zaidi na tatizo la umaskini.
87.
Mheshimiwa Spika; Katika harakati za kuendeleza Mpango
huu, miradi ifuatayo ilitekelezwa: kuzinduliwa kwa kampuni ya kuagiza na
kukarabati magari, mashine na vipuri mbalimbali (Tsubasa Renewcar EA Ltd); na kuanza kwa ujenzi wa eneo maalum la
uwekezaji raslimali katika eneo la
Mabibo Dar es salaam linalojulikana kama “The
Benjamín William Mkapa Special Economic Zone (BWM-SEZ)”. Vilevile,
kamati ya kusimamia ujenzi wa Kituo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (ICT-SEZ)
iliundwa na iliendelea na kazi zake chini ya uratibu wa Chuo Kikuu cha Dar es
Salaam.
88.
Aidha, Wataalam walitembelea India Oktoba 2005, ili kupata uzoefu wa
kuanzisha na kuendesha vituo vya aina hiyo hapa nchini. Katika kufanikisha Mpango huu, sheria ya kuanzisha Maeneo Maalum
ya Uwekezaji Rasilimali (SEZs) imepitishwa na Bunge lako Tukufu
Februari, 2006 na kupata kibali cha Rais
Machi, 2006 na kuanza kutumika rasmi tarehe 1 Mei, 2006.
89.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, Mpango huu utakuwa na malengo yafuatayo: kuendelea
na ujenzi na kulitangaza Eneo Maalum la
Uwekezaji la ‘Benjamín William Mkapa
Special Economic Zone’ liloko Mabibo ili kuwavutia wawekezaji wa ndani na
nje ya nchi; kuunda Mamlaka ya Kusimamia Maeneo Maalum ya Uwekezaji (SEZs
Authority); kutoa mafunzo ya muda mfupi kwa Watanzania kutoka nchi zenye
uzoefu wa Maeneo Maalum ya Uwekezaji; na kuanza ujenzi wa kituo cha Teknolojia
ya Habari na Mawasiliano katika Eneo Maalum la Uwekezaji liloko eneo la Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (ICT-SEZ).
(iv) Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na
Biashara Tanzania (MKURABITA)
90.
Mheshimiwa Spika,
Katika kipindi
cha 2005/06, Awamu ya
91.
Kazi nyingine zilizofanyika ni pamoja na: uhamasishaji wa viongozi katika
ngazi mbalimbali juu ya malengo na madhumuni ya MKURABITA; uhamasishaji kwa
walengwa na watendaji kupitia warsha mbalimbali, uhamasishaji wa wafanya
biashara ndogo ndogo na za kati juu ya shughuli za MKURABITA; uandaaji wa
taratibu za ushirikiano na Wizara na Taasisi za Serikali zinazoweza kufanya
shughuli kwa ushirikiano na MKURABITA; na ukamilishaji wa Mpango wa Kazi kwa
ajili ya Awamu ya Pili ya MKURABITA.
92.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, malengo ya MKURABITA ni pamoja na: kufanya
utafiti katika wilaya 26 za Tanzania Bara na Tanzania Zanzibar ili kuandaa
mapendekezo ya awali ya maboresho ya sheria na kanuni zitumikazo katika sekta
isiyo rasmi; kutoa mapendekezo ya awali ya muundo wa kitaasisi (institutional
arrangement); kutoa mafunzo kwa wataalamu wa Kitanzania ili kuhakikisha
umiliki na ushiriki wa Watanzania katika kutengeneza sheria; kutekeleza
shughuli zinazoenda sambamba na maandalizi ya maboresho ili kuendeleza nguvu na
msukumo wa Watanzania ulitokana na taarifa ya utafiti; na kukamilisha “Concept
Document” ya programu ambayo itatumika kama kiongozi cha mpango huu, na
kuendeleza utengenezaji wa tovuti ya MKURABITA.
(v) Mfuko wa Maendeleo ya Jamii
(TASAF)
93.
Mheshimiwa Spika, Kutokana na mafanikio yaliyopatikana katika Awamu ya
94.
Mheshimiwa Spika, Katika kipindi cha Awamu ya Pili ya TASAF kilichoanza Mei 11, 2005,
Serikali imefanikiwa katika: kuhamasisha umma kupitia vipindi vya radio na
televisheni, makala katika magazeti na vipeperushi; kuandaa miongozo ya
utekelezaji wa mradi katika ngazi za Halmashauri za Wilaya, Manispaa, Jiji na
Shehia; na kutafsiri katika lugha ya Kiswahili miongozo mbalimbali.
95.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, TASAF imejiwekea lengo la kuwafikia
wananchi wote wa
(vi) Ubinafsishaji
na Maendeleo ya Sekta Binafsi
96.
Mheshimiwa Spika,
Katika mwaka 2005/06, Serikali kwa kupitia Baraza la Taifa la Biashara (TNBC)
imeanzisha mabaraza ya biashara ya mikoa kwa lengo la kupanua wigo wa
mashauriano kati ya Serikali na Sekta Binafsi ili kuboresha mazingira ya
uzalishaji na biashara katika mikoa na wilaya. Mabaraza hayo yameanzishwa
katika mikoa 12 ifuatayo: Kilimanjaro, Arusha, Manyara, Tanga, Mwanza, Kagera,
Morogoro, Iringa, Mbeya, Ruvuma, Mtwara, na Dodoma. Aidha, Baraza la Biashara
la Zanzibar limeanzishwa chini ya uenyekiti wa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti
wa Baraza la Mapinduzi.
97.
Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Kituo cha Uwekezaji
Tanzania (TIC) iliendelea na juhudi za kuhamasisha na kuratibu
wawekezaji wa ndani na nje katika sekta mbalimbali kwa lengo la kukuza sekta
binafsi. Katika mwaka 2005, Kituo kiliandikisha miradi 550 yenye thamani ya sh.
1,876,063 milioni ambayo ilitoa
fursa za ajira kwa watu 55,663 ikilinganishwa na miradi 454 yenye thamani ya sh. 1,246,040
milioni mwaka 2004. Aidha, TIC
inatekeleza mikakati ya kuibua fursa za uwekezaji mikoani. Ili kutimiza azma
hiyo, tayari kituo kimefungua ofisi katika Kanda ya Ziwa mkoani Mwanza, na
Kanda ya Kaskazini mkoani Kilimanjaro.
98.
Mheshimiwa Spika, Thamani ya uwekezaji wa mitaji ya
kigeni ya moja kwa moja (FDIs) ilikuwa dola za Kimarekani 325 milioni mwaka 2005, ikilinganishwa na
dola za Kimarekani 470 milioni mwaka 2004, sawa na upungufu wa asilimia 30.8. Upungufu huo ulisababishwa hasa na kushuka
kwa uwekezaji katika sekta ya madini.
99.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, malengo ya TIC
ni pamoja na kufungua ofisi katika Kanda ya Kusini; kuendelea kuhamasisha
wawekezaji wa nje kwa mtindo wa “Investor Targeting’’ ili kuongeza mitaji ya
moja kwa moja (FDIs); kuwasaidia wawekezaji wadogo na wa kati (SMEs);
kuanda miradi inayouzika (Bankable Projects); na kusaidiana na mikoa
katika kuandaa na kuratibu warsha za uwekezaji.
100.
Mheshimiwa Spika, Mwaka 2005, jumla ya mashirika 11 yalibinafsishwa na mali 126
ziliuzwa na kufanya jumla ya mashirika
yaliyobinafsishwa kuwa 322 na mali za mashirika kuwa 647 tangu zoezi hili
lianze miaka 13 iliyopita. Mashirika hayo yalibinafsishwa kwa Watanzania na
wawekezaji kutoka nje kwa utaratibu wa kuuza hisa, kuuza mali, na kukodisha.
Aidha, Tume ya Rais ya
Urekebishaji wa Mashirika Umma iliongezewa muda wa miaka minne kuanzia Januari
2004 hadi Desemba 2007 ili kukamilisha ubinafsishaji wa mashirika yaliyobaki.
101.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/07, mashirika 36
yaliyobaki yataendelea na hatua
mbalimbali za marekebisho, yakiwemo TAZARA, vitengo vya kibiashara vya
Mamlaka ya Bandari Tanzania (ukiondoa kitengo cha makontena ambacho
kimeshakodishwa) na Shirika la Bima la Taifa.
PSRC itafikia mwisho Desemba 2007, ambapo zoezi hili linatakiwa
liwe limekamilika. Baada ya hapo, azma ya Serikali ni kubakiza Kitengo cha
Ufuatiliaji na Tathmini (Monitoring
& Evaluation) ya mashirika yaliyobinafsishwa na kuratibu shughuli za
mamlaka za udhibiti.
(vii) Utekelezaji wa Sera ya
Taifa ya Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi.
102.
Mheshimiwa Spika, Uwezeshaji wa Watanzania kiuchumi umekuwa moja ya ajenda
ya muda mrefu katika sera za Taifa letu. Jitihada za uwezeshaji wa wananchi
kiuchumi zimekua zikifanywa na vyombo mbalimbali hata kabla ya Sera ya
Uwezeshaji kuundwa. Bunge lako Tukufu lilishuhudia uzinduzi wa Sera ya Taifa ya
Uwezeshaji Juni 2004 na kupitisha Sheria ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi
Novemba 2004, ambayo ilianza kutumika rasmi Februari 2005. Lengo kuu la Sera ni
kuwawezesha wananchi kushiriki katika shughuli mbali mbali za kiuchumi na kutoa
mwongozo wa jumla utakaohakikisha kwamba, wananchi wanapata fursa za kiuchumi
katika sekta mbali mbali. Aidha, Baraza la Uwezeshaji wa Wananchi Kiuchumi
liliundwa na kuzinduliwa rasmi Novemba 2005. Vilevile, Mhe. Rais alimteua
Katibu wa Baraza la Uwezeshaji tarehe 3 Aprili 2006 akiwa na dhamana ya
kusimamia utekelezaji wa Sera ya Uwezeshaji Wananchi Kiuchumi. Pamoja na
kuteuliwa kwa Katibu wa Baraza shughuli za Sekretariati ya Baraza la Uwezeshaji
zitaanza kutekelezwa rasmi mwaka wa fedha 2006/07 ambapo sh.1.4 bilioni zimetengwa
kwa ajili hiyo.
103.
Mheshimiwa Spika, Katika kutekeleza sera hii, kila sekta inawajibika kuendelea kubuni
mikakati yake, kufafanua na kuchanganua jinsi ya kuitekeleza. Mikakati ya kisekta inaendelea kujikita zaidi
katika kuwaendeleza wananchi kwa kuwapa upendeleo maalumu, na kuwawezesha kwa
kuwapatia huduma bora za elimu na mafunzo ya ujasiriamali, kujenga miundombinu
na kuwapa fursa za kushiriki katika kubuni, kupanga na kutekeleza sera na
mikakati ya kisekta ya uwezeshaji wananchi kiuchumi.
104.
Mheshimiwa Spika, Katika mwaka 2006/2007 baadhi ya
kazi zitakazofanywa na Serikali ni:- kuajiri watumishi wa sekretariati ya
Baraza; kufanya utafiti wa kuainisha mambo muhimu ya kipaumbele (quick wins)
katika kutekeleza Sera; kuandaa mwongozo wa jinsi wananchi watakavyoshiriki
katika kutekeleza Sera; na kuandaa mfumo
wa kuhakikisha kwamba sera ya uwezeshaji inafahamika zaidi kwa wananchi wote.
105.
Mheshimiwa Spika, Licha ya Tanzania kupata mafanikio
makubwa katika uchumi jumla, changamoto
kubwa iliyopo ni kuendeleza na
kuhakikisha kwamba mafanikio hayo yanawafikia wananchi wengi, hususan wananchi
masikini walio vijijini. Aidha, kukamilika na kutekelezwa kwa kikamilifu
miradi ya: Vitambulisho vya Taifa; Upimaji na Utoaji Hatimiliki na Utayarishaji wa Ramani Maalum za Maeneo
zinazosomeka kwa Kompyuta (Geographical Information System - GIS &
National Spatial Data Infrastructure - NSDI) kutafanikisha kupatikana
takwimu sahihi na katika muda muafaka.
Takwimu hizi zitasaidia katika tafiti mbalimbali zinazohusu jamii na maendeleo.
Aidha, katika kuendeleza juhudi za kuwawezesha wananchi kiuchumi Serikali
imeanzisha mfuko wa dhamana kwa SMEs, na
inaendelea kutekeleza mipango na
mikakati mbalimbali iliyoanzishwa ikiwemo: MKURABITA; MKUMBITA; Tanzania
Mini Tiger 2020; na TASAF.
MISINGI NA MALENGO YA MPANGO WA MUDA WA KATI NA BAJETI KWA MWAKA
2006/07-2008/09
106.
Mheshimiwa Spika, Mpango huu na Bajeti hii ni ya kwanza
kutayarishwa na Serikali ya Awamu ya Nne katika kutekeleza MKUKUTA. Misingi na
Malengo ya Mpango wa Muda wa Kati na Bajeti ya Serikali kwa mwaka
2006/07-2008/09 inazingatia utekelezaji wa ahadi ya Ilani ya CCM ya Uchaguzi
Mkuu wa mwaka 2005, inayolenga katika kuyafikia malengo makuu ya Dira ya Taifa
ya Maendeleo 2025 ikijumuisha kuwapo maisha bora ya kila Mtanzania na kupunguza
kabisa umasikini wa kipato ifikapo 2015.
107.
Mfumo wa Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2006/07
utatolewa na Waziri wa Fedha ambapo atabainisha kwa kina mwenendo wa mapato na
matumizi ya Serikali katika mwaka 2005/06 na makadirio kwa mwaka 2006/07 pamoja
na kufafanua maeneo makuu yaliyotengewa fedha.
108.
Mheshimiwa Spika, Misingi ya malengo mapana ya Mpango na
Bajeti kwa kipindi cha muda wa kati 2006/07–2008/09 ni kama ifuatavyo:
i)
Kuendelea kutengemaza uchumi mkuu au uchumi jumla ( Macro economic
stability);
ii)
Kuendelea kutekeleza MKUKUTA kwa ufanisi ikiwa ni pamoja na kuendelea
kutekeleza miradi mikubwa kama MKURABITA, Mpango Maalum wa Kuharakisha
Maendeleo Tanzania, Mradi wa Maji kutoka Ziwa Victoria kwenda Kahama-Shinyanga,
ujenzi wa barabara na madaraja pamoja na miundombinu ya umwagiliaji maji;
iii)
Kuendelea kubuni na kutekeleza mipango na mikakati ya kuharakisha ukuaji wa
uchumi kwa mfano mradi wa Vitambulisho vya Taifa, mradi wa upimaji ardhi na
utoaji hatimiliki, na utayarishaji wa ramani maalum za maeneo zinazosomeka kwa
kompyuta (Geographical Information System–GIS and National Spatial Data
Infrastructure–NSDI);
iv)
Kuimarisha na kusaidia sekta isiyo rasmi, ili ipanuke na kutengemaa kwa
lengo la kuingizwa kwenye mfumo rasmi wa uchumi;
v)
Kuimarisha mifumo ya uratibu na usimamizi wa miradi ya maendeleo katika
ngazi zote;
vi)
Kuendelea kutekeleza sera ya Serikali ya kupeleka madaraka kwa wananchi
kupitia Programu ya Maboresho ya Serikali za Mitaa;
vii)
Jamii kuwa na mwamko, nidhani, na tabia ya kujituma katika shughuli za
maendeleo; na
viii)
Kupatikana kwa rasilimali na kuzitumia ipasavyo.
109.
Mheshimiwa Spika, Kufuatia misingi niliyoitaja hapa juu, matarajio ya malengo ya uchumi
jumla katika kipindi cha mwaka 2006/07-2008/09 ni
i)
Pato halisi la
taifa kukua kwa asilimia 5.9[4] mwaka 2006, asilimia 7.3 mwaka 2007, asilimia 7.7 mwaka
2008, na asilimia 7.9 mwaka 2009;
ii)
Kiwango cha kasi
ya upandaji bei kisichozidi asilimia 4.0 (kwa bei za 2001) kufikiwa ifikapo
mwezi Juni 2007;
iii)
Mapato ya ndani
kuongezeka kufikia asilimia 14.5 ya Pato la Taifa mwaka 2006/07, asilimia 14.7
mwaka 2007/08 na kuongezeka hadi asilimia 14.8 mwaka 2008/09;
iv)
Ujazi wa fedha
kwa tafsiri pana (M2) kudhibitiwa kwa viwango
vinavyowiana na malengo ya ukuaji wa uchumi na kasi ya upandaji bei; na
v)
Akiba ya fedha za
kigeni itakayokidhi mahitaji ya uagizaji wa bidhaa na huduma kutoka nje kwa
kipindi kisichopungua miezi saba.
MAJUMUISHO
110.
Mheshimiwa Spika, Baada ya kuelezea hali ya uchumi wa taifa, misingi na malengo ya mpango
na bajeti kwa kipindi cha 2006/07–2008/09, nachukua fursa hii kusisitiza mambo
muhimu ambayo kama taifa tunahitaji kuyapa kipaumbele katika utekelezaji na
ufuatiliaji wa karibu kwa mwaka 2006/07
i)
Kuhakikisha
kwamba wananchi wanaelewa masuala muhimu yote yaliyobainishwa katika Ilani
ya CCM ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005, na Mkakati wa Kukuza uchumi na Kupunguza
Umasikini
ii)
Kuendelea
kuhakikisha kwamba mipango, mikakati na malengo tunayojiwekea yanalenga katika
kukuza uchumi, kuongeza nafasi za ajira, kuongeza tija, na kuongeza mapato ya
fedha za kigeni na ya ndani;
iii)
Kuendelea
kukasimu baadhi ya madaraka ya Serikali kuu kwa Serikali za Mitaa pamoja na
kuzipatia rasilimali kwa lengo la kuwapa wananchi uwezo wa kuchambua, kupanga,
kutekeleza, kufuatilia na kutathimini mipango na mikakati
iv)
Kuendelea
kuboresha na kuoanisha mifumo ya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji
wa mipango na mikakati ya maendeleo kama ilivyoainishwa katika Ilani ya CCM
ya Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2005 na malengo ya Dira ya Maendeleo 2025 na Mkakati
wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini
v)
Kuendelea
kuhamasisha sekta zote zibuni mikakati madhubuti na endelevu ili kuboresha hali
ya maisha ya wananchi;
vi)
Kuendelea
kuboresha na kurasimisha sekta isiyo rasmi ili ipate kupanuka na kutengemaa kwa
lengo la kuongeza nafasi za ajira nchini;
vii)
Kuendelea
kuhimiza wawekezaji wa ndani kuwekeza katika viwanda vidogo na vya kati vya
kusindika mazao ya kilimo ili kuongeza thamani yake na kuchangia katika kupanua
nafasi za ajira;
viii)
Kuendelea kubuni
na kutekeleza mipango na mikakati ya kuwawezesha wananchi kiuchumi ili waweze
kuboresha na kuendeleza shughuli zao za kijamii na kiuchumi; na
ix)
Kuendelea
kuhuisha mikakati ya kitaifa ya kujitosheleza kwa chakula kwa lengo la kukuza
uchumi na kuondoa umasikini nchini.
111.
Mheshimiwa Spika,
112.
Mheshimiwa Spika, Napenda kuelezea kuwa rasilimali zetu bado ni kidogo ukilinganisha na
matatizo mengi ya kijamii na kiuchumi yanayotukabili kitaifa. Tunaweza kuleta
mabadiliko ya kiuchumi na kijamii kwa haraka zaidi ikiwa tutatumia rasilimali
tulizonazo kwa ufanisi na makini zaidi. Hivyo, wito wangu ni kwa kila mmoja
wetu kutumia fursa zilizopo kwa lengo la kuongeza tija kwa kasi kubwa na kukuza
uchumi wetu kwa nguvu zaidi ili tuondokane na umasikini uliokithiri.
113.
Aidha, ni lazima
jamii iwajibike kudhibiti, kufuatilia, kusimamia kwa karibu utekelezaji wa
mipango na mikakati na kutathimini malengo.
Serikali itaendelea na jukumu la kuwawezesha na kuunga mkono juhudi za
wananchi kwa kuelekeza rasilimali, pamoja na kuendelea kuandaa sera na mikakati
na kutoa miongozo ya kuratibu, kusimamia pamoja na kufuatilia kwa karibu na
kutathmini utekelezaji ili tuwe na maendeleo yenye kuwiana katika kila ngazi.
Hivyo basi, kila mmoja wetu anatakiwa kutimiza wajibu wake ili kufikia azma ya
taifa ya ukuaji wa uchumi unaopanda mwaka hadi mwaka na kwa haraka zaidi na
kufikia malengo ya MKUKUTA na Dira ya Maendeleo ya Taifa 2025.
114.
Mheshimiwa Spika, Mwisho napenda nitambue juhudi za washirika mbalimbali wa maendeleo
yetu kwa misaada na michango
Mheshimiwa Spika, Naomba kutoa hoja.
[1] Takwimu za ukuaji wa Pato la Taifa zilipitiwa
upya kwa kuzingatia matokeo ya takwimu zilizokusanywa na Idara Kuu ya Takwimu.
[2] M
ni fedha zilizo kwenye mzunguko nje ya mabenki; M
= M
+ amana za hundi; M
= M
+ amana za muda maalum + amana za akiba; M
= M
+ amana za fedha za kigeni.
[3] Kiasi hiki ni kikubwa zaidi ya kile kinachoonyeshwa katika machapisho ya Benki kuu kutokana na tarakimu zao kutojumuisha baadhi ya madeni ya serikali yakiwemo ya Mashirika yaliyobinafsishwa au kufilisika.
[4] Ukuaji wa Pato la taifa unatarajia kupungua
kutokana na ukame, kuchelewa kwa mvua na kupanda kwa bei za mafuta ya petroli.