Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoNishati

Uwiano wa nishati nchini Tanzania umeelemea zaidi katika matumizi ya mkaa na kuni, ambayo ndio chanzo kikuu cha nishati kwa maeneo ya mijini na vijijini. Matumizi ya mkaa na kuni ni  zaidi ya 90% ya mahitaji ya msingi ya nishati. Vyanzo vya nishati ya kibiashara kama vile petroli  na umeme ni asilimia 8 na asilimia 1.2 mtawalia, ya nishati ya msingi inayotumika. Makaa ya mawe, nishati ya jua na ya upepo ni chini ya asilimia moja ya nishati inayotumika.

Vyanzo vingine vya nishati asilia, vinavyoweza kutumiwa kukidhi mahitaji ya nishati yanayoongezeka ni pamoja na uzalishaji umeme kwa njia ya maji, makaa ya mawe, gesi asilia, urani, nishati ya jua, upepo na nishati ya jotoardhi. Uzalishaji umeme kwa njia ya maji una uwezo wa kuzalisha 4.7GW, mlimbiko wa makaa ya mawe unakadiriwa kuwa tani milioni 1,200, ambapo tani milioni 304 zimethibitishwa. Gesi asilia nayo inakadiriwa kuwa mita za ujazo bilioni 45.  

Tanzania inaendelea kutegemea bidhaa za petroli kutoka nje. Uzalishaji wa umeme unategemea zaidi nguvu za maji, hali ya kuwa mitambo ya uzalishaji umeme kwa mafuta huzalisha umeme wakati wa matumizi makubwa. Uzalishaji umeme kwa kutumia gesi asilia unaendelea kwa kasi. Usambazaji wa teknolojia za nishati jadidifu umekuwa wa kiwango kidogo kwa kutumia tu majiko sanifu, mbinu za kisasa za uzalishaji mkaa, jua,  bayogesi na upepo na kwa kiwango kidogo umeme mwanga. Jitihada za kuongeza matumizi ya makaa ya mawe kwa uzalishaji wa umeme zinaendelea. 


 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2016-12-13 07:33:21
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page