| .
Uendelezaji
kilimo ni lengo kuu la Taifa. Mkazo umewekwa kwenye uzalishaji wa
chakula na kupunguza umaskini.
Kwa
miaka mingi uzalishaji wa chakula nchini umeshindwa kutimiza
mahitaji ya chakula, na hivyo kusababisha uagizaji kutoka nje na
misaada ili kufidia pengo. Kwa
maana hiyo, Serikali imeruhusu masoko huria masoko na bei.
Sekta
binafsi inasaidiwa ili izalishe chakula, upatikanaji wa pembejeo
na shughuli za masoko. Serikali inatumia mikakati ifuatayo: -
¨
Uboreshaji wa vivutio katika
kurahisisha chakula kwa kukuza uuzaji nje wa mazao yasiyo asilia
na yale ya chakula kwa kuufanya huria mfumo wote.
¨
Kusaidia utafiti na ugani na
kuboresha ufanisi, kukuza ushiriki wa sekta binafsi katika
uzalishaji, usindikaji, uhifadhi, pembejeo na masoko.
¨
Kuboresha miundombinu vijijini.
¨
Kukuza biashara ya mipakani kwa
nchi majirani na uuzaji nje.
¨
Kuzuia upotevu wa chakula baada
ya uvunaji.
¨
Kufuatilia mara kwa mara na
kutathmini hali ya chakula vijijini kwa kupitia utaratibu na mfumo
mzima wa utoaji tahadhari mapema na ufuatiliaji mazao.
¨
Kupitia sheria zinazoathiri
ushirikishwaji wa sekta binafsi kwenye kilimo na masoko katika
sekta ya kilimo.
¨
Kuondoa vikwazo vya biashara
katika ngazi ya taifa, mikoa na wilaya; na kurekebisha sheria
zinazotawala usafirishaji wa chakula kuvuka mipaka ya wilaya,
mikoa na nchi.
¨
Kuunda upya Hifadhi ya Taifa ya
Akiba ya Nafaka ili ifanye kazi kwa ufanisi na tija.
Sekta
binafsi inashiriki katika kununua chakula kutoka kwa wakulima, na
pia kuagiza chakula kutoka nje ya nchi. Kampuni binafsi ni pamoja
na: -
¨
Mohamed Enterprises
¨
EECO Traders
¨
Mbutano Investment
¨
Andre & CIESA
¨
Sky Coach
Masoko ya Kilimo:
Tanzania
bado inategemea uuzaji wa mazao asilia nje, ila inakabiliwa na
tatizo la mabadiliko ya bei katika soko la dunia na kuzorota kwa
biashara katika sekta ya kilimo. Mkakati wa kuuza nje umelenga
katika kuuza mazao tofauti na wakati huo kuhakikisha ubora wa hali
ya juu, na kuyapa thamani zaidi kwa kuyasindika. Soko la mazao ya
kilimo, mifugo na pembejeo limefanywa huria. Makampuni binafsi na
vyama vya ushirika hushiriki kwa viwango tofauti.
Mwitiko
wa sekta binafsi kwa fursa zilizojitokeza kutokana na kuachia
uchumi uwe huria na ubinafsishaji umekuwa mkubwa. Hisa za sekta
binafsi katika masoko ya mazao mbalimbali zimekuwa kubwa. Biashara
yote ya mazao ya chakula inaendeshwa binafsi isipokuwa shughuli za
Hifadhi ya Taifa ya Nafaka.
Tasasi za Sekta Binafsi:
Asasi
kadhaa binafsi zimeanzishwa, zikishughulika na ununuzi wa mazao ya
chakula na biashara, pamoja na pembejeo kwa wakulima. Ni pamoja
na: -
¨
Chama cha Walimaji wa Kahawa
Tanzania,
¨
Chama cha Pamba Tanzania,
¨
Chama cha Korosho Tanzania,
¨
Chama cha Chai
Tanzania,
¨
Chama cha Mkonge, Tanzania,
¨
Chama cha Walimaji Maua Tanzania,
Kuna
tasasi binafsi za jumla zinazowakilisha biashara binafsi na kuwa
na mkabala wa pamoja katika kuwasiliana na kuzungumza na serikali
kuhusu maendeleo ya sekta binafsi. Hizi ni: -
¨
Chama cha Biashara, Viwanda na
Kilimo, (TCCIA)
¨
Shirikisho la Viwanda Tanzania,
(CTI)
¨
Taasisi ya Sekta Binafsi
Tanzania, (TPSF)
Baraza la Taifa la Biashara
|