MAENDELEO
YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI
WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU
KATIKA MAENDELEO | |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Kilimo |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
UJENZI
NA MAENDELEO YA ARDHI |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
UJENZI
229. Mwaka 2003, sekta ya ujenzi ilikua kwa kiwango sawa na cha mwaka 2002 cha asilimia 11. Ukuaji huu wa wastani umeendelea kuchangiwa na kuwepo kwa shughuli za ujenzi wa majengo yasiyo ya kuishi, ujenzi wa barabara, uendelezaji wa ardhi ukijumuisha ujenzi wa nyumba za kuishi. Aidha, mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa halisi ulikuwa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.0 mwaka 2002. 230. Mwaka 2003, matengenezo ya kawaida ya barabara kuu kilometa 5,644 na madaraja 727 yalikamilishwa ikilinganishwa na kilometa 5,057 na madaraja 320 yaliyokamilishwa mwaka 2002. Kilometa 6,587 na madaraja 907 ya barabara za mikoa zilifanyiwa matengenezo mwaka 2003 ikilinganishwa na kilometa 3,780 na madaraja 180 mwaka 2002. Aidha, mwaka 2003 daraja kubwa la mto Rufiji (Daraja la Mkapa) linalilounganisha mikoa ya Dar es Salaam na ile ya Kusini mwa Tanzania lilikamilika. 231. Mafanikio katika sekta hii mwaka 2003 yametokana na utekelezaji wa mikakati na sera ya ujenzi, inayoweka mkazo katika ushirikishwaji wa sekta binafsi. Aidha, kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara nchini zimeendelea kutekelezwa kwa ufanisi hasa kutokana na kuwepo kwa fedha za mfuko wa barabara na taratibu nzuri za udhibiti wa makandarasi na washauri waelekezi. Kwa ujumla, sera ya ujenzi mwaka 2003 imetoa hamasa kubwa kwa wadau wa sekta hii. Mtandao
wa barabara |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Jedwali Na. 15.1: Hali
ya Mtandao wa Barabara Nchini Mwaka 2003
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Makandarasi
233. Kwa kutambua umuhimu wa umakini katika sekta ya ujenzi mwaka 2003, Bodi inayoshughulikia usajili wa makandarasi ilisajili makandarasi 654 ikilinganishwa na makandarasi 717 mwaka 2002, sawa na upungufu wa asilimia 13. Kwa ujumla, makandarasi 2,911 mwaka 2003 walisajiliwa ikilinganishwa na makandarasi 2,565 mwaka 2002, sawa na ongezeko la asilimia 13. Pamoja na usajili wa makandarasi mwaka 2003, tafiti zilizofanywa zimebainisha kwamba makandarasi wengi wazalendo wako kwenye madaraja madogo madogo. Idadi yao ni zaidi ya asilimia 70 na hawawezi kufanyakazi zenye thamani ya zaidi ya shilingi 50 milioni. Kwa upande wa ujenzi wa barabara, karibu asilimia 90 ya makandarasi wazalendo imebainika kwamba hawawezi kufanya kazi yenye thamani ya shilingi 300 milioni, kiwango ambacho ni wastani wa kujenga kilometa moja ya barabara ya lami. Uratibu
wa Kazi za Makandarasi |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| Jedwali Na 15.2: Makandarasi Waliosajiliwa kwa
Taaluma za Madaraja Mbalimbali 2003
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
MAENDELEO YA ARDHI 235. Katika mwaka 2003, Sheria ya Ardhi Na. 4 ya mwaka 1999 ilifanyiwa marekebisho katika vifungu vya 37,125 na 142 kwa lengo la kumwezesha mmiliki wa ardhi kuweza kuitumia kama dhamana ya kupata mikopo kutoka katika mabenki na taasisi za fedha kwa urahisi na ufanisi. Aidha, upimaji wa mashamba katika vijiji 6 vya mfano wilaya ya Mbozi mkoa wa Mbeya ulifanyika. 236. Katika kuendeleza Sera ya Taifa ya Makazi ya mwaka 2000, Mpango wa Kimkakati wa mji wa Tunduma na Rasimu za Hali ya mazingira ya miji ya Lushoto na Masasi ziliandaliwa. Pia utaratibu wa mikopo kwa ajili ya ujenzi wa nyumba kwa watumishi wa Serikali na Rasimu ya Mpango wa Taifa wa Kuendeleza Nyumba (National Housing Programme) zilikamilishwa. Shirika la Nyumba la Taifa lilijenga nyumba 218 katika mikoa ya Dar es salaam, Mwanza (Isamilo) na Arusha (Kijenge). Ukaguzi na uendelezaji wa makazi katika mikoa ya Tabora, Kigoma, Rukwa, Mwanza, Mara na Ruvuma kwa lengo la kutambua maeneo yaliyokuwa tayari kuendelezwa kimji, maeneo ya wazi ya kuhifadhi na uendelezaji wa maeneo kongwe katika miji ya Iringa, Morogoro na Mtwara ulifanyika. Aidha, upimaji kwa kutumia “Global Positioning System” na utayarishaji wa ramani kwa kutumia mashine za kisasa (digital system) ulitumika katika kutayarisha ramani 205 katika uwiano mbalimbali na kupiga picha za anga kwa ajili ya kuandaa ramani katika miji 38 kanda ya Ziwa. Kama inavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 15.3. Katika kipindi cha mwaka 2003, Mradi wa Kupima viwanja katika jiji la Dar es salaam uliendelea ambapo viwanja 26,723 vilipimwa katika sehemu za Tuangoma, Kisota, Mbweni, Buyuni, Mbweni JKT, Bunju, Mwanagati na Mivumoni kama inavyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 15.4. 237. Katika mwaka 2003, hati za kumiliki ardhi 1,037 zilisajiliwa ikilinganishwa na hati 2,976 mwaka 2002. Nyaraka 5,571 zilisajiliwa katika mwaka 2003 ikilinganishwa na nyaraka 4,856 mwaka 2002 kama inavyoonyeshwa kwenye Jedwali Na. 15.5. Ili kutambua viwanja vilivyopimwa na kubaini wamiliki wake, kitengo cha Mfumo wa Mtandao wa Taifa kiliwezesha kutambuliwa viwanja 51,000 katika Jiji la Dar es Salaam na jumla ya hati 86,770 za wamiliki wa viwanja kwa nchi nzima. Aidha, katika kutatua migogoro ya ardhi, jumla ya kesi 134 za ardhi zilifunguliwa katika Mabaraza ya Ardhi mikoani na Baraza la Rufaa la Ardhi ambapo kesi 61 ziliamuliwa. Pia, kesi 678 zilifunguliwa katika Mabaraza ya Nyumba ya Mikoa na katika Baraza la Rufaa la Nyumba na kesi 959 ambazo zilifunguliwa na zilizokuwa zinaendelea ziliamuliwa. 238. Katika kuongeza kasi ya uwekezaji nchini, mfumo wa Hazina ya Ardhi (Land Bank) ulianzishwa. Mfumo huu una lengo la kuainisha sehemu zinazofaa kwa uwekezaji nchini. Jumla ya vipande vya ardhi 743 vyenye ukubwa wa hekta milioni 2.6 vimebainishwa kwa ajili ya kuingizwa kwenye Hazina ya Ardhi. Jedwali Na. 15.3: Orodha ya Miji
Iliyopigwa Picha za Anga
Jedwali Na.15.4: Viwanja
Vilivyopimwa Katika Maeneo ya Jiji la Dar Es Salaam
|
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||