MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU KATIKA MAENDELEO |
MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI
 

Kilimo
Maliasili na Utalii
Madini
Viwanda na Biashara
Ujenzi wa Maendeleo ya Ardhi
Mawasiliano na Uchukuzi
Nishati
Maji
Elimu na Mafunzo
Afya
Maendeleo ya Jamii

         
VIWANDA NA BIASHARA
Ukuaji wa Sekta

218. Sekta ya viwanda ilikua kwa asilimia 8.6 mwaka 2003 ikilinganishwa na asilimia 8.0 mwaka 2002. Mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 8.4 mwaka 2002 ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2003. Kuongezeka kwa ukuaji na mchango wa sekta katika Pato la Taifa kulitokana na kuimarika kwa viwanda na ongezeko la uzalishaji wa bidhaa hususan nguo, mabati na vyakula baada ya viwanda hivyo kufufuliwa. Viwanda hivyo vinafanyakazi vizuri kwa maana ya uzalishaji bidhaa, utoaji wa ajira na ulipaji wa kodi kwa Serikali. Aidha, mafanikio makubwa katika sekta hii yalitokana na kuongezeka kwa tija katika viwanda mbalimbali vilivyobinafsishwa.

Miradi Iliyoidhinishwa
219. Katika mwaka 2003, Kituo cha Uwekezaji (TIC) kiliidhinisha miradi ya viwanda 127 yenye thamani ya sh. 239.6 bilioni ikilinganishwa na miradi 103 yenye thamani ya sh. 195.1 bilioni iliyoidhinishwa mwaka 2002. Mchanganuo wa umiliki wa miradi ya viwanda iliyoidhinishwa unaonyesha kuwa miradi 39 ilikuwa ya wawekezaji wa ndani, miradi 22 ya wawekezaji wa nje, na miradi 20 likiwa ni ya ubia.

Gharama za uzalishaji
220. Gharama za uzalishaji katika sekta ya viwanda katika mwaka 2003 ziliongezeka toka Sh. 826,777 milioni mwaka 2002 hadi Sh. 1,020,449 milioni mwaka 2003. Hii ni sawa na asilimia 23.4 ikilinganishwa na asilimia 22.8 mwaka 2002. Ongezeko hili la gharama za uzalishaji limetokana na matatizo yaliyojitokeza katika baadhi ya viwanda kushindwa kumudu ushindani wa bidhaa kutoka nje ambazo zina bei ndogo kutokana na kukwepa kodi (dumping), gharama kubwa ya umeme, mitambo kwa baadhi ya viwanda ni mipya lakini teknolojia yake ni ya zamani na iliyopitwa na wakati, na miundombinu hafifu hasa barabara za mikoani.

Uzalishaji Katika Baadhi ya Viwanda Nchini
221. Uzalishaji wa chuma kwa mwaka 2003 uliongezeka toka tani 25,418 mwaka 2002 hadi kufikia tani 31,018, sawa na ongezeko la asilimia 22. Uzalishaji wa Aluminium uliongezeka kutoka tani 141 mwaka 2002 hadi tani 199 mwaka 2003 sawa na ongezeko la asilimia 41. Uzalishaji wa rangi uliongezeka kutoka lita 13.6 milioni mwaka 2002 hadi lita 16.8 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 24. Aidha, uzalishaji wa madawa yatokanayo na pareto, madawa ya binadamu na mifugo ulipungua kwa asilimia 56 mwaka 2003.

222. Kwa upande wa viwanda vya bidhaa za ujenzi, uzalishaji wa bati uliongezeka kwa asilimia 31 ikilinganishwa na asilimia 22, toka tani 31,742 mwaka 2002, kufikia tani 41,725 mwaka 2003. Uzalishaji wa saruji uliongezeka kwa asilimia 16 toka tani 1.026 milioni mwaka 2002 kufikia tani 1.186 milioni mwaka 2003. Tani 166,446 za saruji ziliagizwa kutoka nje ya nchi ikilinganishwa na tani 149,079 zilizoagizwa mwaka 2002. Vile vile, mauzo ya saruji nje ya nchi yalipungua kutoka tani 37,203 mwaka 2002 hadi tani 34,396, sawa na upungufu wa asilimia 7.5. Matumizi ya saruji yaliongezeka kwa asilimia 15.9 toka tani 1,137,958 hadi tani 1,318,484 mwaka 2003.

223. Kutokana na marekebisho ya menejimenti na kufufuliwa kwa viwanda vya nguo vya Mwatex, Mutex, Sunguratex na Mbeyatex, uzalishaji wa nguo uliongezeka kwa asilimia 1 toka mita za mraba 106,305 mwaka 2002 hadi mita za mraba 107,408 mwaka 2003. Uzalishaji wa kamba za katani uliongezeka toka tani 5,901 mwaka 2002 hadi tani 6,839 mwaka 2003. Uzalishaji wa nyavu za uvuvi uliongezeka kwa asilimia 37 mwaka 2003 toka tani 30 mwaka 2002 hadi tani 41 mwaka 2003.

224. Uzalishaji wa unga wa ngano uliongezeka kwa asilimia 62 kutoka tani 219,118 mwaka 2002 hadi tani 355,616 mwaka 2003, wakati uzalishaji wa biskuti na tambi uliongezeka kutoka tani 2,284 mwaka 2002 hadi tani 5,906 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 159. Aidha, uzalishaji wa konyagi ulipanda kwa asilimia 25 toka lita 2,937,000 mwaka 2002 hadi lita 3,670,000. Uzalishaji wa bia uliongezeka kutoka lita 175,870,000 hadi lita 194,100,000 sawa na ongezeko la asilimia 10 mwaka 2003. Uzalishaji wa Chibuku ulipungua kwa asilimia 24 mwaka 2003, kutoka lita 19,400,000 mwaka 2002 hadi lita 14,825,000 mwaka 2003. Kwa upande wa uzalishaji sigara, kulikuwa na ongezeko la asilimia 4, kutoka sigara milioni 3,778 mwaka 2002 hadi sigara milioni 3,920 mwaka 2003.

Biashara ya ndani
225. Sekta ya biashara ya jumla na rejareja na mahoteli ilikua kwa asilimia 6.5 mwaka 2003 ikilinganishwa na ukuaji wa asilimia 7.0 mwaka 2002. Mchango wa sekta ya biashara katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 16.8 mwaka 2002 ikilinganishwa na asilimia 16.6 mwaka 2002.

226. Katika kipindi cha mwaka 2002/03, sekta ya biashara ilipanuka kwa maana ya watu wengi zaidi kushiriki katika shughuli za biashara. Idadi ya leseni za biashara zilizotolewa iliongezeka kwa asilimia 3.7. Jumla ya leseni za biashara 99,767 zilitolewa na kuingiza sh.8,670 milioni mwaka 2002/03 ikilinganishwa na leseni za biashara 96,172 zilizoingiza sh.8, 127 milioni mwaka 2001/02 kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali 14.1. Ongezeko hilo lilitokana na kuboreshwa kwa taratibu za utoaji wa leseni za biashara na kuimarika kwa mazingira ya kufanya biashara nchini. Hata hivyo, pamoja na ongezeko hilo, hali ya ukiukaji wa kanuni mbalimbali za biashara ulionekana kuongezeka. Katika mwaka 2002/03, wafanyabiashara wapatao 11,971 walitozwa kiasi cha sh. 460 milioni kama adhabu kwa kukiuka sheria na kanuni mbalimbali za uendeshaji wa biashara, ikilinganishwa na idadi ya wafanyabiashara 6,236 waliotozwa sh. 301.7 milioni kwa mwaka 2001/02, hili ni ongezeko la asilimia 89 kwa idadi ya wafanyabiashara waliotozwa adhabu na ongezeko la asilimia 52.5 kwa kiasi kilichokusanywa.

 

Jedwali 14.1:   Utoaji wa Leseni za Biashara kwa Mwaka 2003

Mkoa

Idadi

ya

Leseni

2001/02

Idadi

ya Leseni

2002/03

Ada

Iliyopatikana

2001/02

Ada Iliyopatikana

2002/03

Idadi

ya Wahalifu

Kiasi kilicho-

tozwa kama Adhabu

Arusha

8614

6,257

398,567,900.00

329,167,189.90

-

50,667,932.90

Dar es Salaam

15,400

18,106

1,866,5 03,113.00

2,310,313,104.00

6389

62,402,005.00

Dodoma

3564

4,074

141,266,610.00

157,902,182.00

-

5,777,370.00

H.Q (Wizarani)

3521

4,100

2,703,507,137.00

2,641,387,973.60

208

79,241,639.20

Iringa

6861

7,456

256,164,163.00

275,658,816.00

927

29,846,390.00

Kagera

2458

2,500

111,827,374.00

112,827,400.00

-

119,556,688.00

Kigoma

2672

2,638

82,025,950.00

94,090,830.00

-

31,215,000.00

Kilimanjaro

6350

6,550

229,120,604.00

230,120,604.00

1280

5,423,368.00

Lindi

1669

2,100

50,749,562.00

60,749,562.00

108

6,507,500.00

Mara

3242

3,740

86,616,600.00

124,489,562.00

108

6,507,500.00

Mtwara

2585

2,695

131,964,860.00

135,964,860.00

-

3,069,500.00

Mwanza

7093

6,926

502,577,883.00

513,308,211.00

-

10,922,110.00

Manyara

-

2,350

-

101,848,308.00

612

7,017,936.00

Morogoro

4551

4,588

226,691,194.00

250,379,792.00

995

7,246,235.00

Mbeya

5080

5,318

328,616,643.00

419,906,810.00

-

5,310,600.00

Pwani

2421

2,751

94,946,454.00

106,979,849.00

285

5,261,450.00

Ruvuma

2884

2,178

95,379,916.00

98,611,826.00

218

7,733,000.00

Rukwa

2000

-

76,199,410.00

-

-

 

Shinyanga

4174

4,544

196,003,676.00

208,983,103.00

471

2,335,160.00

Singida

2300

2,509

91,119,585.00

75,349,250.00

-

6,556,100.00

Tabora

2670

2,787

116,377,204.00

136,614,847.00

-

2,560,800.00

Tanga

5019

5,600

271,348,944.00

285,958,578.00

298

3,675,054.00

Jumla

95,128

99,767

8,057,514,182.00

8,670,612,657.50

11,791

458,833,338.10

 

 

 

Chanzo: Wizara ya Viwanda na Biashara

Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-Salaam
227. Kwa mwaka 2003, washiriki wa maonyesho ya kimataifa ya biashara ya Dar es Salaam (DITF), waliongezeka kwa kiasi cha asilimia 33.9 ikilinganishwa na mwaka 2002. Idadi ya washiriki wa maonyesho hayo walikuwa 1,882 ikilinganishwa na washiriki 1,405 kwa mwaka 2002. Ongezeko hili lilitokana na kuboreshwa kwa miundo mbinu katika Uwanja wa Maonyesho, kukua kwa elimu juu ya mbinu bora za kukuza biashara na ushindani wa soko unaoongezeka siku baada ya siku kutokana na serikali kuzidi kuboresha sekta ya biashara. Idadi hii ilijumuisha washiriki 350 kutoka mataifa 22 ya nje ikilinganishwa na 331 kutoka mataifa 11 mwaka 2002. Pia, washiriki 1,500 toka ndani ya nchi walishiriki maonyesho hayo mwaka 2003, ikilinganishwa na washiriki 1,250 mwaka 2002. Aidha, kiasi cha maulizo yenye thamani ya dola 2,239 Milioni yalipokelewa toka nje wakati wa maonyesho ya DITF 2003, ikilinganishwa na maulizo yenye thamani ya dola 15.5 milioni yaliyopokelewa mwaka 2002. Hii ikiwa ni ongezeko la asilimia 30.8. Pia kiasi cha dola 811 millioni zilikusanywa katika mauzo ya papo kwa papo wakati wa maonyesho ya mwaka 2003 ikilinganishwa na dola 610 millioni zilizokusanywa mwaka 2002, ikiwa ni ongezeko la asilimi 32.9.

Jedwali 14.2:   Washiriki wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa wwa Kipindi cha 2000 – 2003

 

Waonyeshaji

2000

2001

2002

2003

Wawakilishi wa kiserikali toka nje

13

14

11

10

Nchi zilizoshiriki

28

30

30

22

Makampuni toka nje ya nchi

300

315

331

350

Washiriki wa Ndani

1,145

1,250

1,405

1,500

Jumla

1,486

1,609

1,405

1,882

Chanzo: Bodi ya Biashara ya Nje

228. Mwaka 2003, kwa mara ya kwanza, katika eneo la Afrika Mashariki, Tanzania ilikuwa mwenyeji wa maonyesho ya sita ya kimataifa ya kibiashara ya nchi za kiafrika na Kiarabu “ (6th Afro-Arab Trade Fair) yaliyofanyika Dar es Salaam kati ya tarehe 5 – 14 Desemba 2003. Maonyesho haya yalihudhuriwa na nchi 33 za Kiafrika na Kiarabu na Mashirika ya Kimataifa 5. Makampuni zaidi ya 1000 kutoka ndani yalishiriki maonyesho haya. Pia, maagizo ya kibiashara yenye thamani ya dola 171,439,429.37 yalitolewa yakihusisha asilimia 71 ya mauzo ya nje na asilimia 28 kuagiza na asilimia 1 mauzo ya ndani.

Jedwali Na.58(MATUMIZI YA SARUJI NCHINI)

Jedwali Na.59(UZALISHAJI WA BAADHI YA BIDHAA VIWANDANI)

Jedwali Na.60(VIWANDA: IDADI YA WATU WALIOAJIRIWA*)

Jedwali Na.61(VIWANDA: GHARAMA ZA KAZI*)

Jedwali Na.62(VIWANDA: MUHTASARI WA MATOKEO *)

Jedwali Na.63('VIWANDA - MUHTASARI WA MATOKEO KIMKOA*)

Jedwali Na.65(VIGEZO VYA UFANISI KATIKA SEKTA YA VIWANDA)

Back Top