MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
||||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | ||||||||||
Kilimo |
||||||||||
MADINI |
||||||||||
Ukuaji
wa Sekta
206. Sekta ya madini ilikua kwa asilimia 15.6 mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 18.0 mwaka 2003. Kupungua kwa kiwango cha ukuaji kulitokana na kukamilika kwa uwekezaji katika migodi mikubwa mingi. Hata hivyo, mchango wa sekta ya madini katika Pato la Taifa mwaka 2004, uliongezeka na kufikia asilimia 3.2 ikilinganishwa na asilimia 3.0 mwaka 2003. Aidha, jumla ya mauzo ya madini nje yalikuwa ni dola 656.3 milioni mwaka 2004 ikilinganishwa na dola 553.1 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 18.6. Utafutaji Madini 207. Mwaka 2004, jumla ya leseni 602 za utafutaji na uchimbaji madini mbalimbali zilitolewa ikilinganishwa na leseni 314 zilizotolewa mwaka 2003. Katika mwaka 2004, leseni za utafutaji zilikuwa 572 na za uchimbaji 30, ambapo mwaka 2003 leseni za utafutaji zilikuwa 297 na za uchimbaji 17. Uchimbaji na Uuzaji wa Madini: Almasi 208. Jumla ya karati 303,920 zilizalishwa mwaka 2004 ikilinganishwa na karati 239,382 zilizozalishwa mwaka 2003. Ongezeko hilo lilitokana na kugundulika kwa kiasi kikubwa cha almasi katika migodi ya Mwadui. Aidha, thamani ya almasi iliyouzwa ilikuwa ni dola 33.6 milioni ikilinganishwa na dola 31.9 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 5.3. Dhahabu 209. Mwaka 2004, jumla ya kilo 46,219 za dhahabu zilizalishwa ikilinganishwa na kiasi cha kilo 48,018 zilizopatikana katika mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 3.7. Hata hivyo, mapato ya mauzo ya dhahabu iliyouzwa nje kwa mwaka 2004, ilifikia dola 593.2 milioni ikilinganishwa na dola 504.1 milioni kwa mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 17.7. Ongezeko hili la la mapato limetokana na kupanda kwa bei ya dhahabu katika soko la nje mwaka 2004. Vito vya Thamani 210. Jumla ya kilo 1,613,848.5 zilipatikana mwaka 2004 ikilinganishwa na kilo 1,531,547.7 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 5.4. Jumla ya dola 26.9 milioni zilipatikana kutokana na mauzo ya vito vya thamani mwaka 2004, ikilinganishwa na dola milioni 19.1 mwaka 2003. Makaa ya Mawe 211. Uzalishaji wa makaa ya mawe uliongezeka kutoka tani 54,610 mwaka 2003 hadi tani 65,041 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 19.1 kutokana hasa na kuongezeka kwa utumiaji wa mkaa na Kiwanda cha Saruji Mbeya. Jedwali Na.56(UCHIMBAJI WA MADINI: KIASI KILICHOPATIKANA) Jedwali Na.57(MADINI YALIYOUZWA NCHI ZA NJE 1997 - 2004) |
||||||||||