.

 

Dira Jukumu

Dira ya ofisi ya Makamu wa Rais ni kufikia kiwango cha juu cha maendeleo endelevu kwa binaadamu, kuondoa umasikini,  matumizi mazuri ya rasilimali kwa ajili ya kujipatia riziki kwa sasa na vizazi vijavyo bila kuharibu mazingira au kuhatarisha afya au usalama; na kuendeleza umoja kati ya Serikali za Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Jukumu la Ofisi ya Makamu wa Rais ni kuandaa sera  na mikakati ya kuondoa umasikini, kulinda mazingira na mashirika yasiyo ya kiserikali  pamoja na kuratibu mambo yote yanayohusu  umoja baina ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano Tanzania na Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.

Kazi za Ofisi ya Makamu wa Rais

  • Kuratibu masuala ya Mwuungano, kiungo kati ya Serikali ya Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kuhusu mambo ambayo hayamo ndani ya Serikali ya Mwungano, Kuandaa sera zinazohusu utunzaji wa mazingira, kusimamia na kuratibu shughuli za Baraza la Mazingira la Taifa , na kupambana na umasikini.

  • Sera na mikakati. Kuratibu na kufuatilia miradi ya kuondoa umasikini katika sekta mbalimbali. Kuratibu mashirika yasiyo ya kiserikali na Mashirika ya Kijamii.

Vitengo

  • Kukomesha Umasikini

  • Mazingira

  • Mashirika yasiyo ya Kiserikali
    Kitengo cha Mashirika yasiyo ya Kiserikali kina jukumu la kuratibu shughuli za mashirika hayo nchini na kazi kubwa ya kitengo hiki ni  masuala ya sera na kanuni na kuratibu na kusimamia shughuli za mashirika yasiyo ya kiserikali ya hapa nchini na ya nchi za nje.