MAENDELEO
YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA
SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU
KATIKA MAENDELEO | |
|||||||||
| MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | |||||||||
Hali
ya Uchumi wa Taifa |
|||||||||
RASILIMALI
WATU |
|||||||||
Idadi ya Watu na Maendeleo 119. Kwa kuzingatia viwango vya ongezeko la idadi ya watu nchini vilivyopatikana katika Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, idadi ya watu nchini mwaka 2003 iliongezeka hadi watu 35,257,081 kutoka watu 34,443,603 waliohesabiwa katika Sensa ya 2002, sawa na ongezeko la watu 803,478. Katika jumla hiyo, inakadiriwa kwamba watu 34,249,546 walikuwa Tanzania Bara na watu 1,007,534 walikuwa Tanzania Visiwani. 120. Sura ya mgawanyo wa watu kwa umri inakadiriwa ilibaki vilevile kama ilivyokuwa mwaka 2002 ikionyesha kwamba Tanzania ni taifa la watu vijana. Zaidi ya asilimia 44 ya watu wako katika umri chini ya miaka 15. Wazee wa umri wa kuanzia miaka 65 na zaidi wanakaribia kuwa asilimia 4 ya watu wote. Watu wa umri wa miaka 15 hadi 64 ambao kiumri ndiyo kundi linalounda nguvukazi ni asilimia 52 ya watu wote. Sura hiyo ya mgawanyo wa watu kwa umri inatoa changamoto ya kukuza uwezo wa kutoa huduma za elimu, mafunzo, afya na nafasi za ajira ili ziendane na kuongezeka kwa mahitaji yanayotokana na ongezeko la idadi ya watu nchini. 121. Kiwango cha wastani wa ukubwa wa kaya pia kinakadiriwa kubaki kile cha mwaka 2002 cha watu 4.9 kwa kaya ambacho pia ndiyo kiwango cha Tanzania Bara; wakati kwa Zanzibar ni wastani wa watu 5.3 kwa kaya. Kutokana na kuongezeka kwa idadi ya watu, viwango vya msongamano wa watu viliongezeka hadi watu 40 kwa kila kilometa ya mraba kwa Tanzania, watu 39 kwa Tanzania Bara, na watu 409 – Zanzibar, mwaka 2003 kutoka watu 39, 38, na 397, kwa mtiririko huo mwaka 2002. Maeneo ya mijini yameendelea kuwa na msongamano mkubwa wa watu kuliko maeneo ya vijijini. Kimkoa, Lindi iliendelea kuwa mkoa uliokuwa na msongamano mdogo zaidi wa watu 12 ambapo Dar es Salaam iliendelea kuwa mkoa na mji wenye msongamano wa juu kabisa wa watu 1,850 kwa kila kilomita mraba. 122. Utekelezaji wa sera ya idadi ya watu nchini uliendelea vizuri na jitihada za kuhuisha sera iliyopo ziliendelea. Katika utekelezaji wa sera hiyo mkazo umeendelea kuwekwa katika uboreshaji wa huduma za afya ya uzazi, kuhamasisha na kuelimisha viongozi, watendaji na wananchi kuhusu dhana ya haki na usawa wa kijinsia na pia kuhimiza uwezeshwaji wa wanawake. Vile vile, jitihada ziliendelea kuelekezwa katika kuzipatia wilaya uwezo wa kuzingatia masuala ya idadi ya watu katika mchakato wa upangaji mipango ya maendeleo kwa kuwapatia maofisa mipango wilaya 60 mafunzo ya taaluma ya uzingatiaji masuala ya idadi ya watu katika mipango. Aidha, wilaya 36 zilipatiwa tarakishi. 123. Umaskini umeendelea kuwa tatizo kubwa linalowakabili watanzania wengi katika mwaka 2003. Ukosefu wa uhakika wa chakula, mazingira duni ya kuishi, kuenea kwa maradhi ya kuambukiza likiwemo janga la UKIMWI, huduma duni za jamii ikiwemo afya na elimu, vifo vingi vitokanavyo na maradhi ya kuambukiza na pia vifo vingi vya watoto na mama wajawazito; yote haya yameendelea kuwa vielelezo vikubwa vya umaskini uliopo nchini. Uhaba wa rasilimali nao umeendelea kuwa kikwazo kikubwa katika jitihada za wananchi na taifa kujikwamua kutoka kwenye umaskini. Nguvukazi
na Ajira 125. Watu wasio na kazi ni asilimia 12.9 kwa nchi nzima. Karibu nusu ya wasiokuwa na kazi wanaishi mijini. Katika Jiji la Dar es Salaam peke yake, asilimia 46.5 ya wenye uwezo wa kufanya kazi hawana kazi, miji mingine, asilimia 25.5 na vijijini, asilimia 8.4. Aidha, ukosefu wa ajira ni mkubwa zaidi kwa vijana wenye umri kati ya miaka 10 na 34. Kijinsia, vijana wa kike ndio wanaoathirika zaidi na tatizo hili. Uchambuzi wa sekta za ajira unabainisha kuwa sekta rasmi ya umma, ambayo siku za nyuma ilikuwa ndiyo mwajiri mkuu (wa kazi za mshahara), imeshuka sana katika kutoa nafasi za ajira. Badala yake, sekta ya kilimo, sekta isiyo rasmi na sekta rasmi binafsi ndizo zinazoajiri watu wengi zaidi. Kwa miaka mingi ijayo, kilimo kitaendelea kuwa tegemeo la watu walio wengi. 126. Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 pamoja na mambo mengine, inatoa mwongozo kushughulikia changamoto ya ajira na kuondoa umaskini. Sera ya Taifa ya Ajira inayoandaliwa itajenga mazingira yanayowezesha sekta binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali (NGOs) na vikundi vya jamii (CBOs) kushiriki kikamilifu katika ukuzaji wa ajira. Ili kuinua uzalishaji katika sekta ya kilimo, serikali inachukua hatua mbalimbali zitakazoboresha miundombinu na elimu vijijini, huduma za ughani, umilikaji wa ardhi, masoko ya mazao ya wakulima na upatikanaji wa bidhaa kwa wanavijiji. Hatua hizo zitawawesha wakulima kuzalisha ziada kubwa zaidi na kujiongezea mapato. Aidha, serikali inahimiza matumizi ya teknolojia sahihi na pembejeo zinazofaa kwa wakulima ili wazalishe mazao zaidi na yaliyo bora zaidi. Serikali pia inahimiza uwekezaji katika viwanda vya kusindika mazao ili kuyaongezea thamani. Wawekezaji wa nje na wa ndani wanapewa vivutio ili wawekeze katika viwanda vikubwa vitakavyohudumia sekta ya kilimo na sekta isiyo rasmi na kutoa nafasi za ajira na kuchangia katika pato la taifa. Sekta isiyo rasmi ina nafasi kubwa ya kupanuka na kutoa nafasi nyingi za ajira kuliko sekta rasmi. Asilimia 61 ya kaya zote za mijini na asilimia 27 ya kaya za vijijini zinafanya shughuli za sekta isiyo rasmi. Asilimia 75 ya wanaojishughulisha na biashara ndogo ndogo hawana mafunzo ya aina yo yote. Hatua zinazochukuliwa na Serikali kuiendeleza sekta hii ni pamoja na kuweka utaratibu wa kuwakopesha wanaojiajiri vifaa vya kufanyia kazi, kuwatengea maeneo ya kufanyia biashara (hasa mijini), kurahisisha upatikanaji wa malighafi na masoko kwa mazao yao, kuwapa elimu ya uendeshaji wa biashara na utunzaji wa mahesabu na kurekebisha sheria zinazowagandamiza. Jedwali
Na. 33(JUMLA YA IDADI YA WATU NCHINI
TANZANIA KIMKOA: 1990-2002) |
|||||||||