.

Dira Jukumu

Wizara ya Fedha inataka kufikia kiwango cha juu cha maendeleo endelevu ya kiuchumi, na uchumi uasioyumba, usimamizi mzuri wa fedha na matumizi mazuri ya fedha

Jukumu la wizara hii ni kusaidia na kukuza ubora katika usimamizi wa fedha za umma, kupanga bajeti, na thamani ya fedha, kuwa kituo cha ubora katika kuandaa sera na mikakati ya hazina, kiunua kiwango cha ujuzi kwa  wafanyakazi na kuwa na wafanyakazi wenye kuzingatia maslahi ya wateja, kusaidia na kukuza matumizi ya teknojia ya kisasa katika huduma za umma

Kazi za Wizara

  • Kuandaa mambo ya sera zinazohusiana na tathmini ya uchumi wa nchi unaojumuisha sekta zote, hazina, fedha na sera ya madeni na mikakati

  • Kusimamia masuala ya fedha kwa maslahi ya Serikali kama mwenye hisa kwa umma, na makampuni binafsi, na kuishauri serikali juu ya masuala mbalimbali kuhusu uwekezaji

  • Kutayarisha malengo ya matumizi, kupitia utendaji wa matumizi na kutayarisha miongozo ya bajeti

  • Kutayarisha na kutekeleza sera za misaada kutoka nje, kuhamasisha na kuratibu misaada kutoka nje na ushirikiano baina ya nchi za Afrika

  • Kusimamia Ulipaji wa Mishahara kwa Wafanyakazi Serikalini

  • Kusimamia shughuli zote za mapato na matumizi ya Serikali

Taasisi na Mashirika

Benki Kuu ya Tanzania

Benki Kuu ya Tanzania imeanza shughuli zake tarehe 14 Juni, 1966 chini ya sheria ya Benki Kuu ya mwaka 1965. Sheria hii inatoa ruhusa kwa Benki Kuu kufanya kazi zote kuu zinazopaswa kufanywa na Benki

Sheria ya Benki Kuu ta Tanzania ya mwaka 1965, inachukuwa nafasi ya sheria ya awali na madhumuni makubwa ya sheria hii ni kuanzisha mazingira za fedha yanayofaa kwa kuweka msimamo wa bei usioyumba.

Madhumuni ni kuanzisha na kutekeleza sera ya fedha itakayoweza kulinda mfumko wa bei na kukuza uchumi wa Tanzania

Website:www.bot-tz.org

Shirika za Bima la Taifa

Benki ya Rasilimali Tanzania (TIB)

Benki ya Posta Tanzania (TPB)

National Micro-finance Bank (NMB)

Bahati Nasibu ya Taifa

Duka la Kubadilishia Fedha za Kigeni la Taifa

Baraza la Taifa la Wahasibu na Wakaguzi wa Mahesabu (NBAA)

Shirika la Ukaguzi wa Mahesabu la Tanzania  (TAC)

Shirika la Akiba ya Wafanyakazi (PPF)

Chuo Cha Usimamizi wa Fedha (IFM)

Chuo cha Uhasibu cha Arusha

Chuo cha Uhasibu cha Dar es Salaam (DSA)

Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA)
Katika mwaka wa fedha wa 1996/97, Serikali ilianzisha sera ya hazina ili kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuboresha matumizi kwa kudhibiti matumizi kwa lengo la kupunguza nakisi katika matumizi ya serikali. Kwa upande wa mapato juhudi zilizochukuliwa ni pamoja na kuimarisha utawala kwa kuanzisha Mamlaka ya Mapato Tanzania.

Kuanzishwa kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania
Sheria ya Mamlaka ya Mapato ya mwaka 1995 ilianzisha mamlaka hii kama wakala wa serikali,  chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha.

Kazi za Mamlaka
Kazi kuu za Mamlaka ya Kodi ya Mapato ni

  • Kukadiria, kukusanya na kuhesabu matapo yote ya serikali

  • Kusimamia utekelezaji wa Sheria zote za Mapato za Serikali Kuu

  • Kuishauri Serikali juu ya mambo yanayohusu sera ya fedha

  • Kukuza ari ya wananchi ya kulipa kodi

  • Kuinua ubora wa huduma kwa walipa kodi

  • Kupambana na udanganyifu na njia nyingine za kukwepa kodi

  • Kutoa takwimu za biashara na matangazo mengine

Muundo wa Utawala wa Mamlaka ya Mapato Tanzania
 

Bodi ya Wakurugenzi
Bodi ya Wakurugenzi ndiyo kiongozi Mkuu wa Mamlaka na  jukumu lake ni kuandaa na kutekeleza sera kwa ajili ya Mamlaka, Bido ina wajume sita ambao ni:-

Mwenyekiti ambaye anateuliwa na Rais wa Jamhuri ya Mwungano wa Tanzania baada ya

  • kupata mapendekezo kutoka Wizara ya Fedha

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Muungano

  • Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar

  • Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania

  • Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania

Katibu wa Tume ya Mipango

Na wajumbe wengine wanne wanaoteuliwa na Waziri wa Fedha, ambao wana ujuzi na uzoefu katika mambo ya fedha, biashara, uchumi au sheria kutoka Taasisi za fedha, biashara, sheria au uchumi zenye maslahi katika Mamlaka.

Kamishna Mkuu

Kamishna Mkuu ni mtendaji mkuu katika Mamlaka. Chini ya usimamizi na udhibiti wa Bodi, Kamishna anawajibika na kazi za kila siku  za Mamlaka,  kusimamia fedha, mali na shughuli za Mamlaka na kuendesha,  kupanga na kudhibiti maafisa wengine na wafanyakazi wa Mamlaka.

Idara za Mapato

Mamlaka inaundwa na idara tatu za Mapato zinazoshughulikia ukusanyaji wa mapato kwa kusimamia sheria za kodi zinazohusika. Idara hizi ni:

  • Idara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT)

  • Idara ya Kodi ya Mapato

  • Idara ya Ushuru wa Forodha

Makamishna wa mapato ambao wanateuliwa na Bodi wanaongoza Idara hizi. Manaibu Kamishna wa Dar es Salaam na mikoa mingine wanamsaidia Kamishna wa Mapato. Maafisa Mapato wa Mikoa wanafanya kazi chini ya  Manaibu kamishna wa mikoa yao.

Idara Saidizi

Mamlaka ina idara saidizi saba kama zifuatavyo:

  • Ukaguzi wa Kodi na Uchunguzi

  • Fedha na Nguvu kazi

  • Habari

  • Utafiti na Sera

  • Uenezi na Elimu kwa Walipa Kodi

  • Ukaguzi wa Ndani wa Mahesabu

  • Mambo ya Sheria

Kodi zinazokusanywa na Mamlaka

Kodi za Biashara za Kimataifa

Idara ya Ushuru wa Forodha inasimamia kodi zote za biashara za kimataifa. Kodi hizi ni pamoja na kodi ya kuingiza bidhaa nchini, ushuru wa forodha na Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa zinazoingizwa nchini kutoka nje ya nchi.

Kodi ya Kuingiza Bidhaa kutoka nje ya nchi.

Kodi hii inatozwa bidhaa zinazoingizwa kutoka nje ya nchi. Kodi hii kwa kawaida inahesabiwa kama kodi ya ongezeko la thamani ya mabadilishano katika biashara kwa kuzingatia gharama ya mali iliyoingizwa pamoja na usafiri. Kodi hii inakusanywa kabla mali haijaondolewa sehemu iliyoingilia iwe ni bandari, uwanja wa ndege au mpakani kwenda nchi inayohusika au kwenye ghala au bohari inayohusika.

Kuna viwango vitano vya  kodi hii vinavyotumika:

  • 0% ( au kusamehewa kabisa) inayotumika kwa bidhaa kama mbolea, kemikali na madawa ya mimea na wanyama

  • 5% (asilimia tano) inayotumika kwa pembejeo za kilimo

  • 10% (asilimia kumi) inayotozwa kwa kuingiza mali ghafi na mali za mtaji

  • 20% (asilimia ishirini) kwa kuingiza bidhaa za kati ambazo zitauzwa tena

  • 30% (asilimia thelathini) kwa kuingiza nchini bidhaa zilizokwisha tengenezwa kwa matumizi makubwa na ya muda mrefu.

Utaratibu wa Kusawazisha Ushuru unatumia kupanga bidhaa kwa madhumuni ya kutoza kodi pamoja na kukusanya Takwimu za Biashara. Kuhimiza biashara baina ya nchi za  Umoja wa Kibiashara wa nchi za Kusini mwa bara la Afrika, (COMESA) bidhaa zinazoingizwa kutoka nchi wanachama wa Umoja huo zinatozwa ushuru wa chini ikilinganishwa na bidhaa kutoka nchi nyingine  ambazo si wanachama

Ushuru kwa Bidhaa zinazoingizwa kutoka Nje

Ushuru unatozwa kwa baadhi ya bidhaa zinapoingizwa nchini.  Kwa kawaida bidhaa zinazotozwa ushuru huu ni zile ambazo zinaonekana kama hazina maadili mazuri kwa jamii kama vile sigara, pombe na bidhaa ambazo matumizi yake yanaonekana kama ni ya anasa kama vile mafuta ya petroli.  Katika Tanzania, zaidi ya kutoza ushuru huu kwa bidhaa kama vinywaji na magari, pia zinatozwa ushuru kwa kuongeza mapato.

Ushuru wa forodha unatozwa kwa bidhaa maalum au kufuata na thamani ya bidhaa, na kima cha kodi ambayo inafuatana na thamani ya bidhaa in Thamani ya bidhaa pamoja na Usafiri na kodi ya kuingia nchini.  Viwango vya kodi inayotokana na thamani ya bidhaa ni kama vifuatavyo:

  • 10% inayotozwa magari madogo ya kutembelea yenye ukubwa wa injini unaozidi 2000cc

  • 30% inayotozwa bidhaa zote zenye matumizi ya kifahari na vipodozi

Zifuatazo ni viwango maalumu  na bidhaa zinazopaswa kutozwa ushuru kwa kiwango maalum

  • Sigara

  • Divai na pombe kali

  • Bia

  • Vinywaji baridi

  • Mazao ya Petroli

  • Saruji

Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa Bidhaa zinazoingizwa kutoka Nje

Kodi hii inatozwa kwa bidhaa zinazoingwa Tanzania Bara kwa kiwango kimoja tu cha asilimia ishirini (20%). Thamani inayotozwa kodi hii ni thamani ya bidhaa pamoja na usafiri pamoja na ushuru wa forodha na kodi nyingine zinazotwa bidhaa zinazoingizwa nchini.

Wafuatao wamesamehewa kulipa kodi ya ongezeko la thamani wanapoingiza bidhaa nchini

  • Mabalozi na maafisa wa Ubalozi

  • Bidhaa zinazoingizwa nchini chini ya Mikataba ya Misaada ya Kiufundi

  • Mizigo ya Wasafiri

  • Serikali au Taasisi zake, endapo bidhaa zinazoingizwa zitatumika kukisaidia chombo kinachohusika kutelekeza majukumu yake.

  • Rais wa Jamhuri ya Mwuungano wa Tanzania

Uingizaji wa bidhaa zifuatazo umesamehewa kodi ya Ongezeko la Thamani

  • Madawa ya kuulia wadudu, mbolea n.k.

  • Bidhaa za kutolea huduma ya afya

  • Zana za Elimu

  • Vitabu na Magazeti

Bidhaa zote za kibishara zinazosafirishwa kuja nchini zenye thamani ya zaidi ya dola za Kimarekani elfu tano (US $ 5,000/=) ni lazima zikaguliwe. Kampuni iliyopewa kazi hii ni “Societe Generale de Surveillance” ya Afrika ya Kusini (SGS) Kampuni hii inapaswa kuhakikisha ubora, wingi, thamani na kiwango cha daraja la kodi vipo sawa kama vilivyoonyeshwa na msafirishaji.

Bidhaa chache zilizochaguliwa, ambazo ni maarufu kwa kukweka kodi, ni lazima zikaguliwe bila kujali ni nani anayezisafirisha.

Dhahabu, vito vya thamani na madini, kazi za sanaa, baruti, mabomu na silaa za kivita, wanyama na bidhaa zinazooza, magazeti mapya na majarida, vifaa vya majumbani na  vifaa vya wasafiri vimesamehewa ukaguzi. Bidhaa nyingine zilizosamehewa kukaguliwa ni zile zinazoingiwa na mabalozi au wafanyakazi wa ofisi zao, mashirika ya dini, mashirika ya misaada au magari mapya yanayoingizwa na  wawakilishi wa makampuni yanayotengeneza magari.

Kodi ya Matumizi:


Kodi ya Ongezeko la Thamani kwa Bidhaa za hapahapa nchini

Kodi ya Ongezeko la Thamani ni kodi inayotozwa katika bidhaa na huduma mbalimbali Kodi hii inatozwa kwa kila thamani inayoongezwa kwa bidhaa au huduma na wazalishaji na wafanya biashara katika kila hatua ya uzalishaji au usambazaji. Wafanyabishara wanasajiliwa kama mawakala wa kukusanya kodi hii kwa niaba ya serikali. Kodi hii ilianzishwa Tanzania tarehe 1 Julai mwaka 1998 na inachukuwa nafasi ya kodi za mauzo ya bidhaa na huduma, stakabadhi na stemp ya ushuru, kodi ya hoteli, na kodi ya viburudisho walizokuwa wanatozw3a wafanya biashara waliosajiliwa kulipa kodi ya ongezeko la thamani.

Kodi ya Ongezeko la Thamani inatozwa kwa kiwango kimoja tu cha asilimia ishirini (20%). Thamani inayotozwa kodi kwa bidhaa na huduma za hapa hapa nchini ni kiasi cha fedha ambacho mteja amelipa kununua bidhaa au huduma, au thamani ya soko huru ya bidhaa au huduma.

Hakuna kodi ya Ongezeko la Thamani kwa bidhaa zinazouzwa nje ya nchi. Lakini Wafanya Biashara waliosajiliwa kulipa kodi hii ambao wanasambaza bidhaa na huduma kwa ajili ya kusafirisha nje ya nchi wanaweza kudai kurejeshewa kodi hii katika bidhaa wanazoingiza kutoka nje. Utaratibu huu unawasaidia wafanyabiashara hawa kuingia katika soko la Kimataifa na kuwafanya waweze kuhimili ushindani.

Shughuli za ugavi wa bidhaa na huduma nyingi muhimu ambazo zinatumiwa kwa wingi na wananchi wenye kipato cha chini hazitozwi kodi ya Ongezeko la Thamani. Na Endapo mfanyabiashara atasamehewa kulipa kodi ya Ongezeko la Thamani, haruhusiwi kuwatoza kodi hiyo wateja. Aidha hawana haki ya kudai kurejeshewa kodi hiyo wakati  wanapolipa kodi kwa ajili ya manunuzi ya bidhaa au huduma.

Ugavi wa baadhi ya bidhaa na huduma zimepewa msamaha maalum wa kodi ya ongezeko la thamani. Hizi ni bidhaa au huduma zinazotolewa kwa Serikali au Taasisi zake kwa ajili ya matumizi ya kuiwezesha serikali au Taasisi hizo kutekeleza majukumu yao ya kikatiba.  Bidhaa au huduma ambazo zimesamehewa kulipa kodi, zinatozwa kodi, lakini kodi hiyo baadaye inarudishwa kwa muhusika. Wafanyabiashara wanaosambaza bidhaa na kuduma kwa serikali na taasisi zake zinaruhusiwa kupata muamana wa kodi wanaponunua bidhaa au huduma.

Ushuru wa Forodha kwa Bidhaa Zinazotengenezwa Nchini

Ushuru wa forodha pia unatozwa kwa bidhaa zinazozalishwa hapa nchini. Kwa kawaida ushuru huu unatozwa kwa sigara na bia na bidhaa nyingine ambazo matumizi yake yanaonekana kama ni ukiukaji wa maadili mema ya jamii. Ushuru huu pia unatozwa kwa vinywaji baridi kwa ajili ya kuongeza mapato. Aidha katika utozaji wa ushuru wa forodha kuna viwango maalum au kwa kufuata thamani ya bidhaa inayohusika.  Kiwango cha chini cha Kodi hii ni asilimia kumi na kiwango cha juu ni asilimia thelathini.

Ushuru wa Stempu

Ushuru wa Stempu unatozwa kwa kiwango cha asilimia mbili ya mapato ya wafanyabiashara wenye mikataba na mamlaka ya Mapato Tanzania. Kwa wafanyabiashara ambao wanatumia mihuri inayopigwa juu ya stakabadhi zao za malipo, wanalipa asilimia 3.6% ya mauzo.  Ushuru huu unalipwa na wafanyabiashara ambao hawakujisajili kulipa kodi ya ongezeko la thamani.

Kodi ya Magari.

Licha ya kodi za kuingiza magari nchini, magari yanatozwa kodi mbalimbali ambazo zinakusanywa na Idara ya Kodi ya Ongezeko la Thamani kama zifuatazo:

Kodi ya Kusajili Gari

Kodi hii inakusanywa wakati gari linaposajiliwa kwa mara ya kwanza nchini. Kodi  ni inatozwa kwa kiwango  kimoja tu cha Sh. 95,000/= kwa kila gari inayosajiliwa na Sh. 32,000/ kwa kusajili pikipiki.

Kodi ya Faida itokanayo na Gari

Makampuni yote binafsi ya biashara ambayo hayajihusishi ya biashara ya usafirishaji wanalazimika kulipa sh. 100,000 kwa kila gari inayomiliki.

Malipo ya Kibali cha Magari ya Kigeni na yanayoingizwa nchini kwenda nchi jirani.

Magari yote ya kigeni yanayoingizwa nchini kwa muda yakiwa njiani kwenda nchi nyingine yanalipa ada ya dola za Kimarekani ishirini kwa kila siku thelathini yanapokuwa hapa nchini.  Magari ya kigeni ya kibiashara yenye matela (ekseli) matatu yanatozwa dola za Kimarekani sita zaidi kwa kila kilometa mia moja yanayotembea hapa nchini.

Kodi ya Mapato, Faida na Utajiri kwa Ujumla.

Kodi ya Mapato ya Kampuni

Makampuni yote yaliyosajiliwa na/au kufanya biashara zao nchini, yanatozwa kodi kutokana na faida wanayopata kwa kiwango cha asilimia thelathini . Kwa kawaida kodi hii inalipwa katika ngazi mbili.  Katika hatua ya kwanza mlipa kodi anakadiria mwenyewe mwanzoni mwa mwaka wa biashara., na katika hatua ya mwisho kodi inalipwa baada ya maafisa wa kodi kufanya tathmini ya mapato yote ya kampuni katika mwaka unaohuiska.

Katika kufikia kiwango cha mapato ya kutozwa kodi au faida, punguzo linaruhusiwa kwa matumizi yote yaliyotumika katika mwaka unaokusudiwa kwa ujumla au kwa kiasi cha uzalishaji wa mapato hayo.

Aidha punguzo la matumizi na uchakavu linaruhusiwa kwa mashine zinazomilikiwa na kampuni inayohusika na ambazo zinatumika katika biashara.  Utaratibu wa kuzingatia uchakavu unatumiaka na kufuata viwango vifuatavyo. Asilimia 37.5 kwa mashine za daraja la kwanza ambazo ni pamoja na matrekta, mashine za kuvunia mazao ya kilimo, mashine za kuchimbia ardhi na nyingine kama hizo.  Asilimia ishirini na tano kwa mashine za daraja la pili  kama vile ndege na asilimia 12.5 kwa mashine nyingine kama meli.

Punguzo la Uchakavu kwa majengo ni asilimia nne kwa majengo ya viwanda na asilimia sita  majengo ya mahoteli. Aidha kuna bonasi ya asilimia ishirini ya punguzo la kuwekeza linaloruhusiwa kwa matumizi ya majengo ya viwanda, mahoteli na mashine zinazowekwa humo.

Katika sekta ya kilimo, asilimia ishirini inaruhusiwa kwa ujenzi wa karakana zote za kilimo. Asilimia 100 inaruhusiwa kwa matumizi ya mtaji katika kilimo na upandaji wa mazao ya kudumu na asilimia 100 inaruhusiwa kwa matumizi ya mtaji katika kuzuia mmomonyoko wa udingo katika ardhi inayotumika kwa kilimo.

Kodi ya Mapati ya Mtu Binafsi

Kodi hii inatozwa kwa wananchi kutokana na mapato yao kwa mwaka duniani kote na kwa Tanzania inatozwa kutokana na mapato ya wakazi wasio raia wa nchi hii. Mapato yananyotozwa kodi ni pamoja na mapato yote au faida kutoka katika biashara zao, ajira au huduma wanazotoa, gawio au riba wanayopata kutoka benki zinazofanya kazi hapa nchini. Kodi hii inatozwa kufuatana na kipato cha muhusika na kuna mafungu kumi na mbili ya vipato kuanzia sh. 20,000. Kiwango cha chini cha kodi ni asilimia 7.5 na kiwango cha juu ni asilimia thelathini na tano kwa vipato vinavyozidi sh. 700,000.  Mafungu ya viwango vya kodi hii yanapatikana katika jedwali na. 1.

Kodi ya mapato kwa watu binafsi nchini Tanzania inakusanywa kwa kutumia njia mbili. Kwa waajiriwa wenye mishahara kodi hii inaitwa PAYEE na inakusanywa na waajiri kwa kutumia viwango vilivyotajwa hapo juu wakati wa kutayarisha mishahara. Waajiri wanawajibika kuwasilisha kodi hii kwa Kamishna wa Kodi za Mapato. Njia ya pili inatumika kwa wafanya biashara na wananchi waliojiajiri wenyewe ambapo makisio ya mapato yao ya mwaka yanatokana na mapato waliyoonyesha wakati wa kuomba leseni za biashara.  Na hawa wanatakiwa kulipa kodi hii kila baada ya miezi mitatu.

Kodi ya Mishahara

Kodi hii inalipwa na waajiri binafsi wenye wafanyakazi wanne au zaidi.  Kwa sasa kodi hii inatozwa kwa kiwango cha asilimia nne ya mishahara ya wafanyakazi. Kodi hii haikatwi kutoka kwenye mishahara ya wafanyakazi.

Zuio la Kodi

Zuio ni mpango wa ulipaji kodi unaosimamiwa na Idara ya Kodi ya Mapato ambapo kodi inayotozwa inabaki katika sehemu inayokusanywa. Kodi zinazobakizwa zinapunguzwa wakati wa malipo ya kodi binafsi au kodi binafsi za makampuni kwa walipa kodi wazawa,  na kama kodi hiyo ni malipo ya mwisho kwa  walipa kozi wageni.  Kama kuna riba, gawio na mapato ya pango, kodi hii ni ya mwisho kwa wananchi wazawa na wageni.

Riba

Mtu yeyote anayepata riba inayozidi sh. 150,000/= anawajibika kulipa kodi ya zuio kutokana na riba anayopata. Na kiwango kinachotumika ni asili mia 15% kwa wote wazawa na wageni. Taasisi za fedha ni mawakala wa kukusanya kodi hii.

Gawio

Gawio linalipwa kwa raia wa nchi hii  kutoka Kampuni iliyorodheshwa katika Soko la Hisa la Dar es Salaam linapaswa kulipowa kodi ya gawio kwa kiwango cha asilimia tano (5%) na asilimia kumi na tano (15%) kwa makampuni yasiyoorodheshwa. Pato la gawio lilolipwa kwa mkazi mgeni linatozwa asilimia ishirini bila kujali kama kampuni inayohusika imeorodheshwa au la. Kodi ya Gawio inapaswa kubaki katika kampuni kama kodi ya mwisho.  Katika Sekta ya madini magawio yanayotolewa kwa wakazi wageni yanatozwa kodi kwa kiwango cha asilimia kumi (10%). Makampuni yanayotangaza magawio ndiyo wakusanyaji wa kodi hii.

Pango.

Mapato yanayotokana na kukodisha na kupangisha yanayozidi sh. 500,000/= kwa mwaka yanapaswa kulipiwa kodi ya zuio, ambayo pia ni kodi ya mwisho ya mapato kwa aina hii ya mapato. Kodi hii inatozwa kwa kiwango cha asilimia 15 kwa wazawa na asilimia 20 kwa wageni.

Ada ya Usimamizi na Utaalam

Malipo yanayofanywa kwa mkazi mgeni, zaidi ya malipo yanayofanywa kwa mwaajiriwa na mwajiri wake, yanayochukuliwa kama huduma yoyote ya utawala, ufundi au utaalam yanapaswa kulipiwa kodi ya salio ya asilimia  ishirini (20%). Kwa sekta ya madini kodi ya zuio ya asilimia tatu (3%) inatozwa kwa makandarasi wadogo na ada ya usimamizi endapo ada ya usimamizi haizidi asilimia mbili ya gharama za uendeshaji.

Bidhaa na Huduma

Malipo ya utoaji wa bidhaa na huduma, ukiondoa kodi ya ongezeko la thamani, yanatozwa kodi ya zuio ya asilimia mbili kwa kila  malipo  kwa malipo yote ambayo ni sawa au zaidi ya sh. 100,000/=. Wazunuzi wa bidhaa na huduma kama hizo wanapaswa kuwa mawakala wa serikali wa kukusanya kodi ya zuio.  Wanaomiliki hati za machimbo ya madini wanasamehewa kulipa kodi za zuio kwa bidhaa au huduma za hapa hapa nchini ingawa wanapaswa kubakisha kodi hiyo kwa wanaotoa huduma au bidhaa hizo.

Kodi nyingine za zuio

Kodi nyingine za zuio ni

  • Kodi ya Chanzo cha Mapato

  • Ada ya hati miliki (asilimia 20)

  • Malipo ya Pensheni kwa wageni (asilimia 15)

  • Ushuru wa barabara (kwa wazawa) (asilimia 4)

  • Ushuru wa barabara (kwa wgeni) (asilimia 15)

  • Kodi ya Usafirishaji wa meli (asilimia 2)

  • Ukodishaji wa ndege (asilimia 10)

  • Asilimia ya Faida inayotokana na biashara ya Bima (asilimia 7.5)

  • Kodi za matumizi

  • Kodi ya Huduma za Kuondokea Katika Viwanja vya Ndege
    Kodi ya Huduma za Kuondokea za Uwanja wa Ndege inatozwa kwa wasafiri wote wa ndege wazawa na wageni  katika viwanja vya ndege nchini. Wasafiri wa ndani wanalipa sh 2,000/= kwa kila safari na wasafiri wanaokwenda nje ya nchi wanalipa dola za Kimarekani ishirini (US $ 20) kwa kila safari.  Kodi hii inajumushwa katika bei ya tiketi na mawakala wa mashirika ya usafiri wanapaswa kuwa mawakala wa serikali katika kukusanya kodi hii. Abiria wanaopita na watoto chini ya miaka miwili wamesamehewa kulipa kodi hii.

  • Kodi ya Huduma za Kuondokea Bandarini
    Kodi hii inatozwa kwa abiria wanaosafiri  kwenda humu humu nchini na  nchi za nje kwa kutumia meli za abiria. Wananchi wazawa wanalipa sh 500/- na wageni  wanaosafiri kwa kutumia bandari za Jamhuri ya Mwuungano ya Tanzania wanalipa dola za Kimarekani tano kwa kila safari. Kodi hii pia imejumuishwa katika bei ya tiketi.

Idara ya Kusimamia Bima

Idara hii ni wakala wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ya Tanzania ilianzishwa chini ya kifungu Na. 5 cha sheria ya Bima  Na 18 ya mwaka 1996 ili kutoa leseni na kurekebisha mifumo yote ya biashara ya bima nchini. Idara hii inaongozwa na Kamishna wa Bima 

Kwa maelezo zaidi wasiliana na  IDS@Africa-online.co.tz