.

Dira Jukumu

Mwelekeo wa Wizara hii ni kuwa na jamii yenye mtazamo wa kijinsia ambayo itakuwa na uwezo wakutambua matatizo na uwezekano wa kuinua ubora wa maisha kijamii na kiuchumi.

Jukumu la Wizara hii ni kusaidia uundaji, utekelezaji, na kusimamia sera zinazolenga jinsia katika jamii,  kutengeneza mazingira yatakayoweza kujenga uwezo wa wanawake na wanaume kushiriki kikamilifu katika shughuli za maendeleo ya kijamii na kiuchumi.

Kazi za Wizara

  • Kuanzisha sera ya maendeleo ya wanawake na watoto

  • Kupiga vita dhidi ya unyanyasaji wa watoto na ajira kwa watoto

  • Kupigania usawabaina ya wanawake na wanaume katika nyanja za kijamii na kisiasa

  • Kutoa mafunzo kwa wanawake juu ya masuala ya kiuchumi na kijamii

  • Kuifahamisha jamii juu ya athari za kuwabagua wanawake

Vyuo vya Maendeleo ya Jamii

Tengeru          -           Arusha
Buhare            -           Musoma
Rungemba      -           Mafinga
Misungwi         -           Mwanza

Vyuo vya Maendeleo Vijijini

Uyole               -            Mbeya

Mlale                -            Songea
Monduli            -            Arusha

Mabughai        -            Lushoto