Fomu ya Maoni


   | 
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  
 
  • Mwl. Julius K. Nyerere
  • Mh. Amani Abeid Karume
Nifanyeje
Soma zaidi » ...
Mwanzo MatangazoMawasiliano

Umuhimu wa Sekta ya Mawasiliano kwa mwezeshaji wa maendeleo ya uchumi ya haraka kwa Tanzania dhahiri. Sekta hiyo inatoa mchango muhimu sana katika kuwezesha sekta nyingine za uchumi kwa kutoa miundombinu ya mawasiliano ya huduma ili kuruhusu utiririko wa habari ya haraka, kubadilishana na kushirikiana miongoni mwa wateja kwa ajili ya kuongeza ufanisi kuimarisha utendaji na tija. Ulegezaji masharti katika sekta hii ulio katika hatua kubwa kuanzia huduma za mawasiliano kutoka kwenye sehemu hii.

Huduma zake nyingi zinatolewa na sekta binafsi na kutokana na gharama kubwa zinazohitajika katika kuanzisha shughuli, umilikaji mkubwa ni wa kigeni ingawa kuna sehemu nyingine ambazo washiriki wazalendo wanamiliki hisa. Sekta ya mawasiliano inasimamiwa na Sera ya Mawasiliano ya Simu (1997), Sera ya TEHAMA (2003), Sera ya Utangazaji Habari (2004) na sera ya posta (2003). Sekta hii inasimamiwa na mamlaka ya mawasiliano(TCRA) wa chombo kilichoanzishwa na sheria ya usimamizi wa udhibiti wa mawasiliano Tanzania(2003). Sekta ndogo zote (mawasiliano ya simu, posta, usafirishaji, vifurushi, habari na tekinolojia za mawasiliano, huduma zinazojumuisha utangazaji) hivi sasa zinahesabiwa kuwa ni sekta moja kutokana na kushirikiana  tekinolojia, huduma na kanuni.

Bado kuna uwezekano wa kupanua zaidi huduma za mawasiliano nchini Tanzania kutokana na ukubwa wa nchi na kuongezeka haraka kwa mahitaji ya huduma za mawasiliano kunakosababishwwa na ongezeko la idadi ya watu. Utapata taarifa  ya kina kuhusu program mbalimbali za maendeleo, sera, mipango mkakati yenye lengo la kupata huduma bora zaidi, zenye tija na zinazofikika na wote. Huduma hizi zinatolewa na sehemu zinazofanyakazi vizuri na endelevu za sekta ya mawasiliano, sayansi na teknolojia kupitia wizara zinazojumuisha: Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania ( TCRA), Taasisi ya Sayansi na Teknolojia, Dar es Salaam (DIT), Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya (MUST), Chuo Kikuu cha Nelson Mandela cha Sayansi na Teknolojia, Arusha (NIMAIST), Shirika la  Posta Tanzania (TPC), Kampuni ya Mawasiliano  ya Simu Tanzania(TTCL) Tume ya Nguvu za Atomiki Tanzania (TAEC) na Tume ya Sayansi na Teknolijia Tanzania (COSTECH).

 

Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania Taasisi ya Teknolojia Dar es Salaam
Chuo Kikuu cha Sayansi na Teknolojia Mbeya Taasisi ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Arusha ( NM- AIST)
Shirika la Posta Tanzania Kampuni ya Simu Tanzania
Tume ya Nguvu za Atomiki Tume ya Sayansi na Teknolojia
 
Chanzo: Kamati ya Taarifa za Tovuti Kuu ya Serikali, Taarifa hizi Zilirekebishwa : 2015-10-12 19:15:02
Kufaa
0.0
0 Jumla
Inafaa Sana 0
Inafaa Kiasi 0
Sina Hakika 0
Haifai Sana 0
Haifai Kabisa 0
Urahisi wa kutumia
0.0
0 Jumla
Rahisi Sana 0
Rahisi Kiasi 0
Sina Hakika 0
Si Rahisi Sana 0
Si Rahisi kabisa 0

Click here to subscribe this page
Subscribe new content on this page