Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo Mambo ya NjeUhusiano wa Kimataifa

Tanzania ina uhusiano mzuri na majirani wake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa mshiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhilishi wa migogoro kwa njia ya amani. Tanzania ni mwanachama wa vikundi vya kimataifa na kikanda pia inashiriki kwa dhati katika ushirikiano wa baina ya nchi na ushirikiano wa kimataifa. Tanzania pia ilisaidia mazungumzo ya amani kumaliza mgogoro nchini Burundi na kuunga mkono makubaliano ya Lusaka kuhusu mgogoro wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Tanzania pia imetoa mchango mkubwa katika kuhifadhi wakimbizi wa kutokea nchi za jirani ikiwemo Msumbiji, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi na Rwanda. Mwezi Machi 1996, Tanzania, Uganda na Kenya zilifufua mazungumzo ya kiuchumi na ushirikiano wa kikanda. Mazungumzo haya  yamesababisha kutiwa saini kwa Mkataba wa Ushirikiano wa Afrika Mashariki, mwezi Septemba, 1999 ambao baada ya muda utasaidia ushirikiano wa kiuchumi kupitia kuanzishwa kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki.

Mahali pa kuanzia Jumuiya ya Afrika Mashariki ni kuanzishwa kwa Umoja wa Forodha na Soko la Pamoja ambapo mikataba ya uanzishaji inatarajiwa kukamilishwa ndani ya kipindi cha miaka minne kuanzia Novemba 1999: Hatua nyingine zaidi ya ushirikiano ni kuanzishwa kwa Umoja wa Fedha ambao hatimaye utaleta Shirikisho la Kisiasa. Jumuiya ya Afrika Mashariki inakusudia kuimarisha ushirikiano wa kiuchumi wa nchi hizi kwa msingi wa kuchagua na kutenda, ikiwemo uwezeshaji wa biashara kupitia uwianishaji wa ushuru wa forodha, malipo, uchukuzi, kusafiri kwa watu na uwianishaji wa maeneo mengine yenye maslahi kwa wote kama vile, nyanja za siasa, jamii na utamaduni.

Tanzania ni nchi pekee ya Afrika Mashariki iliyo mwanachama wa Jumuiya ya Maendeleo ya Kusini mwa Afrika (SADC) tangu ilipoanzishwa mwanzoni mwa miaka ya 1980. SADC ni jumuiya ya nchi 13 ambazo ni Angola, Botswana, Lesotho, Malawi, Mauritius, Msumbiji, Namibia, Afrika Kusini, Swaziland, Tanzania, Zambia, Zimbabwe na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo. Nchi Wanachama wa SADC  wameridhia mkataba wa Biashara (25 Januari 2000) wenye lengo la kuanzisha eneo la biashara huru kwa ajili ya kutoa uhuru zaidi wa biashara ya bidhaa na huduma baina ya nchi za SADC na utumiaji wa sheria za biashara zinazohusika (kutoeneza bidhaa hafifu, ruzuku, ushuru unaopingana na hatua za kulinda).

Kipengele hiki kinaelezea Tanzania ilivyokuwa na uhusiano mzuri na jirani zake, Sera ya Mambo ya Nje ya Tanzania, Ushirikiano Baina ya Nchi, Hati za Makubaliano na nchi zingine, makubaliano ya kimataifa pamoja na Tanzania katika Umoja wa Mataifa ikizingatia Tanzania ina uhusiano mzuri na majirani zake na katika miaka ya hivi karibuni imekuwa ikishiriki kwa ukamilifu katika juhudi za kuhimiza usuluhishi wa migogoro kwa njia ya amani.

Sera ya Mambo ya Nje Tanzania katika Umoja wa Mataifa
Makubaliano ya Kimataifa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-02 06:46:46
Kufaa
4.8
4 Jumla
Inafaa Sana 3
Inafaa Kiasi 1
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
5.0
4 Jumla
Rahisi Sana 4
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page