Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Mwanzo Serikali

Sehemu hii inakupa taarifa za kuwezesha kuijua serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mamlaka iliyonayo katika kuongoza. Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni nchi moja yenye Bunge la demokrasia ya vyama vingi. Mamlaka yote ya dola katika Jamhuri ya Muungano yanafanywa na kudhibitiwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar. Kila Serikali Kuu ina mihimili mitatu: Mtendaji Mkuu; Mahakama na Baraza la Kutunga Sheria, yenye mamlaka ya kufanya mambo ya umma. Aidha Mamlaka za Serikali za Mitaa husaidia kila Serikali Kuu.

Sehemu hii inaeleza kwa muhtasari vipengele mbalimbali vya serikali, viongozi wa mihimili mikuu, sera, nyaraka, sheria na kanuni zinazoongoza utumishi wa umma, ajira ikiwemo haki na wajibu wa watumishi, mipango ya maendeleo inayowalenga wananchi, bajeti za serikali kila mwaka kutoka Wizara ya Fedha na wizara nyingine, takwimu za fedha, idadi ya watu na habari za matukio ya hivi karibuni kutoka wizara mbalimbali kwa njia ya vijarida mtandao.

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 06:00:00

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page