Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoUchukuzi

Sekta ya Uchukuzi inatoa mchango mkubwa katika shughuli za kila siku za maendeleo ya uchumi. Ni miongoni mwa mihimili ya uchumi na uwekezaji katika sekta hii una manufaa makubwa sana katika uchumi wote. Ni mwezeshaji mkubwa wa sekta za uzalishaji, biashara na utawala inayohusisha ugavi na usambazaji wa bidhaa na huduma kwenda na kutoka kwenye soko la ndani na la kimataifa.

Kwa kuwa biashara inahusisha usafirishaji wa bidhaa na huduma kwenda na kutoka kwenye soko, bila shaka mfumo wa uchukuzi uliowianishwa kwa ukamilifu, ulioendelezwa, uliosalama, wa kuaminika, wenye tija na ufanisi. Miundo mbinu na huduma ni vipengele muhimu kwa ajili ya uhimizaji na uwezeshaji wa biashara ya ndani pamoja na biashara ya kimataifa. Kwa hiyo uendelezaji wa sekta hiyo ni muhimu. Mfumo wa uchukuzi ulioendelezwa vizuri, unapunguza gharama za uendeshaji na kuokoa muda; ambavyo ni muhimu kwa biashara.

Sekta hii inasimamiwa na Sera ya Uchukuzi ya Taifa (2003) inayojumuisha aina zote za uchukuzi kama vile kwa barabara, majini, reli na usafirishaji kwa njia ya anga. Kuna vyombo viwili vya usimamizi: Mamlaka ya Usimamizi wa Usafirishaji wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) na Mamlaka ya Usafiri wa Anga (TCAA)

katika sehemu hii, utapata taarifa  za kina zinazohusu Sekta ya Uchukuzi  ambayo ni kubwa na  yenye wingi wa mitindo ya kushindana na namna mbadala za umiliki na uendeshaji katika sekta ya umma na binafsi. Kwa taarifa zaidi tembelea Wizara ya Uchukuzi

Usafiri wa Barabara Marekebisho katika Sekta ya Uchukuzi
Usafiri wa Majini Korido ya Kati
Usafiri wa Reli
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-09 20:01:48
Kufaa
5.0
1 Jumla
Inafaa Sana 1
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page