.

 

Dira Jukumu

Ni kuwa kitovu cha elimu na mshauri mkuu wa serikali juu  ya mambo yanayohusiana na usimamizi wa uchumi pamoja na mipango ya muda wa kati na muda mrefu ya maendeleo ya uchumi kijamii.

Jukumu la Ofisi ya Rais, Mipango na ubinafsishaji ni kuinua kiwango cha ukuaji endelevu na na unaolingana wa uchumi, pamoja na kuboresha ustawi wa jamii kwa kuwa na usimamizi na mwongozo nzuri wa uchumi wa Taifa.

Kazi za Ofisi ya Rais Mipango na Ubinafsishaji

  • Kuandaa na kutathmini Sera za Idadi ya Watu na Uchumi

  • Kutoa miongozo ya usimamizi wa uchumi

  • Kubuni na kufanya utafiti katika nyanja mbalimbali za maendeleo ya Uchumi

  • Kutengeneza na kutekeleza mipango ya maendeleo

  • Kuratibu mipango ya maendeleo na kutoa miongozo ya bajeti kwa ajili ya matumizi ya rasilimali za Taifa

  • Kuratibu utekelezaji wa sera ya Taifa ya Idadi ya Watu

  • Kuratibu uendeshaji wa  mtandao-kompyuta wa Taifa

  • Kuhakikisha maendeleo ya nguvu kazi

  • Kutoa miongozo kuhusu mapatano ya kibiashara ya Sekta za Nchi za Nje na Mipango ya Misaada.

  • Kusimamia Baraza la Taifa la Uongezaji Tija

  • Kutoa miongozo kuhusu ubinafsishaji

  • Kuweka utaratibu wa kusimamia na kutathmini makampuni yaliyobinafsishwa

  • Kukusanya, kuandaa, kutunza, na kusambaza takwimu

  • Kuwasiliana na Mashirika ya Kimataifa na kuratibu shughuli za mashirika hayo nchini. ( Mashirika hayo ni Banki ya dunia, Shirika na Maendeleo la Umoja wa Mataifa, RDA, RCDC, MIGA, UCSID)

  • Kuandaa na kupanga mikakati ya uwekezaji katika Taasisi za umma

  • Kueleza kwa ufasaha sera na mikakati ya Maendeleo ya Sekta mbalimbali nchini

Taasisi na Mashirika

Ofisi ya Taifa ya Takwimu

Kituo cha Uwekezaji Tanzania

Baraza la Tija la Taifa

Chuo cha Mipango Dodoma

Taasisi ya Utafiti wa Kiuchumi na Kijamii (ESRF)

Chuo Cha Takwimu Cha Afrika Mashariki (EASTC)

Tume ya Rais ya Kurekebisha Mashirika ya Umma