.

 
 

Dira Jukumu

Kuratibu na kuhakikisha kuwa utoaji wa maamuzi nchini  uunazingatia utaalam, malengo,  uadilifu, ukamilifu, kutokuwa na upendeleo, uwazi na uwajibikaji

Kuendesha nchi kwa mujibu wa katiba, kuinua hali ya maisha  na ustawi wa kijamii na kiuchumi wa Watanzania wote.

Majukumu

  • Kusimamia Baraza la Mawaziri na Utawala Bora

  • Kuzuia rushwa, utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Uchunguzi juu ya Rushwa

  • Kusimamia miiko ya uongozi, matumizi mabaya ya madaraka, uwajibikaji na uwazi

  • Kuratibu vyombo vya kitaifa vya  kuzuia rushwa ma maadili (Taasisi ya kuzuia rushwa, Tume ya Uchunguzi wa Tabia za Viongozi) na kujenga uwezo

  • Kuimarisha vyombo vya Kiesheria ( Sheria za kuzuia rushwa na mfumo wa kurekebisha maadili)

  • Kuunganisha Serikali na wananchi, ushirikishwaji, elimu, mipango ya kuzuia rushwa, na vyombo vya habari.

  • Sherehe za Kitaifa

  • Kuendeleza nguvu kazi chini ya ofisi hii

Ofisi ya Katibu Mkuu Kiongozi

Maelezo Baadaye.....

Ofisi ya Masuala ya Baraza la Mawaziri

  • Kuandaa ratiba ya mikutano ya baraza la mawaziri na kutayarisha ajenda kwa kila mkutano.

  • Kuandika  na kutunzakumbukumbu za mikutano ya baraza la mawaziri

  • Kutoa taarifa na maelezo ya maamuzi ya Baraza la Mawaziri kwa kila mtu au taasisi inayohusika na uamuzi huo na

  • Kufanya kazi na kutekeleza majukumu mengine kama itakavyoelekezwa na Mheshimiwa Rais.

Ofisi ya Utawala Bora

Ofisi ya Utawala Bora ikiwa na dira na mwelekeo wa kuunda Tanzania ambayo itazingatia sheria na kulinda haki za binaadam na ambayo itakuwa na msimamo usiyoyumba kisiasa, kiuchumi na yenye amani. Kazi za ofisi hii ni:

  • Kusimamia maadili ya uongozi wa umma, matumizi mabaya ya madaraka, uwajibikaji na uwazi

  • Kuratibu vyombo vya kitaifa vya kuzuia rushwa na vya maadili na kujenga uwezo

  • Kuimarisha uwigo wa sheria, sheria za kuzuia rushwa, maadili, na mfumo wote wa sheria

  • Kuunganisha serikali na wananchi wake, ushirikishwaji, elimu, mipango ya kizuia rushwa na vyombo vya habari

Idara zinazojitegemea Chini ya Ofisi ya Rais

Tume ya Utumishi Serikalini

Utawala na usimamizi wa utumishi serikalini (ajira, vyeo, nishamu nk.)

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Tume ya Utumishi Serikalini

Simu: (+255 22) 2120901, 2120909, 2126811–4

 

Sekretariat ya Maadili ya Uongozi
Kusimamia viongozi wa umma, matumizi mabaya ya madaraka, uwajibikaji,na uwazi; utafiti na takwimu; elimu na uenezi.

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:
Sekretariat ya Maadili ya Uongozi

Simu:(+ 255 22) 2114715, 2111810/11

 

Tume ya Uchunguzi wa Tabia za Viongozi

Kusimamia uchunguzi juu ya tabia za viongozi; utafiti na uenezi

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Tume ya Uchunguzi wa Tabia za Viongozi

Simu + 255 22 2113690; 2110607/141

 

Taasisi ya Kuzuia Rushwa

Kuzuia rushwa na utekelezaji wa mapendekezo ya Tume ya Kudumu ya Tabia za Viongozi kuhusu rushwa

 

Kwa taarifa zaidi wasiliana na:

Mkurugenzi Mkuu,

S.L.P 4865,

Dar es Salaam.

Simu:(+255 22) 2150047, 2150043 na 2150046