|
Usafiri
wa Reli
Shirika
la Reli Tanzania
241.
Shirika la Reli Tanzania lilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani 1,442,713
mwaka 2003 ikilinganishwa na tani 1,445,757 mwaka 2002, sawa na upungufu
wa asilimia 0.2. Kwa upande wa abiria, Shirika lilisafirisha abiria 683,481
mwaka 2003 ikilinganishwa na abiria 684,796 mwaka 2002 sawa na upungufu
wa asilimia 0.2. Aidha, kutokana na huduma zilizotolewa, Shirika limeweza
kupata mapato ya shilingi 61.5 bilioni mwaka 2003 ikilinganishwa na shilingi
58.3 bilioni zilizopatikana mwaka 2002, sawa na ongezeko la asilimia 5.5.
Pamoja na kupungua kwa uchukuzi wa mizigo na abiria, mapato ya shirika
yaliongezeka kutokana na kupanda kwa bei za usafirishaji. Aidha, katika
mwaka 2003, Shirika la Reli Tanzania lilikabiliwa na matatizo ya uchakavu
na uhaba wa mabehewa na injini, uchakavu wa njia za mawasiliano, na ajali.
Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)
242. Katika mwaka 2003, mizigo iliyosafirishwa kupitia Mamlaka ya Reli
ya Tanzania na Zambia (TAZARA) ilipungua hadi kufikia tani 613,693 toka
tani 677,000 mwaka 2002, sawa na upungufu wa asilimia 9.4. Idadi ya abiria
waliosafirishwa katika mwaka 2003 ilishuka kwa asilimia 4.4 kutoka abiria
1,068,287 mwaka 2002 hadi abiria 1,021,384 mwaka 2003. Mamlaka ilipata
jumla ya shilingi 26,266 milioni mwaka 2003, ikilinganishwa na shilingi
24,335 milioni mwaka 2002, sawa na ongezeko la asilimia 7.9. Pamoja na
ongezeko la mapato katika mwaka 2003, yalikuwepo matatizo ya uhaba wa
fedha za uendeshaji wa shughuli za Mamlaka, uchakavu na uhaba wa vitendea
kazi ikiwa ni pamoja na injini na mabehewa.
Usafiri
wa Anga
243. Katika mwaka 2003, huduma za usafiri wa anga nchini ziliendelea kutolewa
na mashirika kadhaa ya ndege ambayo idadi kubwa humilikiwa na sekta binafsi.
Baadhi ya makampuni ya ndege ya ndani ya nchi ambayo yaliendelea kutoa
huduma hizo ni pamoja na Air Tanzania Company Limited (ATCL), Precision
Air, Wakala wa Ndege za Serikali, Coastal Travel, Regional Air Services,
Eagle Air, Air Excel, Flight Link, na Zan Air. Katika mwaka 2003, safari
za anga ziliongezeka toka 123,136 mwaka 2002 hadi 153,465 mwaka 2003,
sawa na ongezeko la asilimia 24.6. Idadi ya abiria wa ndani na kutoka
nje iliongezeka kufikia 1,521,191 mwaka 2003 ikilinganishwa na abiria
1,356,525 mwaka 2002. Kulikuwepo ushindani mkubwa katika usafiri wa anga
kwenye masoko ya ndani na nje ya nchi.
Kampuni
ya Ndege Tanzania (ATCL)
244. ATCL ilitimiza mwaka mmoja tangu ilipoanza shughuli zake mwaka 2002.
Jumla ya abiria 149,540 walisafiri kwa ndege za Kampuni mwaka 2003, ikilinganishwa
na abiria 134,370 mwaka 2002, sawa na ongezeko la asilimia 11.2. Aidha,
kati ya wasafiri hao, 70,342 walikuwa wa safari za nje ya nchi, na 79,198
wa safari za ndani. Kwa upande wa mizigo, jumla ya tani 1,488 za mizigo
zilisafirishwa mwaka 2003 ikilinganishwa na tani 2,232.6 mwaka 2002, sawa
na upungufu wa asimilia 33.4. Pamoja na upungufu huo, kulikuwepo na mafanikio
katika ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya mara mbili kutoka dola 1.2 milioni
mwezi Desemba, 2002 hadi dola 2.8 milioni mwaka 2003. Aidha, mafanikio
mengine yaliyopatikana ni pamoja na ongezeko la vituo vya safari kutoka
7 mwaka 2002 hadi 15 mwaka 2003; ongezeko la safari kutoka 28 mwaka 2002
hadi 97 mwaka 2003; ongezeko la kiwango cha ndege kutoka asilimia 5 mwaka
2002 hadi asilimia 90 mwaka 2003; na ongezeko la ndege kutoka moja mwaka
2002 hadi tano mwaka 2003.
Makampuni
mengine ya Ndege
245. Katika mwaka 2003, makampuni mengine binafsi ya ndege yalisafirisha
nchini abiria 579,107 ikilinganishwa na abiria 475,734 mwaka 2002, sawa
na ongezeko la asilimia 21.7. Jedwali 16.2 linaonyesha idadi ya abiria
waliosafirishwa na ndege nchini.
Jedwali na. 16.2: Idadi ya
Abiria Waliosafirishwa
na Ndege
Nchini
| Kampuni za Ndege |
Idadi ya Abiria Waliosafirishwa |
|
Mwaka 2002 |
Mwaka 2003 |
| Kampuni ya Ndege Tanzania
(ATCL) |
134,370 |
149,540 |
| Precision Air |
174,926 |
248,375 |
| Coastal Travel |
64,762 |
76,856 |
| Regional Air Services |
30,241 |
23,179 |
| Eagle Air, |
4,799 |
Imesimamisha huduma |
| Air Excel |
14,220 |
Imesimamisha huduma |
| Flight Link |
1,357 |
413 |
| Zan Air |
30,044 |
35,372 |
| Makampuni Mengineyo |
31,015 |
45,372 |
| Jumla |
475,734 |
579,107 |
Chanzo: Wakala wa Usalama
wa Anga (TCAA)
Usafiri
wa Majini
Uchukuzi
wa Baharini
246. Katika mwaka 2003, bandari ya Dar-es-Salaam ilihudumia jumla ya
tani 4,861 milioni ikilinganishwa na tani 4,557 milioni katika mwaka
2002, sawa na ongezeko la asilimia 6.3. Kati ya shehena yote iliyohudumiwa
katika bandari ya Dar-es-salaam, tani 1,868 milioni, sawa na asilimia
38.4 ilihudumiwa na Kitengo cha Kontena chini ya mwendeshaji binafsi.
Aidha, mwaka 2003, jumla ya meli 4,034 zilihudumiwa ikilinganishwa na
meli 3,894 zilizohudumiwa mwaka 2002, sawa na ongezeko la asilimia 3.6.
Kwa upande wa tija mwaka 2003, makontena 22.6 yalihudumiwa kwa saa ikilinganishwa
na makontena 20 kwa saa katika mwaka 2002. Pia, muda wa makontena kukaa
bandarini uliendelea kushuka toka wastani wa siku 11.6 mwaka 2002 hadi
siku 11.3 mwaka 2003.
SINOTASHIP
247. Katika mwaka 2003, meli za kampuni ya SINOTASHIP inayomilikiwa
na Serikali za China na Tanzania zilifanya safari 25 ikilinganishwa
na safari 41 mwaka 2002. Kupungua kwa safari za meli kumetokana na ukosefu
wa mizigo, ushindani mkali uliopo katika biashara ya uchukuzi na hali
mbaya ya uzalishaji wa mazao ya biashara iliyosababishwa na ukame. Aidha,
kampuni ilisafirisha jumla ya tani 253,241 za shehena mwaka 2003 ikilinganishwa
na tani 497,979 mwaka 2002, sawa na pungufu ya asilimia 49.1. Mapato
ya kampuni yalipungua toka dola 9.3 milioni mwaka 2002 hadi dola 6.5
milioni mwaka 2003, sawa na pungufu ya asilimia 30.
Usafiri
katika Maziwa
248. Huduma za uchukuzi na usafiri katika maziwa ya Victoria, Tanganyika
na Nyasa hutolewa na Kampuni inayomilikiwa na Serikali iitwayo Kampuni
ya Huduma za Meli pamoja na makampuni binafsi. Kampuni ya Huduma za
Meli ina jumla ya meli 15, kumi ziko katika Ziwa Victoria, tatu katika
Ziwa Tanganyika na mbili katika Ziwa Nyasa. Meli hizi hutoa huduma za
ndani ya nchi na jirani zilizoko katika mwambao wa maziwa hayo. Nchi
hizo ni pamoja na Kenya na Uganda katika Ziwa Victoria; Burundi, Jamhuri
ya Kidemokrasia ya Kongo na Zambia katika Ziwa Tanganyika; na Malawi
katika Ziwa Nyasa. Mwaka 2003, Kampuni ilisafirisha jumla ya abiria
347,564 ikilinganishwa na abiria 370,588 mwaka 2002, sawa na pungufu
ya asimilia 6.2. Kwa upande wa mizigo, Kampuni ilisafirisha jumla ya
tani 143,751 mwaka 2003 ikilinganishwa na tani 144,473 mwaka 2002, sawa
na pungufu ya asimilia 0.5.
HUDUMA
ZA MAWASILIANO
Shirika
la Posta
249. Katika mwaka 2003, barua zilipungua kwa asilimia 2.7 kutoka barua
18.7 milioni mwaka 2002 hadi barua 18.2 milioni. Hata hivyo, barua ziendazo
nchi za nje ziliongezeka kwa asilimia 4.8 kutoka barua 6.2 milioni mwaka
2002 hadi kufikia barua 6.5 milioni mwaka 2003. Barua za rejesta ziliongezeka
kwa asilimia 32.5 kutoka barua 324,204 mwaka 2002 hadi kufikia barua
429,688 mwaka 2003. Pia, barua za rejesta ziendazo nje ya nchi ziliongezeka
kwa asilimia 45 kutoka 31,204 mwaka 2002 hadi kufikia 46,218 mwaka 2003.
Mwaka 2003, vifurushi vilivyotumwa ndani ya nchi vilipungua kwa asilimia
7.9 kutoka vifurushi 31,969 mwaka 2002 hadi vifurushi 29,422 mwaka 2003.
Aidha, vifurushi vilivyotumwa nje ya nchi viliongezeka kwa asilimia
17.5 kutoka vifurushi 5,700 mwaka 2002 hadi kufikia vifurushi 6,699
mwaka 2003.
250.
Huduma ya kutuma barua, fedha na ujumbe kwa njia ya EMS, zimeonyesha
mafanikio makubwa mwaka 2003. Vitu vilivyotumwa ndani ya nchi kwa njia
ya EMS viliongezeka kwa asilimia 18.9 kutoka vitu 260,486 mwaka 2002
hadi vitu 309,736 mwaka 2003. Kwa vilivyotumwa nje ya nchi kwa EMS,
kulikuwa na ongezeko la asilimia 49.5 kutoka vitu 19,675 mwaka 2002
hadi kufikia vitu 29,418 mwaka 2003. Utumaji wa fedha kwa njia ya EMS
uliongezeka kwa asilimia 14.7 kutoka utumaji 188,790 mwaka 2002 hadi
kufikia utumaji 216,700 mwaka 2003. Kwa upande wa ujumbe, kulikuwa na
ongezeko la asilimia 41.8 kutoka mara 13,515 mwaka 2002 hadi kufikia
19,164 mwaka 2003. Katika mwaka 2003, Kampuni ya Posta ilipata faida
ya jumla ya sh. 14.9 bilioni.
Huduma
za Simu
251. Katika mwaka 2003, uwezo wa mitambo ya simu za msingi wa Kampuni
ya Simu Tanzania (TTCL) ulipungua kutoa njia 244,381 hadi kufikia 233,352,
sawa na punguzo la asilimia 4.7. Hii ilitokana na kuondoa mitambo ya
zamani na kuweka mitambo mipya ya kisasa kulingana na mahitaji ya wateja.
Pia, idadi ya simu zilizounganishwa zilipungua kutokana na zoezi la
kuhakiki na kuweka takwimu sahihi za wateja halali ambalo lilisababisha
wateja wasiolipa ankara zao kwa muda mrefu kuondolewa. Zoezi lilikumba
wateja wengi na hivyo kusababisha idadi ya simu zilizounganishwa kupungua
sana.
252.
Idadi ya watumiaji wa simu za mkononi iliongezeka kwa asilimia 61 kutoka
simu za mkononi 805,000 mwaka 2002 hadi simu 1,298,000 mwaka 2003. Ongezeko
hili limetokana na mahitaji makubwa ya simu za mkononi kwa wateja. Katika
mwaka 2003, kampuni za simu za mkononi ziliendelea kuwa ni Celtel, Vodacom,
Zantel na Mobitel. Mchanganuo wa ongezeko la wateja wa simu za mkononi
ni kama ilivyoainishwa katika jedwali Na. 16.3 hapa chini.
Jedwali Na. 16.3:
Ongezeko la Simu za Mkononi kwa Kampuni
Jina la Kampuni |
Idadi ya
Wateja |
| 2002 |
2003 |
| MOBITEL |
190,000 |
210,000 |
| VODACOM |
430,000 |
700,000 |
| ZANTEL |
35,000 |
68,000 |
| CELTEL |
150,000 |
320,000 |
| JUMLA |
805,000 |
1,298,000 |
Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
Udhibiti wa
shughuli za Mawasiliano
253. Mwaka
2003, Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mawasiliano ilianzishwa kufuatia
kuunganishwa kwa Tume ya Mawasiliano Tanzania na Tume ya Utangazaji
Tanzania na kupata Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania. Kazi za Mamlaka
mpya ni pamoja na kudhibiti makampuni yanayotoa huduma za kusafirisha
vifurushi na vipeto na kuboresha, kupanga na kusimamia matumizi ya masafa
ya mawasiliano. Mchanganuo wa watoa huduma za aina mbalimbali za mawasiliano
ni kama inavyoonyeshwa katika Jedwali No. 16.4.
Jedwali Na.16.4: Mchanganuo
wa Watoa Huduma za Mawasiliano
| Watoa Huduma |
Idadi ya Watoa Huduma |
|
2002 |
2003 |
| Simu za Mkononi |
4 |
4 |
| Watoa huduma za kusafiririsha takwimu
kwa mtandao wa Tarakishi |
14 |
18 |
| Watoa huduma za mtandao
wa Tarakishi |
19 |
21 |
| Posta |
15 |
16 |
Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania
|
|