Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Mwanzo Taifa Letu

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni Taifa katika Afrika Mashariki lililopakana na Kenya na Uganda upande wa Kaskazini, Rwanda, Burundi na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo kwa upande wa Magharibi na Zambia, Malawi na Msumbiji upande wa Kusini. mashariki inapakana na Bahari ya Hindi.

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ni moja yenye mikoa 30. Rais wa sasa wa nchi ni Jakaya Mrisho Kikwete aliyechaguliwa mwaka 2005. Tangu mwaka 1996, mji mkuu wa Tanzania ni Dodoma, ambako Bunge na baadhi ya ofisi za serikali zipo. Kati ya Uhuru na 1996 mji wa mwambao wa Dar es Salaam umekuwa mji mkuu wa Serikali. Hivi sasa Dar es Salaam imebaki kuwa mji mkuu wa biashara wa Tanzania na makao makuu ya taasisi nyingi za serikali. Ni bandari kuu ya nchi na nchi za jirani zisizo na bandari.

Kipengele hiki kinakuletea habari zinazohusu Utamaduni wa Tanzania,Urithi,Sikukuu na sherehe za kitaifa,Wasifu wa Tanzania,Picha za matukio mbalimbali kama sherehe za kitaifa,Utamaduni na urithi pamoja na picha za miradi  ya maendeleo,Historia na Alama za Taifa,Fedha inayotumika,Muziki na Michezo maarufu pamoja Hotuba zilizotolewa na viongozi mbalimbali maarufu. 

Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-01 07:33:32

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page