MAENDELEO
YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI
WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU
KATIKA MAENDELEO | |
||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | ||||||||
Kilimo |
||||||||
MAJI |
||||||||
Utangulizi
261. Katika mwaka 2003, Serikali iliendelea kutekeleza Sera ya Maji kwa kupanua wigo wa ushiriki wa jamii katika uandaaji wa miradi ya maji, ujenzi wa miundombinu ya maji, uendeshaji, ukarabati na utunzaji wa miradi ya maji nchini. Aidha, Serikali, iliendelea kutekeleza mikakati mbalimbali inayolenga kuboresha na kuimarisha mfumo wa ukusanyaji wa takwimu na taarifa za maji juu na chini ya ardhi kwenye mabonde yote nchini. Huduma
ya Maji Vijijini 263. Kumekuwepo na ongezeko la usambazaji wa maji vijijini kutoka asilimia 52.8 mwaka 2002 hadi asilimia 53.5 mwaka 2003 kutokana na kukamilika kwa miradi mikubwa ya kitaifa. Baadhi ya miradi hiyo ni ya Wanging'ombe, Handeni, Kiabakari, Makondeko, Maswa, Ntomoko/ Mwisanga, Isaka, Magu na Chalinze. Katika mwaka 2003, kulifanyika ukarabati wa miundombinu katika maeneo ya Dumila, Migoli, Malya, Kiponzelo, Mwamapuli/Bulenya, Uchira, Njombe, Umbwe-Onana, Rombo, Chalinze, Igunga, Hanang', Lushoto, Mugango/Kiabakari, Magu, Iramba, Musoma Vijijini, Manyoni, Nachingwea, Same, Tunduma na Masasi. 264. Hadi kufikia mwaka 2003 bodi 30 za kusimamia mamlaka za maji zimeanzishwa katika wilaya mbalimbali nchini. Pia, kufikia Desemba 2003, jumla ya kamati za maji 8,363 zilianzishwa kukiwepo mifuko ya maji 7,226 yenye jumla ya shilingi bilioni 1.3. Jumla ya mamlaka za aina hii 46 zilizoanzishwa katika wilaya mbalimbali hapa nchini zilikuwa chini ya bodi za wilaya. Katika mwaka 2003, visima vipatavyo 7 vilifanyiwa ukarabati, pia kulifanyika utafiti wa maeneo ya kuchimba visima. Aidha, visima 190 vilichimbwa kwa gharama za watu binafsi na mashirika yasiyo ya kiserikali. Mradi wa Hifadhi ya Mazingira, katika Ziwa Victoria chini ya Kitengo cha Ubora wa Maji na Mfumo wa Ikolojia uliendelea. Huduma
ya Maji Mijini Jedwali Na.77(IDADI YA MAENEO YALIYOFANYIWA UTAFITI WA MAJI CHINI YA ARDHI KWA MWAKA 2002) Jedwali Na.79(JUMLA YA VISIMA VILIVYOCHIMBWA NCHINI MWAKA 2000/2001) Jedwali
Na.79A(HALI YA KAMATI ZA MAJI NA MIFUKO YA MAJI VIJIJINI- 2002) |
||||||||