MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU KATIKA MAENDELEO |
MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA

Hali ya Uchumi wa Taifa
Hali ya Uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa
Sekta ya Nje
Fedha za Serikali
Fedha na Taasisi za Fedha
Rasilimali Watu

     
SEKTA YA NJE
 
MAUZO NJE
Biashara ya Bidhaa

40. Mwaka 2003 thamani ya mauzo ya bidhaa nje iliongezeka kwa asilimia 26.6 kutoka dola 902.5 milioni mwaka 2002 kufikia dola 1,142.4 milioni. Kuongezeka kwa thamani ya mauzo ya bidhaa nje kulichangiwa na kuongezeka kwa mauzo ya madini hasa dhahabu. Mauzo ya dhahabu pekee yalichangia asilimia 43.7 ya thamani ya bidhaa zote zilizouzwa nje ambapo mauzo ya bidhaa asilia yalichangia asilimia 19.5.

Bidhaa Asilia
41. Mwaka 2003, thamani ya mauzo ya bidhaa asilia iliongezeka kwa asilimia 8.1 kufikia dola 222.7 milioni ikilinganishwa na dola 206.1 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa asilia kulitokana na kuongezeka kwa kiasi cha mauzo ya kahawa, pamba na karafuu pamoja na ongezeko dogo la bei katika soko la dunia kwa kahawa, pamba, na katani. Wastani wa bei ya kahawa uliongezeka kwa asilimia 12.2, pamba asilimia 15.5 na katani asilimia 0.3. Aidha, bei katika soko la dunia kwa mauzo ya chai, tumbaku, korosho na karafuu ilipungua. Pamoja na kuwa thamani ya mauzo ya bidhaa asilia iliongezeka, mchango wake kwa bidhaa zilizouzwa nje mwaka 2003 uliendelea kupungua na kufikia asilimia 19.5 ikilinganishwa na asilimia 22.8 katika mwaka 2002 kutokana na kuongezeka mauzo ya bidhaa zisizo asilia.

Kahawa
42. Thamani ya mauzo ya kahawa mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 42.0 na kufikia dola 50.0 milioni ikilinganishwa na dola 35.2 milioni mwaka 2002. Hii ilitokana na ongezeko la kiasi kilichouzwa nje na ubora wake na bei iliyopatikana katika soko la dunia. Kiasi cha kahawa kilichouzwa nje mwaka 2003 kiliongezeka kwa asilimia 26.5 na kufikia tani 46,000 ikilinganishwa na tani 36,370 mwaka 2002. Wastani wa bei ya kahawa katika soko la dunia uliongezeka kwa asilimia 12.2 kutoka dola 968.4 kwa tani mwaka 2002 hadi dola 1,087.0 kwa tani mwaka 2003. Kuongezeka kwa wastani wa bei katika soko la dunia kulichangiwa na kushuka kwa uzalishaji wa kahawa nchini Brazil na katika nchi nyingine kulikosababishwa na kupungua sana kwa wastani wa bei ya kahawa katika soko la dunia kwa kipindi cha miaka minne mfululizo iliyotangulia.

Pamba
43. Thamani ya mauzo ya pamba kwenye soko la dunia iliongezeka kwa asilimia 62.7 kutoka dola 28.6 milioni mwaka 2002 na kufikia dola 46.6 milioni mwaka 2003. Kuongezeka kwa mapato ya mauzo ya pamba katika soko la dunia kulichangiwa na kuongezeka kwa kiasi cha pamba kilichouzwa kutoka tani 33,320 mwaka 2002 hadi tani 46,900 mwaka 2003, na kuongezeka kwa wastani wa bei katika soko la dunia kutoka dola 859.4 kwa tani mwaka 2002 hadi dola 992.8 kwa tani mwaka 2003. Kupanda kwa wastani wa bei ya pamba kulitokana na uzalishaji mdogo katika nchi za Marekani na China ambazo ni wazalishaji wakubwa wa pamba duniani.

Katani
44. Mwaka 2003, thamani ya mauzo ya katani kwenye soko la dunia ilibakia katika kiwango cha mwaka 2002 cha dola 6.6 milioni. Aidha, kiasi cha katani kilichouzwa nje kilibakia katika kiwango cha mwaka 2002 na wastani wa bei katika soko la dunia haukubadilika sana kutoka dola 516.4 kwa tani mwaka 2002 hadi dola 517.8.

Chai
45. Thamani ya mauzo ya chai mwaka 2003 ilipungua kwa asilimia 16.2 hadi dola 24.8 milioni ikilinganishwa na dola 29.6 milioni katika mwaka 2002. Kiasi cha mauzo ya chai katika soko la dunia kilipungua kwa asilimia 14.0 kutoka tani 24,310 mwaka 2002 hadi tani 20,900 mwaka 2003. Wastani wa bei ya chai katika soko la dunia ulipungua kwa asilimia 2.4 hadi dola 1,188.2 kwa tani mwaka 2003 kutoka dola 1,217.8 kwa tani mwaka 2002. Kupungua kwa wastani wa bei ya chai katika soko la dunia kulichangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa chai duniani.

Tumbaku
46. Thamani ya mauzo ya tumbaku mwaka 2003 ilipungua kwa asilimia 24.0 na kufikia dola 42.2 milioni kutoka dola 55.5 milioni mwaka 2002. Kupungua kwa thamani ya mauzo ya tumbaku kulichangiwa na kupungua kwa kiasi kilichouzwa pamoja na kushuka kwa bei katika soko hilo. Kiasi cha tumbaku kilichouzwa nje kilipungua kwa asilimia 20.0 kutoka tani 25,370 mwaka 2002 hadi tani 20,300 mwaka 2003. Bei ya tumbaku katika soko la dunia ilipungua kwa asilimia 5.2 kutoka dola 2,188.6 kwa tani mwaka 2002 hadi dola 2,076.1 kwa tani mwaka 2003. Kupungua kwa matumizi ya tumbaku duniani kunakoenda sambamba na juhudi za kupiga vita uvutaji wa sigara ni sababu kubwa iliyochangia kupungua kwa mauzo ya bidhaa hii katika soko la dunia.

Korosho
47. Thamani ya mauzo ya korosho iliyouzwa nje katika mwaka 2003 ilipungua kwa asilimia 9.5 na kufikia dola 42.2 milioni ikilinganishwa na dola 46.6 milioni mwaka 2002. Kupungua kwa mapato yatokanayo na mauzo ya korosho nje kulichangiwa na kupungua kwa wastani wa bei katika soko la dunia kwa asilimia 1.0 mwaka 2003 na kupungua kwa kiasi kilichouzwa kwa asilimia 8.6 kutoka tani 75,680 mwaka 2002 hadi tani 69,200 mwaka 2003.

Karafuu
48. Thamani ya mauzo ya karafuu iliyouzwa nje mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 160 na kufikia dola 10.3 milioni ikilinganisha na dola 4.0 milioni mwaka 2002. Kiasi cha mauzo ya karafuu katika soko la dunia kiliongezeka kutoka tani 1,220 mwaka 2002 hadi tani 5,600 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 359. Ongezeko hili kubwa la kiasi na thamani ya mauzo lilitokana na kuuzwa kwa kiasi cha karafuu kilichokuwa kimelundikana katika maghala kufuatia kupungua kwa bei ya karafuu katika soko la dunia. Kupungua kwa bei ya karafuu katika soko la dunia kulitokana na nchi ya Indonesia ambayo ni mnunuzi mkuu wa karafuu duniani kupunguza ununuaji wa karafuu kutoka nje kufuatia kuimarika kwa uzalishaji wa ndani.

Bidhaa zisizo Asilia
49. Thamani ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia kwa mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 32 na kufikia dola 919.7 milioni ikilinganishwa na dola 696.5 milioni mwaka 2002. Mauzo ya madini hasa dhahabu yaliendelea kutoa mchango mkubwa katika ongezeko la mauzo ya bidhaa zisizo asilia. Vile vile, mauzo ya bidhaa za viwandani, samaki na mazao ya samaki, bidhaa za mboga na maua yalichangia katika ukuaji wa mauzo ya bidhaa zisizo asilia. Kwa ujumla, mauzo ya bidhaa zisizoasilia yalichangia asilimia 80.5 ya mauzo yote ya bidhaa nje mwaka 2003 ikilinganishwa na asilimia 77.2 mwaka 2002. Mwenendo huu ni matokeo ya sera za jumla za kurekebisha uchumi na juhudi za serikali za kuendeleza uwekezaji wa vitega uchumi nchini.

Madini
50. Thamani ya mauzo ya madini mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 42.9 hadi dola 548.3 milioni kutoka dola 383.8 milioni mwaka 2002. Mauzo ya dhahabu yaliongezeka kwa asilimia 46.3 na kufikia dola 499.0 milioni ukilinganisha na dola za marekani 341.1 milioni mwaka 2002. Kuongezeka huku kwa mauzo ya dhahabu kulichangiwa na kuimarika kwa uzalishaji wa dhahabu.

Bidhaa za Viwandani
51. Thamani ya mauzo ya bidhaa za viwandani mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 51.6 hadi dola 99.9 milioni kutoka dola 65.9 milioni mwaka 2002. Kuimarika kwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani kunatokana na uwekezaji katika teknolojia ya kisasa na kuanzishwa kwa viwanda katika maeneo huru (EPZ).

Samaki na Mazao ya Samaki
52. Mwaka 2003, thamani ya mauzo ya samaki na mazao ya samaki, iliongezeka kwa asilimia 16.4 na kufikia dola 136.2 milioni kutoka dola 116.8 milioni mwaka 2002. Bei nzuri katika soko la Jumuia ya Ulaya kunatokana na mafanikio ya kulinda ubora wa bidhaa hizo.

Mazao ya Mboga na Maua
53. Thamani ya mauzo ya mazao ya mboga na maua mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 25.7 na kufikia dola 13.7 milioni kutoka dola 10.9 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa uzalishaji pamoja na bei nzuri ndio chanzo cha mafanikio haya.

Bidhaa nyinginezo zilizouzwa Nje
54. Thamani ya bidhaa nyingine zilizouzwa nje katika mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 1.6 na kufikia dola milioni 121.6 kutoka dola milioni 119.2 zilizopatikana mwaka 2002. Mafanikio yalipatikana kutokana na kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa mbalimbali katika nchi za jirani.

Biashara ya Huduma
55. Mapato yaliyotokana na huduma kwa mwaka 2003 yaliongezeka kwa asilimia 2.9 na kufikia dola 685.3 milioni ikilinganishwa na dola 665.8 milioni zilizopatikana mwaka 2002.Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka kwa mapato yaliyotokana na usafirishaji wa mizigo kwa asilimia 14.5, huduma za mawasiliano asilimia 51.8 pamoja na utalii asilimia 1.1. Kuongezeka kwa mapato yaliyotokana na usafirishaji wa mizigo kulichangiwa hasa na kuongezeka kwa ufanisi katika bandari ya Dar es salaam ambayo imekuwa kivutio kwa usafirishaji wa bidhaa za nchi jirani baada ya kitengo cha kontena kuongeza uwezo wake wa kupakua na kupakia mizigo kwa muda mfupi ikilinganishwa na bandari nyingine za nchi jirani.

     
BIDHAA ZILIZOAGIZWA KUTOKA NJE

56. Thamani ya bidhaa (f.o.b) zilizoagizwa kutoka nje katika mwaka 2003 iliongezeka kwa asilimia 30.5 na kufikia dola 1,973.0 milioni kutoka dola 1,511.3 milioni zilizoagizwa mwaka 2002. Kasi ya ongezeko la uagizaji wa bidhaa ni kubwa zaidi ya ile ya ongezeko la mauzo ya bidhaa. Mwenendo huu umetokana na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za kukuza mitaji, bidhaa za kati na bidhaa za matumizi ya kawaida (kujumuisha chakula) pamoja na kuboreshwa kwa ukusanyaji taarifa za uingizaji wa bidhaa toka nje.

Bidhaa za ukuzaji Mitaji
57. Uagizaji wa bidhaa za kukuza mitaji uliongezeka kwa asilimia 18.1 na kufikia dola 852.4 milioni mwaka 2003 kutoka dola 721.2 milioni zilizoagizwa mwaka 2002. Uagizaji wa vifaa vya usafirishaji, vifaa vya ujenzi pamoja na mashine uliendelea kuongezeka kutokana na kupanuka kwa sekta za usafirishaji, ujenzi, na viwanda.

Bidhaa za Kati
58. Katika mwaka 2003, uagizaji wa bidhaa za kati uliongezeka kwa asilimia 60.2 hadi dola 679.7milioni ikilinganishwa na dola 423.0 milioni mwaka 2002. Uagizaji wa bidhaa za kati uliongezeka kwa sababu ya kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za mafuta ya petroli, mbolea na malighafi za viwandani. Thamani ya mafuta ya petroli yaliyoagizwa iliongezeka kwa asilimia 107.0 hadi dola 403.4 milioni mwaka 2003 kutoka dola 194.8 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa thamani ya mafuta yaliyoagizwa kulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa bei ya mafuta katika soko la dunia na pia kuongezeka kwa uagizaji wa mafuta hasa katika mwezi wa Aprili na Mei mwaka 2003 kulikochangiwa na matumizi makubwa ya mafuta ya kuendeshea mitambo ya kuzalisha umeme kutokana na ukame. Katika mwaka 2003, uagizaji wa malighafi za viwandani uliongezeka kwa asilimia 19.0 na kufikia dola 247.7 milioni kutoka dola 208.0 milioni. Hii ilisababishwa na kuimarika kwa sekta ya viwanda kufuatia kuongezeka kwa uwekezaji na hatua za ubinafsishwaji wa viwanda vingi vilivyokuwa vinamilikiwa na serikali.

Bidhaa za Matumizi ya Kawaida
59. Uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida katika mwaka 2003 uliongezeka kwa asilimia 23.1 na kufikia dola 636.0 milioni, kutoka dola 516.6 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa uagizaji kulisababishwa na kuongezeka kwa uagizaji wa chakula kwa asilimia 24.3 kutoka dola 147.3 milioni mwaka 2002 hadi dola 183.1 milioni mwaka 2003 kufuatia kuwepo kwa uhaba wa chakula nchini. Vile vile, uagizaji wa bidhaa nyingine za matumizi ya kawaida, kama vile madawa, bidhaa za plastiki, nguo, karatasi na bidhaa zingine za matumizi ya nyumbani kuliongezeka kwa asilimia 22.6 kutoka dola 369.3 milioni mwaka 2002 hadi dola 452.9 milioni mwaka 2003.

Malipo ya Huduma
60. Malipo ya huduma yaliongezeka kwa asilimia 8.7 na kufikia dola 774.5 milioni mwaka 2003 kulinganisha na dola 712.6 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa malipo ya huduma kulichangiwa na kuongezeka kwa gharama za usafirishaji wa mizigo kulikotokana na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa nje mwaka 2003. Malipo ya huduma za mawasiliano yaliongezeka hasa kutokana na kupanuka kwa sekta ya mawasiliano hapa nchini. Aidha, kumekuwepo na ongezeko la malipo ya bima yaliyotokana na kuongezeka kwa ada zinazotozwa na mashirika ya bima duniani kufuatia kuongezeka kwa wasiwasi wa usalama duniani.

Mwenendo wa Biashara baina ya Tanzania na nchi Mbalimbali
61. Tanzania imeendelea kuwa na mahusiano mazuri ya kibiashara na nchi mbalimbali duniani zikiwemo jumuia za uchumi za kikanda kama vile Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika. Katika mwaka 2003, biashara ya bidhaa kati ya Tanzania na nchi za Jumuiya ya Uchumi ya Ulaya iliongezeka zaidi ya ilivyokuwa mwaka 2002. Thamani ya mauzo ya bidhaa za Tanzania kwa nchi hizo iliongezeka kwa asilimia 36.5 na kufikia dola 638.7 milioni ikilinganishwa na dola 467.80 milioni mwaka 2002. Bidhaa ambazo zimekuwa zikichangia katika mafanikio haya ni pamoja na madini, bidhaa asilia, samaki na mazao ya samaki pamoja na bidhaa za mboga na maua. Kwa upande wa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, biashara ya bidhaa imeongezeka hasa baina ya Tanzania na Kenya. Thamani ya mauzo ya bidhaa kwa Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iliongezeka kwa asilimia 117.2 na kufikia dola 88.6 milioni ikilinganishwa na dola 40.8 milioni mwaka 2002. Kwa nchi za SADC, mauzo yaliongezeka na kufikia dola 79.81 milioni ukilinganishwa na dola 51.3 milioni mwaka 2002. Kwa ujumla mauzo ya bidhaa kwa bara la Afrika yaliongezeka kwa asilimia 69.0.na kufikia dola 173.5 milioni ikilinganishwa na dola 99.4 milioni mwaka 2002. Kwa nchi za Asia thamani mauzo ya bidhaa kwa Japan na India iliendelea kuwa nzuri ambapo bidhaa zenye thamani ya dola 88.15 milioni ziliuzwa nchini Japan, wakati bidhaa zenye thamani ya dola 69.6 millioni ziliuzwa nchini India.

62. Mwaka 2003, thamani ya bidhaa (c.i.f) zilizonunuliwa kutoka nje ya nchi iliongezeka na kufikia dola 2,168.2 milioni kutoka dola 1,658.4 milioni mwaka 2002. Bidhaa kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya zilifikia thamani ya dola 422.5 milioni ikilinganishwa na dola 362.2 milioni mwaka 2002. Kwa nchi za Afrika ya Mashariki, uagizaji wa bidhaa ulifikia dola 124.1 milioni kutoka dola 97.9 milioni; ambapo kwa nchi za SADC uagizaji uliongezeka kufikia dola 323.4 milioni ikilinganishwa na dola 211.1 milioni mwaka 2002. Ongezeko hili limechangiwa hasa na uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika ya Kusini uliofikia dola 306.4 milioni. Kiwango hiki cha uagizaji wa bidhaa kutoka Afrika ya Kusini ni kikubwa ikilinganishwa na uagizaji wa bidhaa kutoka nchi nyingine yeyote duniani. Kwa nchi za Asia, bidhaa ziliagizwa kwa wingi kutoka Japan, China na India.

Jedwali Na. 3.1: Urari wa Biashara ya Bidhaa Kati ya Tanzania na Jumuiya Mbalimbali,

U$  milioni

Jumuiya

              1997

           1998

            1999

             2000

           2001

            2002p

            2003p

Jumuiya ya Ulaya (EU)

-113.68

-253.98

-177.35

31.27

52.83

105.64

211.17

 Jumuiya ya nchi za SADC

-117.64

-164.74

-182.54

-175.99

-200.57

-159.8

-243.62

 Jumuiya ya A. Mashariki (EAC)

-73.18

-75.54

-75.37

-58.29

-63.85

-57.07

-35.56

Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji

Jedwali Na. 3.2:           Thamani ya Bidhaa Zilizouzwa Nje
US$ Milioni

Jumuiya / Nchi

1997

1998

1999

2000

2001

2002p

2003p

Umoja wa Ulaya

217.9

229.8

211.7

358.8

427.9

467.8

633.7

Jumuiya ya Maendeleo ya  nchi za Kusini  mwa Afrika(SADC)

 Afrika ya Kusini

7.9

6.3

6.6

12.1

8.7

16.5

37.3

Zambia

10

3.7

2.8

4.7

5.5

17.4

17.7

Msumbiji

2.6

0.1

0.7

1.5

1.4

1.6

2.2

 Jamhuri ya Kidemokrasi ya Kongo (DRC)

1.8

5

3.7

0.1

5.4

15.8

22.6

Jumla ya Mauzo  SADC

22.3

15.1

13.8

18.4

21

51.3

79.8

Jumuiya ya Afrika ya Mashariki (EAC)

 

 

Kenya

12.8

26

21

32.2

38.1

35.3

78.3

Uganda

11.6

6.5

4.7

8.5

5.5

5.5

10.3

Jumla ya mauzo  EAC

24.4

32.5

25.7

40.7

43.6

40.8

88.6

Mauzo kwa Nchi nyingine za Afrika

4.5

0.5

3.5

4.7

6.2

7.3

5

Jumla ya mauzo Afrika

51.2

48.1

43

63.8

70.8

99.4

173.5

Mauzo Amerika Kaskazini

Marekani

21.4

12.8

18

15.2

15.1

13.5

11.3

Canada

1.7

0.7

0.6

0.5

0.5

1.4

1.65

Jumla ya mauzo Amerika Kaskazini

23.1

13.5

18.6

15.7

15.6

14.9

12.95

Mauzo kwa Nchi Nyingine

India

66.5

114.8

112.8

98.5

82.2

64.2

69.6

Japan

60

45.5

43.9

34.2

68.5

96.3

88.2

Umoja wa Falme za Kiarabu

5

6.8

6.7

6.3

9.6

14.4

15.4

Hong Kong

18.2

5

7.8

8.8

8.7

11.2

9.9

Nyinginezo

310.6

125

98.8

77.2

92.9

134

139.4

Jumla Kuu

752.5

588.5

543.3

663.3

776.2

902.2

1142.5

 


 

Jedwali Na. 3.3: Thamani ya Bidhaa Zilizoagizwa Nje (c.i.f)

US$  Milioni

Jumuiya/Nchi

1997

1998

1999

2000

2001

2002p

2003p

Jumuiya ya Ulaya

331.58

483.78

389.05

327.53

375.07

362.16

422.5

Afrika

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini  mwa Afrika (SADC)

 

 

 

 

Afrika ya Kusini

95.99

130.72

170.8

174.38

203.44

188.78

306.4

Zimbabwe

4.73

14.56

5.6

4.52

3.01

1.98

1.2

Zambia

25

17.04

7.26

2.4

1.8

4.32

2

Msumbiji

5.08

5.49

0.05

0.12

0.43

0.03

0.9

Jamhuri ya K. ya Kongo

0.19

0.5

0.11

0.11

0.24

0.37

0.7

Swaziland

8.95

11.53

12.52

12.86

12.65

15.62

12.2

Jumla ya Uagizaji kutoka SADC

139.94

179.84

196.34

194.39

221.57

211.1

323.4

Jumuiya ya A. Mashariki (EAC)

Kenya

95.66

105.79

95.04

93.37

96.08

95.21

115.9

Uganda

1.92

2.25

6.03

5.62

11.37

2.66

8.2

Jumla ya Uagizaji kutoka EAC

97.58

108.04

101.07

98.99

107.45

97.87

124.1

Amerika ya Kaskazini

Marekani

52.63

81.31

99.29

58.92

65.31

91.38

69.7

Canada

12.5

16.67

26.65

32.3

23.08

17.69

19.6

Jumla

65.13

97.98

125.94

91.22

88.39

109.07

89.3

Nchi nyingine za Amerika

15.48

38.86

37.87

24.53

7.87

8.03

32.9

Nchi zote za Amerika

80.61

136.84

163.81

115.75

96.26

117.10

122.2

Nchi nyingine

 

 

 

 

 

 

338.5

Japan

74.04

130.96

178.16

142.27

150.7

138.72

169.9

Umoja wa Falme za Kiarabu

93.45

59.73

51.01

56.95

108.98

97.08

146.8

China

61.54

48.75

58.01

68.03

70.55

78.97

116.7

India

77.51

89.76

94.57

88.78

87.47

106.84

167.7

Jumla  No. 4

306.54

329.2

381.75

356.03

417.7

421.61

939.6

Nyinginezo

670.37

680.18

722.47

797.24

913.83

870.12

236.4

Jumla Kuu

1320.26

1588.73

1572.83

1533.91

1714.35

1658.37

2168.2

Chanzo : Benki Kuu ya Tanzania

 
 
MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE
   
Urari wa Biashara ya Bidhaa

63. Urari wa biashara ya bidhaa mwaka 2003 ulikuwa na nakisi ya dola 830.6 milioni ikilinganishwa na nakisi ya dola 608.7 milioni mwaka 2002. Kuongezeka kwa nakisi katika urari wa biashara ya bidhaa kulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ikilinganishwa na ongezeko la mauzo ya bidhaa nje.

Urari wa Biashara ya Huduma
64. Nakisi katika urari wa biashara ya huduma kwa mwaka 2003 iliongezeka na kufikia dola 89.3 milioni ikilinganishwa na nakisi ya dola 46.7 mwaka 2002. Kuongezeka huku kwa nakisi kulichangiwa na kuongezeka zaidi kwa malipo ya huduma mbalimbali kama malipo ya uchukuzi wa mizigo, huduma za mawasiliano na gharama za bima ikilinganishwa na ongezeko la mapato kutokana na huduma hizo.

Urari wa Mapato na Malipo Mbali mbali.
65. Kwa mwaka 2003 nakisi ya urari wa mapato na malipo mbali mbali yanayojumuisha fidia kwa wafanyakazi, gawio litokanalo na mitaji ya kifedha na riba iliongezeka na kufikia dola 43.7 milioni ikilinganishwa na nakisi ya dola 16.3 milioni mwaka 2002. Kuongezeka huku kwa nakisi kulitokana na kuongezeka kwa riba na gawio lililolipwa nje.

Urari wa Uhamisho Mali wa Kawaida
66. Urari wa uhamisho mali wa kawaida unaojumuisha uhamisho wa fedha, misaada na unafuu wa kulipa madeni chini ya mpango wa “HIPC” uliongezeka kwa asilimia 48.9 na kufikia dola 626.4 milioni ikilinganishwa na dola 420.7 milioni mwaka 2002. Ongezeko hili limetokana zaidi na kuongezeka kwa misaada iliyotolewa kwa serikali kutoka dola 420.7 mwaka 2002 hadi dola 619.6 milioni mwaka 2003.

Urari wa Malipo ya Kawaida
67. Nakisi katika Urari wa malipo ya kawaida ambao unajumuisha urari wa biashara ya bidhaa, huduma, malipo mbali mbali, na uhamisho mali wa kawaida iliongezeka kwa asilimia 34.3 na kufikia dola 337.2 mwaka 2003 kutoka nakisi ya dola 251.1 mwaka 2002. Ongezeko la nakisi lilichangiwa hasa na nakisi katika biashara ya bidhaa, ambapo uagizaji wa bidhaa ulizidi uuzaji kwa dola 830.6 milioni.

Urari wa Mapato ya Vitega Uchumi
68. Urari wa mapato ya vitega uchumi unaojumuisha misada ya vitega uchumi na ufutaji wa madeni unaofanywa na nchi marafiki uliongezeka kwa asilimia 91.3 na kufikia dola 677.7 milioni mwaka 2003 ikilinganishwa na dola 354.1 milioni mwaka 2002. Kufutiwa kwa madeni yenye thamani ya dola 319.5 milioni mwaka 2003 kulichangia kwa kiasi kikubwa kuongezeka kwa urari huo.

Urari wa Malipo Yote
69. Kwa mwaka wa pili mfululizo urari wa malipo yote umeendelea kuonyesha ziada. Urari katika malipo yote kwa mwaka 2003 ulionyesha ziada ya dola 402.8 milioni ikilinganishwa na ziada ya dola 330.1 mwaka 2002. Kuongezeka kwa ziada katika urari huu kulitokana na misaada pamoja na ufutiwaji wa madeni uliofanywa na nchi mbalimbali mwaka 2003.

Akiba ya Fedha za Kigeni

70. Akiba ya fedha za kigeni imekuwa ikiongezeka mwaka hadi mwaka, hivyo kuiongezea serikali uwezo wa kuagiza bidhaa kutoka nje. Akiba ya fedha za kigeni iliongezeka kutoka dola 1,529.0 milioni mwaka 2002 hadi dola 2,037.8 milioni mwaka 2003. Kiasi cha akiba ya fedha za kigeni mwaka 2003 ni sawa na uagizaji wa miezi 8.9 ikilinganishwa na miezi 8.3 mwaka 2002.

Wastani wa thamani ya Fedha ya Tanzania
71. Thamani ya fedha ya Tanzania kwa mwaka 2003 ilikuwa ni wastani wa shilingi 1,038.6 kwa dola moja ya Marekani ikilinganishwa na wastani wa shilingi 966.6 kwa dola moja ya Marekani mwaka 2002. Hii inaonyesha kuwa sarafu yetu inaendelea kupungua thamani mwaka hadi mwaka na hivyo kufikia upungufu wa wastani wa asilimia 7.4 kwa mwaka 2003.

Jedwali Na.17(THAMANI YA BIDHAA ZA BIASHARA BAINA YA TANZANIA NA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.20( WASTANI WA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.21( WASTANI WA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE

MWENENDO WA BEI YA PAMBA NA KAHAWA ILIYOUZWA NCHI ZA NJE(US$/TANI)

Jedwali Na.22(FAHIRISI YA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.23(AINA NA THAMANI YA BIDHAA ZILIZOAGIZWA TOKA NCHI ZA NJE)

MWENENDO WA URARI KATIKA MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE

Jedwali Na.24(MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE)