.

Dira Jukumu

Dira ya Wizara ya Mawasiliano na Uchukuzi ni kutoa miundo mbinu ya kuaminika na huduma nzuri za usafiri na mawasiliano

Kutoa huduma nzuri na bora za usafiri na mawasiliano nchini na kimataifa.

Kazi za Wizara

  •  Kusimamia utekelezaji wa Sera ya Mawasiliano na Uchukuzi, Leseni za Uchukuzi, Viwanja vya Ndege,  viwanja vidogo vya ndege,  Usafiri wa Anga, Utabiri wa Hali ya Hewa, Posta na Simu, Reli, Ndege za Serikali, Usafiri  na Uchukuzi kwa kutumia ndege, bandari, huduma za zimamoto katika kiwanja cha ndege.

  • Kutoa mafunzo kwa Wafanyakazi wa Wizara hii

  • Kusimamia Idara, mashirika ya umma na miradi iliyo chini ya Wizara

  • Kuratibu shughuli za Mawakala wa Serikali zilizo chini ya Wizara hii

Taasisi na Mashirika

Mamlaka ya Kanuni za Usafirishaji Tanzania (TTRA)

Serikali itaanzisha Mamlaka ya Kanuni za Usafirishaji Tanzania (TTRA) hivi karibuni. Mamlaka haya yataanzishwa chini ya Sheria ya Kanuni za Ushafirishaji na yatakuwa na jukumu la kusimamia uendeshaji nzuri wa barabara na usafiri wa barabara, reli, bandari, usafiri wa majini, viwanja vya ndege na usafirishaji kwa njia ya anga.

Mamlaka ya Usafiri wa Anga Tanzania (TCAA)

Taasisi hii iliundwa Marchi, 1999. Kazi kubwa ya Mamlaka ni

  1. Kurekebisha shughuli za Usafiri wa anga katika Tanzania

  2. Kutumia viwango vya usafiri wa anga vya kimataifa

  3. Kukagua na kusajili ndege

  4. Kutoa ushauri kwa  waendeshaji wa shughuli za usafiri wa anga na watumiaji

  5. Kuhakikisha kuwa sheria zinafuatwa

  6. Kutoa mafunzo na leseni kwa marubani na wahandisi wa ndege

  7. Kutoa leseni ya viwanja vya ndege

Mamlaka ya Leseni za Usafiri shaji Tanzania (CTLA)
Taasisi hii kazi yake ni kusimamia utekelezaji wa kanuni na sheria. Kazi yake kubwa ni kutoa leseni za usafiri wa barabara.  Mamlaka ya Leseni za Usafiri za mikoa zimeruhusiwa kutoa leseni kwa wasafirishaji katika mikoa inayohusika.

Tanzania Central Freight Bureau (TCFB)
Sheria ya mwaka 1982 iliyoanzisha kampuni hii imerekebishwa mwaka 2000 ili kwenda na mabadiliko katika mazingira ya soko. Wajibu wa Kampuni hii ni kuharakisha maendeleo katika sekta ya usafiri wa majini kwa kusimamia  na kuhakikisha kuwa kunakuwa na ushindani na biashara halali kwa nia ya kuinua maendeleo ya biashara hiyo na kuhakikisha upatikanaji wa taarifa za usafiri wa majini.

Tume ya Mawasiliano ya Tanzania (TCC)
Tume ya Mawasiliano ilianzishwa chini ya sheria ya Mawasiliano ya Tanzania Na 18 ya mwaka 1993 ambayo ilianza kutumika mwaka 1994. Tume iliundwa kufuatia kuvunjwa kwa Shirika la Posta na Simu ikiwa ni sehemu ya juhudi za serikali za kuunda upya sekta ya mawasiliano. Tume ina jukumu la kurekebisha shughuli za watoa huduma za posta na simu. Majukumu mengine ni  kufanunua sera za kuunganisha simu na viwango vya bei, kugawa na kusimamia njia za Redio, na kutayarisha mipango ya namba, kupanga taratibu za kugawana mapato, na kusimamia  na kuona kuwa viwango vilivyowekwa vinafuatwa.

Shirika la Utabiri wa Hali ya Hewa

Kwa habari zaidi wasiliana na
Mkurugenzi Mkuu
S.L.P. 3056
Simu: 255 22 2110231
Dar es Salaam
E-mail:  met@meteo_tz.org