MAENDELEO
YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA
SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU
KATIKA MAENDELEO | |
|||||||
| MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | |||||||
Hali
ya Uchumi wa Taifa |
|||||||
FEDHA
ZA SERIKALI |
|||||||
MAPATO
72. Sera za bajeti ya mwaka 2003/04 zililenga kutekeleza Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Mkakati wa Kupunguza Umaskini na kuchochea maendeleo ya nchi kwa ujumla. Kwa kuzingatia sera hizo, bajeti ya Serikali ililenga kukusanya mapato ya ndani ya sh. 1,393,026 milioni, sawa na asilimia 13.3 ya Pato la Taifa, ikilinganishwa na asilimia 12.3 mwaka 2002/03. Mapato yatokanayo na kodi yalikadiriwa kufikia jumla ya sh. 1,264,161 milioni na yale yasiyo ya kodi sh. 128,865 milioni. Misaada na mikopo kutoka nje ikijumuisha mapato yanayotokana na msamaha wa deni la nje kwa utaratibu wa HIPC, ilikadiriwa kufikia jumla ya sh. 1,014,911 milioni. Mapato
ya Ndani 74. Katika kipindi cha Julai – Desemba 2003, mwenendo wa mapato ya ndani ulikuwa wa kuridhisha kutokana na kuongezeka kwa ufanisi katika ukusanyaji wa kodi, hususan kodi ya ongezeko la thamani (VAT) kwa bidhaa ya petroli inayoagizwa kutoka nje ya nchi na kodi ya mapato. Pia, makusanyo ya kodi katika kipindi hicho nayo yalikuwa ya kuridhisha kutokana na mabadiliko ya mfumo na usimamizi wa kodi yaliyotokana na kuboreshwa kwa mazingira ya ulipaji wa kodi kama ilivyoainishwa katika Mpango wa mwaka 2003 – 2008 wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA). Aidha, makusanyo ya kodi za ushuru wa forodha na bidhaa zinazozalishwa nchini yaliongezeka katika kipindi cha Julai – Desemba 2003 ikilinganishwa na kipindi kama hicho mwaka uliotangulia kutokana na ongezeko kubwa la uagizaji wa bidhaa kutoka nje ya nchi katika kipindi hicho. Makusanyo ya mapato yasiyotokana na kodi hayakuwa ya kuridhisha katika kipindi hicho kutokana na kupungua kwa shughuli zinazochangia mapato hayo kwa baadhi ya wizara, idara za serikali na mikoa. 75. Hadi kufikia mwisho wa Machi 2004, mapato ya ndani kwa mwaka 2003/04 yalifikia sh. 1,089,260 milioni, sawa na asilimia 78.2 ya makisio ya mwaka. Mapato hayo ni zaidi ya makisio ya sh. 1,050,866 milioni kwa kipindi hicho kwa asilimia 3.7. Kutokana na mwenendo huo, lengo la mapato ya ndani kwa mwaka 2003/04 linatarajiwa kupitwa na kufikia sh. 1,400,605 milioni ifikapo Juni 2004, sawa na asilimia 0.54 juu ya makisio ya mwaka. Kiwango hicho cha makusanyo kitakuwa sawa na asilimia 14 ya Pato la Taifa kwa makadirio ya mwaka 2003/04, ikiwa ni zaidi ya lengo la kukusanya asilimia 13.3 ya Pato la Taifa katika kipindi hicho. Misaada
na Mikopo ya Nje 77. Hadi mwezi Machi 2004 jumla ya fedha kutoka nje ya nchi ikijumuisha misamaha ya madeni yaliyo katika mpango wa HIPC zilifikia sh. 964,338 milioni. Kati ya fedha hizo, sh. 612,697 milioni zilitokana na ruzuku na sh. 351,641 milioni zilikuwa ni mikopo kwa ajili ya programu na miradi. Fedha zilizotokana na misamaha katika utaratibu wa HIPC zilifikia sh. 56,687 milioni. Kutokana na mwenendo huo, mapato ya misaada na mikopo ikijumuisha misamaha ya madeni kwa utaratibu wa HIPC, yanatarajiwa kufikia sh. 1,076,748 milioni, ifikapo Juni 2004. Mikopo
ya Ndani na Mapato ya Ubinafsishaji MATUMIZI 79. Sera za bajeti kwa upande wa matumizi ya fedha za serikali kwa mwaka 2003/04 zililenga katika kuendeleza na kuimarisha usimamizi mzuri wa matumizi ya fedha za serikali ili kufikia malengo yaliyowekwa katika kukuza uchumi na kuondoa umaskini. Kwa kuzingatia sera hizo, serikali ilikadiria kutumia jumla ya sh. 2,418,337 milioni, sawa na asilimia 24.2 ya Pato la Taifa. Kati ya fedha hizo, matumizi ya kawaida yalikadiriwa kuwa sh. 1,610,897 milioni na matumizi ya maendeleo kuwa sh. 807,440 milioni. Mgawanyo wa matumizi ulikuwa kama ifuatavyo : sh. 464,061 milioni, sawa na asilimia 28.8 ya matumizi ya kawaida, zilitengwa kwa ajili ya kulipia mishahara ya watumishi wa umma; sh. 334,497 milioni, sawa na asilimia 20.8 ya matumizi ya kawaida zilitengwa kwa ajili ya sekta zilizopewa kipaumbele katika Mkakati wa Kupunguza Umaskini na matumizi mengineyo yalitengewa jumla ya sh. 424,141 milioni sawa na asilimia 26.3 ya matumizi yote ya kawaida. 80. Matumizi yote ya Serikali katika nusu ya kwanza ya mwaka 2003/04 (Julai-Desemba 2003) yalifikia jumla ya sh. 1,044,510 milioni, sawa na asilimia 93.1 ya makadirio ya sh. 1,121,774 milioni katika kipindi hicho. Kiwango hiki cha matumizi ni sawa na asilimia 43.2 ya bajeti yote ya matumizi katika mwaka 2003/04. Matumizi ya kawaida katika kipindi hicho yalifikia sh. 768,593 milioni, sawa na asilimia 96.5 ya makadirio ya sh. 796,733 milioni kwa kipindi hicho na matumizi ya maendeleo yalifikia sh. 275,916 milioni, sawa na asilimia 84.9 ya makadirio ya sh. 325,041 milioni. Katika kipindi hicho, Serikali ilitumia sh. 229,781 milioni kulipa mishahara ya watumishi wa umma na sh. 159,390 milioni zilitumika kwa ajili ya sekta zilizopewa kipaumbele katika Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Kwa ujumla, kiwango cha matumizi ya bajeti ya kawaida kilikuwa chini ya lengo katika kipindi hicho kutokana na kushindwa au kuchelewa kufanya ununuzi kutokana na kutozoeleka vya kutosha kwa sheria mpya ya manunuzi ya mwaka 2001. Hata hivyo, ikilinganishwa na mwaka 2002/03, matumizi ya bajeti ya kawaida yamekuwa ya kuridhisha kutokana na kuanza kueleweka kwa sheria mpya ya ununuzi ya mwaka 2001. 81. Matumizi ya maendeleo, katika kipindi cha Julai – Desemba 2003 yalifikia sh. 275,916 milioni, sawa na asilimia 85 ya makadirio kwa kipindi hicho. Kutofikiwa kwa lengo la matumizi ya maendeleo, kwa kiwango kikubwa kumetokana na ucheleweshaji wa taarifa za matumizi, hususan kwa miradi inayotekelezwa kwa fedha za wafadhili wa nje. 82. Matumizi yote ya serikali hadi kufikia mwisho wa Machi 2004 katika mwaka 2003/04 yalifikia sh. 1,875,690 milioni, sawa na asilimia 77.6 ya bajeti ya mwaka. Kutokana na mwenendo huo, ifikapo Juni 2004, matumizi yote ya serikali yanatarajiwa kufikia sh. 2,559,090 milioni, sawa na asilimia 105.8 ya makadirio ya bajeti ya mwaka. 83. Katika mwaka 2003/04 serikali iliendelea kuimarisha usimamizi na nidhamu katika matumizi ya serikali kwa madhumuni ya kuongeza ufanisi katika uwajibikaji. Katika kupanga matumizi ya fedha kwa mwaka 2003/04, mgao mkubwa wa fedha za serikali ulielekezwa kwenye sekta zilizopewa kipaumbele katika Mkakati wa Kupunguza Umaskini (afya, elimu, barabara vijijini, maji, kilimo na utawala bora). Aidha, kutokana na upungufu wa chakula uliojitokeza, serikali ilitenga fungu la fedha kwa ajili ya ununuzi wa chakula kwa maeneo ya nchi yaliyohitaji chakula cha msaada. 84. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya afya katika mwaka 2003/04 ilikuwa asilimia 7 kama ilivyokuwa katika mwaka 2002/03. Hata hivyo, kiwango cha fedha za bajeti kilichoelekezwa sekta ya afya kiliongezeka kutoka sh. 148,437 milioni mwaka 2002/03 hadi sh. 182,704 milioni mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa sekta ya elimu ilipungua kutoka asilimia 19.2 mwaka 2002/03 hadi asilimia 17.3 mwaka 2003/04, ingawa fedha zilizoelekezwa sekta hiyo ziliongezeka kutoka sh. 409,362 milioni mwaka 2002/03 hadi sh.446,247 milioni mwaka 2003/04. Katika sekta ya kilimo, misitu, uvuvi na uwindaji; sehemu ya bajeti iliongezeka kutoka asilimia 3 mwaka 2002/03 hadi asilimia 3.5 mwaka 2003/04. Bajeti ya utafiti wa kilimo ilikuwa asilimia 2.8 ya bajeti yote iliyoelekezwa katika sekta hiyo. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya madini, viwanda na ujenzi iliongezeka kutoka asilimia 4 mwaka 2002/03 hadi aslimia 6 mwaka 2003/04, kutokana na kuongezeka kwa miradi ya ujenzi nchini. Fungu la bajeti lililoelekezwa kwenye miradi ya maendeleo ya ujenzi pekee lilikuwa asilimia 83.5 ya bajeti iliyotengwa katika sekta hiyo. Kwa upande wa usafirishaji na mawasiliano, sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta hiyo iliongezeka kutoka asilimia 6.9 mwaka 2002/03 hadi asilimia 8.3 mwaka 2003/04. 85. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta za huduma za kawaida ilipungua kutoka asilimia 19.2 mwaka 2002/03 hadi asilimia 17.7 mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya usalama iliongezeka kutoka asilimia 4.4 mwaka 2002/03 hadi asilimia 4.5 mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye matumizi mengineyo ilipungua kutoka asilimia 20.4 mwaka 2002/03 hadi asilimia 18 mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya huduma za uchumi (biashara, utalii, huduma za kazi nk.) iliongezeka kutoka asilimia 3.2 mwaka 2002/03 hadi aslimia 4.4 mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa katika sekta ya usalama wa jamii, ustawi na huduma za jamii ilipungua kutoka asilimia 1.7 mwaka 200/03 hadi asilimia 1.6 mwaka 2003/04. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya ulinzi na huduma ilishuka hadi asilimia 6 mwaka 2003/04 kutoka asilimia 6.8 mwaka 2002/03. Sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye sekta ya mafuta na umeme ilipungua kutoka asilimia 0.15 mwaka 2002/03 hadi asilima 0.14 mwaka 2003/04. Na sehemu ya bajeti iliyoelekezwa kwenye huduma nyingine za jamii ilikuwa sawa na kiwango cha mwaka 2002/03 cha asilimia 0.1. Deni
la Taifa 87. Sheria mpya ya kusimamia mikopo na misaada ya mwaka 2003, iliyorekebisha sheria iliyokuwepo ya mwaka 1974 ilianza kutumika mwezi wa Julai, 2003. Makusudi ya sheria hiyo ni kuimarisha usimamiaji wa mikopo na misaada kwa taifa. Pamoja na sheria hiyo, hatua mbalimbali zimechukuliwa kuimarisha na kukijengea uwezo kitengo cha madeni kilichopo Wizara ya Fedha kwa kukiongezea wataalam na vifaa. Aidha, serikali iliendelea na juhudi zake za kuhamasisha na kushawishi nchi wahisani kuipunguzia na/au kuifutia Tanzania madeni chini ya taratibu za HIPC. Deni
la Nje 89. Deni la nchi wahisani lilipungua kutokana na misamaha ya madeni, wakati ambapo deni la mashirika ya kimataifa ya fedha liliongezeka kutokana na serikali kupokea mikopo nafuu mipya inayotolewa na mashirika hayo kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 90. Katika jumla ya mikopo halisi iliyotolewa kufikia Desemba 2003, serikali ilikuwa imekopa kiasi cha dola 6,089.9 milioni, sawa na asilimia 90.5, ambapo mashirika ya umma yalikuwa yamekopa dola 154 milioni, sawa na asilimia 2.3, na sekta binafsi ilikopa jumla ya dola 487 milioni, ambazo ni sawa na asilimia 7.2 ya jumla ya mikopo yote ya nje. 91. Mgawanyo wa mikopo iliyopokelewa toka nje (bila riba) kisekta hadi kufikia Desemba 2003, ni kama ifuatavyo: - kusaidia mizania ya malipo na nchi za nje, dola 1,219.1 sawa na asilimia 18.1; mawasiliano na usafirishaji dola 1,113.6 sawa na asilimia 16.5; kilimo dola 978.0 sawa na asilimia 14.5; madini dola 931.0 sawa na asilimia 13.8; viwanda dola 360.5 sawa na asilimia 5.4; elimu dola 326.9 sawa na asilimia 4.9; sekta ya fedha dola 90.3 sawa na asilimia 1.3; utalii dola 91.1 sawa na asilimia 1.4 na sekta nyinginezo dola 1620.2 sawa na asilimia 24.1. Mpango wa Kuzipunguzia Madeni Nchi Maskini
zenye Madeni Makubwa (HIPC) Deni
la Ndani 94. Mabenki ya biashara nchini yaliendelea kuwa wakopeshaji wakubwa wa serikali, kwa kuikopesha kiasi cha dola 295.4 milioni, sawa na sh. 314,186.3 milioni, ikiwa ni asilimia 34.2 ya deni la serikali la ndani. Benki Kuu ilikuwa inaidai serikali kiasi cha dola 224.2 milioni, sawa na sh. 238,478.5 milioni, au asilimia 25.9 ya deni lote la ndani. Mikopo kutoka mashirika ya umma ilichangia kiasi cha dola 2.7 milioni, sawa na sh. 2,862.5 milioni au asilimia 0.3 ya deni lote na dola 33.4 milioni, sawa na sh. 35,543.3 milioni au asilimia 3.9 ya deni lote lilitokana na mikopo kutoka sekta binafsi. Jedwali Na. 25(MWENENDO WA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALI)MWENENDO WA MAPATO NA MATUMIZI YA SERIKALIl Jedwali Na. 26(MGAWANYO WA HUDUMA ZA SERIKALI ) |
|||||||