Elimu

 

Matokeo ya Uchaguzi ya Kuingia Kidato cha Tano na Vyuo vya Ufundi

Muundo wa mfumo rasmi wa Elimu na Mafunzo nchini Tanzania unajumuisha miaka miwili ya mwanzo ya (elimu ya chekechea) kumtayarisha mtoto kabla ya kuanza darasa la kwanza, ikifuatiwa na miaka 7 ya elimu ya msingi, miaka 4 ya elimu ya awali ya Sekondari (ordinary level), miaka 2 ya mwisho ya Sekondari (high level) na kumalizikia na miaka 3 au zaidi vyuo vikuu (tertiary levels).

 

Wizara ya Elimu na Utamaduni na Wizara ya Sayansi, teknolojia na Elimu ya Juu ndizo zinazosimamia na kuratibu shughuli zote za sekta ya Elimu hapa nchini.  Kadhalika, Wizara ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa nayo pia inasimamia Elimu ya Msingi.

 

Idadi ya vyuo na vyuo vikuu hapa nchini ilifikia 28 mwaka 2000.  Kati ya vyuo hivyo, 9 vinatambuliwa kama vyuo vikuu vya Serikali na vya binafsi, 7 kama vyuo vikuu vishiriki na 12 vyuo vya kawaida vya mafunzo.  Idadi ya shule za msingi na Sekondari za Serikali na za binafsi inaweza kupatikana katika mtandao wa kompyuta kwa kutumia anuani: www.tzonline.org

 

·        Lugha ya kufundishia

 

Kiswahili na Kingereza ndizo lugha kuu mbili za masomo nchini Tanzania.  Kingereza ni muhimu kwa vile kinasaidia kuiunganisha Tanzania na nchi nyingine za dunia katika masuala ya teknologia, biashara na utawala.  Kiswahili nacho kinawasaidia wanafunzi katika kuendeleza mila na utamaduni wao wa Kitanzania.  Kingereza kinatumika kama somo mojawapo la lazima katika elimu ya msingi wakati ambapo katika ngazi za elimu zinazofuata (post-primary education) kinatumika kama lugha mahsusi ya kufundishia.  Kiswahili nacho kinatumika kama lugha mahsusi ya kufundishia katika elimu ya msingi na kutumika kama somo mojawapo la lazima katika elimu ya Sekondari.  Katika vyuo siyo somo la lazima.

 

·        Washika Dau/Taasisi za Elimu

 

-     Taasisi ya Elimu Tanzania:  Ilianzishwa mwaka 1964 kama sehemu ya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chuo Kikuu cha Afrika Mashariki).  Mwaka 1975 iligeuzwa rasmi kuwa taasisi ya kujitegemea chini ya Sheria ya Bunge Na. 13 ya 1975, na kuitwa Taasisi ya Elimu Tanzania. Mawasiliano yote yanafanywa kwa kupitia kwa Mkurugenzi, Taasisi ya Elimu Tanzania, S.L.P. 35094, Dar es Salaam, TANZANIA.  Simu: 255-22-73005/74420.  Fax: 255-22-74420. Waraka umeme: educate@intafrica.com

 

-     Taasisi ya Elimu ya Watu Wazima:  Ilianzishwa kwa Sheria ya Bunge Na. 12 ya       1975.  Kazi yake kubwa ni kufanya utafiti, kushauri na kushughulikia maendeleo       ya elimu ya watu wazima nchini, ikiwa ni pamoja na kuendesha kampeni za       kushawishi wananchi wajiunge na mpango wa elimu ya watu wazima.  Anuani:        S.L.P. 20679, Dar es Salaam, TANZANIA.

 

-                     Baraza la Mitihani Tanzania:  Hili ni Baraza lililoanzishwa chini ya Sheria ya Bunge Na. 23 ya 1973.  Kazi yake mahsusi ni kusimamia na kuratibu shughuli zote za mitihani hapa nchini.  Pia linatoa stashahada rasmi za elimu ya msingi, sekondari na elimu ya juu isipokuwa ya Chuo Kikuu.  Anuani:  S.L.P. 2624, Dar es Salaam, TANZANIA.  Simu: 255-22-700493/4.

 

-                     Baraza la Sanaa la Taifa:  Lilianzishwa chini ya Sheria ya Bunge Na. 23 ya 1984.  Kazi yake maalum ni kuhimiza maendeleo ya sanaa, msukumo mkubwa ukiwa kwenye muziki, sanaa za maigizo na kazi za sanaa.  Shughuli za sanaa zinafanywa na watu wasiopungua milioni 4 nchi nzima, waliojitayarisha katika makundi, vyama, Kampuni na watu binafsi.  Anuani:  Kituo cha Sanaa Ilala, S.L.P. 4779, Dar es Salaam, TANZaNIA.  SIMU:  255-22-2863749.

 

-                     Baraza la Kiswahili Tanzania:  Baraza hili limepewa jukumu la kutekeleza sera ya Kukuza lugha ya Kiswahili hapa nchini.  Vilevile imetayarisha mipango ya utekelezaji wa Sera ya Utamaduni ya 1997.  Anuani:  Coronation Building, Mtaa wa Azikiwe/Samora, S.L.P. 4766, Dar es Salaam, TANZANIA, Simu: 255-22-23452/24139.

 

-                     Tume ya Sayansi na teknologia (COSTECH).  Anuani:  SOSTECH, S.L.P. 4302, Dar es Salaam. TANZNAIA.  Simu: 255-22-2227515.  Waraka Umeme: costech@costech.opc.org

 

-                     Baraza la Usajili wa Elimu ya Juu (HEAC).  Anuani:  HEAC, S.L.P. 6562, Dar es Salaam, TANZANIA.  Simu:  255-22-2137585.

 

-                     Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE).  Anuani:  NACTE, S.L.P. 7109, Dar es Salaam, TANZANIA.  Simu: 255-22-2137585.

 

 

Title

.

Title

.

Title

.