MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI

MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI
   

Kilimo
Maliasili na Utalii
Madini
Viwanda na Biashara
Ujenzi wa Maendeleo ya Ardhi
Mawasiliano na Uchukuzi
Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
Nishati
Maji
Elimu na Mafunzo
Afya
Maendeleo ya Jamii

         
TEKNOLOJIA YA HABARI NA MAWASILIANO
 

Utangulizi

257. Teknolojia ya Habari na Mawasiliano kwa miaka ya karibuni imekuwa chombo muhimu katika uchumi na maendeleo ya nchi. Mchango wa sekta hii katika mwenendo wa uchumi unaendelea kukua. Mwaka 2003, serikali iliandaa Sera ya Habari na Teknolojia ili kuhakikisha kuwa teknolojia hiyo inatumika ipasavyo katika kusaidia kuleta maendeleo ya kiuchumi na kijamii. Matumizi ya Teknolojia ya Mawasiliano na Habari yameboresha utendaji kazi katika wizara, mikoa, idara na wakala mbalimbali wa serikali pamoja na sekta binafsi.

Usajili wa Kampuni za Mtandao

258. Hadi Desemba 2004, Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ilikuwa imesajili kampuni 23 za mtandao. Kati ya hizo, 15 zilikuwa zinatoa huduma za mtandao na kampuni 8 zilipata usajili lakini zilikuwa bado hazitoi huduma hizo. Baadhi ya kampuni hizo ni pamoja na Simba Net, TTCL, University Computing Centre, Raha.com. Kampuni hizo zinatoa huduma za tovuti katika mikoa, wizara, idara na wakala mbalimbali wa serikali. Mwaka 2004, jumla ya tovuti 113 zilisajiliwa ikilinganishwa na tovuti 98 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 16.3. Hii ilitokana na kuongezeka kwa watumiaji nchini.

Jedwali Na. 16.1: Idadi ya Vituo vya Tovuti na Huduma za Mitandao Zilizosajiliwa 2000-2004

Mwaka

2000

2001

2002

2003

2004

Tovuti

56

70

90

98

113

Huduma za mtandao

11

17

20

22

23

Chanzo: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania

Radio na Televisheni

259. Hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini, Tanzania Bara ilikuwa na radio moja tu ambayo ni Radio Tanzania Dar-es-Salaam. Mwaka 1993, Bunge la Tanzania lilipitisha sheria ya kuruhusu vyombo binafsi kuingia katika shughuli za habari. Kupitishwa kwa sheria hiyo kulitoa fursa kwa sekta binafsi kuanzisha vituo vya radio na televisheni. Mwaka 1994, kituo cha kwanza binafsi cha radio na televisheni kilianzishwa na kuanza kurusha matangazo yake hewani. Fursa hii ya kuruhusu sekta binafsi kutoa huduma ya habari na utangazaji ilileta changamoto ya kuanzishwa kwa vituo vingi zaidi vyenye ushindani wa kimaendeleo. Hadi kufikia mwaka 2004, jumla ya vituo 33 vya radio vilisajiliwa. Kati ya hivyo, 2 vinamilikiwa na serikali na 31 sekta binafsi. Vituo vya televisheni vilifikia 15 ambapo kimoja kinamilikiwa na serikali na 14 vinamilikiwa na sekta binafsi.

Radio

260. Mwaka 2004, idadi ya vituo vya redio iliongezeka hadi 33 kutoka 29 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 14.0. Vituo vya mitambo ya kurushia matangazo viliongezeka kutoka vituo 59 mwaka 2003 hadi 63 mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 6.7. Kasi ya ukuaji huu ilitokana na kuongezeka kwa mahitaji na idadi ya watumiaji wa vyombo hivi kupata habari za matukio na masuala mbalimbali ya kiuchumi, kisiasa, kijamii na burudani. Vile vile, kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano kumechangia kuongezeka huko. Jedwali Na. 16.2 linaonyesha idadi ya vituo vya radio na television vilivyosajiliwa mwaka 1994 – 2004.  

Jedwali Na. 16.2: Vituo vya Radio na Televisheni vilivyosajiliwa kuanzia mwaka 1994 – 2004

Mwaka

Radio

Television

1994

4

3

1995

5

4

1996

8

4

1997

8

4

1998

9

6

1999

12

9

2000

16

13

2001

22

13

2002

27

15

2003

29

15

2004

33

15

Chanzo: Tume ya Mawasiliano Tanzania

Televisheni

261. Hadi mwaka 2002, idadi ya vituo vya televisheni vilivyokuwa vimesajiliwa nchini vilifikia 15, idadi ambayo haikubadilika hadi mwaka 2004. Kutokana na kuongezeka kwa mahitaji ya kupata taarifa mbalimbali kupitia televisheni, baadhi ya Miji na Halmashauri za wilaya zilianzisha vituo vya televisheni ambavyo hurusha bure matangazo ya vituo vingine, hivyo kuwawezesha watumiaji kupata huduma hiyo kwa urahisi zaidi. Hadi mwaka 2004, vituo hivi vilifikia 16, kama inavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 16.3. Aidha, vituo mbalimbali vilitoa huduma kwa malipo yanayowawezesha wananchi kupata matangazo ya vituo vya televisheni kwa kuwaunganisha watumiaji na matangazo ya vituo mbalimbali. Hadi mwaka 2004, vituo hivyo vilifikia 16, kama ilivyoonyeshwa katika Jedwali Na. 16.4. Hadi kufikia mwaka 2004, kulikuwa na vituo 5 vinavyorusha matangazo kwa njia ya satellite, ikilinganishwa na 3 mwaka 2003. Vituo hivyo ni TVT, ITV, Star TV, Channel Ten na Channel 5.  

Jedwali na 16.3: Vituo vya Televisheni vinavyorusha matangazo ya Televisheni nyingine.

Kituo

Sehemu kituo kilipo.

Mkoa

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Njombe

Njombe

Iringa

Televisheni ya Halmashauri ya Manispaa Iringa

Iringa

Iringa

Televisheni ya Halmashauri ya Mji Musoma

Musoma

Mara

Televisheni Shule ya Sekondari Mwakaleli

Tukuyu

Mbeya

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Rungwe

Rungwe

Mbeya

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Mbozi

Mbozi

Mbeya

Televisheni ya Kiwanda cha Kubangulia Kahawa Mbozi

Tunduma Highway

Mbeya

Televisheni ya Halmashauri ya Manispaa Mbeya

Mbeya

Mbeya

Televisheni ya Chuo Kikuu Mzumbe

Mzumbe

Morogoro

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Masasi

Masasi

Mtwara

Televisheni ya Mgodi wa Dhahabu Ashanti

Geita

Mwanza

Televisheni ya Halmashauri ya Mji Songea

Songea

Ruvuma

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Tunduru

Tunduru

Ruvuma

Televisheni ya Halmashauri ya Wilaya ya Iramba

Iramba

Singida

Televisheni ya Halmashauri ya Mji Sumbawanga

Sumbawanga

Sumbawanga

C.G TV Transmission Centre

Tabora

Tabora

Chanzo: Taasisi ya utangazaji Tanzania .

 Jedwali na 16.4: Vituo vya televisheni vinavyorusha matangazo kwa kuwaunganisha wateja kwa kutumia waya maalumu.

Kituo

Sehemu kituo kilipo.

Mkoa

Bharat Video Centre

Arusha

Arusha

Millan Video Centre

Arusha

Arusha

Arusha CTV

Arusha

Arusha

CTV DAR-ES-SALAAM.

DSM

DSM

WIN CTV

DSM

DSM

IECTN Moshi

Moshi

Kilimanjaro

Babati CTV

Babati

Manyara

Space Satellite CTV

Musoma

Mara

CTV Mbeya

Mbalizi Road

Mbeya

CTV Morogoro

Taifa Road

Morogoro

Mwanza Satellite CTV

Mwanza

Mwanza

Ghana CTV

Mwanza

Mwanza

Tabora CTV

Tabora

Tabora

Califonia CTV

Tabora

Tabora

CTV Tanga

Tanga

Tanga

Bahma Satellite Cable Television

Tanga

Tanga

Chanzo: Taasisi ya Utangazaji Tanzania.

 Taasisi ya Utangazaji Tanzania (TUT)

262. Mwaka 2004, Taasisi ya Utangazaji Tanzania ilianzishwa baada ya kuunganishwa kwa Radio Tanzania Dar-es-Salaam (RTD) na Televisheni ya Taifa (TVT). Taasisi hii hutoa huduma za kijamii na kibiashara. Mwaka 2004, Taasisi ilipata jumla ya sh. 1,516.6 milioni kutokana na mapato ya biashara ikilinganishwa na sh. 1,289.2 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 16.6. Kiwango hiki cha mapato kilifikiwa kutokana na mikakati mizuri ya masoko na kuboreshwa kwa vipindi mbalimbali. Jedwali Na 16.5. linaonyesha mwenendo wa mapato.

Jedwali na. 16.5: Mwenendo wa mapato mwaka 2001 - 2004

sh. milioni

Mwaka

RTD

TVT

Jumla

2001

667.0

285.2

952.2

2002

654.8

333.3

988.0

2003

830.8

458.4

1,289.2

2004

987.6

528.4

1,516.0

Chanzo: Taasisi ya Utangazaji Tanzania .

 263. Hadi mwishoni mwa mwaka 2004, Taasisi iliweza kufikia asilimia 80 ya usikivu kwa upande wa radio kupitia mitambo yake 9 ya kurushia matangazo. Uwezo huu ulitokana na kukarabatiwa kwa mtambo wa Kunduchi. Aidha, urushwaji wa matangazo kwa njia ya televisheni ulifikia asilimia 40 baada ya kufungwa mitambo katika mikoa ya Dodoma, Arusha na Mwanza.

Jedwali Na. 16.6 : Vituo vya mitambo ya kurushia matangazo ya Radio na Televisheni.

Mtambo wa kurushia Matangazo.

Usikivu Kimikoa

Radio

Televisheni

Radio

Televisheni.

Dar-es-Salaam.

Dar-es-Salaam na Kisarawe

Dar es Salaam , Pwani, Morogoro na Tanga.

Dar es Salaam na Pwani

Dodoma

Dodoma

Dodoma na Singida.

Dodoma

Arusha

Arusha

Arusha na Kilimanjaro*

Arusha

Kigoma

 

Kigoma na Tabora*.

 

Mbeya

 

Mbeya na Rukwa*

 

Songea

 

Ruvuma na Iringa*.

 

Lindi

 

Lindi na Mtwara.

 

Mwanza

 

Mwanza, Shinyanga* na Kagera*.

Mwanza

Chanzo: Taasisi ya Utangazaji Tanzani a

 * Usikivu hauko eneo zima.

 Magazeti na Majarida

264. Magazeti na majarida yanayochapishwa hapa nchini huandaliwa kwa lugha ya Kiswahili na Kingereza. Hadi Desemba mwaka 2004, jumla ya magazeti na majarida 693 yalikuwa yamesajiliwa ikilinganishwa na 654 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 6.0. Asilimia 90.0 ya magazeti na majarida yote yaliyosajiliwa, husambazwa mijini na zaidi ya asilimia 50.0 husambazwa katika mkoa wa Dar-es-Salaam. Aidha, kati ya magazeti na majarida yaliyokuwa yamesajiliwa, 171 pekee ndiyo yalikuwa yakitolewa kwa kipindi kilichopangwa.

Jedwali Na. 16.7: Magazeti na Majarida yaliyosajiliwa Mwaka 1990 - 2004 .

Mwaka

Idadi

1990

213

1991

227

1992

242

1993

297

1994

321

1995

360

1996

397

1997

428

1998

449

1999

486

2000

528

2001

586

2003

654

2004

693

Chanzo: Idara ya Maelezo na Habari Tanzania .

Jedwali na 16.8: Vituo vya Radio vilivyosajiliwa kuanzia Mwaka 1994 hadi Mwaka 2004.

Kituo

Makao Makuu

Mitambo ya kurushia matangazo

Mwaka wa kutolewa kwa leseni.

Radio Tanzania

Dar es Salaam

Dar es Salaam , Dodoma, Mwanza, Arusha, Nachingwea, Lindi, Masasi, Songea, Kigoma

1994

PRT (Powerful Realistic Trustworth)

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1994

Radio One

Dar es Salaam

Dsm, Arusha, Mwanza, Dodoma, Moshi.

1994

Radio Tumaini

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1994

Radio Kwizera

Ngara

Kagera

1995

Radio Free Africa

Mwanza

Mwanza, Arusha, Shinyanga, DSM, Mbeya

1996

Radio Sauti ya Injili

Moshi

Moshi, Arusha, Same, Mlalo, Lushoto, Kibaya Simanjiro.

1996

Radio Maria

Songea

Songea

1996

Clouds Entertainment Radio FM.

Dar es Salaam

Dar es Salaam, Arusha, Mwanza

1998

Classic FM Radio

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1999

Radio 5

Arusha

Arusha

1999

Radio Chemichemi

Sumbawanga

Sumbawanga

1999

Radio Kiss FM

Mwanza

Arusha, Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya

2000

Radio Sky FM

Dar es Salaam

DSM,Moshi, Mwanza, Dodoma, Arusha

2000

Radio East Africa FM

Dar es Salaam

Dar es Salaam

2000

Radio Uhuru

Dar es Salaam

Dar es Salaam

2000

Radio Tumaini International

Dar es Salaam

Dar es Salaam

2001

Magic FM

Dar es Salaam

Dar es Salaam

2001

Radio Ukweli

Morogoro

Morogoro

2001

Radio Sauti FM

Nyegezi

Mwanza

2001

Aboob Radio

Morogoro

Morogoro

2001

Radio Faraja

Shinyanga

Ngokolo Shinyanga

2001

Radio Choice

Dar es Salaam

DSM

2002

Business Times Radio

Dar es Salaam

DSM

2002

Wapo Radio

Dar es Salaam

DSM

2002

Orkonekerei FM Radio

Manyara

Manyara

2002

Sunrise Radio

Arusha

Arusha

2002

Radio Mwangaza

Dodoma

Dodoma

2003

Radio Imaan FM

Morogoro

Morogoro

2003

Triple 'A' FM

Arusha

Arusha

2004

Victoria FM

Musoma

Mara

2004

Praise Power Radio

Dar es Salaam

Dar es Salaam

2004

Sibuka FM

Maswa

Shinyanga

2004

Chanzo: Taasisi ya utangazaji Tanzania.

 Jedwali na 16.9: Vituo vya televisheni vilivyosajiliwa kuanzia mwaka 1994 hadi waka 2004.

Kituo

Makao Makuu

Mitambo ya kurushia matangazo.

Mwaka wa kutolewa kwa leseni.

Coastal Television Network (CTN)

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1994

Dar es Salaam Television (DTV)

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1994

Independent Television (ITV)

Mikocheni Dar es Salaam

Dar es Salaam

1994

Sua Television

Morogoro

Morogoro

1995

Cable Entertainment Network-(CEN)

Dar es Salaam

Dar es Salaam

1997

Abood Television

Morogoro

Morogoro

1998

C2C Television

DSM

DSM

1999

Television Burudani (Arusha)

Kijenge

Arusha

1999

Television Burudani (DSM)

University Hill DSM

DSM

1999

Television Ya Taifa -(TVT)

DSM

DSM

2000

Dar-Es Salaam Television Pay TV (M-Net, Super Sport And Movie Magic)

DSM

DSM

2000

Channel 5

DSM

DSM

2000

Star TV

Mwanza

Mwanza

2000

Channel Ten Television

DSM

DSM

2002

Agape Television-(ATV)

Mbezi DSM

DSM

2002

Chanzo: Taasisi ya Utangazaji Tanzania.

   
Back Top