MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA

Hali ya Uchumi wa Taifa
Hali ya Uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa
Sekta ya Nje
Fedha za Serikali
Fedha na Taasisi za Fedha
Rasilimali Watu

   
   
HALI YA UCHUMI NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA
HALI YA UCHUMI DUNIANI
Ukuaji wa Uchumi Duniani

24. Mwaka 2004, pato la dunia lilikua kwa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 4.0 mwaka 2003. Ukuaji huo ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuimarika kwa uchumi wa nchi zilizoendelea hasa Marekani na pia kasi kubwa ya ukuaji wa uchumi wa nchi za Asia zinazochipukia kiviwanda hususan, China na India. Aidha, kuongezeka katika uwekezaji rasilimali, biashara, na uzalishaji viwandani kulichangia ukuaji huo kwa kiasi kikubwa.

25. Pato la nchi zilizoendelea lilikua kwa asilimia 3.4 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 2.0 mwaka 2003, kutokana hasa na ongezeko la uzalishaji viwandani, ukuaji wa uwekezaji rasilimali katika biashara, na kuimarika kwa soko la ndani. Kwa upande wa nchi zinazoendelea, pato lilikua kwa asilimia 7.2 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 6.4 mwaka 2003. Ongezeko la pato kwa nchi zinazoendelea lilichangiwa na kuongezeka kwa uwekezaji rasilimali, na kuimarika kwa shughuli za uzalishaji viwandani kutokana na utekelezaji wa sera za kurekebisha uchumi. Pato la Afrika lilikua kwa asilimia 5.1 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2003, kiwango ambacho ni cha juu kabisa katika kipindi cha miaka kumi iliyopita.

Jedwali 2.1: Pato la Dunia 2000-2004 (Ukuaji %)

Sehemu

2000

2001

2002

2003

2004

Pato la Dunia

4.6

2.5

3.0

4.0

5.1

Nchi zilizoendelea

3.8

1.2

1.6

2.0

3.4

Nchi zinazoendelea

5.8

4.2

4.7

6.4

7.2

Nchi za Asia zinazoendelea

6.5

5.8

6.5

8.1

8.2

Amerika ya Kusini

3.6

0.5

-0.1

2.2

5.7

Afrika

3.2

4.0

3.6

4.6

5.1

Afrika Kusini mwa Jangwa la Sahara

3.4

3.9

3.6

4.2

5.1

Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Aprili 2005; Taarifa ya Hali ya Uchumi Duniani

Mwenendo wa Biashara Duniani

26. Mwaka 2004, kiwango cha biashara ya bidhaa na huduma duniani kiliongezeka kwa asilimia 9.9 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 4.9 mwaka 2003. Tofauti na ilivyokuwa mwaka 2003, ongezeko la biashara mwaka 2004 lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na nchi zilizoendelea kutokana na kuimarika kwa uchumi wa nchi hizo hususan, Marekani na Japan. Uuzaji wa bidhaa nje kwa nchi zilizoendelea uliongezeka kwa asilimia 8.1 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 2.8 mwaka 2003, ambapo kwa upande wa nchi zinazoendelea, uuzaji wa bidhaa nje uliongezeka kwa asilimia 13.8 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 10.7 mwaka 2003. Uagizaji bidhaa kwa nchi zilizoendelea uliongezeka kwa asilimia 8.5 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 3.6 mwaka 2003, na kwa upande wa nchi zinazoendelea uagizaji wa bidhaa uliongezeka kwa asilimia 15.5 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 8.9 mwaka 2003.

27. Farihisi ya bei ya bidhaa za viwandani iliongezeka kwa asilimia 8.8 mwaka 2004, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 13.4 mwaka 2003. Bei ya mafuta yasiyosafishwa iliongezeka kwa asilimia 30.7 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 15.8 mwaka 2003. Ongezeko kubwa la bei ya mafuta lilisababishwa hasa na kuongezeka kwa mahitaji ya nishati zitokanazo na mafuta katika nchi zinazochipukia kiviwanda hususan China na India. Bei ya bidhaa asilia iliongezeka kwa asilimia 18.8 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 7.1 mwaka 2003. Ongezeko la bei ya bidhaa asilia lilitokana hasa na kuongezeka kwa mahitaji ya bidhaa hizo kama malighafi katika viwanda vya nchi za Asia. Kasi ya upandaji bei kwa nchi zilizoendelea ilikuwa ni asilimia 1.6 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 1.5 mwaka 2003. Kwa upande wa nchi zinazoendelea, kasi ya upandaji bei ilikuwa asilimia 5.7 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 6.0 mwaka 2003. Kwa nchi za Afrika, kasi ya upandaji bei ilikuwa asilimia 7.7 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 10.6 mwaka 2003.

Hali ya Uchumi wa Bara la Afrika

28. Mwaka 2004, pato la bara la Afrika lilikua kwa asilimia 5.1 ikilinganishwa na asilimia 4.6 mwaka 2003. Mafanikio hayo yalichangiwa na kuimarika kwa uchumi wa dunia, misamaha ya madeni kwa nchi za Afrika, kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo, kuimarika kwa bei za bidhaa asilia, pamoja na kutekelezwa kwa sera za kurekebisha mifumo ya kuendesha uchumi. Hata hivyo, kiwango cha ukuaji wa pato la Afrika katika mwaka 2004 bado hakitoshi kuifikisha Afrika katika Malengo ya Maendeleo ya Milenia ifikapo mwaka 2015.

29. Pato la nchi za Afrika kusini mwa Jangwa la Sahara lilikua kwa asilimia 5.1 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2003. Ukuaji huo ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kupanda kwa bei za mafuta kulikozinufaisha nchi zinazotoa mafuta kama Angola, Chad na Equatorial Guinea, na pia kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo. Kupanda kwa bei ya mafuta kwenye soko la dunia kwa kiasi fulani kulizinufaisha nchi zinazozalisha mafuta na wakati huo huo kuathiri nchi zinazoagiza mafuta ikiwemo Tanzania. Bei ya mafuta yasiyosafishwa ilifikia zaidi ya dola za Marekani 50 kwa pipa mwishoni mwa mwaka 2004, kutoka wastani wa dola 30 mwaka 2003. Hata hivyo, migogoro ya kisiasa na vita iliendelea kuziathiri baadhi ya nchi kama vile Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Ivory Coast, na Zimbabwe.

30. Pamoja na matatizo ya kiuchumi yanayoikabili nchi ya Zimbabwe, pato la nchi za kusini mwa Afrika, ukiondoa Afrika Kusini, lilikua kwa asilimia 4.9 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 2.5 mwaka 2003. Kuimarika kwa uchumi katika sehemu hii ya Afrika kulitokana hasa na kuongezeka kwa uzalishaji wa mafuta nchini Angola kulikochochewa pia na kuongezeka kwa bei ya bidhaa hiyo muhimu. Pato la Afrika Kusini lilikua kwa asilimia 3.7 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 2.8 mwaka 2003. Aidha, pato la nchi za Kaskazini mwa Afrika, lilikua kwa asilimia 4.9 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 6.1 mwaka 2003. Kupungua kwa ukuaji kulisababishwa na ukame ulioathiri shughuli za kilimo hasa katika nchi ya Morocco.

31. Pamoja na machafuko ya kisiasa nchini Sudan, pato la nchi za Pembe ya Afrika lilikua kwa asilimia 9.1 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 1.9 mwaka 2003. Ukuaji huo mkubwa ulichangiwa kwa kiasi kikubwa na kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo kutokana na hali nzuri ya hewa hasa nchini Ethiopia na pia nchi za eneo hilo kuendelea kunufaika na misamaha ya madeni chini ya Mpango wa Kuzipunguzia Madeni Nchi Maskini. Ethiopia ilichangia sehemu kubwa ya ukuaji huo kwa pato lake kuongezeka kwa asilimia 11.6 mwaka 2004, baada ya kupungua kwa asilimia 3.9 mwaka 2003.

32. Kwa nchi za Maziwa Makuu ikiwemo Tanzania, pato lilikua kwa asilimia 5.4 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 4.1 mwaka 2003. Ukuaji huo ulisababishwa hasa na kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ya kilimo. Kwa upande wa nchi za Afrika ya Kati na Magharibi, pato lilikua kwa asilimia 5.6 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 7.2 mwaka 2003. Ukuaji uliathirika kutokana hasa na migogoro ya kisiasa na vita ya ndani hususan nchini Ivory Coast.

Jedwali Na. 2.2:  Mwenendo wa Baadhi ya Viashirio vya Uchumi kwa Baadhi ya Nchi za Afrika:   2001-2004       

 

Nchi

Pato (Badiliko %)

Bei kwa Mlaji [1]

(Badiliko %)

 Urari wa Malipo ya Kawaida [2] (Badiliko %)

2001

2002

2003

2004

2001

2002

2003

2004

2001

2002

2003

2004

Afrika

3.6

3.5

4.6

5.1

13.0

9.7

10.6

7.7

-0.1

–1.5

-0.3

0.2

Afrika Kaskazini

   Algeria

   Morocco

   Tunisia

4.1

2.1

6.5

5.2

3.3

4.0

3.2

1.7

6.1

6.9

5.2

5.6

4.9

5.3

3.5

5.8

2.6

4.2

0.6

1.9

2.1

1.4

2.8

2.8

2.2

2.6

1.2

2.8

3.1

3.6

2.0

3.6

7.2

12.9

4.8

-4.3

4.5

7.8

4.1

–3.5

7.2

13.3

3.6

-2.9

6.8

13.3

1.2

-2.1

Kusini mwa Jangwa la Sahara

Pembe ya Afrika [3]

   Ethiopia

   Sudan

 

3.8

6.1

7.7

5.3

 

3.6

4.1

1.6

6.0

 

4.2

1.9

-3.9

6.0

 

5.1

9.1

11.6

7.3

 

21.6

1.8

-7.1

4.9

 

12.1

1.3

7.2

8.3

 

13.3

10.6

15.1

7.7

 

9.1

8.6

9.0

8.4

 

-3.9

-7.4

-4.2

-0.3

 

–3.5

–8.4

–5.7

–9.6

 

-2.7

-6.7

-2.7

-8.2

 

-1.9

-6.7

-6.1

-6.8

Maziwa Makuu [4]

   DRC

   Kenya

   Tanzania

   Uganda

2.3

-2.1

1.2

5.6

5.5

4.8

3.5

1.0

7.2

6.8

4.1

5.7

1.6

7.1

4.7

5.4

6.8

3.1

6.3

5.9

54.6

356.7

5.8

5.2

4.5

8.3

25.3

2.0

4.6

5.7

8.2

12.8

9.8

4.5

5.1

6.9

3.9

11.5

4.6

5.9

-3.9

-4.7

-3.5

-1.5

-6.8

–3.0

–2.8

–3.8

–6.0

-2.4

-1.5

-0.2

-2.4

-6.2

-4.0

-2.5

-3.7

-5.8

-1.9

Kusini mwa Afrika [5]

   Angola

   Zimbabwe

   Msumbiji

 

2.9

3.2

-8.8

13.0

 

2.3

14.4

11.1

7.4

 

2.5

3.4

-10.0

7.1

 

4.9

11.2

-4.8

7.8

 

35.2

152.6

76.7

9.0

 

44.2

108.9

140.0

16.8

 

59.9

98.3

431.7

13.4

 

40.3

43.6

282.4

12.6

 

-4.8

-2.0

-9.7

-21.4

 

–2.9

–1.4

–2.6

-22.3

 

-4.0

-5.2

-5.0

-16.8

 

-0.1

6.5

-5.3

-12.4

Afrika ya Kati na    Magharibi [6]

    Ghana

    Nigeria

 

4.0

4.2

2.8

 

3.6

4.5

1.5

 

7.2

5.2

10.7

 

5.6

5.5

3.5

 

12.0

32.9

18.9

 

8.4

14.8

13.7

 

9.4

26.7

14.0

 

8.2

12.6

15.0

 

-2.7

-6.6

2.7

 

–6.9

0.5

11.1

 

-3.6

1.7

-3.7

 

-0.4

1.2

2.8

   CFA Franc zone [7]

     Cameroon

     Côte d’Ivoire

4.9

5.3

0.1

4.4

6.5

-1.6

5.4

4.5

-1.6

7.6

4.3

-0.9

4.2

2.8

4.4

4.0

6.3

3.1

1.3

0.6

3.3

0.7

0.3

1.5

-6.7

-1.7

-2.0

–4.3

–7.0

6.1

-4.0

-2.4

3.9

-2.6

-1.7

3.1

Afrika Kusini

2.8

3.6

2.8

3.7

5.7

9.2

5.8

1.4

-0.1

0.6

-0.9

-2.5

Nchi Zinazonunua Mafuta

3.8

3.2

3.5

4.7

11.9

8.9

10.1

6.8

-2.4

–1.8

-1.8

-2.7

Nchi Zinazotoa Mafuta

3.0

4.5

8.3

6.2

16.8

12.3

12.4

10.6

6.2

–0.7

3.9

7.7

 


Chanzo: Shirika la Fedha la Kimataifa (IMF), Aprili 2005.


[1] Kwa kutumia wastani wa mwaka.    

[2] Asilimia ya Pato la Taifa

[3] Inajumuisha Djibouti

[4] Inajumuisha Burundi na Rwanda

[5] Inajumuisha Botswana, Comoros, Lesotho, Madagascar, Malawi, Mauritius, Msumbiji,   Namibia, Shelisheli,  Swaziland, na Zambia.

[6] Inajumuisha Cape Verde, Gambia, Guinea, Mauritania, Sao Tome na Principe, Sierra Leone, na ukanda wa CFA.

[7] Inajumuisha Benin, Burkina Faso, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Chad, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Equatorial

   Guinea, Gabon, Guinea Bisau, Mali, Niger, Senegal na Togo.

   
 
USHIRIKIANO WA KIUCHUMI KIMATAIFA  
   
Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

33. Kulingana na mkataba wa kuanzisha Jumuiya, shughuli zilizoendelea kutekelezwa zilihusu sekta za fedha, biashara, uwekezaji rasilimali, vitega uchumi, miundombinu, nishati pamoja na kuendeleza bonde la Ziwa Viktoria. Katika azma ya kufikia malengo ya ushirikiano, tarehe 2 Machi 2004, Wakuu wa Nchi za Tanzania, Kenya na Uganda, walitia saini Itifaki ya Ushuru wa Pamoja kuhusu utaratibu wa kuondoa ushuru wa bidhaa zinazotoka nchi moja kwenda nchi nyingine, utaratibu wa kuthibitisha uasili wa bidhaa, na wigo wa pamoja wa ushuru wa forodha kwa bidhaa zinazoingia katika Jumuiya. Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania liliridhia Itifaki ya Ushuru wa Pamoja wa Afrika Mashariki Oktoba 2004.

34. Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Viwanda Afrika Mashariki ulipitishwa na Baraza la Mawaziri wa Jumuiya mwezi Januari 2004. Pia, nchi wanachama ziliridhia mikataba inayohusu usafiri kwenye maziwa; matumizi bora ya Bonde la Ziwa Victoria; kutafuta na kuokoa watu wanaopata ajali majini pamoja, na itifaki inayohusu usafiri wa barabara.

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

35. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za SADC uliofanyika Agosti 2004 nchini Mauritius ulizindua Mkakati wa kupunguza na kumaliza matatizo yanayohusiana na Siasa, Ulinzi na Usalama ikiwa Mkakati mmojawapo wa Utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Ushirikiano kwa kipindi cha miaka kumi na mitano ijayo uliozinduliwa rasmi Machi 2004. Vile vile, Mkutano huo uliunga mkono uzinduzi wa majadiliano kati ya Umoja wa Ulaya na SADC kuhusu makubaliano ya kibiashara. Maeneo yaliyopewa kipaumbele katika majadiliano hayo ni upatikanaji wa masoko na utaratibu wa kuthibitisha uasili wa bidhaa, biashara ya huduma, mahitaji ya kisheria, na mifumo. Nchi zinazoshiriki katika majadiliano haya chini ya SADC ni Tanzania, Angola, Botswana, Lesotho, Msumbiji, Namibia na Swaziland.

36. Wakuu wa Nchi na Serikali za SADC walikutana mwezi Mei, 2004 Dar es Salaam, Tanzania katika mkutano maalum juu ya Kilimo na Usalama wa Chakula ili kutafuta ufumbuzi wa tatizo la muda mrefu la ukosefu wa chakula katika Jumuiya kwa kuweka mikakati endelevu ya kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo. Mkutano huo uliidhinisha mpango wa muda mfupi na muda mrefu wa kufufua sekta ya kilimo, na utekelezaji wa mikakati iliyoainishwa ili kuhakikisha inatekelezwa, hususan suala la kuanzisha mfuko maalum wa kikanda kuhusu hifadhi ya chakula kwa kila nchi mwanachama kuzingatia kutenga akiba ya kukidhi mahitaji ya dharura ya chakula kwa kipindi kisichopungua miezi mitatu, na muda wote kuwa na taarifa za hali ya usalama na upatikanaji wa chakula. Pamoja na maendeleo yaliyopatikana, bado ukosefu wa chakula cha kutosha na tatizo la ugonjwa wa UKIMWI viliendelea kuwa changamoto kubwa zinazokabili nchi za Jumuiya.

Mpango Mpya wa Ushirikiano wa Kuleta Maendeleo Afrika - NEPAD

37. Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Umoja wa Nchi za Afrika ulifanyika Addis Ababa, Ethiopia mwezi Julai 2004, na waliazimia kutoa kipaumbele katika utekelezaji wa programu za maendeleo ili kuleta mabadiliko na kuongeza uwekezaji katika sekta muhimu za kilimo, miundombinu, afya, maendeleo ya nguvu kazi, na elimu. Pia, waliazimia kuchukua hatua za kuainisha sera za kitaifa za maendeleo na nyinginezo zenye mwelekeo huo.

38. Mwaka 2004, maandalizi ya utekelezaji wa Mkakati Mpana wa Kuendeleza Kilimo Afrika yalianza. Mkazo ulielekezwa katika programu ya kuongeza uzalishaji katika sekta ya kilimo kwa kuhusisha nchi mbalimbali. Benki ya Dunia ilitoa dola 500 milioni katika kuanzisha Programu ya Mkakati huo. Aidha, Mpango wa Utekelezaji wa Muda Mfupi kuhusu miundombinu, Benki ya Maendeleo ya Afrika ilikubali kufadhili miradi ya uwekezaji inayogharimu dola 580 milioni. Benki ya Dunia iliidhinisha miradi ya Mpango wa Utekelezaji wa Muda Mfupi inayogharimu dola 570 milioni. Miradi ya kipaumbele kuendelezwa kikanda inahusu sekta za nishati, uchukuzi, mawasiliano pamoja na kujenga uwezo.

39. Mwaka 2004, Tanzania iliandaa orodha ya miradi inayohusisha sekta mbalimbali na kuiwasilisha katika sekretarieti ya NEPAD. Vile vile, Tanzania ilitia saini mkataba wa kujiunga na utaratibu unaotoa fursa kwa nchi kujitathmini na kujipima zenyewe (African Peer Review Mechanism - APRM) kuhusiana na utekelezaji wa vigezo muhimu vya NEPAD kwenye Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Afrika Julai 2004. Nchi kumi na nne (14) zilijiunga na utaratibu wa APRM kwa mwaka 2004 na kufanya nchi zilizojiunga kufikia 23.

Ushirikiano wa Kiufundi Baina ya Nchi Zinazoendelea (TCDC)

40. Mawaziri wa nchi wanachama wa Kundi la Nchi 77 pamoja na China walikutana Sao Paulo, Brazil mwezi Juni 2004, kwa ajili ya maadhimisho ya kumbukumbu ya miaka 40 ya uanzishwaji wa Umoja wa Nchi Zinazoendelea na Azimio la 28 la Mkutano wa Mawaziri wa Kundi la Nchi 77. Katika maadhimisho hayo mawaziri walisisitiza umuhimu wa kuimarisha ushirikiano baina ya Kundi la Nchi 77 ili kuleta faida kwa pande zote.

41. Katika mwaka 2004, Tanzania iliendelea kufaidika na misaada ya Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa –UNDP na serikali ya China. Wataalam wa kitanzania wapatao 20 kutoka wizara na taasisi mbalimbali za kiserikali walihudhuria mafunzo nchini China kwenye maeneo ya teknolojia ya mianzi, uzalishaji na usambazaji wa mboga, teknolojia ya tarakishi, uchimbaji wa maji, uzalishaji wa maua, uzuiaji wa jangwa, tahadhari na kinga juu ya matetemeko ya ardhi, utabiri wa hali ya hewa, matibabu ya magonjwa ya kisukari kwa kutumia dawa za kiasili za China, uendelezaji nishati ya maji, utunzaji na usalama kwa mabwawa, pamoja na utafiti wa madini. Mafunzo haya yalikuwa na manufaa kwa kujenga uwezo wa wataalam na kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi na kiufundi baina ya serikali ya Tanzania, UNDP, China, na nchi nyingine.

Mkutano wa Kimataifa Kuhusu Eneo la Maziwa Makuu

42. Mkutano wa Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu uliofanyika Dar es Salaam Novemba 2004, ulihitimisha awamu ya kwanza kwa Wakuu wa Nchi waanzilishi kumi na moja kutia saini Azimio lenye kutoa mwongozo juu ya taratibu na sera za kudumisha amani, usalama, demokrasia na maendeleo katika eneo la Maziwa Makuu. Azimio hilo linalenga kuwezesha nchi kuheshimu uhuru na mipaka ya nchi nyingine, haki za kila taifa pamoja na kutoingilia mambo ya ndani ya taifa lingine. Azimio hilo pia linalenga kuendeleza juhudi za amani, kuwawezesha viongozi kupiga vita mauaji ya kimbari, kudumisha hali ya amani na usalama, kunyang’anya silaha vikundi vya waasi hasa katika Jamhuri ya Demokrasia ya Kongo na Burundi, kuwakamata na kuwapeleka kwenye mamlaka husika wanaochochea mauaji, pamoja na wahusika wa mauaji ya Rwanda ya mwaka 1994 ili kuondokana na vitendo au mitazamo inayoweza kuathiri usalama na amani. Wakuu wa Nchi za Maziwa Makuu waliunda kamati ya mawaziri ya kuandaa rasimu ya Itifaki yenye mpango na programu za muda mfupi, kati na mrefu inayotekelezeka, kutathminika na kupimika. Kamati hii ilianza kufanya kazi kwa kushirikiana na kamati ya Kanda ya Maandalizi yenye wawakilishi wa makundi ya kijamii wakiwemo wanawake, vijana na wataalam. Theluthi moja ya wawakilishi wake walitakiwa kuwa wanawake.

Mpango wa Marekani wa Kusaidia Maendeleo ya Nchi za Afrika – AGOA

43. Tanzania bado haijaweza kunufaika vizuri kutokana na fursa hii kwani mauzo ya bidhaa kwenda Marekani yameongezeka kidogo toka dola 11.3 milioni mwaka 2003 hadi dola 13.7 milioni mwaka 2004. Bidhaa zilizouzwa ni nguo, madini, bidhaa za misitu, kilimo na bidhaa za kusindikwa. Uagizaji wa bidhaa kutoka Marekani uliongezeka kutoka dola 69.7 milioni mwaka 2003 hadi dola 78.1 milioni mwaka 2004.

Shirika la Kimataifa la Biashara – WTO

44. Katika mwaka 2004, hatua mbalimbali za mashauriano zilichukuliwa ili kuondoa mambo yaliyokwamisha mafanikio ya Mkutano wa Tano wa Mawaziri wa nchi wanachama wa WTO uliofanyika Cancun, Mexico, Septemba 10-14 mwaka 2003. Maeneo muhimu ya majadiliano yalihusu: masuala ya kilimo, ambayo lengo la majadiliano yake ni uondoaji wa ruzuku ili kuinua kilimo na kupanua masoko kwa bidhaa za kilimo kutoka nchi maskini; upunguzaji wa ushuru kwa bidhaa zisizo za kilimo ili kulinda viwanda, ajira, maduhuli ya serikali; kuondoa ushuru na vikwazo visivyo vya kiushuru kwa bidhaa za nchi zinazoendelea ziingizwapo katika masoko ya nchi zilizoendelea; kufungua masoko kwa biashara ya huduma na kuhakikisha kuwa nchi zinazoendelea zinanufaika na biashara ya huduma ikiwa ni pamoja na upatikanaji wa teknolojia; na kutoa upendeleo maalum kwa nchi changa na zile zinazoendelea ili kuziwezesha kushiriki katika ushindani wa soko la dunia.