Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiAjira

Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025,inatia moyo na kuongeza matumaini ya Taifa ya kupata ukuaji mkubwa wa kiuchumi na ajira kukidhi mahitaji na matarajio ya Watanzania wote. Hii imeimarisha ari ya kujenga uchumi imara wa aina mbalimbali na wa ushindani utakaotoa fursa za ajira za kutosha na endelevu nchini Tanzania. Sera ya Ajira ya Taifa inayokusudia kuchochea ukuaji wa ajira wa kutosha katika uchumi wetu, ili kupunguza ukosefu wa ajira na viwango vidogo cya kuajiri na hatimaye kupata ajira kamili yenye uzalishaji na inayofaa kwa Watanzania wote. Dira ya jumla ya Sera ya Ajira ya Taifa ni kuwa na jamii inayoshiriki katika kazi inayofaa inayoweza kuzalisha kipato cha kutosha kukimu na kupunguza umasikini kama ilivyotarajiwa katika Dira ya Maendeleo ya Taifa ya 2025, Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umasikini wa Taifa ( MKUKUTA ) pamoja na kukabili changamoto za tofauti za Soko la Ajira katika  uchumi wa utanda wazi.

Uongezaji wa Ajira ni suala lenye upana mkubwa linalowahusisha Watanzania wote, Wizara za Serikali, Idara  na Wakala( MDA), Mamlaka za Mikoa na Wilaya, Sekta Binafsi, Vyama vya waajiri na vya wafanyakazi, Wabia wa Maendeleo na Asasi Zisizo za Serikali (AZISE) na Asasi za Kiraia za aina mbalimbali.Kwa kuwa, Soko la Ajira linahusu ongezeko kubwa la wanafunzi wanaomaliza shule, wahitimu wa vyuo na watu wazima wasiopata ajira kwenye sekta rasmi.Sehemu hii inakupa taarifa muhimu zitakazokusaidia kujua mfumo wa ajira na taasisi pamoja na vyombo vinavyohusika na ajira.Kwa taarifa zaidi tembelea  Wizara ya Kazi na Ajira . 

Wakala wa Huduma za Ajira Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma
Tume ya Usuluhishi
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 16:54:44
Kufaa
4.5
14 Jumla
Inafaa Sana 10
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 3
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
4.4
11 Jumla
Rahisi Sana 8
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 2
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page