MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI
 

Kilimo
Maliasili na Utalii
Madini
Viwanda na Biashara
Ujenzi wa Maendeleo ya Ardhi
Mawasiliano na Uchukuzi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Nishati
Maji
Elimu na Mafunzo
Afya
Maendeleo ya Jamii

         
MAWASILIANO NA UCHUKUZI

Ukuaji wa Sekta

238. Sekta ya mawasiliano na uchukuzi ilikua kwa asilimia 6.2 mwaka 2004 ikilinganishwa na asilimia 5.0 mwaka 2003. Ongezeko la ukuaji limetokana na kuongezeka kwa uwekezaji katika huduma za mawasiliano hususan simu za mikononi. Sehemu kubwa ya mafanikio haya yamechangiwa na uwekezaji wa sekta binafsi. Mchango wa sekta ya mawasiliano na uchukuzi katika Pato la Taifa ulibakia katika kiwango cha mwaka 2003 cha asilimia 5.4.

UCHUKUZI

Usafiri wa Abiria Mijini

239. Mwaka 2004, usafirishaji wa abiria mijini uliendeshwa kwa ushindani mkubwa kutokana na kuongezeka kwa ubora wa mtandao wa barabara mijini. Ushindani uliopo katika sekta hii umesaidia kuboresha huduma za usafiri mijini. Idadi ya mabasi ya abiria imeendelea kuongezeka katika baadhi ya miji mikuu ya mkoa. Kwa upande wa jiji la Dar es Salaam, idadi ya mabasi iliongezeka kutoka 5,801 mwaka 2003 hadi 6,600 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 8.0. Ongezeko hili lilitokana na mahitaji makubwa ya usafiri wa mabasi katika Jiji la Dar es Salaam. Mchanganuo wa idadi ya mabasi ya abiria mijini ni kama unavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 15.1.

Jedwali Na. 15.1: Idadi ya Mabasi ya Abiria Mijini

Miji

Idara ya Mabasi

2003

2004

Dodoma

153

170

Arusha

1118

1045

Moshi

225

720

Lindi

3

11

Tanga

120

169

Morogoro

312

300

Kibaha (Pwani)

-

130

Dar es salaam

5801

6600

Sumbawanga (Rukwa)

13

32

Mtwara

35

29

Songea

52

76

Iringa

97

113

Shinyanga

-

-

Mbeya

355

475

Singida

7

9

Tabora

17

37

Kigoma

70

472

Bukoba

25

21

Mwanza

660

776

Musoma

49

47

Manyara (Babati)

-

47

Jumla

9,088

11,279

Chanzo: Ofisi ya Taifa ya Takwimu

 
Usafiri wa Reli

Shirika la Reli Tanzania

240. Shirika la Reli Tanzania lilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani 1,333,249 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 1,450,000 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 8.1. Kati ya mizigo hiyo, asilimia 27.5 ilikuwa ya nchi za jirani. Kwa upande wa abiria, Shirika lilisafirisha abiria 464,000 mwaka 2004 ikilinganishwa na abiria 666,000 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 30.3. Shirika lilipata sh. 56.4 bilioni mwaka 2004 ikilinganishwa na sh 61.5 bilioni mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 8.3.

241. Shirika liliendelea kukabiliwa na matatizo ya uchakavu na uhaba wa mabehewa na injini na uchakavu wa njia za mawasiliano. Shirika la Reli la Trans Africa lilisafirisha mizigo yenye uzito wa tani 111,712 mwaka 2004 ikilinganishwa na tani 118,772 mwaka 2003.

Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia (TAZARA)

242. Mwaka 2004, Mamlaka ya Reli ya Tanzania na Zambia ilisafirisha jumla ya abiria 929,000 ikilinganishwa na abiria 1,021,384 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 9.0. Kwa upande wa mizigo, jumla ya tani 610,286 zilisafirishwa mwaka 2004 ikilinganishwa na tani 613,693 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 0.5. Mwaka 2004, Mamlaka ilikusanya jumla ya sh. 32,970 milioni ikilinganishwa na mapato ya sh. 26,266 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 25.5. Ongezeko hilo la mapato limetokana na ukusanyaji mzuri wa malimbikizo ya madai kutoka kwa wadaiwa mbali mbali. Mamlaka iliendelea kukabiliwa na uhaba wa fedha za uendeshaji, uchakavu wa injini na mabehewa, na uhaba wa vitendea kazi.

Usafiri wa Anga

243. Mwaka 2004, makampuni ya ndege ya ndani ya nchi ambayo yaliendelea kutoa huduma ni pamoja na Air Tanzania Company Limited (ATCL), Precision Air, Wakala wa Ndege za Serikali, Coastal Travel, Regional Air Services, Air Excel, Flight Link, na Zan Air. Jumla ya abiria 1,950,383 wa ndani na nje walisafirishwa mwaka 2004, ikilinganishwa na 1,876,553 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 3.9.

244. Idadi ya abiria wa ndani iliongezeka kutoka abiria 973,262 mwaka 2003 hadi 1,074,035 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 10.4. Aidha, idadi ya safari za ndege za kimataifa iliongezeka kwa asilimia 23.8 kutoka 20,060 mwaka 2003 hadi 24,835 mwaka 2004.

Kampuni ya Ndege Tanzania (ATCL)

245. Mwaka 2004, Kampuni ya Ndege Tanzania inayomilikiwa na Serikali ya Tanzania na Shirika la Ndege la Afrika ya Kusini iliongeza idadi ya ndege zake kutoka moja mwaka 2003 hadi nne. Jumla ya abiria 268,168 walisafiri kwa ndege za Kampuni mwaka 2004 ikilinganishwa na abiria 149,540 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 79.3. Ongezeko hili kubwa la abiria lilitokana na juhudi kubwa za uboreshaji wa huduma za usafiri wa Kampuni. Mapato ya Kampuni yaliongezeka kutoka sh. 15 bilioni mwaka 2003 hadi sh. 38 bilioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 153.3.

Makampuni mengine ya Ndege

246. Mwaka 2004, makampuni mengine ya ndege yalisafirisha nchini abiria 535,165 ikilinganishwa na 429,567 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 24.6. Jedwali 15.2 linaonyesha idadi ya abiria waliosafirishwa na ndege nchini.

Jedwali Na. 15.2: Idadi ya Abiria Waliosafirishwa na Ndege Nchini

Kampuni za Ndege

Idadi ya Abiria Waliosafirishwa

Mwaka 2003

Mwaka 2004

Kam puni ya Ndege Tanzania (ATCL)

149,540

268,168

Precision Air

248,375

314,720

Coastal Travel

76,856

90,277

Regional Air Services

23,179

29,353

Air Excel

-

17,773

Flight Link

413

173

Zan Air

35,372

45,641

Makampuni Mengineyo

45,372

37,228

Jumla

579,107

803,333

Chanzo: Wakala wa Usalama wa Anga (TCAA)

 Usafiri wa Majini

Uchukuzi wa Baharini

247. Bandari ya Dar-es-Salaam ilihudumia jumla ya shehena zenye jumla ya tani 5,761 milioni mwaka 2004 ikilinganishwa na tani 5,107 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 12.8. Kati ya shehena hizo, tani 2,286 milioni, sawa na asilimia 39.7 zilihudumiwa na Kitengo cha Kontena chini ya mwendeshaji binafsi, ikilinganishwa na tani 1,868 milioni mwaka 2003. Jumla ya meli 3,897 zilihudumiwa mwaka 2004, ikilinganishwa na meli 4,034 mwaka 2003, sawa na upungufu wa asilimia 3.4. Makontena 22.8 yalihudumiwa kwa saa mwaka 2004, ikilinganishwa na makontena 22.6 kwa saa mwaka 2003. Muda wa makontena kukaa bandarini uliongezeka kutoka wastani wa siku 11.3 mwaka 2003 hadi siku 13.2 mwaka 2004. Hali hiyo iliyochangiwa na utendaji hafifu wa Shirika la Reli Tanzania, TAZARA, na uchukuzi kwa njia ya barabara.

Usafiri katika Maziwa

248. Katika mwaka 2004, sheria mpya ya Bandari ilipitishwa ambapo bandari zote za mwambao nchini na maziwa makuu ya Victoria, Tanganyika na Nyasa zitamilikiwa na kuendeshwa chini ya usimamizi wa mamlaka mpya. Mamlaka hiyo itahusika na umiliki wa bandari hizo, wakati shughuli zote za kibiashara zitafanywa kupitia waendeshaji binafsi. Hivyo, Kampuni ya Huduma za Meli Tanzania ilianza kuendesha shughuli zake kwa kuzingatia sheria mpya. Kampuni ilisafirisha jumla ya abiria 483,619 mwaka 2004, ikilinganishwa na 347,564 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asimilia 39.1. Kwa upande wa mizigo, Kampuni ilisafirisha jumla ya tani 167,177 mwaka 2004, ikilinganishwa na tani 143,751 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 16.3.

HUDUMA ZA MAWASILIANO

Shirika la Posta

249. Katika mwaka 2004, barua zilizotumwa nchini ziliongezeka hadi 19 milioni ikilinganishwa na 18.2 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 4.4. Hali kadhalika, barua ziendazo nje nazo ziliongezeka kutoka 6.7 milioni mwaka 2003 hadi 7.1 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 6.0. Vifurushi vilivyotumwa nchini navyo vimeongezeka kutoka 29,832 mwaka 2003 hadi 42,710 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 43.2. Kwa upande wa vifurushi vya nje vimeongezeka kutoka 6,664 mwaka 2003 hadi 7,531 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 13.0.

250. Barua za rejesta ndani ya nchi ziliongezeka kutoka 405,100 mwaka 2003 hadi 542,327 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 33.9. Rejesta zilizotumwa nje ya nchi nazo ziliongezeka kutoka 42,386 mwaka 2003 hadi 69,699 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 64.4. Huduma za amana za haraka ilipungua kutoka 269,209 mwaka 2003 hadi 246,317 mwaka 2004, sawa na upungufu wa asilimia 9. Thamani ya amana za haraka mwaka 2003 ilikuwa sh 9.3 billioni ikilinganishwa na sh. 7.8 billioni mwaka 2004.

251. Nyaraka na Vipeto vilivyosambazwa ndani ya nchi viliongezeka kutoka 268,708 mwaka 2003 hadi 290,254 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 8.0. Nyaraka na vipeto vilivyosambazwa nje ya nchi navyo viliongezeka kutoka 19,671 mwaka 2003 hadi 29,210 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 48.5. Kadhalika, utumaji wa fedha kwa njia za ”Money Fax” zimeonyesha mafanikio, kwa kuongezeka kutoka 203,821 mwaka 2003 hadi 277,531 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 36.2.

252. Utumaji wa taarifa za haraka kwa njia za EMS na ujumbe mbali mbali nao uliongezeka kutoka 18,826 mwaka 2003 hadi 20,964 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 11.4. Jedwali Na. 15.3 linaonyesha mtandao wa Posta nchini 2003 – 2004.

Jedwali Na.15.3: Mtandao wa Posta nchini mwaka 2003 - 2004.

Maelezo

Mwaka 2003

Mwaka 2004

Posta Kamili

154

156

Posta Kamili Wakala

85

92

Posta Ndogo

149

166

Mail Delivery Centres

27

27

Masanduku yaliyosimikwa

168,881

171,654

Masanduku Yaliyokodishwa

143,691

145,037

Vibali vya kuuza Stempu

3,715

3,487

Mifuko ya barua ya pekee

215

222

Chanzo : Shirika la Posta Tanzania

Huduma za Simu

253. Mwaka 2004, Kampuni ya Simu Tanzania ilifanikiwa kumaliza mgogoro uliodumu kwa muda mrefu kati ya wabia wa Celtel International na serikali kuhusu malipo ya pili ya ununuzi wa hisa za asilimia 35.

254. Uwezo wa mitambo ya simu za msingi za Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) uliongezeka kutoka 243,722 mwaka 2003 hadi 244,536 mwaka 2004, sawa na ongezeko asilimia 0.3. Hii ilitokana na kuondoa mitambo ya zamani na kuweka mitambo mipya ya kisasa kulingana na mahitaji ya wateja. Idadi ya simu zilizounganishwa iliongezeka kutoka 146,075 mwaka 2003 hadi 148,360 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 1.6. Aidha, idadi ya simu kwa kila watu 100 iliongezeka kutoka 0.40 mwaka 2003 hadi 0.41 mwaka 2004.

255. Idadi ya wateja wa simu za mkononi iliongezeka kutoka 1,298,000 mwaka 2003 hadi 1,942,000 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 49.6. Ongezeko hili limetokana na mwamko kwa wananchi kuhitaji simu za mkononi kwa ajili ya urahisi wa mawasiliano. Mchanganuo wa wateja wa simu za mkononi ni kama ilivyoainishwa katika Jedwali Na.15.4.

Jedwali Na.15.4: Wateja wa simu za mkononi kwa Kampuni

Jina la Kampuni

Idadi ya Wateja

2003

2004

MOBITEL

210,000

258,000

VODACOM

700,000

995,749

ZANTEL

68,000

85,000

CELTEL

320,000

450,000

JUMLA

1,298,000

1,788,749

Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

Udhibiti wa Shughuli za Mawasiliano 256. Mwaka 2004, Mamlaka ya Udhibiti wa Shughuli za Mawasiliano iliendelea kutekeleza majukumu yake ya kudhibiti shughuli za mawasiliano na habari nchini. Wateja wa huduma za mawasiliano wameongezeka kutoka 1,014,110 mwaka 2003 hadi 2,090,360 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 106 kwa muda huu mfupi ambapo Mamlaka hii imeanzishwa. Mchanganuo wa watoa huduma za aina mbalimbali za mawasiliano inaonyeshwa katika Jedwali Na. 15.5.

Jedwali Na.15.5: Mchanganuo wa Watoa Huduma za Mawasiliano

Watoa Huduma

Idadi ya Watoa Huduma

2003

2004

Simu za Mkononi

4

4

Watoa huduma za kusafiririsha takwimu kwa mtandao wa Tarakishi

18

18

Watoa huduma za mtandao wa Tarakishi

21

21

Posta

16

16

Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania 

 

Jedwali Na.67(SHIRIKA LA RELI TANZANIA)

Jedwali Na.68(RELI YA UHURU - TAZARA )

Jedwali Na.69(USAFIRISHAJI KWA MELI: DAR ES SALAAM)

Jedwali Na.70(HUDUMA ZA POSTA)

Jedwali Na.71(HUDUMA ZA SIMU)

Jedwali Na.72(HUDUMA ZA SIMU)

Jedwali Na.73(SHIRIKA LA NDEGE TANZANIA (ATC)+)

Back Top