Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiKilimo

Nchini Tanzania, Sekta ya Kilimo ni muhimili wa maendeleo ya uchumi. Sekta hii inachangia kiasi cha nusu ya pato la Taifa, robo tatu ya bidhaa zinazouzwa nje ya nchi na chanzo cha chakula pamoja na utoaji wa fursa za ajira zaidi ya 75% ya Watanzania. Kilimo kina uhusiano na sekta zisizo kuwa za kilimo kupitia uhusiano wa usafishaji kwenda kwenye usindikaji wa mazao ya kilimo, matumizi na uuzaji nchi za nje;Inatoa malighafi kwa viwanda na soko kwa bidhaa zilizotengenezwa. Tanzania inazalisha takribani 97% ya mahitaji yake ya chakula. Uzalishaji wa mazao ya chakula unatofautiana mwaka hadi mwaka kutegemea kiasi cha mvua kilichopatikana.

Maendeleo ya kilimo yamekuwa chini ya Serikali/fedha za umma kwa kipindi kirefu. Hata hivyo marekebisho ya uchumi kwa jumla yamekuwa na yanaendelea kuwa na matokeo ya muhimu kwenye sekta ya kilimo. Marekebisho ya kiuchumi yamesababisha kufunguka sekta hiyo kwa uwekezaji binafsi katika uzalishaji na usindikaji , uagizaji pembejeo za kutoka nchi za nje na usambazaji na masoko ya kilimo. Serikali imebaki na kazi ya usimamizi na usaidizi wa umma na dhima ya uwezeshaji.

Taarifa  iliyojumuishwa kwenye  sehemu hii itakusaidia mwananchi kuelewa kuhusu upimaji wa udongo na rutuba, uhifadhi, masoko na upangaji wa bei, ulishaji wa mifugo, mbolea na viuatilifu, taratibu bora kwenye kilimo cha kutumia mbolea ya asili, ufugaji wa nondo wa hariri, kilimo cha bustani, ufugaji wa samaki, kilimo cha maua na namna ya kupata mikopo ya kilimo na ruzuku. Kwa taarifa zaidi tembelea  Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika 

Utafiti kilimo Mafunzo ya Kilimo
Uendelezaji wa Mazao Kilimo cha Bustani
Huduma za Afya ya Mimea Huduma za Ugani za Kilimo
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 15:21:12
Kufaa
4.0
15 Jumla
Inafaa Sana 9
Inafaa Kiasi 2
Sina Hakika 1
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 2
Urahisi wa kutumia
4.4
12 Jumla
Rahisi Sana 7
Rahisi Kiasi 4
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 1
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page