|
Mfuko wa Huduma za Jamii
(NSSF)
Mfuko wa Huduma za Jamii (NSSF)
ulianzishwa chini ya Sheria ya Bunge Na. 28 ya mwaka 1997 ambayo imeanza
kutumika kuanzia Tarehe 1 Julai mwaka 1998.
Mfuko huu unahudumia sekta
yote binafsi nchini, waliojiajiri na kila mtu ambaye hana mpango mwingine wa
mafao.
Kwa mujibu wa Sheria
iliyoanzisha mfuko huu, mfuko huu unatoa mafao ya aina mbili; mafao ya muda
mfupi na ya muda mrefu. Mafao ya mudamfupi ni pamoja na msaada wa mazishi, uzazi,
kuumia kazini na huduma za matibabu. Mafao ya muda mrefu ni mafao ya uzee,
kutojiweza kutokana na maradhi, malipo kwa wafiwa na malipo maalum yanayotolewa
kwamkupuo. Wakati mafao yote ya muda mrefu yanatolewa na Mfuko hivi sasa, mafao
ya muda mfupi yanayotolewa ni misaada ya maziko na uzazi tu. Hata hivyo
matayarisho yapo katika hatua za mwisho kwa ajili ya kutoa mafao ya kuumia
kazini na huduma za afya.
Mamlaka ya Vyuo vya
Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA)
Sheria mpya ya elimu na
mafunzo ya ufundi stadi ilipitishwa bungeni mwaka 1994. Chini ya sheria hii mpya,
taratibu za kutoa mafunzo ya ufundi stadi zimeimarishwa kwa kuanzishwa Mamlaka
ya Vyuo vya Mafunzo ya Ufundi Stadi (VETA) ambayo kazi yake ni kusimamia
maendeleo ya mafunzo ya ufundi stadi nchini. Mamlaka hii inaongozwa na bodi
ambayo ina wawakilishi kutoka serikalini, waajiri, vyama vya wafanyakazi na
taasisi zisizo za kiserikali.
Taasisi ya Uongezaji
Tija (NIP)
Taasisi hii imeanzishwa ili
kuinua huduma za ushauri, na kusimamia mafunzo kwa nia ya kuongeza tija. Taasisi
hii imeanzishwa chini ya Sheria ya Mashirika ya Umma ya mwaka 1969 na Tangazo la
Serikali Na 124 la tarehe 10 Mei, 1974.
Hivi karibuni, Taasisi hii
imeanza kuzisaidia sekta binafsio hasa zile zinazoendeshwa na watu wenye kiwango
kidogo cha elimu kama vikundi vya akina MAMA LISHE na wafanyakazi na wamiliki wa
migahawa midogo midogo na kantini.
Taasisi ya Taifa ya Mafunzo ya Ustawi wa
Jamii
Taasisi hii imeanzishwa kwa
ushirikiano baina ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya Uholanzi kupitia
Shirika la Maendeleo la nchi hiyo (NVIB). Taasisi hii imeanzishwa chini ya
sheria ya Bunge Na. 26 ya mwaka 1873.
Chuo kinaendesha mafunzo na
kozi za aina mbalimbali kama ifuatavyo;
-
Stashahada ya Juu ya
Ustawi wa Jamii
-
Stashahada ya Juu ya
Usimamizi Kazini
-
Cheti cha Ustawi wa
Jamii
-
Cheti cha Usimamizi
Kazini
|