MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Hali
ya Uchumi wa Taifa |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
HALI
YA UCHUMI WA TAIFA |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
|
Ukuaji wa Uchumi
1. Katika mwaka 2004, Pato la Taifa halisi lilikua kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 mwaka 2003. Ukuaji ulichangiwa hasa na sekta za kilimo; biashara ya uuzaji jumla na rejareja, na mahoteli (ikijumuisha utalii); na mawasiliano na uchukuzi. Viwango vya ukuaji katika sekta za bidhaa za viwandani na ujenzi vilikuwa kama vile vya mwaka 2003. Aidha, viwango vya ukuaji wa sekta za fedha na huduma za bima; na uendeshaji wa serikali na huduma nyingine, viliongezeka kidogo. Viwango vya ukuaji wa sekta za madini na uchimbaji mawe; na maji na umeme, vilishuka. 2. Pato la Taifa lilikuwa shilingi 11,287,318 milioni mwaka 2004 au shilingi 2,094,516 milioni kwa bei za mwaka 1992. Idadi ya watu Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa 35.3 milioni mwaka 2004, hivyo, pato la wastani la kila mtu lilikuwa shilingi 319,754 kwa bei za mwaka 2004 au shilingi 59,335 kwa bei za mwaka 1992. Ongezeko halisi la pato la wastani kwa kila mtu (kwa bei za mwaka 1992) ni sawa na asilimia 3.4 ikilinganishwa na asilimia 3.8 mwaka 2003. 3. Sekta ya kilimo ilikua kwa asilimia 6.0 katika mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 4.0 mwaka 2003. Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji katika sekta ndogo ya mazao, kwa asilimia 6.2 na sekta ndogo ya uvuvi, kwa asilimia 6.9 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 3.6 na asilimia 6.4 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. Kiwango cha ukuaji wa sekta ya misitu na uwindaji kilishuka kutoka asilimia 4.2 mwaka 2003 hadi asilimia 4.0 mwaka 2004. Kiwango cha ukuaji katika sekta ndogo ya mifugo kilibakia kama cha mwaka 2003, cha asilimia 5.0. Pamoja na kuongezeka kwa ukuaji wa sekta ya kilimo, mchango wake katika Pato la Taifa ulishuka kutoka asilimia 46.7 mwaka 2003 hadi asilimia 46.4 mwaka 2004. 4. Ukuaji wa sekta ya madini na uchimbaji wa mawe ulishuka kutoka asilimia 18.0 mwaka 2003 hadi asilimia 15.6 mwaka 2004. Kushuka kwa ukuaji wa sekta kulitokana na kukamilika kwa uwekezaji katika baadhi ya migodi mikubwa. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 3.0 mwaka 2003 hadi asilimia 3.2 mwaka 2004. 5. Ukuaji wa sekta ya bidhaa za viwandani katika mwaka 2004 ulibakia kwenye kiwango cha mwaka 2003 cha asilimia 8.6 kutokana na kuongezeka kwa uzalishaji katika baadhi ya viwanda kama saruji, chuma, vinywaji na vyakula (kama biskuti na unga wa ngano). Mchango wa sekta ya bidhaa za viwandani katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 8.6 mwaka 2003 hadi asilimia 8.8 mwaka 2004. 6. Ukuaji wa sekta ya umeme na maji ulishuka kutoka asilimia 4.9 mwaka 2003 hadi asilimia 4.7 mwaka 2004. Kiwango cha ukuaji cha sekta ndogo ya umeme kilishuka kutoka asilimia 5.0 mwaka 2003 hadi asilimia 4.9 mwaka 2004. Kiwango cha ukuaji wa sekta ndogo ya maji pia kilishuka hadi asilimia 3.0 mwaka 2004 kutoka asilimia 4.3 mwaka 2003. Kushuka kwa ukuaji katika sekta hii kulitokana na upungufu wa mvua katika baadhi ya maeneo nchini. Sekta hii imeendelea kuchangia asilimia 1.6 katika Pato la Taifa kwa miaka miwili mfululizo. 7. Mwaka 2004, ukuaji wa sekta ya ujenzi ulibakia kwenye kiwango cha asilimia 11.0 cha mwaka 2003. Sekta ya ujenzi ilichangia asilimia 5.5 katika Pato la Taifa mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 5.2 mwaka 2003. Ukuaji huo ulichangiwa na kuongezeka kwa ujenzi wa majengo ya kuishi na uendelezaji ardhi. 8. Sekta ya biashara, inayojumuisha uuzaji wa jumla na reja reja, mahoteli na utalii ilikua kutoka asilimia 6.5 mwaka 2003 hadi asilimia 8.0 mwaka 2004. Ukuaji wa sekta hii ulitokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii nchini. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa uliongezeka kutoka asilimia 16.8 mwaka 2003 hadi asilimia 17.0 mwaka 2004. 9. Mwaka 2004, sekta ya mawasiliano na uchukuzi ilikua kwa asilimia 6.2, ikilinganishwa na asilimia 5.0 mwaka 2003. Ukuaji huu ulichangiwa na ongezeko la uwekezaji katika mawasiliano ya simu za mikononi; ujenzi na ukarabati wa viwanja vya ndege na barabara; na kuongezeka kwa wakala wa usafirishaji. Mchango wa sekta ya mawasiliano na uchukuzi katika Pato la Taifa ulibakia katika kiwango cha mwaka 2003, cha asilimia 5.4. 10. Sekta ya fedha na bima, mali na huduma za kibiashara, ilikua kwa asilimia 4.5 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 4.4 mwaka 2003. Ongezeko katika ukuaji lilitokana na kukua kwa kiasi kikubwa kwa sekta ndogo ya fedha na bima, na huduma za kibiashara kutoka asilimia 3.2 na 5.5 mwaka 2003 hadi asilimia 4.5 na 5.7 mwaka 2004, kwa mtiririko huo. Ukuaji wa sekta ndogo ya upangishaji majengo ulishuka kutoka asilimia 5.1 mwaka 2003 hadi asilimia 4.5 mwaka 2004. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa ulipungua kutoka asilimia 9.9 mwaka 2003 hadi asilimia 9.7 mwaka 2004. 11. Ukuaji wa sekta ya uendeshaji serikali na huduma nyingine uliongezeka kutoka asilimia 4.1 mwaka 2003 hadi asilimia 4.5 mwaka 2004. Ongezeko la ukuaji wa sekta hii lilitokana na kukua kwa sekta ndogo ya uendeshaji wa serikali kutoka asilimia 2.5 ya mwaka 2003 hadi asilimia 3.0 mwaka 2004. Ukuaji wa sekta ndogo za elimu na afya ulipungua kutoka asilimia 7.0 na 6.5 mwaka 2003 hadi asilimia 6.8 na 6.2 mwaka 2004, kwa mtiririko huo. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa ulishuka kidogo kutoka asilimia 7.2 mwaka 2003 hadi asilimia 7.1 mwaka 2004. Majedwali Na.1 - 4D yanaonyesha mchanganuo wa mwenendo wa ukuaji wa Pato la Taifa mwaka 1993 – 2004. Mwenendo wa Bei 12. Uchambuzi wa mwenendo wa bei kwa mwaka 2004 ulizingatia matokeo ya mapitio ya kapu la bidhaa na huduma, na uzito katika Fahirisi ya Bei za Walaji Kitaifa kutokana na Tafiti ya Mapato na Matumizi ya Kaya ya Mwaka 2000/2001. Kuanzia Septemba, 2004, takwimu za Fahirisi ya Bei za Walaji Kitaifa zilianza kutolewa kwa kutumia kapu na uzito mpya. Jedwali Na.1.1 linaonyesha uzito wa zamani wa mwaka 1994 na mpya wa mwaka 2001. Jedwali Na. 1.1: Uzito wa Fahirisi ya zamani na mpya
13. Kasi ya upandaji bei ilikuwa inashuka mfululizo tangu mwaka 1994 hadi mwaka 2003, kutoka asilimia 35.5 hadi asilimia 4.4 mwaka 2003, kwa bei za mwaka 1994. Hata hivyo, mwenendo huo ulibadilika mwaka 2004 na kupanda kwa asilimia 5.9. Kwa upande mwingine, katika mwaka 2004, kasi ya upandaji bei iliongezeka kwa asilimia 4.2 ikilinganishwa na asilimia 3.5 mwaka 2003, kwa bei za mwaka 2001. Kuongezeka kwa kasi ya upandaji bei mwaka 2004 kulitokana na kupanda kwa wastani wa bei ya chakula kufuatia upungufu wa chakula uliojitokeza mwishoni mwa mwaka 2003 na mwanzoni mwa mwaka 2004. Aidha, kupanda kwa bei ya bidhaa za mafuta ya petroli kulisababisha kuongezeka kwa gharama za usafirishaji na hivyo kusababisha kuongezeka kwa wastani wa bei za bidhaa na huduma nyingine. 14. Katika mwaka 2004, fahirisi ya bei katika makundi ya bidhaa na huduma ya chakula, na nguo na viatu ilipanda, na kwa kuzingatia uzito wa makundi hayo katika kapu la walaji (asilimia 62.3), makundi hayo mawili yalichangia kwa kiasi kikubwa kupanda kwa wastani wa kitaifa wa kasi ya upandaji bei. Fahirisi ya bei ya makundi hayo ilipanda kwa asilimia 5.9, na 5.1 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 4.5, na 2.0 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. Fahirisi ya bei ya usafiri ambao pia una uzito mkubwa katika kapu la walaji ilipanda kwa kiwango kidogo cha asilimia 1.0 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 1.2 mwaka 2003. Fahirisi ya bei ya kodi ya nyumba ilipanda kwa asilimia 2.2 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 2.0 mwaka 2003. Pamoja na kupungua kwa uzito katika kapu la walaji, fahirisi ya bei ya huduma za afya ilipanda kwa kiwango kidogo cha asilimia 0.5 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 2.9 mwaka 2003. Vinywaji na sigara ni kundi pekee ambalo wastani wa kiwango cha ongezeko la bei ulipungua kwa asilimia 0.5 mwaka 2004 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 1.5 mwaka 2003. Wastani wa viwango vya ongezeko la bei katika makundi mengine ya bidhaa na huduma ulipanda kwa viwango vya chini mwaka 2004 ikilinganishwa na ilivyokuwa mwaka 2003. Wastani huo ni kama ifuatavyo: (viwango vya 2003 katika mabano): umeme, mafuta ya taa na maji, asilimia 2.3 (asilimia 5.9); fenicha na vyombo vya nyumbani asilimia 0.2 (2.1); huduma na mahitaji ya nyumbani asilimia 0.9 (1.1); na elimu asilimia 0.6 (2.2). 15. Uchambuzi wa fahirisi ya bei za bidhaa na huduma kwa tabaka mbali mbali za wananchi kimapato unaonyesha kuwa kundi la watu wa kipato cha chini liliathirika zaidi na ongezeko la kasi ya upandaji bei. Fahirisi kwa kundi hili ilipanda kwa kiwango cha asilimia 8.2 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 4.9 mwaka 2003. Aidha, katika kundi hili, viwango vya ongezeko la bei kwa bidhaa na huduma nyingi (ikiwemo chakula na huduma na mahitaji ya nyumbani) viliongezeka mwaka 2004 ikilinganishwa na mwaka 2003. Bidhaa hizo hutumiwa kwa wingi na watu wa tabaka hili. Fahirisi ya bei ya chakula na huduma na mahitaji ya nyumbani ilipanda kwa asilimia 8.2 na 19.9 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 3.3 na 6.4 mwaka 2003, kwa mtiririko huo katika kundi hili la kima cha chini. Katika makundi ya watu wa kima cha kati na juu, fahirisi ya bei iliongezeka kwa asilimia 8.2 na 7.1 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 7.1 na 6.8 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. 16. Hali ya mwenendo wa bei za bidhaa na huduma kwa wakazi wa jiji la Dar es Salaam ilikuwa na taswira mchanganyiko. Hata hivyo, wastani wa jumla wa fahirisi ya bei kwa makundi ya kima cha chini, kati na juu uliongezeka kwa asilimia 8.2, 8.2 na 7.1 mwaka 2004, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 3.4, 7.2 na 6.8 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. Wakazi wa Dar es Salaam wa kipato cha juu na kati waliathirika sana na kupanda kwa gharama za usafiri kufuatia kupanda kwa wastani wa bei za bidhaa za petroli ambazo zinatumiwa kwa wingi na makundi haya. Fahirisi ya bei ya usafiri katika makundi hayo ilipanda kwa asilimia 25.5 na asilimia 6.2 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 4.8 na asilimia 3.7 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. Kwa upande wa wakazi wa Dar es Salaam wa kipato cha chini, fahirisi ya bei ya usafiri ilishuka kwa asilimia 0.7 mwaka 2004 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 0.6 mwaka 2003. Hata hivyo, matokeo ya kupanda kwa wastani wa bei za bidhaa za petroli yalijitokeza zaidi katika kupanda kwa wastani wa bei ya chakula kwa wakazi wa Dar es Salaam wa tabaka zote. Wastani wa bei ya chakula kwa makundi ya kima cha juu, kati na chini kwa wakazi wa Dar es Salaam ulipanda kwa asilimia 13.6, 10.8 na 8.2 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 4.7, 6.6 na 3.3 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. Majedwali Na. 8 – 16 yanaonyesha mwenendo wa fahirisi ya bei kwa makundi na sehemu mbalimbali, mwaka 1977 – 2004. Ukuzaji Rasilimali 17. Ukuzaji rasilimali uliongezeka kutoka sh. 571,275 milioni mwaka 2003 hadi sh. 670,264 milioni mwaka 2004, kwa bei za mwaka 1992, sawa na ongezeko la asilimia 17.3. Ukuzaji rasilimali kwa bei za miaka husika uliongezeka kwa asilimia 14.8 mwaka 2004 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 25.0 mwaka 2003. Mwaka 2004, uwiano wa ukuzaji rasilimali na Pato la Taifa ulikuwa asilimia 32.0 kwa bei za mwaka 1992, ikilinganishwa na asilimia 27.8 mwaka 2003. 18. Ukuzaji rasilimali katika shughuli za ujenzi wa majengo uliongezeka kutoka sh. 181,775 milioni mwaka 2003 hadi sh. 216,659 milioni mwaka 2004. Kiwango cha ukuaji katika shughuli za ujenzi wa majengo kilishuka kutoka asilimia 32.1 mwaka 2003 hadi asilimia 19.2 mwaka 2004. Kushuka huku kulitokana na kupungua kwa kiwango cha ukuaji wa ujenzi wa majengo yasiyo ya kuishi kutoka asilimia 75 mwaka 2003 hadi asilimia 17.1 mwaka 2004. Shughuli nyingine za ukuzaji rasilimali katika ujenzi wa majengo ya kuishi na ujenzi vijijini ziliongezeka kutoka asilimia 3.5 na 7.0 mwaka 2003 hadi asilimia 30.0 na 16.7 mwaka 2004, kwa mtiririko huo. 19. Shughuli nyingine za ujenzi (uendelezaji ardhi, barabara na madaraja, na usambazaji wa maji) ziliongezeka kutoka sh. 96,673 milioni mwaka 2003 hadi sh.120,190 milioni mwaka 2004, kwa bei za mwaka 1992, sawa na ongezeko la asilimia 24.3 mwaka 2004 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 11.8 mwaka 2003. Kupanda kwa ongezeko katika shughuli za ujenzi kulitokana na kuongezeka kwa ukuaji katika shughuli za uendelezaji ardhi kutoka asilimia 62.3 mwaka 2003 hadi asilimia 161.2 mwaka 2004. Shughuli nyingine za barabara na madaraja, na usambazaji wa maji zilikua kwa asilimia 15.3 na 20.3 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 30.6 na 17.7 mwaka 2003, kwa mtiririko huo. 20. Uagizaji vifaa nchini uliongezeka kutoka sh. 287,586 milioni mwaka 2003 hadi sh. 326,555 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 13.6, kwa bei za mwaka 1992. Thamani ya ununuzi wa vifaa vya usafiri ilipungua kwa kiwango cha asilimia 17.4 ikilinganishwa na asilimia 29.6 mwaka 2003. Ununuzi wa mitambo na vifaa vinginevyo uliongezeka kwa asilimia 38.6 mwaka 2004 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 26.0 mwaka 2003. 21. Uwekezaji katika rasilimali za kudumu ambayo inajumuisha rasilimali za majengo, shughuli nyingine za ujenzi na vifaa uliongezeka kutoka sh. 566,035 milioni mwaka 2003 hadi sh. milioni 663,404 mwaka 2004, kwa bei za mwaka 1992, sawa na ongezeko la asilimia 17.2. Ongezeko hilo lilichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa vifaa nchini kwa asilimia 49.1. Aidha, shughuli nyingine za rasilimali za majengo na ujenzi ziliongezeka kwa asilimia 32.7 na asilimia 18.1, kwa mtiririko huo. 22. Limbikizo la rasilimali kwa bei za mwaka 1992 liliongezeka kwa asilimia 30.9 mwaka 2004, ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 10.6 mwaka 2003. Thamani ya limbikizo ilikuwa sh. 6,860 milioni mwaka 2004 ikilinganishwa na sh. 5,240 milioni mwaka 2003. Limbikizo la rasilimali kwa bei za miaka husika liliongezeka kutoka sh.19,738 milioni mwaka 2003 hadi sh. 22,798 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 15.5 ikilinganishwa na ongezeko la asilimia 10.6 mwaka 2003. 23. Ukuzaji rasilimali katika sekta ya umma uliongezeka kutoka sh. 896,162 milioni mwaka 2003 hadi sh. 950,077 milioni mwaka 2004 kwa bei za miaka husika, sawa na ongezeko la asilimia 6.0 . Mchango wa sekta ya umma katika ukuzaji rasilimali kwa mwaka 2004 ulikuwa asilimia 36.6 ikilinganishwa na asilimia 39.7 mwaka 2003. Ukuzaji rasilimali katika sekta binafsi uliongezeka kutoka sh.1,343,118 milioni mwaka 2003 hadi sh.1,620,627 milioni mwaka 2004 kwa bei za miaka husika, sawa na ongezeko la asilimia 20.7. Mchango wa sekta binafsi katika ukuzaji rasilimali ulikuwa asilimia 62.5 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 59.5 mwaka 2003. Majedwali Na. 5 – 7 yanaonyesha mwenendo wa ukuzaji wa rasilimali kwa aina ya shughuli, na katika sehemu za uchumi wa kitaifa na binafsi. Jedwali Na. 1 (PATO LA TAIFA (GDP) KISEKTA KWA GHARAMA ZAKE) Jedwali Na. 1A( PATO LA TAIFA (GDP) KISEKTA, KWA GHARAMA ZAKE - SEHEMU INAYOUZIKA NA ISIYOUZIKA( Kwa bei za miala inayohusika)) Jedwali Na. 2(MCHANGO WA SEKTA KWA PATO LA TAIFA (% of GDP) KWA GHARAMA ZAKE) Jedwali Na. 2A(MCHANGO WA SEKTA KWA PATO LA TAIFA (% of GDP) KWA GHARAMA ZAKE - SEHEMU INAYOUZIKA NA ISIYOUZIKA( Kwa bei za miaka inayohusika)) Jedwali Na. 2B(PATO LA TAIFA NA MATUMIZI YAKE KWA BEI ZA SOKO) Jedwali Na. 3(PATO LA TAIFA (GDP) KISEKTA KWA GHARAMA ZAKE ) Jedwali Na. 3A(PATO LA TAIFA (GDP) KISEKTA KWA GHARAMA ZAKE - SEHEMU INAYOUZIKA NA ISIYOUZIKA) Jedwali Na. 4(UKUAJI WA PATO LA TAIFA (PTL) KISEKTA, KWA GHARAMA ZAKE ) Jedwali Na. 4A(UKUAJI HALISI WA PATO LA TAIFA (REAL GDP GROWTH) KI SEKTA KWA GHARAMA ZAKE - SEHEMU INAYOUZIKA NA ISIYOUZIKA) Jedwali Na. 4B(MCHANGO WA SEKTA KWA PATO LA TAIFA (PTL), Kwa gharama zake ( Bei za mwaka 1992)) Jedwali Na. 4C(MCHANGO WA SEKTA KWA PATO LA TAIFA (% of GDP) KWA GHARAMA ZAKE - SEHEMU INAYOUZIKA NA ISIYOUZIKA) Jedwali Na. 5(UKUZAJI RASILIMALI KWA AINA YA SHUGHULI) Jedwali Na. 6(UKUZAJI RASILIMALI KWA AINA YA SHUGHULI) Jedwali Na. 7(UKUZAJI WA RASILIMALI KATIKA SEHEMU ZA UCHUMI WA KITAIFA NA BINAFSI) Jedwali Na. 8( FAHIRISI YA BEI ZA REJAREJA YA BIDHAA ZITUMIWAZO NA WATU WA KIPATO CHA CHINI DAR-ES-SALAAM (2001=100)) Jedwali Na. 9(FAHIRISI YA BEI ZA REJAREJA YA BIDHAA ZITUMIKAZO NA WATU WA KIPATO CHA CHINI DAR ES SALAAM (2001 =100)) Jedwali Na. 10( FAHIRISI YA BEI YA BIDHAA NA HUDUMA ZITUMIWAZO NA WAFANYAKAZI WA KIMA CHA KATI - DAR-ES-SALAAM (2001 =100)) Jedwali Na. 11( FAHIRISI YA BIDHAA NA HUDUMA ZITUMIWAZO NA WAFANYAKAZI WA KIMA CHA KATI DAR-ES-SALAAM (2001 =100)) Jedwali Na. 12(FAHIRISI YA GHARAMA YA MAISHA YA WENYE KIPATO CHA JUU DAR-ES-SALAAM (2001 =100)) Jedwali Na. 13(FAHIRISI YA GHARAMA YA MAISHA YA WENYE KIPATO CHA JUU DAR-ES-SALAAM (2001=100)) Jedwali Na. 14( FAHIRISI YA BEI YA BIDHAA NA HUDUMA ZITUMIWAZO NA WAKAZI WA MIJINI - TANZANIA BARA (DEC.2001=100)) |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||