|
Jamhuri
ya Muungano wa Tazania ilianzishwa kutokana na muungano wa nchi
huru mbili, Tanganyika na Zanzibar.
·
Tanganyika
ilipata uhuru wake tarehe 9 Desemba 1961 na kuwa Jamhuri mwaka
uliofuata (1962).
·
Zanzibar
ilipata uhuru tarehe 10 Desemba, 1963 na Jamhuri ya Watu wa
Zanzibar ilianzishwa baada ya mapinduzi ya tarehe 12 Januari 1964.
Nchi
mbili hizi ziliunda Jamhuri ya Muungano wa Tanzania tarehe 26
Aprili, 1964.
Jamhuri
ya Muungano wa Tanzania inaongozwa na Serikali ya Jamhuri ya
Muungano na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar inashughulikia masuala yasiyohusu muungano. |