MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | SUALA MAALUMU KATIKA MAENDELEO |
MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI

Uendelezaji wa Sekta Binafsi
Masuala Maalum Yanayohusu Sekta Zote

Maendeleo ya Juhudi za Kupambana na Umasikini

   
MAENDELEO YA JUHUDI ZA KUPAMBANA NA UMASKINI  
Utangulizi

157. Katika mwaka 2003, serikali iliendelea na juhudi za kupambana na umaskini nchini kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa ndani na nje ya nchi. Wiki ya Umaskini iliyofanyika Oktoba mwaka 2003 ilitoa fursa kwa wadau kuweza kujadili kwa kina utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini nchini na hatua zilizofikiwa. Aidha, katika Wiki ya Umaskini ulifanyika uzinduzi wa kufanya mapitio Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Hii inatokana na serikali kujiwekea malengo ya kila baada ya miaka mitatu kupitia upya Mkakati huu. Taarifa ya utekelezaji wa Mkakati ya mwaka 2002/03 ilihitimisha awamu ya kwanza ya miaka mitatu.

Mapitio ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini
158. Utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini nchini ulifikia katika mwaka wa tatu na wa mwisho katika awamu ya kwanza ya utekelezaji wake. Kulikuwepo na mafanikio katika utekelezaji wa Mkakati wa kwanza nchini hasa katika sekta zilizopewa kipaumbele, hususan elimu, afya, barabara vijijini, na maji. Pia, kulikuwepo na mafanikio katika maeneo ya masuala ya uchumi jumla na katika mageuzi kwenye sekta mbalimbali zikijumuisha sekta za fedha, utumishi wa umma na serikali za mitaa. Majadiliano kuhusu mapitio ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini yalianza katika ngazi za wadau mbalimbali ikijumuisha serikali, mashirika yasio ya kiserikali, vikundi vya hiari, asasi za dini na binafsi. Madhumuni ya kufanya mapitio ya Mkakati huu ni kubaini mafanikio katika utekelezaji; matatizo yaliyojitokeza; na mapungufu yanayoweza kuwepo kwa lengo la kuuboresha na kuharakisha utekelezaji wa awamu ijayo ya Mkakati. Katika kufanya mapitio ya Mkakati, mkazo umewekwa katika kupanua zaidi ushirikishwaji na umiliki wa mchakato.

Ufuatiliaji na Tathmini ya Umaskini
159. Mfumo wa Kufuatilia umaskini nchini uliendelea kama ulivyobainishwa katika Mpango Kamambe wa Ufuatiliaji kupitia vikundi vya Sensa na Uchunguzi; Utafiti na Uchambuzi; Takwimu za Kiutawala; na Usambazaji Taarifa, Uhamasishaji na Uelimishaji. Mafanikio ya mfumo huu katika mwaka 2003 ni pamoja na kuchapisha Taarifa ya Umaskini na Maendeleo ya Watu ya mwaka 2003, Taarifa ya Utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini ya mwaka 2002/03; Usambazaji wa matokeo ya Tafiti ya Mapato na Matumizi ya Kaya-2000/01 na matokeo ya jumla ya Sensa ya Watu na Makazi 2003; na kufanyika kwa Wiki ya Umaskini nchini mwezi Oktoba 2003. Aidha, mfumo huu umewezesha kufanyika kwa utafiti shirikishi wa kutathimini umaskini nchini uliokusanya maoni ya wananchi katika sehemu na hali ya maisha mbalimbali ya jamii kuhusu masuala ya umaskini. Pia, warsha mbalimbali za kikanda zilifanyika kwa ajili ya kupata takwimu za kiutawala.

Hali ya Utekelezaji wa Mkakati wa Kupunguza Umaskini Katika Sekta za Kipaumbele
160. Katika mwaka 2002/03, serikali iliendelea kuelekeza sehemu kubwa ya rasilimali kwenye sekta zilizobainishwa katika kupunguza umaskini kwa lengo la kukuza maendeleo ya rasilimali watu; utoaji wa huduma za msingi za kijamii; kuimarisha miundombinu ya kiuchumi na kuongeza uzalishaji katika kilimo na kuhakikisha upatikanaji wa chakula.

Maendeleo ya Rasilimali Watu
161. Katika mwaka 2002/03, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali iliendelea kutekeleza Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi uliokuwa na malengo ya kupanua uandikishwaji wa watoto ; kuongeza ubora wa elimu ; kujenga uwezo ; kuboresha na kuimarisha utawala na mpangilio wa kiasasi. Mafanikio katika mwaka 2003 yanaoneshwa katika jedwali lifuatalo. Katika mwaka 2002/03, serikali ikishirikiana na wadau wengine wa sekta hii iliandaa awamu ya pili ya Mkakati wa Sekta ya Afya unaolenga kutekeleza malengo muhimu ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini. Aidha, serikali katika uendelezaji wa sekta ilianzisha mkakati wa Kitaifa wa kupambana na UKIMWI; kufanya marekebisho katika Sera ya Afya ya mwaka 1990; na kuongeza chanjo za surua hadi kufikia asilimia 89. Katika mwaka 2002/03, usambazaji wa maji vijijini uliongezeka kutoka asilimia 52.8 mwaka 2002 hadi asilimia 53.5 mwaka 2003. Aidha, katika kipindi hicho upatikanaji maji sehemu za mijini ulibakia asilimia 73 kama ilivyokuwa mwaka 2002 wakati ambapo huduma ya maji taka iliongezeka kwa asilimia 10 mwaka 2002 hadi asilimia 17 Juni 2003.

Jedwali: 9.1     Baadhi ya Viashirio Katika Sekta ya Elimu

Viashiria

Kipimo

2002

2003

Utambuzi wa shule(school mapping)

Wilaya

82

98

Kiwango cha Jumla  ya uandikishaji

Asilimia

100.4

105.3

Kiwango halisi cha Uandikishaji - miaka (7-13)

Asilimia

80.7

88.5

Walimu mafunzoni

Idadi

9728

15285

Uandikishwaji shule za sekondari

Idadi

323,318

345,411

Uwiano wa uandikishaji kijinsia

Uwiano

1:0.87

1:0.93

Waliokatisha masomo

Asilimia

6.6

4.7

Chanzo: Wizara ya Elimu na utamaduni

Kilimo
162. Katika mwaka 2002/03, kipaumbele kilikuwa katika kuimarisha uwezo wa kuzalisha kwa wakulima wadogo na wafugaji pamoja na kuweka mazingira mwafaka ya kisheria yanayolenga katika kusukuma uwekezaji wa sekta binafsi. Mambo yaliyotekelezwa ni pamoja na marekebisho ya kodi na kufutwa kwa kodi ambazo zinaleta kero; kuongezeka kwa kilimo cha umwagiliaji; kupatiwa mafunzo kwa wataalam wa ughani 6,688 na mabwana na shamba wa vijiji 1,130.

Barabara
163. Katika mwaka 2002/03, serikali iliendelea kutenga kiasi cha sh. 1.84 bilioni kila mwezi kwa ajili ya kuimarisha barabara zinazounganisha mikoa mbalimbali kwa kufanya matengenezo ya kiwango cha lami sehemu zilizo kwenye barabara ya Ukanda wa Kusini ambazo ni Dar es Salaam-Lindi-Mingoyo na Ukanda wa Kati ambayo ni Dar es Salaam-Dodoma-Singida. Aidha, mpango wa ukarabati wa haraka ulianzishwa kwa ajili ya maendeleo ya barabara za wilayani, mijini na zile za vijijini zinazoingia barabara kuu. Jumla ya kilometa 7,049 sawa na asilimia 51.4 kati ya kilometa 13,727 za barabara vijijini zilifanyiwa matengenezo.

Jedwali Na. 9.2:  Matumizi ya Serikali Kuu Katika Sekta za Kipaumbele, Mwaka 1998/99 – 2003/04                                                                                                                                                                                                                                           Sh.bilioni

 

1998/99

1999/00

2000/01

2001/02

2002/03

2003/04

Halisi

Halisi

Halisi

Halisi

Halisi

Matarajio

Jumla ya Matumizi

338.9

414.3

499.6

753.8

953.7.0

1124

Elimu

164.9

218.0

254.9

344.9

436.2

502.3

Afya

72.5

81.2

100.7

142.1

186.7

197.3

Maji

14.4

14.5

18.3

32.5

51.9

64.4

Kilimo

14.9

21.6

19.1

31.9

60.2

93.1

Barabara

66.7

70.8

92.5

179.6

190.2

213

Mahakama

5.5

8.3

9.2

18.8

23.8

32.7

TACAIDS

0.0

0.0

0.0

4.0

5.3

21.2

Matumizi ya Kawaida

233.0

282.0

347.5

490.2

720.1

836.8

Elimu

117.6

158.9

189.2

282.1

422.9

471.1

Afya

50.7

53.9

70.3

90.9

149.1

177.6

Maji

7.1

5.4

8.1

15.5

16.5

17.5

Kilimo

8.6

13.7

10.3

17.2

36.0

47.7

Barabara

43.9

42.

60.7

65.7

71.9

84.5

Mahakama

5.

7.9

8.8

14.8

18.9

24.9

TACAIDS

0.0

0.0

0.0

4.0

4.5

8.1

Matumizi ya Maendeleo

105.9

132.4

147.1

263.5

248.3

293.3

Elimu

47.3

59.1

65.7

62.8

13.3

31.3

Afya

21.9

27.3

30.4

51.2

37.6

19.6

Maji

7.3

9.1

10.1

17.0

35.4

46.9

Kilimo

6.3

7.9

8.7

14.7

24.2

45.4

Barabara

22.8

28.6

31.7

113.9

118.3

128.5

Mahakama

0.3

0.4

0.4

4.0

4.2

7.8

TACAIDS

0.0

0.0

0.0

0.0

0.8

13.2

Chanzo:  Wizara ya Fedha

 
Back Top