MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI
 

Kilimo
Maliasili na Utalii
Madini
Viwanda na Biashara
Ujenzi wa Maendeleo ya Ardhi
Mawasiliano na Uchukuzi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Nishati
Maji
Elimu na Mafunzo
Afya
Maendeleo ya Jamii

         
VIWANDA NA BIASHARA
 

Ukuaji wa Sekta

212. Mwaka 2004, sekta ya viwanda ilikua kwa kiwango sawa na cha mwaka 2003 cha asilimia 8.6. Aidha, mchango wa sekta ya viwanda katika Pato la Taifa ulikuwa asilimia 8.8 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 8.7 mwaka 2003. Kuongezeka kwa ukuaji na mchango wa sekta katika Pato la Taifa kulitokana na mafanikio ya sera ya ubinafsishaji ambapo viwanda vingi vimepata wawekezaji wenye uwezo na uzoefu wa kuendesha viwanda. Aidha, sera ya uwekezaji pia imewavutia wawekezaji wapya kuhamasika kuanzisha viwanda vipya hasa katika sekta ya usindikaji wa mazao ya chakula, mbegu za mafuta ya kula, chai, sukari, usindikaji wa matunda, usagishaji wa nafaka, bidhaa za mbao, viwanda vya bidhaa za chuma, na vifaa vya ujenzi.

213. Vile vile, utekelezaji wa programu za sera ya viwanda vidogo na biashara ndogo uliwawezesha wananchi wengi zaidi kuhamasika kuanzisha viwanda vidogo na biashara ndogo na hivyo kutoa mchango mkubwa kwa njia ya bidhaa zinazozalishwa, ajira na mapato ya wananchi katika juhudi za kupunguza umaskini.

Gharama za Uzalishaji

214. Gharama za uzalishaji katika sekta ya viwanda ziliongezeka kutoka sh. 1,103,768 milioni mwaka 2003, hadi sh. 1,337,908 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 21.2. Ongezeko hilo lilitokana na kiwango kikubwa cha Kodi ya Ongezeko la Thamani na gharama kubwa za umeme hivyo, kufanya bidhaa zinazozalishwa nchini kuwa na bei ya juu na kushindwa kushindana katika soko na bidhaa zinazotoka nje.

Uzalishaji Katika Baadhi ya Viwanda Nchini

215. Uzalishaji wa chuma na bidhaa za chuma uliongezeka kutoka tani 40,057 mwaka 2003 hadi tani 46,559 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 16.2. Uzalishaji wa Aluminium ulipungua kutoka tani 199 mwaka 2003 hadi tani 140 mwaka 2004, sawa na upungufu wa asilimia 29.6. Kuhusu vifaa vya ujenzi, uzalishaji wa bati ulikuwa tani 29,750 ikilinganishwa na tani 31,018 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 4.1. Uzalishaji wa rangi ulipungua kutoka lita 16.8 milioni mwaka 2003 hadi lita 15.9 milioni mwaka 2004, sawa na upungufu wa asilimia 5.3. Uzalishaji wa saruji uliongezeka kutoka tani 1,186 milioni mwaka 2003 hadi tani 1,280 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 7.9.

216. Uzalishaji wa nguo ulikuwa mita za mraba 109,848,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na mita za mraba 116,714,000 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 5.9. Uzalishaji wa magunia ya katani ulikuwa magunia 1,739,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na magunia 1,375,000 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 26.5. Uzalishaji wa kamba za katani ulikuwa tani 6,494 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 6,839 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 5.0. Uzalishaji wa magunia ya “Polythene” ulikuwa magunia 85,107,000 ikilinganishwa na magunia 67,945,000 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 25.3.

217. Uzalishaji wa mafuta ya kupikia ulikuwa tani 91,593 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 89,386 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 2.5. Uzalishaji wa unga wa ngano ulikuwa tani 333,789 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 355,616 mwaka 2003 sawa na upungufu wa asilimia 6.1. Uzalishaji wa biskuti na tambi ulikuwa tani 9,117 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 5,906 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 54.4. Uzalishaji wa sukari ulikuwa tani 202,261 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 212,908 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 5.0. Uzalishaji wa majani ya chai (blended tea) ulikuwa tani 5,201 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 4,997 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 4. 1.

218. Uzalishaji wa bia ulikuwa lita 203,218,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na lita 194,100,000 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 4.7. Uzalishaji wa vinywaji baridi ulikuwa lita 255,581,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na lita 212,502,000 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 20.3. Uzalishaji wa kibuku ulikuwa lita 10,119,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na lita 14,825,000 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 31.7. Uzalishaji wa Konyagi ulikuwa lita 4,470,000 mwaka 2004, ikilinganishwa na lita 3,670,000 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 21.8. Uzalishaji wa sigara ulikuwa sigara 4,220 milioni mwaka 2004, ikilinganishwa na sigara 3,920 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 7.7.

Biashara ya Ndani

219. Sekta ya biashara ya jumla, rejareja na mahoteli ikijumuisha na utalii ilikua kwa asilimia 8.0 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 6.5 mwaka 2003. Mchango wa sekta hii katika Pato la Taifa uliongezeka kwa asilimia 17.0 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 16.8 mwaka 2003.

220. Jumla ya leseni za biashara 99,296 zilitolewa mwaka 2003/04 ikilinganishwa na leseni 99,767 mwaka 2002/03, ambazo ziliingizia serikali jumla ya sh. 8,585 milioni, ikilinganishwa na sh. 8,670 milioni mwaka 2002/03. Aidha, idadi ya wafanyabiashara 1,690 walitozwa kiasi cha sh. 162 milioni ikiwa ni adhabu kwa kukiuka sheria na kanuni mbalimbali za uendeshaji wa biashara, ikilinganishwa na 11,971 waliotozwa kiasi cha sh. 460 milioni mwaka 2002/03. Sababu zilizochangia ongezeko la idadi ya wafanyabiashara wenye leseni ni kuondolewa kwa ada kwa biashara zote zenye mauzo yasiyofikia sh. 20 milioni, kupunguzwa kwa ada na kuwa sh. 20,000, kuondolewa ada za leseni kwa waombaji wapya, na kuondolewa kwa ada kwa biashara zote zenye kupata au kulipia ada kwenye mamlaka nyingine.

 

Jedwali Na. 13.1: Utoaji wa Leseni za Biashara 2002/03 – 2003/4

S/No

Mkoa

Idadi ya Leseni 2002/03

Idadi ya Leseni 2003/04

Ada

Iliyopatikana

2002/03

Ada

Iliyopatikana 2003/04

Idadi ya Wahalifu

Kiasi Kilichotozwa Kama Adhabu

1.

Arusha

6,257

6,404

329,167,189.90

407,395,502

-

16,336,035

2.

Dar es Salaam

18,106

16,673

2,310,313,104.00

1,988,109,848

-

 

3.

Dodoma

4,074

4,502

157,902,182.00

206,042,977

-

10,130,038

4.

H.Q (Wizarani)

4,100

4,205

2,641,387,973.60

2,649,162,274

-

97,501,849

5.

Iringa

7,456

1,046

275,658,816.00

20,837,705

270

1,661,000

6.

Kagera

2,500

3,637

112,827,400.00

155,014,290

380

6,251,900

7.

Kigoma

2,638

2,770

94,090,830.00

98,795,372

-

-

8.

Kilimanjaro

6,550

7,884

230,120,604.00

235,283,546

-

-

9.

Lindi

2,100

1,954

60,749,562.00

80,871,491

-

-

10.

Mara

3,740

3,927

124,489,562.00

130,714,040

-

-

11.

Mtwara

2,695

2,830

135,964,860.00

142,763,103

-

-

12.

Mwanza

6,926

6,925

513,308,211.00

564,030,825

-

10,377,330

13.

Manyara

2,350

2,930

101,848,308.00

108,652,000

140

1,641,000

14.

Morogoro

4,588

5,073

250,379,792.00

278,664,405

-

-

15.

Mbeya

5,318

5,444

419,906,810.00

463,986,088

-

-

16.

Pwani

2,751

2,916

106,979,849.00

117,677,834

-

-

17.

Ruvuma

2,178

2,689

98,611,826.00

137,309,334

410

5,773,221

18.

Rukwa

-

1,564

-

38,514,049

-

-

19.

Shinyanga

4,544

4,480

208,983,103.00

261,976,652

-

2,106,000

20.

Singida

2,509

2,394

75,349,250.00

80,793,230

-

5,632,700

21.

Tabora

2,787

3,200

136,614,847.00

141,374,585

-

-

22.

Tanga

5,600

5,849

285,958,578.00

277,152,890

490

5,277,200

Jumla

99,767

99,296

8,670,612,657.50

8,585,122,040

1,690

162,688,273

Chanzo: Wizara ya Viwanda na Biashara: Taarifa za Utoaji leseni za Mikoa na Wizara


Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya Dar-es-Salaam

221. Idadi ya washiriki wa maonyesho ya biashara ya kimataifa ya Dar es Salaam ilikuwa 2,187 mwaka 2004 ikilinganishwa na 1,882 mwaka 2003. Ongezeko hilo lilitokana na kuboreshwa kwa miundo mbinu katika uwanja wa maonyesho na kuhamasika kwa wafanyabiashara. Idadi hii ilijumuisha washiriki 365 kutoka mataifa 28 ya nje ikilinganishwa na 350 kutoka mataifa 22 mwaka 2003. Pia, washiriki 1,780 wa ndani walishiriki mwaka 2004, ikilinganishwa na 1,500 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 18.7.

Jedwali 13.2: Washiriki wa Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa kwa Kipindi cha 2000 - 2004

WAONYESHAJI

2000

2001

2002

2003

2004

Wawakilishi wa kiserikali toka nje

13

14

11

10

14

Nchi zilizoshiriki

28

30

30

22

28

Makampuni toka nje ya nchi

300

315

331

350

365

Washiriki wa Ndani

1,145

1,250

1,405

1,500

1,780

Jumla

1,486

1,609

1,405

1,882

2187

Chanzo: Bodi ya Biashara ya nje

222. Aidha, kiasi cha maulizo yenye thamani ya dola 31.7 milioni yalipokelewa kutoka nje mwaka 2004 ikilinganishwa na maulizo yenye thamani ya dola 22.39 milioni mwaka 2003. Maulizo ya uagizaji kutoka nje yalifikia dola 41.2 milioni 2004, ikilinganishwa na dola 9.06 mwaka 2003. Pia, kiasi cha sh. 1.2 bilioni zilikusanywa katika mauzo ya papo kwa papo mwaka 2004, ikilinganishwa na sh. 610.8 milioni mwaka 2003.

Jedwali Na.58(MATUMIZI YA SARUJI NCHINI)

Jedwali Na.59(UZALISHAJI WA BAADHI YA BIDHAA VIWANDANI)

Jedwali Na.60(VIWANDA: IDADI YA WATU WALIOAJIRIWA*)

Jedwali Na.61(VIWANDA: GHARAMA ZA KAZI*)

Jedwali Na.62(VIWANDA: MUHTASARI WA MATOKEO *)

Jedwali Na.63('VIWANDA - MUHTASARI WA MATOKEO KIMKOA*)

Jedwali Na.65(VIGEZO VYA UFANISI KATIKA SEKTA YA VIWANDA)

Back Top