MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA

Hali ya Uchumi wa Taifa
Hali ya Uchumi na Ushirikiano wa Kimataifa
Sekta ya Nje
Fedha za Serikali
Fedha na Taasisi za Fedha
Rasilimali Watu

     
SEKTA YA NJE
 
MAUZO NJE
Biashara ya Bidhaa

45. Thamani ya mauzo ya bidhaa nje iliongezeka kwa asilimia 18.2 mwaka 2004, hadi dola 1,334.9 milioni, ikilinganishwa na dola 1,129.2 milioni mwaka 2003. Ongezeko hilo lilichangiwa zaidi na bidhaa zisizo asilia hususan, dhahabu. Kwa jumla mauzo ya bidhaa asilia yalichangia asilimia 21.9 na yasiyo asilia yalichangia asilimia 78.1 ya mauzo yote ya bidhaa nje mwaka 2004.

Bidhaa Asilia:

46. Tofauti na mwenendo wa kushuka ulioonekana katika miaka ya 2001 na 2003, thamani ya mauzo ya bidhaa asilia iliongezeka kutoka dola 220.5 milioni mwaka 2003 hadi dola 292.3 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 32.6. Mafanikio haya yalichangiwa na kuongezeka kwa kiasi cha mauzo ya pamba kwa asilimia 60.4, tumbaku asilimia 44.3, na korosho asilimia 62.9. Aidha, matokeo haya yalichangiwa na hali nzuri ya hewa, na utumiaji sahihi wa mbolea na madawa ya kuulia wadudu. Kiasi cha mauzo ya kahawa, chai, katani na karafuu katika soko la dunia kilipungua ambapo bei ya kahawa, pamba, chai, korosho na karafuu ziliongezeka kwa viwango vya wastani kati ya asilimia 11 na 38.

Kahawa

47. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya kahawa ilipungua kidogo na kufikia dola 49.8 milioni kutokana na kupungua kwa kiasi cha kahawa kilichouzwa nje kwa asilimia 16.5 kufikia tani 38,600, kutoka na tani 46,200 mwaka 2003. Mwenendo huu ulichangiwa na kupungua kwa uzalishaji wa kahawa nchini. Hata hivyo, mapato yaliyotokana na mauzo ya kahawa hayakupungua sana kwa kuwa wastani wa bei ya kahawa katika soko la dunia uliongezeka kwa asilimia 19.3 kutoka dola 1,081.7 kwa tani mwaka 2003, na kufikia dola 1,290.4 kwa tani mwaka 2004. Kuongezeka kwa bei kulitokana na matarajio ya mahitaji makubwa ya kahawa katika kipindi cha baridi pamoja na uzalishaji mdogo wa kahawa katika nchi ya Brazil kwa mwaka 2004/05.

Pamba

48. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya pamba iliongezeka kwa asilimia 60.4 hadi dola 74.6 milioni kutoka dola 46.5 milioni mwaka 2003. Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka kwa kiasi cha mauzo ya pamba kwa asilimia 52 kutoka tani 46,900 mwaka 2003 hadi tani 71,300 mwaka 2004. Kuongezeka kwa kiasi kikubwa cha mauzo ya pamba kulichangiwa na kuongezeka kwa uzalishaji wa pamba nchini. Aidha, wastani wa bei ya pamba katika soko la dunia uliongezeka kwa asilimia 5.4 hadi kufikia dola 1,045.7 kwa tani mwaka 2004, ikilinganishwa na dola za marekani 992.0 kwa tani mwaka 2003.

Katani

49. Thamani ya mauzo ya katani, ilipungua kidogo na kufikia dola 7.2 milioni mwaka 2004, kutoka dola 7.3 milioni mwaka 2003. Hii ni kutokana na kupungua kwa kiasi cha mauzo ya katani iliyouzwa nje kwa asilimia 13.7 na kufikia tani 12,000 mwaka 2004, kutoka tani 13,900 mwaka 2003. Kupungua kwa kiasi cha mauzo ya katani iliyouzwa nje kulichangiwa na kupungua kwa uzalishaji wa katani nchini. Wastani wa bei ya katani katika soko la dunia uliongezeka kwa asilimia 15.1 hadi kufikia dola 602.8 kwa tani mwaka 2004, ikilinganishwa na dola 523.5 kwa tani mwaka 2003.

Chai

50. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya chai iliyouzwa nje ilikuwa dola 24.7 milioni, karibu sawa na thamani ya mauzo ya mwaka 2003 ya dola 24.8 milioni. Hali hii ilichangiwa na kupungua kwa kiasi cha mauzo nje kutoka tani 21,200 mwaka 2003, hadi tani 20,000 mwaka 2004, ingawaje wastani wa bei ya chai katika soko la dunia iliongezeka kwa asilimia 5.7 na kufikia dola 1,237.2 kwa tani mwaka 2004. Kupungua kwa kiasi cha chai iliyouzwa nje kulisababishwa na kupungua kwa uzalishaji wa chai nchini.

Tumbaku

51. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya tumbaku iliongezeka kwa asilimia 44.4 hadi dola 57.6 milioni kutoka dola 39.9 milioni mwaka 2003. Ongezeko kubwa la thamani ya mauzo ya tumbaku lilitokana na kuongezeka kwa kiasi cha mauzo ya tumbaku. Kiasi cha mauzo ya tumbaku kiliongezeka kwa asilimia 48.6 kutoka tani 18,300 mwaka 2003, hadi tani 27,200 mwaka 2004, kufuatia kuongezeka kwa uzalishaji wa tumbaku nchini. Hata hivyo, wastani wa bei ya tumbaku katika soko la dunia ulipungua kwa asilimia 2.6, kutoka dola 2,177.0 kwa tani mwaka 2003 hadi dola 2,120.4 kwa tani mwaka 2004.

Korosho

52. Thamani ya mauzo ya korosho iliongezeka kwa asilimia 62.9 na kufikia dola 68.1 milioni mwaka 2004, ikilinganishwa na dola 41.8 milioni mwaka 2003. Ongezeko kubwa la mapato ya mauzo ya korosho lilitokana na kuongezeka kwa kiasi cha mauzo nje kwa asilimia 28.6 kutoka tani 65.1 mwaka 2003 hadi tani 83.7 mwaka 2004 na kuongezeka kwa wastani wa bei katika soko la dunia. Wastani wa bei uliongezeka kwa asilimia 26.8 kutoka dola 641.6 kwa tani mwaka 2003, hadi dola 813.6 kwa tani mwaka 2004. Ongezeko la kiasi cha korosho iliyouzwa nje lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji wa korosho nchini.

Karafuu

53. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya karafuu ilibakia kuwa dola 10.3 milioni sawa na ilivyokuwa mwaka 2003. Kiasi cha karafuu iliyouzwa nje kilipungua kwa asilimia 23.2 kutoka tani 5,600 mwaka 2003, hadi tani 4,300 mwaka 2004. Hii ilitokana na kupungua kwa uzalishaji wa karafuu nchini. Pamoja na kupungua kwa kiasi kilichouzwa nje, thamani ya mauzo haikupungua kutokana na ongezeko la wastani wa bei ya karafuu katika soko la dunia kwa asilimia 28.6 kutoka dola 1,845.2 kwa tani mwaka 2003 hadi dola 2,372.8 kwa tani mwaka 2004.

Bidhaa Zisizo Asilia:

54. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia iliongezeka kwa asilimia 14.7 na kufikia dola 1,042.6 milioni kutoka dola 908.7 milioni mwaka 2003. Ongezeko hili lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na mauzo ya madini na hasa dhahabu ambayo bei yake iliongezeka katika soko la dunia. Bidhaa nyingine zilizochangia ongezeko hilo ni bidhaa za viwandani, na bidhaa za mboga na maua. Kwa jumla, mwaka 2004, mauzo ya bidhaa zisizo asilia yalichangia asilimia 78.1 ya mauzo yote ya bidhaa nje ikilinganishwa na asilimia 80.5 mwaka 2003. Dhahabu peke yake ilichangia asilimia 47.2. Aidha, thamani ya mauzo ya bidhaa zisizo asilia iliendelea kuongezeka mfululizo kutoka dola 232.2 milioni mwaka 1998 hadi dola 1,042.6 milioni mwaka 2004.

Madini

55. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya madini iliongezeka kwa asilimia 24.3 na kufikia dola 686.5 milioni kutoka dola 552.2 milioni mwaka 2003. Ongezeko la mauzo ya madini lilichangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la mauzo ya dhahabu ambayo ilichangia dola 629.5 milioni. Hii ni kutokana na ongezeko la wastani wa bei ya dhahabu katika soko la dunia kwa asilimia 24.0 na kufikia dola 10.5 kwa gramu mwaka 2004, kutoka dola 8.6 kwa gramu mwaka 2003. Hata hivyo, kiasi cha mauzo ya dhahabu nje kilipungua kwa asilimia 5.0 hadi kufikia gramu 50,000,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na gramu 52,499,000 mwaka 2003. Hii ilichangiwa na ongezeko la utengenezaji wa bidhaa za dhahabu hapa nchini.

Bidhaa za Viwandani

56. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya bidhaa za viwandani iliongezeka kwa asilimia 32.0 hadi kufikia dola 110.6 milioni kutoka dola 83.8 milioni mwaka 2003. Kuongezeka kwa mauzo ya bidhaa za viwandani ni matokeo ya kuongezeka kwa uzalishaji wa bidhaa za viwandani nchini kutokana na ubinafsishaji na uwekezaji.

Samaki na Mazao ya Samaki

57. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya samaki na mazao ya samaki ilipungua kwa asilimia 8.8 hadi dola 124.2 milioni kutoka dola 136.2 milioni mwaka 2003. Upungufu huo ulitokana na sababu mbalimbali ikiwemo mabadiliko ya hali ya hewa.

Mazao ya Mboga na Maua

58. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya mazao ya mboga na maua iliongezeka kwa asilimia 4.4, kutoka dola 13.7 milioni mwaka 2003 hadi dola 14.3 milioni. Ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka kwa uzalishaji nchini sambamba na kuongezeka kwa bei katika soko la dunia.

Bidhaa Nyinginezo Zilizouzwa Nje

59. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya bidhaa nyinginezo zikiwemo nafaka na matunda, zilizouzwa nje ilipungua kwa asilimia 13.0 hadi kufikia dola 106.9 milioni, kutoka dola 122.9 milioni mwaka 2003. Kupungua kwa mauzo ya bidhaa nyinginezo nje kulitokana na kupungua kwa kiasi cha bidhaa hizo zilizouzwa nje hasa nchi za jirani.

Biashara ya Huduma

60. Mapato yaliyotokana na huduma yaliongezeka kwa asilimia 33.1 hadi dola 913.7 milioni mwaka 2004 kutoka dola 686.6 milioni mwaka 2003. Ongezeko hilo lilitokana na kuongezeka kwa mapato ya usafirishaji wa mizigo kwa dola 80.1 milioni, huduma za utalii kwa dola 620.7 milioni na huduma nyinginezo (zikiwemo mawasiliano, ujenzi, bidhaa, fedha, tarakishi, taarifa, serikali, ada ya malipo na shughuli binafsi na huduma nyingine za kibiashara) kwa dola 213.0 milioni. Kuongezeka kwa mapato ya huduma kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na ongezeko la mapato yaliyotokana na huduma za usafiri na kuongezeka kwa ufanisi katika kitengo cha makontena katika Bandari ya Dar es Salaam.

BIDHAA ZILIZOAGIZWA KUTOKA NJE

61. Mwaka 2004, thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje (f.o.b.) iliongezeka kwa asilimia 18.0 hadi kufikia dola 2,281.2 milioni, ikilinganishwa na dola 1,933.5 milioni mwaka 2003. Kiasi cha uagizaji wa bidhaa kiliongezeka zaidi kuliko kile kilichouzwa nje na hivyo kuleta nakisi kubwa zaidi katika urari wa biashara ya bidhaa. Kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za kukuza mitaji, bidhaa za kati na bidhaa za matumizi ya kawaida kulichangia kuongezeka kwa thamani ya uagizaji wa bidhaa kutoka nje.

Bidhaa za Ukuzaji Mitaji

62. Mwaka 2004, uagizaji wa bidhaa za kukuza mitaji uliongezeka kwa asilimia 17.5 kutoka dola 814.8 milioni mwaka 2003 hadi dola 957.1 milioni. Kuongezeka kwa thamani ya uagizaji kulichangiwa na uagizaji mkubwa wa vyombo vya usafirishaji, mitambo na vifaa vya ujenzi. Uagizaji wa vyombo vya usafirishaji uliongezeka kwa asilimia 8.3, mitambo asilimia 20.7, na vifaa vya ujenzi asilimia 22.1. Mwenendo huu ulitokana na kupanuka kwa shughuli za viwandani, madini na utalii nchini.

Bidhaa za Kati

63. Thamani ya uagizaji wa bidhaa za kati iliongezeka kwa asilimia 6.8 kutoka dola 679.5 milioni mwaka 2003 hadi dola 725.4 milioni mwaka 2004. Kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za kati kulichangiwa zaidi na kuongezeka kwa uagizaji wa bidhaa za mafuta kwa asilimia 3, malighafi za viwandani asilimia 1, na mbolea asilimia 108.4. Kuongezeka kwa thamani ya mafuta yaliyoagizwa kutoka nje kulichangiwa na ongezeko la bei katika soko la dunia na kiasi cha mafuta yaliyoagizwa. Ongezeko la uagizaji wa bidhaa za kati ni matokeo ya kupanuka kwa shughuli za uchumi hasa uzalishaji viwandani na katika sekta za madini, utalii, biashara na mahitaji makubwa ya mbolea kwa kilimo.

Bidhaa za Matumizi ya Kawaida

64. Mwaka 2004, uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida uliongezeka kwa asilimia 30.8 hadi dola 824.4 milioni kutoka dola 630.3 milioni mwaka 2003. Ongezeko kubwa la uagizaji wa bidhaa za matumizi ya kawaida lilichangiwa zaidi na uagizaji wa chakula ambao uliongezeka kwa asilimia 49.8 kutoka dola 182.5 milioni mwaka 2003 hadi dola 273.4 milioni mwaka 2004 kulikosababishwa na ukame katika msimu wa 2003/2004. Uagizaji wa bidhaa nyingine za matumizi ya kawaida (zikiwemo dawa, bidhaa za plastiki, nguo, bidhaa za makaratasi na mpira,) uliongezeka kwa asilimia 33 kutoka dola 447.9 milioni mwaka 2003 hadi dola 550.9 milioni mwaka 2004, kutokana na kupanuka kwa mahitaji nchini.

Malipo ya Huduma

65. Malipo ya huduma yaliongezeka kwa asilimia 30.2 kutoka dola 769.5 milioni mwaka 2003 hadi dola 1002.0 milioni mwaka 2004. Kuongezeka kwa malipo ya huduma kulisababishwa na ongezeko kubwa la malipo ya gharama za usafiri (utalii), usafirishaji mizigo na huduma nyinginezo (zikiwemo mawasiliano, ujenzi, bima, fedha, tarakishi, taarifa, serikali na huduma nyingine za kibiashara). Malipo ya gharama za usafiri yakiwemo malipo ya elimu, posho za usafiri na gharama za matibabu yalikuwa dola 432.3 milioni. Malipo ya gharama za usafirishaji wa mizigo yalikuwa dola 250.3 milioni na huduma nyinginezo, dola 319.4 milioni.

Mwenendo wa Biashara baina ya Tanzania na Nchi Mbalimbali

66. Tanzania inafanya biashara na nchi zaidi ya 168 za Afrika, Ulaya, Marekani, Asia na Australia na inayo mahusiano ya kibiashara na Jumuiya za ushirikiano kikanda kama Jumuiya ya Umoja wa nchi za Ulaya, Jumuiya ya Afrika ya Mashariki, na Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za Kusini mwa Afrika.

67. Mwaka 2004, thamani ya mauzo ya bidhaa kwa nchi za Jumuiya ya Ulaya iliongezeka kwa asilimia 1.4 kutoka dola 644.9 milioni mwaka 2003 hadi dola 654.1 milioni. Ongezeko hilo lilichangiwa na mauzo ya bidhaa za madini, samaki na mazao ya samaki, bidhaa za mboga na maua na bidhaa asilia. Thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za Jumuiya ya Ulaya (C.I.F) iliongezeka kwa asilimia 9.9 kutoka dola 434.4 milioni mwaka 2003 hadi dola 477.3 milioni mwaka 2004.

68. Thamani ya mauzo ya bidhaa kwa nchi za Jumuiya ya Afrika ya Mashariki iliongezeka kwa asilimia 7.7 kufikia dola 95.4 milioni mwaka 2004 kutoka dola 88.6 milioni mwaka 2003. Mauzo kwa nchi ya Kenya yalichangia kiasi kikubwa cha ongezeko hili. Thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nchi za Afrika ya Mashariki iliongezeka kwa asilimia 11.1 hadi dola 137.7 milioni mwaka 2004 kutoka dola 124.1 milioni mwaka 2003.

69. Kwa nchi za SADC, thamani ya mauzo iliongezeka kwa asilimia 60.7 na kufikia dola 151.9 milioni mwaka 2004 kutoka dola 94.5 milioni mwaka 2003. Wakati huo huo, uagizaji uliongezeka kwa asilimia 11.3 na kufikia dola 365.3 milioni mwaka 2004 kutoka dola 328.2 milioni mwaka 2003. Ongezeko hili lilichangiwa na uagizaji mkubwa wa bidhaa kutoka Afrika ya Kusini, ambao ulikuwa asilimia 74.9 ya jumla ya uagizaji kutoka nchi za SADC. Aidha, thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka Afrika ya Kusini iliongezeka kwa asilimia 7.8 kutoka dola 306.4 milioni mwaka 2003 hadi dola 330.4 milioni mwaka 2004.

70. Kwa jumla, thamani ya mauzo ya bidhaa kwa nchi za bara la Afrika iliongezeka kwa asilimia 30.2 kutoka dola 205.3 milioni mwaka 2003 hadi dola 267.3 milioni mwaka 2004. Uagizaji kutoka nchi zote za Afrika uliongezeka zaidi ya mara nne kutoka dola 124.1 milioni mwaka 2003 na kufikia dola 565.7 milioni mwaka 2004.

     

Jedwali Na. 3.1: Urari wa Biashara ya Bidhaa Kati ya Tanzania na Jumuiya Mbalimbali za Ushirikiano Kikanda

Dola milion

Jumuiya/ Mwaka

1997

1998

1999

2000

2001

2002

2003

2004P

Jumuiya ya Ulaya

-113.68

-253.98

-177.35

31.27

52.83

118.6

-210.5

176.7

Jumuiya ya nchi za SADC

-117.64

-164.74

-182.54

-175.99

-200.57

143.6

-233.7

-213.4

Jumuiya ya Afrika Mashariki

- 73.18

- 75.54

-75.37

- 58.29

63.85

-57.07

-35.6

-42.3

Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania, Ofisi ya Rais, Mipango na Ubinafsishaji .

Jedwali Na. 3.2: Thamani ya Bidhaa Zilizouzwa Nje

Dola milioni

JUMUIYA/ NCHI

1997

1998

1999

2000

2001

2002

2003

2004p

JUMUIYA YA ULAYA

226.5

241.2

214.7

362.1

432.2

479.9

644.9

654.1

AFRIKA

 

 

 

 

 

 

 

 

Jumuiya ya maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC)

Afrika ya kusini

7.9

6.3

6.6

12.1

8.7

16.5

37.3

113.8

Zambia

10

3.7

2.8

4.7

5.5

17.4

17.7

6.8

Swaziland

-

-

-

-

-

-

-

2.8

Zimbabwe

-

-

-

-

-

-

-

1.2

Msumbiji

2.6

0.1

0.7

1.5

1.4

1.6

2.2

3.4

Jamhuri ya kidemokrasia ya Kongo

1.8

5

3.7

0.1

5.4

15.8

22.6

10.1

Nchi nyingine za SADC

-

-

-

-

-

20.3

24.7

13.8

Jumla- SADC

22.3

15.1

13.8

18.4

21

71.6

94.5

151.9

Jumuiya ya Afrika ya Mashariki

Kenya

12.8

26

21

32.2

38.1

35.3

78.3

83.7

Uganda

11.6

6.5

4.7

8.5

5.5

5.5

10.3

11.7

Jumla - EAC

24.4

32.5

25.7

40.7

43.6

40.8

88.6

95.4

Nchi nyingine za Afrika

4.5

0.5

3.5

4.7

6.2

22.9

22.2

20.0

JUMLA -AFRIKA

51.2

48.1

43

63.8

70.8

135.3

205.3

267.3

BARA LA AMERIKA

USA

21.4

12.8

18

15.2

15.1

13.5

11.3

13.7

Canada

1.7

0.7

0.6

0.5

0.5

1.4

1.7

4.8

Nchi nyingine za Bara la Amerika

-

-

-

-

-

1.3

2.7

2.6

JUMLA- BARA LA AMERIKA

23.1

13.5

18.6

15.7

15.6

16.2

15.7

21.1

India

66.5

114.8

112.8

98.5

82.2

64.2

69.6

100.7

Japan

60

45.5

43.9

34.2

68.5

96.3

88.2

64.3

Umoja wa Falme za Kiarabu

5

6.8

6.7

6.3

9.6

14.4

15.4

17.5

Hong Kong

18.2

5

7.8

8.8

8.7

11.2

9.9

12.3

Nchi nyinginezo

451.7

285.7

267

221.7

257.6

85.0

79.9

197.6

JUMLA KUU

752.5

588.5

543.2

663.2

776.4

902.5

1,129.2

1,334.9

Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania

p = Ya muda

Takwimu zimebadilishwa kutoka shilingi kwenda dola kwa kutumia wastani wa viwango vya fedha kwa dola. 2002- (966.6/=); 2003- (1038.6/=); 2004- (1089.6/=)

Jedwali Na. 3.3: Thamani ya Bidhaa Zilizoagizwa Nje (C.I.F)

Dola milioni

JUMUIYA/ NCHI

1997

1998

1999

2000

2001

2002

2003

2004p

JUMUIYA YA ULAYA

367.1

514.57

413.09

344.61

389.74

369.6

434.4

477.3

AFRIKA

Jumuiya ya Maendeleo ya Nchi za Kusini mwa Afrika (SADC)

Afrika ya Kusini

95.99

130.72

170.8

174.38

203.44

188.8

306.4

330.4

Zimbabwe

4.73

14.56

5.6

4.52

3.01

1.98

1.2

1.5

Zambia

25

17.04

7.26

2.4

1.8

4.32

2

6.1

Msumbiji

5.08

5.49

0.05

0.12

0.43

0.03

0.9

1.6

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo

0.19

0.5

0.11

0.11

0.24

0.37

0.7

0.8

Swaziland

8.95

11.53

12.52

12.86

12.65

15.62

12.2

17.2

Nchi nyingine za SADC

 

 

 

 

 

4.0

4.8

7.7

Jumla -SADC

139.94

179.84

196.34

194.39

221.57

215.16

328.2

365.3

Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC)

Kenya

95.66

105.79

95.05

93.37

96.08

95.21

115.9

130.1

Uganda

1.92

2.25

6.03

5.62

11.37

2.66

8.2

7.6

Jumla -EAC

97.58

108.04

101.08

98.99

107.45

97.87

124.1

137.7

Nchi nyingine za Afrika

0.18

0.05

0.09

0.01

0.17

9

17.8

43.2

JUMLA NCHI ZOTE ZA AFRIKA

237.7

287.93

297.51

293.39

329.19

322.1

124.1

565.7

BARA LA AMERIKA

USA

52.63

81.31

99.29

58.92

65.31

91.38

69.7

78.1

Canada

12.5

16.67

26.65

32.3

23.08

17.69

19.6

39.7

Nchi nyingine za Bara la Amerika

15.48

38.86

37.87

24.53

7.87

13.73

32.9

32.6

JUMLA NCHI ZA BARA LA AMERIKA

80.61

136.84

163.81

115.75

96.26

122.8

122.2

150.4

Japan

74.04

130.96

178.16

142.27

150.7

138.72

169.9

180.6

Umoja wa Falme za Kiarabu

93.45

59.73

51.01

56.95

108.98

97.08

146.8

184.7

China

61.54

48.75

58.01

68.03

70.55

78.97

116.7

171.4

India

77.51

89.76

94.57

88.78

87.47

106.84

167.7

216.1

NCHI NYINGINE

634.85

649.39

732.09

780.16

899.16

429.1

236.4

304.0

JUMLA KUU

1320.3

1588.7

1572.8

1533.9

1714.4

2092.99

2168.2

2,280.8

Chanzo: Benki Kuu ya Tanzania

 p = Ya muda

Takwimu zimebadilishwa kutoka shilingi kwenda dola kwa kutumia wastani wa viwango vya vya fedha kwa dola. 2002- (966.6/=); 2003- (1038.6/=); 2004- (1089.6/=).

 
 
MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE
   
Urari wa Biashara ya Bidhaa

71. Nakisi katika urari wa biashara ya bidhaa iliongezeka kwa asilimia 17.5 hadi dola 946.3 milioni mwaka 2004, ikilinganishwa na nakisi ya dola 804.2 milioni mwaka 2003. Kuongezeka kwa nakisi katika urari wa biashara ya bidhaa kulichangiwa zaidi na ongezeko la thamani ya bidhaa zilizoagizwa kutoka nje ikilinganishwa na ongezeko la mauzo ya bidhaa nje.

Urari wa Biashara ya Huduma

72. Nakisi katika urari wa biashara ya huduma iliongezeka kwa asilimia 6.4 kutoka nakisi ya dola 83.0 milioni mwaka 2003 hadi dola 88.3 milioni mwaka 2004. Kuongezeka kwa nakisi katika urari wa biashara ya huduma kulichangiwa na kuongezeka zaidi kwa malipo ya huduma mbalimbali zikiwemo huduma za utalii, uchukuzi wa mizigo, mawasiliano na bima.

Urari wa Mapato na Malipo Mbalimbali

73. Mwaka 2004, nakisi ya urari wa mapato na malipo mbalimbali yanayojumuisha fidia kwa wafanyakazi, gawio litokanalo na mitaji ya kifedha na riba kwa mwaka ilipungua kwa asilimia 8.9 na kufikia dola 40.3 milioni, ikilinganishwa na nakisi ya dola 43.9 milioni mwaka 2003. Kupungua kwa nakisi kulitokana na kupungua kwa malipo ya riba na gawio litokanalo na mitaji iliyolipwa nje.

Urari wa Uhamisho Mali wa Kawaida

74. Urari wa uhamisho mali wa kawaida unaojumuisha uhamisho wa fedha, misaada na unafuu wa kulipa madeni chini ya mpango wa “HIPC” uliongezeka kwa asilimia 18.1 na kufikia dola 646.1 milioni mwaka 2004, kutoka dola 546.9 milioni mwaka 2003. Ongezeko hili limechangiwa na ongezeko la misaada kwa serikali la asilimia 18.1 kutoka dola 543.3 milioni mwaka 2003 hadi kufikia dola 641.7 milioni mwaka 2004.

Urari wa Malipo ya Kawaida

75. Nakisi ya urari wa malipo ya kawaida ambao unajumuisha urari wa biashara ya bidhaa, huduma, malipo mbalimbali, na uhamisho mali wa kawaida iliongezeka kwa asilimia 11.6 na kufikia dola 428.8 milioni mwaka 2004, kutoka dola 384.2 milioni mwaka 2003. Kuongezeka kwa nakisi kulichangiwa zaidi na nakisi katika biashara ya bidhaa ambapo uagizaji wa bidhaa ulizidi uuzaji kwa dola 946.3 milioni.

Urari wa Mapato ya Vitega Uchumi

76. Urari wa mapato ya vitega uchumi unaojumuisha misaada ya vitega uchumi na ufutaji wa madeni unaofanywa na nchi marafiki ulipungua kwa asilimia 22.0 na kufikia dola 293.6 milioni mwaka 2004 kutoka dola 358.2 milioni mwaka 2003. Kupungua kwa urari huu kulitokana na kupungua kwa misaada ya vitega uchumi hadi kufikia dola 253.7 milioni kutoka dola 320.9 milioni mwaka 2003. Vile vile thamani ya madeni yaliyofutwa ilipungua na kufikia dola 265.7 milioni mwaka 2004, ikilinganishwa na dola 319.5 milioni mwaka 2003.

Urari wa Malipo Yote

77. Urari wa malipo yote kwa mwaka 2004, ulionyesha nakisi ya dola 98.1 milioni ikilinganishwa na ziada ya dola 69.9 milioni mwaka 2003. Nakisi katika urari huu ilitokana na kuongezeka kwa nakisi ya urari wa biashara ya bidhaa na ya huduma, na kupungua kwa misaada ya vitega uchumi na ufutiwaji madeni.

Akiba ya Fedha za Kigeni

78. Akiba ya fedha za kigeni iliongezeka kutoka dola 2,037.8 milioni mwaka 2003 hadi dola 2,296.1 milioni mwaka 2004. Kiasi cha akiba ya fedha za kigeni mwaka 2004, ni sawa na uagizaji wa miezi 8.4 ikilinganishwa na miezi 9.0 mwaka 2003.

Wastani wa Thamani ya Fedha ya Tanzania

79. Mwaka 2004, thamani ya fedha ya Tanzania ilikuwa na wastani wa sh. 1,089.6 kwa dola moja ya Marekani, ikilinganishwa na wastani wa shilingi 1,038.6 kwa dola moja ya Marekani mwaka 2003, sawa na kushuka thamani ya shilingi kwa asilimia 5.0. Aidha, thamani ya shilingi kwa dola moja ilikuwa sh.1,042.9 mwishoni mwa Desemba 2004 ikilinganishwa na sh. 1,063.6 mwishoni mwa Desemba 2003, sawa na ongezeko la thamani ya shilingi la asilimia 2.0. Jedwali Na.17(THAMANI YA BIDHAA ZA BIASHARA BAINA YA TANZANIA NA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.20( WASTANI WA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.21( WASTANI WA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE

MWENENDO WA BEI YA PAMBA NA KAHAWA ILIYOUZWA NCHI ZA NJE(US$/TANI)

Jedwali Na.22(FAHIRISI YA BEI YA BIDHAA MUHIMU ZILIZOUZWA NCHI ZA NJE)

Jedwali Na.23(AINA NA THAMANI YA BIDHAA ZILIZOAGIZWA TOKA NCHI ZA NJE)

MWENENDO WA URARI KATIKA MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE

Jedwali Na.24(MIZANIA YA MALIPO NA NCHI ZA NJE)