Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliBunge

Baraza la Kutunga Sheria au Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lina sehemu mbili, yaani Rais na Wabunge. Rais anatekeleza madaraka yote aliyokabidhiwa na Katiba kwa kuridhia miswada ya sheria ya bunge ili kukamilisha mchakato wa kutunga sheria kabla ya kuwa sheria.

Sehemu hii inakupa taarifa kamili kuhusu bunge ambalo ndicho chombo kikuu cha Jamhuri ya Muungano ambacho kina madaraka kwa niaba ya wananchi, kusimamia na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano na vyombo vyake vyote katika utekelezaji wa majukumu yake. Bunge lina aina nne za wabunge, yaani:Wabunge waliochaguliwa moja kwa moja kuwakilisha majimbo ya uchaguzi Tanzania Bara na Zanzibar; Wabunge watano waliochaguliwa na Baraza la Wawakilishi kutoka miongoni mwa wajumbe, Mwanasheria Mkuu; Wabunge wasiozidi kumi walioteuliwa na Rais na wabunge wanawake wasiopungua 15% ya makundi mengine yote kwa msingi wa uwiano wa uwakilishi miongoni mwa vyama vilivyomo katika Bunge. Kwa taarifa zaidi tembelea  Bunge la Tanzania 

Kazi za Bunge Kamati za Bunge
Wajibu wa Katibu wa Bunge Historia
Muundo wa Bunge Wabunge
Maswali na Majibu Mwendelezo wa Vikao vya Bunge
Ufuatiliaji wa Miswada ukaguzi wa kazi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 13:00:54
Kufaa
4.4
17 Jumla
Inafaa Sana 11
Inafaa Kiasi 3
Sina Hakika 2
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 1
Urahisi wa kutumia
4.5
11 Jumla
Rahisi Sana 6
Rahisi Kiasi 4
Sina Hakika 1
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page