Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo SerikaliMatokeo Makubwa Sasa

Kama sehemu ya juhudi ya kuitoa nchi kutoka kwenye kipato cha chini kwenda kipato cha kati,kuanzia mwaka wa fedha wa 2013/2014, kwa msaada wa wabia wa maendeleo, Tanzania inatekeleza mpango wa Matokeo Makubwa Sasa; kwa kutumia mfumo wa maendeleo uliopata mafanikio makubwa nchini Malaysia.

Mfumo kabambe wa utekelezaji wa maendeleo, ulioelezwa kuwa una ukuaji wa haraka unaotokana na wananchi “marathoni” unazingatia maeneo sita ya kipaumbele yaliyoelezwa katika dira ya maendeleo ya Taifa ya 2025: nishati na gesi asilia, kilimo, maji, elimu, usafirishaji na utafutaji wa rasilimali. Matokeo Makubwa Sasa ulizinduliwa na Rais Kikwete, Februari, 2013. Mafunzo ya wiki 8 yaliyoongozwa na wataalamu wa sera wa Malaysia yalitumia uzoefu wa kitengo cha utendaji wa Menejimenti na utoaji huduma kupanga na kutekeleza mfumo utakaofaa kwa Tanzania.

Ili nchi ipate kipato cha kati ifikapo mwaka 2025, ni muhimu kwamba upangaji wa maendeleo usiwe tena mchakato wa siri kwa watendaji wakuu peke yao na kwamba wananchi washirikishwe kwa ukamilifu katika kujifunza kuhusu mipango ya maendeleo na kutoa michango yao itakayozingatiwa. Uwazi na ufanisi ni dhana zinazoongoza na upunguzaji wa rushwa utakuwa muhimu sana.

Usimamiaji wa utelekezaji wa Matokeo Makubwa Sasa ni jukumu la kitengo cha utoaji huduma (kilichopo Ofisi ya Rais). Chombo hiki kinawakutanisha wataalamu na wadau muhimu wanaoamua na kukubaliana kuhusu vipaumbele na kuviboresha ili viweze kutekelezeka. Mara nyingi udhaifu wa mara kwa mara umesababisha vipaumbele vya Tanzania kupuuzwa; Matokeo ya Haraka Sasa inakusudiwa kuhakikisha kuwa kuna mabadiliko ya mwenendo huo wa zamani, kwa kutayarishwa taratibu zitakazohakikisha kuwa viongozi wa ngazi za juu wa serikali wanashughulikia vipaumbele kwa uthabiti zaidi na kuonyesha matokeo na kutimiza malengo yaliyowekwa. Sehemu hii inakupa taarifa kuhusu sekta sita za kipaumbele za mpango wa Matokeo Makubwa Sasa.

Vipaumbele Matokeo
Shughuli Makusudio
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2016-01-01 09:39:36
Kufaa
4.0
2 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 1
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
3.0
1 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 1
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page