MAENDELEO
YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI
WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU
KATIKA MAENDELEO | |
||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | ||||||||
Kilimo |
||||||||
NISHATI |
||||||||
Mfumo wa Nishati 254. Nishati ni nyenzo muhimu katika kuchochea ukuaji wa uchumi, kuboresha huduma za jamii na kupambana na umaskini. Vyanzo vikuu vya nishati ni mafuta, umeme unaotokana na nguvu za maji, makaa ya mawe na gesi asilia inayopatikana Songo Songo itakayoanza kuzalishwa mwaka 2004. Mwenendo wa matumizi ya nishati katika Tanzania unaonyesha kwamba kiasi cha asilimia 90 inatokana na tungamotaka, asilimia 8.0 hutokana na mafuta ya petroli na asilimia 1.2 hutokana na umeme. Vyanzo vingine vya nishati kama makaa ya mawe, mionzi ya jua na upepo huchangia chini ya asilimia 10. 255. Mchanganuo wa nishati kutokana na vyanzo mbalimbali unaonyesha kuwa watanzania wanategemea nishati itokanayo na bidhaa za misitu. Mkaa unaotokana na kuchoma kuni huuzwa katika miji na huchangia sana kuharibu mazingira. Tanzania ina rasilimali kubwa ya vyanzo vya nishati ya umeme, gesi asilia, tungamotaka, makaa ya mawe na nishati inayojadikika. Vyanzo vingi vya nishati bado havijaendelezwa. Hata hivyo juhudi na mikakati ya kuendeleza vyanzo vya nishati ya gesi asilia, makaa ya mawe, umeme wa nguvu za maji pamoja na utafutaji wa mafuta zinafanyika. Umeme 257. Uwezo uliowekezwa wa kuzalisha umeme unaotokana na nguvu za maji (hydo-power) na mafuta kwa ajili ya Gridi ya Taifa ulikuwa megawati 618.6 mwaka 2003. Uwezo uliowekezwa kwa IPTL ni megawati 100, kampuni ya makaa Kiwira megawati 4, na ulionunuliwa kutoka Uganda, megawati 8, na Zambia megawati 5. Kiasi cha umeme kilichozalishwa kwa kutumia maji na mafuta kilipungua na kufikia saa za gigawati 2,553.9 mwaka 2003 ikilinganishwa na saa za gigawati 2720.1 zilizozalishwa mwaka 2002. Uwezo uliowekezwa wa kuzalisha umeme katika mifumo inayojitegemea ulikuwa megawati 26.1 mwaka 2003. Aidha, uzalishaji wa umeme katika mifumo inayojitegemea uliongezeka kutoka saa za gigawati 71.2 mwaka 2002 hadi kufikia saa za gigawati 114.3 mwaka 2003. 258. Mauzo ya umeme kwa matumizi ya nyumbani yalipungua kutoka saa za gigawati 1,120 mwaka 2002 na kufikia saa za gigawati 1016.6 mwaka 2003. Aidha, wateja waliounganishiwa umeme waliongezeka kutoka wateja 465,763 mwaka 2002 na kufikia wateja 514,870 mwaka 2003. Mauzo ya umeme kwa matumizi ya viwandani na biashara yalipungua na kufikia kilowati 775.1 mwaka 2003 ikilinganishwa na kilowati 823 mwaka 2002. Pia kiasi cha umeme kilichouzwa Zanzibar kiliongezeka kutoka saa za gigawati 133 mwaka 2002 hadi kufikia saa za gigawati 145.8 mwaka 2003. Umeme uliopotea njiani uliongezeka na kufikia kilowati 730.7 mwaka 2003 ikilinganishwa na kilowati 714.0 mwaka 2002. Petroli 260. Wastani wa bei za rejareja za mafuta kwenye vituo vya mafuta mwaka 2003 zilikuwa sh.672 kwa lita ya petroli, sh.639 kwa lita ya dizeli na sh. 505 kwa lita ya mafuta ya taa ikilinganishwa sh. 576 kwa lita ya petroli, sh. 546 kwa lita ya dizeli na sh. 426 kwa lita ya mafuata ya taa mwaka 2002. Katika mwaka 2003, matumizi ya mafuta ya petroli yaliongezeka na kufikia tani za ujazo 1.3 milioni ikilinganishwa na tani za ujazo 1.1 milioni mwaka 2002. Jedwali Na.74(UWEZO WA MITAMBO YA UMEME NA KIASI CHA UMEME ULIOTENGENEZWA KWA VITUO) Jedwali Na.75(MAUZO YA UMEME KWA WATUMIAJI MBALIMBALI) Jedwali
Na.76(MAUZO YA UMEME KWA MIKOA (GWH)) |
||||||||