Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo WananchiMakazi

Uendelezaji wa nyumba nchini Tanzania kwa kiasi kikubwa hufanywa na sekta binafsi. Kumekuwa na jitihada za Serikali za kuendeleza sekta ya nyumba tangu  uhuru. Juhudi hizo ni pamoja na uundwaji wa Shirika la Nyumba la Taifa Mwaka 1962. Shirika hili lilikuwa na wajibu wa kupunguza upungufu wa nyumba katika maeneo ya mijini. Benki ya Nyumba Tanzania iliyokufa ilianzishwa mwaka 1972 kutoa mikopo ya ujenzi wa nyumba na ukarabati wa nyumba katika maeneo ya makazi yasiyo rasmi yaliyoboreshwa. Katika miaka ya hivi karibu Serikali imekuwa ikifanya juhudi za uwezeshaji kwa kuweka mazingira yanayowezesha kwa sekta binafsi, mtu mmoja mmoja na taasisi nyingine kushiriki katika uendelezaji wa nyumba.

Uendelezaji wa nyumba unaongozwa na Sera ya Maendeleo ya Makazi ya Mwaka 2000. Katika utekelezaji wa Sera, Idara imeandaa mpango wa Ujenzi wa Nyumba wa Taifa ulioidhinishwa hivi karibuni. Idara hiyo pia ina wajibu wa kusimamia uendelezaji wa nyumba bora nchini kwa kushirikiana na Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa UN-HABITAT. Kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha, imetayarishwa ripoti itakayowezesha kuanzishwa kwa mikopo ya uendelezaji nyumba. Inatarajiwa kwamba taasisi kama vile PPF, NSSF na nyingine zitahimizwa kutoa mikopo ya nyumba ya masharti nafuu kuwawezesha watu wenye kipato kidogo kujenga nyumba bora.

Wizara kupitia sehemu hii kwa kushirikiana na Shirika la Nyumba la Taifa inapitia upya Sheria Na. 2 ya Mwaka 1990 kuwezesha Shirika la Nyumba kukusanya mapato kutoka nyumba zilizopo na kulimbikiza mtaji ili kuongeza ufanisi wa uendelezaji wa nyumba. Serikali ina mpango wa kuimarisha sehemu hii kuwa idara kamili na kufungua ofisi kwenye mamlaka za Serikali za mitaa zote. Aidha Serikali ina mpango wa kuanzisha kikosi cha ujenzi wa nyumba na ushiriki wa ujenzi wa nyumba katika wilaya zote kuharakisha ujenzi wa nyumba bora Tanzania. Sehemu hii inakupa taarifa mbalimbali zinazohusu jitihada na mipango mbalimbali ya utekelezaji ya Serikali katika kuboresha huduma za nyumba. kwa taarifa zaidi tembelea tovuti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Makazi na Shirika la Nyumba la Taifa.

 

NHBRA NHC
TBA
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 18:28:16
Kufaa
3.7
3 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 1
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
3.5
2 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 1
Sina Hakika 1
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page