MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI | |||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Kilimo |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
MALIASILI
NA UTALII |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Ukuaji
wa sekta
191. Sekta ya maliasili inajumuisha sekta ndogo za misitu na nyuki, wanyamapori, na Uvuvi. Katika mwaka 2004, sekta ndogo ya misitu na nyuki ilikua kwa asilimia 4.0 ikilinganishwa na asilimia 4.2 mwaka 2003, na sekta ndogo ya uvuvi ilikua kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asilimia 6.4 mwaka 2003. Kupungua kwa kiwango cha ukuaji katika sekta ndogo ya misitu na nyuki kulitokana na kushuka kwa mazao ya misitu yaliyouzwa nje ya nchi, kwa sababu ya kudhibiti uuzaji wa magogo nje ya nchi. Aidha, kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji katika sekta ndogo ya uvuvi kulitokana na kuongezeka kwa mazao ya uvuvi yaliyouzwa katika soko la ndani. Misitu na Nyuki 192. Katika mwaka 2004, miche ya miti 78,621,948 ilikuzwa ikilinganishwa na miche 49,055,230 mwaka 2003, ikiwa ni ongezeko la asilimia 60.3. Kiasi cha hekta 7,061 zilipaliliwa na kazi ya kupunguza na kupogoa matawi zilifanyika katika hekta 2,310. Katika kutekeleza sera na sheria za misitu, misitu ya asili na mashamba ya miti yaliendelea kufanyiwa doria na kuwekewa mipaka na alama za kudumu za utambulisho. Mipango ya uhifadhi kwa vijiji 27 iliandaliwa katika misitu ya mikoko na ile ya asili kwa kuzingatia usimamizi shirikishi wa misitu. Upimaji na Uchoraji ramani za maeneo ya misitu ya asili ulifanyika katika vijiji 15 na utengaji maeneo ya ufugaji nyuki kwa vijiji 6 katika mikoa ya Singida, Tabora na Rukwa. Maandalizi ya kutenga maeneo ya misitu kwa ajili ya hifadhi yalifanyika kwa vijiji 46 katika wilaya ya Mufindi. 193. Mpango wa uendelezaji na uhifadhi wa misitu ulifanyika katika vijiji 10 chini ya Mradi wa Hifadhi Ardhi Dodoma (HADO). Upimaji wa hekta 33.2 za misitu wa hifadhi ya Geita ulifanyika na hesabu ya miti iliendeshwa katika misitu ya Lupilo. Aidha, misitu 9 ya hifadhi ilipimwa na kurekebishwa mipaka. Mipango ya uendelezaji wa misitu ya hifadhi ya Geita na Ilomelo ilitayarishwa. Wavamizi waliendelea kutolewa katika maeneo ya misitu ya Kazimzumbwi-Pugu. Hali kadhalika, katika mwaka 2004, jumla ya miti 139,934,591 ilipandwa katika mikoa yote nchini ikilinganishwa na miti 133,271,038 mwaka 2003. Kuongezeka kwa idadi ya miti iliyopandwa kulitokana na hali nzuri ya hewa ambapo mikoa mingi nchini ilipata mvua za kutosha. Uvunaji na Uuzaji wa Mazao ya Misitu na Nyuki 194. Katika mwaka 2004, magogo yenye mita za ujazo 759.6 yalivunwa katika msitu wa kupandwa wa Sao Hill ikilinganishwa na magogo ya mita za ujazo 4,556.3 katika mwaka 2003. Kupungua kwa idadi ya magogo yaliyovunwa mwaka 2004 kulitokana na udhibiti wa uuzaji wa magogo nje ya nchi. Mazao ya misitu na nyuki yaliyouzwa nje yalikuwa na thamani ya sh. 0.15 bilioni ikilinganishwa na sh. 7.2 bilioni zilizopatikana katika mwaka 2003. Wanyamapori 195. Katika mwaka 2004, miundombinu iliongezwa na kuboreshwa ili kuwezesha shughuli za utalii. Njia 5 za ndege (air strips) zilitengenezwa katika mapori ya akiba ya Mpanga-Kipengere, Rungwa-Kizigo-Muhesi, Ugalla na Usangu. Jumla ya kilometa 553 za barabara mpya zilitengenezwa ikilinganishwa na kilometa 85 mwaka 2003. Kilometa 956 za barabara zilikarabatiwa katika mapori ya akiba ya Mpanga-Kipengere na Usangu ikilinganishwa na kilometa 756 mwaka 2003. Kuongezeka kwa utengenezaji na ukarabati wa barabara kulitokana na kuimarishwa kwa vifaa vya ujenzi ikiwa ni pamoja na matengenezo na manunuzi ya mitambo mipya. 196. Katika kupambana na ujangili dhidi ya rasilimali ya wanyamapori na mazingira yao, jumla ya doria 17,523 ziliwekwa ndani na nje ya hifadhi ambapo idadi ya kesi za ujangili zilipungua hadi 321 ikilinganishwa na kesi 780 mwaka 2003. Mwaka 2004, kesi 122 zilimalizika na majangili 78 kufungwa jela. Aidha, doria za upelelezi na ukaguzi wa wafanyabiashara wa nyara za serikali ziliendeshwa ambapo nyara za serikali mbalimbali zilikamatwa. Nyara zilizokamatwa ni pamoja na meno ya tembo 48 na kilo 537 za vipande vya meno ya tembo; meno ya kiboko 1,272; ndege hai 7, na meno ya ngiri 2. 197. Katika mwaka 2004, waombaji 332 walipewa leseni za nyara ikilinganishwa na waombaji 388 mwaka 2003, ikiwa ni pungufu kwa asilimia 16.8. Ada za leseni hizo ziliingizia Serikali mapato ya sh. 141,325,000. Vile vile, mapato yatokanayo na rasilimali za wanyamapori yaliongezeka kwa kiwango cha sh. 1,591,024,463.4, sawa na asilimia 17.4, kutoka sh. 9,160,318,242.50 zilizokusanywa mwaka 2003 hadi sh.10,751,342,705.90 mwaka 2004. Ongezeko hili linatokana na kuongezeka kwa vibali vya kusafirisha nyara nje ya nchi, kukamata wanyamapori, na uwindaji wa kitalii. 198. Katika mwaka 2004, kulikuwepo na vitalu vya uwindaji 145, ikilinganishwa na 142 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 2.1. Biashara ya uwindaji wa kitalii iliingizia Taifa mapato ya dola 9.9 milioni mwaka 2004 ikilinganishwa na mapato ya dola 8.8 milioni mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 11.1. Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka kwa vibali vya kusafirisha nyara nje ya nchi na vibali vya kukamata wanyamapori. Uvuvi 199. Katika mwaka 2004, sekta ya uvuvi ilikua kwa asilimia 6.9 ikilinganishwa na asiimia 6.4 mwaka 2003. Kuongezeka kwa kiwango cha ukuaji kulitokana na kuongezeka kwa leseni za uvuvi katika ukanda wa bahari, na kuimarika kwa doria na udhibiti katika maeneo yenye rasilimali za uvuvi. Aidha, sekta hii iliweza kukusanya maduhuli ya jumla ya sh. 9,709,487,990.7 katika soko la ndani, ikilinganishwa na sh. 7,800,911,198.8 zilizokusanywa mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 24.5. 200. Mapato kutokana na mauzo ya mazao ya uvuvi nje yalishuka kutoka sh. 132,502,001,939 mwaka 2003 hadi sh. 121,898,147,693 mwaka 2004, sawa na upungufu wa asilimia 8. Katika kusimamia utekelezaji wa sera, sheria na kanuni za uvuvi, jumla ya kaguzi 715 kuhusu ubora wa samaki na mazao yake zilifanyika katika maeneo ya uvuvi, ikiwa ni pamoja na kufanyia uchunguzi sampuli 285 za minofu ya samaki. Aidha, wavuvi wadogo wapatao 237 na wafanyabiashara wadogo wapatao 37 walipatiwa mafunzo kuhusu sheria na kanuni mbalimbali za uvuvi. 201. Katika hatua ya kudhibiti uvuvi haramu, kanuni za uvuvi zilifanyiwa marekebisho baada ya Sheria ya Uvuvi Na. 22 ya mwaka 2003 kupitishwa na Bunge. Aidha, wavuvi wadogo katika Ziwa Victoria wamekuwa wakishirikishwa katika kudhibiti uvuvi haramu kwa kuanzisha vikundi vya ulinzi wa rasilimali za uvuvi. Kadhalika, jumla ya vipindi 5 vya redio na televisheni vya kuhamasisha jamii kuhusu uhifadhi na matumizi endelevu ya rasilimali za uvuvi, viliandaliwa katika mikoa ya Dodoma, Tanga na Morogoro. Utalii 202. Katika mwaka 2004, jumla ya watalii 582,807 walitembelea maeneo mbalimbali ya utalii ikilinganishwa na watalii 576,000 waliotembelea maeneo hayo mwaka 2003. Ongezeko hili la watalii limetokana na kuongezeka kwa jitihada za kutangaza utalii wa Tanzania nchi za nje, kushiriki katika maonyesho mbalimbali ya utalii ya kimataifa, kusambaza nyaraka mbalimbali zinazotangaza vivutio vya utalii na kutumia balozi zetu zilizoko nje ya nchi katika kutangaza vivutio vya utalii. Aidha, mapato yaliyotokana na biashara ya utalii yaliongezeka kutoka dola 731.0 milioni mwaka 2003 hadi dola 746.1 milioni mwaka 2004, sawa na ongezeko la asilimia 2.1. 203. Katika mwaka wa 2004, Bodi ya Utalii nchini (TTB) ilishiriki katika maonyesho saba nje ya nchi kama inavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 11.1. Jedwali Na.45(UPANDAJI WA MITI (MICHE ILIYOOTESHWA)) Jedwali Na. 11.1: Ziara za Maonyesho ya kuutangaza Utalii nje ya nchi kwa mwaka 2004
Chanzo:Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). 204. Bodi ya Utalii iliendelea kutangaza utalii ndani na nje ya nchi kwa kuandaa, kuchapisha na kusambaza ramani za maeneo ya vivutio vya utalii mbalimbali 15,000, vipeperushi 13,000, nakala za Filamu 20,000, majarida 124,000 ya Afrika halisi ni Tanzania na “Tanzania Conference Directory” 15,000. Aidha, Kongamano kuhusu Maendeleo ya Utalii Endelevu na Kuondoa Umaskini lililofanyika mjini Arusha na kuhudhuriwa na washiriki 162 kutoka katika nchi za Ethiopia, Gambia, Kenya, Lesotho, Mauritius, Msumbiji, Uholanzi, Swaziland, Uganda, Zimbabwe na Zambia. Utalii wa Mambo ya Kale 205. Katika mwaka 2004, sekta ya utalii wa mambo ya kale ilikusanya jumla ya sh. 187,085,567.06 ikilinganishwa na sh. 113,815, 776.10 mwaka 2003, sawa na ongezeko la asilimia 64.4. Ongezeko hili lilitokana na kuongezeka kwa idadi ya watalii wa ndani na nje waliotembelea maeneo ya mambo ya kale kama inavyoonyeshwa katika Jedwali Na. 11.2. Jedwali Na 11.2: Wageni waliotembelea Maeneo ya Makumbusho Nchini mwaka 2000 – 2004:
Chanzo: Wizara ya maliasili na Utalii Jedwali Na.47(MAUZO YA BIDHAA ZA MISITU NCHI ZA NJE) Jedwali Na.48(MWENENDO WA BIASHARA YA NDEGE, WANYAMAPORI NA VIPUSA NCHI ZA NJE) Jedwali Na.48A(MWENENDO WA BIASHARA YA WANYAMA HAI NA UWINDAJI WA KITALII) Jedwali Na.48B(IDADI YA WAWINDAJI (TOURIST HUNTERS)) Jedwali Na.49(MAUZO YA WANYAMA HAI NA PEMBE NCHI ZA NJE) Jedwali Na.50(UZALISHAJI KATIKA SEKTA YA UVUVI 1993-2004) Jedwali Na.51(MAUZO YA MAZAO YA UVUVI NCHI ZA NJE (2000-2003)) Jedwali Na.51A(MUHTASARI WA MAUZO YA MAZAO YA UVUVI NCHI ZA NJE - 1996-2004) Jedwali Na.51B(MWELEKEO WA MAUZO YA SANGARA NJE YA NCHI -1996-2004) Jedwali Na.52(IDADI YA WATALII, SIKU ZAO HOTELINI NA MAKADIRIO YA FEDHA ZA KIGENI ZILIZOPATIKANA) Jedwali Na.53(IDADI YA WATALII WALIOINGIA NCHINI NA KIASI CHA FEDHA ZILIZOPATIKANA (1990-2002)) Jedwali Na.54(SAFARI KATIKA HIFADHI ZA TAIFA) Jedwali
Na.55(NAFASI KATIKA HOTELI NA MATUMIZI YAKE+) |
|||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||