|
Dira |
Jukumu |
|
Dira ya
Wizara hii ni kuhakikisha utunzaji endelevu wa mali asili,
utamaduni na Utalii na kuhakikisha ushirikishwaji wa jamii
zinazohusika, mashirika yasiyo ya kiserikali na kusimamia
matumizi ya mali asili kwa faida ya vizazi vya sasa na vijavyo
|
Jukumu la
wizara hii ni kuandaa sera na mikakati ambayo itaongoza
utunzaji endelevu wa mali asili, utamaduni na mazingiza.
Kuinua na kuongeza aina ya vivutio vya utalii na kuongeza
mchango wa sekta hii kwa pato la taifa na uingizaji wa fedha
za kigeni.
|
|
Kazi za Wizara |
-
Kusimamia sera ya Utalii,
Maendeleo ya Hifadhi za Taifa, Mbuga za Wanyama, Maendeleo ya fukwe na vivutio
vya utalii, urithi wa taifa, makumbusho na kumbukumbu nyingine,
mali asili, misitu na upandaji miti, uvuvi na
ufugaji wa nyuki.
-
Kuendeleza nguvu kazi
chini ya Wizara
-
Kusimamia shighuli za
Idara Kuu za Serikali, Mashirika ya Umma na miradi iliyo chini ya Wizara
-
Kusimamia shughuli za
mawakala wa Serikali walio chini ya Wizara
|
|
Taasisi na
Mashirika |
Sekta ya Misitu
-
Taasisi ya Utafiti wa
Misitu Tanzania (TAFORI)
S.L.P. 1854 Morogoro,
Tanzania
Simu: 255 023 2263725
Taasisi hii inafanya
utafiti kugundua na kusambaza maarifa ya kisayansi kwa washikadau ambayo
itachangia usimamizi na maendeleo endelevu ya rasilimali za misitu nchini.
-
Mpango wa Taifa wa Mbegu
za Miti (NTSP)
S.L.P. 373 Morogoro,
Tanzania
Simu: 255 023 2563192
Fax: 255 023 2563275
Mpango huu unafanya kazi
kama kitengo chini ya Idara ya Misitu na unawajibika kukusanya mbegu za misitu
zanye ubora nzuri kwa madhumuni ya kutosheleza mahitaji ya mbegu za miti nchini
na kusafirisha nchi za nje.
-
Chuo cha Misitu cha Olmotonyi
S.L.P. 943, Arusha
Tanzania
Simu: 255 027 50441
Chuo hiki kinatoa mafunzo
ya vyeti na stashahada za Misitu na Ufugaji wa Nyuki. Aidha kuna vituo vya
mafunzo kwa wafanyakazi wa Misitu huko Iringa na Rongai, Moshi.
-
Chuo Kikuu cha Kilimo cha
Sokoine
Kitivo cha Misitu, Morogogo,
Tanzania
Simu: 255 023 2263511
E-mail:
Forestry@hhettan.gn.apc.org au
Forestry@costach.gn.apc.org
Kitivo kinatoa digrii za
kwanza za Sayansi katika misitu (B.Sc. in Forestry)
Sekta ya Uvuvi
Taasisi ta Utafiti wa
Uvuvi Tanzania (TAFIRI)
Shughuli za utafiti
zinafanywa kwenye maji ya bahari na maji ya mengine (mito, mabwawa,na maziwa).
Taasisi inashughulika na utafiti katika rasilimali za uvuvi na kusambaza matokeo
ya utafiti kwa ajili ya maendeleo ya uvuvi na matumizi endelevu ya rasilimali
hii nchini. Taasisi pia inatoa mafunzo na kufanya utafiti juu ya teknolojia ya
uvuvi na tathmini ya idadi ya samaki.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Wizara ya Mali Asili na
Utalii
Idara ya Uvuvi
S.L.P 2462, Dar es Salaam,
Tanzania.
Simu: 255 022 2650043/44
Chuo cha Mafunzo ya
Uvuvi cha Kunduchi
Chuo hiki kinatoa mafunzo
ya stashahada za Uvuvi. Mafunzo haya ni pamoja na uhandisi wa vyombo vya majini,
uvuvi, teknolojia ya vyakula vinavyotokana na samaki, na sayansi ya ubaharia.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi
cha Kunduchi
S.L.P. 60091, Dar es
Salaam, Tanzania
Simu: 255 022 2650011
Kituo cha Maendeleo ya
Uvuvi cha Mbegani
Kinatoa mafunzo ya
stashahada ya uvuvi. Mafunzo hayo ni pamoja na uundaji wa mashua, usindikaji wa
samaki na udhibiti wa ubora, ufundi mitambo wa vyombo vya majini, uhandisi wa
vyombo vya majini na mafunzo mengine yanayotolewa kwa vikundi maalum.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Kituo
cha Maendeleo ya Uvuvi cha Mbegani
S.L.P. 83, Bagamoyo,
Tanzania
Chuo cha Mafunzo ya
Uvuvi cha Nyegezi
Kinatoa mafunzo ya
stashahada ya uvuvi
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Chuo cha Mafunzo ya Uvuvi
cha Nyegezi
S.L.P. 1213, Mwanza,
Tanzania
Sekta ya Wanyamapori
Mamlaka ya Hifadhi za
Taifa Tanzania (TANAPA)
Hili ni shirika la umma
ambalo kazi yake ni kurekebisha, kuendeleza na kusimamia hifadhi za taifa za
Serengeti, Tarangire, Arusha, Kilimanjaro, Ruaha, Manyara, Katavi na Mikumi.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na
Mamlaka ya Hifadhi za Taifa
(TANAPA)
S.L.P. 3134, Arusha,
Tanzania
Simu: 255 27 2508040
Fax: 255 27 2508216
E-mail:
tanapa@habari,co,tz
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo la Ngorongoro
Eneo lililo chini ya
Mamlaka haya ni kilometa za mraba elfu nane na mia tatu (8,300). Eneo hili
linajumuisha wanyamapori, binaadam , na maeneo ya kumbu kumbu za kihistoria
barani Afrika. Pia linaongoza kwa majaribio ya matumizi ya aina mbalimbali ya
ardhi.
Kazi za Mamlaka
-
Kuendeleza maisha ya
pamoja ya binaadam na wanyama pori katika
mfumo wa asili na utamaduni.
-
Kuhifadhi anuwai ya
kibaiolojia na msimamo wa kiikolojia wa mfumo wa ikolojia wa Serengeti na
Milima ya Ngorongoro.
-
Kuhifadhi maeneo kuhimu
kimataifa katika kumbukumbu ya mambo ya kale
-
Kutunza na kuendeleza
yale yote ambayo yameifanya sehemu hii ya nchi yetu kuwa sehemu muhimu ya urithi
wa dunia na hifadhi ya sehemu ya dunia ambayo uhai unawezekana kuwepo.
Kwa taarifa zaidi wasiliana
na:
Mamlaka ya Hifadhi ya eneo
la Ngorongoro
S.L.P. 1, Ngorongoro,
Tanzania
Simu: 255 27 2504619
Fax: 255 27 2503339
E-mail:
ncaa-hq@yako.habari.co.tz
Taasisi Utafiti wa
Wanyamapori Tanzania (TAWIRI)
Taasisi hii inafanya
utafiti wa wanyama pori na magonjwa ya wanyamapori.
-
Inakusanya, kuhifadhi na
kusambaza matokeo ya utafiti kuhusu wanyamapori na kutoa ushauri juu ya
maendeleo endelevu ya rasilimali za wanyamapori kwa washikadau.
-
Kuratibu shughuli za
utafiti zinazofanywa na watafiti kutoka nje ya nchi kwa kushirikiana na Tume ya
Sayansi na Teknolojia.
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Taasisi ya Utafiti wa
Wanyamapori
S.L.P. 661, Arusha Tanzania
E-mail:
harawii@online.no
Chuo cha Maafisa wa
Wanyamapori cha Afrika
Kazi zake
Kutoa mafunzo kwa maafisa
wanyamapori kwa nchi za Kiafrika zinazozungumza Kiingereza.
Kwa taarifa zaidi wasiliana na
Chuo cha Maafisa wa
Wanyamapori cha Afrika
S.L.P. 32031, Moshi,
Tanzania
Fax: 255 27 2551113
Sekta ya Utalii
Bodi ya Utalii Tanzania
Bodi ya Utalii inakuza
maendeleo ya Utalii Tanzania
Kazi zake
-
Kuzitangaza sehemu za
utalii Tanzania ndani na nje ya nchi.
-
Kendesha kampeni za
matangazo (Kutangaza, uhusiano na umma, maonyesho ya barabarani) kwa lengo la
kuwavutia watalii.
-
Kuandaa na kuchapisha
vipeperushi na nyaraka nyingine za matangazo
-
Kutoa taarifa za Kitalii
Kufanya utafiti wa
masoko ili kutoa taarifa mpya za kumbukumbu za utalii nchini
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na.
Bodi ya Utalii Tanzania
S.L.P. 2485, Dar es Salaam,
Tanzania
Simu: 255 22 2110908,
2111244/5 2136105
Fax: 255 22 2116420
E-mail:
md@ttb.ud.or.tz au
Safari@ud.co.tz
Mtandao:http://www.tanzania-web.com/home2.htm
Chuo Cha Mafunzo ya
Hoteli na Utalii
Kazi zake
Kwa taarifa zaidi
wasiliana na:
Chuo Cha Mafunzo ya Hoteli
na Utalii,
|
|