MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
|||||||||
| MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | |||||||||
Hali
ya Uchumi wa Taifa |
|||||||||
RASILIMALI
WATU |
|||||||||
Idadi ya Watu na Maendeleo 124. Makadirio ya idadi ya watu kwa kutumia takwimu za Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2002 yanaonyesha kuwa kwa mwaka 2004, Tanzania ilikuwa na watu wapatao 36,308,189. Kati ya hao, wanawake wanakadiriwa kuwa 18,524,586, sawa na asilimia 51 na wanaume wanakadiriwa kuwa 17,783,603, sawa na asilimia 49. Tanzania Bara ilikadiriwa kuwa na watu 35,268,073 wakati Tanzania Zanzibar ilikadiriwa kuwa na watu 1,040,116. Vile vile, kutokana na matokeo ya Sensa ya mwaka 2002, hali ya mgawanyo wa watu mijini na vijijini inaonyesha kwamba asilimia 77 ya watu wanaishi vijijini na asilimia 23 wanaishi mijini kwa upande wa Tanzania Bara. 125. Makadirio yaliyofanywa mwaka 2004 yanaonyesha kuwa watu wanaishi katika hali ya mtawanyiko. Aidha, msongamano huu unatofautiana mkoa hadi mkoa. Kwa upande wa Tanzania Bara mkoa ulio na msongamano mkubwa ni Dar es salaam ambao ulikuwa na watu 1931 kwa kilomita ya mraba, ukifuatiwa na Mwanza watu 159, na Kilimanjaro watu 107. Mikoa iliyo na msongamano mdogo ni Ruvuma na Rukwa yenye watu 18 kwa kilomita ya mraba, ikifuatiwa na Lindi yenye watu 12. Kwa upande wa Tanzania Zanzibar, karibu mikoa yote ina msongamano mkubwa wa kati ya watu 114 na 1,841 katika kilomita ya mraba. 126. Kutokana na matokeo ya uchambuzi wa Sensa ya mwaka 2002, kiwango cha vifo nchini kimeonyesha kuongezeka kidogo kutoka vifo 15 kwa kila watu 1000 mwaka 1988 hadi vifo 16 kwa kila watu 1000 mwaka 2002. Vifo vya watoto walio chini ya umri wa mwaka mmoja vimepungua kutoka 115 mwaka 1988 hadi 95 kati ya watoto 1000 wanaozaliwa hai mwaka 2002. Vile vile, vifo vya watoto walio chini ya umri wa miaka mitano vimepungua kutoka 191 mwaka 1988 hadi 153 kwa kila watoto 1000 mwaka 2002. 127. Kiwango cha uzazi nchini kimepungua katika kipindi cha miaka 14 iliyopita. Mwaka 1988, kiwango cha uzazi kilionyesha kuwa kila mwanamke mwenye umri wa kuzaa, alizaa wastani wa watoto 6.5, ikilinganishwa na wastani wa watoto 6.3 mwaka 2002. Kiwango hiki kimepungua hasa kutokana na kuongezeka kwa elimu na umri wa kuolewa. 128. Mwaka 2004, jitihada za kuhuisha Sera ya Taifa ya Idadi ya Watu ziliendelea na kukamilishwa. Katika kuimarisha utekelezaji wa Sera hii, aliteuliwa afisa mipango mmoja kutoka kila wilaya ili kuratibu masuala ya idadi ya watu wilayani. Maafisa mipango na wakurugenzi watendaji wa wilaya walipatiwa mafunzo ya kuainisha masuala ya idadi ya watu katika mipango ya maendeleo. Nguvukazi na Ajira 129. Matokeo ya Utafiti wa Nguvukazi wa mwaka 2000/01 yanaonyesha kuwa watu wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa milioni 17.8 kwa kipindi hicho. Makisio yanaonyesha kuwa kati ya watu 650,000 hadi 750,000 wamekuwa wanajiunga na soko la ajira kila mwaka. Asilimia themanini ya nguvu kazi ni watu wenye uwezo wa kufanya kazi, na kati ya hao, asilimia 84 wamejiajiri katika sekta ya asili ya kilimo; asilimia 6.0 katika sekta isiyo rasmi; asilimia 4.0 katika sekta rasmi binafsi; asilimia 3.5 katika kazi za nyumbani; asilimia 2.0 serikalini na asilimia 0.5 katika mashirika ya umma. Uchambuzi wa ajira unabainisha kuwa sekta ya kilimo; sekta isiyo rasmi na sekta rasmi binafsi ndizo zinazo ajiri watu wengi zaidi na, kwa kipindi kirefu, kilimo kitaendelea kuchukua nafasi kubwa ya ajira kuliko sekta zingine zinazoajiri. 130. Watu wasio na ajira kwa nchi nzima walikuwa milioni 2.3. Karibu nusu ya watu wasiokuwa na kazi walikuwa wakiishi mijini. Katika jiji la Dar es Salaam peke yake, asilimia 46.5 ya wenye uwezo wa kufanya kazi walikuwa hawana kazi, wakati miji mingine ni asilimia 25.5 na, maeneo ya vijijini ni asilimia 8.4. Hali ya kutokuwa na ajira ni kubwa miongoni mwa vijana, hasa wenye rika kati ya miaka 10 hadi 34. Wanawake ndiyo wanafanya kundi kubwa zaidi la wasio na ajira ikilinganishwa na wanaume. 131. Juhudi za Serikali zinazolenga kutatua matatizo ya ukosefu wa ajira na umasikini ni pamoja na kuandaa programu ya kukuza ajira nchini chini ya Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) na programu ya mafunzo ya ujuzi inayoendana na mahitaji ya soko. Ukuzaji wa biashara ndogo na za kati uliendelea kwa kuondoa urasimu katika uandikishwaji na kufanya marekebisho ya viwango vya kodi na leseni. Utekelezaji wa Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania (MKURABITA) unaendelea. Jedwali
Na. 33(JUMLA YA IDADI YA WATU NCHINI
TANZANIA KIMKOA: 1994-2004) |
|||||||||