MAENDELEO YA UCHUMI JUMLA | UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | MAENDELEO KATIKA SEKTA MBALIMBALI |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| UENDELEZAJI WA SEKTA BINAFSI | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Uendelezaji
wa Sekta Binafsi |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
| MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA MKAKATI WA KUPUNGUZA UMASKINI | ||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||
Utangulizi
166. Mkakati wa Kupunguza Umaskini awamu ya kwanza ulitekelezwa katika kipindi cha miaka mitatu, 2000/01 – 2002/03 na ulilenga katika sekta zilizopewa kipaumbele (elimu, afya, maji, barabara vijijini, kilimo, UKIMWI, na mahakama na sheria). Mwaka 2004/05, serikali ilitenga kiasi cha sh. 1,473.0 bilioni kwa ajili ya matumizi katika sekta hizo, sawa na asilimia 44.0 ya makadirio ya matumizi yote ya serikali, ikilinganishwa na asilimia 44.5 ya matumizi halisi mwaka 2003/04. Mafanikio yaliyopatikana ni pamoja na kuboreshwa kwa huduma za kijamii (elimu ya msingi), na huduma za kiuchumi (barabara). Jedwali Na. 9.1: Matumizi ya Serikali Kuu katika sekta za kipaumbele, 1999/00 - 2004/05
Chanzo : Wizara ya Fedha Umaskini wa Kipato 167. Hali ya umaskini wa kipato nchini bado hairidhishi. Viashirio vya umaskini wa kipato vinaonyesha kuwepo kwa tofauti ya hali ya umaskini kati ya wakazi wa maeneo ya mijini na vijijini, na kati ya, na miongoni mwa wilaya na mikoa. Pamoja na kwamba matokeo ya Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya yalionyesha kupungua kwa kiwango cha wananchi wasioweza kupata huduma za msingi, bado idadi kamili inaongezeka kila mwaka. Matokeo hayo yanaonyesha kupungua kutoka asilimia 38.6 mwaka 1991/92 hadi asilimia 35.7 mwaka 2000/01. Hata hivyo, kwa mujibu wa makadirio ya matokeo ya Sensa ya Idadi ya Watu na Makazi ya mwaka 2002, viwango hivyo vinawakilisha idadi ya watu milioni 9.3 na 11.7, kwa mtiririko huo, sawa na ongezeko la wastani wa watu zaidi ya 200,000 kila mwaka. Pia, matokeo ya tafiti za vipindi hivyo viwili yanaonyesha kuongezeka kwa tofauti ya kipato kutoka 0.34 hadi 0.37 kwa mujibu wa Kipimo cha Ulinganifu wa Kipato (Gini-Coefficient). 168. Umaskini wa kipato una uhusiano na ukuaji wa uchumi katika sekta za uzalishaji na huduma. Mwaka 2004, Pato la Taifa lilikuwa kwa asilimia 6.7 ikilinganishwa na asilimia 5.7 mwaka 2003. Sekta ya kilimo ilichangia sehemu kubwa ya ukuaji huo. Kilimo kilikua kwa asilimia 6.0, kilichangia asilimia 46.4 ya Pato la Taifa, na asilimia 21.9 ya mapato yatokanayo na mauzo nje ikilinganishwa na asilimia 4.0, 46.7 na 19.5 kwa mtiririko huo mwaka 2003. Mbali na kutoa malighafi za viwandani na chakula, sekta hii hutegemewa na zaidi ya asilimia 80 ya wananchi, hivyo ufanisi katika sekta hii ni muhimu kwani matokeo yake yanawafikia wananchi walio wengi. Sekta nyingine zikiwemo za uzalishaji viwandani, madini, biashara pia zilikuwa na ongezeko la ukuaji mwaka 2004 ikilinganishwa na mwaka 2003. Hata hivyo, mafanikio ya ukuaji wa uchumi kwa ujumla, hayajaweza kuwafikia wananchi wengi. Hivyo, changamoto kubwa ni jinsi ya kuzifanya sekta hizo, kwa namna ya kipekee na kwa kushirikiana na sekta nyingine kuchangia katika kupunguza umaskini kupitia ongezeko la kasi ya uzalishaji, ufanisi na tija. Umaskini Usio wa Kipato Elimu ya Msingi 169. Katika miaka mitatu ya Utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini, viashirio vingi vya elimu ya msingi vimekuwa na maendeleo makubwa kufuatia utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa Elimu ya Msingi (MMEM). Kiwango cha jumla cha uandikishwaji kiliongezeka kutoka asilimia 105.3 mwaka 2003 hadi kufikia asilimia 106.3 mwaka 2004. Kiwango halisi cha uandikishaji kiliongezeka kufikia asilimia 90.5 mwaka 2004 kutoka asilimia 88.5 mwaka 2003. Aidha, uwiano wa wasichana katika shule za msingi umeongezeka kufikia asilimia 48.8 ya wanafunzi wote mwaka 2004, kutoka asilimia 48.7 mwaka 2003. Kiwango cha wanafunzi wanaoingia kidato cha kwanza kimeongezeka kutoka asilimia 21.7 mwaka 2002 hadi kufikia asilimia 30.1 mwaka 2003, kutokana na kuongezeka kwa shule mpya za sekondari na kuanza kwa utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Sekondari (MMES). Aidha, kiwango cha kukatisha masomo kimeshuka kutoka asilimia 4.7 mwaka 2003 hadi asilimia 3.75 mwaka 2004 hasa kutokana na kuboreshwa kwa mazingira ya kufundishia na kujifunzia. Jedwali Na. 9.2: Sehemu (Asilimia) ya Wanafunzi Wanaomaliza Darasa la Saba na Kuingia Kidato cha Kwanza (1990 - 2003)
Chanzo: Wizara ya Elimu na Utamaduni
170. Pamoja na mafanikio hayo katika elimu ya msingi, bado changamoto kubwa imebaki juu ya kuinua ubora wa elimu na kuongeza idadi na ujuzi wa walimu ili kukidhi upungufu uliojitokeza kufuatia kuongezeka kwa wanafunzi, madarasa na shule za msingi. Changamoto hiyo inajidhihirisha katika wastani wa uwiano wa mwalimu na wanafunzi ambao umeendelea kuongezeka toka 1:57 mwaka 2003, hadi 1:58 mwaka 2004, ikilinganishwa na kiwango cha kimataifa ambacho ni 1:45. Afya 171. Kwa mujibu wa Utafiti wa Kipato na Matumizi ya Kaya wa mwaka 2000/01, asilimia 91.4 ya wananchi wanaishi umbali wa kilometa chini ya kumi kutoka kilipo kituo cha huduma za afya na asilimia 75.4 wanaishi umbali wa kilometa chini ya 6. Pamoja na hali hiyo, watu wengi, hususan, wanawake na watoto hufa hata kabla ya kufika kwenye vituo vya afya. Watoto 8 kati ya 10 wanafia nyumbani na 6 kati yao hufa bila hata kupata huduma za matibabu kwenye vituo vya afya. Karibu asilimia 90 ya vifo vya watoto hutokana na magonjwa yanayoepukika kama vile malaria, utapiamlo, UKIMWI, na kuharisha. Uwiano wa huduma za uzazi zinazotolewa na wataalam wa afya na katika vituo vya afya umepungua na hii iliendelea kuathiri vifo vya mama na watoto. Malaria iliendelea kuwa ugonjwa unaoongoza kwa vifo vingi, karibu asilimia 17 ya vifo vyote mwaka 2004. 172. Pamoja na kupiga hatua katika kupambambana na tatizo la upungufu wa lishe, utapiamlo uliendelea kuwa mkubwa, na hivyo kuathiri hali za afya za watoto hususan walio chini ya miaka mitano. Tofauti ya lishe duni pia imejitokeza kati ya maeneo ya mijini na vijijini na kati ya watoto wanaotoka katika kaya maskini na tajiri. Kutokana na ukosefu wa lishe bora, asilimia 44 ya watoto wana kimo pungufu kuliko umri wao, asilimia 5 ya watoto wamedumaa, na asilimia 29 wana uzito mdogo usioendana na umri wao. Hali hii inafanya uwezekano wa kufikia malengo ya MKUKUTA ya kupunguza viwango hivyo kwa zaidi ya asilimia 50 mwaka 2010 kuwa mgumu. Kwa ujumla, utoaji wa huduma bora za afya umekuwa ukikabiliwa na matatizo ya miundombinu, upungufu wa wataalam wa afya, uwezo mdogo wa usimamizi na gharama kubwa za uendeshaji. Maji 173. Katika mwaka 2004, kulikuwepo na ongezeko la usambazaji wa huduma ya maji mijini na vijijini. Hata hivyo, sehemu kubwa ya wananchi walikuwa hawapati maji safi na salama. Asilimia 46.5 ya wakazi wa vijijini na 26 ya wakazi wa mjini walikuwa wanatumia maji kutoka katika vyanzo visivyo salama mwaka 2004, ikilinganishwa na asilimia 47 na 26 kwa mtiririko huo mwaka 2003. Pamoja na kuongezeka kwa usambazaji, wakazi wa mijini, hususan, maskini wanakabiliwa na gharama kubwa za kuweza kupata huduma za maji. Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) 174. Katika mwaka 2003/2004, serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali ilifanya mapitio ya kina ya miaka mitatu ya utekelezaji wa awamu ya kwanza ya Mkakati wa Kupunguza Umaskini (MKU). Wiki ya Umaskini iliyofanyika kuanzia Novemba 1, 2004 ilihitimisha zoezi hilo. Mapitio hayo yalionyesha juhudi zaidi zinahitajika kuongeza na kuboresha huduma za kiuchumi na kijamii ili kupata matokeo yalio bora katika azma ya kupunguza umaskini kwa wananchi wengi. Katika dhamira ya kuwezesha kupata mafanikio zaidi na endelevu katika kukuza uchumi na hatimaye kupunguza umaskini, Mkakati mpya, unaoitwa Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA) umeandaliwa na utatekelezwa katika kipindi cha miaka mitano (2005/6 – 2009/10). 175. Maandalizi ya Mkakati huu yalifanyika kwa kuzingatia tafiti mbalimbali za uchambuzi na maoni kutoka kwa wananchi. Mkakati huu ni mpana zaidi ya uliopita kwa kuhusisha sekta zote na wadau wote wa maendeleo na umelenga katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2025 na Malengo ya Kimataifa ya Milenia. MKUKUTA umeweka kipaumbele katika matokeo ya maeneo makuu matatu: ukuzaji wa uchumi na kupunguza umaskini wa kipato; kuinua ubora wa maisha na ustawi wa jamii; na utawala bora na uwajibikaji. Changamoto kubwa iliyopo ni utekelezaji wa MKUKUTA wenye upeo mpana zaidi tofauti na kuangalia sekta za kipaumbele kama ilivyokuwa kwa mkakati wa awamu ya kwanza. |
||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||||