Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoFedha

Sekta ya fedha nchini Tanzania imepitia mabadiliko mengi ya muundo tangu program ya Tathmini ya Sekta ya Fedha (FSAP) ya mwaka 2003. Rasilimali za sekta ya fedha zimeongezeka haraka sana, kutokana na ukuaji wa mikopo ya sekta binafsi. Hali hii imeongeza taasisi za ukopeshaji fedha , na hivyo huzidi kusaidia ukuaji wa uchumi. Utekelezaji wa marekebisho ya sekta ya fedha ya kizazi cha pili, iliyotumia kiasi fulani cha mapendekezo ya FSAP ya mwaka 2003, umeimarisha maendeleo haya .

Sekta ya benki nchini Tanzania ilianzisha mpango wa ulegezaji masharti ya fedha mwaka 1992 ili kumudu ukuaji wake wa uchumi. Mpango huu ulitimizwa kwa utafutaji wa fedha pamoja na kuongeza ushindani katika soko la fedha na kuzidisha ubora na ufanisi wa fedha za mikopo. Kutokana na ulegezaji masharti huko, sekta ya benki nchini Tanzania imeendelea kukua sana hasa katika kipindi cha miaka michache iliyopita kutokana na hali hiyo kumejitokeza benki za wafanya biashara, benki za biashara, maduka ya kubadilisha fedha za kigeni, kampuni za bima, masoko ya hisa na taasisi za fedha nyingine kwenye soko.

Maendeleo makubwa yamefikiwa katika kufungamanisha mfumo wa sheria, kuimarisha usimamizi wa benki kuwa Mpango wa Uendelezaji wa Biashara (BCP): Kuipa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) mamlaka ya kutosha ya kutekeleza madaraka yake kama mamlaka yenye wajibu wa kutoa leseni, kusimamia na kudhibiti shughuli za tasnia ya benki 18. Utoaji leseni hivi sasa hufanywa na Benki Kuu peke yake kuepuka kuingiliwa na siasa na upitiaji mbinu ya kina na mahiri inayofanywa na Benki kuu. Ili kuimarisha uchunguzi wa nje ya kituo cha kazi, benki zote zinazowajibika kwa Benki Kuu zimeunganishwa kwa mitambo inayojiendesha yenyewe na kupatikana kwenye Mfumo wa Usimamizi  wa Taarifa za Benki  (BSIS). Sehemu ya fedha ikiwemo vyombo vinavyosimamia na kudhibiti fedha, taasisi za benki, bima, mifuko ya pensheni, wakala za serikali na taasisi za mafunzo. Kwa maelezo zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Fedha na Benki Kuu ya Tanzania

Mamlaka za Usimamizi Taasisi za Kibenki
Bima Shirika la Changamoto ya Milenia
Taasisi za Mafunzo Wizara ya Fedha
Utaratibu wa Kudhibiti Madeni Tanzania Dira ya Maendeleo ya Tanzania 2025
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-11-26 10:40:36
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page