MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
||||||||||||||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | ||||||||||||||||||||
Kilimo |
||||||||||||||||||||
MAJI |
||||||||||||||||||||
Utangulizi
271. Katika mwaka 2004, Serikali iliendelea kutekeleza Sera ya Maji ya Taifa ya mwaka 2002 kwa kujenga mazingira ya kuwezesha sekta hii kukua ili kuwawezesha wananchi kuishi maisha bora na kuchangia katika kupunguza umaskini. Utekelezaji wa sera ulilenga kushirikisha wananchi na watendaji wa halmashauri za wilaya. Aidha, utekelezaji ulilenga kuhamasisha ushiriki wa taasisi za kimataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali na sekta binafsi. Vilevile, serikali iliendelea kutekeleza mikakati inayolenga kuimarisha upatikanaji, usambazaji na usimamizi wa maji; kukarabati mifumo ya maji na kufanya utafiti wa kuchimba visima. Pia, nakala 16,250 za sera zilisambazwa kwa wadau mbalimbali. Huduma ya Maji Vijijini 272. Utoaji endelevu wa huduma ya maji safi ya kutosha na salama vijijini, uliendelea. Miradi ya maji Morogoro, Dodoma na Tabora ilikamilika. Upatikanaji wa huduma ya maji safi vijijini uliongezeka kutoka asilimia 53.0 mwaka 2003 hadi asilimia 53.5 mwaka 2004. Idadi ya watu waliopata huduma ya maji safi iliongezeka kutoka 13,825, 161 mwaka 2003 hadi 14,553,853 mwaka 2004. 273. Idadi ya kamati za maji na thamani ya mifuko ya maji ilibakia 8,363 na sh. 1.3 bilioni, kwa mtiririko huo kama ilivyokuwa mwaka 2003. Hata hivyo, idadi ya mifuko iliongezeka kutoka 7,226 mwaka 2003 hadi mifuko 7,254 mwaka 2004. Hii inatokana na kuhamasika zaidi kwa wananchi juu ya umuhimu wa kuchangia huduma za jamii. Aidha, bodi za kusimamia mamlaka za maji ziliongezeka kutoka 30 mwaka 2003 hadi 39 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 30. Vyombo vingine vya maji vijijini vilivyoundwa kisheria ni pamoja na jumuiya za watumiaji maji 62, vikundi vya watumiaji maji vijijini 1,709, vyombo vya udhamini 3, na makampuni ya maji 23. 274. Katika kuhamasisha na kuratibu utunzaji wa vyanzo vya maji maeneo yaliyofanyiwa utafiti kwa ajili ya kuchimba visima virefu na vifupi yalifikia 1,033 mwaka 2004 kutoka maeneo 618 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 67.2. Huduma ya Maji Mijini 275. Ukarabati wa mifumo ya maji katika miji ya Morogoro, Dodoma, Tabora, Arusha, Moshi na Tanga umeongeza upatikanaji wa maji kutoka jumla ya meta za ujazo 103,600 mwaka 1988/89 hadi meta za ujazo 109,110 mwaka 2004. Upatikanaji wa huduma ya maji safi mijini kwa mwaka 2004 umeendelea kuwa asilimia 74.0 kama ilivyokuwa mwaka 2003 kutokana na ongezeko la watu mijini. Aidha, uondoaji wa maji taka mijini umeongezeka kutoka asilimia 10 kwa mwaka 2003 hadi asilimia 17 mwaka 2004. Jedwali Na.18.1: Maeneo Yaliyofanyiwa Tafiti za Kuchimba Visima na Sampuli za Maji Zilizochunguzwa na Maabara Kuu
Jedwali Na.77(Hali ya Huduma ya Maji Vijijini kwa mwaka 2004) Jedwali Na.77A(Hali ya Huduma ya Maji Vijijini kwa mwaka 2004) Jedwali Na.78(Hali ya Huduma ya Maji Vijijini kwa mwaka 2004) Jedwali
Na.79(USAMBAZAJI WA MAJI VIJIJINI) |
||||||||||||||||||||